You are on page 1of 7

East African Journal of Swahili Studies, Volume 3, Issue 1, 2021

Article DOI: https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349

East African Journal of Swahili Studies


eajss.eanso.org
Volume 3, Issue 1, 2021 EAST AFRICAN
NATURE &
Print ISSN: 2707-3467 | Online ISSN: 2707-3475
SCIENCE
Title DOI: https://doi.org/10.37284/2707-3475
ORGANIZATION
Original Article

Si T̪end̪i zot̪ʰe za Kabla ya Karne ya Ishirini ni Utambaji wa Kingano


Nyengine ni Ufunzaji: Kiyelelezo cha Ut̪end̪i wa Siri li Asrari
Mohamed Karama1, Rocha Chimerah2 & Kineene wa Mutiso3
1 Chuo Kikuu cha Kabianga, S.L.P 2030 – 20200, Nairobi, Kenya.
* ORCID ID: https://orcid.org/0000-0003-2341-9966; Barua pepe ya mawasiliano: mkarama@kabianga.ac.ke

DOI ya Nakala: https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349

Tarehe ya Uchapishaji: IKISIRI

26 Juni 2021 Fikra iliyomo katika mawand̪a ya fasihi ya Kiswahili ni kuwa ut̪ end̪i ni maelezo
marefu ya mapisi ya jamii kiushairi. Makala haya yanat̪ aka kuonesha kwamba
Istilahi Muhimu: si t̪ end̪i zot̪ ʰe zenye madhumuni haya. Kupitiya Ut̪ end̪i wa Siri li Asrari
tut̪ aonesha kwamba mtʰunzi Mwanalemba alikuwa na niya t̪ angu mwanzo ya
Siri li Asrari, kuweka d̪arasa kuhusu hirizi ya majina ya Mwenyezi Mungu. D̪arasa hii
Utendi, ameigawanya kama namna t̪ aasisi za kielimu zinavopendekeza ienreshwe
Darasa, kiskuli na ameyat̪ owa mawazo yake kit̪ aalamu. Nadhariya ya Usemezano
Hirizi, kupitiya dhana ya Unrimi imetusaidiya kuuwangaziya ut̪ end̪i huu na
Islam. tumefaidika na vigezo va: maudhui, ut̪ euzi wa misamiat̪ i na mitinro ya
uwasilishaji, na mukt̪ adha wa matʰumizi ya maneno hayo kama njiya ya
kutambuwa aina ya lugha inayotʰumika. Kwa kwangaziya mitinro ya
uwasilishaji katika d̪arasa ya hirizi tumepata kujuwa kwamba mtʰunzi alikuwa
na dhamira ya kutufunza badala ya kutamba hadithi ya kingano.

APA CITATION
Karama, M., Chimerah, R. & Kineene, M. (2021). Si T̪end̪i zot̪ ʰe za Kabla ya Karne ya Ishirini ni Utambaji wa Kingano
Nyengine ni Ufunzaji: Kiyelelezo cha Ut̪ end̪i wa Siri li Asrari. East African Journal of Swahili Studies, 3(1), 51-57.
https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349.
CHICAGO CITATION
Karama, Mohamed, Rocha Chimerah and Mutiso Kineene. 2021. “Si T̪end̪i zot̪ ʰe za Kabla ya Karne ya Ishirini ni Utambaji wa
Kingano Nyengine ni Ufunzaji: Kiyelelezo cha Ut̪ end̪i wa Siri li Asrari”. East African Journal of Swahili Studies 3 (1), 51-57.
https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349.
HARVARD CITATION
Karama, M., Chimerah, R. and Kineene, M. (2021) “Si T̪end̪i zot̪ ʰe za Kabla ya Karne ya Ishirini ni Utambaji wa Kingano
Nyengine ni Ufunzaji: Kiyelelezo cha Ut̪ end̪i wa Siri li Asrari”, East African Journal of Swahili Studies, 3(1), pp. 51-57. doi:
10.37284/eajss.3.1.349.

IEEE CITATION
M. Karama., Chimerah, R. and Kineene, M., “Si T̪end̪i zot̪ ʰe za Kabla ya Karne ya Ishirini ni Utambaji wa Kingano Nyengine
ni Ufunzaji: Kiyelelezo cha Ut̪ end̪i wa Siri li Asrari”, EAJSS, vol. 3, no. 1, pp. 51-57, June. 2021.

51 | This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
East African Journal of Swahili Studies, Volume 3, Issue 1, 2021
Article DOI: https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349

MLA CITATION
Karama, Mohamed, Rocha Chimerah and Mutiso Kineene. “Si T̪end̪i zot̪ ʰe za Kabla ya Karne ya Ishirini ni Utambaji wa
Kingano Nyengine ni Ufunzaji: Kiyelelezo cha Ut̪ end̪i wa Siri li Asrari”. East African Journal of Swahili Studies, Vol. 3, no. 1,
June. 2021, pp. 51-57 doi:10.37284/eajss.3.1.349.

UTANGULIZI haswa mfano Parker (1982) akinukuliwa na Shariff


(1984, uk. 152), kuwa ni maudhui yenye kueleza
Ut̪ end̪i wa Siri li Asrari (soma Siri) una bet̪ i t̪ isaini kisa kingano. Anapozungumziya uwamilifu wa
na zaidi zenye kuzungumziya hirizi ni nini na ut̪ end̪i Shariff (1991, uk. 45) anasema kwamba, “
umuhimu wake katika maisha haya na ya akhera. ut̪ end̪i una umuhimu mkubwa katika kuelimisha na
Mwanamwarabu bint̪ i Bwanalemba1 (ajulikana piya kufurahisha jamii.” Makala haya yat̪ aonesha
kama Mwanalemba), mtʰunzi mwanamke wa ut̪ end̪i kwamba kwelimisha huku kwatokana na kufunza
huu, anamsemesha mhusika wake, Malaika Jibril, kwenye mandhari ya d̪arasani. Njogu na Chimerah
katika bet̪ i hizo kwa njiya isiyo ya kimasimulizi ya (1999) na Chimerah (1989) wanat̪ owa kiyelelezo
kingano yenye kueleza ‘hadithi’ au ‘hekaya’ ili cha namna d̪arasa lat̪ akikana liyenreshwe wakat̪ i wa
wasikilizaji wasikize na kufurahiya ufunzaji kama inavyopend̪ekezwa na T̪aasisi ya
yanayotʰongolewa. Makala haya yat̪ aonesha Kut̪ ayarisha Mt̪ alaa wa Elimu ya Kenya (K.I.C.D)
kwamba Siri ni d̪arasa yenye muunro maalumu wa na kiyelelezo hichi nricho kinachotufahamisha
kiuwasilishaji wa kit̪ aalamu na una malengo kwamba kwelimisha kuna mfumo na mfumo huu
makhsusi yanayot̪ arajiwa kupatikana. una miyunro inayotʰumiwa ili lengo linalot̪ arajiwa
Imetuthubut̪ ukiya katika mapitiyo yetʰu kuhusu lipatikane. Makala haya hayat̪ ofwata, mguu kwa
ut̪ end̪i huu kuwa suala hili la Siri ina shabaha ya mguu, mpangiliyo huu wa T̪aasisi; imet̪ osheleza
kufunza halijashughulikiwa kamwe. kutujuza kwamba kuna miyunro ya kufunza na
mtʰunzi aliitʰumiya miyunro fulani ili kufunza
Vijelezi vinavyot̪ olewa na fikira inayoenrelezwa hadhira yake – wasomaji na wasikilizaji wa ut̪ end̪i
kuhusu ut̪ end̪i ni kwamba, “ni utʰungo mrefu wenye wake.
kwelezeya kisa au jambo kuhusu mtu/jamii”
(Shariff, 1988:94). T̪end̪i maarufu katika fasihi ya Bakhtin (1986) anasema kwamba lugha ina lugha
Kiswahili Hamziya, Al Inkishafi, Mwanakupona, nyingi nrani yake ambazo hujit̪ okeza katika
Rasil Ghuli, Mwana Fatuma zaeleza kuhusu mawanda t̪ afauti t̪ afauti na mikt̪ adha t̪ afauti t̪ afauti.
matʰukio fulani katika maisha ya mtʰu (aghalabu Lugha hii inabeba maudhui ya yat̪ akayosemwa;
Mtʰume Muhammad) na majagina wa Kiislamu. mitinro ya lugha makhsusi it̪ akayotʰumiwa
Ut̪ end̪i wa Mwanakupona umejit̪ owa katika kunri kuyasema mawazo hayo; na, muhimu zaidi,
hili la visa na kujiangaza kama mawaidha (wasiya). mukt̪ adha upi ut̪ akaosababisha mawazo hayo
Ijapokuwa Siri ni masimulizi ya vita baina ya kusemwa kwa namna inavot̪ arajiwa. Mambo haya
Mtʰume Muhammad (nguli wa ut̪ end̪i huu) na matatu nriyo yanayoleta athari ya kuyasema
Andharuni (nruli wa ut̪ end̪i huu), sehemu hii ya vita, maneno hayo. Kut̪ okana na msingi wa nadharia hii
ambayo iko mwanzo wa ut̪ end̪i wenyewe, ina lengo ya Usemezano inayoshadidia kuwako kwa nrimi
la kit̪ aalamu na wala si kutamba kisa au hadithi katika lugha moja basi makala haya yat̪ ashika aina
kama tut̪ akavothibit̪ isha katika makala haya. moja ya nrimi zilizorat̪ ibishwa nayo ni: usemaji wa
kit̪ aalamu. Bakhtin (1986) anasema kila ulimi
Mapitiyo yetʰu ya yaliyoandikwa kuhusu ut̪ end̪i huu (lugha) una misamiat̪ i na mtinro t̪ afauti wa
yaonesha kwamba bado hayajashughulikiya mada uwasilishaji inayoitambulisha kuwa ni sajili kamili
hii ya lengo la kiufunzaji – kwa maana ya kufanya t̪ afauti na sajili nyengine. Kwa mint̪ arafu hii ya
d̪arasa kuhusu jambo kwa mpangiliyo wa kit̪ aalamu t̪ afauti za kimitinro, makala haya yat̪ aangazia
au kiskuli. Maelezo kuhusu ist̪ ilahi ya t̪ end̪i katika namna lugha hii ya kit̪ aalamu inavojit̪ okeza na
fasihi ya Kiswahili inajulikana, na kushikiliwa nrivo

1
Katika Dammann (1940:274) “bwanalemba” alimtaja Bwanalemba kuwa Ahmad bin Alwy bin
inatanbihishwa kuwa ni lakabu. Kulingana na Ustadh Muhammad Faqihil Muqaddam “Swahibul A’maim”
Muhammad Al Beidh (r.a) katika “Hali ya Afrika (mwenye malemba).
Mashariki” ZCTV Live Agosti 2011 kwenye Youtube,

52 | This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
East African Journal of Swahili Studies, Volume 3, Issue 1, 2021
Article DOI: https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349

kuut̪ afautisha Siri na t̪ endi nyengine maarufu tunaweza kuangaliya misamiat̪ i inayotumiwa
kiufunzaji. pamoja na mitinro ya kusema mawazo hayo. Kwa
kufuwata vidokezi hivi viwili, katika sehemu hii
UFUPISHO WA SIRI tut̪ aweka wazi ainat̪ i za nrimi alizotʰumiya mtʰunzi
wa Siri kwenresha d̪arasa yake hadi tufunukiwe
Siri unaanza kwa kutʰongolewa hadithi ya vita baina kwamba Siri ilidhamiriwa kufunza na wala si
ya Mtʰume Muhammad na Andharuni. Andharuni utambaji wa kihadithi. Kiyelelezo cha Njogu na
aliwanyanyasa wakaaji wa mji wa kwao na wanat̪ i Chimerah (1999, uk. 141) kinaeleza kwamba
wakamlalamikiya Mtʰume Muhammad kuwaokowa d̪arasa, kama inavyopend̪ekezwa na K.I.E (sasa
na vit̪ imbi va Andharuni. Mtʰume Muhammad K.I.C.D), ina mpangiliyo huu: Juma (la ngapi katika
akaitikiya mwitʰo huwo kwa kupeleka jeshi la mfululizo wa ufunzaji), Kipindi, Funzo, Mada,
waislamu kuonrosha udhalimu wa Andharuni. Shabaha (lengo), Somo (hatuwa mbalimbali za
Awali, Andharuni alionesha ujabari mkuu kwa somo hilo), Marejeleo, Vifaa, Mazoezi, na
kuwapiga waislamu bila huruma kut̪ okana na nguvu T̪athmini/Kujit̪ athmini. Hii nriyo miyunro-mbinu
za hirizi aliyoirithi kut̪ oka kwa mababu zake. ya mpangilio wa d̪arasa. Makala haya yat̪ achukuwa
Mtʰume Muhammad kusikiya hayo alikuja kiyelelezo hichi kama kurunzi ya kutwangaziya
kuviyona vita hivi na akaomba nusura kwa Mola ili miyunro-mbinu hii lakini hatut̪ otumiya mbinu zot̪ ʰe
waislamu madhaifu wasiangamizwe na Andharuni. wakat̪ i wa kuuweleza Siri.
Mungu akamjulisha, kupitiya malaika Jibril,
Mtʰume Muhammad kwamba Andharuni ana hirizi Kufungua D̪arasa
na nriyo inayompa nguvu hizo za kiajabu. Mtʰume
Muhammad akaomba apawe yeye hirizi hiyo na Siri umeanza kama t̪ end̪i nyengine za kale kwa
alipopawa bado alienreleya kushinrwa katika vita kumtaja Mungu mwanzo kabla ya kutʰongowa
hivi. Baadaye, Mtʰume Muhammad akaomba t̪ ena ut̪ end̪i wenyewe. Baada ya kumsifu na Mtʰume
kwa Mungu na akamshinra Andharuni. Katika Muhammad na jamaa zake na kuonesha ut̪ ukufu wa
sehemu ya pili, Mtʰume Muhammad anakuja Muumba, Siri unaanza kwa kut̪ owa anwani ya
kwelezewa na Mwalimu Jibril (malaika mtukufu) ut̪ end̪i huu. Mtʰunzi anasema:
faida ya hirizi hiyo ambayo ni ya majina mat̪ ukufu
ya Mwenyezi Mungu. Mwandishi anatusisitiziya 21. Nimependa kunudhumu
tushikamane na hirizi hiyo ya majina ya Mungu ili Hadithi ya muungamu
itufaidi hapa duniyani na kesho akhera. Katiti iliyo tamu
Sikizani watambuzi.
Kifani, ut̪ end̪i huu unaanza na kumalizikiya kama
t̪ end̪i nyengine maarufu za Kiswahili kwa sifa 22. Hadithi hinu hiyari
ambazo zimedokezwa na Shariff (1988) na Mazrui Isimu tawakhubiri
na Syambo (1992). Katika utangulizi kuna Ni Siri li Asrari
kumwomba Mungu na kumswaliya Mtʰume Ndio itwao wayuzi.
Muhammad na jamaa zake. Halafu ni sehemu ya Katika bet̪ i hizi mbili mtʰunzi anatʰwambiya jina la
vita baadaye inakuja sehemu ya mafunzo ya hirizi, ut̪ end̪i huu. Katika ubet̪ i wa 22 mshororo wa tatu
na hatimaye, kuna kufunga darasa pamoja na mtʰunzi anasema ut̪ end̪i huu waitʰwa Siri li Asrari
maombi kwa waislamu. Mwisho kabisa ni kutaja yaani ‘siri ya masiri’. Kimuunro sehemu hii imekuja
jina la mtʰunzi na nasaba yake na t̪ arehe ya baada ya sehemu ya utangulizi ambayo ililemeya
kukamilisha kuutʰunga ut̪ end̪i huu. katika kumuomba Mungu ampe mtʰunzi usahali wa
kutʰongowa ut̪ end̪i wake. Kwa hivyo, kwa kutupa
D̪ARASA YA SIRI sisi anwani ya masimulizi yake, mtʰunzi
ametupeleka mpaka d̪arasani kutwonesha kwamba
Tumesema huko nyuma kwamba kufunza d̪arasani maneno yake yot̪ ʰe mada yake ni ‘Siri li Asrari’.
kuna mtinro wake maalumu wa uwasilishaji. Katika
mtinro huu kuna miyunro-mbinu ambayo hutumiwa Pili, katika ubet̪ i wa 21 mshororo wa kwanza
ili lengo linalot̪ arajiwa lipatikane. Pili, tumesema mtʰunzi ametumiya neno ‘nudhumu’ ambalo lina
kwamba katika kujuwa t̪ afauti za lugha/sajili maana ya kit̪ aalamu. Hii ni ist̪ ilahi ya kifasihi

53 | This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
East African Journal of Swahili Studies, Volume 3, Issue 1, 2021
Article DOI: https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349

inayot̪ afautisha ‘nudhuma’ na ‘shairi’. Kulingana na anamweleza kuhusu hirizi ni nini na piya kumpa
Ust̪ adh Mahmoud Mau (maongezi naye Novemba faida zake. Pili, anamfund̪isha Mtʰume Muhammad
2012, Lamu) pana t̪ afauti baina ya ‘nudhumu’ na bila ya yeye Mtʰume kutiya neno hata moja katika
‘shairi’. Anasema ‘nudhumu’ ni “tʰungo zenye d̪arasa hii. Tatu, anamfunguliya Mtʰume
kumili kwenye mas’ala ya kidini na hasa Muhammad kwamba hirizi hii ni ya majina
yaliyotʰuna na huwa hazina ubunifu (urongo). mat̪ ukufu ya Allah. Na mwishowe, anamwambiya
‘Shairi’ ni “tʰungo zenye kulemea kwenye mada kwamba ni jina moja t̪ ukufu la Mwenyezi Mungu
ambazo hazina ukali, kama mahaba na mambo nriyo liliyomo ndani ya hirizi hino.
mengine ya kikawaida katika jamii.” Tʰungo za
kishairi zaweza kuwa za kibunifu na zaweza kutiwa Mtinro wa uwasilishaji wa aina hii hupatikana
urongo nrani yake. Tukumbuke neno hili nudhumu aghalabu katika mihadhara ya kichuwo au
ndilo alilotʰumiya mwenye Al Inkishafi. Kwa hivo, makongamanoni. Mhadhiri hupawa nafasi yake
mtʰunzi alianza ut̪ end̪i wake kwa kutupa anwani ya aelezee waliyohudhuriya maelezo yake yot̪ ʰe bila ya
masimulizi yake na kutʰwambiya kweupe kwamba kukatizwa ili mawazo yawaingiye sawasawa
ni nudhumu ambayo haina urongo ndani yake. waliyohudhuriya. Piya, mhadhiri nriye aliyepawa
Mas’ala ya kweleza ukweli mtupu (facts) jukumu la kusema kwa kipinri hicho na wengine
hupatikana katika mazingira ya kit̪ aalamu na wot̪ ʰe ni wangoje hadi mwisho ikiwa wana maswali
hukusudiwa kuwapasha habari muhimu au mushkili wowot̪ ʰe waulize. Kwa hivyo, kwa
wasikilizaji. Lakini piya ni d̪arasani ambako kuwa kuna mhadhiri na kuna waliyohudhuriya
mwalimu hut̪ owa mada ya somo la siku mwanzo wa t̪ aswira hii tʰwaweza kuiyona katika d̪arasa wakat̪ i
d̪arasa kama kiyelelezo cha K.I.C.D hapo juu mwalimu anapowafunza wanafunzi kwa sababu
kinavoashiriya. yeye nriye mjuzi na wanafunzi wametʰuliya
wakimsikiza mwalimu awambiyayo.
Usuli Na Kwenreleza D̪arasa
Kurejeleya Mawazo ya Wengine
Kama ilivo katika mapendekezo au t̪ ʰafit̪ i katika
tangulizi zao huwa kuna ‘usuli wa ut̪ afit̪ i’. Katika Kurejeleya mawazo ya wengine yanapotʰumika
sehemu hii huelezwa nrani yake asili ya t̪ asnifu ya katika kazi zozot̪ ʰe za kit̪ aaluma nriyo uungwana na
mpend̪ekezaji ilianza vipi. Kwa maneno mengine, inavot̪ akikana kihakika. Mawazo hayo yanapawa
huweza kwelezwa ilikuwaje mpaka somo hilo la marejeleo ili ikihit̪ ajika ithibat̪ i basi wat̪ aalamu
ut̪ afit̪ i likaonekana lafaa kut̪ afit̪ iwa. Maelezo haya wat̪ afwatiliya kazi zilizorejelewa na kuhakikisha;
ya ‘usuli wa somo’ tunayapata katika maelezo ya kut̪ orejeleya mawazo ya wengine ni hat̪ iya kubwa
mukht̪ asari wa ut̪ end̪i ambao kwetu sisi si hadithi ya katika t̪ aaluma. Mtʰunzi Mwanalemba hakuwacha
vita baina Mtʰume Muhammad na Andharuni kurejeleya hadithi ya ut̪ end̪i huu aliipata wapi.
(kutoka ubet̪ i wa 32 hadi 376) bali ni maelezo ya Anasema:
kad̪imu kuhusu hirizi hii yenye nguvu za kiajabu.
Yanateka muhadhara mwanzo kwa kuwapa mapisi 28. Panenewa, huwambia
ili waelewe maelezo muhimu yat̪ akayokuja baadaye Katika hadithi piya
kuhusu hirizi. Kwetʰu sisi, hii ni mbinu Nyingi zimezotukia
inayopatikana katika sehemu za kit̪ aaluma na Sahihi ya matongozi.
maelezo haya yana jukumu yanayot̪ ekeleza katika 29. Zilio sahihi, tama
kufikisha t̪ asnifu ya msemaji. Japo tʰwaweza Katika hadithi njema
kusema ni utambaji wa hadithi ya kingano kut̪ okana Za mtume wa kadima
na matʰumizi ya lugha ya kitamathali lakini Nayo hiyo ni azizi.
kiufunzaji ina jukumu la kut̪ owa ushahidi wa jambo
lililotʰukiya au kuwapa wanafunzi asili ya watʰu 30. Yalipokewa, yuwani
kufwata au kufanya jambo fulani. Na Anasa muumini
Bunu Maliki, mneni
Jinsi ya kupeleka d̪arasa tunaiyona kwanziya ubet̪ i Mola mezompa razi.
wa 429 – 532. Katika ut̪ end̪i huu, Mwalimu Jibril
(mtʰunzi amemwita hivo nrani ya ut̪ end̪i)

54 | This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
East African Journal of Swahili Studies, Volume 3, Issue 1, 2021
Article DOI: https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349

Katika ubet̪ i wa 30 mtʰunzi anasema maelezo yake ina kazi kubwa inayofanya katika kut̪ ibu maradhi.
yanat̪ okana na upokezi kut̪ oka kwa Anas bin Malik, Anasema hivi:
huyu alikuwa swahaba wa Mtʰume Muhammad.
Katika bet̪ i za 28 na 29 mtʰunzi anatʰwambiya 455. Hirizi hinu Mtumi
kwamba hii ni Hadithi sahihi – ni ya daraja ya juu Huzidi li aksami
katika ukweli. Kwa hivo, anayoyasema mtʰunzi Kwa mara mia msemi
yana thika ya ukweli na kwamba yanayoelezwa Ifadhiliye wayuzi.
yanafuwata t̪ arat̪ ibu za kit̪ aaluma ya dini kwa kutaja 456. Li aksami shafi'a
marejeleo ya mpokezi wa maelezo haya. Mbali ya Izidiye manufaa
kutaja mpokezi wa hadithi hii ni nani piya mtʰunzi Kwa ya sefu li kati'a
anafanya uwad̪ilifu wa kit̪ aaluma kwa kumtaja Ifadhiliye majazi.
shekhe au msimulizi wa kisa hichi kila inapofika
457. Na sefu li kata'ani
hat̪ uwa ya kuonesha maneno hayo si yake bali ni ya
Ifadhiliye yakini
mtʰu mwengine, shekhe au mpokezi wa hadithi hii.
Kwa maratu thalathini
Anarud̪iya usemaji huu mara kadhaa katika Siri,
Imezidi maongezi.
mfano:
458. Na fadhili yenye siti
108. Kala Shekhe mtukufu Za sefu li kati'ati
Unenee msanifu Huzidi mbingu na nti
Mwenye radhi ya Latifu Kwa mara kumi ndombezi.
Na Mtume muongozi.
Bet̪ i hizi zinatupa ufunuwo kwamba hirizi ina
148. Kala shekhe amenena ‘aksami’ (ubeti wa 455 mshororo wa pili) yaani ina
Mwenye kurawi maana sehemu/vigawanyo. Kuna sehemu ya ‘kat̪ i’a’,
Hadithi ya nabiyana ‘kat̪ i’at̪ i’, ‘kat̪ a’ani’ na kila sehemu ina nguvu zake.
Muhamadi Muhijazi. Sehemu ya ‘kat̪ i’a’ (ubeti wa 456 mshororo wa tatu)
ina kazi yenye kuleta pozo la magonjwa yot̪ ʰe.
Tut̪ aona katika bet̪ i hizo kwamba mtʰunzi
Sehemu ya ‘kat̪ i’at̪ i’ (ubet̪ i wa 458 mshororo wa
anatʰumiya ‘kala shekhe’ yenye maana ya
pili) ina uwezo zaidi ya uzitʰo wa mbingu na ardhi
‘amesema shekhe’ na ‘amenena mwenye kurawi’
mara kumi yake. Sehemu ya ‘kat̪ a’ani’ (ubeti wa
yenye maana ya ‘amesema mwenye kuisimuliya
457 mshororo wa kwanza) ina nguvu zaidi ya mara
hiyo hadithi’ kurejeleya alivosema huyo
thalathini. Nilipomuuliza Ust̪ adh Mahmoud Mau
mtʰongowaji wa hadithi. Ni dhahiri kuwa mtʰunzi
(khj) kuhusu vigawanyo hivi alinambiya yaweza
mbali ya kuwa ni kazi ya kifasihi lakini alijuwa
kuwa hirizi hii ni hiyohiyo moja lakini mtʰunzi
kaida za kit̪ aalamu za kurejeleya mawazo ya
ameipa sehemu kadhaa kwa sababu ya kut̪ imiza
wengine ili asije akakoseya adabu za kaida hizo,
arudhi ya kina katika ut̪ end̪i. Walakini, kwa dhahiri
sembuse kuwafikiyana na mfumo wa uwasilishaji
na maelezo ya mtʰunzi mwenyewe katika ut̪ end̪i,
darasani wa Njogu na Chimerah (khj).
tunaona kwamba kuna sehemu tatu za hirizi hii
Ufafanuzi Juu ya Hirizi t̪ ukufu na kila moja ina kazi na uwezo wake.
Kid̪arasa huu ni ufafanuzi wa ziyada ili wanafunzi
Mwalimu baad̪a ya kut̪ owa anwani na kut̪ owa waelewe kwa uzuri dhana ya hirizi na vigawanyo
kijelezi kuhusu mada anayoiyeleza siku hiyo vake.
huweza kut̪ owa ufafanuzi zaidi kuhusu mada yake.
Faid̪a za Hirizi
Kwa mfano, ikiwa mada anayoshughulikiya ina
vigawanyo katika maelezo basi at̪ avit̪ owa hivo
Katika masomo ya, kwa mfano, jiografiya ya
vigawanyo ili wanafunzi wapate kuelewa vema
binadamu, wanafunzi huelezwa sekta zot̪ ʰe za
mada. Azma ya mwalimu ni wanafunzi waiyelewe
kiuchumi nchini na piya huelezwa faida za sekta
dhana pamoja na sehemu kadha wa kadha katika
mbalimbali zinavojenga nchi. Mbinu hii ina
dhana hiyo. Mtʰunzi Mwanalemba anatupa maana
ushawishi wa kuwat̪ aka wanafunzi watiliye
ya hirizi na piya anakuja kutʰwambiya kwamba
maanani sekta hizi na wao wajishughulishe katika
hirizi hii ina sehemu tatu ndani yake na kila sehemu

55 | This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
East African Journal of Swahili Studies, Volume 3, Issue 1, 2021
Article DOI: https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349

ujenzi wa taifa kupitiya sekta hizi. Mfano huu wa amezirat̪ ibisha moja baada ya nyengine katika bet̪ i
kut̪ owa dhana na halafu kut̪ owa faida iliyo nazo kwa moja moja kama wafanyavo walimu wa shule
binadamu tunaushuhudiya katika Siri. Katika ut̪ end̪i mad̪arasani. Kuhusu faid̪a ya hirizi mtʰunzi
huu mtʰunzi amet̪ owa faida kumi na sit̪ a za hirizi na anatʰwambiy:

402. Ni matukufu pulika 474. Siku ya kufa basiri


Maina yakwe Rabuka Hawaonani umuri
Na mtu mwenye kwandika Na Munkar wa Nakiri
Menali mangi majazi. Hawamwandiki maozi.

404. Mtu hoyo mfadhala 475. Wala kabisa haoni


Kinwa maina ya Mola Zituko za kaburini
Wepukane na madhila Mtu hoyo kwa yakini
Milele hana kinyezi. Ya Rabi memhifazi.

405. Hangiwi maisha yake 476.Yuwa mtume rasuwa


Ni msiba mpulike Dua hinu ikuziwa
Katika moyoni mwake Ulimwenguni ni dawa
Ila kwitwa ni Azizi. Kwa kula mawi marazi.

406.Walau hamu na ghamu 477. Na Ahira ni zaidi


Hawi nayo kwa dawamu Hutekeleza ahadi
Mtu hoyo muadhamu Na kuokoka na abadi
Mungu amemhifazi. Na harufu na kinyezi.

407. Na siku hiyo bashiri 479. Humpa Mola Mkwasi


Ya Kiyama kudhihiri Pepo ya Firdausi
Hufungamana umuri Kangiya ndani upesi
Na maina ya Muyuzi. Ziunguni kabarizi.

472. Dua hinu Mustwafa 507. Manufaaye basiri


Ni kama mtu wa sifa Nda Rihi li Ahmari
Alowakifu Arafa Huziwiya kula shari
Siku ya Juma muyuzi. Na baa za wazimzi.
473.Thawabuze tatongowa 516. Na yambo ulitakalo
Mtu takoitukuwa Lolote ulipendalo
Dua hinu ya sitawa Ukalinuwiliyalo
Hapati la kumuuzi. Hulipata uli razi.

Katika bet̪ i hizo hapo juu, maneno tuliyoweka kwa bila wasiwasi t̪ ena anatuonesha mahali na wakat̪ i
herufi za mlazo nrizo faid̪a za hirizi. gani.
Tunafahamishwa kwamba hirizi hii inaweza kut̪ ibu:
magonjwa ya kiwiliwili (ubeti wa 404, 405, 406), Hit̪ imisho La D̪arasa
magonjwa ya kiakili ya majini wabaya (ubeti wa
507), kuepusha mateso ya kaburini (ubeti wa 474, Wakat̪ i mwalimu anapokaribiya kufunga d̪arasa
475), mwenye hirizi hii haogopi misukosuko ya siku yake huweka sehemu ya hit̪ imisho ili kut̪ owa
ya kiyama (ubeti wa 407, 477), na huko akhera mtʰu mukht̪ asari na piya kusisitiza lengo la somo hilo. Hii
huyo at̪ apawa pepo ya juu kabisa ‘jannat̪ u firdausi’ ni mbinu ya kimasomo ili kusakinisha mawazo
(ubeti wa 479). Niya ya mtʰunzi-mwalimu ni kut̪ aka ambayo yamet̪ olewa katika d̪arasa na kumshawishi
kushawishi kwamba hirizi hii inaweza kufanya kazi msikilizaji akubali yale aliyoelezewa baad̪a ya
kuyafahamu. Bakhtin anasema katika masemezano

56 | This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.
East African Journal of Swahili Studies, Volume 3, Issue 1, 2021
Article DOI: https://doi.org/10.37284/eajss.3.1.349

huwa kuna ‘sentensi za mst̪ ari wa mbele’ ambazo, aliyotʰumiya mtʰunzi wa Siri ili kutufunza d̪arasa
mosi, hujulisha mipaka ya kauli za wasemezanao yake juu ya hirizi: vigawanyo vake, ufaafu wake
na, pili, hubeba msisitizo wa yale yaliyosemwa kwa magonjwa tuyaonao na tusiyoyaona, na ithibat̪ i
katika kauli nzima. Ni mpaka kwa sababu huonesha ya kufanya kazi kwake katika hali ya kijamii kama
kauli ya mtʰu mmoja iliyanza wapi na imekomeya kwenye vita baina ya Mtʰume Muhammad na
wapi. Sentensi hizi huwa na sifa ya kurudiliya niya Andharuni. Kut̪ okana na tuliyobainisha ni wazi
yenyewe ya maneno kusemwa. Katika ut̪ end̪i huu Mwanalemba alitupa d̪arasa na alilipanga namna ya
kuna bet̪ i mbili ambazo ziko mbali mbali kimaweko kutujuza mengi katika d̪arasa hiyo na kwamba si
lakini zasema kauli moja. Mtʰunzi anasema hivi: kama inavofikiriwa kwamba t̪ endi za Kiswahili za
kabla ya karne ya ishirini ni utambaji wa hadithi za
Tena ina manufaa kingano tu. Tʰwaregeleya tena kuwa ut̪ end̪i wa Siri
Mtu atakaovaa bado haujashughulikiwa kwa mapana na marefu
Humwepukiya baa yake kuna mas’ala yasiyo ya kidini kama muktadha
Na zitimbi za gharazi. na mandhari ya kutʰungwa kwake yahit̪ aji ufafanuzi
ili upate kweleweka kwa uzuri zaid̪i.
551. Hirizi hinu wendaka
Mtu kombe kilandika MAREJELEO
Anwapo na kuipaka
Hasaliwi ni marazi. Bakhtin, M. M. (1981). The dialogic imagination.
Micheal H. (mtafsiri na mhariri) Austin: The
Bet̪ i hizi mbili ambazo ziko mahala t̪ afauti katika
University of Texas Press.
ut̪ end̪i zinarejeleya jambo moja – umuhimu wa
hirizi hii ya majina ya Mwenyezi Mungu. Katika Bakhtin, M.M. (1986). Speech genres and other late
ubet̪ i wa 25 mtʰunzi anatʰwambiya kwamba hirizi essays. Caryl, E. & Micheal H., (wah.) Austin:
hii mtʰu at̪ akapokuwa nayo basi hashikwi na The University of Texas Press.
magonjwa yoyot̪ ʰe. Na katika ubet̪ i wa 551 mtʰunzi
anaregeleya mawazo yayo hayo. Mwanzo wa ut̪ end̪i Chimerah, R. M. (1989). The implications of the
anatupa fununu kwamba hirizi hii ina manufaa selected works of Ngugi in theeducational
makubwa na katika hit̪ imisho lake la ut̪ end̪i piya thinking and practices of Kenya. Tasnifu ya
anatʰwambiya vivyo. Juu ya kwamba ni sentensi za Uzamifu (Haijachapishwa). Ohio University,
mstari wa mbele lakini kwetu sisi bet̪ i hizi zaonesha Ohio.
hit̪ imisho la mwalimu katika d̪arasa yake na
zasisitiza kauli yake t̪ angu mwanzo kwamba Dammann, P. E. (1940). Dichtungen in der Lamu
maelezo anayoyat̪ owa nriyo ‘siri ya masiri’. mundart des Suaheli Band 28.Hamburg:
Freiderichesen.
HIT̪IMISHO
Mazrui. A. & Syambo, B. K. (1992). Uchambuzi wa
Makala haya yamejaribu kupinruwa kauli kwamba fasihi. Nairobi: East AfricanEducational
t̪ endi za kabla ya karne ya ishirini zilitʰungwa Publishers.
kweleza mapisi ya mtʰu/jamii t̪ u. Kut̪ okana na
Njogu, K. & Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa
miyunro-mbinu ya namna mtʰunzi anavoenreleza
fasihi: Nadharia na mbinu. Nairobi: The Jomo
maudhui yake imedhihirika kwamba Mwanalemba
Kenyatta Foundation.
alikuwa na dhamira ya kutufunza kuhusu hirizi na
umuhimu wake na aligawanya darasa yake katika Shariff, I. N. (1984). Letters to the Editor. Katika
vigawanyo venye kulanrana sawasawa na maelezo Research in African Literatures, 15 (1), 150-156.
ya K.I.C.D. Hatukuchukuwa kiyelelezo chote cha Imesomwa
K.I.C.D kuwa mfano wa kuenresha d̪arasa ya https://www.jstor.org/stable/3819755 .
mtʰunzi bali tumet̪ aka kuonesha, kwa ithibat̪ i,
kwamba kufunza kuna muunro unaopendekezwa na Shariff, I. N. (1988). Tungo zetu: Msingi wa
t̪ aasisi za kielimu. Kwa kufwata muunro huu, mashairi na tungo nyenginezo. New Jersey: The
tumedhihirisha madhumuni mbalimbali Red Sea Press.

57 | This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License.

You might also like