You are on page 1of 6

JINSI YA KUMLEA MTOTO

namna kijana anavyokua, huwa inaamuriwa na malezi ya wazazi au walezi


mithali 22:6
JINSI YA KUMLEA MTOTO AU KIJANA WA KIMUNGU
VITABU 1 Yohana 2:14

“Nimewaandikia ninyi,vijana,kwa sababu mna nguvu,na neon la Mungu linakaa ndani yenu,nanyi
mmemshinda yule mwovu”

Mithali 22:6 “Mlee motto katika njia impasayo , naye hataiacha,hata atakapokuwa mzee

Mhubiri 12:1 “Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako,kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala
haijakaribia miaka utakaposema, mimi sina furaha katika hiyo”

UTANGULIZI

Maana ya neno LEA katika;

FAMILIA- Ni kutunza na kufundisha motto mpaka akue;kuweka chini ya uangalizi

Kufundisha- Ni kutoa mafunzo au kuelimisha.

Kutunza- Ni kutoa mahitaji ya msingi.

KANISA-Ni kuelimisha vijana kuhusu Mungu wa kweli.

2 Timotheo 1:5-6

MTOTO- anakumbushwa sharia ya baba yake, huyu ndiye mara nyingi anaadhibiwa kutokana na makosa.

MWANA/KIJANA- anaishi na sharia ndani yake.

Mzazi anawajibu na maamuzi kuwa motto wake azidi kuwa mtoto kadri miaka inavyoenda au
awe kijana.Wokovu ambao utamkuzia mtoto utaambatana na matendo yake.

“Matendo ya waamini hayaathiri dunia, lakini dunia inaathiri kanisa” Hii Ni sababu kijana
hajatengenezwa.

KIINI

Maswali unayoweza kujiuliza

1. Kwanini, kumtengeneza kijana?

i. Ana nguvu
ii. Anaangalia Zaidi mbele,yaani ana maono. Mithali 29:18 “pasipo maono watu huacha kujizuia”
iii. Rahisi kufundishika
iv. Mwepesi kuthubutu
v. Anategemewa kuishi miaka mingi mbele. Yohana 21:18

2. Kwanini, kumtengeneza kijana ambae haaminiki?

o Hapana, kijana anaaminika, watu wachache wenyte akili na maono ya mbali ndiyo
wanaohangaika na vijana. Usimwombee kijana tu, balui husika pia na kumwelekeza.
MAENEO 3 YANAYOMTENGENEZA KIJANA
Familia- Tabia na uvumbuzi wa vipaji

Kanisa- Maisha ya kiroho na utumishi

Taifa- Elimu

FAMILIA- Mambo ambayo mzazi /mlezi anapaswa kufanya:

a) Msaidie kujua kusudi la kuzaliwa kwake, ambalo kususdi la kwanza ni kumwabudud Mungu.

Luka 1:13-17

Maswali ya kumuuliza:

 Vitu ambavyo akifanya hatumii jitihada nyingi


 Vitu gani akifanya anajionea fahari
 Vitu gani ambavyo mtu mwingine akifanya akakosea,yeye anaumia
 Vitu ambavyo akiwa anafanya anaweza kusahau kula
 Vitu ambavyo anaweza kulipia kwa pesa nyingi ili kujifunza
 Kaa naye chini, kisha mwoneshe ukoo wake, pande zote mbili

b) Msaidie kupata elimu


o Elimu ya maarifa ya kimungu Mdo 2:42
o Maarifa ya kibinadamu Mithali 4:13

c) Mfundishe kufanya kazi1 samweli 3:1, aache uvivu na usingizi.Bidii yake ndiyo
itakayomtofautisha katika jamii. Awe Na bidii katika maombi pia.
1 Timotheo 4:13
Mungu tu mwenyewe hasinzii wala halali, anapiga kazi na wanaofanya kazi.
Mhubiri 3:1
”Kazi ni utu (ubinadamu-wajibu)

d) Mfundishe kufanya maamuzi binafsi


-asiingiliwe baadhi ya maamuzi, hasa katika mavazi.
-kupitia maamuzi binafsi utajua amejaza nini ndani yake na namna gani ya kumsaidia, kupitia
neno la Mungu na hekima yako uliyonayo.
Umuhimu: Inamkuza kiufahamu na kujitegemea.
Luka 15:11-24, Kumb la torati 30:19

e) Mfundishe kumpenda Mungu

1 Yohana 2:15,

1 Timotheo 4:7b
Maeneo yanayoangaliwa kwa kijana:

1. Uongozi na siasa
2. Uchumi na uzalishaji
3. Sanaa na michezo
4. Teknolojia na habari

“Msaidie namna gani atumike katika Nyanja hizo kwa uangalifu”

TAFAKARI YAKINIFU:

Vijana katika biblia walikuwa na nini ambacho hawa wa sasa hawana?

Mithali 24:32

a) Walifanya mambo kwa bidii


b) Hawakukata tamaa
c) Hekima (wapenda falsafa)
d) Werevu (shauri na uweza)
e) Maarifa (kumcha Bwana)
f) Ufahamu (elimu na lugha tofauti tofauti)
g) Adabu, busara, methali,na vitendawili (bonus)
h) Haki, adili, na uaminifu.

MSAIDIE KIJANA UMLEE KATIKA:


1. Apokee Roho Mtakatifu na neno la uzima, apende maombi
2. Apate elimu; mtengenezee mazingira tangu akiwa mdogo kwamba elimu ni kwa manufaa ya
ufahanu wake,ili apende elimu(kwa mapenzi)
3. Awe mwenye bidii. Watot wa mwisho wasidekezwe sababu wataisumbua jamii.
4. Mfanye ajifunze lugha tofauti,apende kusoma vitabu mbalimbali. Mpe muda wa kusoma vitabu
sio Runinga peke yake tangu akiwa mdogo.
5. Usimruhusu kutumia muda mwingi nje akiwa na marafiki; lakini usimzuie kuonana na marafiki
zake.
6. Mshirikishe uchumi wa familia
7. Mfundishe kujiongoza
8. Tambua kipaji chake na ukiendeleze
9. Mfundishe somo la mahusiano kwa werevu, hekima na undani Zaidi

WAJIBU WA KIJANA /MTOTO KWA WANAOMTENGENEZA

 Kusikiliza
 Kutii
 Kuyashika
 Kuchanganua (maelekezo yaliyo katika mfumo wa mafumbo) na kutendea kazi
YAKUYATUNZA NDANI:

o Utiifu
o Bidii
o Utauwa 1 Timotheo 34:7b, Mhubiri 12:1
o Maarifa

Hitimisho

Waamuzi 13:8

Haya yote mzazi na mtoto au kijana, hayawezekani pasipo mkono wa Mungu:inatubidi kuomba, kusoma
neon, na kumtunza Roho Mtakatifu.

Jina la Bwana libarikiwe, MARAN ATHA


MWANDISHI

Jina ni Hellen Edward, kutoka katika kanisa la Pentekoste Mwananyamala chini ya Askofu, Mchungaji
Fidel Migabo.

You might also like