You are on page 1of 14

WAHUSIKA NA MOTIFU YA SIRI KATIKA KAZI TEULE ZA

NATHARI TEULE ZA FASIHI YA KISWAHILI

• BEATRICE NYAMBURA NJERU


• AM12/29214/17
• WASIMAMIZI:
• PROF. JOHN KOBIA
• DKT. ALLAN MUGAMBI
• CHUO KIKUU CHA CHUKA
YALIYOMO
• UTANGULIZI
• SUALA LA UTAFITI
• LENGO LA UTAFITI
• SWALI LA UTAFITI
• UMUHIMU WA UTAFITI
• UPEO WA UTAFITI
• MWAUO WA MAANDISHI
• MISINGI YA KINADHARIA
• MBINU ZA UTAFITI
• MATOKEO YA UTAFITI
• MAPENDEKEZO YA UTAFITI WA BAADAYE
UTANGULIZI
• Motifu- kipengele cha kijadi kinachohusu kurudiwarudiwa kwa wazo au dhamira fulani katika sehemu
kubwa ya kazi za fasihi (Mulokozi, 1996).

• Ni wazo linalotawala kazi ya fasihi (Allen, 2000).

• Siri- habari au jambo au jambo lililofichwa (TUKI,2004).

• Motifu ya siri- matumizi ya mbinu ya kuficha mambo yanayojitokeza na kujirudiarudia katika kazi ya fasihi
na kuitawala kazi hiyo ya fasihi (Karama na wengeni, 2018).

• Nathari- bunilizi au tungo za kisanaa zinaziwasilishwa kwa lugha ya kawaida na ya mjazo.

• Mhusika- mtendaji katika kazi ya kifasihi na huwa ni kielelezo cha viumbe wanaopatikana ulimwenguni
ingawa si lazima sifa zote za mhusika zifungamane na za binadamu (Wamitila, 2008).
SUALA LA UTAFITI

• Kadri mtafiti ajuavyo, hakuna utafiti ambao umefanywa ili kuweka


suala kuhusu mchango wa wahusika katika ujenzi wa motifu ya siri
wazi katika kazi teule za nathari za fasihi ya Kiswahili, pengo ambalo
utafiti ulilenga kuziba.
LENGO LA UTAFITI
• Kuchunguza jinsi wahusika wanavyofanikisha ujenzi wa motifu ya siri
katika kazi teule za nathari za fasihi ya Kiswahili.
SWALI LA UTAFITI
• Je, wahusika katika kazi teule za nathari za fasihi ya Kiswahili
wamefanikisha ujenzi wa motifu ya siri?
MWAUO WA MAANDISHI
• Macharia (1988), ameangazia motifu ya safari katika kazi za Ayi Kwei Armah kama
kipengele cha kimuundo ili kuonyesha namna vipengele vya kimuundo vinaweza
kufanikisha utunzi wa kazi ya kifasihi na kujenga motifu ya safari.

• Wamitila (1997), amehakiki baadhi ya kazi za Kezilahabi kwa kuzingatia kigezo cha
motifu ya dunia na maisha.

• Nyabunga (2005), ametafitia motifu ya safari katika riwaya ya Bina-damu!

• Ngesa (2015), ametafiti kuhusu mwingilianomatini katika tamthilia za Kiswahili za


Mashetani na Kijiba Cha Moyo. Ameangazia motifu kama kipengele cha
kimwingilianomatini tu kwa kuongozwa na Nadharia ya Mwingilianomatini.
…MWENDELEZO
• Karama na wengine (2018), wamehakiki utanzu wa ushairi kwa
kuangazia utenzi wa Siri La Asrari uliotungwa kwa kuendeleza motifu
ya siri.

• Matundura (2018), ameeleza kuhusu motifu ya siri na kupendekeza


kazi mbalimbali zinazoendeleza motifu ya siri katika ukuzaji wa
dhamira na maudhui ya waandishi wa kazi hizo. Alipendekeza kuwa
motifu ya siri iangaziwe katika kazi zile kwa kuangalia kama kazi hizo
zinaingiliana ama zinatofautiana kimtindo na kimaudhui.
MISINGI YA KINADHARIA
• Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na
Kristeva (1969).

• Wataalamu wa nadharia hii huamini kuwa msomaji wa kipekee ni


mwandishi anayesoma kazi nyingine ya fasihi na kuiona kazi hiyo
kama kazi inayojisoma tena na tena na kujiandika.

• Wataalamu wengine waliorejelea nadharia hii ni: Abram (1981), Leitch


(1983), Eagleton (1983), Coyle na Wengine (1990), Barry (1995), Allen
(2000), Wamitila (2002) na Kehinde (2003).
…MWENDELEZO
MIHIMILI
• Waandishi hutunga matini zao kutokana na matini za awali wala hawaziandiki kutokana na mawazo yao.

• Maana ya matini haipatikani katika matini yenyewe, bali inajengwa na msomaji katika matini husika na
mseto wa matini nyingine zinazotajwa na kurejelewa katika usomaji.

• Mawasiliano baina ya mtunzi na msomaji huambatana na mwingiliano uliopo baina ya maneno na namna
yalivyokuwa katika matini za awali.

• Matini ya kifasihi inaweza kujidhihirisha au kujihusisha na matini nyingine kiwaziwazi, kwa kunukuu,
kudondoa, kutaja, kurejelea au kusilimisha sifa za matini za awali au kwa kuwa katika mkumbo mmoja
kifasihi.

• Matini yoyote ile inahusiana na muktadha wa kitamaduni au kijamii uliozalishwa na haiwezi


kutenganishwa nao.
MBINU ZA UTAFITI
Utafiti wa kifasihi uliochukua mwelekeo wa kimaelezo uliohitaji kueleza
data iliyokusanywa.

Ulifanyika maktabani

Sampuli maksudi iliteuliwa na ilihusisha vitabu vinne vya riwaya na vitatu


vya fasihi ya watoto vilivyokuwa na dhana ya siri kwenye mada.

Data ilichanganuliwa kwa njia ya kimaelezo kwa kuongozwa na lengo la


utafiti
MATOKEO YA UTAFITI
• Kategoria nane za wahusika:
• Mhusika bui- mwandani (Musa kwa Bi. Mwalongo)

• Mhusika bapa- asiyebadilika (mkutubi, Sajin Melik)

• Mhusika mfoili- kinyume cha mhusika nguli na husaidia kuibua sifa halisi za nguli (Musa- mpelelezi, Mateso- mwoga)

• Mhusika huria- wahusika wengi katika mmoja (Bi. Mwalongo, Mwanaziza)

• Mhusika kani- anabadilika mwanzoni na mwishoni mwa hadithi na kutoeleweka (Majimarefu, Mheshimiwa Assad)

• Mhusika akisi- habadiliki na hutumiwa na mwandishi kuyatazama mambo fulani ambayo yangepita bila kutambuliwa (Liyongo, Chiku,
Fadhili)

• Mhusika nguli- shujaa (Musa, Liyongo)

• Mhusika ghibu- mpinzani wa nguli (Majiarefu, Daudi Mringwari)


MAPENDEKEZO YA UTAFITI WA
BAADAYE
• Utafiti wa baadaye utafitie vipengele vingine kama mbinu za uandishi
zinazofanikisha ujenzi wa motifu ya siri

• Utofauti unaojitokeza katika nathari teule kwa kuangazia vipengele


vilivyoangaziwa au kujiegemeza kwa vipengele vingine vya kimtindo
na kimuundo

• Kutumia nadharia zingine


•#TAMATI#

•SHUKRANI

You might also like