You are on page 1of 2

OFISI YA RAIS - TAMISEMI

HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA


MTIHANI WA KUJIANDAA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI - 2023
SOMO: URAIA NA MAADILI DARASA: VII MUDA: SAA 1:30

SEHEMU A: Chagua herufi ya jibu sahihi.


1. Umri sahihi wa kupiga kura ni miaka___ A. 13 B. 14 C. 16 D. 18 E. 20 ( )
2. Chama cha TANU kilianzishwa mwaka gani? A. 1958 B. 1972 C. 1952 D. 1960 E. 1954 ( )
3. Jambo moja kati ya haya ni wajibu wa mtoto.
A. kutii wazazi B. kusomeshwa C. kutelekezwa D. kufunzwa E. kusoma ( )
4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huadhimishwa kila mwaka tarehe____
A. 07 Julai B. 1 Mei C. 26 April D. 12 Januari E. 9 Septemba ( )
5. Mwenyekiti wa kijiji huchaguliwa na____ A. Madiwani B. Halmashauri ya kijiji
C. Wanakijiji D. Chama Tawala E. Mkuu wa Wilaya ( )
6. Usafi wa mazingira kwa ujumla ni jukumu la___ A. Wageni B. Wataalam wa mazingira C. Serikali za mitaa
D. Mtendaji wa Kijiji E. Kila mwananchi ( )
7. Afisa kilimo na mifugo wa kata hushughulikia___ A. Elimu B. Afya C. Umeme
D. Kilimo na mifugo E. Mazingira ( )
8. Lugha kuu ya Taifa letu ni__ A. Kisukuma B. Kiswahili C. kizaramo D. kifaransa E. kimakonde ( )
9. Zifuatazo ni haki za watoto isipokuwa___ A. kuishi B. Kupata Elimu C. Kusikilizwa
D. kuajiriwa E. kupata matibabu ( )
10. Kiongozi mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ni___ A. Mkurugenzi wa Halmashauri B. mwenyekiti wa
Halmashauri C. Meya wa Wilaya D. Mkuu wa Wilaya E. Afisa tarafa ( )
11. Meya wa Halmashauri ya wilaya huchaguliwa na___
A. wananchi B. Baraza la madiwani C. Mkurugenzi wa manispaa
D. waziri wa TAMISEMI D. Mkuu wa Mkoa E. Mkuu wa Wilaya ( )
12. Mambo unayotakiwa kuwatendea watu wengine ni__
A. haki B. Mila C. wajibu D. Utashi E. Utamaduni ( )
13. Chombo cha serikali chenye mamlaka ya kupambana na kuzuia rushwa____
A. mahakama B. Bunge C. Polisi D. TAMISEMI E. TAKUKURU ( )
14. Diwani wa kata huchaguliwa kila baada ya miaka___ A. 10 B. 8 C. 3 D. 5 E. 4 ( )
15. Tanzania iliamua kuwa na mfumo wa vyama vingi mnamo mwaka__
A. 1992 B. 1962 C. 1995 D. 1954 E. 1964 ( )
16. Hapa Tanzania kuna lugha za makabila zaidi ya____ A. 120 B. 102 C. 200 D. 201 E. 210 ( )
17. Ulinzi wa mikapa ni wa___ A. JKT B. POLISI C. JKU D. Magereza E. JWTZ ( )
18. Rangi ya bluu katika bendera huonesha__
A. Nishati B. rangi ya mtanzania C. Uoto D. Madini E. maji ( )
19. Uchaguzi uliohusisha vyama vingi kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka___
A. 2010 B. 2005 C. 1995 D. 2000 E. 1992 ( )
20. Wafuatao ni viongozi wa kuchaguliwa na wanachi isipokuwa
A. madiwani B. wakuu wa wilaya C. raisi D. Mwenyekiti wa kijiji E. wabunge ( )
21. Kitu kinachosababisha hatari / balaa huitwa___ A. mafuriko B. Njaa C. janga D. tetemeko ( )
22. Yafuatayo ni mazao ya biashara isipokuwa__
A. katani B. chai C. tumbaku D. Mahindi E. kahawa ( )
23. Sheria kabla haijawekwa saini na Rais huitwa___
A. Mswada B. katiba C. Haki D. sheria ndogo D. sheria ( )
24. Vitu vifuatavyo ni vielelezo vya utamaduni isipokuwa__
A. sanaa B. mavazi C. lugha D. bendera E. kuabudu ( )
25. _____ ni mambo yanayofanywa na jamii kulingana na asili au mazingira.
A. sanaa B. Mila C. Utamaduni D. desturi E. biashara ( )
26. Kupiga vita magonjwa kama UKIMWI na malaria ni jukumu la ___
A. wanafunzi B. wauguzi C. kila rais D. Viongozi E. walimu ( )
27. _____ ni kiongozi wa kata anaepatikana kwa kuteuliwa. A. diwani B. Mwenyekiti
C. kitongoji D. balozi wa nyumba 10 E. Afisa Mtendaji kata ( )
28. Shirika la Umoja wa m ataifa linaloshughulikia masuala ya watoto huitwa___
A. CHAVITA B. UNICEF C. TAMWA D. MEWATA E. CHAWATA ( )
29. Madaraka anayopewa mtu ya kusimamia kazi au shughuli flani huitwa___
A. Uongozi B. Utawala C. demokrasia D. wajibu E. haki ( )
30. ____ ni ugonjwa unaoongoza kuuwa watu nchini.
A. UKIMWI B. Korona C. Malaria D. Kifua kikuu E. kansa ( )
31. Vifuatavyo ni vyombo vya usafiri isipokuwa___
A. meli B. Jahazi C. Rubani D. Mitumbwi E. boti ( )
32. Mwenyekiti wa serikali ya kijiji au mtaa huchaguliwa na__ A. serikali ya kijiji B. kamati ya Ulinzi
C. Kamati ya kuzuia rushwa D. Diwani E. wananchi wote wa kijiji au mtaa ( )
33. Alama ya mwenge kwenye nembo ya Taifa humaanisha__
A. Uhuru wa taifa B. Biashara za watanzania C. Umoja wa wafanyakazi ( )
D. Nguvu itokayo na umoja wa watanzania E. umoja wa wafanyabiashara
34. Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi kwa sasa ni___ A. Mrisho J. Kikwete B. Samia Suluhu Hasani
C. JK Nyerere D. J.P. Magufuli E. Kasimu majaliwa ( )
35. Mtu anayesimamia shughuli flani hadi kufanyika vizuri ni__
A. tarishi B. kiranja C. kiongozi D. Mwalimu E. mwenyekiti ( )
36. Mojawapo ya kazi za kamati ya shule ni__
A. kufundisha wanafunzi B. kusimamia ujenzi wa majengo ya shule C. kugawana fedha za shule
D. kuwalipa walimu mishahara yao E. kuwaadhibu walimu ( )
37. Jambo linalolazimu mtu kulitimiza ni___ A. Wajibu B, Sheria C. Kanuni D. Haki E. katiba ( )
38. Madini moja wapo ambayo hupatikana Tanzania tu ni___
A. dhahabu B. Almas C. Tanzanaiti D. Chokaa E. chuma ( )
39. Katika kesi za jinai mlalamikaji huwa ni__
A. jamuhuri ya Muungano B. Jeshi la Mgambo C. Jeshi la wananchi
D. Jeshi la Polisi E. Mtu anayevunja sheria ( )
40. Moja ya kazi za mahakama ni___ A. kuwafunga gerezani watuhumiwa B. Kutafasiri sheria zilizotungwa na bunge
C. Kukomesha wizi nchini D. kuwaachilia huru watuhumiwa E. kufundisha sheria. ( )

SEHEMU B: Jaza nafasi iliyoachwa wazi


41. Jeshi la ………………………………………………… ndio lenye dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
42. ………………………………………….. ni mfumo wa kuendesha serikali iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu
43. Utawala bora ni utawala wa ……………………………………………………………………………………………………………………
44. Bajeti ya serikali hupitishwa na ………………………………………………………………………………………………
45. Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilianzishwa mnamo mwaka ………………………………

You might also like