You are on page 1of 3

PARADISE EDUCATION CENTRE

JARIBIO LA KISWAHILI 1
KIDATO CHA 6
Muda; Saa 3 Tarehe; 04/03/2022
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane (8).
2. Jibu maswali yote katika sehemu A na maswali matatu (3) kutoka sehemu B.
3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
5. Andika jina lako katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 40)

1
Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kwa umakini kisha jibu kwa usahihi maswali
yanayofuata:
Nchi ya Tanzania hufanya uchaguzi wake kila baada ya miaka mitano, uchaguzi mkuu
huhusisha uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani. Octoba 2020 watanzania wote
walikuwa katika pilikapilika za kuwapata viongozi wa kuwawakilisha katika matatizo
yao.

Mtanzania aliyekuwa huru kuchagua viongozi wake alitakiwa kutimiza masharti


yafuatayo:- Awe amejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, awe na umri
wa miaka kumi na nane na kuendelea, awe raia wa Tanzania na awe na akili timamu.

Uchaguzi ulifanyika kwa amani, wananchi waliweza kuelemishwa kupitia vyombo vya
habari kama redio, magazeti, Runinga pamoja na majarida. Kwa kutumia vyombo hivyo
vya habari zilifika sehemu zote za nchi yaani mijini na vijijini, kila mtanzania alijua
uchaguzi ni muhimu kwake kwani hutupatia viongozi bora kuendeleza demokrasia,
kuleta mabadiliko nchini na kutatua migogoro mbalimabli katika jamii pamoja na
kuondoa ubaguzi. Watanzania tushikamane kuendeleza amani nchini.

Maswali
a) Pendekeza kichwa cha habari kifaacho kwa habari hiyo.
b) Uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mingapi hapa Tanzania?
c) Taja sifa tatu za mtu anaetakiwa kupiga kura.
d) Unafikiri uchaguzi una umuhimu? Kama ndio au hapana toa hoja tatu.
e) Toa ujumbe kutokana na habari hii.

2. Unaelewa nini kuhusu neno rejesta? Kwa kutumia mifano fafanua aina za rejesta katika
lugha ya Kiswahili.

3. Toa maana za istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika lugha ya Kiswahili.


(a) Kiima
(b) Kiarifu
(c) kishazi tegemezi
(d) Kishazi huru
(e) Unominishaji

4. a) Tunga sentensi kwa kutumia ngeli zifuatazo;


(i) U-I
(ii) Li-ya
(iii) Ki-vi
(iv) I-zi
(v) U-zi

2
b) Tunga sentensi tano zinazoonesha o-rejeshi.

SEHEMU B (Alama 60)


Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii. Swali la nane (8) ni la lazima.
5. Jifanye wewe ni Afisa Habari wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi. Andika tangazo la
upatikanaji wa usafiri wa ndege katika uwanja wa Songea kuanzia tarehe 30/09/2020 saa
kumi jioni. Jina la mtoa tangazo liwe Zainabu Juma.

6. Vyombo vya habari vimetoa mchango mkubwa katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili
nchini Tanzania. Kwa kutoa hoja sita (06) jadili namna vyombo vya habari vilivyotimiza
azma ya kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.

7. Onyesha tofauti sita (6) kati ya Lugha ya mazungumzo na Lugha ya maandishi.

8. Nini maana ya ukalimani? Elezea dhima nne za ukalimani.

UMEANDALIWA NA MWALIMU JOHN EDWARD


SIMU; 0757189316/0789049283

You might also like