You are on page 1of 3

UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI

Uhakiki ni kazi au kitendo cha kutafakari, kuchambua na kufafanua kazi ya Fasihi ili kuweka
bayana maadili na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi. Hivyo mhakiki sharti asome kazi ya
fasihi andishi au kusikiliza masimulizi Kwa makini ili aweze kuyahakiki Mhakiki ni mtu
anayejishughulisha na kazi za kisanaa hususan za kifasihi Za wasanii asilia.
VIPENGELE VYA FANI NA MAUDHUI KATIKA KAZI ZA FASIHI ANDISHI:
a) MAUDHUI.
Maudhui katika kazi ya Fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumziwa Pamoja na
mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui Hujumlisha mawazo, pamoja na
mafunzo mbali mbali yaliyomsukuma Msanii hadi kutunga kazi Fulani ya Fasihi.
Vipengele vya maudhui:
DHAMIRA
Hili ni wazo kuu au mawazo mbali mbali yanayojitokeza katika kazi ya Fasihi ambayo
mwandishi huyajengea hoja. Dhamira hutokana na jamii na Zipodhamira kuu na dhamira
ndogo ndogo. Dhamira kuu ni zile za kisiasa, Kiuchumi na kiutamaduni. Dhamira kuu ndicho
kiini cha kazi ya fasihi na
Dhamira ndogondogo ni zile zinazoambatana na dhamira kuu.
MIGOGORO
Migogoro ni mivutano na misuguano mbali mbali ambayo huibuliwa na Mwandishi katika
kazi ya fasihi. Mgogoro kati ya wahusika ama vikundi vya Wahusika, familia zao matabaka
yao n.k.
UJUMBE NA MAADILI
Ujumbe katika kazi ya fasihi ni mafunzo mbali mbali yapatikanayo baada ya Kuisoma kazi
ya fasihi. Ujumbe huwa sanjari na maadili mbali mbali Ambayo mwandishi amekusudia jamii
iyapate.
FALSAFA:
Huu ni mwelekeo wa imani ya msanii. Msanii anaweza kuamini kuwa, Mwanamke si kiumbe
duni Kama wengine wanavyoamini au, kwa wale Wapinga usawa, wanaweza kuwa na falsafa
ya kumwona mwanamke kuwa Kiumbe duni au chombo cha starehe.
MSIMAMO:
Hii ni hali ya mwandishi kuamua kushikilia na kutetea jambo Fulani bila Kujali kuwa jambo
analolishikilia linakubalika au la.
MTAZAMO
Ni jinsi msanii anavyoyatazama mambo katika ulimwengu wa kifasihi. Hapa tunapata
mitazamo ya aina mbili.
a) Mtazamo wa kiyanifu ambao unaegemea katika kuyajadili mambo Kiuhalisia,
msanii mwenye mtazamo huu hujadili mambo kama Yanavyojitokeza katika jamii.
Kwa ujumla mtazamo huu Hushadadiwa sana na wanasayansi ambao huhitaji
kuthibitisha Kila kitu kisayansi.
b) Mtazamo wa kidhanifu, huu una misingi yake katika kudhani kuwa Mungu ndiye
suluhisho la kila kitu hivyo waandishi wenye Mtazamo huu hujibainisha wazi kupitia
kazi zao hasa kwa kujadili Mambo kiujumlajumla mathalani “kuon a kuwa mapenzi
bora Ndiyo suluhisho la matatizo katika jamii” huu ni mtazamo wa Kidhanifu.Wengi
wa wanadini hufuata mtazamo huu.
FANI
Fani katika fasihi ni ule ufundi wa kisanaa anaoutumia msanii katika Kufikisha ujumbe wake
kwa jamii inayohusika.
VIPENGELE VYA FANI
MUUNDO
Ni mgawanyo, mpangilio na mtiririko wa kazi hiyo kwa upande wa visa Na matukio. Ni jinsi
msanii wa kazi ya fasihi alivyoifuma, kuiunda na Kuunganisha tukio moja na lingine, sura
moja na nyingine, ubeti na ubeti, na Hata mstari wa ubeti na mwingine.
AINA ZA MIUNDO:
a) Muundo wa moja kwa moja/msago, Huu ni muundo wa moja kwa Moja ambao
matukio huelezwa kwa kuanza la mwanzo hadi la Mwisho. Kwa mfano, mhusika
huzaliwa, hukua, huchumbia au Huchumbiwa, huoa au huolewa, huzaa watoto,
huzeeka, hufa.
b) Muundo wa kioo/rejea, Huu ni muundo unaotumia mbinu rejeshi Ambayo huweza
ama kumrudisha nyuma msomaji wa kazi ya Fasihi katika mpangilio wa matukio yake
au kuipeleka mbele Hadhira ya kazi hiyo.
c) Muundo wa rukia, Huu ni muundo ambao visa na matukio Hurukiana. Katika
muundo huu kunakuwa na visa viwili ambavyo Hurukiana katika kusimuliwa kwake,
na mwisho visa hivi huungana Na kujenga kisa kimoja. Mfano Njama.
MTINDO
Mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii huiwasilisha kazi Yake kwa jamii.
Ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa Njia ambayo hudokeza upekee wa
mwandishi. Katika mtindo huangaliwa:

 Matumizi ya lugha
 Nafsi zilizotumiwa
 Matumizi ya monolojia (maelezo/ masimulizi) na dialojia (majibizano).
 Mbinu ya kutumia tanzu nyingine za fasihi simulizi
 Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi
 Matumizi ya barua n.k.
WAHUSIKA
Wahusika ni watu, vitu ama viumbe waliokusudiwa kubeba dhamira Mbalimbali kwa lengo la
kuwakilisha tabia za watu katika kazi ya fasihi.
Aina za Wahusika:
a) Wahusika Wakuu, Hawa ni wale ambao wanajitokeza kila mara Katika kazi za
fasihi, hutokea tangu mwanzo hadi mwisho. Wahusika hawa hubeba kiini cha dhamira
kuu na maana ya hadihti Yote. Vituko, visa na matendo yote hujengwa kuwahusu au
Kutokana nao.
b) Wahusika wadogo / wasaidizi, Hawa hujitokeza hapa na pale Katika kazi ya fasihi ili
kuukamilisha ulimwengu wa kazi hiyo. Hawa husaidia kuijenga dhamira fulani katika
kazi ya fasihi na Hasa hubeba dhamira ndogo na kwa minajili hiyo huitwa wahusika
Wadogo ingawa wakati Fulani husaidia kujenga na kuikamilisha Dhamira kuu.
c) Wahusika wajenzi, Hawa ni wahusika ambao wamewekwa ili Kukamilisha dhamira
na maudhui Fulani, kuwajenga na Kuwakamilisha wahusika wakuu na wasaidizi.
Wahusika wakuu na Wadogo huweza kuwekwa katika aina tatu:

Matumizi ya lugha
Lugha ndiyo njia (nyenzo) aitumiayo msanii wa fasihi kuyaelezea mambo Mbali mbali
yahusuyo jamii kwa njia ya ubunifu na usanii. Hivyo lugha Ndiyo mzizi wa kazi ya fasihi na
bila yenyewe kuwapo haiwezekani kuwa na Fasihi.

You might also like