You are on page 1of 25

34

MAFUNDISHO YA UMISHENI
I

KUHUBIRI NA KUFUNDISHA
Muhtasari: Elekeza kwa mada ilioko hapa chini nayo itakuelekeza kwa mada hiyo.

I. Lengo la Kiuzi Hiki


II. Ufafanuzi wa Biblia

A. Ufasili
B. Tafsiri ya Maandiko
C. Maana ya Maandiko
D. Kutumia Maandiko

III. Vifaa
IV. Kuhubiri
A. Utangulizi
B. Kuchagua Mahubiri
C. Mahubiri ya Ufasiri
1. Kuchagua Maandiko
2. Kukuza Muhtasari na Maandiko
3. Mazoezi ya Kuwasilisha
4. Kuwasilisha na Maoni
D. Mahubiri ya Mada
E. Uchunguzi wa Mhusika
V. Kufundisha
A. Utangulizi
B. Somo
1. Ufasiri
a. Kiini
b. Kifungu kwa kifungu
2. Mada
3. Kuchunguza Mhusika
VI. Habari Zaidi
VII. Kazi ya Ziada
A. Hubiri Mahubiri Mawili
B. Ongoza Madarasa Mawili

Haki za Kunakili © 2009 Shirika la Mafunzo ya Umisheni. Haki Zimehifadhiwa.


KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

I. Lengo la Kiuzi Hiki

Baada ya kusoma kiunzi hiki cha mafundisho, unafaa:

• Uwe na uwezo wa kufafanua istilahi za kimsingi zinazohusiana na kiuzi hiki.


• Uwe na uwezo wa kuchagua tafsiri ya Biblia isiyo na hitilafu
• Kujua kanuni za kufafanua Biblia
• Kujua vifaa vya kujifunza Biblia
• Kuelewa kanuni za kutoa mahubiri
• Uweze kuchagua mada ya mahubiri
• Uweze kuchagua aina ya mahubiri
• Uweze kupata Maandiko yanayoambatana na mahubiri
• Kujua kukuza muhtasari wa mahubiri
• Kukariri chemshabongo zinazotumiwa katika matumizi ya mahubiri
• Kuweza kutenda kulingana na mahubiri
• Kuelewa baadhi ya njia za kukuwezesha kutoa mahubiri kwa njia inayofaa.
• Kujua hatua zinazohusika katika kutayarisha aina tofauti za mahubiri
• Uweze kuelewa kanuni za kufunza Biblia
• Kuwa umechunguza baadhi ya wavuti zilizo na manufaa katika kuhubiri na
kufunza.

RUDI KWA MUHTASARI ¾ ¾


KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

II. Ufafanuzi wa Biblia

Lengo la kiuzi hiki ni kutoa muhtasari wa jinsi ya kujifunza Biblia, kuhubiri


Biblia, na kufunza Biblia. Mafunzo zaidi yaweza kupatikana katika wavuti na
umeorodheshwa hapo chini kwa mada ya “kwa habari zaidi.”

Kabla ya kuhubiri na kufundisha, tunahitaji kuamua yale Maandiko


yanamaanisha na jinsi tunavyoweza kutumia Maandiko katika maisha yetu. Na
tuchunguze jinsi ya kutafsiri Maandiko.

A. Ufasili

Kamusi ya Merriam-Webster inatupa mwongozo wa matamshi yaliyoandikwa


na yakusikiza ili kutusaidia kutamka maneno kwa lugha ya Kiingereza.

http://www.m-w.com/

Katika theolojia, hermeneutics ni sayansi ya kufafanua Maandiko. Fasili ya


Maandiko (Exegesis) ni utumizi wa kanuni za kufafanua Maandiko. Ufasiri
(Exposition) ni jinsi ya kueleza watu Maandiko. Kwa hivyo mhubiri hutumia
kanuni za hermeneutics kufafanua Maandiko ili kueneza mahubiri
yanayoeleweka. Tunataka kuepuka isogesis—kujaribu kuweka mawazo yetu
kwa Maandiko, au kujaribu kubadilisha Maana iliyo katika Maandiko. Fasili ya
maandiko (Exegesis) ni “kusoma kutoka “ kwa Maandiko, na isogesis ni
“kusoma ndani ya” Maandiko.

Pericope ni kifungu cha Maandiko kilicho na wazo kamili. Wakati mwingine


ukurasa katika Biblia waweza kuwa pericope. Wakati mwingine sehemu ya
ukurasa au zaidi ya ukurasa mmoja waweza kuunda pericope. Ili tuweze
kueleza Maandiko kinaganaga, tunahitaji kutambua mahali pericope inaanzia
na mahali inaishia.

B. Tafsiri ya Maandiko

Maandiko ya Biblia ya asili yalikuwa yameandika kwa Kiebrania, Kigriki na


Aramaic. Maandiko yametafsiriwa katika lugha nyingi na kutengenezwa upya
jinsi lugha zinavyoendelea kugeuka. Ni vyema uweze kuchagua tafsiri isiyo
na hitilafu ambayo yaweza kueleweka na watu unaofundisha. Ni lazima
tafsiri hiyo iwe imekubalika na makanisa yaliyo na mwelekeo tawala,
ikilinganishwa na tafsiri iliyoandikwa na madhehebu ya uasi. Huwa natumia
tafsiri ya Union. Habari Njema pia ni tafsiri njema. Kwa Kiingereza huwa
natumia New International Version (NIV). Tafsiri nyingine nzuri ni New
American Standard, ambayo hutafsiri neno kwa neno. Tafsiri ya King James
ni nzuri, ila hutumia lugha ambayo imepitwa na wakati, na kuifanya kuwa gumu
kueleweka. Ni vyema kuchagua kifungu kimoja kama chanzo cha msingi
badala ya kubadilisha kutoka kifungu kimoja hadi kingine. Kuwa na chanzo
kimoja cha msingi hutuwezesha kukariri Maandiko kwa urahisi.

Ungependa kutumia vifaa vya ziada katika masomo yako kwa kutumia tafsiri
iliyofafanuliwa- ambayo haifuati utaratibu katika kutafsiri Maandiko ili
kuyafanya kuwa rahisi kuelewa. Tafsiri iliyofafanuliwa hutaka kuwa “sawa
kabisa” na maandiko ya asili. Kwa sababu Biblia zilizofafanuliwa hazijatafsiriwa
neno kwa neno kutoka kwa Maandiko ya asili, sitayatumia kama Maandiko ya
msingi. Biblia ya Habari Njema ni tafsiri iliyofafanuliwa. Kama Kiswahili chako
siyo sanifu, waweza kutumia Biblia iliyoandikwa kwa lugha ya kimsingi.
Biblia inajumuisha Agano la Kale na Agano Jipya, na imeandikwa kwa kutumia
misamiati ya kimsingi ya maneno 1,000 pekee.1

Hapo chini kuna mtandao unaoeleza Biblia zilizoandikwa kwa lugha ya


Kiingereza, na zimepangwa kulingana na uhalisi wake. Baadhi ya Biblia ni
tafsiri ya neno kwa neno na zingine zimefafanuliwa. Tazama chati ya
“Tafsiri za Biblia” iliyoko mwisho wa ukurasa wa wavuti huu.

http://preceptaustin.org/inductive_bible_study.htm

C. Maana ya Maandiko

Tafsiri njema ya Biblia hutueleza yale Maandiko yanayosema. Lakini Maandiko


yalimaanisha nini nyakati za Biblia? Tumetenganishwa na waandishi wa Biblia
na nyakati, Jiografia, na tamaduni. Kifungu nyakati za Biblia chaweza kuwa
kilikuwa na maana tofauti na kifungu hicho hicho wakati huu. Kwa hivyo ni
lazima tutumie kanuni za kufafanua Maandiko (hermeneutical principles) ili
kuamua yale mwandishi wa Biblia alitaka tujue. Zifuatazo ni baadhi ya kanuni
zinazotumika kufafanua Maandiko.

1. Biblia ina Mamlaka. Tunaamini kuwa vitabu 66 vya Agano la Kale na


Agano Jipya ni Neno la Mungu lililo na Mamlaka. Mungu alitia msukumo
ndani ya waandishi wa Biblia ili kupasha ukweli.

16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa


kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa
kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili,
amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. (2 Timotheo 3:16,17)

2. Ni lazima Maandiko yaangaliwe katika muktadha. Tunapojifunza


kifungu au pericope, chunguza pia fungu la maneno na kitabu ambacho
kifungu hicho kilitolewa. Kiini cha kitabu ni gani? Kwa nini mwandishi
aliandika kitabu hicho? Ni nani aliandika Kitabu na alikuwa anaandikia
nani? Kitabu hicho kiliandikwa lini na wapi? Chunguza historia , tamaduni,
jiografia na hali ya muktadha.

3. Amua namna (aina ya fasihi). Kitabu au vifungu vya Maandiko ni cha


nyimbo, mashairi, unabii, historia, nyaraka, Injili au Sheria? Lugha huwa
na maana tofauti kwa aina tofauti.

4. Chukulia maana hasa ya maneno isipokuwa kama kuna sababu ya


kuchukulia vingine. Kwa jumla Biblia humaanisha yale inayosema-
hasa. Aina na muktadha yaweza kuonyesha kuwa maneno mengine ni ya
kitamathali. Biblia inajumuisha sitiari, tashbihi, mithali, istiari na mbalagha.
Kwa mfano lugha ya kitamathali imetumika kwa wingi kwenye fasihi ya
kutabili mambo ya maafa makubwa yaliyoko katika kitabu cha Ufunuo.

5. Amua maana ya maneno. Mara nyingi ufafanuzi wa Maandiko unahusu


kujifunza neno ili kuamua neno hilo lilikuwa na maana gani wakati
lilipoandikwa.

6. Fuata kanuni za sarufi. Wanafunzi wa Biblia wanahitaji kuelewa utumizi


wa kitenzi, nomino, kivumishi, kielezi, shamilisho halisi na sehemu
zinginezo za usemi.

7. Ruhusu Maandiko yafafanue Maandiko. Vifungu vya Biblia


vinavyoeleweka hueleza vifungu vya Maandiko visivyo eleweka vizuri.
Fikiria maelezo sambamba, kama yale yalioko katika vidokezo vya Injili
(Mathayo, Marko na Luka). Tumia marejeo, kama yale yalioko katika
Biblia za Marejeo, ili uweze kupata vifungu vilivyo na mada
zinazoambatana. Pia Biblia ya upatano na Biblia za Mada husaidia
kupata vifungu vinavyoambatana.

8. Kitu kinapotajwa kwa mara ya kwanza chaweza kueleza maana yake


mahali pengine popote kitakapotajwa. Jambo likitokea au neno
linapotumika kwa mara ya kwanza maana yake huwa inaelezwa. Kwa
hivyo angalia kwenye Biblia ya mapatano ili uweze kupata mara ya
kwanza ya jambo hili kutokea au kwa neno kutumika.

9. Biblia ni ufunuo unaoendelea. Waandishi wa kwanza wa Biblia


hawakuwa na habari nyingi kama vile waandishi wa Biblia waliofuata. Kwa
mfano, mafumbo tofauti yalifunuliwa wakati Kristo alikuja kwa mara ya
kwanza. Manabii wa Agano la Kale hawakupewa habari kuhusu kanisa.
Manabii wa Agano la Kale hawakuelewa kwamba Masiha angekuja
duniani mara mbili. Hata kama ufunuo unaendelea, habari zilizotolewa
katika Agano la Kale ni muhimu.
10. Tumia vifaa kando na Biblia. Biblia ni maandishi ya msingi ya kujua
mapenzi ya Mungu. Lakini vifaa vingine ni muhimu ili uweze kuelewa
Biblia na tamaduni za Biblia. Baadhi ya vifaa hivyo vimeorodheshwa
katika sehemu ilioko hapo chini.

D. Kutumia Maandiko

Ili uweze kujifunza Maandiko vyema, ni lazima tutumia mafunzo yake. Ni lazima
tuongozwe na Maandiko. Kenson Kuba anatoa chemshabongo inayotumika
kwa wingi kusaidia kutumia Maandiko.

DAMAMK

Dhambi – Kunazo dhambi ninazohitaji kukiri?


Ahadi – Kuna ahadi ninazohitaji kudai?
Matendo/Mtazamo - Kuna mtazamo au matendo nahitaji kutwaa au kuepuka
Amri – Kuna amri ninazohitaji kutii?
Mifano – Kuna mifano ninayoweza kufuata?

Kweli – Kunazo kweli za kuamini? 2

1
1. Kwa habari zaidi kuhusu Biblia katika lugha ya kimsingi, andika kwa
Cambridge University Press, New York, New York, USA.

2
Kenson Kuba, "Vitabu vya Bure vya masomo ya Uanafunzi ", Masomo ya
Uanafunzi kitabu cha 3, ukurasa 21 katika mtandao.

http://biblestudycd.com/books/book3.pdf

RUDI KWA MUHTASARI ¾ ¾


KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

III. Vifaa

Vifaa vya mtandao vya kutafsiri Biblia vya bure vyaweza kupatikana katika wavuti
ufuatao.

http://www.preceptaustin.org/

Vifaa hivyo vya mtandao katika wavuti ulioko hapo juu vinajumuisha vifaa
vifuatavyo:

1. Elekeza kwa mada “Kamusi ya Biblia” Ili uweze kutafuta misamiati ya


Biblia, ensaiklopidia na kamusi ya maneno ya Kiebrania na Kigriki.

2. Elekeza kwa mada “Ramani za Biblia” ili ufikie ramani za mahali


panapotajwa katika Biblia.

3. Elekeza kwa mada “Ni Giriki Kwangu ” kwa vifaa vitakavyokusaidia


kujifunza maneno.

4. Elekeza kwa mada “Tangazo Mfululizo wa Biblia (Bible Commentary)” ili


ufikie tangazo zingine nyingi.

Wavuti uliko hapa chini unakuruhusu kupata mada ya Biblia, neno au kifungu
cha kumbukumbu katika tafsiri tofauti na katika lugha tofauti. Kwa hivyo
inatumika kama Biblia ya mada, Upatano, na hutafuta vifungu vya Biblia
kulingana na ukurasa na nambari ya kifungu.

http://www.biblegateway.com/

Nyingi ya vifaa vilivyoko katika mtandao vinapatikana kwa mfumo wa kitabu.


Kwa orodha ya vitabu vilivyopendekezwa, tazama “Vitabu vya Bure vya
Mafunzo ya Uanafunzi,” Mafunzo ya Uanafunzi kitabu cha 3 katika wavuti
ufuatao.
http://biblestudycd.com/

Wavuti ulioko hapa chini ni Kamusi ya Theolojia. Inakuwezesha kuelewa istilahi


za kitheolojia, na kueleza imani ya kimsingi ya kanisa.

http://www.carm.org/dictionary.htm

Vifaa vya kujifunza Biblia (baadhi yake zinapatikana bila malipo) vyaweza
kupatikana katika:
http://bible.crosswalk.com
Mojawapo ya vifaa vya kujifunza Biblia vinavyopatikana katika wavuti uliko hapo juu
ni Biblia ya msambamba (katika lugha saba, ambayo inasaidia sana wakati
unatumia Biblia ya kujifunza lugha nyingine).

Wavuti ufuatao unatoa habari kuhusu alfabeti za Kiebrania, lugha na tamaduni.

http://www.hebrew4christians.com/

RUDI KWA MUHTASARI ¾ ¾


KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

IV. Kuhubiri

A. Utangulizi

Homiletics ni ustadi wa kuhubiri. Homily ni mahubiri. Kazi ya wahubiri ni


kueneza Injili – Habari Njema ya Yesu Kristo. Wale ambao hueneza habari
isiyo katika Biblia, huwa hawahubiri Injili. Wale ambao hutoa mahubiri ambayo
hugeuza Biblia huwa hawahubiri Injili. Wahubiri waaminifu hufuata Roho
Mtakatifu wanapoeneza ukweli wa Maandiko.

Mara nyingi wachungaji ndio hutoa mahubiri. Kama wewe ni mchungaji,


wewe ni mchungaji wa kondoo – washiriki wa kanisa la mtaa. Huwa
unawasilisha sio tu maneno ya mahubiri; huwa unawasilisha wewe ni mtu
wa aina gani. Una uhusiano wa kipekee na washiriki walioko katika kanisa la
mtaa. Wewe pamoja na washiriki ni mwili wa Kristo. Lakini washiriki
hukutazamia kwa uongozi na faraja – maneno yaliyo na ufunuo wa Mungu.
Hukutazama kama mfano wa kufuata. Mwishowe Kristo ndiye mfano wa
kufuata. Lakini kondoo hufuata mchungaji, nao washiriki hufuata mchungaji.
Washiriki wanataka kujua ni mambo gani unayoyajua, lakini zaidi ya yote
wanataka kujua kama unawajali. Wanataka kujua kwamba unawajali. Baada ya
yote, amri zile kuu mbili zinahusu upendo – upendo kwa Mungu na kwa
wengine. Mahubiri mengi hufanyika katika mazingira ya upendo unaoendelea
kati ya mhubiri na wasikilizaji.

Wahubiri hunena nyakati fulani katika histora, kwa watu fulani, katika mahali
fulani. Ukweli wa Maandiko haubadiliki, lakini lugha ambayo inatumiwa
kuwasilisha ukweli hubadilika na wakati, na kutoka kwa tamaduni moja hadi
nyingine. Kwa hivyo ni lazima muhubiri anene kwa lugha ya moyo wa
wasikilizaji. Lugha ya moyo kwa mtu mmoja ni lugha ya kujichagulia kwa
mwingine – lugha ambayo hutumika nyumbani.

Unapohubiri, ni lazima uhubiri kutoka kwa roho kwa nguvu za Roho


Mtakatifu. Wasikilizaji wanataka kujua kwamba unaamini yale unayohubiri.

Unapohubiri, inasaidia ukielekeza maneno yako kwa mtu binafsi, si kwa


washiriki wote. Hiyo ni kusema, hubiri kama unazungumza na mtu binafsi.
Tazama watu, si kwa ukuta au sakafu. Mahubiri yasichague mtu binafsi, lakini
mhubiri awasiliane na mtu binafsi. Maneno ya mahubiri hayaelekezwi kwa
mtu mmoja tu. Badala yake maneno ya mahubiri huelekezwa kwa washiriki.
Mhubiri hunena kama ananena na mtu mmoja, nao washiriki wengine
wanasikiza. Kwa kweli mhubiri atanena kwa sauti kuliko vile anavyoongea na
mtu mmoja. Mhubiri aweza kubadili sauti kuliko jinsi anavyobadili akiongea na
mtu mmoja. Lakini, bado huhubiri akitazama mtu mmoja, baadaye mwingine,
baadaye mtu wa tatu n.k.
Unapotayarisha mahubiri, ni vyema uweze kujadili mahubiri
yanayopendekezwa na watu wengine ambao wana ufahamu wa Maandiko
kabla ya kuhubiria washiriki. Wakristo wengine huwa na utambuzi na
wanaweza kukuonyesha makosa kabla ya kuhubiria washiriki. Wachungaji
waweza kukutanika kwa ushirika na kutayarisha mahubiri. Mhubiri aweza
kujifunza kutoka kwa wachungaji wengine, lakini mhubiri asinakili mahubiri ya
wengine.

30 "Basi kwa sababu hiyo, Mimi ni juu ya manabii hao, asema BWANA,
wanaompokonya kila mtu jirani yake maneno yangu. 31 Tazama," mimi
ni juu ya manabii, asema BWANA, wanaotumia ndimi zao na kusema,
Yeye asema,' 32 Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri ndoto za uongo,
asema BWANA, na kuzisema, na kuwakosesha watu wangu kwa uongo
wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini mimi sikuwatuma, wala
sikuwapa amri; wala hawatawafaidi watu hawa hata kidogo, asema
BWANA. (Yeremia 23:30-32)

Kama Mungu amekuita kuhubiri, atakupa maneno ya kunena. Vile


unavyozungumza itakuwa tofauti kutoka kwa wengine kwa sababu wewe ni wa
kipekee. Mungu alinena kupitia kwa manabii wa Biblia na kila mmoja wao
alikuwa na mtindo wake wa kunena na kuandika. Siku hizi, Mungu hunena
kupitia kwa wahubiri, na kila mhubiri ana mtindo wa kipekee.

Katika kuhubiri, na katika maisha ya Kikristo kwa jumla, ni lazima tuwe


wanyenyekevu. Tunapoulizwa maswali ya kitheolojia ambayo hatuna majibu
yake, hatuogopi kusema “Mimi sijui.” Tunapokosea katika mahubiri, tuseme
tumekosea. Njia bora ya kuongea kuhusiana na maswali magumu ya kitheolojia
ni, “Mimi naelewa hivi . . .” Na ni jambo la busara kutohubiri juu ya mambo
ambayo hatuna ufahamu wa kutosha juu yake.

B. Kuchagua Mahubiri

Ni lazima wahubiri waelekezwe na Roho Mtakatifu wanapochagua mahubiri.


Mungu anaweza kuweka dhana kwenye akili ya mhubiri ambayo inaongoza
mhubiri kuhubiri juu ya mada fulani. Unapofuata Roho Mtakatifu kuamua
mahubiri, weka maanani mahitaji ya washiriki. Washiriki wanahitaji faraja,
onyo, au uongozi katika jambo la kitheolojia? Fikiria juu ya mambo
yanayokuhusu, furaha, au utambuzi wa kipekee. Mungu ameweka nini ndani ya
roho yako? Omba ili Mungu akupe maneno ya kunena.

Unapochagua mahubiri au mfululizo wa mahubiri, chagua aina ya mahubiri:


ya ufasiri, mahubiri ya mada, uchunguzi wa mhusika. Katika mahubiri ya
ufasiri, mhubiri hueleza ukweli uliko katika vifungu vya Biblia. Katika mahubiri
ya mada, mhubiri huchagua mada baadaye hueleza ukweli ulioko katika Biblia
nzima unaohusiana na mada hiyo. Katika mahubiri ya uchunguzi wa
mhusika, mhubiri huchagua mhusika mmoja kutoka kwa Biblia baadaye
anaeleza kuhusu mhusika huyo.

C. Mahubiri ya Ufafanuzi

Mahubiri ya Ufafanuzi yana manufaa unapowasilisha ukweli wa maandiko


kwa kina kuliko mahubiri ya mada au mafunzo kuhusu mhusika. Mnenaji
anapoendelea kuhubiri kutoka kwa Biblia nzima, kweli nyingi huelezwa, sio tu
kweli zilizoko kwenye mada zilizoteuliwa.

1. Kuchagua Maandiko

Unapoendelea kusoma Maandiko wakati wa masomo yako ya Biblia,


kuna vifungu fulani ambazo zinaathiri fikra zako. Waweza kujisikia
kuwa kuna hitaji la kueleza wengine vifungu hivyo. Hii ni njia moja ya
kuchagua Maandiko.

Njia nyingine ya kuchagua Maandiko ni kukariri vifungu vya Biblia,


na kusoma Maandiko kila siku; kisha ruhusu Mungu alete Maandiko
katika akili yako. Kisha kama vile Roho Mtakatifu anavyokuongoza
unene juu ya mada fulani, atakukumbusha Maandiko yanayoambatana
na suala hilo. Ikiwa hautakumbuka kumbukumbu ya Maandiko, lakini
unaweza kukumbuka maneno machache ya kifungu, waweza kutafuta
kifungu hicho kutoka kwa mtandao. Au waweza kutazama kwa kitabu
chenye maneno muhimu ya Biblia au Biblia ya mada.

Njia ya tatu ya kuchagua vifungu vya Biblia ni kwa kutumia Biblia ya


mada au kitabu cha maneno muhimu ya Biblia (concordance)
kuangalia fungu la maneno yanayolingana na wazo fulani. Kitabu
kubwa chenye maneno muhimu ya Biblia kilichofupishwa na fahirisi
za mada zaweza kupatikana nyuma ya Biblia ya mafundisho. Au
waweza kutembelea mtandao kutafuta Kitabu pana chenye maneno
muhimu ya Biblia na fahirisi za mada.

http://www.biblegateway.com/

Kitabu chenye maneno muhimu ya Biblia na fahirisi za mada yaweza


kukuongoza kwa vifungu vya Biblia. Kisha chagua vifungu jitwalia ambazo
utatumia kutoa mahubiri.

Mara tu unapochagua maandiko, unatakiwa kuamua mwanzo na mwisho


wa kifungu au pericope. Kama neno la mwanzo wa kifungu ni neno kama
vile “kwa hivyo”, kifungu hicho ni hitimisho la andiko lililotangulia. Kwa
hivyo utahitaji kutambulisha kifungu kwa washiriki kwa kutoa muhtasari
mfupi wa andiko lililotangulia.
Hata kama unahubiri kuhusu kifungu fulani, wakati mwingine utahitaji
kuleta Maandiko ya ziada kwenye mahubiri. Wakati mwingine utahubiri
kwa zaidi ya kifungu kimoja. Lakini utataka kulenga mada moja –
wazo moja – kwenye mahubiri.

2. Kukuza Muhtasari na Maandiko

Wakati mwingine waweza kupata kuwa una muda mfupi kuliko unaohitaji
wa kutayarisha mahubiri. Ni vyema kuweka kando muda wa kutosha wa
kujifunza na kutafakari Maandiko. Watu hutoa wakati wao kuja kusikiza
mahubiri. Wakati wa mahubiri ni wakati ambao unao usikivu wa kundi la
watu au umati wa watu. Maneno yako wakati huo ni ya muhimu sana.
Hata kama unataka kufanya utafiti wa mahubiri yako, wakati mwingine,
hauna muda. Pengine ulitakiwa kufanya ibada ya wafu au uwe pamoja na
mshiriki mahututi. Ni vyema ukiweza kutayarisha mahubiri kadhaa
kabla, na kuyaweka kwa ajili ya wakati maalum ambao hautakuwa na
nafasi ya kutayarisha mahubiri. Kuna wakati ambao ni lazima utoe
mahubiri bila kupata nafasi ya kujiandaa. Njia moja ya haraka ya kukuza
mahubiri ya ufasiri ni kama ifuatayo:

a. Omba uongozi wa Roho Mtakatifu.

b. Fikiria washiriki na fursa. Uliza, “Ni nini kitahubiriwa wakati kama


huu?”

c. Kama hauna nafasi ya kutosha ya kujitayarisha, chagua kifungu


kinachofaa ambacho unaelewa vyema.

d. Tambua muktadha. Kifungu hiki kinatoka katika kitabu gani? Nani


aliyeandika Kitabu hicho? Kiini na kusudi la Kitabu ni nini? Kitabu
hicho kiliandikwa lini? Kitabu hicho kiliandikiwa nani? Kitabu hicho
kiliandikiwa wapi? Paulo, kwa mfano aliandika Nyaraka za Wafilipi
akiwa gerezani. Kujua hayo kunatia nguvu maneno yake. “Furahini
katika Bwana sikuzote. . .” (Wafilipi 4:4). Kama vile mwandishi wa
habari, jiulize maswahili kuhusu kifungu” Nani? Nini? Lini? Wapi?
Kwa nini? Jinsi gani?

e. Kama una muda na vifaa, somo kifungu katika zaidi ya tafsiri moja ya
Biblia. Weka maanani tofauti zilizoko kwenye tafsiri tofauti.

f. Kuza muhtasari wa mahubiri. Muhtasari utafanana na fahirisi ilioko


mwanzo wa kiuzi hiki. Tambua wazo muhimu la kifungu. Kwa jumla,
mahubiri katika tamaduni za magharibi huwa na wazo tatu, lakini
mahubiri yaweza kuwa na chini au zaidi ya hizo, kulingana na dhana
zinazopatikana kwenye kifungu. Mahubiri kwenye tamaduni za
magharibi kwa kawaidia huchukua muda wa dakika 15 hadi 30.

Tambua vifungu ambavyo vinahusiana na kila wazo kuu. Unapotoa


mahubiri, waweza taka kusoma sehemu ya vifungu au vifungu vyote.
Kama kifungu ni kifupi, waweza kusoma kabla ya mahubiri. Au
unaweza kusoma vifungu vifaavyo kila unapotaja wazo kuu ya
mahubiri.

g. Amua kiini cha kifungu. Kiandike chini. Utataka kuweka mkazo kwa
kiini hiki. Unapotoa mahubiri, utataka kurudia kiini, labda ukitumia
maneno sawa kwa ajili ya kusisitiza, au labda kwa kutaja kiini tena
kwa maneno tofuati.

h. Tambua wazo la kushawishi chini ya kila wazo kuu.

i. Ikiwa una swali kuhusu maana ya Maandiko, tazama vifaa tofauti


(kama vile kitabu cha maoni) kilichoorodheshwa hapo juu.

j. Fikiria juu ya kielezo kwa kila wazo. Kwa kawaida kielezo kimoja kwa
kila wazo kinatosha. Vielezo hufanya msikilizaji afurahie mahubiri.
Vielezo viwe vitu ambavyo washiriki wanaelewa. Vielezo ni daraja
kutoka kwa Maandiko ya Biblia hadi kwa maisha ya wasikilizaji. Kwa
hivyo jiweke katika nafasi ya wasikilizaji, na uchague vielezo
ambavyo wataelewa.

Kama itawezekana, lugha inayotumika katika mahubiri iwe mifano


thabiti, sio lugha ya dhahania. Watu huelewa na hukumbuka mifano
thabiti. Neno “upendo” ni dhahania. Kueleza mama akimpa busu
mwanawe ni picha thabiti ya upendo. Kwa hivyo vutia hisia za asili
za watu. Unapowasilisha wazo, jiulize, “Hii inakaa aje?” “Inaoja
kama nini?” “Inasikikaje ikiguswa?” “Sauti yake iko aje?” “Inanusia
aje?”

k. Kuza utangulizi wa mahubiri. Kwa kawaida huwana wakati wa


kufikiria kuhusu kiegemeo namuktadha wa kifungu. Kumbuka
kwamba washiriki hawajakuwa na wakati kama huo. Kwa hivyo
unahitaji kutoa utambulisho ili kuwatayarisha kusikiza ujumbe.

l. Mwanzo kabisa wa mahubiri, ni lazima ueleze unahubiri kuhusu nini.


Ni lazima washiriki wajue kiini. Ni jambo la kuvunja moyo kusikiza
kwa zaidi ya dakika chache bila kuelewa jambo ambalo mhubiri
anazungumzia. Kwa hivyo mwanzo wa mahubiri, tambulisha kiini
chako.

m. Haya ni mahubiri ya ufasiri, kwa hivyo mahubiri yako yaweza


kupangwa katika mojawapo ya njia hizi mbili.
• Utangulizi
• Ufasiri
• Kutumia
• Hitimisho
• Utangulizi
• Ufasiri: Wazo la 1
• Kutumia: Wazo la 1
• Ufasiri: Wazo 2
• Kutumia: Wazo 2
• Ufasiri: Wazo 3
• Kutumia: Wazo 3
• Hitimisho

n. Unapopanga mahubiri, uliza maswali wakati wote, “Kwa hivyo nini?”


“Kutakuwa na mabadiliko gani nikitoa mahubiri haya?” Andika jibu
lako. Kama hakutakuwa na mabadiliko yo yote ukihubiri mahubiri
yako, basi unapoteza wakati wako. Utahitaji kurekebisha mahubiri
yako au uchague kifungu kingine.

o. Buni mahubiri ambayo yataelekeza msikilizaji kufanya uamuzi.


Unataka wasikilizaji wafanye nini au wafikirie nini kutokana na
ujumbe,? Ikiwa kusudi la mahubiri ni kufanya uinjilisti, basi wasikilisaji
wanatakiwa kuombwa wampokee Kristo kama Bwana na Mwokozi.
Kama mahubiri yamekusudiwa kuwatia moyo kutoa kwa ajili ya
maskini, basi msikilizaji aulizwe atoe.

p. Kuwa na ushawishi. Sihi nia ya wasikilizaji. Kiwango cha mahitaji


huwapa motisha watu: wanataka chakula, mavazi na makao, na
mahitaji haya ya kimsingi yakitimizwa, basi watataka mali au umaizi
au mamlaka, au heshima ya kibinafsi2. Elewa ni kitu gani huwapa
motisha washiriki fulani. Motisha zingine ni nzuri na zingine ni baya.
Biblia hufundisha kuwa tusikimbilie mali na mamlaka , lakini tutafute
ufalme wa Mungu, na mahitaji yetu yatatimizwa. Kwa hivyo twaweza
kusihi motisha za watu, au kuwashawishi wabadili nia zao.

q. Kuza jinsi ya kutumia mahubiri yako kwa ukamilifu. Tazama


chemsabongo DAMAMK hapo juu katika Kutumia Maandiko.
Kwanza kabisa mhubiri hufunza watu Maandiko wakati wa
ufasiri, na mhubiri huhubiri wakati wa kutumia Maandiko. Ikiwa
wewe ni mhubiri, usisahau kuwa mkamilifu kwa kutumia Maandiko.
r. Hifadhi vidokezo vya mahubiri. Labda utahitaji kuvitumia tena wakati
na mahali pengine. Labda utahitaji kuhubiri juu ya kiini kama hiki
kwa washiriki hawa. Kuna mtu alisema kuwa mhubiri ni lazima
ahubiri wazo mara saba ili washiriki waweza kuikubali na kuitumia.
Bila shaka, ni kweli kuwa sio kila mmoja kwenye ushirika
atakumbuka na kutumia kila kitu mhubiri atakachosema kwa mara
ya kwanza.

s. Hubiri kwa njia mabayo ni rahisi kukumbuka. Panga fikira zako, ili
uweze kuzikumbuka kwa kutumia maneno machache ya ukumbusho
au bila kutumia hata kidogo. Kama hutakumbuka mahubiri, yaweza
kuwa vigumu kwa msikilizaji kukumbuka yale utakayohubiri.

Ni rahisi kwako na kwa msikilizaji kukumbuka kukumbuka hadithi.


Yesu alitumia mithali. Tamaduni nyingi kwanza kabisa hutegemea
hadithi kuwafundisha watoto wao. Hadithi huwa zimepangwa
kulingana na nyakati - kitendo hufuata wakati hufaao.

Waweza kuchagua maneno au fungu rahisi la maneno ili


kukukumbusha mambo muhimu ya mahubiri. Kwa mfano, mambo
muhimu ya mahubiri yaweza kuwa “tambaa, tembea, kimbia” au
“maombi, nguvu, hubiri.”

Tumia fungu la maneno ambayo watu wa tamaduni fulani


watakumbuka kwa urahisi. Huko Amerika, kuna kipindi cha upelelezi
kinachojulikana sana kwenye televisheni nao hutumia fungu la
maneno , “Ukweli pekee, mam.”

t. Sehemu ya mwisho ya mahubiri ndiyo sehemu muhimu zaidi. Katika


sehemu hii, waweza kufanya muhtasari wa yale uliyoyazungumzia,
ukitilia mkazo wazo kuu au kiini cha mahubiri. Baadaye sihi washiriki
waweze kufanya uamuzi.

u. Kama hauna ujuzi wa kuhubiri, inasaidia ukiandika mahubiri yako


yote kabla. Hii itakusaidia usiwe na makosa mengi ya sarufi, na
uweze kuchagua maneno vyema. Waweza kukagua mahubiri na
kufanya marekebisho. Inakusaidia kupanga fikira zako vyema.

Hata kama kumekuwa na wahubiri wanaofaa katika tamaduni


zingine ambao hutoa mahubiri yao kwa kuwasomea washiriki, ni
vyema zaidi usiposoma mahubiri yako. Wahubiri wengine waweza
kusisitiza mambo fulani kwenye maandiko, na kutumia sehemu za
maandiko zilizosisitizwa kama mwongozo wakati wa mahubiri. Kwa
kawaida ni vyema zaidi kuhubiri kutoka kwa muhtasari au kuhubiri
bila muhtasari. Kuhubiri bila muhtasari kunamruhusu mhubiri
kutembea anapotoa mahubiri yake. Inaruhusu mhubiri kutazama
washiriki wake macho kwa macho. Kama utatumia muhtasari,
waweza kuuweka ndani ya Biblia, ili uweze kufuata muhtasari huo na
pia uweze kusoma Maandiko kutoka kwa Biblia.

v. Urefu wa mahubiri ni tofauti kutoka kwa tamaduni moja hadi


nyingine. Usipitishe wakati ambao washiriki wako watasikiza.
Washiriki wanapoacha kusikiza, unapoteza wakati wako na wao.

w. Aina nyingine ya mahubiri ya ufasiri ni kueleza kifungu baada ya


kifungu. Katika aina hii ya mahubiri hautahitaji kujitayarisha saba
kama vile kwa mahubiri mengine yote. Utaratibu huu unasaidia
wakati unatoa mahubiri mafupi. (sermonette), au wakati una muda
mfupi sana au hauna muda kabisa wa kujitayarisha. Mhubiri husoma
kifungu, anaeleza kifungu na kukitumia katika maisha ya kila siku.
Baadaye mhubiri anasoma kifungu kingine, anaweza kukieleza/ na
kukitumia, kama vile Roho Mtakatifu anavyomwongoza. Mnenaji
huongozwa na Maandiko pamoja na Roho Mtakatifu. Vifungu fulani
vinafaa kwa aina hii ya ufafanuzi. Vifungu ambavyo vina wazo
ambalo linajisimamia katika kifungu kimoja au viwili yafaa zaidi.
Mifano ni pamoja na 1 Wakorintho 13 au Mathayo 5:1-16.

3. Mazoezi ya Kuwasilisha

Baada ya kutayarisha muhtasari wa mahubiri pamoja na Maandiko, ni


vyema uweze kufanya mazoezi ya kuwasilisha mahubiri. Waweza kupitia
mahubiri pamoja na rafiki. Uliza rafiki yako kama ameelewa kila wazo.
Uliza rafiki akupe marekebisho anayopendekeza kwa Maandiko na katika
kuwasilisha. Waweza kutoa mahubiri mbele ya kioo. Mwanzo wa kazi
yake, mhubiri mmoja alikuwa akihubiria miti msituni. Kama una kamera
ya kuchukua video au kinasa sauti, inasaidia kurekodi ujumbe wako,
baadaye uikague. Fanya mazoezi mpaka uweze kuiwasilisha bila kutumia
kumbukumbu. Lakini usijaribu kukariri mahubiri yote. Hii itakunyima uhuru
wa kutoa ujumbe. Itafanya mahubiri yasikike kuwa rasmi mno badala ya
kuwa inatoka kwa roho. Kariri mambo muhimu peke yake. Afadhali
uwachane na mambo yasiyo ya muhimu sana unapowasilisha mahubiri
badala ya kuwasilisha kila kitu kwa njia isiyosawishika, na njia rasmi
mno. Wachia nafasi Roho Mtakatifu aweze kulete habari mpya kwa
hotuba inapowasilishwa. Ni vyema kuweza kujianzia.

Watu wengi wana hofu ya kunena mbele za watu. Vitu ambavyo husaidia
kushinda uoga wa aina hii ni kama zifuatazo:

• Kuwa tayari. Fahamu yaliyo katika mahubiri. Fanya mazoezi jinsi ya


kuwasilisha mahubiri.
• Kuwa mnyenyekevu lakini mkakamavu. Elewa kuwa Mungu amekuita
uhubiri, na atakupa kila kitu unachohitaji ili utii mwito.

• Usiige mtu mwingine. Nena kutoka kwa roho yako. Waweza kutumia
mbinu kutoka kwa wanenaji wengine maarufu, lakini wewe si nakili wa
mnenaji mwingine.

• Tumia vielezo vinavyopendeza na lugha thabiti katika mahubiri yako


yote. Wasikilizaji wakiwa wasikivu wakati wa mahubiri, utakuwa na
uhakika katika kuwasilisha mahubiri.

4. Kuwasilisha na Maoni

Unapowasilisha ujumbe wako kwa washiriki, ongea kwa sauti ili walio katika
viti vya nyuma waweze kusikia. Njia moja ya kuwa na uhakika ni kutazama
mtu mmoja aliye nyuma kabisa , na kuongea kama vile unazungumza naye.
Badili sauti na mwendo wa hotuba yako, unaposisitiza mambo muhimu. Tua
kwa muda kwa wakati ufaao, ili uwape watu nafasi ya kufikiria kuhusu wazo
muhimu. Unapotua kwa muda , endelea kutazama wasikilizaji, ukitarajia
wafikirie kuhusu yale ambayo umesema.

Kuwa na msisimko kuhusu yale unayosema! Kama utaonyesha shauku,


wasikilizaji wako watakuwa na shauku. Tumia uhai. Tumia mikono jitwalia.

Onyesha washiriki heshima na upendo. Tarajia mema kutoka kwao.


Onyesha upendo huu katika hotuba yako na uonyeshe kwa uso wako. Kwa
kawaida anza mahubiri kwa tabasamu.

Kuna nyakati ni lazima uonye washiriki kutoka kwa dhambi au kosa. Kuna
wakati pia utahitaji kuwatia moyo wale wanaoumia. Kuna msemo
unaosema kuwa mhubiri “huumiza walio starehe, na kufariji walioumia.”

Tumia vielelezo jitwalia. Wakati mwingine manabii katika Biblia walieleza


jambo kwa kuigiza kisa au kwa kutumia chombo kueleza ujumbe wao.
Mbinu hii inafaa hasa wakati unaponena na watoto.

Pata maoni. Waweza kuchagua watu wachache unaoamini na walio na


maarifa mkutane nao baada ya kutoa mahubiri ili wakueleze sehemu
walizohisi kuwa na nguvu na sehemu dhaifu za mahubiri yako. Kama
umeoa, mwenzako anaweza kukupa maoni.

D. Mahubiri ya Mada

Mahubiri ya ufasiri yanajishughulisha na kweli tofauti zinazopatikana katika


Maandiko ya Biblia, bali mahubiri ya mada hujishughulisha na mada fulani.
Hatua zinazohusika katika kutayarisha mahubiri ya mada ni kama zifuatazo:
1. Kwa maombi chagua mada.

2. Tumia Biblia ya Mada au muhtasari wa mada na kitabu cha maneno


muhimu ya Biblia ili uweze kupata Maandiko yanayoambatana na mada.

3. Kama kuna marejeo mengi juu ya mada hiyo, utahitaji kupunguza mada
yako. Kwa mfano, badala ya kuhubiri kuhusu dhambi kwa jumla, unaweza
kupunguza mada yako ili iseme, “dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu.”
Marejeo ya Biblia yaliyo katika wavuti ilioko hapo juu yaweza kukusaidia
kupunguza uchunguzi wako.

4. Somo marejeo yote yanayohusu mada yako, ukiyaangalia kulingana na


muktadha.

5. Weka marejeo chini ya mambo machache muhimu ambayo unataka


kusisitiza kwenye mahubiri yako.

6. Kutoka kwa kweli utakazowasilisha, amua kiini cha mahubiri yako.

7. Kuza mahubiri mengineyo kama vile ungekuza mahubiri ya ufasiri.


Tayarisha utangulizi, wazo la kushawishi, vielezo, hitimisho n.k.

8. Ili kupunguza makosa, pata maoni kutoka kwa Wakristo wenye maarifa
kabla ya kuwasilisha mahubiri.

E. Kuchunguza Mhusika

Kuchunguza mhusika au mahubiri yanayoeleza maisha ya mtu ni ufasiri wa


maisha ya baadhi ya wahusika katika Biblia. Hatua zinazohusika katika
kutayarisha mahubiri haya ni kama zifuatazo:

1. Chagua mhusika wa Kibiblia kwa maombi.

2. Kwa kutumia Biblia ya mada na upatanifu, tafuta marejeo yote ya mhusika


huyo. Panga haya kulingana na mfululizo wa nyakati.

3. Soma marejeo ya Maandiko katika muktadha wake.

4. Tafuta maoni kutoka kwa ensaiklopidia ya Biblia, Kamusi ya Biblia, au


maelezo ya Biblia kwa habari zaidi kuhusu mhusika katika Biblia. Vifaa
katika wavuti vinapatikana hapo juu.

5. Orodhesha matukio makuu katika maisha ya mhusika.

6. Orodhesha mafunzo yaliyofunzwa kupitia kwa maisha ya mhusika.


7. Unaweza kutaka kumwonyesha mhusika kama mtu wa kwanza. Hiyo ni,
unaweza taka kuongea ni kama wewe ndiye Abrahamu au Mariamu
(Mama ya Yesu) au mhusika mwingine.

8. Unaweza taka kuonyesha mhusika kama mtu wa tatu.

9. Unapofuatilia maisha ya mhusika, kulingana na mfululizo wa nyakati,


inakuwa rahisi kukumbuka mawazo makuu ya mahubiri.

10. Kumbuka kumwonyesha mhusika kwa njia ambayo wasikilizaji watajifunza


na kutumia kweli za Kiroho. Kwa mfano, mhusika wa Kibiblia anaweza
onyeshwa kuwa mwenye furaha kwa kumtii Mungu au mwenye huzuni
kwa kutomtii Mungu.
2
Tazama Abraham Maslow’s vyeo vya mahitaji:
http://en.wikipedia.org/wiki/Maslow's_hierarchy_of_needs
3
Kenson Kuba, “Vitabu vya bure vya Mafunzo ya Uanafunzi,” Kitabu cha
mafunzo ya Uanafunzi cha 3, Ukurasa 21 katika mtandao.
http://biblestudycd.com/books/book3.pdf

RUDI KWA MUHTASARI ¾ ¾


KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

V. Kufundisha

A. Utangulizi

Kanuni nyingi zinazotumika katika hermeneutics pia hutumika katika


mafundisho. Kama kuhubiri kunaweza tofautishwa na kufundisha, kwa
kawaida kuhubiri kunahimiza kumsihi msikilizaji kufanya uamuzi wakati huo,
lakini kufundisha kunahimiza kumjulisha mshiriki ili afanye uamuzi mwafaka
baadaye. Msingi wa kufundisha ni uhusiano kati ya mwalimu na wanafunzi.
Tunawafunza watu, sio masomo. Wanafunzi wanaompenda mwalimu, wana
uwezekano mkubwa wa kujifunza kutoka kwa mwalimu kuliko wanafunzi
ambao hawampendi mwalimu.

Mbinu za kufundisha hutofautiana kulingana na umri ya wahusika, ukubwa wa


kundi, na maarifa ya washiriki. Watu wazima hujifunza vyema wanapohusika
katika majadiliano. Kwa hivyo kama kuna walimu wa kutosha, ni vyema
kuwafunza watu wazima katika makundi ya watu sio zaidi ya kumi na mbili.
Majadiliano kwa kawaida hufanyika katika makundi madogo, lakini mhadhara
hutumika vyema kwa makundi makubwa. Kama hakuna walimu wa kutosha wa
kufunza makundi madogo, mwalimu anaweza kuwagawanya watu wazima
katika makundi madogo ili wajadiliane yale yaliyowasilishwa kwa kundi nzima.
Watu wazima wanapokomaa katika imani na maarifa ya Kibiblia, majadiliano
zaidi hufanyika na mhadhara hufanyika kwa uchache. Mhadhara unawafaa
watoto. Ni wazi kuwa watoto wana usikivu mfupi kuliko watu wazima. Kwa
hivyo vitendo vinahitajika kwa watoto. Walimu wanaweza kuwasimulia hadithi.
Masomo ya vielezo yanafana kwa watoto wadogo. Mwalimu anaweza
kuwaonyesha watoto baadhi ya vifaa kama kijiti, na awaelezee ya kwamba
wachungaji hutumia vijiti kuwaongoza kondoo. Mwalimu anaweza kuwaeleza
ya kwamba Mungu anatuongoza. Anaweza kutuongoza katika njia ifaayo.

Watu wanapokutana kujifunza Biblia, kunafaa kuwa na ushirika na maombi.


Kwa hivyo mikutano inaweza anza kwa watu kushiriki shangwe na mahitaji
yao. Kama watu katika makundi hawajuani, mwalimu anaweza kuhimiza
majadiliano. Mwalimu anaweza kuufungua mkutano kwa kuuliza jambo
lisilohusika na funzo la Kibiblia. Mifano ya kuanzisha mazungumzo ni kama
ifuatavyo:

“Kila mmoja wenu anaweza kutwambia jina lake na jambo linalo kuhusu
ambalo hatufahamu?”

“Kama ungependa doto yako itimike, doto yako yaweza kuwa gani?”
Washiriki wakiendelea kujuana, hautahitaji kuuliza maswali ya kuanzisha
mazungumzo. Badala yake, mwalimu atawauliza kwa kawaida washiriki
waweze kushiriki mambo yale yametendeka katika maisha yao katika wiki
moja iliyopita. Na watu wanaweza kuuliza maombi.

Watu katika kanisa wanatakiwa kuwa kama familia. Mtu akiwa mgonjwa, watu
walio katika kundi la kujifunza Biblia wanatakiwa kumtembelea. Ikiwa washiriki
wana mahitaji, washiriki wa kundi dogo mara nyingi watajua mahitaji hayo. Ili
kudumisha uhai wa washiriki kanisani, na kusaidia kuanzisha ushirika na
kukua kiroho, washiriki ni lazima wawe sehemu ya kundi dogo katika
mwili wa kanisa.

B. Somo

Kama vile mahubiri, somo la Biblia laweza kuwa la ufasiri, la mada au


kuchunguza mhusika.

1. Ufasiri

Somo la ufasiri laweza kuwa la kiini au kifungu kwa kifungu.

a. Kiini

Kanuni nyingi za mahubiri hutumika kwa kutayarisha somo la ufasiri


wa kiini. Lakini katika mazingira ya kufunza, washiriki wanaweza
kuzungumza na mnenaji na mmoja kwa mwingine. Somo laweza
kuwa ndefu kuliko mahubiri.

b. Kifungu kwa Kifungu

Somo la ufasiri wa kifungu kwa kifungu lafaa katika mafundisho


kuliko kuhubiri. Kila mmoja wa kundi la mafundisho aweza kuuliza
maswali na kuchangia kuhusu vifungu hivyo. Hii huwafanya washiriki
kuwa wasikivu na kuhusika katika somo.

2. Mada

Somo la mada huruhusu wanafunzi kujifunza yale ambayo yanahusu


kundi hilo. Kwa mfano, kanisa laweza kuamua kufunza washiriki wote
wapya theolojia ya msingi. Kwa hivyo somo la mada laweza kutolewa kwa
suala kama Utatu Mtakatifu, Kuanguka kwa Mwanadamu, Mafundisho ya
Wokovu. Kanuni nyingi sawa na zile zinazotumika katika kutayarisha
mahubiri ya mada hutumika kwa kutayarisha masomo ya mada.
3. Kuchunguza Mhusika

Kuchunguza mhusika humruhusu mwalimu kuzoeza washiriki somo. Kwa


mfano, mwalimu anaweza kuchunguza wahusika wa kike katika Biblia kwa
ajili ya darasa la wanawake.

RUDI KWA MUHTASARI ¾ ¾


KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

VI. Habari za Zaidi

Kwa habari za zaidi kuhusu Kujifunza Biblia, Kuhubiri na Kufunza, tazama wavuti
ufuatao. Elekeza kwa “Vitabu vya Kujifunza Uanafunzi vya Bure” na uchague
Kitabu cha Mafunzo ya Uanafunzi cha 3.

http://biblestudycd.com/

Shule ya Biblia ya Ames inatoa kitabu cha kurasa 259- cha bure kwenye mtandao
ambacho kinapeana kanuni za kujifunza Biblia. Tazama “Mitindo bunifu za
Kujifunza Biblia” katika wavuti ufuatao.

http://www.amesbible.org/download.html

Elekeza kwa “Wavuti wenye majina ya Masomo ya Biblia” kwa habari muhimu
kuhusu hermeneutics na mada nyinginezo katika wavuti ufuatao.

http://www.bible-researcher.com/

Huduma za RBC hutoa mafunzo ya Biblia na Kuishi kwa Mkristo. Ili kujiandikisha
lazima mwanafunzi awe na anwani ya imeli na awe na namba ya siri. Enda kwa
kiunganishi kifuatacho.

http://cc.christiancourses.com/

Wavuti ufuatao unatoa habari kuhusu kujifunza Biblia. Elekeza kwa “Wavuti wenye
majina ya Masomo ya Biblia” arafu uelekeze kwa “hermeneutics.”

http://www.bible-researcher.com/

Ifuatayo ni injini ya kutafuta kwenye mtandao wavuti za Kikristo. Ungependa


kuchunguza kutoka kwa wavuti huu kuhusu wavuti zinginezo ambazo zaweza
kukusaidia katika huduma yako.

http://www.crosssearch.com/

Kwa mfano, wavuti ulioko hapo juu unatupa kiunganishi kifuatacho, ambao unatoa
Mafunzo ya Bure ya Biblia kwa Mtandao kwa watoto.

http://www.ebibleteacher.com/index.html

RUDI KWA MUHTASARI ¾ ¾


KUHUBIRI NA KUFUNDISHA

VII. Kazi ya Ziada

A. Hubiri Mahubiri mawili

Kama unaweza kuipanga, ni lazima uhubiri mahubiri mawili ili kumaliza darasa
hili.

B. Ongoza Madara Mawili

Kama unaweza kuipanga, ni lazima ufunze vipindi viwili katika


kundi dogo ili kumaliza darasa hili.

RUDI KWA MUHTASARI ¾ ¾

You might also like