You are on page 1of 12

TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD

MWONGOZO WA HALMASHAURI KUU KUHUSU


MAOMBI YA KUFUNGA YA SIKU 21
Januari 17 – Februari 06, 2022
Wapendwa viongozi wa kanisa zuri la TAG ngazi zote, Pokeeni salamu za upendo
kutoka Ofisi Kuu ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) hapa CBC, Dodoma.
Kamati Kuu ya Utendaji kwa Niaba ya Halmashauri Kuu ya TAG, inawataarifu kuwa
kuanzia Januari 17 hadi Februari 06, 2022 tutakuwa kwenye Maombi Maalum ya
Siku 21 kama ilivyooneshwa kwenye Kalenda yetu ya Shughuli 2022. Maombi haya
yamekusudiwa kuwa ya Kujiweka Wakfu na Kuombea Mipango na Malengo kwa ajili ya
Mwaka 2022. Sasa tunayo nafasi ya kwenda mbele zake na kuzipeleka hoja zetu
zenye nguvu. Tunawaita watumishi wote wa TAG mahali walipo kuwaongoza
washirika wetu katika maombi haya muhimu ya siku 21 (maombi ya Daniel “Dan.
9:3”). Maombi haya yatafanyika katika nyumba zote za ibada nchini. Viongozi
waongoze na kusimamia kwa ufanisi wa hali ya juu maombi haya.
“Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake siku zote” – Zaburi 105:4

Ili kuwa na matokeo ya ushiriki mzuri mambo yafuatayo yazingatiwe:


1. Wachugaji viongozi waweke utaratibu madhubuti wa uongozaji maombi hayo.
Waongozaji wa maombi haya kila siku apangwe mtu mwenye nguvu, uwezo na
hekima ya kiroho ya kusimamia maombi ili washirika wote waombe kwa
kishindo kikubwa cha rohoni na madhihirisho ya kimungu yatokee.
2. Kipindi cha wiki tatu za maombi haya ya kitaifa kila mtumishi na mshirika wa
TAG ajiepushe na ratiba sisizo za lazima zinazoweza kumfanya asishiriki
maombi haya kwa ufanisi, kimsingi kila mmoja atengeneze uwezekano wa
kushiriki maombi haya kwa siku zote.
3. Kabla ya maombi kutakuwepo na kipindi kifupi tu cha sifa na Neno la
utangulizi la robo saa, yaani dakika 15 ili kuwaandaa waamini kuomba.
4. Maombi haya yaombwe kwa pamoja katika siku zote 21 na yasibadilishwe kuwa
ya kupokezana kimnyororo au kushirikisha watu au vikundi vichache tu. Haya
ni maombi ya washirika wote wa TAG Nchi nzima.
5. Siku za Ijumaa mikesha ya usiku izingatiwe kwa kuhamasisha na kusimamiwa
ipasavyo.

1
6. Kamati za section katika kila Jimbo zifuatilie kwa karibu ibada za maombi
haya makanisani na kupeleka mrejesho wake kwa Maaskofu wao wa majimbo
kila wiki ili kupata taarifa nzuri.
7. Baada ya kukamilika maombi haya Mchungaji Kiongozi anaweza kutoa nafasi
ya washirika kushuhudia madhihirsho ya matendo ya Mungu waliyoyaona
wakati wa siku za maombi na hivyo kuzidi kujenga hamasa kubwa kwa Kanisa,

Wapendwa Viongozi, Kamati Kuu ya Utendaji inawatakia Baraka za Mungu na uwepo


wake mwingi wakati wote wa maombi haya ambayo utalisababishia kanisa letu zuri la
TAG kusonga mbele kwa mafanikio makubwa na kimkakati kwa utukufu wake mkuu
tukiwa pamoja na Bwana wa Kanisa.

M A M B O Y A K U O M B E A NA
R A T I B A YA MAOMBI KWA SIKU 21
Tarehe/ Siku Mambo ya kuombea
Siku ya 1 Kuhitaji Rehema za Bwana, Msamaha, Utakaso wa Maisha yetu
17/01/2022 na Kufanywa Upya kama kanisa la TAG (Mithali 28:13;
Jumatatu Kumb 28:1)
1. Tuhitaji na kuomba Rehema za Bwana kibinafsi, Familia, na
Kanisa.
2. Tuombe Msamaha kwa kutofanya kama Mungu apendavyo.
3. Tuombe utakaso na kuhitaji Mungu kutembea nasi kwa upya
4. Tuombe na kumuhitaji Mungu atufanye Upya na kuwa vile Mungu
alivyotuumba kuwa kwa utukufu wake.
Siku ya 2 Kuyakubali Mapenzi ya Bwana Maishani na Kujiweka Wakfu Kwa
18/01/2022 ajili ya Bwana 2022 (2Nya 29:31a;Efe 4:23-24; Yoh 17:19)
Jumanne 1. Kujiweka wakfu kwa Bwana mshirika mmoja mmoja kibinafsi.
2. Kujiweka wakfu kwa Bwana kila familia kwa ajili ya Bwana.
3. Kujiweka wakfu kwa Bwana kama kanisa la Mahali Pamoja.
4. Kujiweka wakfu kwa Bwana kama Idara za Kanisa ngazi zote.
5. Kujiweka Wakfu kwa Bwana kama Kanisa na Jeshi la Bwana kwa
kazi yake.

2
6. Tujiweke Wakfu kwa Bwana kwa Ajili ya Mpango Mkakati wa
Miaka 13 ya Moto wa Uamsho na Kuuombea utekelezaji wake.
(Tunapo ombea hitaji hili kila kanisa litumie Kile Kipeperushi cha
Kujiweka Wakfu Mpango huu wa Pili ili kutumia kuombea Mpango
Mkakati)
Siku ya 3 Kumshukuru Mungu kwa Kuwa ametenda, anatenda na anaendelea
19/01/2022 kutenda. (Zab 7:17; 118:1; 1Thes 5:18).
Jumatano 1. Mshukuru Mungu kwa Mwaka 2021 kwa kutuwezesha kutimiza
malengo na mipango ya kanisa na binafsi kwa ujumla.
2. Mshukuru Mungu kwa Utetezi na Utunzaji wa kimungu katika
maeneo yote ya Maisha na huduma.
3. Mshukuru Mungu kwa kuliimarisha, kulikuza na kulistawisha kanisa
lake, Watumishi wake na Washirika wote wa TAG.
4. Mshukuru Mungu kwa aliyotenda, anayotenda na atakayotenda.
5. Mshukuru Mungu kwa Zawadi ya mwaka 2022 na kwa mambo
makubwa yanayobebwa na mwaka huu kwa utukufu wa Mungu.
Siku ya 4 Kuwaombea Watoto, Kuliombea Kanisa la Watoto, na Kuyaombea
20/01/2022 Mazingira salama ya Watoto wetu kukulia na kuweza kumcha
Alhamisi Mungu na kumtumikia (Zab 17:3; Mithali 22:6)
1. Waombee Watoto, mbengu Mungu aliyoiotesha ndani yao ikue
kufikia makusudi makamilifu ya kimungu.
2. Liombee Kanisa la Watoto litimize kusudi la kuanzishwa kwake
kuwahudumia Watoto.
3. Ombea upatikanaji wa watendakazi na uwezeshaji wa huduma ya
mtoto
4. Ombea Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, Waliopotea
Bwana awarudishe, wanaowindwa na hatari Bwana awalinde na
kuwaponya.
5. Muombe Mungu alipe Kanisa mzigo wa kuwalea Watoto na kujitoa
kwa ajili yao bila kuchoka.
6. Ombea Kanisa, familia na taifa kuwa mahali salama pa watoto
kujifunza na kulelewa ili kumuishia Mungu.

3
Siku ya 5 Kuwaombea Chipukizi na Vijana kuwa hazina ya Kimungu kwa
21/01/2022 kizazi Kilichopo (Zab 119:9-11)
Ijumaa 1. Waombee Chipukizi na Vijana wote kwenye mchakato wa mapito
ya mabadiliko wabadilike pamoja na Mungu na kumfaninia Yeye.
2. Ombea upatikanaji wa watendakazi na uwezeshaji wa huduma ya
Chipukizi na Vijana.
3. Ombea Chipukizi na Vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi,
Waliopotea Bwana awarudishe, wanaowindwa na hatari Bwana
awalinde na kuwaponya.
4. Ombea Watoto wa Kiume na Wa Kike utunzaji wa Kimungu na
malezi salama nyumbani na mashuleni.
5. Muombe Mungu alipe Kanisa mzigo wa kuwalea Chipukizi na Vijana
na kujitoa kwa ajili yao bila kuchoka.
6. Ombea Kanisa, familia na taifa kuwa mahali salama pa Chipukizi
na Vijana kujifunza na kulelewa ili kumuishia Mungu.
7. Ombea Yatima Mungu awainulie wazazi na walezi wa kuvuka nao.
Siku ya 6 Kuwaombea Wanawake kuwa chombo cha Uamsho na Uimara wa
22/01/2022 Familia, Kanisa na Taifa.( Mdo 2:18; Fil 4:2-3)
Jumamosi 1. Waombee Wanawake wawe kile Chombo ambacho Mungu
anakihitaji ili kuujenga na wala sio kuubomoa ufalme wake.
2. Ombea upatikanaji wa watendakazi na uwezeshaji wa huduma ya
Wanawake.
3. Ombea Wanawake wanaoishi katika mazingira hatarishi,
Waliopotea Bwana awarudishe, wanaowindwa na hatari Bwana
awalinde na kuwaponya.
4. Muombe Mungu alipe Kanisa mzigo wa kuwahudumia Wanawake
kwa utakatifu wote na kuwapa nafasi ya kutumika.
5. Ombea Wanawake waweze kutimiza Wajibu wao kulifanya Kanisa,
familia na taifa kuwa mahali salama pa kujifunza na kulelewa ili
kumuishia Mungu.
6. Muombe Mungu ainue na kuita watumishi wanawake kuwa Jeshi
kubwa la Bwana kwenye Miaka hii 13 ya Moto wa Uamsho.
7. Ombea Wanandoa, Wajane, Waleapeke(single Parents), na

4
wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Siku ya 7 Kuwaombea Wanaume Kujitambua na Kusimama kwenye Nafasi
23/01/2022 zao ili kuwa chombo cha Uamsho na Uimara wa Familia, Kanisa
Jumapili na Taifa. (Isaya 40: 1-6, 30-31)
1. Waombee Wanaume wote Kuwa aina ya watu ambao Mungu
atawategemea katika ujenzi wa Ufalme wake.
2. Ombea upatikanaji wa watendakazi watakao simama na huduma ya
Wanaume.
3. Ombea Wanaume waliopoteza Mwelekeo wakawe sawa,
Waliopotea Bwana awarudishe, wanaowindwa na hatari Bwana
awalinde na kuwaponya.
4. Muombe Mungu alipe Kanisa mzigo wa kuwahudumia Wanaume kwa
nguvu na ubunifu wa kuweka mikakati ya Utekelezaji.
5. Ombea Wanaume waweze kutimiza Wajibu wao kulifanya Kanisa,
familia na taifa kuwa mahali panapotawaliwa na Mungu pekee.
6. Muombe Mungu ainue watendakazi miongoni mwa Wanaume na
kuungana na kwenye Miaka hii 13 ya Moto wa Uamsho.
7. Ombea Wanandoa, Wagane, Waleapeke(single Parents), na
wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Siku ya 8 Kuliombea Taifa letu la Tanzania na Serikali Yake (1Timotheo
24/01/2022 2:1-2; Fil 4:6)
Jumatatu 1. Ombea taifa la Tanzania Nafasi ya Mungu ibaki kuwa Nafasi ya
Mungu na hofu ya Mungu ilifunike taifa letu.
2. Ombea Amani, Utulivu na Ustawi wa Taifa la Tanzania tusiwe tu
kisiwa cha Amani bali tuviishi Amani na Utulivu huo.
3. Ombea Mihimili hii mitatu ya Serikali: Rais (Serikali), Bunge na
Mahakama viwe kwa maslahi Mapana ya Taifa letu na Wananchi
wake
4. Ombea vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama, Mungu avitumie.
5. Ombea taifa la Tanzania lisiipungukie Neema ya Mungu katika
Nyanja zote.

5
Siku ya 9 Ombea hali ya Uchumi wa Kanisa na Taifa (Zab89:11-15; 24:1-10)
25/01/2022 1. Bwana awape Watendaji ngazi zote wenye dhamana awape moyo
Jumanne wa uwakili kwa manufaa ya kanisa na Taifa.
2. Rasilimali zote zitumike vema kwa ustawi wa kanisa na jamii.
3. Wapatikane wadau wa Uchumi na Maendeleo walio waaminifu wa
kutumika na kanisa na Taifa letu la Tanzania.
4. Mungu alikuze Pato la kanisa na Serikali na liweze kutumika vema.
5. Mungu atupe macho ya kuzigundua na kuzitumia hazina nyingi
zilizo katika taifa na kanisa.
6. Sekta zote za kiuchumi ziendelee kustawi kwa kumpa Mungu
nafasi ya kwanza na kumtegemea yeye pekee.
7. Mungu aliekeze kanisa kwenye uwekezaji sahihi wenye kuwezesha
taifa na kanisa kutimiza majukumu yake.
Siku ya 10 Ombea Uamsho Mkuu Utokee kwa kanisa na Taifa letu
26/01/2022 (1Kor 1:18, 24; 6:7)
Jumatano 1. Tuombe kupewa neema ya kumwamini Mungu kuwa na uamsho
Mkubwa nchi nzima.
2. Tuombe madhihirisho Makubwa na Umwagiko mkuu wa Roho
Mtakatifu viongezeke kwa kanisa zima la Tanzania
3. Tuombe Mungu kuudhihirisha Uponyaji kwa watu wake, Neema ya
Wokovu, na matendo makuu ya miujiza kutendeka katika
makusanyiko ya watu wa Mungu.
4. Watumishi waliopo Bwana awahuishe tena, Wapya waongezeke na
kuhudhuria mafunzo ya utumishi ngazi husika.
5. Makanisa mengi yafunguliwe, yategemezwe na kustawi.
6. Waliorudi nyuma wamrudie Kristo Yesu na kanisa lake.
7. Imani potofu zisambaratike na kufichuliwa udanganyifu wao.
8. Bwana amimine roho ya maombi na kumtafuta yeye ngazi zote za
kanisa, makongamano ya maombi yawe yenye nguvu za Mungu.
9. Tusimame kinyume na vikwazo na vizuizi vyote vya uamsho wa
kweli.

6
Siku ya 11 Omba Kumuhitaji Bwana wa Wakanisa uwepo wake uwepo katika
27/01/2022 Ibada na Makusanyiko yote ya Kanisa na Idara ngazi zote
Alhamisi (Eze 43:4-5; Mdo 13:2)
1. Bwana wa Kanisa awepo, asimamie, na kuongoza ibada na
makusanyiko yote
2. Kuwepo Roho ya umoja na mshikamano mkubwa katika ibada zetu.
3. Neema ya Mungu ijae katika makusanyiko yetu yote.
4. Ombea afya za wachungaji na viongozi wote wa Kanisa na Idara ili
Mungu awatumie kwa uweza na nguvu ktk makusanyiko yote.
5. Hila zozote za adui na utendaji wa shetani zishindwe na
kusambaratika kwenye ibada na mikusanyiko yote ya kanisa.
6. Ibada na Mikusanyiko yote iwe yenye kulijenge Kanisa kama mwili
wa Kristo kitaifa.
Siku ya 12 Ombea Kazi ya Uinjiisti Mikutano yote ya Injili, Ushuhudiaji wa
28/01/2022 Nyumba kwa nyumba na wa mtu kwa mtu. (Marko 1:15; 8:35)
Ijumaa 1. Omba Mungu atuwezeshe kuzaa wainjilisti wa kukidhi hitaji la
Mavuno kila ngazi ya kanisa.
2. Bwana wa Kanisa aibue, ampake mafuta na kumtumia kila
mwinjilisti na mshirika katika kuvuna roho zilizopotea.
3. Wainjilisti wote pamoja na Timu za watenda kazi wao wote wawe
na afya njema na nguvu ya kuitenda kazi ya injili.
4. Mikutano ya Injili na ushuhudiaji wa aina zote vilete Mavuno
mengi yatakayokaa.
5. Wahudumu wote wa Mikutano na Ushuhudiaji wa aina zote
waifanye kazi kwa Nguvu za Roho Matakatifu, kujituma na
kujidhabihu.
6. Ombea Miundo mbinu yote ya mikutano ifanye kazi vizuri (kama
vyombo vya sauti) ikiwa ni pamoja na mwitikio mzuri wa
mahudhurio makubwa na utulivu.
Siku ya 13 Ombea kanisa la TAG ngazi ya Kitaifa (2Sam 18:3; 1Wafalme
29/01/2022 22:31-33)
Jumamosi 1. Mwombee Askofu Mkuu na Familia yake, Ombea huduma yake ya
kichungaji na Uaskofu, afya yake, ulinzi na Utunzaji wa Kimungu

7
uwe juu yake.
2. Mwombee Makamu Askofu Mkuu na Familia yake, Ombea huduma
yake ya kichungaji na Uaskofu, afya yake, ulinzi na Utunzaji wa
Kimungu uwe juu yake.
3. Mwombee Katibu Mkuu na Familia yake, Ombea huduma yake ya
kichungaji na Ukatibu, afya yake, ulinzi na Utunzaji wa Kimungu
uwe juu yake.
4. Mwombee Mt Mkuunza Hazina na Familia yake, Ombea huduma
yake ya kichungaji na Uhazini, afya yake, ulinzi na Utunzaji wa
Kimungu uwe juu yake.
5. Ombea Idara Zote Kitaifa yaani; Elimu, CAs, CASFETA, Miradi,
Umisheni, Watoto & Wanafunzi, CMF, Maandiko na Uanafunzi,
WWK na Uinjilisti (Ombea kamati zao, Ofisi zao, Watendakazi
wa Idara na Familia zao)
6. Ombea Vitengo vya Makao Makuu – Tumaini Pension Fund (TPF),
Uwezo Financial Service (UFS), TEHAMA, Gazeti la Jibu la
Maisha, Muziki na Sifa, na Kamati ya Maombi Kitaifa (Ombea
kamati zao, Ofisi zao, Watendakazi wa Vitengo na Familia zao)
7. Ombea Wenyeviti na Makatibu wa Kanda Zote Saba, Kamati Zao,
Ofisi zao, watendakazi, na familia zao.
Siku ya 14 Ombea kanisa la TAG Ngazi ya Jimbo (2Thes 1:4; Matendo
30/01/2022 12:1-5,11-12)
Jumapili 1. Mwombee Askofu wa Jimbo lenu na Familia yake, Ombea huduma
yake ya kichungaji na Uaskofu, afya yake, ulinzi na Utunzaji wa
Kimungu uwe juu yake.
2. Mwombee Makamu Askofu wa Jimbo lenu na Familia yake, Ombea
huduma yake ya kichungaji na Uaskofu, afya yake, ulinzi na
Utunzaji wa Kimungu uwe juu yake.
3. Mwombee Katibu wa Jimbo lenu na Familia yake, Ombea huduma
yake ya kichungaji na Kikatibu, afya yake, ulinzi na Utunzaji wa
Kimungu uwe juu yake.
4. Mwombee Mtunza Hazina wa Jimbo lenu na Familia yake, Ombea
huduma yake ya kichungaji na Uhazini, afya yake, ulinzi na

8
Utunzaji wa Kimungu uwe juu yake.
5. Ombea Idara ngazi ya Jimbo, Idara ya Elimu, CAs, CASFETA,
Miradi, Umisheni, Watoto & Wanafunzi, CMF, Maandiko na
Uanafunzi, WWK na Uinjilisti (Ombea kamati zao, Ofisi zao,
Watendakazi wa Idara na Familia zao)
6. Ombea Chuo cha Kupanda Makanisa Katika Jimbo lako (Ombea
Bodi ya Chuo, Uendeshaji, Upatikanaji wa Wanafunzi, Ujenzi,
Watendakazi na Familia zao)
Siku ya 15 Ombea kanisa la TAG Ngazi ya Sehemu (2Samweli 21:15-17)
31/01/2022 1. Mwombee Mwangalizi wa Sehemu yenu na Familia yake, Ombea
Jumatatu huduma yake ya kichungaji na Uangalizi, afya yake, ulinzi na
Utunzaji wa Kimungu uwe juu yake.
2. Mwombee Makamu Mwangalizi wa Sehemu yenu na Familia yake,
Ombea huduma yake ya kichungaji na Uangalizi, afya yake, ulinzi
na Utunzaji wa Kimungu uwe juu yake.
3. Mwombee Katibu wa Sehemu yenu na Familia yake, Ombea
huduma yake ya kichungaji na Ukatibu, afya yake, ulinzi na
Utunzaji wa Kimungu uwe juu yake.
4. Mwombee Mtunza Hazina wa Sehemu yenu na Familia yake,
Ombea huduma yake ya kichungaji na Uhazini, afya yake, ulinzi na
Utunzaji wa Kimungu uwe juu yake.
5. Ombea Idara ngazi ya Sehemu, CAs, CASFETA, Miradi,
Umisheni, Watoto & Wanafunzi, CMF, Maandiko na Uanafunzi,
WWK na Uinjilisti (Ombea kamati zao, Ofisi zao, Watendakazi
wa Idara na Familia zao)
6. Ombea Wachungaji wote familia zao na Makanisa
wanayoyaongoza kwenye sehemu yenu.
Siku ya 16 Ombea kanisa la TAG Ngazi ya Kanisa la Mahali Pamoja
01/02/2022 (Ufu 1:4; 2Thesalonike 3:1-2)
Jumanne 1. Mwombee Mchungaji Kiongozi wenu na Familia yake, Ombea
huduma yake ya kichungaji, afya yake, ulinzi na Utunzaji wa
Kimungu uwe juu yake.
2. Waombee Wachungaji Wasaidizi/wenza wa kanisa lenu na Familia

9
yake/zao, Ombea huduma yake/yao ya kichungaji, afya yake/yao,
ulinzi na Utunzaji wa Kimungu uwe juu yake/yao.
3. Mwombee Wazee wa Kanisa lenu na Familia zao, Ombea huduma
yao ya Uzee wa Kanisa, afya yao, ulinzi na Utunzaji wa Kimungu
uwe juu yao.
4. Ombea Idara ngazi ya Kanisa la Mahali Pamoja, CAs, CASFETA,
Miradi, Umisheni, Watoto & Wanafunzi, CMF, Maandiko na
Uanafunzi, WWK na Uinjilisti (Ombea kamati zao, Ofisi zao,
Watendakazi wa Idara na Familia zao)
5. Ombea Matawi ya kanisa la Mahali Pamoja na Wachungaji wake
wote na familia zao na Makanisa wanayoyaongoza.
6. Ombea mahitaji ya mshirika mmoja mmoja ndani ya kanisa.
(Viongozi wawatie moyo washirka wao walete mahitaji yao mengi
na kanisa liyapeleke mbele za Bwana)
7. Ombea uboreshaji na upanuzi wa miundombinu ya kanisa
Siku ya 17 Ombea vyuo vyetu Tisa vya Biblia (Kol 2:8; Efe 1:14;
02/02/2022 Mithali 2:6-7)
Jumatano 1. Ombea Upanuzi na ukuaji wa vyuo vyetu:- Kanda ya Kati CBC,
ACTS-Dodoma, Kanda ya Kusini SBC-Mbeya, Kanda ya Kaskazini
NBC-Arusha, Kanda ya Kaskazini Mashariki Global Harvest
GHBC-Dar es salaam, Kanda ya Ziwa LVBC-Mwanza, Kanda ya
Kusini Mashariki SEBCO-Lindi, Kanda ya Magharibi WBC-Tabora,
na Global University GU – Dar Es Salaam.
2. Ombea Vyuo hivi kuwa viwanda vya kuzalisha Watendakazi na
Viongozi watumishi wana Uamsho.
3. Ombea watumishi wote wanaoitwa katika kanda hizi watumie
vizuri fursa ya kuwa na vyuo hivi na kujiendeleza kielimu.
4. Ombea afya za waalimu, familia zao na wanafunzi kuwa nzuri na
mahusiano mema kiutendaji.
5. Ombea upanuzi na uboreshwaji wa miundombunu ya vyuo vyote
6. Omba Mungu kuinua wadau watakaosimama na vyuo hivyo.

10
Siku ya 18 Ombea miradi ya Ujenzi (Mithali 16:1-3; 28:20a)
03/02/2022 1. Ujenzi wa Chekechea, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya
Alhamisi Kati na Vya Juu ngazi za Kanisa, Sehemu, Jimbo, Idara na Makao
Makuu ya TAG.
2. Ujenzi wa vyuo vya Elimu
3. Ujenzi wa Makanisa
4. Ujenzi wa vyuo vya kupanda makanisa
5. Ujenzi wa nyumba za Watumishi
6. Ujenzi wa Majengo ya Miradi na Uwekezaji mbalimbali
Siku ya 19 Omba Mungu aliepushe Kanisa na Taifa kutoka kwenye Majanga
04/02/2022 Mbalimbali na Kulihifadhi Taifa letu (2Falm 20:1-6; Isaya 6:16)
Ijumaa 1. Omba kukataa ukame, Wadudu waaribifu na magonjwa ya Mazao.
2. Omba kukemea roho za Ajali, mauti, Magonjwa ya milipuko, na
majanga mbalimbali viondoke katika Taifa letu
3. Ombea Wazee na Waathirika wa Magonjwa na Majanga
mbalimbali uponyaji na Neema ya Mungu ya kuwawezesha
kusonga mbele.
4. Ombea Wanafunzi ngazi zote kutunzwa na Mungu na kufanya
vizuri kitaaluma na kimaadili kemea roho zinazowaharibu.
5. Ombea wafanyakazi Waajiriwa, Wafanyabiashara, Wajasiliamali
na wasaidizi wa kazi za nyumbani wote Mungu awatunze na
awawezeshe kuwa salama.
Siku ya 20 Ombea Umisheni, kanisa katika Bara la Afrika na Dunia Kwa
05/02/2022 Ujumla (Matendo 1:8; Mathayo 28:19)
Jumamosi 1. Ombea Kazi ya Kupeleka Wamishenari 200 Nje ya Nchi na
Upandaji wa Makanisa 300. Mungu ainue Wamishenari hao
miongoni mwetu na kuliwezesha kanisa kutoa kwa ajili ya umisheni
2. Ombea Uongozi wa AAGA – chini ya Askofu Dr. B. Mtokambali.
3. Ombea mavuno ya Africa kwa Yesu na Uamsho Mkubwa
4. Omba Mungu Injili ipenye maeneo magumu Afrika:
- Libya, Tunisia, Algeria, Morocco, Sahara Magharibi, Mauritania,
Nchi za Pembe ya Africa, wamishenari walioko Nchi za Nje na
Nchi wanazofikia.

11
5. Ombea Ukuaji wa kanisa Katika Bara la Afrika na Duniani Kote.
Siku ya 21 Shukrani na Kujiweka Wakfu kwa Bwana: (2Kor 4:15; 9:11;
06/02/2022 Kol 3:15)
Jumapili 1. Kumshukuru Mungu kutuwesha kuomba na kuwa amejibu maombi
yetu Zaidi ya tulivyoomba
2. Tumpe Sifa na Utukufu kwa mambo makubwa ambayo anakwenda
kuitendea TAG katika Mwaka Huu 2022.
3. Tujiweke wakfu kwa Bwana na Kuwa tayari kutumiwa na Mungu
maneo yote.
4. Mungu atupe Neema ya Kuweza Kupokea Miujiza yetu 2022 na
Kuyaishi majibu ya Maombi yetu na kuyakubali mapenzi yake
makamilifu.

12

You might also like