You are on page 1of 9

KISW 335: FASIHI YA KALE YA KISWAHILI

MAJINA NAMBARI

1. MARION KORIR E13/03034/21


2. SHEILA KIPLAGAT E13/02488/21
3. ABEDNEGO PECCY A13/02369/21
4. GEORGE KIAMA A13/02368/21
5. DORIS POTISHOI A13/01582/21
6. KASALE SHANANA E13/03027/21
7. SHADRACK NG’ENO E13/03017/21
8. MONGINA AZANATH A13/01688/21
9. CYNTHIA WAVINYA A13/01466/21
10. SHARON CHEPKOECH E13/03013/21
11. MERCYLINE BOSIBORI A13/01701/21

SWALI

JADILI JINSI MASWALI YA KIDINI YALIVYOANGAZIWA KATIKA UTENZI WA AL-


INKISHAFI.
UTANGULIZI

UTENZI WA AL INKISHAFI

Maana

Wataalamu kama vile Hichens (1972:1) na Miamali (1980:8) wamekubali kwamba Inkishaf ni
neno lenye asili ya kiarabu “Kashaf” kwa maana ya

 Kufichua
 Kufunua
 Kuzindua moyo
 Kupambazukiwa na ukweli

Mtunzi ametumia pia mtindo wake kipekee kwa namna alivyozigawa beti zake ;kwa nfano ,katika
ubeti wa 1-5,mshairi anatoa maombi yake kwa Mwenyezi Mungu ;ub.7-9,anatoa dibajifidhamira
ya kazi yake;11 –ti1 ni kivuko cha kuingia kwenye beti za kutahadharisha moyo wake;anatoa
tahadhari hizo ambapo anauonya moyo dhidi ya udanganyifu wa dunia.Beti za ti4 zinasawiri
maisha ya anasa za mji wa pate;Beti za 44-46 zaeleza maanguko ya mji huo.Ubeti wa 65
umetumiwa kama kivuko kwani mtunzi anaivukisha hadhira yake toka maisha ya dunia hadi
maisha ya peponi.Beti za 66-71 zinaeleza matukio ya siku ya kiyama.Nazo beti za 72-77zinasawiri
vituko vya jehanamu .Mtunzi ametumia pia mtindo wa uzungumzi nafsia ili kutolea maudhui
yake.Twaona jinsi anavyozungumza na moyo wake mwenyewe .Ni kama kwamba anajizungumzia
mwenyewe ,lakini alilenga pia wanajamii.Kwa ufupi,huu ndio mtindo alioutumia Nasir katika
kutoa dhamira yake.
Utenzi wa Al-Inkishafi ni moja wapo ya tungo za kale maarafu sana uswahilini hasa maeneo ya
Pwani kaskazini. Utenzi huu uliandikwa na Seyyid Abdallah Bin Al bin Nassir, mshairi mtajika
aliyeishi katika kisiwa cha pate baina ya 1718-1815.Utenzi huu hueleza matukio makubwa katika
historia ya Jamii na zinazokusudiwa kuadibu, kuasa na kutoa maoni juu ya maadili ya maisha.
Maswala ya kididni ni uchambuzi wa utenzi huu kwa kufuatia maudhui ya dini.

Mwandishi anaanza kwa kumtanguliza na kumtukuza mwenyezi Mungu. Anaanza kwa kusema
“Bismillahi niakadimu” yaani, kwa jina la Allah. Naikadimu” kwa maana ya natanguliza.Kwa.
Kwa. Kwa. Kwa hivyo anaanza utungo kwa kumtanguliza Allah kama wajibu wake “Allah” ndio
jina la dhati la Mwenyezi Mungu katika dini ya kiislamu. Na mwandishi Seyyid Abdallah kuwa
Muislamu lazima angemtanguliza Mwenyezi Mungu.

Mwandishi pia anamtakia rehema mtumwa Muhammadi.Jambo hili linaandamana moja kwa moja
kumtukuza Mwenyezi Mungu. Hii inaonekana katika ubeti wa tatu mara tu baada ya kumtukuza
mwenyezi Mungu katika ubeti wa kwanza na wa pili. Mshairi anasema katika ubeti wa tatu kuwa
“Sala na salamu kiidavaji Jumaa Muhammadi tumsaliye “Seyyid Abdallah anaonyesha wazi
kwamba hana budi pamoja na waislamu wenziwe kumtakia rehema Muhammed.Yeye ndiye
mtume wa mwisho kutoka kwa mwenyezi Mungu kufikisha Uislamu kwa wanadamu wote katika
ubeti wa tano mwandishi anasema “Allahuma Rabbi mukidhi haja,msalie Tumua
aliyekuja.Mshairi anasisitiza wajibu wa kumtakia rehema Tumwa pamoja na Jamii zake na
masahaba zake wanne walioanguka.

Mwandishi pia anaomba dua na kutubu dhambi kwa Mwenyezi kutokana na makossa ambayo
pengine amifanya .Hii inaonekana katika baadhi ya ushairi huu kwa mfano:katika ubeti wa tano
mwandishi anasema Allahuma Rabii,Mukidhi haja.Yaani ,”Ewe Allah,Mola mlezi wa viumbe
wote mwenye kukidhi mahitaji ya waja.Hapo Sayyid Abdallah ananyenyekea kwa Mola wake
.Anaendelea kusema katika ubeti huu wa tano kuwa “Msalie Tumwa aliyekuja na tauhidiyo Mola
wa waja,akatusomesha tafsinye”Hapa anamwomba Mwenyezi Mungu amsalia Tumua,yaani ampe
rehema zake ajili ya ujumbe aliyompa na akautekeleza kwa kuwafundisha watu ukweli wake.

Mwandishi anaonekana kutubu makossa yake. Hii inatokana na Imani ya kiislamu kuwa kila
mwanadamu ni mkosa na hakuna asiyetenda dhambi.Syyid Abdallah anakini hili katika ubeti wa
nane ple anapotubu kwa Mola wake amfutiye dhambi zake kwa utungo anaotaka kutunga.Katika
mshororo wa nane ,mwandishi anasema “Kiza cha dhurubu kinishiye”wanadamu watakaosoma
waelimike na kuonyesha na yaliyomo.Katika ubeti wa tisa Seyyid Abdallah anasema

Kitamsi kiza cha ujuhali

Nuru na mianga tadhalati

Na ambao kwamba ataamali na ambao kwamba ataamali

Iwe toba yakuwe aitubiye

Hapa mwandishi anaomba msamaha kwa muumba wake ili apate radhi zake na asiadhibiwe na
adhab kali ya baada ya kifo.

Maudhui ya dini inaonekana pia pale ambapo mshairi anaikanya nafsi yake kjiepusha na
ulimwengu na kujiandaa kwa ajili ya kifo. Ulimwengu katika dini ya kiislamu una madanganyo
mengi ya kumpoteza mja asifanye aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Kukana ulimwengu
unaonekana wazi katika ubeti wa tatu mshororo wa kwanza na pili ambapo mwanashairi anasema

Huu ulimwengu bahati tesi

Una matumbawa na mangi masi

Hapa anatoa taswira kamili ya ubaya wa ulimwengu ,mshairi anaofananisha na bahari yenye
dhoruba kali iliyosheheni hatari tupu ikiwemo wanyama wabaya .Hii ni jazanda ya namna dunia
ilivyo mbaya kwa binadamu .Mwanadamu mwenye akili ni yule ajiepushaye na ulimwengu.Katika
ubeti wa ishirini na moja hadi ishirini na tano mshairi anaonya binadamu kuwa tukio la kifo liwe
onyo kwao.Pia anasema kwamba kuna watu wengi ambao walijihusisha na maovu ya dunia hii na
hatimiye kifo ikawafika na hatimaye wafuta maisha yao .Kujiadhari na ulimwengu ni jambo
muhimu sana kwa waislamu kwa kuwa Mungu atawahesabu kila tendo ambalo walifanya dunia
hii maovu au mema.
Swala linguine ambalo linajitokezea bayana ni sala Seyyid Abdallah anaiangazia swali hili kwa
kina. Kwa muislamu kutosali atakuwa ameenda kinyume na Imani kwa Allah kienge msingi cha
maudhui ya kiislamu katika ubeti wa sitini na tano anasema

Moyo taadabu sipeketeke

Ata ya yawi,haki ushike

Wend wachokachoka nawe waokoka

Moto wa jahimu usikutwaye

Hapa mwandishi anmweka bayana kuwa sala ndiyo itakayomwokoa mtu na moto pale anaposema
“wendo wachokachoka nawe waokoke .Mshairi isitoshe amebainisha moto wa jahimu
atakaodhibiwa nao wenye kuacha sala.Anasema “Moto wa jahimu usikutwaye” Umuhimu wa sala
katika uislamu pia imejitokeza kataka ubeti wa thelathini pale ambapo mwandashi amesisitiza
Umuhimu wa sala.Jambo linguine ambalo linajitokeza ni adhabu za siku ya mwisho.Mwandishi
ameonekana kuogopa siku hiyo.Kwa hivyo,anajipata akisimulia matukio muhimu ya siku hiyo ya
malipo kuihofisha nafsi yake na wasomaji wake kutahadhari kutoka ubeti wa sitini na sita hadi
sabini na saba .Mshahiri anasema

Yua siku yati kubadiliwa

Na mbingu sabaa zikagezwa

Ukatelezwa mwezi na jua

Ukatelezwa mwezi na jua

Hari na harara zitusitusiye (ubeti 66)

Siku ya maini ndani kuwaka

Na poa za watu kupapatoka

Mbonga malijaa nitaamiye (ubeti 67)


Mwandishi anasema kuwa siku hiyo watu ambao watakuwa wamefanya maovu wataadhibiwa
vikali na masika na mioto yenye kuvuruma kwa ukali.Anaonya binadamu watende mema ili
waepukane na adhabu hiyo .

Shetani anatojwa na mwandishi kama adui mkubwa na mwanadamu shetani anaaminika kuwepo
duniani na kuadhiri maisha ya wtu kwa kutenda maovu.Seyyid Abdallah anazungumzia shetani
anapokanya nafsi yake anasema

Kimako kuisa dibaji yangu

Penda kuonya na moyo wangu

Utitwe na hawa ya ulimwengu

Hila za rajimi ziushuvye (ubeti 10)

Ewe moyo enda sijida yake

Hela tafadhali unabihike

Kesho kakuona kuwa kumaje (ubeti 30)

Kulingana na beti hizo,mshahiri ameweka bayana azma yake katika azma yake katika utenzi
anatoka kuonya myo wake dhidi ya anasa za ulimwengu zinazotokana na shetani rajimi.

Maudhui ya dini pia inajitokeza pale ambapo mwandishi anamtaja Allah au Ar Rahim katika
mshororo wa kwanza ubeti wa tano Seyyid Abdallah anadhibitisha upekee wa Allah kwa maana
ya ewe Allah Mola mlezi “Allah “ na Rabbi ni majina matukufu ya mwenyezi Mungu usiokuwa
na mshirika wala wenye sifa yoyote ya kibinadamu au upungufu wowote .Pia Seyyid Abdallah
anamtaja mtume (Muhammed S.A.W)aliyetumwa na Allah kuwaongoza watu katika Imani ya
kumwabudu Allah pekee basi pia na kumshirikisha na chochote na kuhujumu umoja wake hii
inajitokeza katika ubeti wa tano.

Msalie tumwa aliyekuja

Na tahidiyo Mola wa waja

Akatusomesha tafsinye
Ubeti wa 49, mtunzi anatuchorea picha ya majumba ya fahari, kumbi kubwa kubwa za anasa na
starehe yamekuwa naajala.Nyumba zao wanaishi makinda ,bundi hukoroma .Viwanja na njia
yanatisha kwa magugu yaliyoumana .Anasema hata ukemi haiskiki.

Picha hizi zinatuonyesha ufupi wa maisha, udanganyifu na hada zake.Mtunzi anafaulu kuonyesha
kuwa raha ya duniani haidumu na anaomba moyo wake uzinduke kwani umeona hatima ya
waliotutangulia.

Ubeti wa 75-77, mtunzi anatuchorea picha ya hatima ya waliokumbatia hadaa na anasa za


duniani.Anasema kuwa wadhulumu watadhulumiwa nao walioishi kwa njia nyoofu watapata
dhawabu.Anatuchorea aina mbalimbali ya mioyo itakayoatiki wadhulumu na waliopenda raha
duniani,

JAZANDA

Kwa mujibu wa Mbatia (2000), jazanda ni kunga ya utunzi ambapo lugha inatumia kusawiri picha
fulani kutokana na maelezo yanayotumia maneno teule au tamadhali za usemi.

Kwa njia hii mtunzi anamwezesha msomaji kuona,kuhisi kitu kinachoelezwa .Kwa ufupi,jazanda
inahusisha hali ya kulinganisha falsafa ya kidini .Kwa kutumia taswira ,tashbiha
mbalimbali,mtunzi anaweka wazi uovu,dhiki,masumbuko na hadaa ya maisha duniani.Anauonya
moyo wake dhidi yake kwani mwisho wake ni mauti na mateso.Maanguko ya pate hivyo ni jazanda
ya maisha mafui ya binadamy

Ubeti wa 10- 11

MASWALI BALAGHA

Ni mbinu ambayo hujitokeza kwenye Fasihi, pale ambapo mtunzi huhuliza maswali kwa lengo
kumtanabaisha msomaji au msikilizaji .Haiitaji majibu .Husa kutoa hisi za ndani ya mhusika au
kuweka wazi jambo linalohitaji umakini. Kusisitiza wazo.

Ubeti wa 11-12

Mtunzi anauliza maswali moyo wake ambao umenaswa na tamaa, shetani na udanganyifu wa
ulimwengu. Anauliza moyo wake kwa nini hutabiri yanyokuja baada ya kutekwa na anasa na
kufuatia njia za uovu.
Matumizi ya lugha

Wamitila (2009) amesema matumizi ya lugha katika utenzi ni wa kipekee.Yakilinganishwa na


bahari nyingine .Anauhuru mkubwa wa matumizi ya lugha ,uteuzi wa m,samiati ,ubunifu
wake,kubuni msamiati wa ke kuyaendeleza maneno kwa njia tofauti .Utenzi una kawaida ya
kutumia maneno ya kale.

Tashbiha –ni tamadhali ya usemi ambayo hulinganisha vitu mbili ambayo haziusiani kwa
kutumia viunganishi linganishi.

Ubeti wa (14)” Kama kisima kisicho ombe “ – analinganisha maisha na kisima kifupi ila hapo mna
mwana wa ng’ombe ashambuliaya kwa kichwkwa kichwa .Hii inaonyesha hatari na udanganyifu
wa nmaisha .

Istiari-Ulinganishi usiotumia viunganishi linganishi.

Ubeti wa (15) analinganisha vumbi la muangaza wakati wa jua na ukijaribu kusogelea hutapata
kitu. Maisha ni udanganyifu tu.

Tashihisi –Kukipa sifa za uhai kitu kisicho na uhai.

Beti 10 -14 mtunzi anazungumza na moyo wake

Taswira –Hii ni picha ya kitu au dhana Fulani, katika ubongo wa msomaji au msikilizaji ,kwa
kutumia maneno.Picha ya maneno ikichorwa vizuri ,mtu anaweza kuhisi,kuona ,kugusa ,kuonja
na ata kusiskia .Utenzi wa inkishafi ni taswira ya maanguko ya pate.Tunachorewa picha ya
umaarufu na ufahari wake .Matajiri na sehemu zao.

Ubeti wa 7,mtunzi anadhamiria kutunga ;

Koja kulidawiri,

Mavazi ya duri ikanawiri


Mikanda ya nyuma nitije

Hivi ni picha ya vitu vya dhamani.Mtunzi anamshawishi msomaji kuwa utungo huu ni wa
thamani na atafaidika nayo.

HITIMISHO

Utenzi wa Al Inkishafi ni mojawapo ya kazi ya Fasihi simulizi.Katika lugha ya Kiswahili


uliandikwa na Shaban Robert mshairi maarufu wa kitanzania.Utenzi huu unahusu maisha ya
kiajana aliyeitwa Muhammed ambaye alipitia changamoto nyingi katika maisha yake.Al Inkishafi
ni moja wapo ya kazi ya Fasihi ambazo zinaonyesha ustadi wa lugha na ujuzi wa kina wa tamaduni
za kiafrika .Utenzi huu umekuwa na adhari kubwa katika Fasihi ya Kiswahili na umekuwa
ukifundisha katika shule na vyuo mbali mbali kama kielelezo cha ubunifu na upekee.

You might also like