You are on page 1of 2

Insha ni kifungu cha maneno kinachoeleza juuu ya habari fulani au mada fulani.

Aidha kuna wataamu


mbalimbali waliofasili dhana ya insha, wasili hao nikama wafuatao.( Robert, 1967:16) anasema: insha ni
maandiko mema yakawaida ambayo yanauwezo wa kunburudisha mtu. Hii inamaana mwamba
nimaandiko yasiyokuwa na usanaa wowote ndani, maneno yakawaida na yanaweza kusomwa na kila
mtu akaelewa. Shabani robert anaendelea kufafanua kuwa, "insha ina namna yake ya mpango na
ufasaha; na kila shairi lina namna yake ya sanaa na mtibdo".

Msokile (1993:82) anasema: ni utungo wa nathari wa kitaluma juu ya jambo fulani. Maandishi yanayotoa
habari juu ya jambo fulani; maandishi ya nathari yanayojadili jambo ama wazo moja kwa ufupi ama
mapana juu ya mada ambayo hujadiliwa kwa ufasaha. Wamitla (2007:1) anasema: ni utungo wa kisanaa
unaozungumzia swala au au kusimulia kisa fulani. Utungo huo huwa na urefu wa wastani. Kisa hicho au
suala hilo ndio mada ya utungo huo. Mrikaria (2009:20) anasema: ni utungo wa sentensi zenye kuelezea
juu ya mada au jambo fulani. Vike vile insha unaweza kufasiriwa kuwa na utungo wa maneno kwa
mtindo wa nathari huu ya jambo fulani au habari fulani ambayo inaweza kuwa ni kazi ya ubunifu aua la.

Mlokozi (1996:45) anasema: ni maandiko ya kinathari yenye kuelezea, kuchambua au kuarifu juu ya
mada fulani. Hata ivo, Mlokozi anasema: insha nyingi ni fupi nahuwa na maneno kuazia 5000 mpka
100000. Lakini pia kuna insha chache mfano tasnifu zenye urefu wa kutosha wa kueleza jambo au suala
fulani.

Nagala na mdali (2008:47) wametoa sifa bia za insha, hii inamana kwamba ili insha iweze kuwa bora
lazima iwe na sifa hizi zifuatazo; kwanza, insha hutumia lugha sanifu kuambatana na aina ya insha
husika. Pili, huzingatia alama za uakifishaji ili kumwezesha msomaji kubaini ujumbe uliomo. Aidha,
mada iliyotolewa izingatiwe, mwandishi asi sambayesambaye tu pasi kuzingatia mada inayoandikwa. Na
mwisho, sentensi sahili, changamano na ambatano husaidia kupamba insha. Hivyo basi kupitia sifa hizi
zunasaidia kuonesha ubora wa insha ya mwandishi.

Insha imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni.,

Insha za wasifu. Hizi ni insha ambazo hueleza sifa za watu au wanyama kama wanyama, milima, miti au
mahali fulani. Unsha hizi huandikwa na mwandishi kwa lengo la kutoa sifa au kusifia juu ya kitu fulani au
jambo fulani. Insha za wasifu malanyingi hupendwa sana na watu wengi tofauti na insha za hoja.
Malanyingi watoto hupendelea katika aina hii ya insha kutokana na usanaa unatumika katika uandishi
wa insha hizi. Mfano insha inayo insha zinazo husu milima mikubwa au ya kutisha, insha zinazo husu miti
mikubwa, mazingira au mtu ambaye ni shujaa. Katika insha za wasifu lugha unayotumiwa malanyingi ni
lugha ya kisanaa ambayo humvutia msomaji katika usomaji.

Insha za hoja. Insha hizi huelezezea jambo katika hali ya kijenga hoja ambazo zinatetea msimamo
alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo analo lizungumzia. Kusudi la insha za hija ni kuhabarisha
na kutoa ushahidi kwa hoja. Pia aina hii ya insha imepewa kufundisha uwezo wa wanafunzi kujadili hoja
mbalimbali ili kujenga uelewa kwa kwanafunzi juu ya jambo fulani. Wakati wa kuandika habari hii vi
vema kuzingatia ukweli wa habari badala ya maoni binafsi na upendeleo. Ndalu (2009:46) amesema:
insha inaweza kugawanyika katika makundi ya fuatayo; insha za maelezo, insha za tarifa, insha za wasifu,
insha za kubuni, insha za hadithi, insha ya barua na insha tegemezi. Anaendelea kusema kuwa, insha za
maelezo hizi ni insha zinazo eleza juu ya jambo fulani. Mfano, unaweza kuambiwa kuandika insha
kuelezea juu ya mfululizo wa picha. Pia insha za tarifa hizi ni insha zinazotoa tarifa au habari kwa lengo la
kujulisha. Mathalani, ukiandika insha ya mpango jinsi ya kuepuka ukimwi utakuwa umeandika insha za
tarifa.

You might also like