You are on page 1of 25

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO TANZANIA

IDARA YA HUDUMA ZA FAMILIA

JUMA LA MAOMBI LA UMOJA WA FAMILIA


Septemba 04 – 11, 2021

Mada: NAO WATAKUWA MWILI MMOJA

Fungu Kuu: Mwanzo 2:24

Wimbo: 184

Limeandaliwa na Idara ya Huduma za Familia (STU & NTUC)


Ndugu wapendwa salaam katika Kristo Yesu
Tunaishi kazima zama za mabadiliko makubwa katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu.
Kadiri wakati unavyopita mambo mengi mapya yanatokea yakihanikizwa na kupanuka kwa
matumizi ya teknolojia. Mahusiano ya kifamilia ni moja ya Nyanja zinazoendelea kuathiririka
siku hadi siku. Ni mpango wa Mungu tangu mwanzo kwamba familia iwe kitu kimoja na ndivyo
ilivyokuwa. Adui wa Mungu na war oho za watu amekuwa chanzo cha kuvunja umoja huo wa
familia kinyume na mpango wa Mungu. Ndoa za wake wengi na waume wengi zimeibuka, ndoa
za watu wa jinsia moja zinapigiwa chapuo, vijana wa kike na wa kiume kuanza mahusiano kabla
ya ndoa zinazidi kushamiri, pamoja na mengi yanayofanana nahayo. Familia nyingi zinabubujika
machozi kwa uchungu wa talaka na kutelekezana. Watoto wamekuwa ni wahanga wa kuvunjika
kwa umoja katika familia. Wanawake na wanaume wanalia na kujilaumu kwa nini waliingia
Katika ndoa.
Lakini kuna tumaini. Tumaini pekee la urejeshwaji wa familia zilizosambaratika ni Katika Neno
la Mungu. Masomo ya Juma la Umoja wa Familia yanaweza kuwa sehemu ya uponyaji na faraja
kwa familia zote katika kanisa la Mungu na nje ya kanisa. Tunakuwalika kuhudhuria masomo
haya Yenye kugusa maeneo mengi ya maisha ya familia na umuhimu wake Katika kujenga na
kutumisha umoja wa familia. Mambo yaliyogusiwa Katika somo hili ni pamoja kusudi la Mungu
la kuwafanya mume na mke kuwa mwili mmoja, nafasi ya mume, mke na watoto katika umoja
wa familia, nafasi ya uchumi na Mawasiliano katika umoja wa familia, na hatimaye nafasi ya
Maombi katika umoja wa familia. Masomo yataanza Sabato ya Septemba 04 hadi Sabato ya
Septemba 11, 2021, ambayo itakuwa ni siku rasmi ya Maombi ya Umoja wa Familia katika
Kanisa la Waadventista wa sabato Ulimwenguni.
Waandaaji wa masomo haya ni wakurugenzi wa Idara ya Huduma za Familia Kanisa la
Waadventista wa Sabato Tanzania (NTUC & STU), wakishirikiana na baadhi ya Wachungaji
wastaafu. Waratibu ni Mch. Davis Fue, Mkurugenzi wa Huduma za Familia (NTUC) na Mch.
Herbert I. Nziku, Mkurugenzi wa Huduma za Familia (STU).

Mungu akubariki unaposhiriki Baraka za Juma la Umoja wa Familia.

Somo la Kwanza
(Sabato: Septemba 04, 2021)

NAO WATAKUWA MWILI MMOJA (Sehemu ya Kwanza)

Umoja katika Uumbaji

Marko 10:8
Na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.”
Mungu alipomuumba mtu kwa mfano wake alimwita jina Adamu yaani jina linalosadifu umoja:
Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba,
mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Ni dhahiri kwamba mwanamke na mwanaume
walipoumbwa walikuwa “mtu” na wala si watu. Yaani walikuwa mmoja.

Mwanzo 5:2
“Mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile
walipoumbwa.” Hata baada ya dhambi fungu hili linarejea ukweli ule ule kuwa jina lao lilikuwa
umoja yaani Adamu. Ndio sababu muunganiko wa wanandoa tunauelewa kiurahisi sasa maana
hurejea jina lao walipoumbwa mume na mke ambao waliitwa “mtu”/ “Adamu” yaani mmoja.
Hawawi wawili tena bali huwa mwili mmoja.
Swali la msingi sana la kujiuliza ni kwamba, Je hawa wawili yaani Mume na mke wanapoishi
katika ndoa ambao sasa wanaitwa mmoja, pale Mungu anapowapa watoto wanakuwa bado mwili
mmoja na watoto wao au sasa mwili umeanza kutengana?

Umoja Ndani ya Familia


Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu alikusudia tangu uumbaji ya kwamba mume na mke wawe
mwili mmoja na vivyo hivyo watoto wawe mwili mmoja na wazazi wao. Ni wazi kwamba hata
kibaiolojia uhusiano kati ya mtoto na wazazi ni mkubwa sana, mtoto ameumbwa kutoka kwa huu
mwili mmoja yaani baba na mama, hivyo yeye ni mwili mmoja na wazazi wake.

1Wakorintho 12:14
“Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.” Biblia inapozungumzia umuhimu wa kila
karama ndani ya kanisa, hufundisha jinsi karama zinavyotegemeana katika kulijenga kanisa.
Kadhalika kila mwanafamilia ana sehemu muhimu sana katika kuimarisha familia katika nyanja
zote.

Faida ya kuhamasisha mchango chanya wa kila mwanafamilia katika kulinda umoja wa familia
ambayo ni mwili mmoja umeelezwa kwa uzito katika Neno la Mungu. 1Wakotintho 12:25-26
“25 ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. 26 Na
kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo
vyote hufurahi pamoja nacho.”

Je nimeshika Tofali kujenga au Nyundo kubomoa?


Hata hivyo ni muhimu kuweka katika ufahamu wetu changamoto kubwa tuliyo nayo kanisani leo.
Tunalo kundi kubwa la watoto wa umri tofauti ambao kwakweli hawajui wanawezaje
kuhatarisha umoja wa familia na wanawezaje kuhamasisha na kuwa na mchango chanya katika
kuboresha umoja wa familia.
Lipo fundisho kubwa kutoka katika Biblia linaloonyesha jinsi watoto wanavyoweza kufanya
umoja wa mahusiano katika familia uwe imara au uzorote.

Waamuzi 11:1-2
“Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke
kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha. 2 Mkewe huyo Gileadi akamzalia wana; na hao wana wa
mkewe hapo walipokuwa wamekua wakubwa wakamtoa Yeftha, na kumwambia, Wewe
hutarithi katika nyumba ya babaetu; kwa sababu wewe u mwana wa mwanamke mwingine.”
Mambo ya msingi ya kujifunza katika mafungu haya: Hapa tunaangalia sehemu ya watoto katika
kulinda umoja wa familia. Tunakutana na watoto watatu katika kisa hiki; mama yake Yeftha
ambaye hakutajwa kwa jina, Gileadi, na Yeftha.

Mama yake YEFTHA akiwa binti (mtoto) wa familia ya wazazi wake na ndugu zake wengine
alichagua kuwa kahaba. Kwa vyovyote hakuna mzazi anayefurahia mwanae kuwa kahaba, lakini
pia hakuna mtoto anayefurahia kujitambulisha kwa wenzake kuwa kahaba fulani ni ndugu yake.
Ni dhahiri kwamba familia ya binti huyu iliingia katika mgogoro na taratibu amani ilitoweka.
Wazazi waliokuwa na njozi na matazamio makubwa kwa binti yao walikatishwa tamaa na
uchaguzi mbaya wa mtoto wao. Gharama kubwa walizolipa kumhudumia na kuwekeza kwake
zilifanya shughuli fulani za kifamilia kuahirishwa lakini zote zilikuwa zimepotea. Hutuachi pia
kufikiri uhalisia kuwa huenda palikuwa na hali ya kulaumiana kati ya wazazi huenda mama
alishutumiwa kwa kutomlea mtoto vizuri, tayari mwili huu (familia) haukuwa salama tena. Vipi
kuhusu aibu waliyoingia familia kwa ujumla, kila walikopita walisikia habari mbaya za
mwanafamilia mwenzao. Hata baada ya kazi waliporudi nyumbani kila mmoja alikuwa na la
kusema kuhusu maneno waliyoyasikia kutoka kwa majirani.
➢ Watoto walisikika wakisema; “dada anatuaibisha”
➢ Wazazi; “Jamani huyu mtoto anachotufanyia tunaweka wapi nyuso zetu”
Huyu hatofautiani kabisa na binti aliyekatisha masomo na kuamua kuwa kahaba lakini kama
ilivyo kawaida ya dhambi kwamba huzaa matunda, binti huyu anajikuta ni mjamzito. Sasa si
kwamba tu familia inapitia kipindi kigumu kwa ajili yake, hapa tena tayari ameisababishia
familia changamoto kubwa ya kubeba mzigo wa malezi.

Mtoto wa pili anayetajwa hapa ni Gileadi. Inaonekana kuwa wakati tu akiwa ni kijana hajaoa
bado, alianza tabia ya uzinzi. Huyu ni wa kabila la Manase, kwa hiyo ni Mwisrael huyu, kwa
sasa tungesema ni mtoto wa familia ya kisabato. Tabia hiyo inafikia hatua ya kukomaa mpaka
anazini na kahaba (Mama yake Yeftha). Matokeo yake anampa mimba huyu kahaba, na mtoto
Yeftha anazaliwa.

Hatuhitaji kuambiwa nini kilitokea baada ya hilo. Sisi wenyewe twaweza kueleza tena kwa
usahihi yale yaliyoipata familia ya Gileadi:
❖ Familia kudharauliwa na kusemwa vibaya kwamba mwanafamilia mwenzao amezaa
na kahaba aliyefahamika hapo mtaani kwao. Heshima ya familia haipo tena.
Kama mzaliwa wa kwanza kwenye familia yake Gileadi ameweka mfano mbaya sana kwa
wadogo zake wote. Kuna uwezekano mkubwa watoto waliofuata kuathiriwa na tabia ya kaka
kwa kuiga mwenendo wake mbaya na hatimaye familia ikawa na maisha yasiyomtukuza Mungu.
Tayari umoja katika malengo ndani ya familia umeathiriwa.
❖ Njozi nzuri alizokuwa nazo Gileadi zimeingia katika hatari kubwa. Aliwaza kuwa
na mke mzuri mwadilifu katika maisha yake ili amtukuze Mungu. Sasa mambo
yamebadilika, hawezi kumuoa yule kahaba maana akili inamwambia hafai kuwa
mke wake.
❖ Analazimika kuoa mwanamke mwingine lakini matokeo yake mtoto wake wa
kwanza yaani Yeftha anakosa nafasi nyumbani kwa baba yake na anafukuzwa
maana yeye ni mtoto wa kahaba.
❖ Mahusiano miongoni mwa watoto wake hayapo sawa tena, anawezaje kuwa na
furaha na mke na watoto wasiompenda mtoto wake wa kwanza. Ingawa Yeftha ni
mtoto wa kwanza ananyimwa urithi stahiki.

Kwa hiyo si tu kwamba mahusiano yake kama mtoto na wazazi pamoja na ndugu zake
yameathiriwa, lakini pia mustakabali wa maisha ya familia yake akiwa kama baba yameathirika
kwa sehemu kubwa. Umoja wa familia haupo tena.
Kwa kila mwanafamilia kumbuka kuwa si jambo jema kufanya maamuzi ya kibinafsi bila
kuwafikiria wengine. Kama watoto tunapofikiri kufanya uchaguzi wowote hebu tuwafikirie
wanafamilia wengine, tuufikirie umoja wa familia zetu, tuyape kipaumbele mahusiano chanya
ndani ya familia zetu.

Kila uchaguzi unaofanywa na mwanafamilia hautaishia tu kuleta athari kwa aliyefanya uchaguzi
bali pia utaathiri wanafamilia wengine. Sisi wanafamilia ni mwili mmoja,pamoja kwa chaguzi
mbaya tunaanguka lakini pia pamoja kwa chaguzi sahihi tunasimama na kusonga mbele.
Sikia ombi la Mwokozi kwa familia zote: Yohana 17:20-23 “20 Wala si hao tu ninaowaombea;
lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21 Wote wawe na umoja; kama wewe,
Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate
kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili
wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.

Mambo ya Kuombea:
1. Mungu atuwezeshe kujenga mahusiano chanya ndani ya familia zetu ili tuweze
kudumisha umoja wa familia kwa utukufu wa Mungu
2. Mungu alete uponyaji kwa wanafamilia kwa athari zinazotokana na uhusiano uliovunjika
Katika familia.

Somo la Pili
(Jumapili: Septemba 05, 2021)
NAO WATAKUWA MWILI MMOJA (Sehemu ya Pili)
(Na: Mch. Kenani A. Mwasomola, Mchungaji Mstaafu – Kibaha)

Fungu la Maandiko Matakatifu: “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake
naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja” (Mwanzo 2:24).

“Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako” (Zaburi
45:10).

Utangulizi: Familia ni kitu cha muhimu sana katika taifa na katika kanisa vile vile. Ukweli ni
kwamba kanisa huanzia nyumbani katika familia. kazi ya utume msingi wake ni familia (neuclea
family). Familia kadhaa zikiungana pamoja zinaunda kanisa mahalia. Familia inapasa
kushikamana pamoja na tena kwa umuhimu mno kushikama na Mungu hata kama dunia yote
itamuasi Mungu. Na ifike mahali baba wa familia au kiongozi yeyote wa familia aseme kama
Joshua alivyosema, “15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo
mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au
kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba
yangu tutamtumikia Bwana” (Joshua 24:15). Katika somo tutaona baadhi ya mambo muhimu
kwa familia katika kazi ya utume.

Baba na mama kukaa pamoja


Katika Mwanzo 2:24, tunasoma, “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake
naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja” (Mwanzo 2:24). Lakini mwanamke
yeye anaambiwa, “Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, uwasahau watu wako na nyumba ya
baba yako” (Zaburi 45:10).

Ili kuwepo na umoja kamili kati ya mume na mke mwanaume anaagizwa kuacha baba na mama
yake na mwanamuke anaagizwa kusahau watu wa nyumbani kwake. Hapa maana yake ni nini?
Kwanza kabisa, “maneno ya fungu hili hayawezi kufikiriwa kuwa ni maneno ya kiunabii
yaliyosemwa na Adamu, bali ni maneno yaliyosemwa na Mungu mwenyewe. Ni sehemu ya
agizo la Mungu wakati wa sherehe za ndoa (Mathayo 19:4,5; MB 99).

Maneno haya hueleza kwa undani sana umoja wa kimwili na kiroho kati ya manaume na
mwanamuke na kuiinua juu ndoa ya mume na mke mmoja mbele ya ulimwengu kama ndiyo
iliyoanzishwa na Mungu. Haya maneno hayapendekezi kuacha waiibu wako kwa ndugu zako wa
damu na heshima kwa baba na mama. Lakini kimsingi hurejeshwa kwa wajibu kuwa “upendo wa
mume kwa mkewe uwe ndio kwanza na wajibu wake kwanza kwake. Upendo wake kwa mkewe
unapaswa kupita lakini sio kuchukua nafasi kwa upendo hasa kwa wazazi wake” (SDABC Vol. 1
ukurasa wa 226 – 227).

Lakini binti (mwanamke) anaonywa, “ Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, uwasahau watu
wako na nyumba ya baba yako” (Zaburi 45:10). Maana yake hapa ni nini? Habari ni hii,
“Usitamani sana nyumbani kwenu (kwa baba yako), usilinganishe mazingira mapya na yale ya
zamani. Usijaribu kuleta mawazo mageni katika mazingira yako ,mapya. Usilinganishe ya
zamani na mapya. Vunja miunganiko yako yote ya zamani ambayo yaweza kusimama kati yako
na mumeo. Shikamana na mume wako kikamilifu. Mfano mzuri tuanupata katika kisa cha Ruth
na Naomi (Ruth 1:16 – 18).

Mume na mke wanaokaa pamoja kwa umoja na kushikamana; upendo wa Kristo ukitawala ndani
ya mioyo yao, ni hubiri tosha ambalo haliwezi kupingwa na mtu yeyote. Huo ni ushuhuda tosha
kwamba Mungu aliyeviumba vitu vyote na ambaye ni mwanzilishi wa ndoa kati ya mume na
mke ambao wamekuwa hali hiyo tangu kuzaliwa kwao, yupo na ndiye kiongozi na mwokozi wa
familia inayomwamini na kujitoa kwake kikamilifu. Kupitia familia kama hiyo watu wengi na
familia nyingi zinaweza kumuona Mungu na kumwamini. Na ikumbukwe kwamba matendo
huhubiri zaidio ya maneno. Maisha ya familia ni mahubiri makubwa mno kwa watu wote
wanaoizunguka, kwa wema au kwa ubaya familia inamtangaza Mungu.

Utengano katika familia sio mpango wa Mungu

Kabla ya mapinduzi ya viwanda (Industrial Revolution), familia ilikaa pamoja na kufanya kazi
kwa pamoja na hasa za shamba au uvuvi. Hata kabla ya dhambi kuingia katika dunia hii, Adamu
na Hawa walikaa pamoja na kufanya kazi pamoja katika bustani ya Edeni na hata walipofukuzwa
kutoka katika bustani ya Edeni bado walikaa pamoja. Wakiwa katika bustani ya Edeni, agizo la
malaika kwao lilikuwa: “malaika walimwonya Hawa kujihadhari kwa kutokujitenga kutoka kwa
mumewe wakati wa kufanya kazi zao za kila siku katika bustani; akiwa pamoja naye angekuwa
na majaribu kidogo sana kuliko kama angekuwa peke yake. Akiwa (Hawa) amebobea katika kazi
yake yenye kuvutia, bila ya kujua alijikuta ametengwa kutoka kwa mume wake” (PP, 54).

Akajaribiwa na kuanguka katika dhambi. Leo hii ndoa nyingi sana katika zama hizi za
mapinduzi ya viwanda (Industrial Revolution), zimeingia shida kubwa sana. Mume na mke
hutengana katika harakati za kutafuta ajira ili kuinua kipato cha familia. Utakuta mwanamume
mfano yuko Lindi kijijini ni mwalimu wa shule ya msingi na mwanamke yuko Mwisenge Majita
Musoma akifanya kazi ya uuguzi (Nurse) kwenye kazahanati ka mtu binafsi.akipata mshahara
wa Tshs 250,000.00 kwa mwezi. Mwanaume naye huko Lindi anapata mshahara wa Tshs
550,000.00 kwa mwezi. Jumla ya pato lao kwa mwezi ni shilingi laki nane. Yaani laki nane
ndiyo inafanya ndoa yao iingie matatani. Hivi ninyi watu, kipi bora, kuimarisha ndoa yenu na
kuwalea watoto wenu kwa pamoja katika njia ya Bwana Mungu au hizo laki nane? Ukweli ni
kwamba hata kama mishahara yenu yote kwa pamoja ingekuwa ni Tshs 1,000,000,000.00
(trilioni moja) au zaidi, bado ndoa yenu ni ya thamani kuliko fedha hizo zote.

Baba na mama ambao ajira imewatenganisha, kaeni pamoja na kutafakari hali ya mahusiano ya
ndoa yenu na hali ya watoto wenu. Si vema kabisa mkutane mara mbili kwa mwaka wakati wa
likizo. Huyu achukue likizo mwezi huu na mwingine mwezi mwingine na ndipo eti mkae pamoja
kwa siku 56 tu na siku 304 kila mmoja anakaa kivyake.

Mnapaswa kuwalea watoto wenu kwa pamoja. Ni vema mmoja wenu ahamie mahali pale alipo
mwenzake. Kupata fedha sio lazima wote mfanye kazi za kuajiriwa.
Mwisho lakini sio kwa umuhimu:

Maagizo ya Mungu kwa wana ndoa wote yaani mwanamume na mwanamke ni haya na ni vema
kuyafanyia kazi: “24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye
ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja” (Mwanzo 2:24). Tena “10 Sikia, binti,
utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako” (Zaburi 45:10).
Maagizo hayo yakifuatwa, utume utafaulu sana katika familia na nje ya familia.

Tafakari:

Je, kuna mbinu ya yoyote mbadala ya kuweza kuimarisha ndoa na pia kuwalea watoto katika
Bwana wakati baba na mama hawakai pamoja kwa miezi kumi kila mwaka? Je baba au mama
anaweza kuwa mjumbe wa Mungu na kuaminiwa na watu huko aliko akiwa ametengana na
mwenzi wake? Je kunaweza kuwa na madhara gani kwa wanandoa wakiwa wametenganishwa na
ajira na kuishi mbali mno kutoka kwa mwenzake? Je, watoto wanaweza kupata madhara gani
kutokana na wazazi kutokukaa pamoja? Je wanandoa wakiwa wametengana waweza kuwa
mawakala wa Mungu ipasavyo katika kazi ya utume na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii? Je
sasa ni nini kifanyike ili kuokoa adhari hizo zilizo ainishwa katika kujibu maswali hayo hapo juu?

Mambo ya Kuombea:
1. Mungu awarejeshe wanandoa waliotengana au kutenganishwa kwa sababu mbali mbali.
2. Mungu aponye majeraha ya ndoa na familia zinazoathirika kwa sababu ya utengano
miongoni mwao.

Somo la Tatu
(Jumatatu: Septemba 06, 2021)

NAFASI YA MUME KATIKA UMOJA WA FAMILIA


(Na: Bahati Kaitira Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Familia – NGBF)

FUNGU KUU
“Kwa maana Mume ni kichwa cha Mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa, naye ni
Mwokozi wa mwili” Waefeso 5:23

VIDOKEZO MUHIMU
Katika juma la uumbaji tunaliona tukio kubwa la Mungu kumuumba mwanadamu tena kwa
mfano na kwa sura yake, kisha kumpatia majukumu yaliyothibitisha kuwa mwanadamu ndiye
kiumbe cha thamani kuliko viumbe vyote alivyoviumba kwa kumpatia jukumu la kuvitawala. Pia
tunamuona Mungu akiwa muasisi wa familia ya kwanza ambayo aliibariki katika baraka za uzao
na pia kuikasimishia majukumu ya utawala kwa viumbe wengine aliowaumba Mungu.
“Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi.
na kuitiisha, mkatawale Samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbe
chenye uhai kiendacho juu ya nchi” Mwanzo 1:28.
Tunapotafakari nafasi ya Mume katika ndoa, tunamtafakari Mume ambaye amekamilishwa na
Mwanamke ambapo wote wawili ndio walioanzisha familia ya kwanza. Imeandikwa katika
kitabu cha Mwanzo 2:24 “kwa sababu hiyo, Mume atamwacha baba yake na mama yake, naye
ataambatana na Mkewe, nao watakuwa “MWILI MMOJA.”

Ukamilifu wa Mume ni matokeo ya muungano kati yake na Mwanamke kufanya mwili mmoja.
Mtume Paulo anaweka wazi mtazamo huu katika 1Kor 11:11 akisema “walakini si Mwanamke
pasipo Mume, na Mume pasipo Mwanamke katika BWANA, maana kama Mwanamke alitoka
katika Mume, vile vile Mume naye huzaliwa na Mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa
Mungu.”. Kwa jinsi hii umoja wa familia umeonekana kuanza kupitia muunganiko wa uumbaji
wa mume na mke.

Ikiwa Mke na Mume ni mwili mmoja, muunganiko ambao ni kazi ya Mungu mwenyewe, na
ikiwa Mume ni kichwa cha mke, ni muhimu kutambua kwamba uhusiano wao kama mke na
mume hauwezi kusimama pasipo Mungu kuwa mhimili mkuu wa Ndoa hiyo.
Hii ndiyo sababu hapo awali tulieweka wazi kabisa kwamba Ndoa inajengwa katika msingi wa
imani waliyonayo mke na Mume juu ya Mungu ambaye ndiye mwenye dhamana ya
kuwaunganisha katika agano la maisha yao yote linalowafanya kuwa mwili mmoja.

Ni ukweli usiopingika kwamba, Mume ndiye mwenye dhamana ya kujenga na kutunza uhusiano
kati ya wanandoa na Mungu. Mume ndiye aliyepokea maagizo ya Mungu kabla ya kuumbwa
kwaMwanamke.

Ni katika hali hii tunatambua kwamba hali ya kiroho ya familia inapokuwa imeporomoka,
anayewajibika kwanza kujibu mbele za Mungu ni Mume. Mungu mwenyewe alidhihirisha haya
katika kitabu cha mwanzo 3:9 ambapo tunaona Mungu akimhoji Mume kwanza juu ya anguko
lililotokea. “Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?

Nafasi ya mume katika umoja wa Familia, inaimarishwa na kuwezeshwa na kiwango ambacho


mume amejiunganisha na Kristo ambaye ndiye Kichwa cha Kanisa. Hivyo Mume ana wajibu wa
kujiunganisha na Kristo wakati wote, na katika uhusiano huo Mungu humjengea Mume nguvu na
heshima ambayo humvuta Mwanamke kusimama katika nafasi yake kama mke na hivyo
kuunganishwa na Mume katika familia bora yenye umoja wa kweli. Katika hali hii Baraka
zilizoachiliwa na Mungu kupitia mume huleta umoja wa familia.

WAJIBU WA MUME KATIKA UMOJA WA FAMILIA


1. Baba ni Kuhani wa familia.
Ni wajibu wa baba kutambua kuwa yeye kama kichwa cha familia ndiye KUHANI wa familia
yake akimwakilisha Kuhani Mkuu ambaye ni Mungu. Imempasa mume kuiongoza familia yake
katika kumcha Mungu kwa kufuata maelekezo ambayo Kuhani Mkuu ameelekeza. Mume
ahakikishe kanisa la nyumbani li HAI na IBADA zinafanyika kwa ubora na kwa Utukufu wa
Mungu kama inavyoelezwa katika kitabu cha Kutayarisha njia Sehemu ya kwanza.
“Kadiri mfanyavyo kwa uaminifu wajibu wenu nyumbani baba kama kuhani wa
nyumbani, mama kama mmishenari nyumbani mwazidisha njia za kufanya mema nje ya
nyumba hiyo. Kadiri mnavyotumia vizuri uwezo wenu wenyewe, ndivyo mnavyofanywa
kufaa zaidi kutumika kanisani na jirani. Kwa kufungamana na watoto wenu na
kuwafungamanisha na Mungu, baba na mama na watoto pia huwa watenda Kazi pamoja
na Mungu”. (Kutayarisha njia Uk 163)

2. Kutengeneza maono ya familia ambayo Mungu ameikusudia


Ikiwa Mume ni kichwa cha familia, ni dhahiri kwamba ndiye mwenye wajibu wa kutunza macho
ya kiroho ya familia. Kwa sababu hii, mume ndiye mwenye wajibu wa kutengeza maono ya
familia kwa namna Mungu apendavyo. Tunafahamu kwamba maono ni matokeo ya ufunuo wa
Roho Mtakatifu, kwa jinsi hii ni wajibu wa mume kujiunganisha na Kristo ambaye ndiye
atakayempa maono yaliyo sawa na makusudi ya Mungu kwa familia yake kupitia Roho
Mtakatifu.
Imeandikwa katika mithali 29:18 “…Pasipo Maono watu huacha kujizuia…” maono yatokayo
kwa Mungu ndiyo yanayomwekea msimamo thabiti Mume kuhusiana na maisha anayopaswa
kuishi ili kutimiza kusudi la Mungu. Pasipo kuwa na maono ni vigumu kwa Mume kujizuia na ni
rahisi kwa Mume kuchukuliwa na kila aina ya upepo utakaomletea uharibifu yeye na nyumba
yake.

3. Kuumba na kukuza Imani katika Familia


Ni dhahiri kwamba Mume ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha masikio ya mwili yanasikia
sauti ya Mungu hivyo kuumba na kukuza imani kwa Mungu ndani ya familia. Adamu ndiye
aliyepokea maagizo ya kwanza kutoka kwa Mungu, hali hii bado haijabadilika na bado Mungu
anamhesabu Mume kuwa ndiye mwenye dhamana ya kusikia na kutunza maagizo ya Mungu
ndani ya familia ili kuleta Umoja thabiti wa famila yake. Pia baba wa familia anapaswa
kuwapenda, kuwajali wana familia na kuthamini kazi wanazozifanya kwa kuwapongeza
wanapofanya mambo mazuri. Imeandikwa katika 1Sam 15:22 “Kusikia ni bora kuliko mafuta ya
beberu.”

Mungu anathamini zaidi kusikia kuliko sadaka ya namna yeyote tunayomtolea kwa kuwa ni
katika kusikia ambapo tunapata kutambua Mapenzi ya Mungu katika maisha yetu na hivyo
kutembea sawasawa na kusudi la Mungu yaliyojengwa katika Umoja wa familia.
Baraka zote zinayoambatana na familia kutokana na maisha ya baba, zimefungwa katika bidii ya
kusikia, kutunza na kufanya maagizo ya Mungu.
4. Kutambua na kutunza uwepo wa Mungu katika usafi wa roho na mwili ndani ya familia.
Hisia ya kunusa hutusaidia kutambua uwepo wa kitu fulani katika mazingira tuliyopo. Wanyama
kama Mbwa na Panya ambao kwa asili wana uwezo mkubwa wa kunusa hutumika kutambua
uwepo wa vitu kama madawa ya kulevya na vitu vingine hatari katika maeneo nyeti mfano
viwanja vya ndege.
Ni jukumu la Mume kutambua na kutunza uwepo wa Mungu katika familia kwa ujumla. Mume
akijiunganisha na Kristo anapata kutambua utulivu na amani inayoambatana na uwepo wa
Mungu katika familia yake.
Tunafahamu kwamba Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na Roho wa Mungu anakaa ndani
yetu. Roho wa Mungu akikaa ndani ya Mume humletea utulivu na amani inayoambatana na
uwepo wa Mungu ambayo humuongoza yeye kufanya maamuzi yanayompendeza Mungu
akizingatia usafi wa ndoa na usafi wa tabia katika familia yake na hivyo kuifanya familia kuwa
na harufu nzuri katika jamii na kanisa kwa ujumla ambapo itawavuta wanafamilia na wanajamii
kumuona MUNGU wa kweli na kumtukuza katika Maisha yao.

“Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,
mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa
thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”. 1korintho 6:19-20

5. Kudhihirisha kwa Baraka za Mungu kwa familia


Ni kweli kwamba Mungu huachilia Baraka ya hali ya juu sana kwa familia kupitia maisha ya
Mume lakini ni muhimu kutambua kwamba uwezekano wa kuzifanya Baraka hizi zidhihirike
katika maisha ya wakati baba akiwa kielelezo bora katika matendo yaletayo baraka hizo.
Utakuwa mfano hai ikiwa baba anaiongoza familia katika kuvirudisha VITAKATIFU VYA
BWANA (Zaka na Sadaka) kwa vitendo kwa moyo wa Unyenyekevu tena wa kupenda.
Kushiriki Ibada zote za kanisa kama vile ibada ya jumatano, kufungua Sabato, Ibada ya Sabato,
kufunga Sabato, majuma mbalimbali ya uamsho ama semina, pamoja na Makambi kwa wakati
na kwa kujali sana huku vikiwa vimepewa kipaumbele na uthamani katika ubora wake.
Kwa kufanya hivyo, baba atakuwa amesababisha umoja wa familia kuwa imara siku zote kwa
utukufu wa MUNGU na kumfanya Mungu ainuliwe kupitia familia yake.

“Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia
hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na
kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la” Malaki 3:10

HITIMISHO
Ni hakika na kweli kwamba, Pamoja na Mungu Hakuna Kizuizi, kwani Tunayaweza Yote Katika
Yeye Atutiaye Nguvu. Hivyo ikiwa mume atawajibika kwa ubora chini ya Ustawi na Uongozi
wa Amiri Jeshi Mkuu wa Mbinguni ambaye ni Mungu yetu, ataweza kuwa mchango na mfereji
wa kweli katika kuleta Umoja wa Familia na kuifanya familia kuangaza kwa ubora katika
kuwaleta watu kwa BWANA ili wapata kuuruthi ufalme wa Mbinguni.
Mambo ya Kuombea:
1. Tuwaombee wanaume watambue nafasi na wajibu wao Katika kujenga na kudumisha umoja
wa familia
2. Mungu awape wanaume upendo wa agape ili wawapende wake zao kama Kristo alivyolipenda
kanisa hata akajitoa kwa ajili yake.

Somo la Nne
(Jumanne: Septemba 07, 2021)

NAFASI YA MKE KATIKA UMOJA WA FAMILIA


(Na: Mch. Willy J. Makoba – Mtaa wa Ukara, MC)
Mke ni nani hasa?
Mke ni mwanadamu wa jinsia ya kike aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu,ambaye kwa
hiyari yake mwenyewe ameamua kuingia kwenye uhusiano wa kudumu na mtakatifu wa ndoa
yaani umoja wa maisha na mtu wa jinsia ya tofauti na yake. Mke ni rafiki kipenzi,msiri wa
karibu,mwenzi na msaidiziwa kufanana na mumewe.Ni mwalimu wa kwanza,malkia wa
nyumba na ndiye aliye mama yao wote walio hai.Kama mwenzi na msaidizi wa mume
wake,malkia wa nyumba na mama wa watoto,mke ni kiungo muhimu sana cha umoja wa
familia. Mwanzo.2:21-25.

Wajibu wa mke katika umoja wa familia unadhihirika katika nyanja zifuatazo.

➢ Upendo,anawajibika katika umoja wa familia kwa kulinda hisia za upendo za mume wake
kwa kumfanya mumewe kuhisi amani timilifu moyoni mwake kwa kuwa naye na kujenga
umoja wa fikra na mawazo ya kina ya kimapenzi kati yao.Ili kuhakikisha umoja wa familia
unadumu mke,anawajibika kulikataa wazo la talaka lisipate nafasi akilini mwa mwenzi wake
kwa vitendo,kwa kuendelea kumtii mume wake bila kujaribiwa kupima upendo wa mume
wake kama unapungua au kuongezeka. Mke hatajiuliza swali je mume wangu ni mwenzi
sahihi? Bali kila siku yeye mwenyewe atafanya yote kwa msaadawa mbingu kuwa mwenzi
sahihi kwa mume wake.Umoja huu utawasaidia wenzi hawa kuelekea mbinguni.

➢ Mwenzi na msaidizi,mke anawajibika kuonyesha umoja kwa kutoa ushauri wake katika
shughuli mbalimbali za maendeleo ya familia yake kama vile shule watakayopelekwa
watoto,uanzishwaji wa miradi ya familia na mambo mengine yanayohusu familia yako kwa
ujumla.Kama mwenzi na msaidizi anawajibika katika umoja wa familia kwa kutoa
ushirikiano mkubwa utakao muwezesha mume wake kutimiza wajibu na majukumu ya kila
siku iwe ni katika kazi ya kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe, mkeo aonyeshe umoja kwa
kuisema vizuri kazi inayowapatia familia kipato, kumtia moyo mumewe zinapotokea
changamoto kazini na kumsaidia kufikia malengo ya juu ya shirika, kampuni iliyomwajiri au
mradi unaoendeshwa na familia.Aidha anawajibika katika umoja wa familia kwa kisimamia
vyema matumizi ya mali ya familia ili iendelee kuwa baraka kwa familia, kanisa na jamii.

➢ Malezi na kufundisha,kama mama na mwalimu nyumbani mke anawajibika katika umoja wa


familia kwa kuwafundisha watoto tabia bora ili watoto waweze kufaa katika maisha ya sasa
na ya baadae katika uzima wa milele.Akitambua kwamba ameunganishwa na watoto wake
kiroho na kihisia, mke na mama anawajibika katika umoja wa familia kwa kumnena vyema
baba kwa watoto.Kamwe hata ruhusu maneno hasi na yanayoonyesha tofauti zilizopo kati
yake na mume wake yatoke kinywani mwake, kwa kufanya hivyo atavuruga umoja wa familia
kwa kiwango cha kufisha “Mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mama. Katika kipindi ambacho
ni rahisi sana kuathiriwa na ushawisi na ambacho ni cha kukua haraka, elimu yake kwa
sehemu kubwa imo mikononi mwa mama yake. Mama napewa fursa ya kwanza ya
kufinyanga tabia kwa wema au ubaya” (Elimu ya kweli uk 222) “kila mwanamke aliye na
hekima ujenga nyumba yake; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe”
(mithali 14:1) “ nyumba hujengwa kwa hekima, na kwa ufahamu huthibitika” (mithali 24:3).
Malezi bora yatawafanya wototo kuwa watiifu kwa wazazi, jamii na kwa Mungu wao, hivyo
kudumisha umoja wa familia
➢ Kujenga mahusiano katika jamii, mke awajibike katika umoja wa familia kwa kuunganisha
ndugu, jamaa na marafiki wa pande zote. Atajifunza namna ya kuchukuliana nao ili ndugu,
jamaa na marafiki wa familia wasikie maneno na lugha ya mwili kutoka kwa mke na mama
ikisema “unakaribishwa na kukubalika katika familia hii”. Ustawi wa ndoa, familia, kanisa
na jamii kwa ujumla wake utegemea uwajibikaji wa mke katika kulinda umoja wa familia
yake. Kushindwa kutekeleza jukumu hili la kimkakati alilokabidhiwa na mbingu mke
atakuwa chanzo cha hasira, chuki, maumivu na hata mauaji kwa jamii nzima .

Kujenga umoja wa familia kupitia upishi,


Wajibu mzito wa mke katika kudumisha umoja wa familia upo katika namna ya kuchagua, kupika
na kuandaa chakula mezani. Mke na mama lazima ajiulize maswali haya, je chakula ninacho
chagua kitumiwe na familia yangu kitawaletea uzima na afya je mimi ni mpishi bora au bora
mpishi ?, na je familia yangu ina mda maalumu wa kula? Au kula ni tukio la ajali katika familia
yangu? Kushidwa kutimiza wajibu huu, mke atasambaratisha familia, watoto watakula kwa
majirani na baba atakula magengeni. Kwa kadri tatizo linapozidi kuwa kubwa laweza
kutenganisha familia kwa umilele kama Ellen G. White anavyosema “ watu wanaugua magonjwa
kwa ajili ya upishi mbaya ni maelfu na maelfu. Juu ya makabuli mengi yangeandikwa hivi
“amekufa kwa ajili ya upishi mbaya” “alikufa kwa ajili ya kutumia vibaya tumbo lake” ( Afya na
Rah auk 36) swali la kujiuliza, ni nani aliyemuua mtu huyu kwa chakula kilichopikwa vibaya? Ni
mke na mama asiyejali wajibu mzito wa kudumisha umoja katika familia yake! Hivyo basi nabii
anatoa ushauri huu. “ni wajibu mkuu wa wale wanaopika chakula kujifunza namna ya
kutengeneza chakula kinacholeta afya. Watu wengi ufa kwa ajili ya upishi mbaya. Inatakiwa
uangalifu na fikra kwa kutengeneza ugali au mkate mzuri. Chakula kilichopikwa vizuri huonesha
hal ya kiroho kwa kadri ambavyo wengi hawafahamu. Ni watu wachache tu ambao ni wapishi
kweli kweli. Wanawali wengine hufikiri ya kwamba upishi na kazi nyinginezo za nyumbani ni za
watumishi; na kwahiyo, wanawali wengi wanaolewa na kupata watoto wasijue wajibu unao
wapasa mabibi na akina mama. Upishi si elimu ya kudharauliwa, na ni kazi muhimu zaidi katika
maisha ya kila siku. Ni elimu inayompasa kila msichana kujifunza, na ingefundishwa kwa namna
inayoweza kuwasaidia watu wa aina zote. Kupika chakula vivi hivi, chenye manufaa, tena
kukitengeneza kiwe kitamu, kunataka ujuzi mwingi; lakini inawezekana. Inawapasa wapishi
wajue namna ya kukitengeneza chakula chepesi kwa njia rahisi na ya afya kwa jinsi
kilivyotengenezwa vivi hivi bila kuchanganywa na viungo vingi. Kila mwanamke ambaye ni
mzazi, naye hajui namna ya kupika chakula kinacholeta afya, ingempasa kujitahidi kujifunza
jambo hili ambalo ni la muhimu sana katika afya ya watu wote nyumbani. ( Afya na Rah auk 37)
katika jamii zote chakula kimekuwa kichocheo kikubwa cha umoja wa familia.

Kupeleka injili,
Wajibu wa mke katika umoja wa familia unadhihirika pia katika kutimiza agizo la Yesu. “ Basi,
enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi”
(mathayo 28:19). Mungu alikusudia familia iwe mazingira asili ya kutimiza agizo hilo. Lakini
bila umoja na ushirikiano wa mke katika familia haiwezekani kutimiza agizo hilo kwa upana
wake. Familia ya kikristo iakuwa na uwezo mkubwa wa kufundisha kuhusu Mungu mwenye
upendo na kuhusiana na wengine kwa upendo ( angalia yohana 13:35) “ kama watendakazi wa
Mungu, kazi yetu inapaswa ianzie majumbani mwetu. Hakuna umishionari wa kwanza katika
familia.
Maswali ya kujiuliza yenye changamoto
● Je mimi ni mwanamke ambaye ninakuwa mbaraka kwa familia yangu kila wakati?
● Ni mambo gani ambayo ninatakiwa kuyafanya ili mimi kama mwanamke niwe chanzo cha
kuleta umoja na baraka katika familia yangu na jamii inayo nizunguka
● Nimarekebisho gani ambayo ninatakiwa kuyafanya katika mahusiano yangu na watu wengine
katika kuleta umoja wa familia ya Yesu?
● Nimambo gani ambayo ninahitajika kuungama kwa Familia yangu, Jamii yangu, ambayo
sikuwafanyia vizuri na kusababisha mipasuko na kukusa umoja wa familia yangu?
Wito,
Mke na mama mkristo anayetawaliwa na Mungu, atajali na kuheshimu wajibu huu muhimu wa
kuleta umoja katika familia. kwa kulisoma neno la Mungu na kwa maombi mengi atafanya kila
lianalowezekana kujenga, kulinda na kudumisha umoja wa familia, kwa kufanya hivi wengi
watamuona kristo maishani mwake.

Mambo ya Kuombea:
1. Tuwaombee wake watambue nafasi na wajibu wao Katika kujenga na kudumisha umoja
wa familia
2. Mungu afafanye wake wawe watii na wenye heshima kwa waume za kama kanisa
linabvyomtii Kristo

Somo la Tano
(Jumatano: Septemba 08, 2021)

NAFASI YA WATOTO KATIKA UMOJA WA FAMILIA


(Mch. Adili Ndimangwa Mtaa wa Sabasaba, Mara Confrence)

FUNGU KUU: Kutoka 10:9 Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na
wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa
kumfanyia Bwana sikukuu.
UTANGULIZI
Familia iliyo bora ni ile ambayo watoto wanashirikishwa kujenga umoja wa familiya hiyo.
Familia yenye afya na raha ni familia yenye umoja wa familia. Familia hiyo ni ile iliyo tayari
kusafiri na watoto wao kwenye uzima wa milele. Yesu mwenyewe aliona jinsi ambavyo swala
la umoja lilivyo la muhimu na aliliombea YOHANA 17: 11. Swala la umoja kabila ya kuja
kanisani linaanzia kwenye kanisa la nyumbani.Watoto wetu wanapswa kuelekezwa kumjua
Mungu tangu kwenye kanisa la nyumbani. Yako mambo mengi yakizingatiwa vizuri katika
familia watoto wetu wanaweza kuboresha umoja wa familia. Katika somo hili tutaangalia
baadhi ya mambo hayo.

Watoto husaidia kujenga umoja wa familia neno la Mungu linapopewa nafasi ya


kwanza ndani ya familia KUMBUKUMBU LA TORATI 6:5-7 Mungu alianzisha familia
yeye mweyewe na alitoa maelekezo kwa wazazi kujifunza neno lake na kuliweka moyoni na
kuwafudisha watoto kwa bidii. Wazazi wakitumia mda wao vizuri wa kuwafundisha watoto
wao kumjua Mungu husaidia kujenga umoja wa familia kati ya Mungu, wazazi na watoto.
Ulimwengu leo unataka wazazi mfano wa Enoki. MWANZO 5:21-22 Enoki alipozaa mtoto
wake wa kwaza alimfundisha kumjua Mungu na alizidi kuendalea kuwa karibu zaidi na Mungu.
Aliona jinsi ambavyo mtoto wake alijenga matumaini yake kwa baba yake na yeye akazidisha
matumaini yake zaidi kwa Mungu. Enoki aliongeza upendo na heshima kwa Mungu zaidi hadi
akatwaliwa bila kuonja mauti.

Watoto ni mbaraka wa kuunganisha ndugu kuwa na umoja kama familia ya


Mungu. ZABURU 133:1 Upo wakati Mungu huunyoosha mkono wake juu yetu akitaka umoja
wa familia zetu. Watoto ni sehemu ya kuimarisha umoja wa familia. Kwa mjibu wa fungu hili
Mungu hupendezwa na familia ambazo hudumisha umoja. Umoja wa familia zetu ni ufunguo wa
kuwahubiri walioko nje ya kanisa la Mungu walioko ndani ya kanisa na kuwafanya wamjue
Mungu na kujiunga na kanisa lake la kweli.

Watoto ni kiungo cha upendo katika familia. Soma WARUMI 12:10. Na si salama
kuwachokoza watoto Waefeso 6:4 Kadri wazazi wanavyoonyesha upendo inasaidia hivyo hivyo
kwa watoto, na inasaidia kutengeneza maisha ya watoto. Maswali ya kujiuliza kwa wazazi Je!
Ninatenga mda wa kuonyesha upendo kwa watoto? Ni natenga mda wa kujadili nao pamoja nao
neno la Mungu? Tenga mda wa kujiuliza maswali hayo ikiwa jibu ni hapana fanya
matengenezo ya haraka, ikiwa jibu ni ndio endeleza upendo huo.

Watoto husaidia kuwa na mvuto wa pamoja kwa wazi ndani ya familia. Mahusiano
mazuri ya wazazi ni jambo la muhimu katika malezi ya watoto kwani watoto hujifunza kile
wazazi wanachofanya, wanachosema. Kama watoto wakilelewa kwenye familia zenye
mafarakano na kutoelewana baina ya wazazi tabia hiyo huwaathiri watoto, famili nzuri ni
familia yenye yenye amani. Ikumbukwe kuwa mtoto anapozaliwa hana lugha wala kitambulisho,
mtoto hujifunza kuongea kupitia kwa wazazi wake akijifunza tabia njema hataiacha hata baada
ya kuwaacha wazazi wake baada ya kuwa mtu mzima. Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia
impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Katika ulimwengu wa leo wanatakiwa
watoto watakaosimama kama Yoshua bada ya kukua na kuachana na wazazi watasema mimi na
nyumba yangu nitamtumikia Bwana. Soma Yoshua 24:15

Ili kuweza kuujenga umoja kati ya watoto na wazazi, watoto wanahitaji; mda wa
kuwafundishwa mambo ya Mungu, mda wa kula Pamoja nao, mda wa kuwasikiliza, mda wa
kucheza nao, mda wa kuomba nao, KUMBUKU LA TORATI 6:7 Omba nao chumbani kwao.
Baba au mama au mzazi mlezi aende kuomba nao. Na kuwaelekeza kuwa anayeweza kuwalinda
ni baba yetu wa mbinguni na wanapaswa kufundishwa kumheshimu Mungu wakati wote wakiwa,
kanisani, nyumbani, mjini,kijijini, shuleni, njani.

Watoto husaidia kujenga tabia ya Kristo ndani ya familia zetu. Kalamu ya uvuvio inasema
Mama White anaesema “Mungu anakusudia familia za Duniani ziwe mfano wa familia ya
Mbinguni. Nyumba za Kikristo zilizoanzishwa na kuendeshwa kulingana na mpango wa Mungu,
ni miongoni mwa njia za Mungu zifaazo kwa ajili ya kujenga tabia ya Kikristo na kwa ajili ya
kuendeleza kazi yake”. 6T 430 Katika familia zetu Yesu anatoa wito Luka 18:16 “Bali Yesu
akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie,
kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao”

WITO. Musa alipokwenda kwa Farao alisema Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na
wana wetu, na binti zetu, Na sisi tunapaswa kusema tunakwenda pamoja na watoto wetu katika
uzima wa milele. Ili tuweze kwenda pamoja nao ni lazima kuwe na umoja ndani ya familia zetu.
Watoto wanaweza kuwa mbaraka wa kujenga familia ikiwa wazazi tuko tayari kuwashirikisha.

Mambo ya Kuombea:

1. Mungu atupe utambuzi sisi wazazi na walezi ili tujue na kuthamini kwa vitendo nafasi ya
watoto Katika umoja wa familia.
2. Tuwaombee watoto dhidi ya mivuto mibaya inayowazunguka hasa Katika kizazi hiki cha
ukuaji wa sayansi na tekinolojia, ili wadumishe uadilifu kama viungo muhimu Katika umoja wa
familia.

Somo la Sita
(Alhamisi: Septemba 09, 2021)
NAFASI YA UCHUMI KATIKA UMOJA WA FAMILIA
Na: Mch. Sulemani Mipawa Mange (Mchungaji Mstaafu - SEC)
Uchumi ni kitu cha muhimu sana katika familia, kwani, kila familia, una mahitaji yake ya
muhimu, ambayo ni chakula, yaani, chakula ambacho mwili unahitaji au mlo kamili. Kitu cha
pili ni mavazi, yaani, mavazi mazuri na kwa idadi inayomstahili mtu. Kitu cha tatu ni makazi,
yaani, nyumba bora aliyojijengea mtu mwenyewe kwa ajili ya familia yake. Vitu hivyo,
vinahitajika na binadamu wote duniani, na kuvikosa, au kuvipata kwa kiasi kidogo, kunaweza
kuleta, taabu, maumivu, na hata kifo. Hivyo, familia lazima ishirikiane katika kukuza kipato ili
iweze kukidhi mahitaji yake ya lazima.
Baada ya uumbaji, Mungu alimpa binadamu kazi ya kulima na kutunza bustani ya Edeni (rejea
Mwanzo 2:18), ili binadamu aweze kuendelea kupata chakula toka kwenye bustani hiyo. Adamu
na Hawa walitakiwa kushirikiana katika kazi ya kuilima na kuitunza bustani, kwani, Hawa
alikuwa msaidizi wa Adamu (rejea Mwanzo 2:18). Usaidizi wa Hawa, ulikuwa katika mambo
yote, pamoja na hili la kuilima na kuitunza bustani, au kutafuta kipato kwa ajili ya familia yao.
Familia zina hali tofauti toka familia moja hadi nyingine, kwa upande wa uchumi. Hii inatokana
na familia moja kutofanya kazi kwa bidii, kuchagua aina ya kazi isiyoweza kuwapatia kipato
kikubwa, kutojua namna ya kufanya kazi ili wapate kipato kikubwa, uvivu kwa baadhi ya
wanafamilia na sababu nyinginezo. Watu wote tumepewa saa 24 kila siku. Matumizi mazuri wa
wakati, yanaweza kuifanya familia moja ipate kipato kikubwa na nyingine ipate kipato kidogo.
Nimefanya uchunguzi na kugundua kuwa, baadhi ya wanawake, wanadhani kuwa, wajibu wao
mkuu katika familia ni kuzaa na kutunza watoto kwa kuwapigia chakula na mambo mengine
yanayofanyika nyumbani, Swala la kushiriki katika kutafuta mali, hufikiriwa kuwa linamhusu
mwanamume tu, maana Mungu alimwambia Adamu kuwa: “Kwa jasho la uso wako utakula
chakula” (Mwanzo 3:19). Hivyo, mwanamke ni wa kuletewa kila kitu na kutumia.
Wanawake wengine hudhani kuwa, hata kama wanashiriki katika kutafuta kipato cha familia,
hawatakiwi kujali sana kama wanaleta kipato kikubwa, ila cho chote wanachopata, hata kama ni
kidogo kiasi gani, kinatosha, maana, mwanamke ni msaidizi tu. Hivyo, wanaishia kufanya kazi
za kubandaiza, yaani, kazi za kuwapatia kipato kidogo kisicho na tija kubwa.
Wanaume wengine, wanajisikia kuwa, wake zao wanatakiwa kukaa nyumbani tu kulea watoto na
kutojishughulisha na kazi ya kutafuta kipato kwenye familia, maana, wanawake hawana uwezo
wa kutafuta kipato. Mawazo hayo, ya wanawake kudhani wao ni watu wa kuzaa tu na kulea
watoto na ya wanaume ya kudhani kuwa mwanamke hawezi kufanya kazi ya maana ya kuleta
kipato, si sahihi.
Usaidizi wa mwanamke kwa mwanaume, ni katika mambo yote, hata ya kutafuta kipato. Kuna
baadhi ya wanawake, wanaoishi kwenye familia zao kama wageni, kwani, hawana mchango wo
wote katika kutafuta mali za familia. Hii inampa nafasi mwanaume kutumia mali za familia
atakavyo yeye, maana, anaona kuwa yeye peke yake ndiye aliyezitafuta. Mwanamke anakosa
sauti katika matumizi ya mali za familia, kwani, alipenda kuletewa kila kitu. Bahati mbaya
ikitokea, mme akifa, ndugu humnyang’anya mali mwanamke, kwani, walimwona mme peke
yake akitafuta mali na mke akikaa bila mchango wo wote katika kutafuta mali.
Zaidi ya hayo, wanawake wenye mawazo ya kuzaa na kulea watoto tu, endapo watafiwa na
waume zao, huingia kwenye shida kubwa ya kukosa kipato cha kuendesha maisha yao, maana,
hawajui namna ya kufanya kazi na kuzalisha kipato. Maisha yao baada ya kufiwa na waume zao
huwa mabaya sana. Ni vizuri wanawake waamke toka kwenye usingizi wa kutotambua mambo
na kuanza kufanya kazi zote hata zile zinazodhanini kuwa ni za wanaume, ili wawe na uhakika
wa kujihudumia hata kama wenzi wao watatengwa nao kwa njia ya mauti.
Biblia inaongea juu ya mwanamke kushiriki katika uchumi wa familia kwa kusema kuwa: “Mke
mwema ni nani awezaye kumwona?...Wala hatakosa kupata mapato” (Mithali 31:10-11).
Kama mke mwema hakosi kupata mapato, mke asiyejishughulisha kupata mapato, akimwachia
mme wake kazi ya kupata mapato, si mke mwema. Tunaomba kila mke ajitahidi kupata mapato,
akichanganya na mapato ya mme wake, familia yao haitakuwa na uhitaji wa vitu muhimu.
Neno la Mungu linaendelea kusema: “Hutafuta sufu na kitani; hufanya kazi yake ya mikono
kwa moyo” (mstari wa 13). Hii ina maana kuwa, mwanamke mwema anapenda kufanya kazi za
mikono, wala hafanyi kazi kwa kushurutishwa na hali ya maisha. Ukipenda kazi zako, utafanya
kwa uangalifu na kwa bidii na kupata kipato kikubwa.
Neno la Mungu linaendelea kusema juu ya mwanamke kushiriki kazi za uchumi katika familia
yake kwa kusema: “Anafanana ma merikebu za biashara; huleta chakula chake toka
mbali” (mstari wa 14). Hii ina maana kuwa, mwanamke mwema, anafanya biashara za kutafuta
mali toka mbali, mahali zinakopatikana kwa bei rahisi na kuzileta nyumbani na kuziuza kwa
faida kubwa. Wanawake wasiogope kufuata bidhaa toka China, Dubai na sehemu nyingine,
mahali watakakozipata kwa bei ya chini.
Neno la Mungu linaendela kusema kuhusu mwanamke anayeshiriki kwenye kazi za kuleta kipato
kwenye familia yake kwa kusema: “Huangalia shamba akalinunua kwa mapato ya mikono
yake hupanda mizabibu” (mstari wa 16). Pamoja na kufanya biashara, mwanamke mwema
mwenye kuchangia kutafuta kipato kwenye familia yake, hushiriki kazi za kilimo pia, kwa
kununua shamba toka fedha za shughuli zake na kupanda mazao ya kula na biashara.
Watoto nao wanatakiwa kushiriki kwenye shughuli za uchumi wa familia yao na wala
wahatakiwi kudhani kuwa, kazi yao kubwa na kutafuta elimu, na mambo ya kutafuta mapato ya
familia ni ya wazazi. Kabla hawajaondoka kwa wazazi wao kwenda kujitegemea, wanatakiwa
kuchangia katika kutafuta mali, ili wakienda kujitegemea, wazazi wawe na kipato cha kuwatosha
katika maisha yao ya uzee, na wao, wasihitajike kuwasaidia, maana, wanajitosheleza kabisa.
Watoto hawatakiwi kuwa wategemezi wa wazazi wao kwa kila kitu. Wakiwa wadogo, mchango
wao utakuwa kidogo. Wakiwa wakubwa, tuseme, wamemaliza elimu ya sekondari, kabla ya
kujitegemea, wanatakiwa kufanya kazi za nyumbani, kwa juhudi nyingi, wakijitegemea
wawaache wazazi wao wamejitosheleza hadi mwisho wa maisha yao.
Watoto wasifanye kazi kwa mikono milegevu, huku wakijifariji kuwa, watakapojitegemea,
watafanya kazi kwa juhudi kujenga uchumi wa familia zao. Huo ni ubinafsi. Wanatakiwa
kuelewa kuwa, wanapofanya kazi za nyumbani kwa wazazi wao, wanajifunza namna ya kufanya
kazi na kuzalisha vipato, elimu ya uzalishaji mali wanayojifunza nyumbani kwao, wataitumia
wakiwa katika nyumba zao. Hata hivyo, wazazi wasisubiri kusaidiwa na watoto wao,
wahakikishe wana mapato ya kutosha maishani mwao, wao wenyewe. Kusaidiwa na watoto
kabla ya kujitegemea ni ziada, ambayo wanaweza kuipata au la.
Hivyo, katika familia, baba, akiwa kichwa cha familia, anatakiwa kuangalia sana kazi zinazoleta
kipato kwa familia yake, akamshirikisha mke wake na watoto wake. Familia isikomee kufanya
kazi kwa ajili ya kupata kipato cha kujikimu tu, yaani, kipato kwa ajili ya kupata chakula,
mavazi na makazi, au mahitaji ya lazima. Familia, ijitahidi kupata kipato kwa ajili ya matakwa
yao, au (wants), mfano, kununua gari nzuri, kujenga shule ya kusaidia watu, kujenga hospitali, ni
mambo mazuri sana katika ulimwengu huu. Mtu asijifikirie yeye peke yake na familia yake.
Akitosheka, afikirie na wengine pia. Afikirie namna ya kukwamua maisha ya wengine, ambao
hawakubahatika kuwa na kipato kikubwa. Ni ombi letu kuwa kila familia iwe na kipato kikubwa
cha kutoshereza mahitaji yake ya lazima na baadaye, wawe na kipato cha kusaidia wahitaji na
kutoa kwa ajili ya kazi ya Mungu.
Mambo ya Kuombea:
1. Mungu abariki kazi za kila mmoja wetu ili ziwe baraka kwa kwa familia zetu na kwa kazi
ya Mungu.
2. Tuombee kila mmoja wetu awe na ari ya kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa
familia na kuitegemeza kazi ya Mungu.

Somo la Saba
(Ijumaa: Septemba 10, 2021)

NAFASI YA MAWASILIANO KATIKA UMOJA WA FAMILIA


(Na: Devotha M. Shimbe – Mkurugenzi wa Elimu, STU)
“Hayo mnayajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si
mwepesi wa kusema; wala kukasirika; kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya
Mungu, Yakobo 1: 19 – 20.
“Mimi sielewi nini kimetokea katika ndoa yetu,’’ alisema Kelvin huku akiwa na msongo kubwa
wa mawazo. Kabla hatujaoana tulikuwa na mambo mengi ya kuongea. Sasa hatuongei. Kwa
upande wa Esta ambaye ni mke wa Kelvin anasema “huwa simwambii chochote, na hivyo hana
kitu cha kusikiliza. Havutiwi tena na chochote kinachonivutia mimi”. Hii si changamoto ya ndoa
ya Kelvin pekee bali ni hali halisi inayozikabili ndoa nyingi.
Wataalamu wa mambo ya familia hudai kuwa mojawapo ya mambo makubwa yanayochangia
wanandoa kugombana na hata kufikia kutengana ni suala zima la mawasiliano katika ndoa.
Usahihi wa mawasiliano ni suala moja lakini kupungua au kutokuwepo kwa mawasiliano kabisa
ni suala jingine linalopelekea changamoto katika ndoa nyingi.
Nini maana ya mawasiliano? Mawasiliano ni njia ya mbadilishano katika kutoa na kupokea
taarifa huku yakihusisha siyo tu kuongea, bali kusikiliza au kupokea taarifa na kuzielewa. Kuna
wakati mtu anaweza kusikiliza lakini asielewe kile kilichokusudiwa na hivyo kupelekea
mawasiliano kutokukamilika. Ikimbukwe kuwa mawasiliano hukamilika kwa njia zingine zaidi
ya kuongea na kusikiliza kwani mwonekano, matendo, ishara, hisia na kadhalika huweza
kufikisha ujumbe kwa mlengwa. Kwa kawaida tukiwa macho tunatumia takribani 70% ya muda
wetu kuwasiliana kwa kuongea, kusikiliza, kuandika na kusoma. Katika muda huu, 33%
hutumika katika kuongea na asilimia zingine hubakia kwa mambo mengine. Hivyo,
mazungumzo ni muhimu sana katika kuelezea hisia na kuwaleta watu karibu katika mahusiano.
Mawasiliano ya kuongea husaidia kufafanua fikra zetu, kuimarisha mawazo, kufahamiana na
watu, kuondoa msongo, kutoa maoni na kujenga mahusiano thabiti.
Mawasiliano katika ndoa huweza kukamilika ikiwa wanandoa watazingatia kanuni kuu tatu za
mawasiliano kama zinavyopendekezwa na mwandishi Nancy Van Pelt, katika kitabu chake
kiitwacho To have and to Hold. Nancy anasema, mawasiliano katika ndoa huweza kukamilika
pale:
i. Yanapozingatia sanaa ya kusikiliza na kuongea kwa usahihi
ii. Yanapoweza kutatua matatizo kwa njia za kujenga zaidi kuliko kubomoa
iii. Yanapotumika kila siku kuelezea hisia ya mapenzi na ukaribu kati ya wenzi.
Kanuni hizi ni za msingi sana ili kuhakikisha uhai na furaha katika mahusiano ya ndoa.

Vizuizi katika mawasiliano ya kuzungumza


Wakati mwingine mazungumzo huweza kupata vizuizi mbalimbali hata kupelekea mawasiliano
kukatika. Vizuizi hivi ni pamoja na matumizi ya maneno yenye kushurutisha. Kama vile toka
hapa, fanya haraka. Mfano mwingine ni matumizi ya maonyo na vitisho. Kwa mfano, ukirudia
kufanya hivyo tena…; Ina maana hujui… na kadhalika. Matumizi ya maneno haya pamoja na
ukosoaji usio wenye kujenga, lawama na maneno ya kejeli au dharau huvunja mnyororo wa
mawasiliano kwa kiwango kikubwa sana. Haya humfanya mwenzi kuwa duni na kujiona hafai
kabisa. Matokeo yake, mwenzi huyo anaweza kuamua kukaa kimya tu na kuyaacha maisha
yajiendee tu.
Vizuizi katika kusikiliza
Kwa mujibu wa wanasaikolojia, udhaifu katika kusikiliza ni mojawapo ya kikwazo kikubwa
katika changamoto za mawasiliano kwa wanandoa. Hata kama kuna mbinu bora kiasi gani
zinazoweza kutumika kutafuta suluhu, kuleta maridhiano kihisia na kuondoa kutokuelewana,
ikiwa zitakumbana na msikilizaji mbovu haziwezi kuleta ufanisi. Hii ni kwa sababu wengi wetu
hupenda kuongea kuliko kusikiliza na kuelezea hisia zetu na kutoa mawazo na matamanio yetu
bila kujali kupokea kutoka kwa wengine. Watu wa aina hii wanapokutana na mtu mwenye
mtazamo tofauti na wao mabishano na malumbano yanaweza kutokea maana hawawezi
kumsikiliza ili kuelewa bali husikiliza ili kujibu hoja. Watu wa aina hii ni wasikilizaji wabovu.
Aina za wasikilizaji wabovu
Kuna aina tano za wasikilizaji wabovu, ambao ni kama ifuatavyo
i. Msikilizaji mchovu. Huyu alishasikia yote tangu zamani. Huiweka akili yake katika hali
ya kutohitaji kuongeza kitu tena, hata akitakiwa kutoa mawazo hana cha kuongeza.
ii. Msikilizaji mwenye kuchagua. Huyu huchagua kusikiliza mambo yanayomvutia tu na
kuacha mengine. Wengi wao, hawapendi kusikiliza mambo yaliyo kinyume na mtazamo
wao, wasiyokubaliana nayo na yanayowaudhi. Ni dhahiri kuwa hatuwezi kufanya
maamuzi sahihi ikiwa tutasikiliza baadhi tu ya mambo. Tunahitaji kupata ukweli wote na
uhalisia wa mambo ili kufanya uamuzi sahihi
iii. Msikilizaji mwenye kujihami. Huyu hubadilisha maneno yote yaliyosemwa kuwa
mashambulizi kwake binafsi. Kila lisemwalo ni kwa ajili yake na hapendi kusahihishwa
kwa hali iwayo yote. Hata kama hoja ni ya jumla kwa watu wote, yeye huitazama kama
inayomlenga yeye binafsi.
iv. Msikilizaji mkatizaji. Huyu hutumia muda mwingi kutafuta jibu na siyo kusikiliza kile
kinachozungumzwa. Huvutiwa na mawazao yake tu. Mara zote husubiri kupata upenyo
wa kukatiza mazungumzo ili kuchomeka mawazo yake katikati ya mazungumzo.
Utamsikia akisema, “Hilo ni dogo, nisikilize mimi kilichonitokea juzi… au bora wewe,
mimi zaidi…” Aina hii ya usikilizaji huondoa motisha kwa mzungumzaji na badala yake
humwachia yeye kueleza yote ha hivyo kuvunja mawasiliano.
v. Msikilizaji asiye na hisia. Huyu hawezi kusoma hisia katika maneno yanayotumika
katika mazungumzo. Hili ni tatizo kwa wanaume walio wengi ambao hushindwa kuelewa
hisia zinazowakilishwa na maneno yanayosemwa na wanawake. Kwa mfano, mke
anapoomba kusindikizwa sokoni, anaweza asimaanishe kupelekwa. Hii ni lugha ya
kutaka kujua ikiwa kweli unampenda na kumjali. Jibu la “sina nafasi sasa, nahitajika
kazini au kwani leo kuna nini hadi uombe kupelekwa….,” huleta maumivu kihisia kuliko
kusema, “oh, pole rafiki. Natambua wewe ni mama mwema na umekuwa unapambana
siku zote kwenda sokoni pamoja na uwingi wa kazi ulizo nazo. Kukupa furaha ndiyo
tamanio langu siku zote. Natamani sana nikusindikize,. Lakini sasa hivi nina kazi hii hapa
( aione au kuilewa) na inahitajika leo, natamani iishe ili tufurahi pamoja. Naomba
tushauriane cha kufanya”. Kwa maneno haya mwanamke mwenye akili hawezi
kukasirika wala kuleta lawama.

NINI KIFANYIKE?
1. Zingatia kanuni muhimu za kuwa msikilizaji bora ili kuleta amani katika mahusiano.
Kanuni hizi ni pamoja na:

i. kumtazama mzungumzaji kwa makini, kukaa mkao wa kusikiliza, kuonyesha ishara


za kuvutiwa na mazungumzo, kuuliza maswahi kwa usahihi na ujitahidi kusikiliza
zaidi kuliko kusema.
ii. Tatua matatizo kwa haraka na kwa kutumia njia za kujenga ili kuboresha mawasiliano.
Chagua muda muafaka na mahali sahihi, kuwa wazi, baki kwenye mada, onesha
heshima, weka orodha ya njia za kusuluhisha tatizo, chagua njia sahihi na ufanyie
kazi makubaliano yaliyofikiwa.
2. Zingatia kanuni muhimu za mzungumzaji bora ili kuleta tumaini katika mawasiliano.
Chagua muda muafaka wa kuwasiliana na mwenzi wako, tumia sauti nzuri yenye
amani , sema kwa usahihi kile unachokusudia, jenga mtazamo chanya katika
mazungumzo, jiandae kuheshimu mawazo ya mwenzi wako, jali hisia za mwenzi
wako na mahitaji yake, na jenga mazingira ya kuwa na mazungumzo ya pamoja mara
kwa mara. Kutozungumza mara kwa mara na kila mmoja kuwa na ratiba yake
kunavuruga mnyororo wa mawasiliano.
Ombi. Bwana afanywe kuwa kimbilio na ngome nyakati zote ili kuwa na mawasiano sahihi
katika ndoa. Kumbuka Yakobo 1:20…kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu

Mambo ya Kuombea:
1. Mungu awasaidie wanafamilia kujifunza na kuelewa mbinu za Mawasiliano na kuzitumia
kwa ajili ya kuleta furaha na umoja wa familia zao.
2. Tuombe Mungu asaidie familia zinazoporomoka kwa sababu ya kuvunjika kwa
mawasiliano miongoni mwa wanafamilia; Mawasiliano yarejee ili kuleta uhuru, furaha na
umoja.

Somo la Nane
(Sabato: Septemba 11, 2021)

NAFASI YA MAOMBI KATIKA UMOJA WA FAMILIA


(Na: Mch. Herbert Nziku – Mkurugenzi wa Huduma za Familia, STU)

Mathayo 7:7
Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.

Ni asubuhi na mapema, mama ameamka kwa ajili kujiandaa na kuwaandalia watoto kifungua
kinywa kabla hawajaondoka kwenda shuleni. Baba naye anaamka anajiandaa kwa ajili ya
shughuli za siku nzima. Kwa vile familia hii inampenda Mungu, wanaimba wimbo. Na kamwe
hawaondoki nyumbani kabla ya kujifunza somo la asubuhi na kupiga magoti ili kumwomba
Mungu awabariki na kuwalinda wote kwa siku hiyo.

Jioni wanapokuwa wamerudi nyumbani wanafanya ibada inayoambatana na kuimba, kusoma


neno la siku husika na hatimaye kupiga magoti wakiizunguka meza yao na kuomba.
Wanamshukuru Mungu kwa Baraka, ulinzi na mema aliyowatendea kwa siku nzima. Wanaomba
kwa ajili ya watu wngine pia.

Familia kama hii inakuwa na mwunganiko mkubwa baina yao wenyewe kwa wenyewe, lakini
pia inakuwa na mwunganiko na Mungu.

Uhusiano mbaya wenye mashaka na unaoleta uchungu na huzuni Katika familia unaweza tu
kuponywa kwa wanafamilia kukaa pamoja, kuimba pamoja, kujifunza neno pamoja na kuomba
pamoja.

Ahadi ya Yesu, “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa,”
(Mt. 7:7) inazihusu familia pia. Mahitaji yote ya wanafamilia inapaswa yapelekwe kwa Mungu
kwa njia ya Maombi ya Imani.

Familia ni lazima iwe na muda maalumu kwa ajili ya Maombi ya asubuhi na jioni

Ellen G. White, Katika kitabu cha Child Guidance (uk.520) anasisitiza wazo hilo kwa kuandika,
“Katika kila familia panatakiwa pawepo muda uliopangwa kwa ajili ya ibada ya asubuhi na jioni.
Inafaa kiasi gani wazazi kuwakusanya watoto wao kuwazunguka mbele yao kabla ya kufungua
kinywa, kumshukuru Baba wa mbinguni kwa ulinzi wake wakati wa usiku, na kumwomba
msaada na uongozi wake na ulinzi wake wakati wa mchana! Inafaa kiasigani pia, inapofika jioni.
Wazazi na watoto kukusanyika tena mbele zake na kumshukuru kwa ajili ya Baraka za siku
iliyopita!

Kanuni hii ikifuatwa kwa Uaminifu, pamoja na Baraka nyingi zitakazopatikana, familia zetu
zitakuwa na umoja wa pekee. Kwa watoto, uzoefu huo utadumu Katika kumbu kumbu zao hadi
watakapokuwa watu wazima.

Maombi ya Familia huleta nguvu na mibaraka


“Inatupasa kumwomba Mungu zaidi ya tunavyofanya. Kuna nguvu kubwa na Baraka katika
kuomba pamoja katika familia zetu, pamoja na kwa ajili ya watoto wetu. Watoto wangu
wanapokuwa wamekosea, na ninapokuwa nimezungumza nao kwa wema na kasha kuomba
pamoja nao, sijawahi kuona kuwa ni lazima kuwapa adhabu baada ya hapo. Mioyo yao huyeyuka
Katika upole mbele za Roho Mtakatifu anayekuja kama majibu ya ombi (Child Guidance, uk.
525)

Maombi ya familia yanaweza kuleta upatanifu na uhusiano wenye kuokoa miongoni mwa
wanafamilia. Baraka zitokanazo na nguvu ya msamaha kwa watoto na kwa wazazi huifanya
familia izidi kuwa na mshikamano na umoja usiokuwa wa kawaida.

Wafundishe watoto kuheshimu muda wa Maombi

Watoto wako waelimishwe kuwa wema, wenye kuwafikiria wengine, waungwana, wepesi
kusaidia, na juu ya yote, kuheshimu mambo ya kidini na kuhisi umuhimu wa madai ya Mungu.
Inapasa wafundishwe kuheshimu saa ya Maombi; wanatakiwa kuamka asubuhi ili wawepo
kwenye ibada ya familia.” (Child Guidence, uk. 521)

Ibada ya nyumbani iwe ya kuvutia

Wazazi tujifunze kuzifanya ibada za nyumbani ziwe na mvuto kwa kila mmoja. Tuepuke ibada
za kutimiza wajibu tu, huku mguso wa uwepo wa Roho Mtakatifu ukikosekana. Ellen G. White
akielezea juu ya uzuri wa ibada za nyumbani unavyotakiwa kuwa aliandika:

“Mara nyingi ibada za asubuhi na jioni ni zaidi kidogo tu ya kutimiza wajibu tu, mkusanyiko wa
vifungu kwa maneno mepesi ya kujirudia ambamo roho ya shukrani au ile hali ya uhitaji huwa
haionekani. Bwana huwa hakubali Huduma kama hiyo. Lakini, kusihi kwa kwa moyo
mnyenyekevu na roho ya toba hataidharau. Kufungua mioyo yetu kwa baba yetu wa mbinguni,
kutambua utegemezi wetu wote, kueleza mahitaji yetu, heshima ya upendo wa shukrani – hayo
ndio Maombi ya kweli.” (Child Guidance 518)

Mambo ya Kuombea:
1. Uamsho na matengenezo ya ibada ya Maombi Katika familia zetu
2. Mungu atupe roho ya unyenyekevu na Imani Katika Maombi yetu.

You might also like