You are on page 1of 4

NAMNA YA KUANDIKA ISHA

Isha ni kazi ya kifasihi ya uandishi juu ya jambo la kweli linalojumuisha masimulizi ya


maelezo ya kina na uchambuzi kuhusiana na mada maalumu hasa kutoka kwa mawazo na
hoja binafsi.
Katika uandishi wa insha jambo muhimu kuzingatia ni kwamba insha yoyote inahusisha
vipengele vikuu vitatu. Hapa nimeanisha yanayoweza kuwa malengo yako katika
uandishi wa isha yenye vipengele hivyo;
1. Mwanzo wa isha; vuta mawazo ya msomaji na elezea mwelekeo wako
2. Katikati mwa isha; tunategemea uandishi pointi za
msingi za insha yako na maelezo yake kwa undani.(si
kirefu).
3. Mwisho mwa insha; peleka uandishi wako katika
mwelekeo wa mtazamo wako zaidi.
Vuta hisia za msomaji

MWANZO WA INSHA;
Wakati unaanza isha zingatia yafuatayo;-
• (a)Vuta hisia za msomaji
• (b) Eleza mwelekeo wako
(a).Vuta hisia za msomaji
mfano
Christopher Columbus anasemekana kuwa mtu wa kwanza kugundua bara Eleza uelekeo wako
la marekani ya kaskazini, lakini hali hii inadhaniwa kuwa ni mtazamo
uliopitwa na wakati kwa kadri ya miaka 500. Ugunduzi mpya unaonyesha
kuwa idadi kubwa ya wapelelezi walifika kabla ya Christopher Columbus huko bara
amerika kabla ya mwaka 1492. Ushahidi unaonyesha kuwa mataifa mengi yanaweza
kujinadi kufika amerika kabla ya Columbus.

Hapo juu ni mfano tuu wa namna ambavyo utaweza kuanza insha yako, lakini si hivyo tu
kuna njia/mbinu nyingine unazoweza kuzitumia katika kuanza insha yako.
Mfano;-
• Anza na swali- ni mpelelezi gani wa kale anaetajwa kama aligundua bara
marekani ya kaskazini? (angalizo, sishauri njia hii itumike kujibia isha za mitihani
ya shule/chuo).
• Anza na taarifa za kuvutia/kushangaza- ingawa inasemekana kuwa columbus ni
mpelelezi wa kwanza kufika kugundua bara amerika lakini inadhaniwa kuwa huu
ni mtazamo uliopitwa na wakati kwa miaka 500.
• Anza na nukuu-“inawezekana kuwa amerika haikuwahi kugunduliwa. Mimi
binafsi naweza kusema kwamba iligunduliwa” oscar wilde.(njia hii inafaa zaidi
kama uandishi utaruhusu matumizi/uwepo wa rejea kama insha za elimu ya juu)

Clement Chipindula. Page 1


(b)Eleza uelekeo wako
Kwa kawaida Uandishi mbalimbali wa isha una sentesi ya mwelekeo.(focus) hii ni sentesi
inayoeleza nini hasa ujumbe wa uandishi wa insha husika.
Mfano isha yeyote ya utafiti au uchambuzi ina swali la ubunifu(thesis statement)
Senetensi ya ubunifu-hoja, wazo (linalotolewa kimantiki).(sentensi ambayo
haijathibitishwa lakini inayotoa mwelekeo wa mjadala) wapelelezi wa kale wa dunia
walikua wengi kila mahali katika marekani ya kusini kama nchi ya watu wa jamii tofauti
toka sehemu mbalimbali.
Sentesi yenye Oni, wazo au dhana, isha inayovutia ina oni au wazo linalojenga ushawishi
kwa msomaji. Kuwasili kwa Columbus katika amerika kusichukuliwe au kuitwa kama
ugunduzi wa bara la amerika.

Uandishi wa aya za katikati ya insha


Hapa ikumbukwe kua ni sehemu ambayo mjadala wa oni ,wazo au dhana unatolewa
maelezo, isha isiyokidhi viwango inaweza kuchangiwa na kuwepo kwa maelezo mengi
yasio na maana yeyote zaidi ya kujaza aya za mhandishi bila kujadili yalio ya msingi.
Katika kila aya kunawasilishwa eneo dogo la mjadala (point) , nashauri eneo dogo la
mjadala litajwe mwanzoni mwa aya. Mambo mengine yanayotarajiwa kuwemo ni katika
kila aya ni kama yafuatavyo:-
• Anza na eneo dogo la mjadala(point)
• Toa maelezo ya kukazia(supporting details)
• Tumia viunganishi elekezi kuunganisha mtazamo kati ya wazo dogo moja na
lingine.
• Toa sentesi ya mwisho wa isha( hapa nashauri iwapo unajibu mtihani basi utaje
walao mfano wa jambo linalojadiliwa, kama si mtihani, basi si lazima kutaja
mfano)
Inaaminika waafrika wengi walitemebelea amerika ya kaskazini kabla ya Columbus
kama ushahidi wa spears Columbus uliopatikana marekani kaskazini unavyodhitisha.
Mikuki hii ilifanana kwa kila hali na mikuki ambayo iliundwa afrika. mfano wa mikuki
hiyo ni ile inayopatikana katika nchi ya guinea.
Uikacha hilo, pia waafrika inawezekana walitembelea marekani kabla ya columbus kwa
kuzingatia uthibitisho wa kupatikana kwa mitumbwi inayofanana na ile ya kiafrika.
Mitumbwi hiyo pia yasemekana ina muundo sawa kabisa na ile iliyotumika katika mito
mingi ya kiafrika kama vile nile,congo na niger.
Baada ya hapo pia columbus mwenyewe aliripoti kuwepo kwa waafrika katika nchi ya
panama.hii inamaanisha waafrika hao walifika hapo kabla yake na walifanya shughuli
zao kabla yeye hajagundua bara amerika.

n.b fanya mpangilio wako wa eneo dogo la mjadala wako wa aya uwe mwongozo wako
wa mtiririko wa aya za katikati mwa insha. Ukipanga kulingana na mtiririko itapendeza
zaidi, mfano kufuata umri,ukubwa,kufahamika zaidi na kadhalika
Kwa maoni yangu kipengele hiki kinaonyesha kuwa kuna aya tatu za mjadala, kwa faida
ya kujibia mtihani aya tatu hizi zinaweza kutengwa kama zilivyo zikibeba eneo dogo la
mjadala kila moja,hii itakuwezesha kupata alama kwa kila aya. Hata hivyo inaweza kuwa

Clement Chipindula. Page 2


ni aya moja kwa isha ndefu ambazo si za kujibia mitihani na badala yake zenye lengo
lingine. Hapa aya zinaweza kufanywa kama maelezo ya kukazia na hivyo kuwa aya
moja( inategemea na idadi ya hoja ulizonazo).

Nini hasa ni viunganishi elekezi? (Transitions)


Katika kila baada ya aya moja ya katikakati ya isha tunatumia kiunganishi kutupeleka
katika hoja inayofuata.
Viunganishi elekezi ni maneno au sentesi ambazo zinaunganisha hoja. Hizi zinaweza
kuonyesha yafuatayo.
• Kuonyesha mahali (hapo juu….)
• Kuonyesha muda (baadae ……)
• Kulinganisha hoja/dhana( kama ilivyo……)
• Kutofautisha dhana ( licha ya …….)
• Kukazia mjadala(pia inaweza kuwa….)
• Kuhitimisha(mwisho…..)
• Kuongezea taarifa(kwa kungezea…)
• Kueleza wazi(kwa mfano……mfano mwingine….)
Hii ni baadhi tu ya mifano mingi ambayo unaweza kuitumia kuunganisha aya zako za
isha.
Hapo mwanzo watu walidhani Columbus amagundua amerika. Hata hivyo tunajua sasa
kuwa watu wa Vikings walitia nanga pwani ya amerika miaka 500 iliyopita.
Tunafafahamu walifika newfoundaland lakini ushahidi unaonyesha pia walikaa sehemu
inayojulikana sasa kama USA.

Kwa kuongezea hapo kuhusu Vikings kuna ushahidi kuwa wapelelezi kutoka china afrika
na wales walitia nanga amerika ya kaskazini kabla ya Columbus.
(viunganishi vinaweza kutumika pia ndani ya aya. ni vizuri zaidi kwa isha ndefu)

Namna ya kuandika mwisho wa insha/hitimisho.


Hii ni sehemu ya mwisho ya isha yako. Kumbuka sehemu hii ndipo ambapo msomaji
atagundua hitimisho lako juu ya mjadala ulionza mwanzo wa insha.
Wakati unaandika hitimisho fanya yafuatayo;-
• Elaeza tena mtazamo wako,
• Fupisha hoja zako au sababu/muhtasari
• Mwache msomaji akiwa na jambo la kufikiri kuhusu mjadala.
Kama unaandika insha ya uchambuzi husisha na mwito wa kuchukua hatua.

Hivyo basi inaonekana kuwa Columbus hakuwa wa kwanza kutoka sehemu nyingine za
dunia kufika amerika(mtazamo). Inashangaza na kufurahisha kufikiri kuhusu watu
tofaouti ambao walifika pwani ya amerika kaskazini. (fupisho la hoja zote). Nchi hii
imekua siku zote kama sehemu yenye jamii tofauti hata kabla haijazaliwa.(jambo la
kufikiri)

Clement Chipindula. Page 3


MPAKA HAPO TUMEONA KWA KIFUPI NI JINSI GAni unaweza kuandika insha
kwa kuzingatia vipengele vitatu vya mwanzo,katikati na mwisho mwa insha. Ikumbukwe
kuwa hii si kanuni ya kudumu ya uandishi ni mapendekezo tu ya namna ya uandishi wa
kitaaluma wa insha. Zipo aina nyingi za uamdishi wa insha kwa kutegemea na jambo
husika.
Nawatakia masomo mema tukutane katika matini nyingine tutakapojaribu kuchambua
namna maswali ya isha ynavyoulizwa na jinsi ya kujibu kwa kuangalia maneno ya
msingi/ufunguo (key words) .

Asante
Chipindula C.

N.B(kazi hii imefanywa kwa msaada mkubwa wa ecncyclopedia Encarta 2009)

Clement Chipindula. Page 4

You might also like