You are on page 1of 2

SEMINA YA KUJIFUNZA LITURGIA YA IBADA YA SIKU YA BWANA

1. MAANDALIZI; Maandalizi ya ibada yafanyike wiki nzima kuanzia jumapili jioni hadi jumamosi, ili
kubaini matukio muhimu mapema kama vile matengenezo na siku ya watakatifu n.k,
 Ili kuweza kuimba litrugia vizuri bila kigugumizi, na kuandaa nyimbo mapema kufuatana
na majira na matukio husika katika kalenda; inashauriwa kuwa ni vema nyimbo za
jumapili ijayo itangazwe kwa wakristo na makundi ya kwaya ili wafanyie mazoezi pamoja
na wakristo ili kuondoa kigugumizi ndani ya ibada kwa kulinda uchaji wa ibada.
2. ALAMA ZA MADHABAUNI YAANI LITURGIA YA IBADA; Kariri alama za madhabauni mapema na
utofautishe alama ya kugeukia madhabauni na alama za kugeukia usharika,
-mkono wa kugeukia madhabahu ni mkono wa kushoto(bayshani) na mkono wa kugeukia
usharika ni mkono wa kulia (dakw do /ayma)
 Hii inaonesha kuwa huna kitu unataka kutoka kwa MUNGU na unapeleka matatizo ya
wakristo kwa MUNGU
 Na mkono wa kulia (dakw do /ayma) hii inaonesha unaleta majibu ya mahitaji yetu
kutoka kwa MUNGU.
3. MAELEZO; Alama ni kwaajili ya mchungaji au kiongozi wa ibada kuonesha kuwa wakati
huo ageukie madhabauni, akilenga msalaba wa madhabahu bila kupinda pinda
 Alama ni kuonesha kuwa wakati huo ageukie usharika na mgongo wake
uelekee msalaba bila kupinda pinda
4. MADHABAHU; Madhabahu iandaliwe mapema na wahudumu wa kanisa walioko zamu
wahakikishe kila kilichopo madhabahuni ni sahihi na ipo kwenye majira yake
 NB; Kama wahudumu wa kanisa wamekosekana wazee waandae madhabahu vizuri.
 NB; Kama wote hawapo mwenyekiti wa idara ya wanawake na makamu au katibu
wataandaa madhabahu isipokuwa siyo watu wa kudumu.
5. MAOMBI YA OFISINI KABLA YA IBADA KUANZA; Wafuatao wafanye maombi pamoja wakiwa
ofisini wote wawepo,ikiwa mtu mmoja amekosekana wakati wa maombi hayo akaingia ibadani
wakati ni muhusika yupo zamu, hairuhusiwi kutumika siku hiyo.
I. Kiongozi wa ibada akiwa tayari amevaa vazi la ibada
II. Mhubiri wa ibada akiwa tayari amevaa vazi la ibada
III. Wazee wa zamu wakiwa tayari wamevaa vazi la ibada/huduma
IV. Wahudumu wa zamu wakiwa tayari wamevaa vazi la huduma
V. Mchungaji wa ibada kama yupo akiwa amevaa vazi la ibada
VI. Msomaji wa somo la 1
6. KUZINGATIA NAMBA WAKATI WA KUINGIA IBADANI; Mtiririko huu ufuatwe wakati wa kuingia
ibadani.
I. Wahudumu watangulie mbele wakati wa kuingia ibadani
II. Wazee watafuata baada ya wahudumu
III. Msomaji wa somo la kwanza
IV. Kiongozi wa ibada na muhubiri watafuata,watakuwa wa mwisho pamoja na mchungaji
kama yupo
7. KUINGIA MLANGO WA KANISA; Wazee wahudumu msomaji kiongozi wa ibada na muhubiri
wataingia na wimbo wakati huo wakristo wote wawe wameingia ndani na wote wasimame.
8. KABLA YA KUPANDA MADHABAHUNI; Wahudumu wa zamu wakifika ngazi ya kwanza ya
madhabahu wasogee hatua moja pembeni,moja kulia na mwingine kushoto,
 Wazee wa zamu wakifika ngazi ya kwanza ya madhabahu wote pamoja na wahudumu
watasogea pembeni hatua moja kila mmoja
 Kiongozi na mhubiri watasimama katikati na kiongozi wa ibada akielekea msalaba wa
madhabahuni wote wainame pamoja na wakristo mara moja tu.
9. KUPANDA MADHABAHUNI; Kiongozi wa ibada atatangulia na mhubiriatafuata, wakati kiongozi
wa ibada akiwa madhabahuni na mhubiri,kiongozi wa ibada atasimama katikati akielekea
msalaba wa madhabahuni bila kupinda pinda kisha watasali sala ya kimya au kwa sauti ya chini,
NB; Angalia Tumwabudu MUNGU wetu ukurasa wa 249 maandishi mekundu.

You might also like