Professional Documents
Culture Documents
KF 319
KF 319
Main Menu
Gwivaha Motors
Dhanna za tamthiliya na drama hukanganya sana kwa sababu zimeingiliana sana. Ni kutokana na
kuingiliana huku baadhi ya wataalamu wamekuwa wakiifafanua dhanna ya tamthiliya kama drama na
kinyume chake. Hivyo, katika muhadhara huu tutajikita katika kufafanua dhanna hizi kama dhanna
tofauti.
Dhanna ya Tamthiliya
Mulokozi (1996:188):
Tamthiliya au drama ni fani ya fasihi iliyokusudiwa kutendwa jukwaani kwa ajili ya hadhira Fulani. Hivyo,
kwa lugha ya kawaida, tamthiliya huitwa mchezo wa kuigiza….Istilahi tamthiliya inatokana na neno
mithali ambalo lina maana ya mfano au ishara ya kitu. Hivyo, katika tamthiliya kitu kimoja humithilishwa
au huwakilishwa na kitu kingine.
Katika ufafanuzi huo swali tunalopaswa kujiuliza ni je, tamthiliya ni drama na kinyume chake?
Tamthiliya ni kazi ya kidrama na ya kimaongezi ambayo huigizwa mbele ya hadhira au kazi iliyoandikwa
kusomwa, kimuundo, tamthiliya hugawika katika matendo na maonesho, na mazungumzo huchukua
sehemu kubwa katika uwasilishaji wake na maudhui.
Katika maelezo hayo ni vigumu kubaini mpaka kati ya tamthiliya na drama. Mathalani, tunaweza
kujiuliza ni wakati gani tamthiliya inakuwa drama na ni wakati gani inaendelea kuwa tamthiliya? Hata
hivyo, Wamitila (2010)anatofautisha dhanna hizi kwa kueleza kuwa tamthiliya haiweki msisitizo mkubwa
kwenye suala la uwasilishaji wake jukwaani.
Tamthiliya ni ule utungo ambao unaweza kuwa umeandikwa au haukuandikwa, ambao unaliweka wazo
linalotaka kuwasilishwa katika umbo la tukio la kuliwezesha kutendeka mbele ya hadhira.
Kimsingi katika ufafanuzi huu inaonekana wazi kuwa tamthiliya ni utungo ambao unaweza kuwa
umeandikwa au haukuandikwa. Na kwamba utungo huo huwa na matukio ambayo yanauwezesha
kutendeka mbele ya hadhira. Kutokana na sifa hii ya kuweza kutendeka mbele ya hadhira, Mulokozi
(1996:188) anaiweka tamthiliya katika sanaa za maonesho, sanaa ambazo Muhando na Balisidya (1976)
wanasema ni kitendo chochote chenye sifa nne ambazo ni : Mchezo, mchezaji, uwanja wa kuchezea na
watazamaji.
Kutokana na maelezo hayo tunaweza kusema, tamthiliya ni andiko la kiuigizaji linalotoa simulio kwa
kuonesha maneno na matendo.
Dhanna ya Drama
Drama, kama ilivyo tamthiliya imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali. Miongoni mwa fafanuzi kuhusu
drama ni hizi zifuatazo:
Wamitila (2003) anaifafanua drama kama aina ya utanzu wa fasihi ambayo kimsingi hudhamiriwa
kuigizwa mbele ya hadhira. Anaendelea kueleza kuwa drama inaweza kuwa imeandikwa kama tamthiliya
au isiandikwe.
Kimsingi drama ni utanzu wa fasihi ambao unajidhihirisha katika utendaji. Utanzu huu umebuniwa kwa
ajili ya thieta kwa sababu wahusika hupewa majukumu ambayo huyaigiza katika jukwaa. Drama ni
mabadiliko, ubunifu na usawiri wa uhalisi katika jukwaa (Iwuchukwu, 2008). Kwa hivyo, msingi mkuu wa
drama ni tendo. Hoja hii inaungwa mkono na Mineke Schipper katika makala yake ya Origin and Forms
of Drama in African Context anapoonesha asili ya neno drama. Anasema:
Originally the ancient Greek word drama means, “action.” This term is said to be used for the first time
in connection with what we call drama, about 560 B.C by Greek Thepspis when he enriched his religious
singing and dancing choirs with costumed masked person who expressed a part of action in meaningful
words and gestures. Since that time drama has been the indication of that art which represents human
event in presence of more or less involved audience and which is focused on man.
Hoja hii pia inaungwa mkono na Aristotle ambaye anaifafanua drama kama uigaji wa kitendo. Katika
maana hii Aristotle anaihusisha drama na msukumo wa kuiga uliomo kwa wanadamu kwa mfano,
watoto wanapocheza baba na mama katika michezo ya watoto huwa wanaiga yale wanayoyaona katika
maisha yao ya kila siku. Hii ina maana kuwa uigaji ni sehemu ya maisha.
Hata hivyo, Betolt Bretcht anasisitiza kuwa, drama si uigaji wa kitendo pekee bali pia ni chombo cha
ufafanuzi wa hali za kijamii, si burudani pekee bali pia ni chombo cha mabadiliko ya kisiasa na kijamii.
Kutokana na maelezo hayo tunapaswa kufahamu kuwa, kitendo kinakuwa drama iwapo kitendo hicho ni
mwigo wa kitendo kilichotangulia. Kwa mfano, simulizi ya muwindaji ambaye anakwenda mwituni na
kuua swala na kasha kumpeleka maskani yake hata kama akiwa anacheza si drama. Simulizi hiyo hiyo
itakuwa drama kama itatendwa upya mbele ya hadhira ili kuburudisha au kuelimisha. Kijana anayetaka
kuwa mwindaji anaweza kujifunza kupitia uwasilishaji huo.
Drama za Kijadi
Kumekuwa na madai kutoka kwa wanazuoni wa Kimagharibi kuwa kabla ya ujio wa wageni (wakoloni),
Afrika haikuwa na drama. Madai haya yanaweza kuchukuliwa kuwa ni sahihi kwa kuwa istilahi “drama”
ni ngeni. Hata hivyo, madai haya yanapingwa na baadhi ya wanazuoni, miongoni mwao ni Mineke
Schipperi katika makala yake ya Origin and Forms of Drama in African Context anaposema:
It is of course not correct to use Western drama, in the way it has developed during last centuries, as
criterion to decide whether drama exists in other cultures or not! If for instance, language does not
dominate over all the other elements in the performance of a community this does not mean that there
exists no drama at all in this community, as it has sometimes been assumed in Western countries. One
should always take ito account the norms of the society itself with respect to the forms of drama it
appreciates and performs.
Kimsingi jamii ya asili katika Afrika, Tanzania ikiwamo, jamii ambayo utamaduni wake ulikuwa
haujaingiliwa na utamaduni wan chi za kigeni, ilikuwa na sanaa za maonesho (drama) ambazo
ziligawanyika katika makundi. Muhando na Balisidya (1976) wanataja na kufafanua makundi hayo kama
ifuatavyo:
· Sherehe :zinahusu kuingizwa kwa mwanajamii kwenye kundi la watu wa aina Fulani kutoka katika
kundi la watu wa aina ingine. Kwa mfano, jando na unyago, kutoa jina, kuota meno, kusimika viongozi,
n.k
Sherehe hizi ziliambatana na madaraka mapya yaliyomkabili mwanajamii katika kuingia kundi jipya.
Sherehe hizi, hasa huwa ni kukabidhiwa madaraka ambayo huwekwa katika umbo la vitendo, ukapewa
uzuri wa kisanaa ili uweze kudhihirika kwa mkazo zaidi.
· Ngoma: inaweza kuwa na maana ya chombo, sherehe au uchezeshaji wa viungo vya mwili. Ngoma
hizi ni zile ambazo hazikufungwa katika mfumo wa sherehe. Zina malengo ya kuburudisha, kwa hiyo
huchezwa wakati wowote wa furaha.
· Masimulizi ya Hadithi: Katika usimuliaji wa hadithi kuna vipengele vya drama/sanaa za maonesho.
Kwa upande mmoja, kuna msimuliaji ambaye ni mshairi, muigizaji, mwimbaji na mwanamuziki.
Ø Ni mshairi kwa sababu husanifu upya matini ya kijadi kwa kutumia uwezo wake, akili yake na ujuzi
wake wa fasihi ya jamii husika.
Ø Ni mwimbaji kwa sababu katika sehemu kadhaa zasimulizi yake huimba
Ø Ni mwanamuziki kwa sababu wakati mwingine hutumia vyombo vya muziki k.v. ngoma
Ø Ni muigizaji kwa sababu hutimiza majukumu mbalimbali kwa kutumia ubadilishaji wa sauti, mikono,
macho na viungo vingine vya mwili ili kutia mvuto katika usemi wake
Ø Kwa upande mwingine ni drama/sanaa za maonesho kwa sababu hadhira hushirikishwa katika hatua
mbalimbali.
· Kusalia miungu: Hii hutokea panapokuwa na hali ya kuikumbuka mizimu. Katika jamii mbalimbali
watu walielekeza kwa miungu mbalimbali, matatizo ambayo wao kwa nguvu zao za kibinadamu
yaliwashinda. Hivyo, kusalia miungu kulihusu jamii kuiomba iwaondolee matatizo yao. Na hii hasa ndiyo
ilikuwa dhanna iliyotendeka. Mitindo ya kusalia miungu ilitofautiana.
Waingereza ndio wa kwanza kuleta tamthiliya. Kazi za William Shakespeare za Julias Kaisari na Mabepari
wa Veniszilitumia vigezo vya Ki-Aristotle (Kimagharibi) ambavyo vina sifa kuu nne.
Ø Waigizaji-wahusika
Tamthiliya yoyote yenye kufuata muundo wa Ki-Aristotle husukwa katika mgogoro unaochukua muundo
ufuatao.
B D
A E
AINA ZA TAMTHILIYA
Tamthiliya, kama ilivyo kwa tanzu nyingine za fasihi, imegawanyika katika vitanzu au aina kadhaa. Hivyo,
katika kipengele hiki tutaangalia aina za tamthiliya.
1. Tanzaia/Tragedy
Hii ni tamthiliya yenye huzuni inayogusa hisia za watazamaji/wasomaji kiasi cha kuogopesha na
kumwonea huruma mhusika mkuu ambaye hupatwa na janga (Semzaba, 1997). Mhusika mkuu huwa ni
maarufu, mbabe au shujaa atokaye tabaka la juu. Mtu wa nasaba bora na ambaye huwa anajaribu
kubadilisha hali yake na ya jamii inayomzunguka. Katika hatua yake hiyo hujikuta amefanya kosa au
amefanya uamuzi usio sahihi, uamuzi ambao husababisha anguko lake.
· Shujaa lazima awe mtu mwema, sura nzuri, umbo zuri ili yanayomtokea yasitarajiwe
· Watu huonesha kuumia, kusikitika, n.k kadri mtu anavyoonekana mwema au mzuri wa umbo
· Anguko la shujaa huja kutokana na uamuzi wake au kosa lake mwenyewe
Neno hili linatokana na maneno mawili ya Kiyunani, yaani Tragos lenye maana ya mbuzi na aeidein lenye
maana ya kuimba.
· Zawadi ya mbuzi ilikuwa ikitolewa kama tuzo kwa mshindi wa nyimbo za kikorasi
· Kutokana na hoja ya pili, hoja ya tatu inaibuka kuwa: waimbaji na wachezaji katika miviga ya
kidithramb walivalia ngozi za mbuzi na wakaonekana kama mbuzi wa kafara na mmoja wao alifanya
uigizaji bubu akionesha mateso na kufa na kuibuka upya kwa shujaa. Kutokana na kuuawa kwa mbuzi,
watu wanakuwa na huruma, hivyo wanavaa ushujaa na kuvaa vazi la mbuzi na kufa kama mbuzi na
kuibuka na ushindi.
Hoja ya pili inaweza kuwa na mashiko zaidi kwani ilihusisha kifo cha mnyama kama kafara au mwigo
wake ambao ulileta huzuni ya kifo cha shujaa.
Katika Poetics, Aristotle anaandika kuwa tanzia ilikuwepo kutokana na ufaraguzi uliofanywa na viongozi
wa miviga ya kidithramb ambayo ilihusisha nyimbo na ngoma za kumtukuza Dionizius- mungu wa
mvinyo na rutuba/uzazi.
Lakini katika Poetics ndipo Aristotle anapotoa ufafanuzi wa tanzia kama ijulikanavyo leo, kuwa ni:
· Utungo wa kisanaa ambao unawasilisha anguko la mtu shujaa au mwema kutokana na kosa la
kufisha alilolitenda au kutokana na uamuzi wake mbaya.
· Ni mambo ambayo yanamletea mateso na uchungu mhusika shujaa na katika kuanguka huko,
hadhira inashikwa na woga na kumwonea huruma shujaa.
Kadri jamii ilivyoendelea ndivyo sanaa ilivyoanza kuwekewa sifa bainifu na hata sharia. Na kwa hiyo,
hata ufafanuzi wake uliegemea katika kuonesha sifa maalumu zinazofanya utungo uwe wa kitanzia. Kwa
mkabala huu, Aristotle katika Poetics anasema:
· Na kwamba njia ya kutolea tanzia ni drama, sio nathari (usimulizi) kwa kuwa drama inaonesha kuliko
kueleza.
· Ni tukio la kisanii la kifalsafa zaidi na la kiwango cha juu kabisa kuliko historia. Historia hueleza kile
kilichotokea. Tanzia huonesha kile kinachoweza kutokea ikiegemea katika sharia ya uwezekano na
ulazima (the law of probability and necessity)
· Tanzia ni mwigo wa tukio la dhati, lenye ukubwa na ubora wa kisa kinachojitosheleza, wenye kubeba
lugha na umbo maalumu lenye misingi sita ambayo ndiyo inayoelezea ubora wake.
Ø Ploti:
· Sio hadithi yenyewe, bali ni jinsi mfumo wake ulivyo, jinsi hadithi inavyoelezwa ilivyosukwa. Muundo
wake ambao hupaswa kuwa na mwanzo, kati na mwisho.
· Ni lazima iwe ya kiwango Fulani maalumu, kwa ubora wake na ujazo wake. Sio fupi, iwe ya
kiulimwengu. Tukio linaloweza kutokea popote.
· Kuwe na mabadiliko katika bahati na mageuko ya nia – perpeteia. Nia inageuzwa na kutaka
kurudishwa katika hali ilivyokuwa.
Ø Wahusika
· Jinsi wao wenyewe wanavyojituma wakionesha uhusika wao na kuleta athari kwa hadhira
· Mhusika shujaa awe ni mtu maarufu ili mabadiliko ya bahati yake yakitokea (toka hali nzuri kuwa
mbaya) yaweze kuleta athari ya huruma.
· Anguko la shujaa huletwa na kosa analolitenda, yaani hamartia. Kosa la kufisha la kutesa na kutia
uchungu.
· Anguko hili hutokea sio kwa sababu shujaa ni mkosaji, au ana dhambi, bali kwa kutojua kiasi cha
kutosha. Ni matokeo ambayo hayana budi kuwa kutokana na sharia ya uwezekano. Kwa mfano kisa cha
Edipode katika tamthiliya ya Mfalme Edipode kilichohusu ndoto iliyoanza na baba yake kuwa atapata
mtoto wa kiume ambaye atamuua baba yake na kumuoa mama yake na hatimaye kuleta laana katika
jamii nzima.
· Katika kutapatapa, peripeteia inatokeza anguko zaidi. Ili kupata peripeteia, ni lazima jambo Fulani
liachwe kabisa na kugeukia lile la awali, yaani kubadili nia kabisa.
Ø Uneni:
· Ni namna maneno yanavyosemwa na kuunda maana
· Uneni lazima uwe ni sahihi katika muktadha ule na kwa jinsi unavyotolewa kuhusiana na anavyoutoa,
ploti na tukio la kitanzu.
Ø Wazo
· Ni wazo linaloonekana au la
Aristotle anasema mwanadamu anayetoka tabaka la juu ndiye anayeweza kuwa na hilo wazo au pia
anaweza asiwe nalo.
Ø Mahadhi
· Ni wimbo kama alivyotumia Shakespearekatika kazi zake ambapo anaishia na wimbo, tofauti na kazi
za Kiswahili ambazo zinaanza na wimbo kwa mfano katika Lina Ubani, Penina Muhando ameanza na
wimbo wa bibi mwanzoni. Lakini pia katika tamthiliya ya Kilio Chetu watunzi wameishia na wimbo.
Wimbo una dhima ya kuliwaza na kupoza machungu.
Ø Shani
· Ni kule kuguswa kwa namna Fulani na wimbo. Ni ule utokeaji unaogusa mtu akawa na hisia na
msisimko. Aristotle anasema lazima tanzia iwe na shani.
Peripeteia
· Ni neno la Kiyunani ambapo mtu na kwa muktadha wetu, mhusika katika tamthiliya hubadili nia
iliyopaswa kuwa njema na kurudisha kinyumenyume dhamiri iliyokuwa iwe na matokeo mazuri.
· Mhusika hufanya tukio au kuchukua hatua ambayo humtoa katika usalama na kumwingiza matatani.
Kwa mfano, unapokuwa na nia ya kwenda kumsalimu rafiki yako, halafu ghafla unabadili nia na kwenda
kwa mchumba wako. Balaa unalolipata kule kwa mchumba wako linatokana na wewe kubadili nia yako
ya awali ya kwenda kwa rafiki yako. Na hii ndiyo Peripeteia.
Anagnorsis
· Dhanna nyingine inayoenda sambamba na Peripeteia ni Anagnorsis. Balaa ya mhusika mkuu kubadili
nia yake ya awali na kuamua kwenda upande wa pili au kuamua kufanya tukio jingine ambalo bila yeye
kujua litamwingiza matatani, inafikia wakati sasa anatambua ah!! Nimefanya uamuzi ambao sio sahihi.
Huko kugundua ndiyo Anagnorsis yaani tukio la mwanzo la kupata ufahamu.
· Mhusika mkuu hutambua kuwa amejiingiza matatani kutokana na hatua moja au nyingine. Kwa
mfano, unapomwacha mchumba wako mzuri, mwenye mapenzi ya dhati na kuamua kuolewa na jibaba
lenye pesa zake kwa kudanganywa. Pale unapogundua oh! Kumbe huyu ni mume wa mtu….. hiyo ndiyo
Anagnorsis.
· Kwa mfano katika Mashetani, baada ya binadamu kumuua shetani anaanza kujiuliza maswali fulani ya
kujuta na ansema laity angefuata ule uamuzi wake wa mwanzo.
· Kwa hiyo Peripeteia unabadili nia na kuingia upande wa pili, na katika upande wa pili unagundua
umekosea (anagnorsis)
Hamartia
· Baada ya kubadili nia (Peripeteia) na kugundua kuwa amekosea (anagnorsis), mhusika mkuu hufanya
kosa fulani na kosa hilo ndio Hamartia.
· Mhusika hukosea sio kutokana na kosa la kimaadili, bali zaidi kosa la kiutendaji au kiufundi, yaani mtu
kulenga vibaya shabaha na kupiga sehemu tofauti na kuzua balaa.
· Kwa mfano unapotaka kumuua nyoka, badala ya kumpiga kichwa unampiga mkia au unampiga
kidogo. Matokeo yake atakugonga wewe.
· Kosa la namna hii hujutiwa sana na mhusika mkuu kwa sababu huwa ni kosa la kiuamuzi, dhambi au
matendo maovu na kosa hili ndilo husababisha anguko au kifo cha mhusika mkuu.
· Kwa mfano Mfalme Edipode anapogundua kuwa amemuua baba yake na kumuoa mama yake
anaamua kujitoboa macho.
Katharsis (Utakaso)
· Ili mtu ajiondoe katika hamartia hupaswa kujitakasa na kujitakasa ni kwa kihisia. Tukio hili hujulikana
kama Katharsis.
· Ni tukio au hali ambapo hisia za hadhira au mhusika hubadilika kabisa kutoka katika hisia za
masikitiko, huzuni, majonzi au furaha kuu na kuwa kinyume chake.
· Kwa mfano katika Mashetani, mwisho kabisa Juma anakataa kubadilisha nafasi yake na kuwa
binadamu na Kitaru anasikitika sana kuwa alidhulumiwa sana kwa kucheza nafasi ya binadamu, na
alitaka kujitakasa kwa kucheza nafasi ya shetani na yeye, lakini bahati mbaya Juma alikataa.
Hubris
· Ni matukio au matendo ya kujitapa kupita kiasi au kupindukia na kuonesha kuwa anayejitapa ametia
chumvi mno hata kukiuka uhalisia ulivyo. Kujitapa huwa zaidi kuelekeza kukashifu au kudharau miungu
au Mungu.
· Hii hasa huwapata watu wenye uwezo fulani (wanasayansi,wasomi, n.k) au wenye vyeo na mamlaka.
· Kutokana na hali hii, hubris huonekana kuwa kama dhambi maana huvuka mipaka ya hali ya
kawaida. Kutokana na kutapa huko, husababisha anguko na mateso badaye.
· Kwa mfano katika Mashetani uk. 9, wako wapi waliokuwa wakijitaoa? Binadamu anacheka hadi
kicheko kinamlevya, nah ii ni baada ya kudhani kamuua shetani kumbe wala hakuwa amemuua.
· Hubris inahusishwa na miungu na kujitapa huku baadaye mhusika huyo lazima apate matatizo.
· Kujitapa huku kiasi wakati mwingine huwa ni kwa sababu anayejitapa huwa hana uelewa wa kutosha
au pengine ni kujisikia kulikopita mipaka.
Nemesis
· Kutokana na hali hii, anayesemwa ana hubris hujikuta uso kwa uso na Nemesis yaani kupata
kilichostahiki kwa uwiano, kiwe kizuri au kibaya.
· Nimesis alikuwa malaika wa Kigiriki na alikuwa akiongeza na kupunguza mambo mbalimbali ikiwa
hali ni wingi kupita kiasi, hupunguza na ikiwa ni kidogo mno huongeza. Kama ulikuwa ukijitapa kwa
sababu ya uwezo wako mkubwa basi unapunguzwa.
· Kwa mfano huko Marekani, kupigwa kwa Pentagon, Marekani ilikuwa ikijitapa sana hadi ikakufuru
kwamba hakuna vita iliwahi fanyika nchini humo. Baada ya pigo hilo Marekani ikaweka uwiano, yaani
kwenye uwiano sawa nan chi zingine (ikatoka kwenye kujisifu kuwa nchi isiyoguswa).
2. RAMSA/KOMEDIA
· Ramsa ilikuza sana elimu kuhusu ngono na ushindi wa mungu wa mapenzi – eros. Sigmund Freud
ameandika sana kuhusu hili katika nadhariya yake ya Psycho Analysis.
· Aristotle alisema mahali pa tanzia ni katika mapigano au katika jukwaa wakati mahali pa ramsa ni
bafuni au chumbani – kitandani
· Kutokea katika mwanzo huu, waigizaji wengi walifanya vichekesho mwanzoni wakianza na vinyago
vya uume.
· Kutokana na hali ilivyokuwa hapo kale, kwa kuwa Komosilihusika na vichekesho tu, mwisho wake
ukawa ni vichekesho. Mwisho huu ukachukuliwa kuwa ndio kiini kikubwa cha sanaa ya kiramsa.
· Kwa hiyo, maana ya ramsa ya awali ya kuelekea viungo vya uzazi ikabadilika na hatimaye Aristotle
akaandika kuwa ramsa ichukuliwe kuwa ni tukio/hadithi inayohusu kuinuka kwa kibahati tu kwa mhusika
anayevutia hisia za hadhira au anayehurumiwa na hadhira au anayependwa na hadhira.
· Komedia inatokana na neno Komedia la Kigiriki linalomaanisha sehemu ya kiungo cha uzazi cha
kiume. Ni uneni unaolenga kuleta furaha na kicheko. Ni utanzu wa maigizo ambao unalenga kumfanya
mhusika mhurumiwa kuwa na ushindi utakaoleta kicheko.
· Leo dhanna ya ucheshi imetoka katika viungo vya uzazi na kuzingatia zaidi onesho linaishaje kama
onesho, ramsa huishia na “wakaishi raha mustarehe”.
· Ramsa ni mafanikio yaliyojaa ucheshi ya mhusika mkuu ambaye alionekana mwenye bahati mbaya
na hadhira ikimsikitikia.
· Shujaa wa ki-ramsa sio lazima awe mtu maarufu au mbabe/shujaa. Anaweza kuwa mtu wa kawaida.
Wahusika wengine pia katika ramsa ni watu wa kipato cha kati na chini kama vile: washona viatu, wauza
mitumba, wachoma mishikaki, waalimu, wanafunzi, n.k na dhamira katika ramsa zinahusu watu hawa.
Aristotle anasema shujaa wa ki-ramsa:
- Mtu ambaye katika jamii huwa duni na matendo yake ni ya kiucheshi-ucheshi, ila historia humleta
na kumkuza hata akatoka akawa “fulani” akaishi raha mustarehe.
- Ni mhusika ambaye akifanikiwa kila mtu atafurahia na kutoka akiwa ameridhishwa na mwisho huo.
SIFA ZA RAMSA
· Ni lazima onesho livutie akili na siyo hisia au mihemko
· Ni lazima kuwe na matendo bila kufikiria, kana kwamba mtendaji haba habari
· Ni sharti kuwe na desturi/mila ambazo hadhira inazifahamu toka katika jamii yake
· Inaonesha haja ya kuikomboa nafsi, yaani huona kuwa pamoja na uwepo wa kifo maisha bado yapo
na ya thamani.
Aina za ramsa
v Utani/Vichekesho (Farce)
v Mapenzi/Mahaba (Romance)
- Wapendanao huwekewa vikwazo kama pesa, kabila, hadhi, dini, lakini hatimaye huvishinda vikwazo
hivyo.
v Tashititi/Dhihaka (Satire)
- Mhusika mkuu (ambaye ni kiongozi) huwa na sifa hizo. Anadhihakiwa ili aache rushwa, utapeli,
udhaifu, n.k
- Ramsa hizi ni kama njia ya walalahoi kutoa malalamiko yao kwa viongozi wao.
KWA UJUMLA:
Tanzia ni kinyume cha Ramsa kwa maana kwamba, badala ya kuonesha kuinuka na kufanikiwa kwa
mhusika duni wa tabaka la chini asiyetarajiwa, tanzia huonesha kuanguka na kushindwa kwa mhusika
maarufu, mbabe au shujaa atokaye katika tabaka la juu, mtu wa nasaba bora.
Kwa hiyo, undani hasa wa maana ya ramsa sio tu onesho kumalizika kwa kicheko bali zaidi onesho
kumalizika kwa mafanikio ya mhusika aliyeonekana kutofanikiwa.
3. TANZIA-RAMSA
· Ni tamthiliya inayoishia kwa furaha, yaani inachanganya vipengele vya kitanzia na vya kiramsa.
· Hutumiwa sawa na tamthiliya za kibwege ambazo huonesha kuwa kicheko/furaha ndiyo jibu pekee
kwa watu ambao hawana imani na maisha kwa sababu misingi thabiti ya maisha imeondolewa kama
inavyodhihirika katika tamthiliya ya Amezidi.
CHIMBUKO:
ØUlaya: drama ilitokana na miviga (rituals) na viviga (rites) vya kidini katika jamii ya kale ya Wayunani.
Miviga iliambatana na duru za: kuzaliwa, kufa, kuoza na kuzaliwa upya. Duru hizi zilihusishwa na Mungu
aliyeitwa wa Wayunani aliyeitwa Dionizi.
ØIndia: drama ilitokana na tendi za kidini Mahabharata na Ramayana pamoja na miviga iliyoambatana
na utendaji wa tendi hizo katika mahekalu ya Kihindi.
ØChina na Japan: drama ilitokana na dansi za miviga ya kidini. Baadaye drama hizo zilijitenga na udini na
kuanza kushughulikia masuala ya sanaa na burudani.
ØAfrika: maigizo ya kitamthiliya yalikuwa huko Misri, ambako miviga iliyohusu kufa na kufufuka kwa
Mungu wa Misri, Osiris, ilikuwa ikiigizwa kila mwaka kwa miaka kama 2000 (Brocket, 1979 katika
Mulokozi, 1996).
- Pia kulikuwa na maigizo yasiyoandikwa ambayo yalikuwa ni sehemu ya matendo ya kijamii k.v
miviga, viviga na ngoma.
Kabla ya kuona maana ya sanaa za maonesho, tuone kwanza aina za sanaa za maonesho. Balisidya na
Muhando, P (1976) katika Fasihi na Sanaa za Maonyesho wanatoa aina tatu za sanaa za maonesho.
· Sanaa za uonesho
Ni aina ya sanaa ambayo uzuri wake umo katika umbo la kudumu, mfano mkeka, vyungu, nyumba, n.k
· Sanaa za ghibu
Ni sanaa ambazo uzuri wake umo katika umbo la kugusa hisia, mfano wimbo, shairi.
· Sanaa za vitendo
Ni sanaa ambazo uzuri wake umo katika umbo la vitendo. Ni lazima uone vitendo vikitendeka.
Sanaa za maonesho: ni sanaa za vitendo ambavyo ni lazima viwe na sifa muhimu ambazo ni:
- Mchezaji/mtendaji
- Uwanja wa kutendea
- Mchezo wenyewe
- Watazamaji/hadhira
Ø Huegemea zaidi katika maandishi. Kwao kisichoandikwa hakina nguvu. Walitumia maandishi ili
waafrika waonekane washenzi, wajinga wasio na maandishi mf. Biblia
TAMTHILIYA ZA KIAFRIKA
· Hutumia vipengele vya fasihi simulizi na hazina vipengele vya Ki- Aristotle mf. Tamthiliya ya
Lina Ubani
· Huwa na ukiukwaji wa Uaristotle. Upangaji wa waletao mgogoro ni tofauti mf. Sio lazima
awe ni mbabe au mkinzani
· Mshindi sio lazima awe mbabe, anaweza kuwa mdogo mf. Daudi katika Biblia
Ingawa asili ya tamthiliya katika nchi mbalimbali yaelekea kufanana lakini maendeleo yake yalichukua
mikondo tofauti kutegemeana na historian a utamaduni wa jamii inayohusika. Katika kipengele hiki
tutajikita katika kuangalia maendeleo ya tamthiliya ya Kiswahili kihistoria kama ilivyofafanuliwa na
Mulokozi (1996).
1. Kabla ya Ukoloni
· Zilikuwepo zisizoandikwa, yaani drama zilizoigizwa kwa ajili ya ajili ya kuoneshwa kwenye shughuli
maalumu k.v jando na unyago, kutawazwa viongozi, harusi, mazishi, n.k
Tamthiliya za kizungu
Ø Zilikusudiwa ama kuwaburudisha maofisa na masetla wa Kizungu, ama kufunza Biblia na imani ya
Kikristo
Ø Kenya: zilianza kuigizwa Nairobi na Mombasa kabla ya vita vikuu vya kwanza vya dunia
Ø Tanzania: zilianza kuigizwa shuleni miaka ya 1920, zilitokana na michezo iliyoandikwa na Waingereza
k.v Shakespeare
Ø Zilikuwa za kibwanyenye na chache zilifasiriwa kwa Kiswahili mf. Tabibu Asiyependa Utabibu
Ø Pia vilianzishwa vikundi vya kuigiza tamthiliya za Kizungu k.v Tanzania : Dar es Salaam Players (Little
Theatre, 1947) na Arusha Little Theatres (1953). Kenya:kulikuwa na National Theatre (1952)
iliyotawaliwa na michezo ya wageni hadi miaka ya 1970.
Vichekesho
Ø Nyingi zilikuwa za kidini na ziliandikwa ili kuigizwa tu shuleni na makanisani mf. Imekwisha ya C. Frank
(1951)
Ø Michezo ya mwanzo kabisa ni: Afadhali Mchawi (1957) na Mgeni Karibu (1957) michezo hii iliigizwa
kati ya 1954-1956
Ø Juhudi za Hyslop zilibainika katika vipawa vya wanafunzi wake kwa mf Henry Kuria aliandika tamthiliya
iliyoitwa Nakupenda Lakini…. Iliyoigizwa mwaka 1954 na kuchapishwa 1957
Ø Baada ya Henry Kuria motisha ya kutunga ilishika kasi: Gerishon Ngugi, Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi
(1961) iliyoigizwa 1956; Nyoike, Maisha ni Nini iliyoigizwa mwaka 1955; Kurutu, Atakiwa na Polisi (1957).
· Tamthiliya ya Kizungu
Ø Tamthiliya muhimu zilianza kutafsiriwa mf Juliasi Kaisari na Mabepari wa Venis (J.K. Nyerere);
Makbeth na Tufani (S.S. Mushi)- zote za Shakespeare. Sophocles, Mfalme Edipode (S.S. Mushi); Mkaguzi
Mkuu wa Serikali (C. Mwakasaka); n.k
Ø Pia tamthiliya za kiafrika zilizoandikwa kwa lugha za kigeni na lugha nyingine zilifasiriwa mf Ngugi wa
Thiong’o: Mtawa Mweusi, Soyinka, W: Masaibu ya Ndugu Jero (A.S Yahya); Ngugi wa Thiong’o na
Ngugi wa Mirii: Nitaolewa Nikipenda, n.k
· Vichekesho
Ø Vilichukua sura tofauti. Badala ya kuwasuta washamba vilianza kuwasuta wazungu weusi
Ø Hujaribu kuzungumzia matatizo ya watu wa kawaida k.v matatizo ya kifamilia, ukosefu wa kazi,
UKIMWI, uhalifu, n.k
Ø Vipo vya kisiasa vilivyozungumzia siasa ya ujamaa, ubinafsiwa viongozi, matatizo ya kuanzisha vijiji vya
ujamaa, n,k
ü E. Hussein: Kinjekitile (1969), Mashetani (1971), Jogoo Kijijini na NGao ya Jadi (1989), Arusi (1980),
Kwenye Ukingo wa Thim (1989)
ü P. Muhando: Hatia (1972), Tambueni Haki Zenu (1984), Pambo (1975), Nguzo Mama (1982), Lina Ubani
(1984), n.k
ü E. Mbogo: Giza Limeingia (1980), Tone la Mwisho (1981), Ngoma ya Ng’wanamalundi (1988), Morani
(1993), Sundiata (1995), n.k
Hawa ni baadhi tu ya watunzi kutoka Tanzania. Huko Kenya watunzi wapya walikuwa wengi. Miongoni
mwao ni Thomas, M : Bahati Nasibu (1971); C.N Chacha : Mke Mwenza (1982) na Wingu Jeusi; Jay
Kitsao: Uasi (1980), Tazama Mbele (1981), Malimwengu Ulimwenguni (1983) na Bibi Arusi (1983), n.k
Baada ya kazi mbalimbali za kigeni kutafsiriwa, na kama ambavyo tunafahamu kuwa tamthiliya hizo
zilikuwa na athari ya kiaristotle, tamthiliya ya Kiswahili iliathiriwa katika mambo mbalimbali. Sambamba
na kuibuka kwa waandishi wengi wa tamthiliya lakini pia tamthiliya hizo za Kiswahili zilizotungwa
zilikuwa na athari mbalimbali za tamthiliya za kigeni kwa mfano suala la muundo, mtindo, dhanna ya
umchezo kwa sababu awali drama zetu zilikuwa na udhati, masuala ya ujenzi wa wahusika na kadhalika.
Rejelea sifa za kiaristotle na jinsi zinavyojidhihirisha katika tamthiliya mbalimbali za Kiswahili.
Dhanna ya fasihi ya majaribio inaibuka katika tamthiliya na pengine katika riwaya pia kutokana na athari
ya fasihi ya kimagharibi ambayo ilionekana kumeza kabisa fasihi ya kiafrika. Juhudi za watunzi wazawa
kujirudisha katika utunzi wenye ladha na asili ya kiafrika ndio msukumo wa kuwepo kwa fasihi
inayochanganya vipengele vya kifasihi simulizi katika fasihi andishi na hivyo kuifanya fasihi andishi yenye
misingi ya kimagharibi kuwa na vionjo vya kiafrika.
· Watunzi wengi wa tamthiliya ya Kiswahili wanaiga mbinu na kanuni za tamthiliya ya Ulaya, hasa ya
Ki-Aristotle
· Walianza kuchota mbinu kutoka katika sanaa za jadi za kiafrika, hivyo wakaanzisha tamthiliya ya
majaribio
· Mfano, E. Hussein alijaribu kutumia utambaji wa ngano katika maigizo yake ya Ngao ya Jadi na Jogoo
Kijijini.
· Hali hiyo imeleta mabishano miongoni mwa wataalamu iwapo tungo hizo mbili ziitwe tamthiliya au
tendi.
· Pia P. Muhando katika Lina Ubani na Nguzo Mama alijaribu kutumia mbinu ya utambaji wa ngano.
· Majaribio katika tamthiliya ya Kiswahili bado yanaendelea. Mbinu nyingi zinaendelea kutumika ili
kuifanya tamthiliya ya Kiswahili iendane na utamaduni na mazingira ya Kiafrika.
Geivaha Motors
TAGS:
ALL
RELATED POSTS
TAFSIRI NA UKALIMANI
NEXT
TAFSIRI NA UKALIMANI
FASIHI YA KISWAHILI, NADHARIYA NA UHAKIKI (T.S.Y.M. Sengo)
PREVIOUS
POPULARRECENTCOMMENTS
Dhana ya Nadharia
Dhana ya Nadharia
MAUDHUI
MAUDHUI
BLOG ARCHIVE
► 2021 (45)
► 2018 (674)
▼ 2017 (1504)
► December (2)
► November (206)
► October (284)
► September (277)
► August (64)
► July (76)
► June (4)
► May (146)
► April (114)
▼ March (89)
HEKAYA ZA ABUNUWASI
Sudan
Western Africa
States of Sudan
English Revolution
French Revolution
French Revolution
FRENCH REVOLUTION:
French Revolution
History of capitalism
UTOPIAN SOCIALISM
Utopian Socialism
Utopian socialism
MJENGO WA TUNGO
History of colonialism
Precolonialism
Colonialism
Education
TAFSIRI NA UKALIMANI
NOMINO ZALIKA/UNOMINISHAJI
PHYSICS PRACTICALS
How to Use a Microscope | STEM
COMPOUND MICROSCOPE
Column chromatography
► February (162)
► January (80)
► 2016 (1)
► 2015 (631)
► 2014 (136)
TOTAL PAGEVIEWS
5374231