You are on page 1of 21

CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGUSTINO CHA

TANZANIA

SHULE KUU YA ELIMU


IDARA YA KISWAHILI

SWALI: Kulikoyela Kahigi au Kulikoyela Kahigi na Mugyabuso Mulokozi ndio washairi nguli
kifani kuliko mshairi yeyote wa Kiswahili. Thibitisha hoja hii kwa mifano dhahiri ya mbinu
zake/zao tatu za kifani au kanusha kwa mifano thabiti.

Kwa mujibu wa Mulokozi na Kahigi (1982). Wao wanafasiri kuwa ushairi ni sanaa
iliyopambanuliwa kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha na yenye muwala kwa lugha ya
mkato, picha, sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kuleta wazo au
mawazo, kufunzu au kueleza tukio au hisia fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa
njia igusayo moyo

Kwa mujibu wa Abedi (1954). Ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki
halina maana

Kwa mujibu wa Shaban Robert (1958). Ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kama nyimbo,
mashairi au tenzi zaidi ya kuwa sanaa ya vina, ushairi una ufasaha wa maneno machache au
muhtasari, mawazo, maoni na fikra za ndani zinazoelezwa kwa muhtasari wa ushairi huvuta
moyo kwa namna ya ajabu

Kezilahabi J. M(1976). Ushairi ni tukio, hali au wazo ambalo limeoneshwa kwetu kutokana
na upangaji mzuri wa maneno fasaha yenye mizani kwa kifupi ili kuonesha ukweli fulani wa
maisha

Kwa ujumla, ushairi ni utungo ambao hutungwa kwa kutumia lugha teule ambayo agalau
huwa lugha mkato na lugha fishe, fauku ya hayo, utungo huu huwa na muwala yaani mtiririko au
mpangilio mzuri wa mawazo kutoka neno moja hadi lingine

0
Kwa mujibu wa Sw. M. Wikipedia. Org(2022). Fani ni mbinu anayoitumia mwandishi wa ila
kufikisha ujumbe uliowakusudia hadhira

Kwa mujibu wa Venance Gaspar(2018). Anasema fani ni ufundi au ustadi wa kisanaa


anaotumia msanii kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii. Msanii hutumia ufundi huu katika
kubeba maudhui ya kazi yake. Ufundi huu hujitokeza katika mambo kadha kama muundo,
mtindo na matumizi ya lugha

Kwa mujibu wa Senkoro(2011). Anasema fani ni katika fasihi ni ule ufundi wa kisanaa
anaotumia msanii katika kazi katika kazi yake, ni ufundi wa msanii katika kuumba umbo la kazi
ya fasihi kutokana na ubunifu wake. Anaendelea kusema, fani ni ufundi ambao msanii anautumia
katika kufikisha ujumbe ujumbe kwa jamii

Mbinu za kifani zimegawanyika katika vipengele tofautitofauti kama vile muundo, mtindo,
matumizi ya lugha, wahusika, mandhari/muktadha. Katika swali letu limetutaka kutumia mbinu
tatu za kifani ambapo tumependekeza muundo, mtindo na matumizi ya lugha

Kulikoyela K. Kahigi na Mugyabuso Mulokozi sio washairi nguli kifani katika uandishi
wa mashairi ya Kiswahili kwa sababu hawajazingatia vipengele mbalimbali vya kifani kama vile
muundo wa shairi, mtindo wa shairi pamoja na matumizi ya lugha katika uandishi wa mashairi
yao ambayo ni diwani ya MAGEUZI iliyoandikwa na Kulikoyela K. Kahigi na diwani ya TENZI
TATU ZA KALE iliyoandikwa na Mugyabuso Mulokozi

Katika kipengere cha muundo; muundo ni umbo na mpangilio wa kazi ya fasihi, katika
ushairi wa Kiswahili, mashairi huwa na miundo mbalimbali inayohusisha idadi ya mistari
(vipabde au mishororo katika kila ubeti, mathalani mashairi ya tathimina, tathinia, tathilitha,
tarbia, takhimisa, tasdisa, usaba, unane, utisa na ukumi: Senkoro 2011). Pia muundo wa ushairi
wa Kiswahili huhusisha vipengele mbalimbali kama vile mshororo, vina, mizani, beti kituo au
kibwagizo. Lakini katika diwani ya MAGEUZI iliyoandikwa na Kulikoyela K. Kahigi pamoja
na diwani ya TENZI TATU ZA KALE iliyoandikwa na Mugyabuso Mulokozi. Diwani hizi
katika uandishi wake waandishi hawajaweza kuzingatia vipengele mbalimbali vya muundo kama
vile

1
Beti; katika diwani ya MAGEUZI mwandishi Kulikoyela K. Kahigi hajaonesha idadi ya beti
alizoziandika katika diwani yake. Mfano katika shairi la "Ngao za kienyeji" (uk36), Mwandishi
Kulikoyela Kahigi ameshindwa kuonesha idadi kamili ya beti katika shairi hilo. Pia katika shairi
la "Sikuwa na Haja" uk29. Pia katika diwani ya TENZI TATU ZA KALE mwandishi M.
Mulokozi ametumia mabeti mengi katika kichwa kimoja cha tenzi. Mfano katika utendi wa
"Fumo Liyongo" ametumia mabeti 232 ambapo kichwa kimoja cha shairi kinafaa kisizidi mabeti
20

Mishororo; Ni kila idadi ya mistari katika kila ubeti, katika diwani ya “MAGEUZI”
mwandishi Kulikoyela Kahigi hajafuata kigezo cha mishororo Katika mashairi yake. Mfano
katika shairi la "Ngao za Kienyeji" (uk36), katika ubeti wa kwanza ametumia mishororo mitano
(takhimisa) lakini ubeti wa pili hajabainisha idadi kamili ya mishororo. Pia katika diwani ya
"TENZI TATU ZA KALE" iliyoandikwa na Mugyabuso Mulokozi katika kigezo cha mishororo
ametumia tarbia tu au mashairi yenye mishororo minne tu, Wakati katika mishororo zipo aina
nyingi za mishororo kama vile tamolisa(mashairi yenye mshororo mmoja), tathinia (mashairi
yenye mishororo miwili), tathilitha (mashairi yenye mishororo mitatu), tarbia (mashairi yenye
mishororo minne) na kadhalika....

Vina na Mizani; Mizani ni idadi kamili ya silabi katika kila mshororo lakini vina vipo
vya aina mbili, vina vya kati na vina vya mwisho. Katika diwani ya MAGEUZI mwandishi
Kulikoyela Kahigi hajaonesha vina vya katika na vina vya mwisho katika mashairi yake na pia
mishororo katika kila ubeti haina idadi kamili ya mizani. Mfano katika shairi la "Ngao za
Kienyeji (uk36)"

“Hapo kale kabisa zama za zamani


Katika Kijiji kimoja cha amani
Watu waliishi kwa matumaini
Wakifanya shughuli zao mbalimbali
Kwa mafanikio na ustawi yakin”
Katika mfano huu mshororo wa kwanza, wa pili na wa tano Kuna mizani kumi na tatu, lakini
katika mshororo wa tatu na wa nne kuna mizani kumi na mbili. Hivyo katika mfano huu
mwandishi hajabainisha idadi kamili ya mizani
2
Kipengeli cha Mtindo; Katika mtindo wa kishairi tunachunguza mashairi ya kisasa na ya
kimapokeo. Mashairi ya kisasa ni mashairi ambayo huandikwa bila kufuata urari wa vina na
mizani. Lakini mashairi ya kimapokeo ni mashairi ambayo huandikwa kwa kufuata urari wa vina
na mizani. Katika diwani ya MAGEUZI mwandishi Kulikoyela Kahigi amefuata mtindo wa
kisasa kwani mashairi yaliyoandikwa katika diwani ya MAGEUZI hayajafuata urari wa vina na
mizani. Pia katika diwani ya TENZI TATU ZA KALE mwandishi ametumia mtindo wa
kimapokeo kwani tenzi zilizoandikwa zimefuata vina kwa sababu vina vya mwisho katika kila
ubeti vinafanana

Kutokana na madhaifu tuliyoyabaini kwa waandishi (Kulikoyela Kahigi na Mugyabuso


Mulokozi), kuwa sio washairi nguli kuliko wote katika kipengere cha kifani. Wafuatao ni baadhi
tu ya washairi (waandishi) nguli katika kipengere cha kifani. Waandishi hao ni pamoja na
Zacharia P.Mponzi na Christopher B. Lucas katika diwani ya "NIMEKUJA NA HABARI"
pamoja na Sebastian N. Mbwillow katika diwani ya "MOYO". Waandishi hao wameweza
kufafanua kipengere cha kifani kwa kujikita katika mambo matatu ambayo ni muundo shairi,
mtindo wa shairi na matumizi ya lugha

NIMEKUJA NA HABARI

Ni diwani yenye mkusanyiko wa mashairi yaliyotungwa kwa ufundi wa hali ya juu ili kuleta
ladha murua kwa wasomaji. Mashairi haya yamegubikwa na mitindo mbalimbali ya utungaji wa
mashairi ikihusisha ukopaji wa kaida kutoka katika tanzu nyingine za fasihi, ili kuleta upekee
katika kazi husika. Diwani hii inaangazia masuala yaliyopo katika jamii kama vile suala la ajira,
uzalendo, ukiushi wa maadili, upokwaji wa haki, uchawi na ushirikina, mfumo wa elimu na
kadhalika

MOYO

Ni diwani iliyosheheni maudhui mseto yaliyowasilishwa kwa fani ya kipekee, ni moja kati
ya diwani chache katika katika fani ya ushairi ambayo mashairi yake yamesheheni maumbo
mbalimbali likiwemo umbo la moyo. Diwani hii imekuwa na mchango mkubwa katika kuonesha
nmaendeleo ya ushairi wa Kiswahili

3
Zifuatazo ni hoja zinazothibitisha kuwa diwani ya "NIMEKUJA NA HABARI"
iliyoandikwa na Zacharia P. Mponzi na Christopher B. Lucas pamoja na diwani ya "MOYO"
iliyoandikwa na Sebastian N. Mbwillow ni baadhi ya diwani zilizozingatia vipengele vya kifani.
Vipengele hivyo ni kama vile;

Muundo; Ushairi wa kiswahili huwa na miundo mbalimbali inayohusisha idadi ya mistari


(vipande au mishororo katika kila ubeti). Pia muundo wa ushairi wa Kiswahili huhusisha
vipengele mbalimbali kama vile mshororo, vina, mizani, beti, kituo au kibwagizo. Katika diwani
ya NIMEKUJA NA HABARI pamoja na diwani ya MOYO vipengele vya kimuundo vimeweza
kuthibitika kwa ufasaha katika diwani hizi. Zifuatazo ni hoja zinazofafanua vipengele
mbalimbali vya muundo vilivyojitokeza katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI pamoja na
MOYO, kwa kurejelea bahari za ushairi kwa mujibu wa Wamitila (2008)

Mizani; ni idadi ya silabi katika kila mshororo, katika diwani ya NIMEKUJA NA


HABARI pamoja na diwani ya MOYO mwandishi ametumia mashairi yenye mizani mbalimbali
kama vile

Ukawafi; Ni utungo wa ushairi wenye mizani 15 na wenye vipande tofautitofauti,


vinaweza kuwa vipande vitatu au viwili, mfano katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI
shairi la "Bahari yanuka" (uk45)

“Wingu latanda, pepo mkali, kama sunami,


Woga kupanda, yatakalili, maji si lami,
Damu kaganda, tupo maili, wote tusemi,”
Katika mfano huu, Waandishi Zacharia P. Mponzi na Christopher B. Lucas wameonesha jinsi
ukawafi ulivyojitokeza katika shairi la "Bahari yanuka"

Shairi; Ni utungo wenye mizani 16 katika kila mshororo na wenye mizani 8 katika kila
kipande cha mshororo, mfano katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI shairi la “Fanani na
hadhira” (uk1) ubeti wa kwanza
“Hodi hodi naingia, sipo kupoza dira,
Naomba nipate njia, ila mbona mmefura?
Nataka kusalimia, hamjambo nyi hadhira?
4
Fahari yangu fanani, kazi ipate hadhira”.
Katika mfano huu tunaona kuwa mwandishi ametumia mizani 16 kila mshororo wa ubeti wa
shairi hilo la "fanani na hadhira" pia katika shairi la "tega sikio" (uk2) mwandishi ametumia
shairi lenye mizani 16 katika kila mshororo

Utumbuizo; Ni utungo wa ushairi wenye mizani 14 katika kila mshororo wake wakati
mwingine utungo huu unakuwa hauna idadi kamili ya mizani. Mfano katika diwani ya MOYO
(uk12) shairi la "Mwalimu"

“Ualimu, hivi nayo ni fani?


Mwalimu, hivi na yeye ni muhimu?
Mwalimu, vipi mbona umekonda ?
Mwalimu au wamtaka siwema?”
Katika mfano huu tunaona kuwa mwandishi hajaonesha idadi kamili ya mizani katika shairi la
"Mwalimu". Pia katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI shairi la "Kwetu" (uk5) ni mfano
wa shairi ambalo halina idadi kamili ya mizani hivyo ni utumbuizo

“Hello,
Habari za Leo,
Mjomba hapa nisikilize,
Haya machache nikuelezee,
Haya mafunzo toka kwa Babu"
............(uk5)
Pia katika mfano huu tumeona mwandishi Christopher Lucas hajatumia idadi kamili ya vina na
mizani katika mshororo mmoja kwenda mwingine

Utenzi; Huu ni utungo ambao una mizani nane katika kila mshororo, mara nyingi huwa
ni masimulizi marefu kuhusu maisha au habari. Mfano katika diwani ya NIMEKUJA NA
HABARI, shairi la "Utenzi wa Afrika" (Uk22) mwandishi anasema

"Katika mabara Saba,


Afrika ni nasaba,
Wanakiri lao baba,
5
Watu wengi watamani."
Katika mfano huu mwandishi ametumia utenzi ambao una mizani nane katika kila mshororo

Msuko; Huu ni utungo wa ushairi ambao kibwagizo kinakuwa na mizani michache zaidi ya
mishororo mingine. Mfano katika diwani ya MOYO, mwandishi Sebastian N. Mbwillow
ametumia utungo huu katika shairi la "sintofahamu” anasema

“Habari bora, ni mbaya,

Za kutia fora, ni hekaya,

Watu wa bara, wa kukaya,

Sintofahamu................... "(Uk61)

Katika shairi hili la "sintofahamu" mwandishi ametumia utungo huu wa msuko kuanzia ubeti wa
kwanza hadi wa nne. Pia katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI mwandishi ametumia
utungo huu katika shairi la "Zilizo kweli" mwandishi anasema

“Uongo unashamiri kwa Kasi,


Bila hata kuwa na kiasi,
Mie uongo unanighasi,
Zaidi unanipa makasiko,
Maisha yawa tafrani,
Zilizo kweli kampuni,
Msema kweli yuko wapi?
Nitakwazika! "............... (Uk52)
Katika mfano huu tunaona mwandishi ameonesha jinsi msuko ulivyojitokeza katika shairi la
"Zilizo kweli"

Mishororo; Katika shairi mishororo ni idadi ya mistari katika kila ubeti wa shairi.
Wamitila (2008) ameainisha aina mbalimbali za mishororo. Kwa kurejelea diwani ya
NIMEKUJA NA HABARI pamoja na diwani ya MOYO waandishi wameweza kutumia aina
mbalimbali za mishororo kama ifuatavyo:-

6
Tathmina; Ni shairi lenye mshororo mmoja. Katika diwani ya NIMEKUJA NA
HABARI katika shairi la "katiba" mwandishi ametumia tathmina kama ifuatavyo

"Katiba ibadilishwe!”......... (Uk69)

Pia katika shairi la "Imani" tathmina imetumika

“Niamini nini?”........ (Uk17)

Katika mifano hii tunaona jinsi mwandishi alivyotumia tathmina katika mashairi yake

Tathnia; Ni aina ya shairi ambayo huwa na mishororo miwili katika kila ubeti. Katika
diwani ya NIMEKUJA NA HABARI tathnia imeweza kutumika katika mashairi mbalimbali.
Mfano katika shairi la "Duniani kupeana" (uk32) mwandishi anasema

“Barabara kuwa lama, bomba kutoa asali,

Chagueni leo hii, mjengoni kuingia”

Pia katika shairi la "najivunia nini" (uk96) tathinia imetumika kama ifuatavyo

"Masikini matajiri, mwishoni ni mmoja,

Kuingia sandukuni, kwa marashi na Mataji."

Katika mifano hii tunaona jinsi mwandishi alivyoweza kutumia tathinia katika mashairi yake

Tathilitha; Ni aina ya shairi ambayo huwa na mishororo mitatu katika kila ubeti. Katika
diwani ya MOYO mwandishi ametumia tathilitha katika mashairi yake. Mfano katika shairi la
"tegua kitendawili” (uk29) mwandishi anasema

" Mti wa maajabu, unavipanda viwili,

Mti ulotofauti, mizizi yake ipo juu,

Vipanda chino, juu sana kiwiliwili."

7
Katika mfano huu mwandishi ametumia tathilitha, yaani shairi lenye mishororo mitatu. Pia
katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI mwandishi ametumia tathilitha katika mashairi
yake. Mfano katika shairi la “pesa” (uk115), mwandishi anasema

" Umepewa majina, mkwanja, mawe, maokoto,

Wamaliza shida nyingi, laini ngumu na kokoto,

Unasakwa na wengi, shaibu ajuza watoto."

Pia katika shairi la "fundika" (uk85), shairi la "Mjiajiri shambani" (uk92), shairi la "Mama
Afrika" (uk51) na shairi la "Dunia mgeuko" (uk39) mwandishi ametumia tathilitha katika baadhi
ya mashairi yake. Mfano mashairi tajwa hapo juu

Tarbia; Ni aina ya shairi ambalo huwa na mishororo minne katika kila ubeti wa shairi.
Katika diwani ya MOYO mwandishi ametumia tarbia Katika baadhi ya mashairi. Mfano katika
shairi la "Hautufai" (uk15) anasema

" Pua kua,

Tua Dua,

Shuka au tua

Nimesimama."

Pia katika mashairi ya "Sote tu watumwa" (uk13), shairi la "Mwalimu"(uk12) na shairi la shairi
la" Karibu tena" (uk4), mwandishi ametumia muundo wa tarbia. Pia Katika diwani ya
NIMEKUJA NA HABARI mwandishi ametumia tarbia Katika baadhi ya mashairi. Mfano katika
shairi la "Fanani na hadhira"(uk1), mwandishi ameonesha muundo huo wa tarbia

“Hodi hodi naingia, sipo kupoza dira,

Naomba nipate njia, ila mbona mmefura?

Nataka kusalimia, hamjambo nyi hadhira?

Furaha yangu fanani, kazi ipate hadhira."


8
Pia katika mashairi ya "Tega sikio" (uk2), shairi la "Kuku mgeni" (uk11) na shairi la "Toeni
tamko" (uk15). Mwandishi ametumia muundo wa tarbia katika mashairi yake

Takhimisa; Ni aina ya shairi ambayo huwa na mishororo mitano katika kila ubeti.
Katika diwani ya MOYO mwandishi ametumia muundo huu wa takhimisa katika mashairi
mbalimbali. Mfano katika shairi la "Kwanini waishi" (uk47) mwandishi anasema

“Muulize hakika akueleze,


Kwa nini na wapi maisha? Baeleze,
Wapo waishio haswa, utueleze?
Sisi twang'ang'ana siku tuzisogeze,
Kwa nini waishi leo, jana au kesho”
Pia katika shairi la "Wangu mpenzi" (uk49), shairi la “Chanzo ni mfumo ”, shairi la “Ikawa ”
(uk55). Mwandishi ametumia muundo huu wa takhimisa. Pia katika diwani ya NIMEKUJA NA
HABARI, mwandishi ametumia muundo huu wa takhimisa. Kwa mfano shairi la "Fimbo ya
mnyonge" (uk61)

“Kikao chetu kimoja, tofauti kaleta nani?

Kundi hili nalo lile, kutugawa ka' karanga,

Lililo juu kutamba, na jingine kusanda,

Watumia shekeli, na wengine kutwanga,

Kumbe fimbo ya mbali, ndio kuua nyoka"

Pia katika shairi la "Zoezi zana" (uk97), katika mifano hii waandishi wametumia takhimisa
katika mashairi yao

Tasdisa; Ni aina ya shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti. Katika diwani ya
NIMEKUJA NA HABARI mwandishi ametumia muundo wa tasdisa katika baadhi ya mashairi
yake. Mfano katika shairi la "Majeruhi" (uk105), mwandishi anasema

9
“Habari kemkem, zipo kwa majeruhi,

Kupata uzoefu, enenda kwa waganga,

Huwezi kuelewa, hadi yakukela,

Ukishapatikana, hadithi kuandika,

Wakati unafika, majeruhi pilipili,

Kama unabisha, fata simba aliyejeruhiwa”

Pia katika shairi la" Ardhi inatema" (uk26). Pia katika diwani ya MOYO waandishi ametumia
muundo wa tasdisa katika shairi la "Unatofautiana" (uk57)

“Si kunguru na mwewe, ila sisi si sisi,

Usawa kabisa nami, si sungura na fisi,

Uwezo wa akili wewe, pia unavyojihisi,

Waweza pandisha uchumi, ufanane nasi,

Acha uzembe, kiwewe na wazo mufilisi,

Unatofautiana nam, jiulize kwanza swali”

Pia katika shairi la" Kama si uchizi ni nini?" ubeti wa nne (uk71) mwandishi ametumia tasdisa

Usaba; Ni aina ya mashairi ambayo huwa na mishororo saba katika kila ubeti wake.
Katika diwani ya MOYO mwandishi ametumia muundo huu katika mashairi mbalimbali. Kwa
mfano katika shairi la "Unatofautiana" ubeti wa tatu (uk57) anasema

"Maswali kwangu Mimi, ni mtakaso wa akili,

Kurunziyo niwe mimi, niulize tu maswali,

Nalijiuliza sana mimi, maswali juu ya maswali

Umasikini vipi nami, Elimu vipi nafeli?


10
Kilema wa kiuchumi, nashindwa hata kutafakari,

Tofauti yao nini nami, hata nisiwasawiri?

Wanatofautiana nami? Yaani swali kwa swali"

Pia katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI mwandishi ametumia muundo wa usaba katika
shairi la "Vituko vya daladala" ubeti wa pili (uk20) anasema

“Wewe dada hapo mbele, nimekaa vibaya nitakupa,

Si usimame unipe, siwezi kukupia hapa,

Apo rasta maelekezo, ngoja nigeuke kwanza nakupa,

Bi mkubwa hapo, ngoja isimame nakupa,

Fanya chapu ishasimama, chukua halafu uniache,

Utingo analiza sarafu zake, huku akimtazama Mzee,

Si nimeshakupa we kijana, au unataka tena”

Katika mfano huu tunaona kuwa mwandishi amewaza kutumia usaba katika Shairi Lake

Unane; Ni aina ya mashairi ambayo huwa na mishororo nane katika kila ubeti wake.
Katika diwani ya MOYO unane umeweza kujitokeza katika shairi la "Hatutizamani" (uk54)

"Juzi walikuta, kionyo wakanikazia macho,

Wakanitazama sana, kikejeli wakacheka kimacho,

Jana tukaonana, wakanikata bila hayo macho,

Watacheka tena wazi, hahahahaaaa! Pasi kificho,

Wakanyosha mikono, wakanyanyua miguu, hatua

Wanainama wakiinuka, vichwa kushoto kulia chini

11
Wamejaa haya, hawaoni mbele! Hatutizamani"

Pia katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI shairi la "Kupe" (uk35) mwandishi ametumia
muundo wa unane. Katika mifano hii tunaona kuwa waandishi wameweza kutumia unane katika
uandishi wa mashairi yao

Utisa; Ni aina ya mashairi ambayo huwa na mishororo tisa katika kila ubeti wake.
Katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI shairi la "Utusamehe" (uk67) anasema

"Ee mola wetu wa mbinguni,

Uliyetuweka hapa duniani,

Tumiliki kila kilicho machoni,

Wanyama na hao samaki majini,

Ukatupa na akili nyingi utashini,

Tuyajue yale mema na mabaya Duniani,

Tukikosea tutambue tuje kwako mbinguni,

Tusiwe kama wanyama wa mwituni,

Tuishi tukitambua uwepo wako ulimwenguni. "

Katika shairi hii mwandishi amewaza kutumia muundo wa utisa

Ukumi; Ni aina ya mashairi ambayo huwa na mishororo kumi katika kila ubeti
wake. Mfano katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI mwandishi ametumia muundo huu wa
ukumi katika shairi la "Eliza" (uk64) anasema

“Wewe ni pambo la ulimwengu,

Wamvutia kila mwenye macho,

Mtulivu,

12
Mcheshi,

Mwendo wenye madaha,

Uliouchanganya na mapozi,

Wavutia,

Mdada,

Unasadifu thamani hiyo kubwa,

Kupendwa ni kutunza daima”

Pia katika diwani ya MOYO mwandishi ametumia muundo wa ukumi katika shairi la “Umri wa
busara" (uk37)

Vina; Katika ushairi wa Kiswahili vina vimegawanyika katika makundi mawili, yaani
vina vya kati na vina vya nje. Katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI pamoja na diwani ya
MOYO, kigezo cha vina kimeweza kuthibitika katika mashairi mbalimbali kama ifuatavyo

Ukara; Ni utungo wa ushairi ambao vina vyake vya nje (utao) hufanana shairi zima,
lakini vina vya kati(ukwapi) hutofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Katika diwani ya
NIMEKUJA NA HABARI mwandishi ametumia ukara katika shairi la "Nitozeni" (uk19)

Ubeti 1. “Vijiweni minong'ono, kuyatoa ya moyoni,

Kuyatema na maneno, kujishika viunoni,

.........................................”

Ubeti 2. “Miamala ni michungu, yanitoka mi rohoni,

Mbele yangu ni ukungu, kutazama makatoni

.....................................”

13
Katika ubeti wa kwanza vina vya kati ni "no" na vina vya kati ni "ngu" lakini vina vya nje katika
beti zote ni "ni". Pia katika diwani ya MOYO mwandishi ametumia ukara katika shairi la
"Tamati" (uk76)

Ukaraguni; ni utungo wa ushairi ambao vina havifanani kutoka ubeti mmoja na


mwingine, kila ubeti huwa na vina vyake vya kati na vya nje. Katika diwani ya MOYO
ukaraguni umeweza kutumika katika shairi la "Mpenzi shoni" (uk34), anasema.

Ubeti 1. “Natambua mila zetu, msuli kwao pwani


Nataka uhuru wetu, maumivu nayaburiani
.......................................”
Ubeti 2. “Kujitoza kisabuni, daima nilifanikiwa
Nikajiepusha bombani, kuepa kumwagiwa,
.......................................”
Katika mfano huu tunaona kuwa vina vya kati na vya nje katika ubeti wa kwanza na wa pili
vimetofautiana, kwani vina vya kati ubeti wa kwanza ni "tu" na na vina vya nje ni "ni" lakini
katika ubeti wa pili vina vya kati ni "ni" na vina vya nje ni "wa". Pia katika diwani ya
NIMEKUJA NA HABARI ukaraguni umejitokeza katika shairi la "Toeni tamko" (uk15)

Kikwamba; Ni utungo wa ushairi ambao neno moja huanza katika kila mshororo wa ubeti.
Katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI mwandishi amewaza kutumia kikwamba katika
shairi la "Upendo" (uk9) anasema

“Upendo neno hazimu, nani usiyeupenda ,

Upendo kwa familia, siku zote ni amani,

Upendo ngozo imari, makanisa yahubiri,

Upendo misikitini, mashehe wanausia,”

Katika shairi hii neno upendo imejirudia katika kila mshororo. Pia katika shairi la "Tunda la
roho" (uk82), mwandishi amewaza kuonesha jinsi neno la kwanza katika kila mshororo wa ubeti
yanavyofanana. Katika diwani ya MOYO mwandishi amewaza kuonesha kikwamba katika shairi
la "Mwalimu" (uk12) anasema
14
“Mwalimu, Tina na shoni wanagombana!

Mwalimu, umenisahau wako mpenzi!

Mwalimu, mwanao kapata ajari!

Mwalimu ,sina salari wa tisa sasa”

Katika shairi hii la Mwalimu uk12 ubeti wa pili tunaona jinsi neno "Mwalimu ” linavyojirudia
katika kila mshororo wa ubeti

Mtindo kwa mjibu wa wamitila (2003).katika ushairi wa kiswahili mtindo ni jumla ya mbinu au
sifa zinazomwezesha mwandishi kuwasilia ujumbe wake, huelezea mwandishi anavyounda kazi
yake

Senkoro (1982), anasema mtindo katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi
hiyo na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kaida zilizofuatwa (za
kimapokeo) ama ni za kipekee

Mtindo katika ushairi wa kiswahili huzingatia vipengele vikuu viwili ambavyo ni mtindo wa
kisasa na mtindo wa kimapokeo. Waandishi wa diwani hizi mbili ambazo ni diwani ya MOYO
na NMEKUJA NA HABARI wamezingatia mitindo hii kama ifuatavyo:-

Mtindo wa kimapokeo, ni mtindo ambao mashairi huandikwa kwa kufuata urari wa vina na
mizani, katika diwani ya “NIMEKUJA NA HABARI" shairi la “fanani na hadhira” (Uk.1)
waandishi ametumia shairi la kimapokeo, anasema,

“Hodi hodi naingia, sipokupoteza dira.

Naomba nipate njia, ila mbna mmefura?.

Nataka kusalimia, hamjambo nyi' hadhira?

Fahari yangu fanani, kazi ipate hadhira,”

Katika mfano huu tunaona kuwa mwandishi amefata urari wa vina na mizani. Kwani vina vya
kati ni “a” na vina vya mwisho ni “ra”

15
Mtindo wa kisasa, ni mtindo ambao mashairi huandikwa pasipo kufuata urari wa vina na mizani
mfano katika diwani ya "NMEKUJA NA HABARI" Mwandishi ametumia mtindo wa kisasa
mfano katika shairi la “Tundala Roho” (uk.82)

“Amani ndiyo hali, Tanzania ni amani.

Amani ikiwepo pana, stawi nyumbni.

Amani ilo kweli, twatamba hata njiani

Amani siyo vita, huvutia duniani.”

Pia katika diwani ya "MOYO" mwandishi ametumia mtindo wa kisasa mfano katika shairi la

Waajabu (Uk.39) anasema

“Unauelewa kweli? Au,

U mwehu wewe? Au,

Labda si wewe! Au,

Labda nakufananisha tu”.

Katika mifano hiyo hapo juu tunaona kuwa mwandishi ametumia mashairi ya kisasa kwani
ajafata urari wa vina na mizani katika uandishi wake, pia katika shairi la “Filimbi”. (uk53)
pamoja na shairi la “nakumbuka juzi kati” (uk59) ni mfano wa mashairi ambayo hayajazingatia
urari wa vina na mizani (kisasa)

Matumizi ya lugha, katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI pamoja na diwani ya MOYO


waandishi wa diwani hizi wameweza kutumia vipengele mbalimbali vya matumizi ya lugha
kama ifuatavyo

Tashibiha, ni mbinu ya ulinganishi wa watu au vitu vingine kwa kutumia maneno ya


kuunganisha sentensi kama vile mithili ya, kama, kana kwamba. mfano katika diwani ya
"NIMEKUJA NA HABARI" shairi la “mapenzi kitu gani” (uk4) ubeti wa 4

"Mapenzi kama asali"


16
Neno “kama”ni tashibiha ambayo imetumika kulinganisha mapenzi na asali. Pia katika shairi la
Dunia Mgeuko. (uk.3) "Dama kama kwenye bucha". Hivyo neno kama linathihirisha utokeaji
wa tashibiha.

Sitiari, hii ni sawa na tashibiha ambayo hulinganisha vitu au watu bila kutumia kiunganishi
mfano mithili ya, sawa na. Mfano katika diwani ya NIMEKUJA NA HABARI shairi la
“Upendo” (uk.9) ubeti wa 5

"Upendo siyo bidhaa"

Sentensi hii imekamilika lakini haijatumia kiunganishi chochote.

Tafsida, ni matumizi ya lugha mwala inayokidhi mwelekeo wa jamii kuhusu miiko na makatazo
ya kutumia lugha za uwazi hasa kutumia uchafu wa matusi mfano katika diwani ya
"NIMEKUJA NA HABARI" shairi la X-Wangu (uk.12) ubeti wa 2

“Kama wali ni ubwabwa, haufai harusini,

Kama embe lilo dodo, mbaya yake harufuye,

siyo zile za Bukoba, kumwaga maji chumbani,

Yule ni mbwa hakika, akifa aliwe nyama”.

Shairi hili linamzungumzia mwanamke na tabia zake lakini mwandishi ameficha ukali wa
maneno na akaweka tafsida.

Takriri, ni utokeaji wa mara kwa mara wa kurudia maneno kwa malengo maalumu vile vile
katika diwani ya "NIMEKUJA NA HABARI" shairi la Glory (Uk.14)

“Za bara hata pwani wazijua,

kutulia udambwi udambwi.

...............”

Nidaa. ni neno au tamko linalioonesha mchomo wa moyo kwa sababu ya aidha furaha,
mshangao au huzuni. Katika diwani ya "MOYO" shairi la “Kwa Heri Wangu” (uk.2) ubeti wa 4
17
“Masharo wanakufata kwa swaga zao aaa!”

Neno aaa! linaonesha mshangao ambayo ni nidaa katika shairi hilo

Methali katika ufundi wa utungaji washairi huingiza methali katika kazi zao kwa lengo la aidha
kutoa onyo au msisitizo wa jambo.katika diwani ya "MOYO" shairi la “Karibu Tena” (uk.4)
ubeti wa 3

Ndondo si chururu

Haba na haba

Mdokezo, ni hali inayoonyesha kuendelea kwa kitu au jambo fulani. Hii imejitokeza katika
diwani ya "MOYO" shairi la “Karibu Tena”. (uk 4) ubeti 5

“Nonino na ..............nini sijui”

Misemo na nahau, pia mwandishi ameweza kuhusisha misemo na nahau kwenye kazi yake hii
inadhihirisha unguri wake katika utunhaji wa kazi za kishairi na katika diwani ya "MOYO"
shairi la Mwanangu. (uk 19) ubeti 1

“Asitaajabie ya Musa mamboye,

Yafirauni kuyaona mamboye.

...........................”

Kwa ujumla waandishi nguli wa mashairi ni wale waandishi wanaozingatia kanuni/sheria au


kaida za uandishi wa ushairi. Hivyo basi waandishi wa Diwani ya MOYO na NIMEKUJA NA
HABARI ni waandishi nguli wa maishiri kwani wameweza kuzingatia sheria mbalimbali za
uandishi wa ushairi kwa kuzingatia vipengele mbalimbali vya kifani kama mtindo, muundo na
matumizi ya lugha, ambayo vimesaidia kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira. Lakini
waishiiri (Kulikoyela Kahigi na Mugyabuso Mulokozi) wameshindwa kuzingatia sheria na
kanuni hizo, hivyo hawawezi kuwa washairi nguli kuliko wote.

18
MAREJELEO

Abeid A. (1954). Sheria za kutunga mashairi na Diwani ya AMR. EALB, Nairobi

Kahigi K. K(1979). Diwani ya Mageuzi. Dar es salaam press. Tanzania

Kezilahabi, E , (1976). Ushairi wa Mapokeo na wakati ujao. Katika Mbonde J. P. 121-137

Mbwillow. S. N(2017). Diwani ya Moyo. Mwimbe printers . Bagamoyo- Tanzania

Mponzi Z. P & Lucas. C. B(2023). Diwani ya Nimekuja na habari. CBL Company Limited
Mwanza - Tanzania

Mulokozi M. M(2012). Diwani ya Tenzi tatu za kale. Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili (TUKI)
Chuo kikuu Cha Dar es salaam

Mulokozi, M. M na Kahigi K. K(1982). Kutunga Ushairi na Diwani zetu, TPH, Dar es salaam

Robert S.(1958). Hotuba juu ya Ushairi JeASC 28/1:37-42

Senkoro, F. E.M(2011) Fasihi. Dar es salaam press and publicity centre

Wamitila. K. W(2003). Kichocheo cha fasihi simulizi na andishi Nairobi. Focus publishers

19
.

20

You might also like