You are on page 1of 32

Naratolojia ni dhana inayolejelea usimuliaji katika kazi za kifasihi; huweza kupambanua matukio

mbalimbali kwa uwazi au la kutokana na aina ya usimuliaji. Huweza kujenga uelewa wa maudhui kama
usimuliaji ulikuwa wa moja kwa moja na wa wazi au huweza kufanya maudhui kutoeleweka kwa wazi
kama usimuliaji huakuwa wa wazi. Mfano katika kitabu cha Mzingile kilichoandikwa na E. Kezilahabi.
Vile vile kipengele hiki cha usimulizi ni muhimu kwani ndicho ambacho hubainisha mwendo katika kazi
husika, pia huweza kuonyesha nafasi ya uwakati katika kazi husika.

Kuna aina kuu mbili za usimulizi katika kazi za kifasihi (hasa fasihi andishi) ambao ni usimulizi
shahidi ambazo katika usimuliaji wake hutawaliwa na matumizi ya nafsi ya kwanza kwa kiasi
kikubwa. Pia huweza kuhusisha matumizi ya nafsi ya pili. Huu ni usimulizi bora kwani husimulia
mambo ambayo msimuliaji ana uhakika nayo kwani mara nyingi huwa yamemtokea au kuyaona
yeye mwenyewe. Kwa kuwa husimulia mambo mengi, pia huweza kuufanya mwendo wa kazi
husika kwa wa polepole.

Pia kuna usimulizi maizi ambao hutumia nafsi ya tatu katika kusimulia. Huweza kuruka baadhi ya
mambo na hata kufanya mwendo wa kazi husika kuwa wa kasi kwa sababu msimuliaji husimulia
mambo ambayo kwa namna moja au nyingine husimulia mambo ambayo hayajampata yeye au
kuyashuhudia kwa macho yake na badala yake huwa amesimuliwa tu.

Katika kitabu hiki cha Msako aina hizi zote za nafsi zimetumika kwa namna tofauti tofauti.
Mwandishi Naguib Mahfouz ametumia usimulizi shahidi hasa katika dialojia nyingi kama vile
katika ukurasa wa 47 kuna matumizi ya nafsi ya kwanza umoja pale anaposema;

“Kila nitakapojisikia kufanya hivyo…”

Pia kuna matumizi ya nafsi ya kwanza uwingi katika ukurasa wa 51;

“Tuna habari ya kushangaza kwa ajili yako…”

Mwandishi ametumia nafsi ya kwanza ili kujikaribisha na uhalisi kwa kumpa mhusika maneno na
matendo ambavyo hadhira kuamini kuwa jambo linalosemwalipo kama lilivyo.
Pia kuna matumizi ya nafsi ya pili katika kitabu cha Msako kama ilivyoonekana katika ukurasa wa
46 pale anaposema;

“Umewezaje kuja chumbani kwangu…”

Pia katika ukurasa wa 52 mwandishi anasema;

“Wewe ndiye mgeni, …”

Vilevile kitabu hiki kwa kiasi kikubwa kimesheheni matumizi ya nafsi tatu umoja na uwingi kama
ilivyooneshwa na mwandishi. Mwandishi katika kukisimulia kisa chake kwa kiasi kikubwa
ametumia nafsi ya tatu umoja kama ilivyonukuliwa katika baadhi ya kurasa kama vile katika
ukurasa wa 1 pale anaposema;

“Aliudhiwa na mguso huo na kimyakimya akamlaani huyo aliyemgusa. Mtu huyo ni nguruwe
kama …”

Pia katika ukurasa wa 50 mwandishi anadhihirisha hilo pale naposema;

“Alizinduka huku kijasho chembamba kikimtoka, akipumua kwa nguvu. alikuwa kwenye
chumba chake pale hotelini…”
Pia kuna matumizi ya nafsi ya tatu uwingi kama vile katika ukurasa wa 112 pale anaposema;

“Walimkuta na fedha zilizoibwa.”

Hivyo katika kazi hii matumizi ya nafsi zote yametumika katika kuisimulia kazi hii. Hata hivyo
kwa kiasi kikubwa mwandishi Naguib Mahfouz ameonekana kuegemea zaidi katika matumizi ya
nafsi ya tatu umoja kwa sababu kadhaa lakini kubwa zaidi ni kutaka………

MWENDO

Mwendo ni mtiririko hasi na mshindilio wa vitushi katika riwaya kwa kuzingatia msuko, masafa ya
wakati na masafa ya kijiografia. Mwendo wa riwayahusika hujengwa na msuko wa vitushi,
maudhui, masafa ya kiwakati na ya kijiografia. Hivyo kupitia vipengere hivi msomaji wa riwaya
husika ataweza kung’amua mwendo wa kazi husika. Kutokana na vipengere hivi kuna aina tatu
zamwendo kama ifuatavyo;

Mwendo wa kasi, katika mwendo huu masafa ya kiwakati huenda harakaharaka kwa maana
kwamba katika shughuli nzima ya usimulizi wa hadithi husika, muda au wakati wa matukio na
matendo mbalimbali katika kazi husika huwa ni wa harakaharaka zaidi. Pia maudhui ya kazi
zenye aina hii ya mwendo huwa ni ya kifutuhi asilimia kubwa. mbali na maudhui, masafa ya
kijiografia katika kazi zenye aina hii ya mwendo ambayo huhusisha utajaji wa majina ya maeneo
na sehemu mbalimbali kulingana na madhari iliyotumika katika andikohusika, huwa ni wa
kimasafa ya kasi zaidi kutokana na kutajwa kwa maeneo tofauti tofauti yaliyo mbali kijiografia.
Vilevile katika mwendo huu, huwa kuna msuko wa vitushi uendao haraka. Kwa kifupi katika aina
hii ya mwendo shughulinzima ya usimulizi hufanyika kwa kasi zaidi.

Mwendo wa kati, mwendo huu huchanganya maudhui ya kitanzia na ya kifutuhi na katika hali
nzima ya masimulizi huchukua muda kutoka katika maudhui fulani kwenda katika maudhui
mengine. Mbali na hilo, masafa ya wakati na kijiografia husafiri kwa wastani/taratibu kwa maana
ya kwamba sio wa kasi wala wa polepole.
Pia kuna mwendo wa polepole, sifa za mwendo huu ni kwamba, maudhui ya kitanzia hutawala kwa
kiasi kikubwa katika kazi husika, masafa ya wakati na ya kijiografia huenda polepole, vilevile
katika mwendo huu kuna sifa ya kujilejelea kwa masimulizi na mwisho kabisa, kazi zenye aina hii
ya mwendo huwachosha wasomaji.

Kwa jumla, riwaya ya Msako ni andiko lenye mwendo wa wastani/kati, hii nikutokana na kukidhi
vigezo na sifa za aina hii ya mwendo kama ifuatavyo;

Suala la maudhui, riwaya ya msako ina maudhui changamani. Hii ina maana kwamba kuna
maudhui ya kitanzia na ya kifutuhi. Kwa mantiki hii basi riwaya hii ni ya mwendo wa kati, baadhi
ya maudhui ya kitanzia yanayojitokeza katika andiko hili ni haya yafuatayo;

Suala la mauaji (vifo). Vifo au mauaji ni suala ambalo limezungumziwa katika riwaya hii
ya Msako kwa mfano, mwanzoni kabisa mwa kitabu kunazungumziwa shughuli ya mazishi ya kifo
cha mama yake Suber (Basima Omran). Hali kama hii kwa hakika inaleta huzuni kwa msomaji,
ukizingatia ni suala ambalo huleta huzuni kwa wanajamii katika jamii zetu. Katika uk.1 aya ya
kwanza mwandishi anasema hivi;

“Macho yake yalijawa na machozi. Licha ya jitihada zake dhidi ya mihemko yake na aibu aliyoihisi
kulia mbele ya watu hawa kwa kweli alizidiwa. Kwamacho yenye machozi alitazama kuelekea kwenye
maiti iliyokuwa ikiondolewa kwenye jeneza na kupelekwa kwenye kaburi lililokuwa wazi…….”

Lakini pia katika uk.86 suala la mauaji limejitokeza pale ambapo mhusika Suber anachukua uamzi
wa kumuua mzee Khahili kwa lengo la kumiliki mali na mwanamke wa mzee huyu. Hivyo suala hili
linaleta huzuni kwa wasomaji na hata katika jamii kwa jumla. Katika ukurasa huo aya ya kwanza
mwandishi anasema hivi;
“Aliunyanyua ule mtarimbo. Ghafla Yule mzee alijigeuza kivivuvivu.Suber alijihisi kuganda pale
alipokuwa amesimama, mikono ikiwa imeinuliwa juu, mtalimbo juu ya kichwa chake. Macho yao
yalikutana.Suber alitambua hatari ya jambo hilo na kuachia mikono yake ishike na kutoa pigo kali.
Yule mzee alipiga ukulele mdogo, halafu manung’uniko kidogo, kasha kimya.”

Vilevile, dhamira nyingine yenye kuleta hali yakitanzia ni suala la kufungwa kwa watu
magerezani/jela (vifungo ). Kwa hakika ni suala ambalo linaleta huzuni kwa wasomaji
halikadhalika jamii kwa jumla pale hukumu za kufungwa jela zitolewapo watu huuzunika japo
kwa upande mwingine watuhufurahia hali hii kulingana hasa na matukio yanayosababisha
hukumu kama hizi. Kwa mfano katika uk.17 aya ya pili mwandishi anasema;

“Yote ni kama ndoto ya ajabu. Niliondoka Alexandria kuja huku kumtafuta baba yangu, halafu vitu
vya ajabu vilitokea ambavyo vilinisababisha kusahau lengo langu la awali na hatimaye kunisukumia
jela.”

Lakini pia suala la kufungwa jela lilimtokea mama yake Suber (Basima Omran) pindi alipofanya
mauaji na kufungwa muda wa miaka mitano. Suala ambalo linasababisha kifo chake punde tu
alipolejea nyumbani. Hili linajidhihirisha katika uk.3 mwishoni kabisa mwa aya ya mwisho.

Halikadhalika kuna suala la utengano dhidi ya wanandoa, jambo ambalo lanasababisha watoto
kukua katika malezi ya upande mmoja wa uzazi. Suala hili linaonekana kusababisha malezi na
makuzi ya watoto yasio mazuri (maadili mabaya) mfano alivyolelewa Suber, hakulelewa katika
maadili mazuri kwa kulelewa na kukukzwa katika maisha ya anasa na starehe na mwisho wake
katika harakati za kumsaka baba yake anaishia katika mikono ya nguvu za dora na kutumikia
kifungo cha maisha jela.

Lakini pia mhusika Elhamu kakua katika malezi ya mama tu baada ya kutengana kwa mama na
baba yake kipindi bado yuko mchanga. Katika uk.54 kuanzia aya ya tatu mwandishi anasema;
“Ninaishi na mama yangu. Familia yetu ipo Qalyoub. Mjomba wangu anaishi Heliopolis. Na tuna mtu
tuliyempoteza katika familia yetu”. Kusema kweli wazazi wangu walitengana nilipokuwa ningali motto
mchanga….”

Mbali na maudhui ya kitanzia kuna suala la mapenzi, ulevi, watu kujishughulisha na shughuli
mbalimbali, umuhimu wa elimu nakadhalika, dhamira ambazo zinasababisha riwaya hii kuwa na
maudhui changamani na hatimaye kukidhi vigezo vya kuwa na mwendo wa wastani kama
ilivyotambulishwa awali. Lakini pia hata suala la masafa ya wakati na ya kijiografia, ni ya wastani
kutokana na kutajwa kwa maeneo na nyakati (madhari) mbalimbali katika hali isiyokuwa ya kasi.
Kwa mantiki hiyo basi, riwaya ya Msako ni riwaya yenye mwendo wa kati/wastani.

MTINDO

Senkoro (2001), anabainisha vipengere vikuu vitatu vya mtindo ambavyo ni;

Mbinu za kibunilizi au utunzi, hizi ni mbinu mbalimbali wazitumiazo watunzi katika kazi zao.
Mbinu hizi ni kama vile uingizaji wa fani mbalimbali katika utanzu unaoshughulikiwa kama vile
masimulizi, usemezano baina ya wahusika , utomeleaji motifu za safari na kadhalika. Mwandishi
wa riwaya ya Msako kwa kiasi kikubwa amefaulu katika uteuzi wa mbinu mbalimbali za kibunilizi
mfano dayalojia, masimulizi, motifu za safari nakadhalika. Mfano wambinu aliyoiyumia ni motifu
ya safari.

Motifu ya safari ni mbinu ya kiuandishi anayoamua kuitumia mtunzi au mwandishi kwa lengo la
kusukuma kazi mbele na kupitia msukumo huu ndipo matukio mbalimbali, dhamira na jumbe
mbalimbali, madhari na vipengere vingine huweza kujitokeza. Kwa mfano katika uk.17 aya ya pili,
mbinu hii inajidhihirisha pale Suber anapoianza safari yake kutoka Alexandria kuelekea Cairo.
Mwandishi anasema;
“Alexandria ilififia kwa mbali kadri garimoshi lilivyoongeza mwendo kuelekea Kusini upande wa
Cairo. Robo karne yenye kumbukumbu tele ilififia mbali katika alfajiri ile ya majira ya kipupwe,
ilifunikizwa na mawingu meusi yanayotangaza…..”

Motifu ya ndoto, hii ni mbinu ambayo mwandishi huitumia ili kusukuma mbele kazi yake. Katika
mbinu hii, licha ya kuwa mwandishi anakuwa na lengo la kupeleka mbele simulizi lake lakini
mwandishi hukusudia kufikisha ujumbe fulani kwa hadhira. Katika riwaya ya Msako, mwandishi
ametumia mbinu hii kuanzia ukurasa wa 48-50. Katika mbinu hii tunapata dhamira kama dharau
na nafasi mwanamke katika jamii yaani, mtu mwenye kudhauliwa. Mwandishi anasema;

‘‘Niondolee! Nisikuone tena! Wewe ni takataka tu, kama

Mama yako. Huna chochote unachostahili toka kwangu!’’(uk. 50)

Katika mfano hapo juu, unaonesha pale Saber alipokuwa yuko ndotoni akiwa anaota kuwa
amekutana na baba yake na akachana vyeti alivyokuwa amemuonesha kama uthibitisho na
hatinaye kumfukuza na kumtukana.

Kipengere kingine ni uteuzi wa maneno, hiki ni kipengere muhimu sana katika mtindo wa kazi
husika. Katika kukamilisha mtindo ulio bora zaidi, mtunzi wa kazi ya anapaswa kuwa na weredi
wa hali ya juu katika kuteuwa maneno yenye uzito ili kuleta mvuto kwa wasomaji wa kazi yake.
Ufundi wa uteuzi wa maneno ndio unaofanya kazi ya mwandishi ionekane ya pekee. Mawazo yote
aliyonayo mwandishi akilini tayari yalikwisha fanyiwa kazi na waandishi wengine, hivyo uteuzi wa
manemno mazito yenye kujenga taswira, jazanda na ishara akilini mwa msomaji ndiyo
yanayoleta upya wa kazi yake. Mwandishi wa riwaya hii amedhihirisha hili kwa kuteuwa maneno
mbalimbali. Miongoni mwa maneno hayo ni kamavile;

“Nilichezwa machale” uk,10

“Alipiga pafu moja ndefu” uk.7

“Alikuwa bonge la mwanamke” uk.18

“Hakuna ninachoweza kufanya zaidi ya kuwa gangwe, mhuni, kuwadi” uk.5

“Alistafiani kwa mayai, jibini, bilauri ya maziwa na matunda” uk.79 n.k.

Vilevile kipengere kingine ni matumizi ya lugha ya picha na ishara. Lugha ya picha na ishara ni
tokeo la uweredi wa mtunzi katika suala zima la uteuzi wa maneno. Uteuzi wa maneno ndio zao la
ujenzi wa taswira, picha na ishara akilini mwa msomaji. Maneno mazuri aliyoyatumia yanaweza
kumuathiri msomaji kwa kiasi ambacho msomaji huyo anaweza kujenga taswira akilini mwake.
Taswira hizo ndizo zinazomsaidia msomaji kubaini ishara mbalimbali zinazoweza kugundua dhana
ya kitu au mtu fulani. Kwa mfano katika riwaya hii uk.18 mwandishi anasema;

“Alikuwa bonge la mwanamke! Ghafla alijihisi kuamkwa na tamaa iliyokuwa kama imelala na
kumbukumbu za mbali zilizopotelea kwenye ukungu wa wakati.”
Maneno kama “bonge la mwanamke na kuamkwa na tamaa” ambayo yameteuliwa na mwandishi
yanamsaidia msomaji kujenga taswira ya hisi juu ya haiba ya mwanamke aliyekutana na Suber na
neno kuamkwa na tamaa linamsaidia msomaji kuvuta picha na hali aliyokuwa nayo Suber baada ya
kukutana na mwanamke yule. Hivyo taswira kama hizo ndizo zinazoweza kuupa msomaji picha
nzima ya tukio ambalo lingeweza kutendeka kati ya Suber na mwanamke huyo.

Matumizi ya lugha ndiyo mzizi wa kazi ya fasihi, na bila yenyewe kuwepo haiwezekani kuwepo
kazi yoyote ya fasihi.Mwandishi ametumia lugha katika kuyaibua mawazo yake katika kazi
yake.Matumizi ya lugha hujumuisha methali,misemo,nahau,taswira,lugha ya picha na ishara
pamoja na tamathali za semi.Lugha imesanwa vyema na kumsaidia mwandishi kuwa na ubunifu
wa hali ya juu.Katika riwaya hii ya MSAKO mwandishi ametumia lugha kama ifuatavyo;

Mwandishi ametumia lugha inayoeleweka kwa urahisi na moja kwa moja.Hii haina maana kazi
imepyaya katika fani na matumizi ya lugha kwa jumla.Bali ni kuonesha ufundi wake katika kusana
lugha kifasihi kwa namna inayoeleweka kwa hadhira.Mfano ukurasa wa 134 mwandishi
ameonyesha jinsi Saber alivyokuwa jela kwa kutumia lugha inayoeleweka kwa urahisi.

Sasa Saber uko wapi?Jela,peke yako.Hakuna

anaekutembelea.Hakuna yeyote wa kukutembelea.


Pia mwandishi ametumia tamathali za semi katika kazi yake.Tamathali za semi ni viwakilishi au
vifananisho vya dhana fulani kwa dhana nyingine zinazofanana au zinazotofautiana.Ni usemi
wenye kupanua, kupuuza au kubadilisha maana za dhahiri au za kawaida za maneno ili kuleta
maana nyingine.Tamathali za semi hutia nguvu kazi ya fasihi na kuipamba.Katika riwaya hii
mwandishi ametumia sitisri,tashbiha,tashihisi,lakabu pamoja na takriri.

Kwanza, ametumia sitiari.Sitiari ni tamathali inayounganisha vitu au watu lakini bila ya kutumia
viunganishi linganishi kama vile mithili ya, mfano wa, sawa na, na kama.Tamathali hii
huunganisha vitu na watu kana kwamba vitu na watu hao ni sawa kabisa. Mwandishi ametumia
ulinganisho wa Bwana Khalil na ibilisi mzee na mjinga pale Karima na Saber walipokuwa
wanapanga mipango ya kumuua na kutoroka. Msanii anasema ukurasa wa 60

Yeye ni ibilisi mzee na mjinja. Mara tu akihisi

nitaacha kuonana na wewe.

Pia ametumia sitiari ukurasa wa 84 kuonyesha ulinganisho wa fundi bomba na ibilisi laghai pale
Bwana Khalil alipokuwa anampa maagizo Sawi bawabu na kumsisitiza asisahau.Msanii anasema

Yule ni ibilisi laghai. Alikaribia kufa mara nne,

na bado hajajifunza.

Pia mwandishi ametumia tashbiha.Tashbiha ni tamathali inayolinganisha watu, vitu viwili au zaidi
hulinganishwa na watu ama vitu vingine kwa kutumia maneno kama mithili, kana kwamba, mfano
wa, na kama. Mwandishi ametumia tashbiha kuonyesha Bwana Reheimy alivyomfananisha Saber
na mama yake kuwa ni takataka na hana chochote anachostahili kumiliki.Tashbiha hii imeonyesha
mwanamke amechorwa kama kiumbe duni kwa kulinganishwa na takataka. Mfano ukurasa wa 50
mwandishi anasema

Niondokee! Nisikuone tena! Wewe ni takataka tu,

kama mama yako. Huna chochote unachostahiki

toka kwangu.

Mwandishi kwa kiasi kikubwa ametumia tashbiha katika ukurasa wa (50), (51), (53), (56), (58),
(62), (64), (73), (77), (79), (81), na (84).

Tatu, mwandishi ametumia lakabu. Lakabu ni majina anayopewa au kujipa mtu kutokana na sifa
alizo nazo. Sifa hizo huweza kuwa za kiumbo au za kitabia. Mwandishi ametumia lakabu ya bata
mzinga wa porini kumsawiri baba yake Saber ambaye hatulii sehemu moja.Ukurasa wa 145
mwandishi anasema kwa kumtumia mwanasheria

Wajibu wangu uko katika kuielewa kesi yako kwa

kina na, si kumfukuza bata mzinga wa porini.

Nne, mwandishi ametumia takriri.Takriri ni urudiaji rudiaji wa maneno au sentensi kwa malengo
maalum ya kusisitiza. Mwandishi ametumia takriri ili kuwekea mkazo dhamira na kuisisitiza.
Takriri imejitokeza pale Sawi bawabu anapokwenda kumuamsha Bwana Khalil chumbani kwake.
Baada ya kutoitika hivyo, Sawi akarudiarudia kugonga mlango na kuita ili kumuasha Bwana
Khalil ambaye alikuwa ameuwawa na Saber.Ukurasa wa 92 mwandishi anasema

“Bwana Khalil!Amka!Amka!Bwana Khalil imekaribia

Saa mbili kamili”.

Tano, mwandishi ametumia tashihisi.Tashihisi ni tamathali ambayo vitu visivyo na sifa


walizonazo watu hupewa sifa hizo za watu. Mwandishi ametumia tashihisi pale ambapo Saber
alimgusa Elham mkono na kuhisi kila msuli ndani yake ukiimba. Kuimba hufanywa na watu na
sio msuli hivyo sifa ya kuimba ilipewa msuli. Mfano ukurasa wa 66 mwandishi anasema

Alimgusa mkono wake na kuupigapiga taratibu. Kila

msuli ndani yake ulikuwa ukiimba;halafu alimkumbuka

Karima na mpango wao wa kukutana saa chache zijazo.

Sita, tashihisi imejitokeza ukurasa wa 3 ambapo Saber alikuwa njiani kuelekea nyumbani ambapo
alipepewa na upepo unaomburudisha na kubeba harufu nzuri. Upepo umepewa sifa za
mwanadamu;

Akiwa njiani kuelekea nyumbani upepo mwanana


unaoburudisha ulimpepea,ukibeba pamoja nao harufu

nzuri ya majira ya machipuko.

Vilevile, mwandishi ametumia taswira katika kazi yake.Taswira ni picha mbalimbali zinazojengeka
akilini mwa msomaji kutokana na uteuzi na upangaji wa maneno wa mwandishi. Lugha ya picha
na ishara huchangia kwa kiasi kikubwa ujengaji wa taswira. Mwandishi ametumia taswira pale
ambapo Saber alimtazama ombaomba vizuri na kuhisi kinyaa. Msanii anasema ukurasa wa 87;

Yule ombaomba alimpita. Kwa mara ya kwanza aliweza

kumtazama vizuri. Du, anatia kinyaa! Uso mwembamba,

uliokondeana, pua kubwa na macho mekundu, kama

yaliyovilia damu.

Pia mwandishi ameonyesha tawsira ya harufu ya uvundo aliyokuwa anatoa yule ombaomba. Saber
alipitiwa na harufu ya ombaomba yule. Ukurasa wa 87 mwandishi anasema;

Yule ombaomba alimpita na harufu iliyotarajiwa ya


uvundo ambao uliendana na mwonekano wake.

Vilevile, mwandishi ameonyesha taswira ya harufu ya damu aliyokuwa nayo Saber alipokwenda
kwa Karima kutaka kumuua baada ya kupandwa na hasira mno.Ukurasa wa 128 mwandishi
anasema;

“Saber sasa alishikwa na hasira kali mno za kuehusha.

Harufu ya damu ilikuwa kali kwenye tundu za pua yake”.

Vilevile, mwandishi ametumia misemo mbalimbali. Misemo ni maneno yanayotambulisha


mazingira maalum au kuijulisha hadhira wakati unaohusika katika kazi ya fasihi
inayoshughulikiwa. Mwandishi amemtumia Saber aliyeshindwa kulala usiku kucha kwa kusema
usemi usemao, “kutopata lepe la usingizi”. Ukurasa wa 67 mwandishi anasema;

“Usiku mwingine pasipo kupata hata lepe la usingizi”.

Pia, mwandishi ametumia msemo pale mama Saber alipomwambia Saber akamtafute baba yake
baada ya miaka 30 kupita. Mwandishi alitumia msemo wa “kuchezwa machale”.Ukurasa wa 10;

“kama kwamba nilichezwa machale na kutambua


yale amabayo yangetokea”.

Kipengele kinachofuata ni kipengele cha uhusika na wahusika. Kama vinavyojadiliwa katika fasihi.
Dhana hizi zinafafanuliwa kama ifuatavyo.

Mbunda msokile (1993) anaeleza dhana ya wahusika kuwa, wahusika ni watu, wanyama, au viu
katika kazi ya Sanaa ya kifasihi.

Wamitila, k. w (2002) anaeleza kuwa, wahusika ni viumbe wanaopatikana katika hadithi yoyote ile.
Anaendelea kusema kuwa, viumbe hawa huwa ni sehemu ya kazi nzima .

Kwa ujumla, wahusika ni jumla ya viumbe wote, vitu ama kitu chochote ambacho mwandishi au
msimulizi amekipa uwezo wa kubeba matendo na kuhakikisha ujumbe aliokusudia msimulizi au
mwandishi katika kazi ya fasihi unafikishwa kwa hadhira lengwa.

Mwandishi wa riwaya hii ya Msako amewachora wahusika wake kwa namna tofautitofauti. Hivyo,
katika andiko hili tutaangalia wahusika hawa na jinsi walivyochorwa kuuwakilisha uhusika wao.
Pia, kuna wahusika ambao wanafanana majina, hivyo wahusika hawa watatofautishwa kwa
kupewa namba.

SABER.

Huyu ni mhusika bapa ambaye habadiliki na hakui kisaoikolojia. Hii ni kutokna na matendo yake
na tabia zake kutobadilika. Mwandishi amemchora mhusika huyu kama; muuaji, mwizi, mhalifu,
hana mapenzi ya kweli, ni malaya na mhuni. Mwandishi hakuonyesha mabadiliko yoyote ya tabia
ya mhusika huyu. Mwandishi amemchora Saber kama mhusika bapa ili kuonyesha kuwa katika
jamii zetu kuna watu wasiobadika.
SAYED SAYED EL-REHEIMY (1)

Mhusika huyu amechorwa kama mhusika mkwezwa. Yuhu ndiye baba yake Saber.Yaani amepewa
sifa na uwezo uliopitiliza ukilinganisha na uhalisi wa maisha yake yalivyo. Amechorwa kama mtu
maarufu, mpenda starehe, tajiri na mwenye hadhi. Mafano (uk 9) mwandishi anaeleza sifa za
muhusika huyu. Mhusika huyu amechorwa kama mtu tabaka kwani amekuwa mwakilishi wa
tabaka la wenye nacho, pia, kama mtu binafsi kulingna na tabia zake alizokuwa anafanya.

“Yeye ni mtu mwenye kipato kizuri kabisa. Wakati huo alikuwa mwanafunzi bado, lakini hata wakati
huo alikuwa na uwezo wa kutosha na hadhi.”

SAYED SAYED EL-REHEMY (2)

Huyu ni muhusika msaidikzi ambaye dhima yake kubwa ni kuwakilisha dhamira fulani tu. Hii
inajidhihilisha ambapo mhusika huyu anawakilisha tabaka la wenye navyo wenye kumiliki mali
katika jamii. Mfano (uk13)

“ kama tu bahati ingelikuwa upande wake Sayed Sayed El-Rehemy, mumiliki waduka la vitabu la el-
manshiay.”

SAYED SAYED EL-REHEIMY (3)

Huyu ni muhusika msaidizi. Ni mhusika ambaye tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi). Hivyo, ni
mhusika ambaye amewakilishwa dhahili, mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani
anawakilisha tabaka la wafanyakazi kama madaktari. Yeye huyu ni dakitari bingwa wamagonjwa
ya moyo Cairo. Pia amechorwa kama mtu katili sana kwani, alishindwa kumwonea huruma Saber
(uk. 28) mwandishi anasema;

“kwa bahati mbaya mimi si mamlaka inayoshughulukia waliopotea”

SHEHE

Ni mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani anawakilisha tabaka la
wanadini, kwani anawakilisha kundi la watu wanaoamini dini na watu wanaoabudu.Mfano,
(uk16)

“Shehe ambaye alikuwa ameketi huku amekunja miguu akiwa katika tafakuri nzito, alisema, “tafuta
na utapata.”

BWANA KHALIL ABDUL NAGA

Huyu ni muhusika duara. Ambaye huwa anakua kiakili na anabadilikabadilika na ana sifa kamili
za mtu na ana sifa uzuri na ubaya. Ni mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa na
msimulizi (maizi), hivyo ni mhusika ambaye amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama
kama mtu tabaka kwani anawakilisha tabaka la watu wenye kipato yaani matajiri na yeye ni
miongoni mwa matajiri wa jijini Cairo. Mhusika huyu ni mmiliki wa Hotel ya Cairo, ni mme wa
Karima, ni mzee kiumri, ameuawa na Saber.

ALY SERIAKOUS
Huyu ni mhusika mwenye sifa ya ubapa kwani amekuwa habadiliki wala kukua. Hivyo, yeye ni
kijana mwenye tabia nzuri. Ni mhusika ambaye tumemfahamu kwa kusimiliwa na msimulizi
(maizi) wasifu wake. Vilevile ni mhusika ambaye amewakilishwa dhahili. Pia mhusika
tunamtazama kama mtu tabaka kwani anawakilisha tabaka la watu wenye kipato cha chini na
wenye kuhangaika na vibarua kila siku. Ni mchukuzi katika Hotel ya Cairo, ni kibarua wa Khalil,
alihusishwa na kifo cha Khalil, ni kijana mchangamfu na mchapakazi, pia amesingiziwa kesi ya
mauaji, ni mhusika mdogo.

MOHAMED EL-SAWI

a) Ni bawabu katika Hotel ya Cairo.

b) Pia ni mfanyakazi katika Hotel ghiyo.

c) Mshauri wa karibu wa Khalil.

d) Ni mzee na anaipenda kazi yake.

e) Alifanya kazi kwa uaminifu.

Ni mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani anawakilisha tabaka la
watu wenye kipato cha chini na wenye kuhangaika na vibarua kila siku.
ELHAM

a) Ni mwanamke mchapa kazi na anafanya kazi katika ofisi za gazeti la sphinx.

b) Ni mpole na mwenye huruma.

c) Ni mchumba wa Saber.

d) Hamjui baba yake.

e) Ni mwanamke msomi na anayejitambua.

f) Ana mapenzi ya kweli.

g) Ni mwanamke mwenye msimamo.

Ni mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani anawakilisha tabaka la
wafanyakazi.
KARIMA

a) Ni mke wa Khalil.

b) Ni mwanamke asiye na huruma (mkatili).

c) Ni mwanamke msailiti.

d) Ni mwanamke ambaye mali zote za Khalil zipo chini yake.

e) Ni miongoni mwa wauaji Khalil.

f) Ni mwanamke mwenye tamaa na mali.

g) Ni mhanga wa mila potofu, kwani aliolewa na mwanaume asiyempenda kwa sababu ya


umaskini.

Ni mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu binafsi kwani ni zao ambalo linaweza
kujitokeza kwa namna nyingine tofauti na yeye jinsi alivyo.

IHSANI TANTAWI
a) Ni mfanyakazi katika ofisi za gazeti la sphinx.

b) Mwanaume mwenye huruma.

Ni mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu tabaka kwani anawakilisha tabaka la
wafanyakazi.

AMR ZAYED

a) Ni baba mzazi wa Elham.

b) Alimtaliki mkewe (mamaye Elham)

c) Ni msailiti.

d) Mwanaume aliyeitelekeza familia yake.

Ni mhusika ambaye pia tumemfahamu kwa kusimiliwa (maizi), hivyo ni mhusika ambaye
amewakilishwa dhahili, pia mhusika tunamtazama kama mtu binafsi kwani ni zao ambalo linaweza
kujitokeza kwa namna nyingine tofauti na yeye jinsi alivyo.
Mtagusano, ni dhana inayorejelea mwingiliano wa vipengele mbalimbali katika kazi ya fasihi.
Huhusisha mwigo au uwathiriano katika kazi ya fasihi. Mtagusano huweza kujitokeza katika
kipengele cha mandhari ambapo mwandishi hutumia mandhari ambayo si ya eneo husika lakini
anaelezea mambo yanayohusu eneo hilo. Pia hujitokeza katika kipengele cha lugha ambapo
mwandishi hutumia lugha mbili ndani ya kazi moja yaani inaweza kuwa anatumia lugha ya
Kiswahili na wakati huo huo anatumia lugha ya Kiingereza. Halikadhalika, kipengele hiki
hujitokeza akatika maudhui ambapo mwandishi huonesha maiasha ambayo si halisi katika jamii
anayoiandikia. Wakati mwingine mwandishi anaweza kueleza mambo kwa uwazi kiasi kwamba
yanakwenda kinyume na maadili ya jamii husika. Kwa mfano mwandishi anaweza kuwa naeleza
suala la mapenzi lakini namna alivyoyaeleza ameyaeleza kwa namna ya uwazi kiasi kwamba
anakwenda kinyume na idili na tamaduni za jamii ile kwa jumala.

Katika riwaya ya MSAKO mtagusano umejitokeza katika kipengele cha maudhui ambapo
tunamuona mwandishi ameeleza kuhusu mapenzi lakini namna alivyoyaeleza ameyaeleza kwa
uwazi hali inayopelekea kwenda kinyume na maadili ya waafrika. Jambo hilli hujidhihirisha katika
ukursa wa 22, mwandishi anasema;

Hakuna kidokezo cha maongezi yaliyofanyika kandokando ya bahari

Karibu na mitumbwi iliyobinuliwa chini juu, juu chini. Mazungumzo

Yaliyogubikwa na mahaba na nyege kali ya ngono.

Neno ‘nyege’ kama lilivyotumiwa na mwandishi linaleta ukakasi katika kulitamka mbele za watu
kwani ni kinyume na maadili ya kiafrika kueleza mapenzi kwa uwazi. Mwandishi angeweza
kutumia mbinu ya ufumbaji ili kuifanya hadhira yake isijisikie vibaya wakati wa kuisoma kazi
husika.
Pia katika ukurasa wa 47 mwandishi anasema;

‘‘Kila nitakaposikia hamu ya kufanya hivyo’’, Yule msichna alisema

Walipokuwa hoi baada ya kufikia mshindo. Alimlalia kwenye matiti

yake, akiwa hoi katika namna ya kuburudisha.

Katiak mfano huu maneno, ‘alimlali kwenye matiti’ yanaonesha uelezwaji wa mapenzi kwa uwazi
katika riwaya hii jambo ambalo ni kinyume na idili na tamaduni za muafrika.

MSUKO WA VITUSHI

Msuko wa vitushi ni mtiririko wa mawazo, visa na matukio na namna yanavyopangwa na


kufuatana katika kazi fulani ya kifasihi. Msuko wa vitushi huwa na sifa kadhaa ambazo hujenga
mtirirko wa kazi nzima. Sifa hizo ni kama vile; mjongeo, usababishina msukumo/motifu. Katika
riwaya hii ya Msako sifa hizi zimejitokeza kama ifuatavyo;

Usababishi, Katika riwaya hii matukio yameweza kujengwa kiusababishi ambapo tukio moja
linasababisha kutokea kwa tukio linguine. Kwa mfano; tukio la kufa kwa mama yake Suber
(Basima Omran) linasababisha tukio la Suber kusafiri kwenda Cairo kwa lengo la kumtafuta baba
yake (Sayed el-Reheimy). Hili lilitokea baada ya Suber kubaki mpweke bila ya kuwa na ndugu
wala rafiki. Hivyo akaona ni vyema kuanza harakati za kumsaka baba yake na ndicho hasa chanzo
cha jina la riwaya hii. Katika uk…mwandishi anasema;
“Nitaanza maisha mapya huko Cairo, mbali kabisa na mambo haya huku” “Mungu na airehemu roho
yake. Alikupenda mno kiasi cha kukuharibu kuwezakumudu maisha ya aina nyingine.”

Pia kitendo cha kutoka Alexandria kwenda Cairo kumtafuta baba yake kinasababisha Suber
kujihusisha kimapenzi na wanawake wawili ambao ni Karinma na Elhamu, suala ambalo
linasababisha kutokea kwa tukio la mauaji ya mzee Khahili Abdul kwa sababu ya mapenzi. Na
tama yakutaka kumiliki mali yam zee huhu. Katika uk.86, mwandishi anasema;

“Mwenyewe alishangazwa na nguvu ya pigo lile na matokeo ya kuchefua. Yule mzee alipiga ukulele
mdogo halafu manung’uniko kidogo kasha kimya”

Vilevile tukio hili la mauaji linamsababishia Suber kuwa na mgogoro binafsi pia linasababisha
ashindwe kuishi kwa amani baada ya kuanza kufuatiliwa na mapolisi kila alikokuwa akienda na
hatimaye anaishia mikononi mwa nguvu ya dola kwa kutumikia kifungo jela, suala ambalo
linahitimisha shughuli nzima ya msako dhidi ya baba yake mzazi. Pia tukio hili linahitimisha
masimulizi mazima ya hadithi hii.

Sifa nyingine ni Motifu, hivi ni vitu vinavyosukuma matukio kwenda mbele na kufanya masimulizi
yatoke hatua moja kwenda nyingine. Kuna aina mbalimbali za motifu ambazo hutumiwa sawa
katika kazi za kifasihi, kama vile Motifu ya safari, ndoto, mizimu, mashetani, majini na motifu ya
maji (bahari). Katika riwaya ya Msako, motifu kadhaa zimejitokeza kama ifuatavyo;

Motifu ya safari. Msanii hutumia safari za wahusika wake ili kufikisha ujumbe Fulani alioukusudia
kwa hadhira yake. Kaika uk.16-17, safari imejitokeza kupitia mhusika Suber ambaye anasafiri
kutoka Alexandria kwenda Cairo kumtafuta baba yake. Safari hii ya msako inaibua dhamira ya
mapendo. Katika uk.17 mwandishi ameandika hivi;
“Alexandri ilififia kwa mbali kadri gari moshi lilivyoongeza mwendo kuelekea Kusini upande wa
Cairo.”

Halikadhalika Motifu ya ndoto/njozi imetumika. Hii huhusisha uwepo wa ndoto au matendo ya


kinjozi ambayo hayapo. Msanii humchora mhusika akiwa katika hali ya ndoto au njozi. Kwa
mfano katika riwaya hii motifu ya ndoto imejitokeza kwa kiasi kikubwa kuliko aina nyingine za
motifu. Katika uk.50 mhusika Suber anaonekana kuwa katika ndoto juu ya suala la kumpata baba
yake. Vilevile katika uk.48-50 kuna ndoto imejitokeza, ndoto ambayo inajenga dhamira ya nafasi
ya mwanamke katika jamii. Katika dhamira hii mwanamke amechorwa kama mtu
anayedharaulika.

Motifu ya maji/ bahari, hutumiwa na mwandishi ili kufikisha ujumbe juu ya mambo ambayo
huweza kuwakumba watu pindi wawapo katika safari za majini. Lakini pia mwandishi hulenga
kuisukuma kazi yake mbele katika hali nzima ya usukaji wa matukio na vitushi. Katika uk.89
mwandishi anasema;

“Boti ya injini ilikuwa imemkosakosa nchi chache. Boti yake iliyumbayumba kwa nguvu huku na
huko katika njia yake. Alichukua makasia-bapa na kupiga makasia kurudi mpaka pale
alipochukuliaboti ya kujifurahisha.”

Sifa nyingine ya msuko ni mjongeo, hii ni namna kazi fulani inavyoanza na kuisha. Kwa namna
nyingine mjongeo hulejelea kazi inaendaje kutoka mwanzo hadi mwisho, huhusisha mwanzo wa
mgagaro, kukua kwa mgogoro, kilele cha mgogoro na hatimaye mwisho wa mgogoro ambao hutoa
sululisho fulani ama zuri au baya.

Katika riwaya ya Msako kisa kinaanzia pale anapoambiwa na mama yake kuwa baba yake bado yu
hai tofauti na alivyokuwa amemwambia awali. Na huo ndio unaokuwa mwanzo wa kisa kizima
katika andiko hili. Kisa kinaanza kukuwa baada ya Suber kuamua kusafiri kuelekea Cairo kwa
lengo la kumtafuta baba yake. Kisa kinazidi kukuwa na kufikiafikia kilele chake pale ambapo
Suber amekwishaanza shughuli nzima ya msako huko Cairo, na ndipo katika harakati zake hizi
anaanza kujihusisha na mapenzi na mke wa bwana Khahili pamoja na binti-Elham. Mwisho wa
kisa hiki ni baada ya mhusika Suber kufanya mauaji dhidi ya bwana Khahili mzee aliyekuwa
mmiliki wa hoteli kubwa na maarufu pale mjini Cairo iliyojulikana kwa jina la Cairo Hotel na
tamati kabisa ya kisa hiki ni kufungwa kwa Suber gerezani/jele

Katika riwaya hii ya Msako, mianzo na miisho iliyotumika katika riwaya hii ni ile ya kujirejelea
kwa maana simulizi inaanza kwa kuturejesha katika shughuli ya mazishi ya Basima Omrani
ambaye ni mama yake Saber, mfano sura ya kwanza (uk 1);

Kwa macho yenye machozi alitazama kuelekea kwenye maiti iliyokuwa ikiondolewa kutoka kwenye
jeneza na kupelekwa kwenye kaburi liliokuwa wazi, maiti iliyoonekana kana kwamba haina chembe ya
uzito katika sanda.

Na baada ya hapo, simulizi inaanza kwa kutuonesha Saber na Basima Omrani, wakiwa
wanazungumza kuhusu msako wa kumtafuta baba yake Saber ambaye ni Sayed Sayed el Reheimy
kama invyojidhihirisha (uk 7-8);

“Nilitambua hilo siku ile waliponihukumu.” Alikaa kimya kwa mda usio wake ukiwa katika hali ya
kukata tamaa kbisa. “Saber, hii ina maana kwamba huna budi kuniacha,” alisema.

Niende wapi? Aliuliza akiwa katika hali ya hamaki iliyochanganyika na hasira.

“Kwa baba yako,” alijibu katika sauti iliyosikika kwa shida.

Alinyanyua kope za macho yake na kumaka kwa hasira “baba yngu…”


Aliitikia kwa kichwa.

“lakini amekufa. Uliniambia alikufa kabla sijazaliwa.”

“Nilikwambia hivyo. Lakini haikuwa kweli.”

Baba yangu, yu hai…Haiwezekani… Baba yangu… yu hai.”

Huo ndio mwanzo wa riwaya hii ya msako jinsi ilivyoanza katika kusimuliwa kwake.

Pia, miisho iliyotumika katika riwaya hii ni miisho ya kawaida. Kwa sababu simulizi inatuonyesha
Saber akiwa jela baada ya kufanya mauaji ya bwana Khalil kama inavyoonyeshwa sura ya kumi na
moja (uk92);

Bwana Khalil! Amka! Amka! Bwana Khalil imekaribia saa mbili kamili. Bwana Khalil! Bwana
Khalil! Aliusukuma ule mlango ili kufungua na kwa makini alitazama mle ndani. Bwana Khalil
taratibu. Halafu: “Aah, Mungu wangu bwana Khalil! Bwana! Bwana! Saidia! Saidia! Aly! Aly!
Saidia! Bwana Khalil ameuawa! Polisi! Polisi! Saidia!”

Hatimaye, baada ya Saber kumuua mzee huyo alikamatwa na kufungwa jela. Simulizi inaishia
kumuonesha Saber akiwa jela akiwa na mwanasheria.
mfano (uk134); Yule mwanasheria alitabasamu kwa kuelewa “kuna tu katika yanayofaa”

Saber alipandisha mabega juu na kushusha pumuzi.

Aah! Acha lolote nalitokee sasa.

MBINU ZA KIBUNILIZI

DAYALOJIA

Dayalojia ni mbinu ambayo mtunzi hutumia majibizano dhidi ya wahusika katika kazi ya fasihi.
Wahusika hupewa maneno na kujibizana waokwa wao. Katika riwaya hii mbinu hii imetumika
kwa kiasi kikubwa kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho kwa mfano katika uk.12 kuna
majibizano kati ya Suber na mchunguzi wa mauaji ya bwana Khahili, kuna mahojiano kama
ifuatavyo;

“Jana uliondoka saa ngapi hapa hoteleni?”

“Saa nne asubuhi”


“Uliludi saa ngapi?”

“Baada ya saa sita usiku”……n.k.

Lakinin pia katika uk.123 kuna mazungumzo kati ya Suber na Aly Seriakous kama
anavyothibitisha msanii;

“Aly seriakous. Hawajampata mwingine

“Labda alikiri kosa?”

“sijui”

“Aloishawishiwa na wizi uchwara.”

“Aliukana wizi ule.”….n.k.

Mbinu hii hutumika kwa lengo la kutomchosha msomaji/msikilizaji, lakini pia huonesha ufundi
katika uteuzi wa maneno na kuonesha asilia ya mhusika.

Taharuki, hii ni hamu au shauku ya kutaka kujua nini kitafuata baada ya tukio ama kitendo fuani
katika hali nzima ya usimulizi wa kazi husika ya kifasihi. Ndani ya riwaya hii mbinu hii pia
imejitokeza kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano simulizi yenyewe imeisha kwa kutuachia wasomaji
taharuki ya kutaka kujua hatima ya Suber itakua ipi baada kuwa amekamatwa na polisi na
kupelekwa katika sheria kuamua ama kufungwa au kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa baada ya
kugundulika kuwa amehusika na kifo cha mzee Khahil Abdul. Katika uk.146 mwandishi anasema;

“Yule mwanasheria alitabasamu kwa kuelewa. “Kuna maana tu katika yanayofaa.” Suber alipandisha
mabega mabega yake juu na kushusha pumzi. “Aah! Lolote na litokee sasa.”

Lakini pia taharuki inajitokeza baada ya Suber kuchukua jukumu la kwenda Cairo kumtafuta
baba yake baada kifo cha mama yake kwa sababu hakuwa na namna ya kuishi badala yake baba
yake ndiye atakayekuwa msaada mkubwa katika maisha yake. Hali kama hii inaacha maswali kwa
wasomaji kwa mfano wanaweza kujiuliza, je, atafanikiwa kumpata baba yake?, Atakumbana na
vikwazo vipi katika msako huu? Na maswali mengine kadha wa kadha. Kwa mfano katika uk.8
mwandishi anaonesha suala hili kwa kusema hivi;

“Lakini huenda amekwisha kufa.”

“Au pia yu hai”

“Kwa hiyo niyapoteze maisha yangu nikimtafuta mtu ambaye hata uwepo wake
sina uhakika nao?

Lakini pia katika uk.64 taharuki inajitokeza pale ambapo Suber katika utafiti wake anajawa na
tatizo la kuanza kuishiwa pesa ili hali bado hajafanikiwa kumpata baba yake na huko Cairo hana
mtu yeyote anayewaza kumsaidia kiasi cha pesa ili aweze kujikimu. Katika ukurasa huo mwandishi
anabainisha haya;
“Nini kitatokea endapo fedha zake zitamwishia wakati wowote sasa? Hana wa kumwendea. Kitu pekee
kinachomsukuma ni hofu ya kurudi kwenye maisha yake ya zamani.”

Mbinu hii hutumika kwa lengo la kumshawishi msomaji aweze kuendelea kufatilia kisa husika
katika kazi Fulani ili apate kujua hatima ni nini, vilevile mbinu hii huondoa uchovu kwa wasomaji
na kuwafanya waendelee kuisoma au kusikiliza kazi husika ya kifasihi.

UTANZIA

Utanzia ni mbinu ambayo hutumia vipengele mbalimbali vinavyozua masikitiko, huzuni, na jitimai
kutokana na vitu kama mateso, njaa, vifo, ulemavu, kufungwa jela na kadhalika. Katika riwaya hii
mwanzoni kabisa mwa ukurasa wa kwanza kuna suala la shuguli nzima ya mazishi ya mama yake
Suber (Basma Omran). Suber anaonekana kuwa na machungu sana, vilevile hata wasomaji au
wasikilizaji wa kisa hiki waweza kujawa na hudhuni. Katika ukurasa huu mwandishi anasema;

“Lakini sasa mazingira ya wakati huo yalimwamshia hisia kali za uchungu na huzuni na akatamka,
“Robo karne ya hali ya upendo, kubembelezwa, kujali, yote imepotea imemezwa na ardhi kana
kwamba haikuwahi kutokea.”

Vilevile, mbinu hii imejitokeza pale ambapo mhusika Suber anapofanya mauaji ya kikatili dhidi ya
bwana Khahil kwa kumpiga na mtarimbo kichwani kitendo kinacholeta huzuni kubwa kwa
wasomaji na hata kwa wanajaamii ile pale Cairo hususani wafanyakazi wa kwenye ile hoteli. Hili
limejitokeza katika uk.86, ambapo mwandishi anasema;
“Mwenyewe alishangazwa na nguvu ya ajabu ya pigo lile na matokeo yake ya kuchefua. Yule mzee
alipiga ukulele mdogo, halafu manung’uniko kidogo, kasha kimya.

Ufutuhi na matumizi ya ucheshi, kejeli, ubeuzi, na tanzia. Ni maneno yanayokusudia kufundisha na


kufurahisha. Mfano, Saber alipokuwa anamtafuta baba yake huko Alexandria alipokuwa maeneo
ya marmar alikaribishwa na msichana mmoja. Huyo msichana alimwambia Saber sikuweza kuja
kukupa salamu za rambirambi, lakini nilisubiri mpaka uje Le Canard. Yule msichana
alimwambia Saber kwa sauti laini, je una mikwamo ya kifedha? Yule msichana aliendelea kwa
namna ya ushawishi

“mtu kama wewe hawezi kuwa na shida ya fedha” uk 15.

Walipeana mikono pasipo kusema lolote na kuondoka zake yale maneno ya kule msichana yalimjia
akilini tena, mtu kama wewe huwezi kuwa na shida ya fedha. Hii ni kejeli au dhihaka. Pia kuna
kauli inayofurahisha na kufanya mtu afikirie kuhusu mwonekano au umbo la hicho kitu uk,19 aya
ya pili.

“Yule msichana alinyanyua kichwa chake na kuonyesha uso wake wenye mikunjo mikubwa na pua
kubwa iliyojikunja kwa mbele.

You might also like