You are on page 1of 39

MWONGOZO WA CHOZI LA HERI: MASWALI NA MAJIBU

(Assumpta K. Matei)

Na

Kirimi Nyagah

1
UTANGULIZI

Mwongozo huu umetayarishwa kimaksudi kwa lengo la kumwelekeza mwanafunzi katika


uchambuzi wa vipengele mbalimbali vya fasihi katika riwaya ya Chozi la Heri. Vipengele hivi ni
pamoja na ploti, dhamira, maudhui, mbinu za lugha, wahusika na uhusika wao. Uchambuzi huu
umefanywa kwa namna inayooanisha dhamira ya mwandishi na hali halisi katika jamii. Isitoshe,
mchakato mzima wa kuwasuka wahusika na kuyajenga maudhui umeweza kuelezwa kwa njia
sahili inayomwezesha msomaji kuielewa zaidi kazi husika. Ni mwongozo ambao unarahisisha
uelewaji wa masuala yanayoonekana changamano na tata kwa kutoan msuko ulio sahili.
Mwongozo huu ni wa kipekee kwa maana una maswali kadha ya kumchokonoa mwanafunzi,
Isitoshe, maswali haya yametolewa majibu yenye hoja za kuridhisha. Majibu haya yanalenga
hasa matarajio ya watahini na mitindo mipya ya kutahini ambapo unapata mwanafunzi
anahitajika kuandika hoja kumi na nne kujibu swali moja. Kuna aina mbalimbali za maswali.
Kuna yale ya dondoo, ya kujadili pamoja na yale ya kuthibitisha kauli ama usemi fulani kutoka
kwenye riwaya. Kwa kifupi, huu ni mwongozo wa aina yake ambao haumwonjeshi tu msomaji
asali bali unampa fursa ya kuchovya moja kwa moja ndani ya buyu lenyewe.

1.0 RIWAYA: CHOZI LA HERI (Assumpta K. Matei)

1.1 MSUKO/PLOTI

1.1.1 Sura ya Kwanza

Ridhaa anatazama jumba lake la kifahari linaloteketea. Ndani ya jumba hili ameteketea Terry
mkewe, watoto wake wawili: Annatila (Tila) na Mukeli pamoja na Lily Nyamvua (mkaza mwana)
na Becky (mjukuu wake). Nyamvula ni mke wa Mwangeka (Kitinda mimba wa Ridhaa).
Mwangeka hakuwepo wakati wa mkasa huu kwa maana alikuwa amesafiri kudumisha amani.
Ridhaa anakumbuka mjadala aliokuwa nao na mkewe usiku wa kuamkia msiba. Anakumbuka
akisikia mlipuko mkubwa uliomtia uziwi. Anazimia. Anaelekea shambani, mimea yake
imeteketezwa pia. Anarudi katikakati ya chumba. Humu ndimo alimozaliwa Mwangeka. Ridhaa
anakumbuka dayalojia yake na binti yake Tila kuhusiana na nchi ya Wahafidhina kutokua
kidemokrasia licha ya kujipatia uhuru miaka hamsini iliyopita.

2
Ridhaa anakumbuka walivyojipata katika Msitu wa Heri. Walihamishiwa huku na babake Mzee
Msubili kwani ardhi yake haingewatosha wanawake kumi na wawili na watoto kadha. Ridhaa
alikuwa na umri wa miaka kumi. Anapoanza masomo anasutwa na watoto wenyeji kwa kuitwa
Mfuata Mvua. Ridhaa anajitahidi masomoni na kuhitimu udaktari.

Uharibifu huu wote wa kuchomewa mali na familia ulikuwa umesababishwa na Mzee Kedi pamoja
na majirani wake wa miongo mitano kwa kumuona kama mgeni baada ya Mwekevu kutawazwa
kama kiongozi wa Wahafidhina. Majirani hawa wanamtenda Ridhaa licha ya ukarimu na mchango
wake kwa sehemu hii.

1.1.2 Sura ya Pili

Sura hii inamulika ghasia zilizotukia baada ya uchaguzi na maisha ya wakimbizi katika Mlima wa
Mamba. Kaizari ndiye msimulizi. Baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya wa kike, Mwekevu,
ghasia zilishamiri kwa maana kulingana na baadhi ya Wahafidhina mwanamke hakufaa kuongoza.
Vurumai hii inasababishwa na wafuasi wa mpinzani wa kiume wa Mwekevu. Mali iliteketezwa,
nao biadamu wakapoteza uhai. Vijana waliokuwa wakiandamana nao wakaishia kupigwa risasi.
Baadhi ya Wahafidhina, wakiwemo Kaizari, Ridhaa, Selume na aliyekuwa Waziri wa Fedha,
Bwana Kute, Bwana Kangata na wengine wanakimbilia katika Msitu wa Mamba. Humu
wanakuwa wakimbizi. Kuna changamoto tele; hamna chakula, maji safi, misala na vyumba. Wengi
wao wanakufa kutokana na homa ya matumbo. Wanajenga mabanda. Hamna faragha.
Wanamowasili hamna utabaka miongoni mwao. Ndugu Kaizari anahimiza wenzake kuchimba
misala.

Selume naye pia ameungana na wakimbizi wengine. Alikuwa amehitilafiana na wakwe zake
waliodai kuwa alikuwa mfuasi wa Mwekevu. Baada ya siku ya ishirini, chakula cha msaada
kinaletwa na dhehebu moja la kidini. Bwana Waziri Mstaafu na Kaizari wanasaidia kukigawa
sawa.Hata hivyo baadhi ya wakimbizi hawa wanabuni ujanja ili kugawiwa kingi zaidi mathalani,
Bwana Kute, aliyekuwa Diwani wa Wahafidhina anaigawa familia yake kuwili.

3
1.1.3 Sura ya Tatu

Ridhaa yuko uwanjani wa ndege wa Rubia akisubiri kuwasili kwa kitinda mimba wake, Mwangeka
kutoka ughaibuni. Ridhaa, Kaizari na familia yake (Subira mkewe na mabinti zake Mwanaheri na
Lime) wamesharudishwa nyumbani kupitia mradi ulioitwa Operesheni Rudi Edeni. Walikuwa
wameishi Msiti wa Mamba kwa miezi sita.Ridhaa anaona kurudishwa huku kama kurudishwa
Misri matesoni. Akiwa Msitu wa Mamba alikuwa amepewa ushauri wa kukabiliana na hali yake.
Ridhaa anakumbuka yaliyotokea anaporudishwa katika ganjo lake, anashindwa kujihimili na
kuzirai. Anapozinduka anakumbuka mchezo wake na Becky pamoja na utani wake na mkewe
Terry.

Ridhaa anapomsubiri Mwangeka, anaanza kumwona Tila mawazoni mwake akitoka shuleni na
kushiriki dayolojia ndefu. Wanazungumzia masuala nyeti ya uongozi, siasa na haki za kibinadamu.
Tila anaona kuwa dhiki zinazowasonga wananchi ni tokeo la uongozi mbaya. Tila alitaka kuwa
jaji katika mahakama ya juu.

Mwangeka anapowasili Ridhaa anamkaribisha na kuhakikishiana kuwa wangali hai. Ridhaa


anamjuza kuhusiana na tanzia iliyowafika. Mwangeka anaona kuwa babake aalikuwa amebadilika
sana. Ridhaa anamwagiza waende nyumbani kupumzika na kuzungumza mengine.

1.1.4 Sura ya Nne

Ridhaa anampeleka Mwangeka kwenye gofu la kasri lake. Madhara ya moto yalikuwa wazi.
Mwangeka anashangaa ni kwa nini babake hakuchimba kaburi la pamoja kuzika mabaki ya familia
yao. Ridhaa anamjibu kuwa kuna baadhi ya mambo yanayopaswa kutendwa kinyume maishani.
Ridhaa anamsimulia kadhia yote iliyowafika tangu Mwangeka alipoondoka nyumbani kuanzia na
kupoteza majumba yake mawili, kifo cha ami yake, Makaa, aliyeteketea akijaribu kuwaokoa
wasomba mafuta. Aidha, anamsimulia kuhusiana na kuteketezwa kwa jumba lao pamoja na familia
yake kwa ujumla pamoja na changamoto zilizomkumba akiwa kwenye Msitu wa Mamba kama
mkimbizi lakini anashukuru kwa kujifunza thamani ya maisha, utu na amani.

Mwangeka hakuishi na babake kwa muda mrefu. Hakustahimili kuona mahali ilipoangamia
familia yake kila asubuhi. Alipata kiwanja karibu na ufuo wa bahari anapojenga jumba na
kidimbwi cha kuogelea. Anapotazama kidimbwi hiki anakumbuka changamoto za ukuaji wake.

4
Anakumbuka wanuna wake: Annatila, Mukeli na hata Dede aliyekufa, Mwangeka akiwa na umri
wa miaka sita.Anakumbuka viviga alivyofanyiwa Dede na kichapo alichokipata baada ya yeye na
wanuna wenzake kujaribu kuiga kwa kuigiza viviga vya wanajamii.

Mwangeka anakumbuka alivyoamua kumakinika shuleni hadi chuo kikuu alipohitimu uhandisi na
kukutana na Lily alipokuwa akisomea Uanasheria. Mwangeka anajiunga na kikosi cha wanamaji.
Awali, Nyamvua aliupinga uamuzi huu lakini akaja kuridhia shingo upande. Sasa Mwangeka
anajuta kutomsikiliza mkewe; labda angewaokoa. Magharibi inapoingia, Mwangeka anainuka
kwenda kukabiliana na usiku wenye upweke.

1.1.5 Sura ya Tano

Sura hii inaturudisha nyuma kwenye msitu wa Mamba. Wakimbizi wanaingiwa na tamaa ya utajiri
wa msitu huu. Wanakata miti kwa lengo la ujenzi na kilimo. Punde majumba yenye mapaa ya
vigae na maduka ya jumla yanatawala msitu huu. Familia ya Bwana Kangata ilikuwa miongoni
mwa kundi hili. Kabla ya kuja kwenye msitu huu, Kangata alikuwa akiishi kwa tajiri wake Kiriri.
Kwenye msitu wa Mamba, Kangata aliendeleza ujuzi wake wa kilimo.Baada ya kifo cha Kangata
na mkewe, Ndarine, mtoto wake wa kiume Lunga Kangata ndiye anayeridhi mali ya babake. Sasa
imepita miaka mitano tangu mauko ya Bwana Kangata.Lunga Kangata amesomea kilimo. Aliwahi
kuwa mkurugenzi katika Kitengo cha Uhifadhi wa Nafaka katika Shirika la Maghala ya Nafaka
kabla ya kupigwa kalamu kutokana na msimamo wake wa kupinga mahindi yenye sumu kuuziwa
binadamu. Katika Msitu wa Mamba anatononoka si haba. Anakuwa msitari wa mbele kuharibu
mazingira licha ya msimamo wake wa awali wa kutetea uhifadhi wake.Sasa ana mashamba
makubwa, analima mimea na kufuga ndege na wanyama.

Tofauti za kitabaka zinaanza kudhihirika. Kunatokea uchangamano na vita vya wenyewe kwa
wenyewe viazuka. Serikali inaanza kuhimiza umuhimu wa amani pamoja na kutumwa kwa vikosi
vya walinda usalama. Serikali inagundua kwamba wakazi hawa wamo humo kiharamu. Awamu
ya pili ya Operesheni Rudi Edeni inatekelezwa. Lunga Kangata anahamishiwa Mlima wa Simba
walikoishi mababu zake.Hata hivyo haijulikani ni wapi mali walizoziacha Msitu wa Mamba
zilizoenda ingawa matrekta ya kubeba mbao husikika usiku ijapokuwa u marufuku kwa binadamu.

5
1.1.6 Sura ya Sita

Mwalimu Dhahabu anamhimiza Umukheri kurejesha mawazo yake darasani. Hii ni kwa sababu
fikra zake zilikuwa kwenye dhiki alizokuwa anapambana nazo. Umu ni bintiye Lunga Kangata na
Naomi. Baada ya kuhamishwa kutoka Msitu wa Mamba hadi Mlima wa Simba hali ya maisha
ilimwia vigumu. Alishindwa kukubali hali hii ya maisha. Alishindwa kuwasomesha wanawe hata
katika shule wa kima cha wastani. Mkewe Naomi anatoroka na kumwandikia ujumbe mfupi kuwa
alikuwa ameenda kutafuta namna ya kusaidia kuikimu familia.Lunga anaachiwa mzigo wa kulea
wanawe watatu: Umukheri (kidato cha kwanza, Dick (darasa la saba) na Mwaliko (darasa la
kwanza). Lunga anafariki kutokana na shinikizo la damu mwilini na kuacha wanawe chini ya ulinzi
wa kijakazi Sauna.

Asubuhi moja Umu anagundua Dick na Mwaliko walikuwa wametoweka. Akaamua kupiga ripoti
katika kituo cha polisi.Inabainika kuwa Sauna ndiye aliyewatorosha Dick na Mwaliko katika
biashara ya nipe nikupe na ulanguzi wa dawa za kulevya. Umu anaamua kutorokea jijini Karaha
kuepuka madhila ya Sauna. Umu aliwahi kutembea jijini humu. Anakumbuka alivyomrai mamake
kumpa shilingi mia moja awape watoto ombaomba. Umu anapopitia jijini hili anakutana na Hazina
yule ombaomba aliyewahi kumsaidia. Hazina anamjulisha kwa Julida, mama aliyesimamia makao
yao. Julida anamkaribisha na kumwakikishia kuwa angeendelea na masomo yake kupitia ufadhili
wa serikali. Mwezi mmoja baadaye, Umu anajiunga na shule ya Tangamano. Mwalimu Dhahabu
anabaini upesi unyonge wa Umu na kufuatilia usuli wake kupitia mwalimu wa darasa la Umu.

1.1.7 Sura ya Saba

Wanafunzi wanne (Kairu, Mwanaheri, Zohali na Chandachema) wamo katika bweni.


Wanamhimiza Umu kuzoea maisha ya mapya ya shule ya Tangamano. Kila mmoja wa vijana hawa
anajaribu kusimulia kadhia zilizowafika maishani ili Umu aone msiba wake kuwa mwepesi. Kairu
anaeleza alivyookotwa njiani na watu waliovalia mavazi ya IDR na kusombwa kambini
(Walikuwa wamefurushwa kwao na vijana) baada ya ndugu yao mdogo kufa kutokana na makali
ya njaa. Mamake Kairu alikuwa muuza samaki. Kairu alikuwa amezaliwa nje ya ndoa. Naye
Mwanaheri anaeleza makuruhu yaliyompata mamake Subira. Mzozo unaibuka baina yake na
wakwe zake (wazazi wa Mzee Kaizari). Subira alikuwa ametoka kabila tofauti na Mzee Kaizari.
Subira anamwandikia Umu kijibarua akimtaka atunze nduguye, Lime wamtii baba yao na

6
kuzingatia masomo. Anahamia mjini Kisuka anakofia kwa kunywa kinywaji kikali. Mzee kaizari
anaendea maiti hiyo. Kwa upande wake, Zohali anatorokea mjini anakookolewa na kupelekwa
kwenye Wakfu wa Mama Paulina na wenzake. Kwenye wakfu huu, Mtawa Pacha anamtafutia
Zohari nafasi katika shule ya Tangamano. Zohali alitoroka kwao baada ya wazazi wake kumkana,
kumtishia na kumfanyisha kazi tele japo alikuwa mjamzito bado akiwa kidato cha pili.
Chandachema naye alitoroka alikokuwa akilelewa na nyanya yake. Chandachema alikuwa mtoto
wa Rehema na Mwalimu wake, Fungo. Wazazi wa Rehema wanakataa Rehema kuolewa na
mwalimu wake. Baada ya kifo cha bibi huyu, Chandachema anahifadhiwa na jirani Satua ambaye
anamwona mzigo baada ya muda mfupi. Chandachema anaamua kukabili changamoto zake.
Anaenda katika kijiji walimoishi wafanyikazi wa Shirika la Chai la Tengenea. Anamkabili Bi.
Tamasha, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kilimo anayemuunganisha na Bwana Tenge
kupata hifadhi. Mfadhili wake anapewa uhamisho. Anachukuliwa na Shirika la kidini la
Hakikisho la Haki na Utulivu na kupelekwa kwenye makao ya watoto mayatima ya ya Jeshi la
Wajane wa Kristu.

1.1.8 Sura ya Nane

Ni alasiri. Mwangeka ashaoanana na Apondi. Wambo nyumbani wakitazama watoto wao


wakiogelea kidimbwini. Watoto hawa ni Sophie, Ridhaa na Umulkheri. Ridhaa ndiye mtoto wa
Mwangeka na Apondi. Wamempa jina la babake Mwangeka. Sophie ni mtoto wa Apondi na
marehemu mumewe Mandu aliyefia ughaibuni akidumisha amani. Mwalimu Dhahabu anawaomba
wazazi hawa hasa rafiki wake Apondi kumchukua na kumfadhili Umu. Umu ni binti yake Mzee
Kaizari ingawa hamna anayebaini hili kwa sasa.

Mwangeka anakutana na Apondi kwenye warsha iliyoandaliwa kuhusu jukumu la vikoso vya
askari katika kudumisha usalama, amani na maridhiano. Apondi alikuwa mmoja wa wasilishaji.
Alikuwa akifanya kazi katika Wizara ya Vijana na Masuala ya Kijinsia. Mwangeka anavutiwa na
uwasilishaji murua wa Apondi.

1.1.9 Sura ya Tisa

Dick yumo kwenye uwanja wa ndege. Amesimama katika mlolongo mkubwa wa watu wanaongoja
kukaguliwa kwenye afii za forodha. Dick ameratibiwa kusafiri ughaibuni kwa ndege ya asubuhi
kwenda kununua bidhaa za biashara yake. Ameamua kubadilika na kuanza kujitegemea. Dick

7
anakumbuka alivyoanza kusafiri kwa ndege. Alikuwa amelazimishwa kulangua dawa za kulevya
na mwajiri wake kwa lakabu, Buda. Dick alikuwa ameuzwa kwa tajiri huyu na kijakazi Sauna
akiwa na umri wa miaka kumi. Siku za mwanzo mwanzo, Dick alikataa kushiriki walakini
akaridhia baadaye shingo upande maadam tajiri huyu alitishia kumsingizia wizi. Adhabu ya wizi
ilikuwa kifo. Dick anakumbuka kisa cha rafiki yake Lemi alivyouawa na umma kwa kutuhumiwa
wizi. Dick aliamua kuacha biashara hii haramu na kuanzisha biahara ya kuuza vifaa vya umeme.
Hata ameshasomea Teknolojia ya Mawasiliano ya Simu. Ameshapanua mawanda ya biashara
yake. Anasafiri ng`ambo kununua bidhaa anazouzia mashirika yanayotoa huduma za mawasiliano.

Kisadfa, Umulkheri naye alikuwa nyuma yake katika foleni hii akisindikizwa na familia yake
mpya kwenda ng`ambo kwa shahada yake ya Uhandisi katika Masuala ya Kilimo. Dick anasikia
sauti ya Mwangeka ikimwarifu kuwa ndege yake ilikuwa tayari.Dick na Umu wanakutana na
kukumbatiana kwa furaha huku wasafiri wengine wakiwatazama kwa mshangao. Wanasafiria
ndege moja.

1.1.10 Sura ya Kumi

Ridhaa ameamua kuhamia mtaa wa kifahari wa Afueni kuyajenga upya maisha yake. Shamsi kwa
lakabu Bwana Dengelua anapita usiku wa manane huku akiimba. Wimbo huu umejaa masimango
kwa wanaomsikiliza maadam hawakumwauni yeye na babake walipokuwa wakidhulumiwa.

Selume ameajiriwa kama Muuguzi Mkuu naye Kaizari akaajiriwa kama Afisa wa Matibabu katika
kituo cha afya cha Mwanzo Mpya kilichokuwa kimejengwa na Ridhaa. Selume amemaliza zamu
yake hivyo anamwarifu muuguzi mwenzake Meko hali ya wagonjwa. Kuna waliojeruhiwa
vichwani,waliokufa kutokana na unywaji pombe, kuna Tuama aliyemwaga damu baada ya
kupashwa tohara kwa hiari yake, na Pete aliyejaribu kujitoa uhai kwa maana alikuwa na mimba
ya tatu.

Pete anasimulia dhiki za maisha yake. Baada ya kukanwa na wazazi wake analelewa na nyanyake.
Anapovunja ungo, mama yake na ndugu zake wanamuoza kwa lazima kwa Mzee Fungo na
kukatisha masomo yake. Pete anazalishwa na mzee huyu. Anamtoroka Mzee huyu hadi mjini na
kuajiriwa katika kampuni ya Patel ya kushona nguo. Anahamia kwa Nyangumi ambaye
anamfurusha baada ya mke wake wa kwanza kumrudia. Anajihusisha na uuzaji wa pombe
anapobakwa na mmoja wa walevi hivyo kutamauka na kutaka kujitoa uhai.

8
1.1.11 Sura ya Kumi na Moja

Polisi wanafika mafichoni ya Bi. Kangara kuja kuwakamata Sauna na bibi huyu. Bi Kangara
amekuwa na mtandao wa kuiba watoto na vijana. Wasichana wanapelekwa madanguroni nao
vijana kuuziwa matajiri kwa lengo la kushiriki ulanguzi wa dawa za kulevya. Sauna alikuwa
amewaiba Dick na Mwaliwa (nduguze Umu na watoto wa Lunga na Naomi). Dick anauzwa kwa
tajiri kwa jina Buda kushiriki uuzaji wa mihadarati. Mwaliko anabaki kwa Bi. Kangara ili
akomazwe.

Sauna haipendi kazi hii. Anawazia kiini cha ukatili wake. Anaeleza kuhusu makuruhu aliyowahi
kufanyiwa. Sauna aliwahi kubakwa na Bwana Maya, babake wa kambo. Mama Sauna anamhimiza
kumsamehe baba huyu asije akamwahibisha, Mama Sauna anamsaidia kuiavya mimba. Mama
Sauna ni mjane wa Bwana Kero. Sauna anatamauka. Anaanza kufanya kazi duni kwa mfano katika
machimbo ya mawe. Wanakutana na Bi Kangara anayemwingiza katika biashara hii haramu. Polisi
wanawafikisha mahakamani wanakoshtakiwa. Mwaliko anapelekwa katika kituo cha polisi cha
Benefactor wanakofika Mwangem na Neema kumpanga kama mwanao.

1.1.12 Sura ya Kumi na Mbili

Mwaliko ameajiriwa katika kampuni ya magazeti ya Tabora. Ameshahitimu kwa shahada ya


uzamili katika Taaluma ya Mawasiliano. Mwaliko anamwandalia babake mlezi, Mwangemi,
sherehe ya kuzaliwa kwake katika hoteli ya Majaliwa. Inasadifu kwamba, Mwangeka na Apondi
wamemwandalia Umulkheri (Dadake Mwaliko) hafla hiyo hiyo katika hoteli hii. Dick alipokelewa
na wazazi hawa wapya wa Umu ambao wamempa mshawasha hadi akapanua biashara yake.
Mwaliko anapata fursa ya kupatana na ndugu zake Umu na Dick baada ya kutengana kwa muda
mrefu. Kukutana kwa binamu hawa wawili, Mwangeka na Mwangemi kunamkumbusha
Mwangeka siku za utoto namna alivyoweza kuvumbua gari la kienyeji, wakapiganisha majogoo
na adhabu waliyopata kwa kujaribu kumuiga na kumtania babu Msubili.

Wazazi hawa wanawahimiza Umu, Dick na Mwaliko kuanza kumsaka mama yao Neema
aliyewatoroka. Kile hawakujua ni kwamba mama yao alihamia mjini alikoajiriwa na Bwana
Kimbaumbau katika biashara ya kuuza nguo kuukuu. Bwana huyu anamfuta Naomi kazi kwa
maana alikataa kushiriki mapenzi naye. Naomi alijutia kitendo cha kuiacha familia yake. Aliwahi
kurudi Mlima wa Simba asiwapata hata akawasaka katika vituo vya polisi. Kwa sasa Naomi

9
amefungua kiafisi katika chuo Kikuu cha Mbalamwezi anakopigia wasomi chapa na kuisarifu
miswada yao. Watoto hawa wanakubaliana kumsamehe na kumtafuta mama yao.

1.2 MAUDHUI

1.2.1 Athari za vita vya wenyewe kwa wenywe

i. Jamii mbili zinapigana kwa sababu za misimamo ya kisiasa, Mwekevu anachaguliwa


kutoka jamii ya Waombwe lakini jamii ya Anyamvua haimtaki.
ii. Vita vinazua uharibifu wa mali.Nyumba ya Ridhaa inachomwa na kubaki vifusi.magari
yanachomwa.
iii. Mauaji yanatokea. Mke wa Ridhaa na wanawe wanauawa.
iv. Uporaji wa mali. Waandamanaji walipora maduka ya Kihindi na Kiarabu kabla ya
kunaswa na polisi uk.20.
v. Misafara ya wakimbizi wakihama makwao na kuyaacha mali yao nyuma.
vi. Mauaji ya watu na wanyama. Mizoga imetapakaa kila mahali. uk.20.
vii. Uharibifu wa mali, mimea na mazingira.
viii. Vijana kuchoma magari.uk21
ix. Ubakaji- Lime na Mwanaheri wanabakwa familia na wapinzani wa Mwekevu familia
yao ikitazama.uk25

1.2.2 Mgogoro wa ardhi

i. Wakoloni na walowezi walinyakua ardhi katika maeneo yenye rotuba na kuwaachia


Waafrika kusiko na rotuba.
ii. Jamii za Anyamvua na Waombwe zinapigana kwa sababu ya mashamba.
iii. Wanyamvua wanafurushwa na wenzao kwa sababu ya ardhi.
iv. Wanajamii wanahamishwa kutoka msitu wa Mamba licha ya kuwa na hatimiliki za
ardhi

1.2.3 Uhifadhi wa mazingira

i. Kuna wanaharakati wa kutunza mazingira.Lunga anashiriki katika hamasisho la


wanafunzi shuleni kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.

10
ii. Kuna juhudi za kupanda miti na kubadilisha mazingira.Ridhaa anachangia upanzi wa
miti katika Eneo la Heri na kubadilisha sura yake.
iii. Serikali inaondoa umma katika msitu wa Mamba ili kuepusha uharibifu wa mazingira.
iv. Lunga anahimiza wanajamii kuepuka kulima karibu na misitu kuepuka kuchafua
mazingira.
v. Lunga analalamika kuwa wanyama wamenyang’anywa makao yao na binadamu
anayelenga kupanua kilimo na ujenzi.
vi. Kuna kuundwa kwa vyama vya kutunza mazingira. Lunga anaasisi chama cha watunza
mazingira shuleni.

1.2.4 Ukosefu wa kazi

i. Vijana wananuia kuleta mabadiliko katika jamii ili kubuni nafasi za kazi. Maandamano
ya vijana yanalenga kuleta mabadiliko katika jamii.
ii. Kazi zinawaendea wale walio na uwezo wa kuhonga. Shamsi anakosa kazi kwa sababu
hakuwa na uwezo wa kuhonga.
iii. Vijana wanafunzu vyuoni na shahada mbalimbali lakini hawapati kazi.24.
iv. Kusoma hakumhakikishii mtu kazi. Shamsi amesoma lakini hana kazi ya thamani.

1.2.5 Utamaduni

i. Kuna ndoa za wake wengi. Babu Mshubili anaoa wake kumi na wawili.
ii. Wasichana bado wanapashwa tohara. Pete anapashwa tohara kabla ya kuozwa Fungo.
iii. Wasichana wanaozwa kwa nguvu. Pete anaozwa kwa Fungo kama mke wa nne na
mamake.
iv. Wanawake hawapewi nafasi za kuingoza jamii, wanaume wanatawala. Vita vinazuka
Mwekevu anaposhinda, Wanaume hawaamini wanaweza ongozwa na mwanamke.
v. Wanawake wanahesabiwa kama mali. Babu Mwimo anaoa wake wengi kwa kuwa
inaaminika wake wengi ni ishara ya utajiri.
vi. Wakoloni wanavunja mpangilio na sera ya umiliki wa ardhi wa mwafrika kitamaduni.
Waafrika walilima popote bila kubinafsisha ardhi.
vii. Wanawake wanaangaliwa kama wasiomiliki au kurithi mali.

11
viii. Adhabu ya kiboko kama ulivyo utamaduni wa kiafrika inasisitizwa. Babu Mwimo
Mshubili anawaadhibu Mwangemi na Mwangeka kila wanapokosea.
ix. Kazi ya mwanamke ni jikoni. Babu Mwimo anaandaliwa uji na mwanamke lakini
anahudumiwa na mwanamume. Mwanamke haruhusiwi kumhudumia mwanamume.
x. Kesi za jamii zinatatuliwa katika mabaraza ya kijadi. Babu Mwimo anachukua muda
mrefu kutatua kesi za kijamii katika tarafa ya Heri.
xi. Wanajamii wanapokufa kunafanywa viviga, Dede anapokufa kunakuwa na viviga
kama vya kulia, kujishika kichwa, kuzunguka ua..nk.

1.2.6 Ulanguzi wa binadamu

i. Sauna na Bi. Kangara wanaendesha biashara hii, Bi. Kangara ana mtandao mrefu wa
biashara ya binadamu
ii. Dick anauzwa kwa Buda anakoshirikishwa katika ulanguzi wa dawa za kulevya
iii. Wasichana wanauzwa katika madanguro ili waendeleze biashara ya ukahaba.
iv. Wengine wanauzwa ughaibuni kama watumwa wanakofanyishwa kazi ngumu.

1.2.7 Madhila ya wakimbizi

i. Ukosefu wa chakula. Wakimbizi wanalazimika kula mimea na mizizimiti. Ridhaa


analizimika kula mizizimiti katika kambi ya wakimbizi.
ii. Magonjwa yanayotokana na uchafu na hali ya hewa.Wakimbizi wanashikwa na homa
ya matumbo kwa sababu ya maji machafu.
iii. Njaa inatishia kuwaangamiza. Wakimbizi wanategemea chakula cha msaada,
iv. Vifo vya watoto-Kitindamimba wa Kairu anakufa kwa sababu ya njaa wanapokuwa
katika msafara wa wakimbizi.
v. Ukosefu wa huduma bora za kijamii. Kambini hakuna vyoo wanajamii wanalazimika
kuchutama majanini.
vi. Msongamano katika vibanda vidogo. Akina Kairu wanalazimika kutumia chumba
kimoja familia nzima, miko inavunjwa.

12
1.2.8 Jaala

i. Jaala inalazimu wanajamii kuhama. Bbabu Mwimo analazimika kuhamishia wake


wake wawili wa mwisho Msitu wa Heri kwa sababu ya uhaba wa nafasi.
ii. Walioachana wanaletwa pamoja na jaala.Dick na Umu wanakutanishwa na maumbile.
Wanakutana kisadfa.
iii. Mwaliko anakutanishwa na familia yake na nguvu za maumbile, haikupangiwa.
iv. Apondi na Mwangeka wanakutanishwa na kufunga ndoa kwa nguvu za kijaala.
v. Lunga analazimika kuharibu msitu aendeleza kilimo baada ya kufutwa kazi hakupanga
vile.

1.2.9 Umaskini

i. Waafrika wanajikuta katika umaskini katika majilio ya wakoloni. Mashamba yao


yananyakuliwa na kufanywa maskwota.
ii. Vijana wanaandamana kupinga utawala mbovu ulioleta umaskini.Wanaume
wanadhani kuchagua wanawake ni kuwazika katika ukata zaidi.
iii. Umaskini unaleta maovu ya kijamii kama upikaji pombe haramu, ukahaba na uhalifu.
Shamsi analewa kujipurukusha na umaskini wake.
iv. Matajiri wanafukarisha maskini zaidi. Babake Shamsi ananyang’anywa shamba lao na
tajiri.
v. Uoga wa maskini unawafukarisha zaidi. Mabavu anachukua shamba la maskini nao
wanafya ndimi zao wasimuulize.
vi. Umaskini unasababishwa na michafuko ya kijamii. Ridhaa na Kaizari wanafukarika
baada ya mali yao kuharibiwa wakati wa vita vya kijamii.

1.2.10 Ndoa

i. Kifo kinatenganisha wanandoa. Ridhaa anatenganishwa na mkewe Terry.


ii. Umaskini unavunja ndoa. Naomi anatoroka kwa sababu ya mabadiliko ya kimaisha ya
Lunga.
iii. Kuna ndoa za kulazimishwa.Pete analazimishwa na mamake na wanjomba wake
kuolewa na mzee Fungo.

13
iv. Katika ndoa kuna kutoaminiana.Tenge anazini na wanawake wengine wakati Bi. Kimai
yuko mashambani.
v. Ndoa zinakabiliwa na shida za watoto.Mwangemi na Neema wanalazimika kumpanga
mtoto Dick.
vi. Baada ya ndoa kusambaratika wahusika wanaanza upya. Mwangeka anamwoa Apondi
baada ya kifo cha Lily Nyamvula.
vii. Jamii zinapinga ndoa za makabila. Kangata anakatazwa kumwoza Lucia kwa jamii ya
Waombwe kutokana na imani za kijamii.
viii. Katika ndoa kuna kusalitiana. Annette anamwacha Kiriri na kuhamia ng’ambo,
anaisaliti ndoa yao.

1.2.11 Utengano wa kijamii

i. Jamii zinatengana kwa sababu ya mashamba. Jamii ya Waombwe na Wanyamvua


zinatengana na kufarakana kwa sababu ya migogoro ya mashamba.
ii. Kuna utengano wa familia kwa sababu za kikazi. Mwangeka anatengana na Mkewe
Mwangeka anapoenda kudumisha amani nchi ya nje.
iii. Kifo kinatenganisha familia. Ridhaa anatenganishwa na mkewe Terry na kifo.
iv. Familia zinatenganishwa na hali. Mwangeka anatenganishwa na babake na familia
yake kwa sababu za kikazi.
v. Kuna utengano wa kitabaka. Jamii ya Msitu wa Mamba inakua na kuwa na matabaka
mawili. Maskini na matajiri.

1.2.12 Mauti

i. Kuna vifo vinavyotokana na mauaji.Tila, Terry na Beka wanauliwa katika mizozo ya


kijamii.
ii. Vifo vingine ni vya kutuhumiwa. Lemi anapigwa kitutu kwa kusingiziwa kuiba rununu.
iii. Vifo vingine ni vya maradhi. Lunga anakufa kwa sababu ya shinikizo la damu kwa
upweke wa kuachwa na Naomi.
iv. Kuna vifo vya kujiua. Subira anajiua kutokana na mateso ya mama mkwe.
v. Wengine wanakufa kifo cha kawaida. Kangata na mkewe wanakufa kifo cha kawaida.

14
1.2.13 Ukoloni Mamboleo

i. Mashamba ya kikoloni yanatwaliwa na waafrika binafsi.Mashamba ya Theluji Nyeusi.


ii. Hata baada ya mkoloni kuondoka waafrika wamefanywa maskwota. Wenyeji
wamefanywa maswota na Myunani.
iii. Waafrika wanawekwa mahali pamoja na kuishi kwa ujamaa.Walowezi wametwaa
maekari ya ardhi.
iv. Vijana wanauawa kinyama wanapoandamana kujiondoa kutoka kwa utawala wa
kikoloni. Wanapigania uhuru wa tatu.uk23.
v. Madini yanachimbwa na kampuni za mataifa ya nje. Tila analalamika kuwa kampuni
za nje zinachimba madini na kuajiri wenyweji kwa mshahara duni faida kubwa inaenda
nje ya nchi.

1.2.14 Nafasi ya mwanamke

i. Imani za kijamii zinalenga kumkandamiza mwanamke asishiriki katika maendeleo ya


kijamii. Wanaume kama vile Tetei wanasema kuwa jamii yao haiwezi ikaongozwa na
wanawake.
ii. Historia na visakale vinatumiwa kumchora mwanamke kama dikteta mkandamizaji. Kisa
cha mwanamke anayewakandamiza wanaume enzi za istimari.
iii. Wanawake wanajitolea kuingilia siasa na kumkabili mwanamume. Bi. Mwekevu
anachaguliwa kama kiongozi wa Wahafidhina kwa sababu ya historia yake ya maendleo.
iv. Mwanamke anayajali masalahi ya jamii. Mfano Bi. Mwekevu anachaguliwa na wanawake
na wanaume kwa sababu ya kuwainua raia alipokuwa mkurugenzi wa Shirika la
Chemichemi.uk.18.
v. Mwanamke anakiuka jadi na kutawala. Mwekevu anajitoza siasani na kuwabwaga
wanaume.
vi. Mwanamke ni mwajibikaji. Selumu anahudumu kama muuguzi, Apondi anatoa hotuba
kuhusu uwajibikaji wa vikosi vya usalama.
vii. Mwanamke anakandamizwa na mwanamke mwenzake.Sauna anaingizwa katika biashara
haramu na Bi. Kipanga, Sauna anaingiza wasichana katika ukahaba.

15
1.2.15 Mabadiliko
i. Vijana wanadai wanataka mabadiliko.Kijana mwenye shati lililoandikwa Hitman
analalamikia hali duni ya maisha ya vijana na kusema wakati wa mabadiliko umewadia.
ii. Jamii inawachagua wanawake kushika usukani wa utawala kwa sababu ya ndoto zao za
maendeleo. Mwekevu anachaguliwa kinyume na matarajio ya wengi.
iii. Wanafunzi katika shule mfano Tila anamwambia Ridhaa kuwa wakati wa mabadiliko
umefika. Ridhaa hakubaliani na hili lakini inambainikia baada ya machafuko ya
kikabila.uk.38-44
iv. Mpinzani wa Mwekevu anakubali kushindwa baada ya kura kuhesabiwa tena. Anaisihi
jamii kudumisha amani. Anabadilisha msimamo wake wa hapo awali.
v. Vijana wanatambua kuwa wanatumiwa na viongozi wenye tamaa kama vilipuzi vya
kuharibu mshikamano wa kijamii na kusitoisha mapigano.uk49.

1.3 WAHUSIKA

1.3.1 Ridhaa

i. Mwenye bidii- Ni dakatari maarufu anayefanya kazi kwa bidii kuiokoa jamii.Anajenga
kituo cha afya cha Mwanzo Mpya kuikoa jamii yake.
ii. Mwenye mali-Anamiliki majumba ya kifahari yanayobomolewa katika mtaa wa
Tononokeni. Ana jumba la kibiashara analolipangisha wafanyabiashara.
iii. Mwathiriwa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe-Anapoteza aila yake pamoja na
mali yake kupitia vita vya kikabila.
iv. Msomi- Amesoma hadi kufikia kiwango cha kuwa daktari. Ana shahada ya uzamili
katika taaluma ya ufisadi.
v. Mwanaharakati- Anawahamasisha wakimbizi katika Msitu wa Mamba kujenga vyoo
vya mashimo kuzuia mchipuko wa maradhi ya kipindupindu.
vi. Mshirikina- Anaamini kuwa milio ya bundi na kereng’ende ilikuwa ikibashiri
kuvamiwa kwao.

16
1.3.2 Mwangeka

i. Msomi – amesoma sana kiwango cha kuwa mhandisi, amesomea ng’ambo. Anatumwa na
serikali ya nchi yake katika Mashariki ya Kati kudumisha amani.
ii. Mzalendo- Anajiunga na idara ya jeshi ili kuilinda nchi yake. Anaenda ughaibuni na jeshi
la umoja wa mataifa kuhifadhi amani Mashariki ya Kati.
iii. Mwenyeutu-anajitolea kumlea mtoto wa kupanga Umulkheri. Anamlea na kumwonyesha
mapenzi ya mzazi na kufanikisha makutano yake na Dick na Mwaliko.

1.3.3 Mwimo Mshubili

i. Mtamaduni Ana wake kumi na wawili, anaamini mtoto anafaa kukosolewa kwa
kutumia kiboko. Mwangeka na Mwangemi wanaadhibiwa na yeye kila wakoseapo..
ii. Mwenye maarifa- anafahamika kote kwa ujuzi wake wa kutatua na kuamua kesi
katika jamii. Alikuwa hakimu wa kienyeji aliyefahamika kote katika taarafa ya Heri.
Kesi zilizoyashinda mabaraza yote ya kijadi zinaamuliwa na yeye.uk.183.
iii. Mshirikina- anaamini kuwa mwanamume kumwona mwanamke asubuhi ni nuksi na
hawezi akafanikiwa kwa alitakalo. Hawezi akahudumiwa na mwanamke, anapelekewa
uji chumbani mwake na wanaume.uk184
iv. Mbabedume- Anahudimiwa na wanaume, haruhusu mwanamke kumletea chakula
chumbani.Anaamini kumwona mwanamke asubuhi ni ishara kuwa hatafanikiwa kwa
alitakalo.
v. Mwenye bidii- Anailisha familia ya wake kumi na wawili na watoto
ishirini.Anawapeleka watoto wake shuleni licha ya kuwa na familia kubwa.

1.3.4 Ndugu Kaizari

i. Mwathiri wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.Anapoteza mali yake kupitia vita vya
kikabila. Analazimika kuiacha ardhi yake katika Msitu wa Heri kwa sababu za
machafuko ya kikabila.
ii. Mkimbizi- yeye ni sehemu ya wakimbizi wanaotaabika katika Msitu wa Mamba.
Analazimika kuishi maisha ya kiwango cha chini katika kambi hii licha ya kuwa
anatokana na tabaka la juu.Anaona aibu kutumia sandarusi ya kupeperushwa kama
choo.

17
1.3.5 Selume

i. Mvumilivu- anapitia mateso mengi ya kifamilia kama vile kusimangwa kwa kuwa
anatokana na jamii ya Waombwe.
ii. Mwenye bidii- Anafanya kazi kwa bidii ili kuwahudumia wagonjwa kwenye hospitali
mpya ya Mwanzo Mpya inayoanzishwa na Ridhaa.
iii. Msomi – amesoma kiwango cha kuwa muuguzi. Katika hospitali ya Ridhaa anachukua
nafasi ya Mkuu wa wauguzi.
iv. Mwathiriwa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe- Anafukuzwa na mmewe kwa
sababu ya kutofautiana naye kimsimamo wa kisiasa.

1.3.7 Kangata

i. Ni mwenye bidii- analima ekari nyingi za mashamba na kuzalisha kila aina ya chakula.
ii. Mchafuzi wa mazingira- Anachangia kuangamiza msitu wa Mamba kwa tamaa ya
kutaka kuzalisha chakula.
iii. Mwenye msimamo dhabiti- anapinga wazo la jamaa na ami zake la kutomwoza Lucia
kwa jamiiya Waombwe. Anakataa kufuata ushauri wao na kuishia kumwoza Lucia kwa
jamii ya Waombwe. Ndio hii inaleta mshikamano wa jamii hizi mbili.
iv. Mpinga mila potovu- Anaenda kinyume na imani ya jamii kuwa kumwelimisha
mwanamke ni kupoteza pesa na mali. Anawaelimisha binti zake wote, Lucia anaibukia
kutononoka si haba. Uk 67.

1.3.9 Kiriri

i. Ni mhisani- anampa Kangata na familia yake hifadhi. Anawasomesha watoto wa


Kangata kiasi cha wao kujitambulisha na yeye.
ii. Mkiwa- anateseka na kushikwa na kihoro baada ya kuachwa na mkewe anayehamia
ughaibuni.
iii. Mtambuzi- anafahamu kuwa wanaohamia mataifa ya nje kwa madai ya kutafuta kazi
huwa wanajidhalilisha wenyewe kwa kuwatumia wazungu kwa mishahara na kazi
duni.

18
1.3.10 Annete

i. Mbinafsi- anamwacha Kiriri peke yake na kuhamia ng’ambo kuishi na watoto wake
ii. Mwathiriwa wa kasumba ya kikoloni- anaichukia nchi yake kuwa haiwafai wafanyikazi
wake.
iii. Mwenye tamaa- anahamia ng’ambo ili kupata kazi nzuri na kuishi maisha ya raha, anaiasi
kazi yake kwa sababu ya tamaa.

1.3.11 Lunga

i. Mwenye bidii- ni mkulima tajika katika msitu wa Mamba, analima maekari ya ardhi
na kuzalisha vyakula vya aina mbalimbali. Yeye ni mkulima bora aliyelakabiwa
Mukulima Namba Wani.
ii. Ni msomi- Yeye ni Afisa wa Kilimo Nyanjani, anawashauri wakulima namna ya
kulima kilimo kisichohatarisha mazingira.
iii. Ni hatibu bora- Akiwa shuleni alitoa hotuba za kuvutia kuhusu umuhimu wa kulinda
mazingira.
iv. Mwenye misimamo mikali- anapinga kwa dhati msimamo wa wakubwa wa Shirika
la Maghala ya Nafaka wa kutaka kuingiza mahindi yenye sumu nchini. Anafutwa kazi
kwa msimamo huu.uk.70.Anashikilia kuwa Lucia Kiriri ataolewa katika uko wa
Waombwe licha ya pingamizi za ami zake.
v. Mwanaharakati wa mazingira- Lunga alikuwa amirijeshi wa kulinda mazingira.
Anashiriki katika juhudi za kutunza mazingira tangu akiwa shuleni.Akiwa shuleni
alikuwa mwasisi wa Chama cha Watunza Mazingira Wasiokuwa na Mipaka.
vi. Mchafuzi wa mazingira- Lunga anabadilika kutoka mhifadhi tajika wa mazingira hadi
mharibifu mkuu baada ya kufutwa kazi. Analaumu kufutwa kazi kwake kuhusu
mabadiliko yake.
vii. Hatibu bora- Alihutubu kila Ijumaa kwenye gwaride alipokuwa shuleni kwa
mihemko.Anawahamasisha walimu na wanafunzi wenzake kuhusu umuhimu wa
kutunza mazingira. Anakashifu tabia ya binadamu ya kukata miti na kuwanyang’anya
wanyama makao yao.uk69.

19
viii. Mwenye huzuni- Lunga anakufa kutokana na kihoro cha kuachwa na mkewe Naomi
pamoja na kadhia ya kuhamishwa msitu wa Mamba. Anakufa kutokana na shinikizo la
damu.

1.3.12 Umulkheri/Umu

i. Msomi- anasoma kiasi cha kuwa na shahada ya uzamili baada ya kupangwa na familia ya
Mwangeka na Apondi.
ii. Mwenye utu- Anamsaidia mtoto wa mtaani kwa shilingi mia mbili anapokuwa akielekea
kanisani na mamake.
iii. Mshauri bora- anamsihi kijana wa mtaani atumie pesa zake asije akazitumia kununua
gundi.
iv. Mlezi bora- anawalea Dick, na Mwaliko vizuri baada ya kifo cha babake. Dick
anakumbuka kauli ya Umu kuwa atawalea kwa viganja vyake .Anamlea Mtoto wa Apondi
Sophia na kumsaidia kuzidhibiti hasira zake. Apondi anasifu sana kwa hili.
v. Ni mwajibifu- anaripoti kupotea kwa Dick na Mwaliko katika kituo cha polisi.
vi. Mwathiri wa vita vya wenyewe kwa wenyewe- anaipoteza familia yake kutokana na
machafuko ya kijamii, anaishia kulelewa na shirika la kijamii na mwisho kupangwa na
familia ya Mwangeka.

1.3.13 Mwalimu Dhahabu

i. Ni mtambuzi- anatambua kuwa Umu ana mawazo yanayomwandama ndio maana


hafuatilii masomo.
ii. Mshauri bora- anamshauri Umu kusahau yaliyompitikia na kuangalia mbele
kimasomo.
iii. Mhisani- Anamsaidia Umu kujiunga na familia ya Apondi.

1.3.14 Naomi

i. Mwepesi wa kukata tamaa- Anapotea nyumbani baada ya familia ya Lunga


kufukuzwa msitu wa Mamba.
ii. Mwenye majuto- Anajutia kumwacha mumewe wakati alimhitaji zaidi baada ya
kufutwa kazi na Kimbaumbau.

20
iii. Mmwenye kujirudi- anatambua makosa yake ya kuacha watoto na mmewe na kuanza
kuwatafuta.
iv. Mwenye bidii- anaanza kazi ya uhazili kwa tajiri Kimbaumbau ili ajikwamue kutokana
na umaskini
v. Mwenye misimamo mikali- anakataa kabisa kuingia katika mtego wa Kimbaumbau
mwajiri wake. Anafutwa kazi baada ya kukataa kushiriki mapenzi naye.
vi. Katili-Anaiacha familia yake wakati inamhitaji zaidi. Anamwacha Lunga mumewe na
watoto watatu bila kuzingatia malezi yao. Lunga anakufa kwa kuachwa na mkewe.

1.3.15 Sauna

i. Mlanguzi wa watoto- Anawauza watoto wa watu kwa matajiri watumike kama


watumwa. Anaingiza wengine kwenye biashara haramu ya dawa za kelevya na
uasherati.
ii. Mnafiki- Anajifanya mlezi mzuri ili kujiaminisha kwa wazazi wa watoto ili apate
nafasi ya kuiba watoto.
iii. Mwenye majuto- Anajikuta katika mawazo mengi kuhusu maisha yake, anajuta
kushiriki biashara haramu, analaumu jaala kwa mabadiliko yake.
iv. Mwathiriwa wa biashara haramu- Anakamatwa na polisi na kufungwa kwa makosa
ya kukiuka haki za kibinadamu.Anawauza watoto kama makahaba, walanguzi wa dawa
na wafanyakazi watumwa katika mataifa ya nje.

1.3.16 Dickson

i. Mwathiriwa wa biashara ya watoto- anauzwa kwa tajiri Buda ili kushiriki uuzaji wa
dawa za kulevya.
ii. Msomi – anafanikiwa kutoroka kwa tajiri wake na kubadilisha maisha yake, anasomea
Taaluma ya mawasiliano ya Simu.
iii. Mwenye bidii- anapobaleghe, anabadilisha maisha yake na kuishia kuwa
mfanyabiasha maarufu wa vifaa vya mawasiliano. Anajisomesha kwa pesa
anazodunduiza.

21
1.3.17 Kairu

i. Mwathiriwa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe-Anasimulia masaibu


waliyokabiliana nayo baada ya kufurushwa kwao baada ya vita vya kikabila. anaelezea
jinsi walivyompoteza ndugu yao, malazi duni kambini
ii. Mvumilivu- anavumilia masaibu yote anayoyapitia tangu kufukuzwa nyumbani, kifo
cha kitindamimba wao, hali ngumu ya maisha kambini njaa na umaskini. “Tulivumilia
tukawa tunaishi kwa tumaini tukidhani hali itatengenea,…” uk.92.
iii. Mshauri bora- Anamsihi Umulkheri kuyavumilia mazingira magumu katika shule ya
Tangamano kwa kusimulia masaibu ambayo yeye mwenyewe alipitia. “Vumilia,
mwenzangu. Zingatia masomo yako…”uk92
iv. Msomi-Licha ya ufukara wa mamake anahudhuria shule kuendeleza masomo yake.

1.3.18 Mwanaheri

i. Mghani mashairi- Anajaribu kupalilia kipawa chake cha kughani mashairi


mepesi.uk94.
ii. Msomi-Anaendeleza masomo yake katika shule ya Tangamano licha ya misukosuko
ya kifamilia.
iii. Mvumilivu- Anapitia masaibu mengi ya kijamii kama kubakwa, kufurushwa
nyumbani wakati wa machafuko ya kikabila na kufiwa na mamake lakini bado hajakata
tamaa.

1.3.19 Zohali

i. Mwathiriwa wa mimba za mapema-Anapata mimba akiwa kidato cha pili na


kufukuzwa shuleni.
ii. Mdanganyifu- Anamdanganya Mtawa Pacha kuwa yeye ni yatima ambaye wazazi
wake walikufa miaka minane iliyopita. Anamwambia Mtawa Pacha kuwa alihamia
mtaani na ndugu zake baada ya kupokwa urithi na jamaa za wazazi wake.

1.3.20 Fumba

i. Mpotovu wa maadili- Ni mwalimu anayejihusisha kimapenzi na mwanafunzi wake.

22
ii. Mwenye mapuuza- anapuuza malezi ya mtoto wake Zohali, anamwachia mamake
amlee mtoto wake.Hatumi pesa za masurufu kwa nyanyake Zohali.

1.3.21 Chandachema

i. Mwathiriwa wa ajira ya watoto-Anaanza kuchuma majanichai katika mashamba ya


chai ya Shirika la Chai la Tengenea na kupata malipo madogo madogo akiwa darasa la
tano.
ii. Mwenye bidii- anafika katika shamba la Shirika la Chai la Tengenea ili aendeleze
elimu yake na kupata kibarua cha kumwezesha kuyakidhi mahitaji yake.
iii. Mvumilivu-anavumilia masaibu mbalimbali. Analelewa na nyanya ambaye anaaga
dunia na kumwacha mikononi mwa mke wa jirani, amelala kwenye majani chai na
kuchuma majanichai akiwa na umri mdogo.
iv. Msomi-Anakimbilia shamba la majanichai kwa sababu anajua huko kuna shule, alitaka
kuendeleza masomo yake.
v. Mtambuzi- Anafahamu matatizo yanayowaandama wafanyikazi katika mashamba ya
matajiri na walowezi kama vile kuhamishwahamishwa na hali duni ya makazi yao.

1.3.22 Apondi

i. Mhisani- Anamlea Umu kama mtoto wake na kumsomesha.


ii. Hatibu bora- anatoa hotuba nzuri katika warsha ya jukumu la walinda usalama katika
kudumisha amani.
iii. Msomi- Amesoma hadi kuwa kiwango cha kufanya kazi katika Wizara ya Vijana na
Masuala ya Jinsia.

1.3.23 Tindi

i. Mpenda raha- anakesha na Lemi na kushiriki katika densi ya kisasa ambayo


inahusisha upotokaji wa kimadili.
ii. Mtovu wa maadili- anashiriki katika kunengua na kucheza densi chafu.
iii. Mkaidi- anakaidi agizo la mamake kurudi nyumbani mapema baada ya kumaliza
shughuli mjini.
iv. Mbinafsi- Anamwacha Lemi mikononi mwa umma anapoona umma unawaandama.

23
1.3.24 Shamsi

i. Mghani bora- Anapolewa anaghani tungo ndefu zinazosimulia wasifu wake.


ii. Msomi- Katika utungo wake anaakisiwa kama msomi aliyekosa kazi.
iii. Mlevi- Anapindukia kuwa mlevi chakari kwa kuandamwa na maisaibu ya maisha.

1.3.25 Pete

i. Katili- Amejaribu kuavya mara kadhaa, amelazwa hospitalini kutokana na jaribio la


kujitoa uhai.
ii. Mwathiriwa wa ndoa za mapema- Anaozwa na mamake kwa nguvu kwa Mzee
Fungo aliye na wake watatu.
iii. Mwathiriwa wa malezi duni- Analelewa na nyanyake baada ya kukataliwa na babake
wa kambo.
iv. Mwenye majuto-Anajutia hali duni ya maisha amekuwa akiishi. Anajuta kuishi
maisha yasiyokuwa na mwelekeo na kuapa kuyabadilisha.

1.4 MBINU ZA LUGHA

1.4.1 Kinaya

i. Ni kinaya kwa Mzee Kedi kushiriki katika kuiangamiza familia ya Ridhaa ilhali Ridhaa
alikuwa ameisaidia familia ya Mzee Kedi kwa kusomesha wapwa wake wawili.
ii. Ni kinaya kwa vijana kukaidi walinda usalama licha ya kuona wenzao wakifyatuliwa risasi
vifuani. Tunataraji vijana hawa kukimbie ili kuokoa maisha yao.
iii. Moto unapozuka katika mtaa wa Zari, watu wengi wanapoteza maisha kwa maaana wenye
maduka wanafunga milango ya kutorokea kwa kuhofia kuporwa mali yao. Uk 54.
iv. Ni kinaya kwa Lily Nyamvua kufa kutokana na ukosefu wa usalama ilhali mumewe
Mwangeka alikuwa amesafiri Mashariki ya kati kwenda kudumisha usalama na amani.
v. Ni kinaya kwa Lunga Kangata kuchafua mazingira ilhali amesomea kilimo na kuwa
mtetezi wake.U5.
vi. Ni kinaya kuwa watu ambao wanaweza kuzimudu gharama za kukabiliana na makali ya
magonjwa ya UKIMWI na saratani ndio wanaozinyakua dawa hizi badaya ya kupewa
maskini wasiojiweza.

24
vii. Ni kinaya kwa maskini kuuziwa chanjo ya polio ilhali wanashindwa hata kujilisha.
viii. Meko anamweleza Selume kuwa vijana wengi wanaofariki kutokana na unywaji wa pombe
haramu ni vijana wanaosomea shahada ya uzamili. Tunataraji vijana hawa kufahamu
madhara ya pombe hii.
ix. Mzee Fungo anamwita mtoto wa kijalaana ilhali wamemzaa yeye na Pete. Uk 149.
x. Ni kinaya kuona lima la taka likiwa mkabala na dirisha la Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha.
xi. Wazazi wengi wanatupa watoto kwenye jalala baada ya kujifungua. Tunataraji wawalee
watoto wao. Uk 161.

1.4.2 Tashihisi

i. Ridhaa alisimama…akitazama wingu la moshi lililojikokota kwa kedi na mbembwe. Uk 1.


Wingu la moshi linapewa sifa ya binadamu ya kujikokota.
ii. Moyo wa kedi ulipiga kidoko, ukataka kumwonya dhidi ya tabia hii yake ya kike. Uk 2.
iii. Miguu yake Ridhaa sasa ilianza kulalamika. Uk 12.
iv. Mawingu yaliyoshiba yakataka kutapika yanagooka. Uk 15.
v. Ndege kwa jina PANAMA79…ndio inapiga pambaja arddhi. Uk 46.
vi. Hata njaa inaposalimu amri na usingizi kulegeza parafujo za mwili wake dhaifu…uk 187.
vii. Mwangeka alishangaa ikiwa kweli Mwangmi alihisi uchungu ambao ulikuwa unamtafuna
yeye.Uk 187.

1.4.3 Tashbihi

i. Maskini Lily…umekuwa kama jani linalopukutika msimu wa machipuko. Uk 5.


ii. Mitutu yake (bunduki) ilitema risasi jinsi bafe atemavyo mate. Uk 18.
iii. Washikavyo jambo (wanawake) huwa kama duduvule. Uk 19.
iv. Walikita ardhini (vijana) kama mikuki iliyochomekwa hapo.Uk. 24.
v. Anajihisi (Umukheri) kama samaki aliyetiwa kwenye dema. Uk 78.
vi. Kisa (cha Chandachema) kilishabihiana kama sahani na kawa na cha ndugu zake hawa
(Umu, Kairu, Mwanahri na Zohari)
vii. Ewe chupa wangu ninayekuenzi kama mboni ya jicho langu. Uk 128.

25
viii. Alipotuonyesha(Bwana Mabavu) hati miliki bandia, nasi mithili ya
viranga,…tukajikunyata kwa uoga . Uk 131.
ix. Aliamka (jogoo Mumina) kama simba aliyejeruhiwa. Uk 182.

1.4.4Mbinu rejeshi/Kisengere nyuma

i. Kupitia mbinu rejeshi mwandishi anaeleza mambo kadha yaliyotokea kabla ya Ridhaa
kufikwa na msiba wa kuangamia kwa mali na family yake. Ridhaa anakumbuka jinsi
mkewe alivyopiga mayowe akimtaka Mzee Kedi asiwaue. Anakumbuka alivyoisikia milio
ya kunguru na wadudu na jinsi mkewe alivyoibeza. Anakumbuka namna alivyosikia
mlipuko na kisha akazimia.
ii. Ridhaa anakumbuka asili yao jinsi babake mzee Musubili alikuwa na wake na watoto
wengi jambo lililomlazimisha kuhamisha baadhi ya wake zake katika Mlima wa Heri
akiwepo Ridhaa akiwa na umri wa miaka 10. Anakumbuka jinsi walivyosimangwa na
wenyeji kwa kuitwa ‘Wafuata Mvua’. Anasoma hadi anapohitimu udaktari.
iii. Kaizari anasimulia ili kuonyesha kiini cha walivyojipata kambini (Mlima wa Mamba).
Walikuwa wamefurushwa na wafuasi wa mrengo mpinzani wake Mwekevu. Anasimulia
jinsi walivyopoteza mali na wenzao wakaishia msituni ambamo wengi wanaangamia
kutokana na homa ya matumbo na kujichimbia misala.
iv. Maisha ya awali ya kina Kairu, Mwanaheri, Zohali na Chandachema yanaelezwa kupitia
mbinu rejeshi. Vijana hawa walipitia masaibu kadha hadi wanapojipata kwenye makao ya
watoto na shuleni Tangamano. Kairu aliokotwa njiani (walikuwa wamefurushwa kwao na
vijana) baada ya ndugu yao mdogo kufa kutokana na makali ya njaa. Mwanaheri alikuwa
amekabiliwa na changamoto kadha hasa baada ya wazzi wake Kaizari na Subira kuondoka
Msitu wa Mamba mzozo unaibuka baina ya Subira na wakwe zake. Subira anahamia mjini
Kisuka anakofia.Kwa upande wake, Zohali anatorokea mjini anakookolewa na kupelekwa
kwenye Wakfu wa Mama Paulina. Zohari alitoka kwao baada ya wazazi wake kushindwa
kumpokea vyema baada ya kuringwa akiwa kidato cha pili. Chandachema naye alitoroka
alikokuwa akilelewa na nyanya kisha na Bi. Satua, kisha na Bw. Tenge na mwishowe
kuokolewa na Shirika la Hakikisho la Haki na Utulivu baada ya kufuzu vyema.

26
v. Chimbuko la uhusiano kati ya Mwangeka na Apondi unaelezwa kupitia mbinu
hii.Walikutana katika warsha ambamo Apondi alikuwa akiwasilisha, wakapendana,
wakaooana, wakapata mtoto wao Ridhaa kisha wakamchukua Umu kama mtoto wao kwa
kunasihiwa na mwalimu Dhahabu. Pia, wanamlea Sophie (Mtoto wa Apondi na mumewe
marehemu Mandu).
vi. Pete anasimulia mawazoni mwake jambo lililomsukuma kutaka kujiua kwa kumeza dawa
ya panya. Alikuwa amekataliwa na babake. Mama yake Pete akampeleka kulelewa na
nyanya. Pete anatorokea mjini kutokana na ufukara. Mjini, anaringwa mara mbili na
kujaribu kuavya ingawa anashindwa. Mwishowe anaamua kujitoa uhai.
vii. Mamake Umu, Dick na Mwaliko (Naomi) anaeleza wanawe (ingawa hakupata nafasi ya
kuonana nao) masaibu yaliyompata baada ya kuwatoroka.Anawaarifu jinsi alivyorudi
Mlima wa Simba kuwasaka, akawatafuta kwenye vituo vya polisi asiwapate. Anaeleza
kuwa ameamua kuanzisha biashara karibu na Chuo cha Mbalamwezi.

1.4.5 Sitiari

i. Kama ningeusikiliza ushauri wa Tausi wangu labda ningeweza kuiokoa aila yangu hii. Uk
62. Mwangeka anamfananisha Lily moja kwa moja na tausi.
ii. Sauna alikuwa chui ambaye hakupigwa na mshipa kujifanya mwema kwa waajiri wake ili
aaminiwe. Uk 84. Sauna anafananishwa na mnyama chui.
iii. Huyu ndiye mshumaa unaotoa tumaini. Uk 132. Babake Dengelua alimwona Dengelua
kama mshumaa hivyo kujisulubu kumsomesha.
iv. Hatuwezi kumkabidhi mzee wetu huyu kifaranga kiteketeke hivi....Uk 148. Pete
kulinganishwa na kifaranga.
v. Afadhali kuishi jahanamu kuliko kwenye husuni hii yako. Uk 149. Boma la mzee Fungo
linaonwa kama jela.
vi. Wewe pekee ndiwe dawa ya hasira ya Sophie ya kivolkano. Uk 173. Hasira ya Sophie
kulinganishwa na ile ya volkano.

27
1.4.6 Methali

i. Liandikwalo ndilo liwalo. Uk 2. Terry anamtuliza Ridhaa kwani Ridhaa anaona milio ya
ndege hawa kama ishara ya msiba.
ii. Simba akikosa nyama hula nyasi. Uk 16. Ridhaa alikuwa akitafuna mizizi ya mwitu
kambini.
iii. Tabia ni ngozi ya mwili. Uk 33 Bw Waziri Mstaafu anajitolea kuelekeza watu (Wakimbizi
wenzake) wanapopigania chakula cha msaada.
iv. Mganga hajigangi. Uk 55. Ridhaa anashindwa kuhimili masaibu yake japo yeye ni daktari
wa upasuaji.
v. Mungu si Athumani. Uk 86. Umu anajishajiisha anapowasili jijini Karaha.
vi. Tangu lini mavi ya kale yakaacha kunuka? (Mavi ya kale hayachi kunuka). Umu hakuwa
amesahau masaibu yake hata alipokuwa darasani.
vii. Ng`ombe akivunjika mguu malishoni hujikokota zizini kusaidiwa. Uk 100. Zohali anarejea
nyumbani baada ya kupachikwa mimba.
viii. Teke la kuku halimuumizi mwanawe. Uk 100. Wazazi wa Zohali hawangemuumiza.
ix. Amani haiji kwa ncha ya upanga. Uk 113. Apondi anashauri washika dau anapowasilisha
ktika warsha.
x. Ulingo wa Kwae haulindi Manga. Uk 113. Apondi anawaasi washika dau kutotegemea
msaada wa nchi zingine wakati mkasa unapotokea.

1.4.7 Kuchanganya na kuhamisha ndimi

i. “Since when has man ever changed his destiny?” Uk 2. Swali la Terry kwa Ridhaa
kuhusiana na kuhangaika kwa Ridhaa kutokana na kihoro kilichosababishwa na milio ya
ndege na wanyama.
ii. “Ama hii ndiyo ile wanayoiita, Historical Injustice?” Uk. 7. Kauli ya Tila kwa babu ykae
Ridhaa.
iii. “Darling, this will be your home soon after our honeymoon.” Uk. 50. Hakikisho la Billy
kwa Sally.
iv. “This is a nest. I cannot live here, not now, not forever.” Uk 50. Kauli ya Sally kwa Billy.
v. “Mum pliz, jus a ‘red’!. These guys are needy. Uk 86. Rai ya Umu kwa mamake: Naomi.

28
vi. “Poa sana sistee we ni mnoma. Siku moja nitakuhelp hata mimi.” Uk 86. Kijana
ombaomba kwa Umu.
vii. “Easie, nena ukanunue loaf. Na promise hutanunua glue pliz, pliz bratha.” Uk 8. Umu kwa
ombaomba.
viii. “Umukheri, tutakumiss sana.” Uk 128. Sophie akimwambia Umu.

1.4.8 Sadfa

i. Inasdifu kwamba Umu anapotorokea jijini Karaha, anakutana na Hazina, kijana ombaomba
yule ambaye Umukheri aliwahi kumwauni kwa shilingi 200 walipokuwa wanapita na
mamake siku za awali kabla mama yao (Naomi) kuwaacha.
ii. Ni sadfa kwa Dick kukutana na dadake Umu katika uwanja wa ndege baada ya kutengana
kwa muda mrefu. Dick alikuwa anaenda kununua bidhaa za biashara yake naye Umu
alikuwa anaelekea chuoni. Wote wanasafiri kwa ndege moja.
iii. Mwliko anakutana kisadfa na ndugu zake, Umukheri na Dick katika hoteli ya Majaliwa.
Ni sdfa kuwa Umu na Mwangemi (aliyempanga Mwaliko) walizaliwa siku moja hivyo
kupanga sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwao katika hoteli hii ya Majaliwa.
iv. Ni sadfa kuwa Mwaliko analelewa na Mwangemi ambaye ni binamu wa Mwangeka
(anayelea Umu, dadake Mwaliko).

1.4.9 Taswira

i. Taswira ya madhara ya ghasia za baada ya uchaguzi inadhihirika wazi. Mwandishi


anaeleza, “Nchi ya Wahafidhina ilitwaa sura mpya. Misafara kwa misafara ya watu
waliohama kwao bila kujua waendako ilizipamba barabara na vichochoro vya
Wahafidhina. Mizoga ya watu na wanyama, magofu ya majumba yaliyoteketezwa kwa
moto, na viunzi vya mimea iliyonyong`onyezwa na moto ilijikita kila mahali. Taswira hii
inaonyesha ukatili wa binadamu.Uk 20.
ii. Kuna taswira ya jinsi vijana wanavyorashiwa risasi vifuani bila wao kujiokoa. Vijana hawa
wanajikita ardhini na kuapa kutoondoka. Uk 24. Taswira hii inaonyesha ubwege wa vijana.
iii. Maelezo ya Kaizari kuhusiana na uvamizi kwa familia yake yadhihirisha taswira inayozua
huruma. Hodi inasikika mlangoni. Mkewe Subira anazabwa kofi.Wanamkata mikato

29
miwili kwa sime na kuzirai.Mabarobaro hawa watano wanawatendea unyama mabinti
wake, Mwanaheri na Lime mbele yake.Uk 25.
iv. Kuna taswira ya vijana ombaomba mbele ya mkahawa wa kifahari jijini Karaha. Taswira
hii inadhihirisha ufukara wa hali ya juu. Mwandishi anawaona kama wingu la nzige.
Walikuwa na macho mekundu ya kutisha, wengine wameshika gundi, wengine vipande
vya mkate, wengine wamebeba vifurushi vya bidhaa vya kubadilishana na nyingine. Uk
87.
v. Kukutana kwa Umu na Dick uwanja wa ndege kunazua taswira. Wanaangaangaliana, Dick
anaita kwa sauti kubwa, „Umu!Dadangu Umu!” huku akimkimbilia. Wanakumbatiana
huku wasafiri wakiwatazama kwa mshngao. Taswaira hii inadhihirisha furaha na mapenzi
ya ndugu wanapokutana.
vi. Taswira ya Msitu wa Mamba ambao unabadilika na kuwa kambi ya wakimbizi inabainika.
Kuna mahema, wingi wa watu, watu kujisaidia misalani na baadaye kujaribu kuchimba
misala. Wtu kuanza kukata miti kwa minajili ya ujenzi na kilimo. Makasri yenye mapaa ya
vigae kutwaa msitu huu n.k.
vii. Taswira ya uchafu inatokeza akilini kutokana na maelezo ya mwandishi kupitia Neema
alipokuwa akielekea kazini. Ujia alimokuwa akipitia ulikwa kati ya safu mbili za majengo
ya zamani. Viambaza vya majengo haya vilihimili maandishi yenye matusi. Watu
walilazimika kupitia kwenye ujia huu wakiwa wmeziba pua na kujihadhari wasitie nyayo
kwenye tope lisilokanyagika. Aidha kulikuwa na lima la taka lililokuwa mkabala ya dirisha
la afisi ya Waziri wa Fedha. Uk 161. Taswira hii inaonyesha mapuuza ya viongozi
kunadhifisha jiji.
viii. Maelezo kuhusiana na uwasilishaji wa Apondi katika warsha na jinsi Mwangeka
alivyovutika naye inadhihirika. Hata Apondi anapomaliza uwasilishaji wake, Mwangeka
anamsindikiza kwa macho yake. Mwanya uliokuwa kwenye meno ya juu ya Apondi
unamkumbusha Mwangeka marehemu mke wake, Lily. Uk 114.

1.4.10 Takriri

i. Sijui kama inahalisi kumwita mke wangu. Siye, siye, siye-e-e-e, Uk. 16. Kauli ya
Kaizari kutokana na majeraha aliyosababishiwa na mabarobaro watano waliokuwa
wamewavamia nyumbani kwake.

30
ii. Na hakika mja huyu alikuwa kabadilika! Si yule Ridhaa ambaye Mwangeka alizoea
kumwona miaka michache iliyopita. Siye yule baba ambaye angekimbizana naye kila
jioni...si baba ambaye Mwangeka kwa utundu wake wake wa kitoto angemnyang`anya
stethoskopu yake...Uk 48.
iii. Nimechoka kuitwa mwizi wa mayai...Nimechoka mwizi wa mali yangu! Nimechoka
kupigania penzi la mwenzi na mavyaa...Uk 96. Haya ni manenoya Subira kwa
Mwanaheri kupitia barua.
iv. Anakumbuka imani ya Apondi na Mwangeka. Anakumbuka kujitolea kwao...
anakumbuka nasaha yao... anakumbuka urafiki...Uk 172. Haya ni maelezo ya
mwandishi akimrejelea Umu.
v. Tulingoja, tukangoja, moyoni nikiwa na imani ambayo baba alinijaza kuwa anasubiri
hafi. Uk 31. (Kauli ya Kaizari wakingoja usaidizi wakiwa Mlima wa Mamba.)

1.4.11 Nahau

i. Bibi ambaye alikuwa kabugia chumvi ya maisha akarishai. Uk 3. Nyanya yake Ridhaa
alikuwa amezeeka.
ii. Hata ubwabwa wa shingo haujakutoka! Haya ni maneno ya Ridhaa akimrejelea Lily kwa
maana kuwa aliangamia akiwa bado mdogo.
iii. Mustakabali wa ukuaji wetu kiuchumi uligonga mwamba wakati sheria ya mkoloni
ilipompa mzungu kibali cha kumiliki mashamba. Uk. 7. Kauli ya Tila kwa Ridhaa kwa
maana ya kukosa kufanikiwa.
iv. Ndege…ndio inapiga pambaja arddhi. Uk 46. Inaa maana ya kubusu/tua.
v. Mwangeka hakuamini jinsi alivyotekwa bakunja na mzungumzaji huyu (Apondi). Uk
112. Ina maana ya kuvutiwa.
vi. (Ridhaa) Alisalimu amri, akayaacha machozi yamvamie yatakavyo...uk 3. Ina maana ya
kukubali.

1.4.12 Chuku

i. Katikati ya mito hii ya machozi, Ridhaa aliileta picha ya maisha yake mbele ya kipaji
chake. Uk 3. Michirizi ya machozi inatiliwa chumvi kwa kuitwa mito.
ii. Ulikuwa ule usuhuba wa mmoja akijikwaa mwingine anauhisi uchungu wenyewe! Uk.

31
iii. Mwangeka anapoadhibiwa na babu yake, Mzee Msubili, mwandishi anaeleza kuwa,
“...Mwangeka...akitumbuiza kijiji kizima kwa siahi iliyotishia kuporomoha paa la jiko la
mamake.” Uk 186. Usiahi hauwezi kuporomosha jiko.

1.4.13 Litifati

i. Litifati ni mbinu ya kunukuu moja kwa moja usemi wa mhusika mwingine. Mifano:
ii. Wafuasi wa mpinzani wa Mwekevu wanarudia maneno ya Kaizari wanapomjeruhi subira
kwa kumnukuu, “As for me and my family we will support our mother.” Uk 25.
iii. Zohali anaiga sauti nzito ya mwalimu mkuu alivyokuwa akimwarifu dadake Tima,
“Dadake Zohali, samahani sana lakini uchunguzi wetu unabainisha kuwa Zohali ni
mjamzito.” Uk. 99.
iv. Dengelua anaiga bezo la Bwamkubwa, “Nyinyi ni unskilled labourers, mishahara mlonayo
ni kufu yenu.” Uk 133.

1.4.14 Nyimbo

i. Vijana wa mpinzani wa kiume wanaghani mkarara, Tawala Wahafidhina tawala, Mwanzi


wetu tawala Wahafidhina tawala. Uk 20. Wimbo huu unadhihirisha ubwege una ufuasi
sugu wa kipofu miongoni mwa vijana.
ii. Wimbo pendwa wa kidini ambao Terry alizoea kumwimbia Mwangeka kila mara
alipomuona dhaifu.Uk 49.

Salaama, salama

Rohoni, rohoni,

Ni salama, rohoni mwangu.

iii. Mbolezi ya Mwangeka (akiwa mwanafunzi) na wanuna wake wakiomboleza kifo cha
Dede. Uk 60. (Walikuwa wakiiga maombolezi ya wanajamii) Katika wimbo huu, wanampa
Kim (Dedan Kimathi) kwaheri na kumweleza kuwa amewaacha wazazi na ndugu zake kwa
majonzi na ukiwa.

32
iv. Kuna wimbo mrefu wa mlevi (Dengelua). Uk 128.Mlevi huyu anaisifu pombe kwa
kumwondolea adha maishani mwake. Anawasuta majirani wake matajiri aliodhani
walikuwa wakimcheka kuwa hawakufanya chochote wakati dunia ilikuwa ikimtenda.
v. Wimbo wa ndege aliyekuwa akikariri maneno ya mwalimu wa Mwangeka. Uk 187:
Wimbo huu unahimiza watoto kuwa watiifu kwa wazazi na watu wazima. Watoto
wakiwabeza wazazi watakuja kukosa radhi.

1.4.15 Tabaini

i. ...wakapoteza kila kitu, si maisha, si mifugo, si aila. Uk 20. Kaizari anasimulia masaibu
yaliyowapata baahi ya Wahafidhina waliofurushwa.
ii. Kazi za nyumbani zikaniangukia mimi. Si kufua, si kupiga deki, si kupika...Uk 101. Zohari
anasimulia wenzake kadhia iliyomkumba nyumbani kwao akiwa mjamzito.

33
1.5 MASWALI NA MAJIBU

1. Eleza changamoto kumi wanazopitia vijana katika riwaya Chozi la Heri. (alama 20)
i. Kutorokwa na wazazi-Umulheri, Dick na Mwaliwa wanaachwa na mama yao, Naomi.
ii. Vifo vya wazazi- Lunga anakufa kutokana na shinikizo la damu mwilini.
iii. Kutumiwa vibaya na wanasiasa- Wanatumika kuandamana na kuzua ghasia katika nchi
ya Wahafidhina. Wanachoma magari kana kwamba ni taka. Uk 21. Mabarobaro watano
wanatumiwa kutesa familia ya Kaizari.
iv. Mfumo duni wa elimu- Kijana mwenye shati lililoandikwa Hitman, analalamika kuwa
mfumo wa elimu ni ule wa kukariri tu nadharia bila kumfunza mwanafunzi umuhimu
wa kujitegemea na kujiajiri.
v. Umaskini-Pete analelewa na nyanya kiasi cha kukosa sodo. Chandachema vilevile
inabidi kufanya kazi ya kuchuma majani chai kujipatia karo ya shule.
vi. Ujauzito- Zohali anaringwa akiwa bado mwanafunzi.
vii. Shinikizo la vijana-Pete anapashwa tohara ili asitengwe na wenzake licha ya babake
kuwa mstari wa mbele kutetea haki za binadamu.
viii. Ubakwaji-Sauna anabakwa na baba wake wa kambo, Mzee Maya.
ix. Kukataliwa na wazazi-Pete anakataliwa na babake kwa kigezo cha kutoshabihiana.
x. Ulevi/Unywaji- Selume anamwarifu Meko kuwa vijana wengi wanaoangamia ni vijana
wanaosomea shahada za uzamili.
xi. Malezi-Kuna watoto wengi wanaorandaranda mitaani katika mji wa karaha. Watoto
hawa bila shaka wamekosa malezi bora kutoka kwa wazazi wao.

2. “Anajihisi kama samaki aliyetiwa kwenye dema. Haya ni mazingira mageni kwake na
hakuja hapa kwa hiari.”
a. Eleza muktadha huu (alama 4)
Ni kauli ya mwandishi, anarejelea hali ya Umulkheri akiwa darasani. Wazazi wake
wamehamia Mlima wa Simba baada ya kufurushwa Msitu wa Mamba Umulkheri
hafuatilii masomo darasani kwa kuwa katika shule geni. Hali ya ugeni katika shule ya
Tangamo inamfanya kujihisi kama samaki demani.
b. Fafanua wasifu wa mrejelewa na umuhimu wake. (alama8)

34
i. Ni mvumilivu- anavumilia matatizo ya malezi baada ya kuachwa na wazazi wake.
Analazimika kujitafutia shule na makao baada ya kuharibikiwa kwao
nyumbani.Anavumia haya hadi anapofanikiwa.
ii. Mkakamavu- anakabili hali gumu inayomkabili bila kusita.Anatafuta msaada wa
makao kwa rafiki yake Hazina.Anakabili hali gumu inayomkabili kikakamavu.
iii. Msomi- Umu anasoma hadi chuo kikuu na shahada ya uzamili nga’ambo.
iv. Karimu- anamsaidia Hazina mtoto ombaomba mtaani kwa shilingi mia mbili hata
kama mamake anamzuia kufanya hivi.
v. Umulkheri anatumika riwayani kuwakilisha watoto waathiriwa wa migogoro ya
kijamii na mazingira. Anatumika na mwandishi kudhihirisha kuwa watoto wasio
na wazazi wana nafasi ya pili ya kuyaboresha maisha yao.
vi. mwenye matumaini- ana imani kuwa atawapata ndugu zake waliotoroshwa na
Sauna hata kama itakuwa sadfa. Ana imani kuwa atapata msaada wa makazi mapya
na aendeleze masomo yake.uk.85-86.

c. Kwa mifano minane, eleza jinsi wahusika wanajihisi kama samaki aliyetiwa
demani. (alama 8)
i. Ridhaa anajihisi kama samaki aliye demani katika mazingira mageni ya Msitu wa
Mamba. Ridhaa hajayazoea mazingira haya.
ii. Kazi ya uhazili inamfanya Annette mkewe Kiriri kujihisi kama aliye demani.
Annette anaishia kuiacha na kuhamia ng’ambo.
iii. Ridhaa anajihisi kama samaki aliyetiwa demani anapokabiliana na wanafunzi
wageni katika shule aliyojiunga nayo baaada ya babu yake kuhamia Msitu wa Heri.
Mazingira mageni yanamsumbua.
iv. Lunga anajihisi kama samaki demani baada ya kufurushwa kutoka Msitu wa
Mamba hadi Mlima wa Simba. Hayakubali mazingira mageni.
v. Zohali anajihisi kama samaki kweye dema baada ya kupata mimba na kukataliwa
na familia yake. Analazimika kutoroka nyumbani baada ya kufanywa mtumishi wa
nyumba yao.
vi. Subira anajihisi kama samaki kwenye dema kutokana na mateso anayoyapata
kutoka kwa mkwe wake.

35
vii. Chandachema anajihisi kama samaki kwenye dema baada ya kulelewa na nyanya
yake(wazazi wake hawako karibu), nyanyake anafariki, anaishi kwa jirani
anakofukuzwa na mke wa jirani kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
viii. Kairu anaishi kama samaki kwenye dema katika kambi ya wakimbizi
anakolazimika kutumia chumba kimoja na ndugu zake pamoja na wazazi wake.
3. Onyesha namna mwandishi wa riwaya Chozi alivyoangazia suala la elimu. (alama
20)

i. Wanafunzi wanafunzwa kuichambua jamii.Tila ni mwanafunzi wa kidato cha sita,


anafunzwa kuiona jamii wa undani.
ii. Mitaala inaangazi mifumo mbalimbali ya kijamii na athari zake kama vile tamthilia ya
Mashetani.
iii. Mwalimu Meli anawafunza wanafunzi wake umuhimu wa kuzingatia usawa katika
jamii.uk39.
iv. Wanafunzi wa vyuo vikuu wanahitimu na shahada zisizowahakikishia kazi. Kijana
mwenye shati lililoandikwa Hitman katika makabiliano na polisi anasema shahada
vyuoni haviwahakikishii kazi.
v. Wanafunzi vyuoni wanafunzwa kukariri madharia badala ya umilisi. Mafunzo ya
ujasiriamali yamepuuzwa.
vi. Kuna wale wanafaidika na elimu.Ridhaa amesoma kiwango cha kuwa daktari na
kufanya uzamili katika upasuaji.
vii. Wanaosoma na kupita na kutaabika wakitafuta kazi wanaingilia ulevi. Shamsi
anageukia ulevi.
viii. Wanafunzi wa masomo ya juu hawadhamini kifedha na serikali ipaswavyo. Kipanga
mwanafunzi wa uzamili analazimika kunywa pombe kujipurukusha na matatizo ya
chuoni.
ix. Wanafunzi wanalazimika kuhamahama shule kwa sababu za machafuko ya jamii. Umu
analazimika kukabiliana na mazingira magumu katika shule geni ya Tangamano.
x. Walimu wanawajibika kujua shida za kisaikolojia za wanafunzi.Mwalimu Dhahabu
anafahamu kuwa Umu hfuatilii masomo yake kikamilifu, anaamua kumchimba aujue
ukweli.

36
4. “Je, binadamu aliandikiwa kumpoka bidamu mwenzake maisha?”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
Haya ni maneno ya Mwangeka akijesemea baada ya kuwasili katika bomba lao
ambao lilikuwa limeshateketezwa. Mwangeka alikuwa amepokelewa na baba yake,
Ridhaa kutoka uwanja wa ndege. Mwangeka anayasema haya baada ya kuona
uharibu na uhayawani waliokuwa wametendewa.
b) Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea riwaya Chozi la Heri. (alama 16).
i. Mali na familia ya Ridhaa inateketezwa.
ii. Mke wa kaizari, Subira anakatwa kwa sime nao watoto wake, Lime na
Mwanaheri wanabakwa mbele ya Kaizari.
iii. Vijana waliokuwa wakiandamana wanapigwa risasi na walinda usalama.
iv. Lunga Kangata anafutwa kazi kwa kupinga ununuzi na uuzwaji wa mahindi
yenye sumu.
v. Wakimbizi kama vile Kaizari wanafurushwa Msitu wa Simba ingawa walikuwa
na hati milki.
vi. Sauna anawaiba Dick na Mwaliko kwa lengo la kuwauza.
vii. Tajiri Buda anamtumia Dick kijana mdogo kulaangua dawa za kulevya. Dick
analazimishwa kumeza dawa hizo na kuzitapika kwenye masoko ya ughaibuni.
viii. Wakwe zake Subira na Selume wanawasimanga, kuwaonea na kuwatenga
jambo linalowafanya wote kutoroka.
ix. Pete anaozwa kwa lazima jambo linalomfanya kukatisha maisha yake.
x. Naomi anafutwa kazi na Kimbaumbau kwa kukataa afanye mapenzi naye.
xi. Waafrika wanapokwa rasilimali zao na wakoloni. Kwa mfano, Shamsi
analalamika kuwa babake alipokwa shamba lake.
xii. Neema anakiokota kitoto Riziki kwenye biwi la take. Inaelezwa kuwa watoto
waliokuwa wakitupwa walikuwa wengi.

5. Alikuwa amesafiri kwa shughuli za ujenzi wa kitaifa, kama alivyoziita safari zake za
kikazi. Fafanua jinsi jamii inashiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa riwayani.

37
i. Ridhaa anamtibu mgonjwa mwathiriwa wa vita vya kijamii. Anahakikishia taifa
nguvukazi.uk.4.
ii. Mwangeka anaenda kudumisha amani Mashariki ya Kati. Kwa kufanya hivi
anaokoa maisha ya wananchi.uk.5
iii. Ridhaa anafanya juu chini kuhakikisha kijiji kizima katika Msitu wa Heri kimepata
maji ya mabomba. Anasaidia katika uhifadhi wa mazingira katika eneo la
Kalahari.uk11.
iv. Kaizari na Ridhaa wanaisaidia jamii ya wakimbizi katika Msitu wa Mamba kujenga
vyoo vya mashimo ili kuepuka maradhi ya kipindupindu na homa ya matumbo.
v. Shirika la Makazi bora linajitolea kujengea wakimbizi katika Msitu wa Mamba
nyumba bora.uk31. Maisha ya wakimbizi yanakuwa bora kiasi.
vi. Misikiti na makanisa yanakusanya magunia ya chakula kuwalisha wahasiriwa wa
vita vya wenyewe kwa wenyewe kambini.uk31.
vii. Ridhaa anamwelekeza Selume kwa mkuu wa Idara ya Afya ya Jamii katika
Hospitali Kuu ya Tumaini kama njia ya kutafutia ajira.uk35.
viii. Ridhaa anaanzisha Wakfu wa Matibabu unaolenga kuimarisha Afya ya Jamii.
ix. Anajenga zahanati ya Mwanzo Mpya ambayo inatoa huduma za afya kwa
wanajamii kwa gharama ya chini.
x. Wataalamu mbalimbali wanafika katika kambi ya Msitu wa Mamba kutoa nasaha
kwa wahasiriwa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ridhaa anafaidi na mpango
huu na kuepuka kupatwa na maradhi ya shinikizo. uk36.
xi. Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanatembelea kambi ya wakimbizi katika
Msitu wa Mamba kutoa ushauri na matibabu kwa wahasiriwa. Lime na Mwanaheri
wanahudumiwa na mashirika hawa.
xii. Mwalimu Meli anawafunza wanafunzi wake namna ya kuichambua jamii na
kuwachagua viongozi kwa kutumia misingi ya maendeleo na wala si jinsia na
unasaba. Kuelimisha vijana ni kuendeleza jamii.
xiii. Jamii ya Kimataifa inaingilia kati na kurejesha amani baada ya mapigano ya muda
mrefu.

38
xiv. Lunga anashiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa kwa kuwahamasisha wanajamii
dhidi ya kulinda mazingira. Akiwa shuleni anatoa hotuba akikashfu tabia ya
binadamu ya kuharibu mazingira kwa kupania kilimo.uk69.
xv. Lunga anaelimisha wanajamii kuhusu mbinu bora za kilimo. Yeye ni Afisa wa
Kilimo nyanjani. Uk. 67.

39

You might also like