You are on page 1of 13

Swali: Diwani ya karne mpya (Walibora,K ,2007) si mpya kama Mada

inavyodai.Jadili kwa kurejelea,waandishi,mada na muundo wake.

Utangulizi.

A.G. GIBBE (1980) akimnukuu Shaaban Robert anasema kuwa; Ushairi ni sanaa ya
vina inayopambanuliwa nyimbo mashairi na tenzi zaidi ya kuwa ni sanaa ya vina
ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.

Mulokozi na Kahigi (1982) wanasema ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kwa


mpangilio maalumu na fasaha na wenye muala, kwa lugha ya picha, sitiari au
ishara katika usemi, maandishi au maundui ya wimbo ili kuleta wazo au mawazo,
kufunza au kuelekeza tukio au hisia fuani kuhusu maisha au mazingira ya
binadamu kwa njia inayogusa moyo.

Hivyo basi tunaweza kusema kuwa ushairi ni kazi ya sanaa yenye kuandikwa au
kimbwa kwa kufuata kanuni za ushairi ikiwa na maana kuwa ushauri waweza
kuwa wa kimapokeo au wa kisasa ilimradi ushairi huo uwe na ujumbe.

Ushairi wa Kiswahili ni ule ushairi unaotumia lugha ya Kiwahili, utamaduni wa


waswahili, lugha ya picha na lugha ya sitiari na wenye mtiririko mzuri na
mpangilio wa maneno fasaha ili kufikisha ujumbe kwa hadhira.

Kwa kweli mashairi katika diwani hii wengi wao walianza kuandika mashairi
kitambo mno kinyume cha Usasa kama anwani inavyotongoa.

Kwa kurejelea waandishi.

Page 1
Baadhi ya waandishi wa mashairi haya ni wanamapokeo. Hawa ni washairi wa jadi
wanaoshikilia kuwa ili mtungo Fulani uweze kuingia katika kundi la washairi, ni
lazima mtungo hufuate sharia au kanuni Fulani kama vile urari wa vina, mizani ,
idadi ya mishororo katika beti nk,ambazo huitwa arudhi.Kutokana na mtazamo wa
kundi hili ,kukaibuka aina ya mashairi yaitwayo mashairi ya arudhi, mashairi ya
jadi na mashairi ya kimapokeo.Haya ni mashairi yanayoshibisha kanuni zote
zilizokubaliwa katika utunzi wa mashairi.

Sifa za mashairi ya kimapokeo/mashairi ya arudhi

Huwa na urari/usawa/ulinganifu wa mizani.

.Huwa na urari wa vina.

Huwa na urari wa mishororo

Huwa na muundo ulio rahisi kufuatika ukilinganishwa na wa mashairi huru.

Huwa na beti zinazofanana isipokuwa katika bahari ya sarakani


inayochanganya aina mbali mbali za Washairi.

Hutumia lugha ya mkato na yenye mnato

Hutumia tamathali za usemi kwa wingi

Waandishi katika diwani hii si wa karne mpya kama anuani ya diwani hii
inavyodai. Ukiwatazama inabainika kuwa waandishi hawa ni wa kale mno
kinyume na madai ya anuani hii.

Page 2
Baadhi ya waandishi hawa ni pamoja na Shaaban Bin Robert, Euphrase Kezilahabi

na wengine wengi. Kwa kweli hawa niliowataja ni kielelezo bora kuwa diwani hii

inao ukale ndani yake.

Shaaban Robert

Kwanza kabisa kwa kumtazama Shaaban Robert , mwandhishi huyu alizaliwa


tarehe 1/1/1909 katika Kijiji cha Vibambani jirani na Kijiji cha Machui kilometa 10
kusini mwa Jiji la TangaShaaban Robert alianza shule mwaka 1922 na kumaliza
1926 katika shule ya Kichwele ambayo kwa sasa inafahamika kama Uhuru
Mchanganyiko. Alifariki dunia tarehe 22/6/1962 na kuzikwa Machui.

Kwa yakini Shaaban Robert ni miongoni mwa waandishi mashairi wakongwe sana
na mashuhuri ambao mashairi yao yana Ukongwe mwingi sana kulingana na
kusanyiko hili mashairi.

Shaaban Robert alianza kuogelea katika bahari ya uandishi wa ushairi katika


mwaka 1932, akiwa na umri wa miaka ishirini na mitatu. Mwaka wa 1942 alianza
kuandika Utenzi wa Vita vya Uhuru (Kezilahabi, 1993: vi).

Mnamo mwaka 1960 alimaliza kuandika sehemu ya tatu ya maisha yake. Hali
kadhalika, Shaaban Robert alishiriki katika vipindi vya Kiswahili redioni na
akashinda Tuzo la heshima la MBE. Vilevile, alipata zawadi ya kwanza katika
mashindano ya ushairi na riwaya. Kwa mfano: kitabu chake Kusadikika, ni moja
kati ya vitabu vilivyopata zawadi ya kwanza 1949. Shaaban Robert alifariki mwaka
tarehe 22, Juni 1962.

Page 3
Kwa hivyo ni kejeli kwa anuani hii kwa kumweka gwiji huyu katika kapu moja la
waandishi na kuwataja kuwa wa karne mpya. Amekuwa miongoni mwa waandishi
ambao walitamba katika ushairi wa awamu ya urasimi mpya.

Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi amezaliwa mkoa wa Mwanza. Amezaliwa 13 Aprili 1944


katika kijiji cha Namagondo kisiwani Ukerewe. Euphrase Kezilahabini ni
mwandishi kutoka nchini Tanzania. Euphrase kezilahabi Lugha yake ya kwanza ni
Kikerewe lakini huandika hasa kwa Kiswahili ambacho amekipanua kwa kutumia
mitindo ya lugha yake ya asili.

Euphrase Kezilahabi ni mwandishi ambaye anachukuliwa kuwa ndiye mrithi wa


mwandishi nguli Shaaban Robert. Ni mwandishi ambaye ametoa mchango
mkubwa katika fasihi ya Kiswahili. Mwandishi huyu ndiye mwanzilishi wa ushairi
huru (free verse) katika Kiswahili alipoandika vitabu vya ushairi vya kichomi (1974)
na karibu ndani (1988).

Euphrase Kezilahabi anajulikana kwa ushujaa wake wa kujaribu mitindo


mbalimbali ya uandishi wa vitabu. Ukisoma vitabu vyake kama Rose Mistika,
Dunia Uwanja wa fujo, Kichwa maji, Gamba la nyoka na tamthiliya ya Kaptula la
marx utakutana na chembe chembe mpya katika nyanja mbalimbali hasa katika
matuzo ya falsafa mfano riwaya ya Mzingile na Nagona. Msomaji wa vitabu hivi
viwili lazima awe na uelewa wa falsafa za kimagharibi kama (existemutialism,
epistemology, metaphysics, psychoanalysis, aesthetics na phenomenology) na pia
falsafa za kiafrika kama unataka kuelewa chochote kinachozungumzwa katika
vitabu vyake.

Page 4
.Said Ahmed Mohamed

Alizaliwa Pemba, Zanzibar mnamo Desemba 12, 1947. Hakubahatika kupata


malezi ya baba na mama ipasavyo kwani wazazi wake walitengana akiwa na umri
mdogo sana.

Alipenda kusoma, kutunga mashairi na hadithi fupi tangu alipokuwa mwanafunzi


wa darasa la tano. Alitunga mashairi ambayo mengi yalitumiwa na walimu
kufundishia madarasa ya juu.
'Nimfuge Ndege Gani Ili Nipate Salama’ ni shairi lake la kwanza alilolitunga
mnamo 1960.
Mengi ya mashairi yake yalighaniwa katika Radio Zanzibar. Alipata motisha zaidi
kutoka kwa walimu wake, Mohamed Abdallah na Kindi Abubakary
waliomhamasisha pakubwa. Anakiri kurithi kipawa cha usanii kutoka kwa mama
yake “mkubwa” aliyekuwa nyakanga. Mama huyu alikuwa bingwa wa kuimba
nyimbo za unyago.

Pia alikuwa mtunzi mzuri wa mashairi na alipenda sana hadithi za jadi za fasihi
simulizi. Zaidi ya kurithi kipaji kutoka kwa mama yake, uandishi wa Said ulitokana
na mafunzo ya elimu ya dini ya Kiislamu aliyopata katika madrassa. Kazi hizo
zilimzidishia umaarufu na kumfungulia milango ya kupokezwa tuzo za haiba
kubwa ndani na nje ya Afrika.Akiwa mshairi mahiri, Said ametunga diwani
mbalimbali zikiwa ni pamoja na Sikate Tamaa (1980), Kina cha Maisha (1984) na
Jicho la Ndani (2002), kazi zinazozamia masuala ya kisiasa, kiuchumi, mapenzi na
utamaduni.

Page 5
Ujuzi wa fani katika utunzi wa fasihi ni sifa iliyomfanya kufaulu kutumia mtindo wa
uhalisia mazingaombwe katika Kivuli Kinaishi (1990), Amezidi (1995), Babu
Alipofufuka (2001) na Sadiki Ukipenda (2002). Ametumia kwingi mbinu za bunilizi,
utomeleaji na taswira katika tamthilia za Pungwa (1988), Kitumbua Kimeingia
Mchanga (2004) na Posa za Bi Kisiwa (2007) aliyoiandika kwa kumshirikisha
Profesa Kitula King’ei wa Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Nyuso za Mwanamke (2010) ni riwaya aliyoitunga Said miaka 36 baada ya


kuchapishwa kwa Utengano (1980). Anajivunia pia riwaya Kiza Katika Nuru
(1988), Tata za Asumini (1990), Dunia Yao (2006), Mhanga Nafsi Yangu (2012) na
Mkamadume (2013). Ameandika zaidi ya vitabu 60, cha karibuni zaidi kikiwa
Mashetani Wamerudi,tamthilia iliyozinduliwa rasmi Oktoba 10, 2016 katika Tuzo
za Kumi - Kumi za WASTA.

Gharama ya Amani (2014) ni kitabu chake cha hadithi kinachosisitiza umuhimu wa


utu, uadilifu na utaifa miongoni mwa wanajamii. Akiwa miongoni mwa waandishi
wa riwaya za kimapinduzi na kifalsafa, baadhi ya kazi zake zimetafsiriwa kwa lugha
za kigeni. Ametajwa kuwa mwandishi mashuhuri zaidi Afrika Mashariki kutokana
na ukamilifu wake katika kuandika riwaya, tamthilia, mashairi, hadithi fupi, kazi za
watoto na hata vitabu vya kiada vya kufundishia shule za msingi, upili na vyuo.
Ameandika zaidi ya vitabu 60, cha karibuni zaidi kikiwa Mashetani Wamerudi,
tamthilia iliyozinduliwa rasmi Oktoba 10, 2016 katika Tuzo za Kumi - Kumi ambazo
hutolewa kila mwaka na mwasisi wa WASTA Kituo cha Kiswahili Mufti, Guru
Ustadh Wallah Bin Wallah.

Page 6
Mbali na hawa kuna wengine wengi tu ambao wamekuwa katika uga huu wa
uandishi kwa muda mrefu hivyo basi kuonekana kuwa na falsafa ya karne
iliyopita.

Wengine katika diwani hii ni wanamapinduzi .Hawa ni washairi wa kisasa


wanaoaminu kuwa ili mtungo Fulani weze kuingia katika kundi la washairi, si
lazima uzingatie arudhi kama vile urari wa vina, mizani, idadi ya mishororo katika
bet ink. Kundi hili husisitiza kuwa la muhimu katika mtungo sio sharia/kaida hizi
bali ni ujumbe au maudhui ua walemhwa kwa hadhira yake.Kutokana na
mtazamo wa washairi kawa kukaibuka aina nyingine ya mashairi yaitwayo
mashairi huru, mauve, zuhali au mashairi mlegezo.

Mashairi kama haya yana sifa zifuatazo:-

Hayazingatii arudhi kama vile urari wa vina ,mizani ,idadi ya mishororo


katika bet

Huwa na beti tofauti tofauti yaani hamna idadi maalumu ya mistari katika
ubeti mmoja.

Huweza kuwa ma sehemu za ubeti ambazo zimeingia ndani kama njia ya


kuzifanya zionekane wazi kwa msomaji kwa nia ya kusisitiza

Page 7
Hutumika takriri kwa wingi ili kusisitiza ujumbe.

Huhusisha matumizi ya mishororo (mistari) inayokamilika na


inayojitosheleza kimaana iitwayo

mistari toshelezi au mistari ambayo haijakamilika kimaana iitwayo mishata,


na kwa hivyo humbidi

msomaji asome mstari unaofuata ili aweze kuipata ,aama kamili.

Hutumia lugha ya mkato na yenye mnato

Kwa kurejelea mada

Mashairi yaliyomo hapa yameitawala mambo ambayo yaliukumba jamii tangu jadi
hivyo basi ni yale yale tu mambo yaliyokuwepo tangu jadi. Mifano ya mambo wazi
ambayo yameangaziwa katika diwani hii ni pamoja na Ukoloni Mambo leo
Harakati za Mapinduzi/Ukombozi Ujenzi wa jamii mpya . Matabaka Nafasi ya
mwanamke Uongozi mbaya Matumizi mabaya ya madaraka, elimu, mapenzi,
umoja wa jamii, n.k

Kwa hivyo kuhusu mada, mashairi haya yametanda katika maeneo mbalimbali ya
maisha ya binadamu mathalani medani za siasa, Msitu ni ule ule uk 27, kilio cha
Afrika uk 35 , Tazama uk 25.medani ya nasaha: kuteleza siku hizi uk 54, kiumbe
kishauwa uk 49, Mtu ni utu uk 43, kileo bora uk 36. Katika medani ya mapenzi
yapo mashairi yafuatayo: pendo likijizatiti uk 74, Nikubali nilivyo uk.80

Page 8
Medani ya mafumbo, Chini ya mganga uk. 103, Wa-swahili Niambieni uk.96, Ndizi
Gani uk 96, Ugomvi wa Ndizi uk. 109. Ikumbukwe kuwa mafumbo ni mojawapo
wa vipera vya fasihi simulizi.

Kwa kurejea mada,mashairi haya kwa kiwango kikubwa yamezama katika matukio
ya kihistoria ambayo hayaafiki maswala ibuka ya karne hii. Baadhi ya mada hizi ni
kama shairi la Said A. Mohamed kuhusu Ukiniuliza ambalo linasaili mambo yaliyo
wazi kuhusu hali ya maisha, bila kuonyesha Usasa wowote katika shairi zima.

Mbali na shairi hili mengi ya mada ambazo zimeangaziwa humu ni kuukuu kiasi
kwamba haziwezi kuingiliana moja kwa moja na matakwa ya karne hii.

Kwa kurejelea muundo

Tunafaa kufahamu kwamba nguzo ya ushairi wa Kiswahili ni muundo. Ingawa


bahari za ushairi wa Kiswahili zinaweza kuanishwa kwa kutumia vigezo vya
kimaudhui (kama wajiwaji, kasida, madhuma na ushairi burushi), kwa ujumla,
bahari za mashairi ya Kiswahili hubainishwa kimuundo.

Muundo ni mpangilio maalumu wa beti za shairi uliopangwa na msanii kwa nia ya


kufikisha dhamira na maudhui mbalimbali kwa hadhira iliyokusudiwa kama
ilivyokusudiwa (Njogu na Chimerah, 1999). Wanaendelea kueleza kwamba, katika
wakati tulionao muundo wa ushairi ambao umekuwa na mashiko sana ni ule wa
tarbia, yaani kila ubeti wa shairi kuwa na mistari minne yenye vina na mizani kumi
na sita. Haji Gora Haji ni miongoni mwa washairi ambao wanaufuata na kuutumia

Page 9
muundo huu wa tarbia katika utunzi wake wa mashairi. mfano mzuri ni huu
tunaondoa hapa chini.

Takriban mashairi yote ambayo yamo kwenye diwani hii yamezama katika
mashairi kongwe ambayo yamezama katika sheria za utunzi wa mashairi.

Katika diwani hii yapo pia mashairi tele yaliyofuata muundo huu. Haya ni pamoja
na Paul Nabiswa katika ukurasa wa 82 kuhusu NIKUBALI NILIVYO:-

Ni salamu za mabinti,watakao kuolewa

Wa urefu wenye futi, na wafupi wa kutishwa

Ninawapa nikakati, ya wenye kuteuliwa

Adhaniaye yu mufti, aje nitamkagua.

Katika ubeti huu, mashairi anajaribu Kuwapa hosia mabinti ambao wanatarajia
kuolewa kwa kujidai kuwa wao wamekamilika kuwa hakuna binadamu asiye na
dosari hivyo kila mmoja amkubali mwenziwe jinsi alivyo. Mifano mingine ya
mashairi yenye muundo huu wa tarbia ni pamoja na:-kila mtu ale chake uk.
Page 10
26,Msitu ni Ule Ule uk 29. Tujenge nti wanati uk 30,Mihadarati shuleni uk. 39 na
mengine mengi.

Mbali na tarbia kuna mashairi aina kikwamba. Hili ni shairi ambalo neno mpoja au
kifungu hurudiwarudiwa Kutanguliza mishororo au beti za shairi.Asili ya neno hili
ni “ amba” ambalo lina maana ya kunena, kusema au kuzungumzia.Madhumuni
ya mashairi kurudia neno ni kusisitiza ujumbe fulani.

Katika diwani hii, ipo mifano ya mashairi ya aina hii. Haya ni pamoja na shairi
kwenye uk. 24 lililotungwa na Adilatif Abdalla kuhusu KUMEKUCHA ambapo
anamhimiza wananchi kuamka katika usingizi wao wa kifalsafa ya kisiasa baada ya
uchaguzi mkuu wa Kenya, Desemba 2002 ambapo Wakenya waliupigia kura kwa
wingi Muungano wa upinzani, NARC. Kutokana na kitendo hicho, chama cha
KANU ambacho kilikuwa kimetawala kwa miaka 40 kilishindwa.

Mfano mwingine ni shairi la Muchai bin Chui kuhusu MOYO USILIE uk. 136. Shairi
hili linajaribu kuupa moyo nasaha ya maisha katika mambo mbalimbali yakiwemo
kulalama, kutokata tamaa, kutotuhumu na mambo mengine mengi.

Mbali na haya yapo mashairi huru ambayo yameundwa bila kuzingatia arudhi.
Mashairi haya ni ya wanamapinduzi ambao wanashikilia kwamba sio lazima sheria
za utunzi(arudhi) kuzingatiwa bali muhimu ni ujumbe tu.

Haya ndiyo mashairi ambayo huenda yakaonekana kuchukua sehemu kubwa


katika diwani hii. Mifano ya mashairi haya ni TAZAMA la K.W. Wamitila kwenye
uk. 25, UKINIULIZA la Said A. Mohamed uk 27,KIVULI CHA UAFRIKA la Said

Page 11
Mohamed uk 37, MCHEZO WA NJUGUNI la Said A. Mohamed uk 48,CHINI YA
MGUNGA la K.W. Wamitila uk 105 na mengine mengi.

Hitimisho
Kama inavyojitokeza hapo juu ni kuwa diwani hii inakata kuwili sawa na sheria
ambazo ni msumeno ukatao mbele na nyuma. Hali hii inadhihirika wazi kutokana
na vipengele vitatu vikuu ambavyo vimejadiliwa kwa kina hapo juu: Waandishi,
mada na muundo. Hii ni kwa kuwa baadhi ya waandishi hawa wamekuwepo
katika awamu ya urasimi mpya nao wengine wakafuata baadaye ila si muda mrefu
baadaye.
Takriban mashairi yote yamezama katika miundo mikuukuu kama ilivyozingatiwa
na wanamapokezi wa mashairi. Hii ni kusema kuwa zile arudhi za kale ambazo
zilipigiwa upato kutumika katika mashairi ndizo zilizoangaziwa na wengi wa
Washairi hawa.
Bila kusahau muundo ambao umetuwezesha kuyagawa mashairi haya katika
matapo mbalimbali kwa kurejelea vipimo mahsusi.

Marejeleo
a. Abdalla, Abdilatif. 1973. Sauti ya Dhiki. Nairobi: Oxford University Press.
b. Abedi, Kaluta Amri. 1954. Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri.
Nairobi: Kenya Literature Bureau.
c. Heidegger, Martin. 1971. Poetry, Language, Thought. New York: Harper &
Row Publishers.

Page 12
d. Kahigi, Kulikoyela & Mugyabuso M. Mulokozi. 1973. Mashairi ya Kisasa. Dar
es Salaam: Tanzania Publishing House.
e. Kahigi, Kulikoyela & Mugyabuso M. Mulokozi. 1979. Kunga za Ushairi na
Diwani Yetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
f. Kezilahabi, Euphrase. 1974. Kichomi. Nairobi: Heinemann. Kitula, King’ei &
Amata Kemoli. 2001. Taaluma ya Ushairi. Nairobi: Acacia Stantex
Publishers.
g. Kuvuna, S.M, Mvati, M.N & P.A Maliachi. 1992. Nuru ya Ushairi: Mwongozo
na Uchambuzi. Nairobi: Kenya Literature Bureau.
h. Massamba, David. 1983. Utunzi wa Ushairi wa Kiswahili. Fasihi [Makala za
Semina ya Waandishi wa Kiswahili III], imehaririwa na Taasisi ya Uchunguzi
wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: Uk. 55-94.
i. Mayoka, Jumanne M. 1984. Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka. Dar
es Salaam: Tanzania Publishing House.
j. Mazrui, Alamin. 1988. Chembe Cha Moyo. Nairobi. Heinemann Kenya Ltd.
Mberia, Kithaka wa. 1990. Umbo La Mashairi. Mwamko 5 [Jarida La Chama
Cha Kiswahili Chuo Kikuu Cha Nairobi]: Uk. 80-111.
k. Mberia, Kithaka wa. 1997. Mchezo wa Karata. Nairobi: Marimba
Publications Ltd. Mberia, Kithaka wa. 2001. Bara Jingine. Nairobi: Marimba
Publications Ltd.
l. Mnyampala, Mathias. 1965. Diwani ya Mnyampala. Dar es Salaam: East
African Literature Bureau. Mohamed, Said Ahmed. 1980. Sikate Tamaa.
Nairobi: Longhorn Publishers.

Page 13

You might also like