You are on page 1of 11

4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

Neno “utendi” linatokana na kitenzi “kutenda” maanake huwa ni kutenda jambo Fulani.
Chaligha (2013), anaeleza kuwa, kumetumika fomula, kuelezea maana ya Utendi kuwa ni E = M + Ms
yaani (Epic= Mars + Music/muse), yaani Utendi ni mungu, Muziki na Vita (U=M+V). Akifafanuwa
maelezo hayo, Chaligha (kashatajwa), anasema Utendi ni tukio la kimuziki linalozungumzia vita na
miungu.

Mawazo hayo yana mashaka, kwa upande wa Utendi/Utenzi wa Kiswahili. Uswahilini, Utendi na
Utenzi, tofauti ni matamshi. Tendi Uswahilini si lazima zizungumzie miungu kama aonavyo Chaligha.
Uswahilini kote, neno “miungu” ni kufuru.
Chaligha (ameshatajwa), alieleza kuwa, tendi simulizi ni tungo simulizi zenye mtindo wa kifomula,
zinazohusu mambo ya ajabu, ya watu wasio wa kawaida. Masimulizi hayo yanasimuliwa kwa njia ya
mdomo. Utendi/Utenzi wa Kiswahili hughaniwa katika miktadha mingi kama vile, sherehe na msiba.

Mulokozi (1999), anaeleza kuwa, Utendi ni utungo mrefu wa kishairi wenye kusimulia hadithi ya
ushujaa na mashujaa. Kwa jumla, Mulokozi anaona kuwa, Utendi lazima uwe na mhusika shujaa.
Mawazo hayo, hayana ukweli wa moja kwa moja kuhusiana na Utendi wa Kiswahili.
Wamitila (2010), anaelezea kuwa, Utendi ni aina ya Utenzi ambao, unazungumzia maisha na matendo
ya ushujaa au ya mashujaa wa jamii fulani. Tendi ni simulizi, ambazo husimuliwa na mtunzi na
ambazo huchukuwa mkondo unaofanana katika kazi za kishairi. Mawazo ya Wamitila yametoa
mwelekeo tofauti na wa Mulokozi (ameshatajwa), juu ya dhana ya Utendi. Utendi/Utenzi na Nathari
au Tutumbi hukutana kwenye maudhui lakini si kwenye fani, kila utanzu una mitindo, miundo,
kanuni, ada na taratibu zake. Uswahilini, hakuna Utendi ama Utenzi wa kinathari au kitutumbi.

Advertisements

REPORT THIS AD

Utendi/Utenzi ni bahari kuu na kongwe ya Ushairi wa Kiswahili. Kusilazimishwe swala na mbuzi-


mmoja na wapili ni wa majumbani.
Mawazo ya Wamitila (2010), yana upungufu. Kuna vielezea vya Utendi, havikuhusishwa katika
ufafanuzi wake. Vielezea hivyo ni sifa za pekee za fani za Utendi wa Kiswahili, kama vile; muundo wa
beti, bahari ndogo ya kila ubeti, vina na mizani pamoja na urefu wa Utendi huo..
Baada ya kutalii mawazo ya wanataalimu waliotangulia, dhana ya Utendi imeweza kuelezeka kwa
kupambanuliwa kwa sifa ya Utendi/Utenzi ambao hufuata kaida ya urari wa vina na mizani na
huweza kuwa na mhusika shujaa au asiyekuwa shujaa.
https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 1/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

Mhusika huyo mkuu, huitwa nguli. Vile vile, tendi, huelezea masuala yanayoihusu jamii, kama vile,
masuala ya kijamii, ya kisiasa, ya kiuchumi na ya kiutamaduni.
Masimulizi hayo, hutolewa kwa lugha ya kishairi, ambayo ujumi wa lugha hiyo, hutegemea jamii
inayohusika na masimulizi yenyewe yanayotolewa huwa kwa ajili ya jamii, ili kuwa katika mwenendo
bora wa maisha ya hapa Duniani na Akhera.
Utendi ni aina ya ushairi na tanzu moja wapo wa fasihi simulizi ambao husimulia Maisha na matendo
ya mhusika shujaa au wa visasili.

Utenzi ni ni utungo mrefu wa kishairi unaoelezea juu ya mambo Fulani na maranyingi huwa na pande
moja yaani huwa na vina vya kati tu. Utenzi haufuati urari wa mizani.
Katika Kiswahili, kuna tenzi kuu maarufu kama vile utenzi wa tambuka(Bwana mwengu karne ya 18),
utenzi wa mwanakupona(mwanakupona karne ya 19), utenzi wa inkshafi(Abdallah bin ally), utenzi wa
hayati sokoine(kazi ya Charles mloka karne ya 20), utenzi wa hati na adili(shaban robert), utendi wa
Fumoliyongo (muhamad kijumwa 1913)

Utangulizi wa utendi wa Fumoliyongo.

Utendi wa fumoliyongo unamhusu shujaa liyongo. Baadhi ya wataalamu (mbele 1986:138-140) hudai
kuwa jina lake lilikuwa “liyongo fumo” sio Fumoliyongo yaani Fumo alikuwa ni babake. Wengine
wataalamu wakiwemo (knappert 1983:144)”fumo” ilikuwa tu wadhifa wake sawa na mfalme. Bado
kuna utata na mjadala mkubwa kuhusu tarehe ya liyongo, na wengine wanadai kuwa yaweza kuwa
kiumbe tu hadithini ambaye hajapata kuishi.
Hata hivyo, kuenea kwa hadithi yake na umashuhuri wake katika mapokezo na matendo ya kiimla ya
waswahili yanaashiria kuwa huenda mtu huyo aliishi kweli hata kama habari zake za kuishi zimetiwa
chumvi na waenezaji.
Baadhi ya wataalamu (Nabhany 1987, Mbele 1986) wanasema liyongo aliishi karne ya 9 masihiya
(miaka ya kikristo)
Wengine wakiwemo Chiraghdin (1973) naKnappert (1983:167) wanasema liyongo aliishi baina ya
miaka ya 1160-1204 lakini tarehe inayoelekeya kukubaliwa ni ile ya karne ya 13-14. Hii ni kwasababu
kitabu cha Tarekhe ya Pate(Freeman Greenvile 1962:241-299) kinamtaja mtawala wa jimbo la Ozi
aitwaye Fumoliyongo aliyeishi kati ya utawala wa Fumomari.
Fumoliyongo alikuwa shujaa wa kitaifa aliyeishi eneo la mto wa Tana kaskazini mwa Mombasa.
Babake alikuwa kiongozi wa mji wa shaka.
Babake liyongo alikuwa na watoto wawili yaani Liyongo mwenyewe na kakake Daudi mringwari.
Fumoliyongo alikuwa kiongozi mkuu kaskazini mwa pwani ya Afrika mashariki hapo karne ya 9-13.
Anajulikana kama shujaa, kijudu, na mshairi wa mashairi ya jadi, hadithi na nyimbo za waswahili na
hasa zilizohusu mila, harusi na densi za gungu. Miji kadhaa pwani huko Tanzania inadai kuwa ndiko
alizaliwa.
Baadhi ya nyimbo, mashairi na hadithi zake huzungmzia sherehe za harusi za kale, vita, na densi za
gungu kama vile wimbo wa “sifu uta wangu (song of the worrier)”. Pengine liyongo anatambulika
kama mjuzi wa upiga pinde.
Hadithi za kale za liyongo nyingi zilibeba sifa lingani na zile za ulaya kv Achilles, Sigurd, na
Robinhood. Tena aliandika gungu nyngi kama “Sifa la Uta” au “Wimbo wa Mapenzi”
Fumo Liyongo wakati mwingine alikuwa askari na mwandishi wa mashairi katika pwani ya kaskazini
ya Afrika Mashariki kati ya karne ya 9 na karne ya 13.
Fumoliyongo alikuwa kijana mwenye kusifiwa mjini kote, mrefu, mwenye matendo ya kishujaa, nguvu
zisizo za kawaida aliyeishi ungwana na mashaha eneo la shaka jimbo la ozi.
https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 2/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

Kama alivyoeleza Sigurd, liyongo alikufa kutokana na usaliti. Liyongo alisalitiwa na mtoto wake
aliyetoboa siri ya nguvu za babake. Liyongo aliweza tu kufa akidundwa sindano ya shaba kitovuni.
Hiyo ilikuwa siri kati ya liyongo na mamake aliyejulikana kwa jina “Mbwasho”.lakini liyongo
alipoifunua kwa mtotoke, akaangamizwa na damu yake yenyewe.
Inasemekana kwamba, baada ya kifo chake, mwenye nguvu zake Liyongo alizikwa mji wa shaka jimbo
la Ozi.

Kuhusu mwandishi wa utendi wa fumoliyongo;


Katika mwaka wa 1913, mwandishi wa mashairi Muhamad bin Omar Al-Bakry aliyejulikana sana kwa
jina la Muhamadi Kijumwa aliandika juu utendi maarufu uitwao utendi wa Fumo Liyongo, utendi
ambao ulikuwa ukielezea maisha ya Fumo Liyongo, aliyekuwa mshairi na pia mtawala katika eneo la
Pate. Kijumwa kama yeye siye mwandishi bali alipata hadithi hiyo kutokana na simulizi za waswahili
wa mwambao wa Kenya. Kijumwa hakuiandika hadithi bali alisimulia upya kwa njia ya utendi.
Muhamad kijumwa aliishi 1855-1940 alikuwa mwenyeji wa lamu nchini Kenya. Alikuwa msanii
mashuhuri ambaye mbali na kutunga mashairi na tendi, vilevile alikuwa mjomi (mchongaji wa
milango yenye nakshi), msanii-msanifu, msawidi (copyist) na mnukuzi wa miswada ya zamani.
Habari za maisha yake hazijulikani bali anaanza kujitokeza kwenye miaka ya 1890 ambapo alikuwa
anawasaidia watafiti wa kizungu kv Alice werner (1900-1935), William Hichens (miaka ya 1930).
Inasemekana kuwa, muhamad kijumwa alifariki mwanzoni mwa mwaka wa 1940 japo tarehe kamilii
haitambuliki wazi mtoto wake Elesha aliishi Lamu. Kijumwa alitunga masahiri mengi yakiwemo
utendi wa helewa.

Muhtasari wa utendi wa fumoliyongo;


Utendi wa Fumo Liyongo unahusu mgogoro kati ya Fumo Liyongo na kaka yake, sultan wa Pate
ambaye hajatajwa kwa jina. Mwanzoni utenzi unamdokeza Liyongo akiwa ana umri wa makamo hivi,
aidha kimo na nguvu zake za mwili ziliwashangaza wengi kwa hivyo walimsifia mno.
Watu wa kabila la Wagalla walipofika Pate kutafuta chakula ili wanunue, walielezwa sifa za Liyongo
na wananchi, halikadhalika Sultani wa Pate alimsifu Liyongo. Kwa kusikia sifa hizo za ajabu, Wagalla
walitamani sana kumwona Liyongo, kwa hivyo wakamwandikia Liyongo warakawakimwomba aje ili
wamwone.(beti 18,19)

Liyongo akaitikia wito huo, hivyo akapanga safari yake ya kwenda Pate huku amebeba mizigo chungu
nzima.(beti 37,38)Kati ya vitu alivyovibeba ni panda, kinu na mawe. Kwa mwanadamu wakawaida,
safari hiyo ni ya siku nne lakini Liyongo alichukua siku mbili tu na kufika Pate.
Alipokaribia jijini Pate, alipuliza panda ya kwanza hadi ikapasuka.Alipuliza ya pili nayo vile vile
ikapasuka. Alipuliza ya tatu na kuingia mjini hadi barazani kwa sultani.(beti27,30, 31) Watu
walishangaa mno kwa sauti kubwa ya panda. Watu wengi wakakusanyika kumwona, alipotua mzigo
wake umejaa vitu vingi ambavyo vilitosha kuijaza nyumba nzima. Moja kwa moja, Wagalla wakakiri
kuwa kweli Liyongo ni mtu mnene na mwenye nguvu. Wagalla wakatamani sana kuipata mbegu yake,
hivyo walimwomba sultani awaruhusu kupata mbegu hiyo, kiongozi huyo akakubali.
Wakafanya mpango wa kumwoza mke wa Kigalla ambaye alimzalia mtoto wa kiume. Sifa za Liyongo
zilivyozidi kusambaa ndivyo mgogoro kati yake na Sultan wa Pate ulivyozidi.
Mfalme alihofia kuwa huenda Liyongo angemnyang’anya ufalme hivyo akatafuta njia ya
kumwangamiza.
Liyongo alipogundua njama ya Sultan ya kutaka kumwangamiza, akatoroka Pate na kwenda kuishi
nyikani pamoja na Wadahalo, Watwa, Wasanye na Waboni.
Mfalme akafanya mpango wa kisiri pamoja na Wasanye na Wadahalo ili wamuue huko mwituni kwa
kuwahidi malipo ya reale mia moja iwapo wangemletea kichwa cha Liyongo. Watu hao walifanya
urafiki na Liyongo kisha wakashauri wawe wakicheza kikoa
https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 3/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

pamoja. Hivyo wliachaguana kwa kupeana zamu ya kuangua makoma kutoka mtini. Walipanga kuwa
ikifika zamu ya Liyongo, wamngojee apande mkomani kisha wamfume kwa mishale yao wamuue
akiwa mtini.
Kwa uwezo wa kiakili aliokuwa nao Liyongo, akagundua njama hiyo. Badala ya kupanda mtini
aliangua makoma akiwa chini aridhini hivyo wakashindwa kumuua.Watu hao walimpelekea Sultani
ripoti kuwa haiwezekani kumuua Liyongo.

Mfalme aliwaambia warejee alipo Liyongo wamweleze kuwa mjini ni salama na hapana hatari yoyoyte
ili waende naye huko. Waliporudi wakamweleza Liyongo uwongo huo ambao aliuamini kuwa kweli,
kwahivyo akawafuata na kuenda nao mjini Pate.
Sultan akaandaa ngoma ya Gungu na mwao na kuwaalika wapenzi wa aina hiyo ya ngoma, Liyongo
alikuwa mmoja wao. Ngoma iliposhika kasi, askari walimnasa Liyongo na kumtia korokoroni.
Mfalme na watu wake waliamua kumuua Liyongo akiwa gerezani.
Siku ya mauaji kutekelezwa zilipokaribia, Liyongo akapewa muda wakutoa ombi kwa kitu chochote
apendacho. Liyongo akaomba apigigwe ngoma ya mwao naGungu.
Ombi hili likakubaliwa na ngoma ikaandaliwa. Ngoma ilipoandaliwa, Liyongo akatuma ujumbe wa
kishairi kwa mama yake kupitia kwa kijakazi Saada ambaye humletea chakula.(beti 104, 105)

Katika ujumbe huo alieleza kwamba siku hiyo ya ngoma apike mkate wa wishwa na ndani yake atie
tupa ya kukatia minyororo. Mama yake akafanya vivyo hivyo.
Kijakazi Saada alipompelekea chakula, walinzi wakachukua mikate waliyodhania kuwa mizuri na
kuutupilia mbali ule wa wishwa ili umwendee Liyongo. Ngoma iliposhika kasi, Liyongo akatumia
nafasi hiyo kukereza minyororo, hivyo akafaulu kuikata. Akavunja Lango kuu la jela na kutorokea
msituni.
Mfalme alipoona kuwa ameshindwa kumuua Liyongo, akamshawishi mwanawe Liyongo aende
amuulize babake kiwezacho kumdhuru.
Sultani alimpa ahadi ya kumwoza bintiye, kumpa uwaziri katika uongozi wake na mali nyingine ikiwa
angefanikiwa.
Mwanawe Liyongo akafululiza hadi Shaka alipokuwa babake na kumtaka amweleze siri ya yeye
kutodhurika na kitu chochote.
Ingawa Liyongo alitambua njama ya mahasidi wake ya kupitia kwa mwanawe, alikubali kumfichulia
siri.
Alimweleza kuwa kiwezacho kumuua ni sindano ya shaba ikitiwa kitovuni mwake. Sultan alijawa na
furaha sana, alipopewa taarifa hii na kijana huyu wa Liyongo.
Kwa hivyo akampatia sindano ya shaba, akampa ahadi zaidi na kumpa zawadi tele.
Akarejea Shaka tena alipo babake, akamngoja alipokuwa usingizini, akamchoma sindano ya
shabakitovuni. Liyongo alizinduka na kuamka kwa hasira, akachukua mshale wake na kuelekea
kisimani akimtafuta adui.

Akiwa amepiga goti, akatia mshale katika upinde huku akiuelekeza mjini na kukata roho. Umati wa
watu walipomwona akiwa katika hali hiyo, wakadhani yuko hai na kaudhika mno. Kwa hivyo
walijawa na hofu ya kwenda kuchota maji kisimani.
Walipozidiwa na ukosefu wa maji, walikwenda kumwomba mama yake Liyongo aje ambembeleze
aondoke wateke maji. Mama yake akawa anaenda kumpembeleza mara kwa mara lakini alikosa
kufanikiwa.
Hatimaye maiti yake iliaanguka ndipo watu wakabaini kuwa alikuwa ameshakufa.
Sultani alipopata habari ya kifo cha Liyongo alijawa na furaha. Akamwarifu mwanawe Liyongo kuwa
babake amefariki. Badala ya kuwa na maskitiko, huzuni na maombolezo, yeye alifurahi.
https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 4/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

Kitendo hiki kinamuudhi mfalme ambaye alichukua mali yote aliyokuwa amempa. Wanajamii
wakamfukuza kijana huyu asitangamane nao. Siku chache baadaye akakumbana na maradhi
yasiyokuwa na tiba ambayo yalimwangamiza.

Sifa za Fumo Liyongo;


Mwandishi Kijumwa (1973), amemsawiri mhusika Fumo Liyongo kishujaa katika utendi wenyewe.
Kwa upande wangu nachukua mtazamo huo huo wa kishujaa alioutoa mwandishi ili kubaini sifa zake.
Kwa mujibu wa Wamitila (2003), neno shujaa hutumika kueleza mhusika mkuu katika kazi ya kifasihi
ambaye anaweza kuwa wa kike au wa kiume.
Kimsingi neno hili haliashiri wema tu. Kwa upande wake, Mulokozi (1996), anasema kuwa mashujaa
wa utendi ni wa aina tatu: Mashujaa wa kijadi wa kiafrika kwa mfano, Fumo Liyongo katika Utendi wa
Fumo
Liyongo, mashujaa wa kidini kwa mfano, Mtume Muhammed na masahaba wake katika Utendi wa
Ras‘lghuli na mashujaa wa kubuni kwa mfano Tajiri mbaya katika Utendi wa Masahibu.
Mtunzi anamtaja Fumo Liyongo kama jitu nene, lenye kimo kinachozidi cha mtu wa kawaida.
Kimo cha Fumo Liyongo kimeelezwa kwa kina, huku mtunzi akidhamiria kuweka wazi uwezo wa
nguvu alizo nazo na umbo lake la kipekee. Alijulikana mno kwa unene wake kiasi cha kuwashangaza
watu wengi. Watu walitoka mbali kuja kumtazama, kwani Vimo vyao vilimfikia magotini: (beti za 6 na
16).

6. Liyongo kitaka,mali
akabalighi rijali
akawa mtu wa kweli
na haiba kaongeya.
7. Wagalla wakipulika
kwa dhihaka wakateka
wakanena “twamtaka”
na sisi kumwangaliya. Mtunzi anaeleza alivyosafiri safari ya mbali kwa siku chache mno, hali
ambayo ni tofauti na ya mwanadamu wa kawaida. Kwa mfano, aliwahi kutembea kutoka Shaka
hadi jijini Pate, safari ya siku nne lakini yeye akachukua siku mbili tu. Liyongo ni mwenye vipaji
kadhaa: Anawashinda maadui katika kulenga shabaha anapotumia upinde na mishale kuchuma
mikoma bila kukwea mkomani.
Juu ya yote alikuwa muungwana sana na mfano wa kuigwa na watu. Talanta inayojikeza hata zaidi
ni, ufundi wa kutunga nyimbo na mashairi yaliyojulikana kama Gungu. Kwa mfano, akiwa
kizuizini, aliitumia talanta hii kumtumia mamake ujumbe wa kishairi huku akiomba tupa ambayo
aliitumia kukata minyororo ili kujiweka huru: (beti za 104 na 108).
8. kama sada nakutuma
Enda kamwambie mama
Afanye mkate mwema
Kati tupa aitiya.
9. zilizo kikaza kusi
alikikata upesi
hata zikikoma basi
inukani kawambiya.

Liyongo alikuwa hodari katika vita, aliwashinda maadui wake wote hata Wagala walishindwa vita na
Liyongo. Vimo vyao vilimfikia magotini hali hivyo ikawawia vigumu kumshinda vitani.
Pia katika nguvu za kiakili, Liyongo alitumia akili kukataa kupanda mkomani ili aangue
https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 5/11
g
4/5/23, 10:31 AM
y g p g
UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

makoma(ubeti wa 65).

65. Akawambia ngojani


akatowa mkobani
chembe katiya ngweni
makoma kiwanguliya.
Alikuwa na nguvu za kimwili yaani ubabe na mabavu, kama inavyodhihirika katika (beti za 40, 41,
46).

Pia, Liyongo likuwa na nguvu za kiakili na kivita. Liyongo alikuwa na uwezo wa kiakili, kuvumbua
mambo mbalimbali na nguvu za kivita alikuwa nazo.Vilevile sifa ya uganga na sihiri, Liyongo ana sifa
ya uganga. Hivyo alisema hawezi kudhurika kwa njia ya kawaida inayomdhuru mwanadamu yeyote.
Kile ambacho kingemdhuru yeye ilikuwa siri ambayo aliifichua kwa mwanawe. Yaani nikwa
kudungwa sindano ya shaba kitovuni: (ubeti wa 143)

Liyongo ana mshikamano na kundi au makundi ya watu. Aliishi porini na Watwa na kushirikiana nao.
Ushirikiano wake ndio unaomnusuru na njama za mfalme za kutaka kmuua. Liyongo anapokufa watu
wengi waliompenda wanaomboleza kwa masikitiko makubwa: (ubeti wa 224).

Vilevile kulikuwa na ushirikiano wa kifamilia kati ya Liyongo na mamake, ushirikiano huu


unamsaidia kutoroka gerezani baada ya mamake kumpelekea mkate wa wishwa uliotiwa tupa
ndaniye: (beti za 107, 110)

Nakwahivyo, utendi wa fumoliyongo unafunza hasa wanaume kuwa washujaa na wababe, rijali (ub
13), kukiimu mahitaji ya jamii na familia (ub 25), kuwa masihiri ( ub 143) na masuala hayo yana msingi
ya kiume katika jamii ukizingatia nadharia ya ubabedume inayojikita katika kutambua na kuchunguza
nafasi na majukumu ya mwanamume katika jamii ya waswahili.

Mambo kuhusu utamaduni katika utendi wa fumoliyongo;


Utamaduni ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake. Hivyo inajumlisha imani,
ujuzi, sanaa, maadili, sheria, mila na desturi, ambavyo mtu anapokea kutoka jamii anamoishi.
Kama sifa maalumu ya binadamu inayomtofautisha na wanyama wengine, utamaduni ni suala la
muhimu katika anthropolojia ukihusishwa na yale yote kama vile lugha inayowaunganisha watu
wanaohusika, fasihi, mafungamano, ndoa, michezo, ibada, sayansi na tekinolojia (ustaarabu).
Utamaduni pia ni mkusanyiko wa maarifa, itikadi, na tabia za wanadamu ambazo hutegemea sana
uwezo wa kuwasilisha mawazo na mafunzo ya kijamii kwa njia ya ishara.
Utamaduni ni jumla ya tabia za watu pamoja na akili, imani, sanaa, sheria, mila, dsturi, na tabia za
watu wa waishio katika jamii moja.
Nakwahivyo, Utamaduni ni jumla ya mitazamo , kaida, malengo na maadili yanayotambulisha asasi,
shirika, au kundi fulani la watu.
Ukilinganisha fasili hizo, utagundua kuwa utamaduni huwa ni tabia na mienendo ya watu wa jamii
fulani.

Mambo kuhusu utamaduni katika utendi wa fumoliyongo yatagusia vipengele kama imani, mila,
desturi, ndoa, lugha, michezo na burudani yapatikanayo katika utenzi huo huo. Yafuatayo ni baadhi ya
mambo hayo;
Utendi wa fumoliyongo umeegemea utamaduni wa imaani ya dini ya uislamu. Utendi wa Fumo
Liyongo, unatumia mianzo maalumu na kumalizia kwa miisho maalumu yenye dalili za dini ya
kiislamu. Utendi huo umeanza kwa duwa na kumalizia kwa duwa. Duwa hiyo, anaombwa Mwenyezi
Mungu Mmoja, ambaye ndiye Mwenye uwezo wa kila kitu. Aidha, katika duwa hizo, ametajwa Mtume

https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 6/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

Muhammad (S .A .W), ambaye ndiye Mtume wa mwanzo na wa mwisho katika ulimwengu huu. Kwa
mfano, ubeti wa kwanza, kuna duwa:
Bismillahi nabutadi
Kwa ina la Muhammadi
Nandikie auladi
Nyuma watakaokuya
Kutokana na ubeti huo wa kwanza, Utendi wa Fumo Liyongo, mtunzi anaanza jina tukufu la Bismilahi,
kisha, anamtaja Mtume Muhmmad (S.A.W). Hii ni desturi ya waumini wa Dini ya Kiislamu, ambapo,
kila jambo, hulianza kwa mtajo wa Allah (S.W), yaani  Bismi Llahi Rahmani Rahimi .
Vile vile, katika Utendi wa Fumo Liyongo, mtunzi anamalizia kwa kumuomba Mwenyezi Mungu
(S.W), katika ubeti wa 228 na wa 229, ili akirimiwe, na AIlah (Mwenyezi Mungu). Mfano;

228. Tumeziya kukhitimu


Hapo ndio wasalamu
Ilahi tatukirimu
Kwa Baraka na afiya
229. Rabbi tatusahiliya
Na uzito wa duniya
Tena tatujaaliya
Kuwa njema yote niya
Katika mifano hiyo hapo juu, mtunzi anamuomba Mwenyezi Mungu, Amuepushie uzito wa dunia.
Pia, anamuomba Mola, Aifanye vyema niya yake. Mwenyezi Mungu, Ameoneshwa kuwa, ndiye
Mwenye uwezo wa kila jambo kwa mja wake. Mifano hiyo inadhihirisha utamaduni wa imani ya
dini ya uislamu katika utendi wa fumoliyongo.

Kuna utamaduni wa serikali ya utawala wa kifalme katika utendi wa fumoliyongo.


Inasemekana kuwa babake liyongo alikuwa mfalme wa pate na alipofarika, kakake liyongo ajulikanaye
kama Daudi mrinngwari ndiye alilithi uongozi wa babake. Sultwani alikuwa mtawala wa Pate.
Mwanzo alikuwa na mapenzi na Fumo Liyongo.
Hata hivyo, mwisho alijenga uwaduwi mkubwa juu ya Fumo Liyongo. Mtawala huyo, ndiye
aliyefanya kila hila, ili amwangamize Liyongo;

207. Mfalume kipulika


Liyongo ametoweka
Nde mui meanguka
Haya aliazimia.
Mfalme huyo alikuwa ni muuwaji.
208. Fitina zikamngiya
Mfalume miya miya
Kwa hila kakusudiya
Kumuuwa fahamiya.
Beti hizo zinathibitisha serikali ya utawala wa ufalme katika utendi wa fumoliyongo.

Utamaduni unazingatia mfumo wa kuumeni.Tamaduni za waswahili zinamtaja Mwanamume kama


Mkimu Jamii katika utenzi wa fumoliyongo. Hili linadhihirika na tukio la kikoa na makoma, Fumo
Liyongo anapata usawiri wa kuwa mkimu jamii. Anajiunga na wanaume wenzake kukidhi hitaji la
jamii la chakula. Wanashirikiana kutungua makoma kwa zamu.
Katika beti zifuatazo tunafahamishwa namna walivyounda kikoa ili kuhakikisha jukumu lao la
kukidhia jamii linatekelezwa kwa utaratibu:
https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 7/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

56. Siku moya wakanena


natuleni waungwana
kikowa ni tamu sana
karamu ‘sotindikiya
57. Likisa shauri lao
wakenenda kwa kikao
mkoma waupatao
hupanda mtu mmoya
Doyle (1985:107) anadokeza kuwa mwanamume anapaswa kukimu familia kikamilifu kulingana na
matakwa na matarajio ya jamii ya kiasili. Wanakikoa walitaka kutumia tukio la kuunda kikoa kwa
nia mbaya ya kupata nafasi ya kumdhulumu Liyongo kwa kunuia kumwangamiza. Imebainika
wazi kwamba, Liyongo ametimiza matakwa na matarajio ya jamii kuwa mkimu wa jamii akiwa
mwanamume. Kwa hivyo, katika jamii ya kitamaduni ambayo huzingatia mfumo wa kuumeni,
Liyongo ana hadhi na haki ya kudai nafasi yake kama mwanamume, hususan katika jamii ya
Waswahili kwa sababu ametekeleza wajibu wake wa kukidhi jamii kama mwanamume. Asingepata
tunuku la hadhi ya mwanamume pasipo kutimiza jukumu hili.

Utendi wa fumoliyongo umetumia lugha ya kiamu. Utendi huo umetumia lugha ya asili, kutokana na
uasili wa kisa cha Fumo Liyongo.
Aidha, wanajamii, hiyo ndiyo lugha yao, waliyokuwa wakiitumia, na bado inatumika hadi leo katika
eneo hilo. Beti za 14 na 50 zinadhihirishia misamiati ya lugha ya Kipate kama ifuatavyo:

14. Ghafula kikutokeya


Mkoyo hukupoteya
Tapo likakuwiliya
Ukatapa na kuliya
15. Liyongo akatambuwa
Huzengea kuuwawa
Pale Pate kayepuwa
Barani akitembeya.
Beti hizo hapo juu, yaani ubeti wa 14 na 50, kuna matumizi ya maneno ya lugha ya Kiamu. Kwa
mfano, katika ubeti wa 14, neno  mkoya , lina maana ya  mkojo , na neno “ukakuwilia,” lina maana
ya “kutetemeka”. Aidha, katika ubeti wa 50, neno “kapepua” lina maana ya “akajiepusha”.
(Mulokozi, 1999) anasema kutoka ubeti wa kwanza hadi 56 zimetumia lahaja ya kiamu.

Utendi wa Fumo Liyongo umetumia, kwa kiasi kikubwa, misamiati ya Kiswahili cha Kiamu kama beti

184. kuwa liyongo mekwima


Uko nde ya kisima
Sasa watu wamekoma
Mai hawapati ndiya.

Utamaduni katika utendi wa fumoliyongo unaheshimu muda wa michezo na burudani. Hili


linadhihirika tunapoona fumoliyongo anaomba achezewe densi za gungu kabla ya kuuawa. kwamfano
katika ubeti wa 98.
98. Akajibu “usikhini”
Kamwambie sulutwani
Mwao nieutamani
Na gungu liwe pamoya.
https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 8/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

79. Liyongo nikwambiao


Shaha wa gungu na mwao
Tena ni mkuu wao
Huwashinda wut’e pia.
Beti hizi zinaonyesha aina za nyimbo na burudani kama kipengele kimoja cha utamaduni katika
jamii yao.

Mambo kuhusu uislamu katika utendi wa Fumoliyongo;


Utafiti unaonesha kuwa, Utendi wa Fumo Liyongo umebeba mambo ya dini ya Kiislamu wakati
Utendi huo unapoanza kwa mtunzi kuomba duwa kwa Mweyezi Mungu mmoja na kumaliza kwa
duwa. Nabii Muhammad (S.A.W), pia anasifiwa katika utendi huo.
Dua inatangulia maandishi ya utenzi wa fumoliyongo (ub 01) pia huwa ni njia mojawapo ya
kuimarisha imani ya Kiislamu.Aidha kwa mujibu wa Koran tukufu, dua ni kigezo muhimu sana katika
kuimarisha imani ya waumini wa dini ya kiislamu:
Kwa mfano;(ub 01)

1. Bismillahi nabutadi
Kwa ina la Muhammadi
Nandikie auladi
Nyuma watakaokuya
Kutokana na ubeti huo wa kwanza katika Utendi wa Fumo Liyongo, mtunzi anaanza kwa jina
tukufu la Bismilahi, kisha, anamtaja Mtume Muhmmad (S.A.W). Hii ni desturi ya waumini wa Dini
ya Kiislamu, ambapo, kila jambo, hulianza kwa mtajo wa Allah (S.W), yaani  Bismi Llahi Rahmani
Rahimi .
Vile vile, katika Utendi wa Fumo Liyongo, mtunzi anamalizia kwa kumuomba Mwenyezi Mungu
(S.W), katika ubeti wa 228 na wa 229, ili akirimiwe, na AIlah (Mwenyezi Mungu). Mfano;
2. Tumeziya kukhitimu
Hapo ndio wasalamu
Ilahi tatukirimu
Kwa Baraka na afiya
3. Rabbi tatusahiliya
Na uzito wa duniya
Tena tatujaaliya
Kuwa njema yote niya
Katika mifano hiyo hapo juu, mtunzi anamuomba Mwenyezi Mungu, Amuepushe na uzito wa
dunia. Pia, anamuomba Mola Aifanye vyema niya yake. Mwenyezi Mungu Ameoneshwa kuwa
ndiye Mwenye uwezo wa kila jambo kwa mja wake.
Chittick na Murat (1994) vision of Islam, wanasema “Kuwa mwanadamu kamili ni kutekeleza
matendo ya mungu alivyotenda.” Ni wazi kuwa maandishi yaliyomo, kwenye Koran yanatoa
mwongozo wa maisha jinsi mwislamu alivyostahili kuishi. Aidha mandishi yanamtaja fumoliyongo
kama kielelezo bora cha kuigwa hasa kwa waislamu.

Kuimarishwa kwa dini ya kiislamu; Matukio ya kushangaza katika Utendi wa fumoliyongo


yamejengwa ili kuimarisha imani ya waumini wa Kiislamu.
Mwandishi anaonyesha adhabu mbalimbali ambazo watu wanapewa ilikulipia matendo yao maovu.
Kwa mfano mtotowe liyongo alipomaliza kumsaliti babake na kumdunda shindano ya shaba,
alifukuzwa mjini pate na mwishowe akakumbwa na madhabu yaliyomwangamiza. (ub 179

https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 9/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

179. Kamtiya kitovuni,


Naye ulele kwa t’ani
Achamka hamuoni
Kiyana amekimbiya. 216, 213
180. mfalme kabaini
Kabisa huna imani
Epuka mwangu matoni
Na nyumbani nitokeya.
181. mfalme kamtowa
Nguo zakwe kamvuwa
Na watu akatukiwa
Khabari ikaeneya.)
Hayo yote yanatokana matendo maovu.Tukio hili na mengine ni kama onyo kali kwa waislamu
wasitende maovu ya aina hiyo.
Kwa hivyo imani ya dini yaoinaimarika.Waislamu wana imani kuwa wanadamu wote wanaotenda
kinyume na matakwa ya Allah wataadhibiwa vikali:
Utetezi wa binadamu ni ishara ya matendo mazuri katika Koran na hadith. Fumoliyongo katumwa
na nabii muhamed kama Mtume. Hili ni dhihirisho kuwa katika maisha ya sasa, Mungu huwateua
watu wake ambao anawatwika kusimamia binadamu, kama vile,fumoliyongo. Mungu ana
mamlaka ya kuchagua awapendao, na kuwapa majukumu yampendezayo. Liyongo ametumiwa
kudhihirisha utukufu wa Mungu kwani Mungu hapendezwi na nyoyo chafu, za akina Daudi
mringwari na mtoto wake liyongo aliyemsaliti.
Nguvu za mwenyezi mungu pia ni somo hasa kwa waumini waisilamu; Matukio yanayomkumba
Liyongo ni dhihirisho la nguvu za Mwenyezi Mungu. Kutokanana sifa tele za Fumoliyongo,
tunatoa rai kuwa yeye ametumiwa kama mwongozo bora kwa waumini wote wa Kiislamu. Jukumu
lake kuu ni kuwa kilelezo au mfano bora wa kuigwa kwa kila muumini kama watume.
Wakatimwingine, utendi wa Fumoliyongo umekiuka matakwa ya dini tukufu ya uislamu, kinyume
na mafundisho ya hadith na koran tukufu kama;
Matendo ya Sultan wa pate Bw Daudi mringwari kakake Fumoliyongo ya kumpangia njama za
kumwangamiza Liyongo yanayodhihirishwa na mwandishi katika utenzi wa fumoliyongo (beti 87,
71,53) yanakiuka na kuvuka mipaka na kuvunja sheria za hadith pamoja na Koran tukufu. Mtume
Mohamed(SAW) Alikuja kuokoa watu kuhubiri utendaji mazuri kwa wengine sio kutenda maovu,
kwamfano
182. Mfalme kawambiya
‘‘Liyongo kunipatiya
Kitwa mukanieteya
T’awapa riale miya’’
183. Mwambieni tusafiri
Hata pate tukajiri
Hapana tena khatari
Habari tumesikiya.
184. Akatiwa gerezani
Kafungiwa kijumbani
Asikari mlangoni
Kwa zamu wakachangaliya.
Mipango hiyo yote inayooneshwa kwenye beti hizi yanakiuka matakwa ya mtume muhamadi
kutendea watu maovu.
https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 10/11
4/5/23, 10:31 AM UTENDI WA FUMOLIYONGO – Jifunze Kiswahili na mwalimu Johnpaul Arigumaho

Pia, tendo la kumuoza liyongo kiholela na mke wa kigalla linakiuka mipaka ya ndoa katika dini ya
kiislamu ambapo muislamu anapaswa kuozwa kirasmi na kiongozi wa msikiti. (ubeti 45
185. Sharuti wakatimiza
Liyongo wakamuoza
Kwa furaha na kuteza
Nyumbani akaingiya.
186. mke katukuwa mimba
Akazaa mwane simba
Mwanamume wa kutamba
Mwane liyongo sikiya.
Tendo la mtoto wa liyongo la kumsaliti kwa kumdunda sindano ya shaba na kumuua haliambatani
na mafundisho ya dini ya kiislamu. (ubeti 179)
187. kamtiya kitovuni
Naye ulele kwa t’ani
Achamka hamuoni
Kiyana amekimbiya.
Mungu hapendezwi na nyoyo chafu, za akina Daudi mringwari na mtoto wake liyongo
aliyemsaliti. NakwahivyoWaislamu wana imani kuwa wanadamu wote wanaotenda kinyume na
matakwa ya Allah wataadhibiwa vikali.

Katika utenzi wa Fumoliyongo, kuna maswali ambayo pengo halijazibika ama hakika haikutambulika
wazi kama;

Muhamad kijumwa aliandika kuhusu utenzi wa Fumoliyongo kutokana na wenyeji wa mwambao wa


Kenya, je matendo ya liyongo ni ya kweli au mwandishi kaongeza utamu kwa kuweka zaidi ya
aliyoambiwa?
Hadithi inaanza kwa kutuelezea kuwa liyongo alikuwa anaishi mwituni hata kabla ya kuwa na
ugomvi na kakake mringwari, je kama mtoto wa kifalme kwanini aliamua kuishi mwituni na wadahalo
pamoja na makabila mengine sio pate kwenye Ufalme, huenda ulikuwa uongo?
Hatimaye, nakamilisha mjadala huu kwa kusema, uchunguzi zaidi kuhusu maisha na matendo ya
liyongo unahitajika kwa kutembelea hasa panaposemekana kuwa aliishi halafu historia yake
ikagunduliwa rasmi na wenyeji.

https://jifunzekiswahili.art.blog/2021/04/15/utendi-wa-fumoliyongo/ 11/11

You might also like