Professional Documents
Culture Documents
Mwongozo Wa Tamthilia Ya Kijiba Cha Moyo
Mwongozo Wa Tamthilia Ya Kijiba Cha Moyo
Utangulizi.
“Moyo hupenda, moyo huchukia, moyo hukinai, moyo huhurumia, lakini moyo
unapopatwa na dhiki ni rahisi kujua unaponzwa na nini.”
Tamthilia ya kijiba cha moyo ni tamthilia inayoangazia maisha ya Sele kudhaniwa kuwa
mgonjwa, kunyimwa haki zake, na kutotetewa kwa namna yeyote anapopambana na
waiotaka kuiba moyo wake halafu akabaki na kijiba.
Sele ni kijana ambaye amebadilika kitabia katika familia, moyo wake umepatwa na kutu,
familia yake imekosa kupata utulivu kwa kughasiwa na ugonjwa wake. Sele kila tendo
analiona kuwa ni uonevu, sele ana kijiba cha moyo. Je mawaidha ya bibi yatautibu ugonjwa
wa Sele?
Dhamira ya mwandishi..
Tamthilia hii ni miongoni mwa kazi za kifasihi zinazo chunguza uhusiano uliopo baina ya
ubepari wa
mataifa na hali duni ya kiuchumi iliyojiri mataifa ya ulimwengu wa tatu kwa mtindo wa
kinaya. Mwandishi anatalii maudhui ya kiuchumi na mfumo wa kibepari ambao licha ya
kuwakandamiza wakazi wa mabara ya Afrika unapunguza nafsi za wafanyikazi na
kuwafanya kujihisi kuwa duni. Mahusiano haya yameendelezwa kwenye misingi ya
udhalimu.
Mwandishi ameelezea maonevu haya kwa kinaya akitumia sitiari pevu ili kukejeli mfumo
mzima wa uelewaji wa dhana ya uhuru katika uzalishaji mali.
Katika tamthilia hii mwandishi pia analenga kutuonyesha kuwa uongozi uliopata mashiko
yake kwenye mfumo wa kibepari, umemiliki nyenzo za kimsingi za uzalishaji mali kupitia
kwa ufisadi, uongo na zaidi katika kuwakandamiza wale waliopata mwangaza wa kuona
njama hii ya kunyanyaswa. Hili hutekelezwa ili kuzuia juhudi za wale waliopata mwamko
mpya
kisiasa dhidi ya kuwazindua wanyonge wengine katika jamii. Mwandishi kupitia kwa
mhusika nguli (Sele), anasawiri uhusiano uliopo baina ya mataifa ya ulimwengu wa
kwanza ambayo huyapa misaada na kuyamiliki mataifa ya ulimwengu wa tatu kwa
kuyafanya yakose kujitegemea. Mwandishi anasawiri kwa kina misaada inayotolewa kwa
mataifa machanga na kuonyesha kuwa misaada hii haiwafai Waafrika ila tu ni chombo
kinachotumiwa ili kuweza kupata fursa ya kuwanyonya Waafrika rasilimali zao. Hii ni
kinaya kwa kuwa Waafrika wenyewe hawaelewi hali hii.
Arege analenga kutuonyesha kuwa hali ya uhitaji katika mataifa mengi ya bara la Afrika
imesababishwa na unyonyaji wa nguvu za wakazi wake kwa malipo duni. Anaeleza kuwa
mipango ya kuyasukuma mbele kimaendeleo mataifa machanga barani Afrika ambayo
inaamuliwa na kuwekwa na mataifa yanayodai kujitegemea ni chanzo cha kudorora kwa
maendeleo yanayotarajiwa. Hii inatokana na ukweli kwamba walioshikilia (wakoloni)
nguzo za mfumo huu wa kibepari waliwafumba macho wakazi wa nchi changa kwa
kuwapa misaada isiyowafaa.
Falsafa ya mwandishi.
Mtazamo wa mwandishi.
Mwandishi ameegemea Mtazamo wa kisiasa yaani kiyakinifu; Kuungana, kujitahidi na
kujikomboa kimawazo ni suala liwezalo kusaidia waafrika
kujiendeleza kwa misingi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hiki kinabainika baada ya
kutamatisha kusoma tamthilia hii ambapo inabainika kuwa ugonjwa wa Sele si
ule wa kawaida kama ulivyochukuliwa na wahusika tamthiliani bali kuzinduka kutokana na
mwamko mpya wa kisiasa na kijamii.
1.Sele- mumewe Aisha na mtotowe Musa na Zainabu. Sele kulingana na tamthilia ana sifa
zifuatazo;
.Ni mwenye huruma. Tendo la Sele la kukataa kuwala vidagaaa, linamsawiri kama
mhusika mwenye huruma. Sifa hii imedhihirika kupitia mazungumzo ya Zainabu na
Bi. Rahma(uk 15-16) Sele anakwepa kula vidagaa, kwa kuwa anawaonea
huruma kwa kuliwa na papa naye awale.
. Ni mwenye kutoridhika. Tendo la Sele katika tamthilia ya Kijiba cha Moyo la kutaka
kufanyiwa „plastic
surgery‟ linadhihirisha sifa yake ya kutoridhishwa na maumbile yake na nia yake ya
kutaka kuyabadili. Hili limedhihirika katika kurasa 31-36. Hali hii ya Sele
inawakilisha mataifa ya Kiafrika yasiyoridhishwa na hali zao na kutaka kuiga mataifa
ya ng‟ambo.
.Ni mkaidi. Tunamuona Sele anakaidi mashauri ya jamaa zake na pia anakaidi kumeza dawa
kwamba yeye si mgonjwa.
2. Aisha-mkewe Sele.
.Ni mwenye kupenda raha. Hili linadhihirishwa pale alimomwambia mumewe kwamba
waende kujistarehe (uk 03)
.Ni mwenye mapenzi na kumjali mume wake. Hili linadhirika anapoingia chumba walimo
wazee wake na kuwapuuza akienda mbio kutafuta vitabu kuvisoma ili aelewe ugonjwa wa
mume wake ili aweze kumsaidia.(uk20)
.Ni msomi. Amesawiriwa kama msomi. Sifa hii inadhihirika kupitia tabia
yake ya kusomasoma vitabu. Hili linadhihirika kupitia mazungumzo baina ya Aisha,
Zainabu na Bi. Rahma(uk18)
.Ni mwenye heshima. Heshima ya Aisha inadhihirika pale anapowheshimu wazee wake kwa
kutowaita majina.
.Ni mwenye kumjali mwanawe Sele. Zaiabu tunamuona anatembea juu chini akimtafutia
dawa la kumtibu. Tena mwenye hamu kusikiliza muuguzi Jamila wakati alipokuwa anamtibu
kwake nyumbani (uk88)
.Ni mvumilivu kwani tunamuona katika tamthilia nzima anavumilia na ugonjwa wa mtotowe
hata ingawa alimtusi wakati mwingine.
5.Daktari.
.Ni mkatili kwani tunamuona katika tamthilia ndiye aliongoza waliomtembelea sele na
kumpekuapekua alipokuwa amelala. Pia alimkataa kuuliza maswali kuhusu ugonwa wake
Sele.
7.Musa-Babake Sele.
Mwandishi kupitia mhusika Sele anasawiri uhusiano uliopo baina ya mataifa ya ulimwengu
wa kwanza (viongozi) ambayo huyapa mataifa ya ulimwengu wa tatu misaada isiyofaa kv
matibabu ya Sele, ila tu ni chombo cha kupata fursa ya kugawanya rasilimali zao.
Muuguzi jamila pia anaeleza kwamba ugonjwa wa sele haujafikia kiwango cha kutisha
(uk89).
Aisha anamoenda sana mumewe Sele ndiposa anaingia chumba walimo wazee wake na
kuwaluuza akitafuta vitabu akikusudi kusoma ili aelewe ugonjwa wa Sele aweze
kumsaidia(uk18)
8. Unyanyasaji. Ni hali ya kudharau mtu kwa kiburi au kwa kujiona bora dhidi yake.
Tendo la madaktari watatu kuja kumpekuapekua huku na kule mwili mzima ni ishara ya
kudharau na kumnyanyasa.
Tena kunyimwa fursa ya kuuliza daktari na kutopewa habari kuhusu tests zake hospitalini
ninishara ya kumnyanyasa kiakili.
Ukatili unajitokeza pale daktari anapompiga dawa sele akiwa anajua sele si mgongwa ila tu
kwa hamu ya kumyakua pesa zake.(uk52-53) “staki kupoteza muda, time is money bwana” ni
ishara ya ukatili.
10.Utumwa. Ni mfumo unaotoa fursa kwa binadamu kumiliki binadamu mwingine kama
mali yake.
Utumwa unadhihirika pale ambapo Sele ananyimwa fursa ya kupata matokea ya habari
kuhusu “tests” zake hospitalini (uk60, 61)
12. Ndoa. Ni maafikiano rasmi baina ya mwanamke na mwanamume. Ndoa inashihirika kati
ya Sele na Aisha pamoja Musa na Zainabu.
13. Uvuvi.
Ukosefu wa nidhamu katika tamthilia ya kijiba cha moyo unaonyeshwa pale Aisha alipoingia
chumba waliomo wazee wake na kuwapuuza baada ya kuwasalamia tu na akaingia kwenye
chumba kingine akaaanza kutafuta vitabu vya kusoma iki aelewe ugonjwa wa sele. (Uk20)
1.Tashbihi ni tamathali ya usemi ambapo watu ama vitu viwili au zaidi hulinganishwa au
hufananishwa na watu ama vitu vingine.
Tamthilia ya Kijiba cha Moyo imetawaliwa na methali mbalimbali kwa nia ya mwandishi
ya kukuza ujumbe wake. Bi. Rahma analalamikia mapishi ya kisasa na kushuku kuwa
huenda ndiyo yanamkosesha Sele hamu ya chakula. Anamwambia Zainabu:
“… Watavilaje vyakula vya kuharakishwa?
Heri huvutwa kwa subira mama. Vyakula
visivyopata kutua sufuria, vipi vitatua
moyoni?” (uk. 14)
Methali anayoitumia Bi. Rahma ina maana kwamba kizazi cha kisasa hakina subira
katika kutekeleza majukumu hasa kimapishi.
Katika tamthilia ya Kijiba cha Moyo, mwandishi ametuchorea taswira nzuri zaidi
inayoonyesha uhusiano wa mabepari na wanyonge katika jamii. Sele anamweleza Aisha:
“Yapo mengi mengine. Ni kweli papa
ana kiburi kikubwa maana yu mfalme
wa bahari. Mwili wake una uwezo wa
kuzuia mawimbi ya bahari navyo
vidagaa hujificha nyuma yake kujisitiri.
Vidagaa vinajua ni hatari lakini afadhali
hatari ya papa kuvila badala ya kuangamizwa na mawimbi makali. Wajua ni kama
kuku ambaye anakiona kisu cha mchinjaji
afadhali kuliko maisha vichakani…” (uk. 37)
Bi. Rahma anamweleza Sele kama mtu asiye na matumaini. Anamwambia hivi:
…“umekata tamaa kwa kufutwa kazi…” (uk. 28)
Kule kuja kwa daktari mrefu akifuatiwa na daktari mfupi na nyuma yao wakifuatiwa
na mganga wakati Sele amelala inaashiria majio ya wakoloni wakati Waafrika
wenyewe hawatambui. Kujibizana kwa furaha na kukumbatiana na kisha kuzozana
kwa madaktari wakiwa karibu na Sele kunaashiria kutoafikiana kwao kuhusu ugawaji
wa rasilimali kutoka kwa nchiya Kiafrika (Sele) iliyokuwa bado imelala mbele yao.
Wakati wote huu nchi zingine za Afrika (mganga) zilikuwa kando zikitazama.
Hadithi ya papa na vidagaa katika Kijiba cha Moyo, imetumika kufafanua maisha
halisi yalivyo katika ulimwengu wa kihadithi. Ambapo wenye vyeo na mamlaka
wanawagandamiza wanyonge. Nao wanyonge licha ya kudhulumiwa na wenye vyeo
bado wangali wanawategemea hao hao. Tunaelezwa, “…Mwili wake una uwezo wa
kuzuia mawimbi ya bahari navyo vidagaa hujificha nyuma yake kujisitiri. Vidagaa
vinajua ni hatari lakini afadhali hatari ya papa kuvila…” (uk.37). Hali hii ndiyo
iliyompelekea Sele kutafakari upya juu ya uhusiano wao na wafadhili wao na hiki
ndicho kijiba katika moyo wa Sele.