You are on page 1of 4

UMOJA WA SKULI BINAFSI ZANZIBAR

MTIHANI WA PAMOJA WA KIDATO CHA SITA

121/2 KISWAHILI 2

Muda: Masaa 3 Ijumaa, 22/03/2024 Mchana

Maelekezo:

1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya mwaswali nane (8).

2. Jibu maswali yote katika sehemu A na maswali matatu (3) tu kutoka sehemu B. Swali la tano

ni la lazima.

3. Sehemu A inaalama Arobaini (40) na sehemu B ina alama Sitini (60)

4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali

5. Simu za mkononi haziruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani.

6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu cha kujibia
SEHEMU A (Alama 40)
Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

1. Sikuzote fasihi imekuwa ikiyachungulia na kuyafanyia kazi maisha ya jamii na wanajamii


wenyewe katika nyanja mbalimbali za Maisha. Fafanua kauli hii huku ukiegemea katika
mifumo ya historia ya Maisha ya mwanadamu. Tumia hoja tano

2. “Waandishi wa kazi za kifasihi ni nguzo kubwa katika kuzikomboa jamii kiuchumi,


kijamii na hata kisiasa, lakini pia huchukuwa nafasi kubwa zaidi ya kuwa ni mwalimu
bora wa maendeleo katika jamii husika iwapo hawataingiliwa katika uhuru wao”
Ukitumia hoja tano maridhawa onesha ni kwa vipi makali haya ya waandishi wa fasihi
yanaweza kufifia?

3. Ukitumia mifano Madhubuti fafanu aina mbili za tamathali za semi za Mafumbo na aina
tatu za tamathali za semi za Mlinganisho

4. Soma shairi lifuatalo kisha fafanua vipengelevya kisanaa vilivyotumika katika shairi hilo

Wasema humwoni mtu, mbona wewe pia mtu?


Mtu hamzidi mtu, utajiri sio kitu,
Mali twajuwa ni vitu, mithili ya nyama mwitu,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.

Yule pale mwenye njaa, fikiri umtazame,


Ni mtu au mkaa, kakauka kama gome,
Viguu kama vya kaa, yule kaa wa ukame,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.

Wema hauonekani, ila kwa vitu na mali!


Mtu hapendi jirani, waungwana si halali,
Kupenda paka nyumbani, jiraniyo hana hali,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.

Ni ugeni wa akili, kuipenda gari yako,


Ati waiyona ghali, karibu na roho yako,
Na wengine huwajali, barabara yawa yako,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.

Dunia ina kasoro, au ina kisirani,


Akili zawa ugoro, watu hatuna imani,
Vipaji vyawa uchuro, huruma ipo mwituni,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.

Ukurasa wa 2 kati ya 4
Kiule ng’ambo nimeona, kutengana kumezidi,
Kuna wale walonona, anasa imewazidi,
Wengine wanajikuna, chakula kimekaidi,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.

Shwari nayo inanoga, sijuwi mpaka lini,


Hii ni shwari ya woga, ndani yake kuna kani,
Mwenye njaa akichaga, nyoka atoka pangoni,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.

SEHEMU B (Alama 60)


Jibu maswali matatu tu kutoka sehemu hii. Swali la tano (5) ni la lazima.

ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 5 – 8

USHAIRI
Kimbunga – Haji Gora
Mapenzi Bora – Shaaban Robert
Chungu Tamu – Theobald Mvungi
Fungate ya Uhuru – Mohamed S. Khatibu

RIWAYA
Usiku utapokwisha – Mbunda Msokile
Kufikirika – Shaaban Robert
Mfadhili – Hussein Tuwa
Vuta n’kuvute – Shafi Adam Shafi

TAMTHILIYA
Kwenye Ukingo wa Thim – Ebrahim Hussein
Morani – Emanuel Mbogo
Kivuli kinaishi – Said Mohamed
Nguzo Mama – Penina Muhando

5. Ukitumia vipengele vinne (4) vya lugha fafanua jinsi waandishi walivyozipamba kazi zao
na kukamilisha lengo lao kwa hadhira kusudiwa. Tumia hoja tatu (3) kwa kila diwani

6. Dhamira ya siasa ni miongoni mwa dhamira zinazowafikirisha sana wasanii wa kifasihi.


Ukitumia hoja tatu(3) kwa kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma, onesha jinsi
waandishi hao walivyovionesha vipengele mbalimbali vya kisiasa katika kazi zao.

Ukurasa wa 3 kati ya 4
7. Hakuna jamii inayokosa changamoto na matatizo. Onesha jinsi waandishi wa riwaya mbili
ulizozisoma waloivyoonesha matizo yanayoikabili jamii ya Kitanzania kwa sasa. Tumia
hoja nne (4) kwa kila Riwaya

8. Kila mwanajamii ana wajibu wa kuhakikisha haki na usawa vinasimama katika jamii.
Ukitumia tamthilia mbili ulizosoma onesha jinsi waandishi walivyotimiza wajibu huo kwa
jamii zao kwa kutoa hoja tatu kwa kila Tamthilia.

Ukurasa wa 4 kati ya 4

You might also like