Professional Documents
Culture Documents
Chamgosi Fasihi Ni Sanaa Rafik
Chamgosi Fasihi Ni Sanaa Rafik
na binadamu pamoja na maisha yake na huathiri, hugusa au huacha athari fulani na hupatikana
katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii fulani
Simiyu (2011:9), anatoa maana ya fasihi kuwa ni sanaa inayotumia lugha na matendo
kuwasilisha ujumbe juu ya maisha ya binadamu.
Malenya (2012:40) anasema kwamba fasihi ni sanaa maalum ya matumizi ya lugha inayotoa
mafunzo ambayo yanatumiwa kuielekeza jamii.
Katika fasili hizi za wanazuoni zilizorejelewa kwa ufupi; ni kwamba, tunaona kuwa wanasisitiza
suala la sanaa (ufundi) kama sifa au kitambulisho cha fasihi. Pia, wanatuonesha kuwa sanaa
hiyo lazima itumie lugha ili kuweza kufikisha kile ilichokibeba. Lakini sanaa hiyo inakuwa na
ujumbe (maudhui) ambayo kwayo ndiyo msingi mkubwa. Ujumbe huu ni maalumu kwa ajili ya
jamii. Kwa mwongozo huu, tunaweza kuhitimisha kwa kauli moja kuwa, fasihi ni sanaa
idhihirikayo kupitia lugha na matendo ya binadamu hasa pale inapotumika kwa dumuni la
kufikisha maudhui yake kwa walengwa (hadhira) wanaoishi katika jamii fulani.
Uteuzi mzuri wa lugha; Kwa kawaida kazi za fasihi, iwe fasihi simulizi au fasihi andishi huwa na
lugha yenye ufundi, lugha hii huwavutia hadhira katika kuisikiliza au kuisoma kwake. Lugha ya
kifasihi ni lugha iliyojaa matumizi ya methali, misemo, nahau na tamathali mbalimbali za semi
na kadhalika.
Msuko wa visa na matukio: Maranyingi wasanii wa kazi za kifasihi hupanga matukio yao katika
kazi zao kwa kutumia ufundi mkubwa. Wasanii wanaweza kupanga kazi zao moja kwa moja
au kurukiana. Kitendo hiki hufanya baadhi ya wasomaji kuweza kuburudika zaidi pindi
wanaposoma kazi hizo.