You are on page 1of 3

UONGOZI

Uongozi ni nini hasa:-


(1) Ni mtiririko wa uelekezaji, udhibiti wa hisia za wengine au tabia zao.
(2) Ni uwezo wa kuhamasisha wengine wafanye yale unataka wafanye. NEH. 2:17-18, Matokeo NEH. 4:6
(3) Ni uwezo wa kuwafanya wengine wafanye yale yanayopaswa kufanywa.
(4) Ni uwezo wa kupandikiza maono, huduma, maisha ndani ya watu. EFESO 4:12
(5) Ni uwezo wa kuelimisha kundi ili liweze kutenda kazi kufikia lengo lilipo.
(6) Ni kukubalika, kutambulika kama kiongozi (Recognize).

KIONGOZI NI NANI? (1KOR. 12:28)


(1) Ni mtangulizi/leader, ni mwelekezaji na yeye mwenyewe akitembea katika njia hiyo (YN. 10:4, MIK. 6:4,
KUT. 15:20-21, KUT. 18:20, AMU. 18:5)
(2) Ni mtendaji mkuu, ndiye mwenye majibu yenye kufanikisha lengo lilipo, ni msimamizi wa mambo ili
yatokee, ni mtawala, ni yule anayeona mbele.
(3) Ni mtu anayewashawishi wengine wafanye wasichotaka (Nguvu za hoja).

KWANINI MUNGU AMEWEKA UONGOZI KATIKA KANISA AU JAMII?


(1) Ili kuwepo utaratibu (Order), tuna kanuni, katiba, miongozo ya kufuata.
(2) Ili kuwepo usimamizi, mipango, uendeshaji, ustawishaji,mawasiliano, maendeleo, uhimizaji,
kuwajibika,kutoa taarifa kwa mamlaka iliyo juu, ukamilishaji/perfecting, kutia moyo.

Kama hakuna uongozi/utawala,basi watu watafanya yao. AMU. 18:1

Mungu ameona tangu zamani umuhimu wa uongozi ndiyo maana inamugharimu muda wa kutosha kuandaa viongozi.

Musa aliandaliwa kwa miaka 40, Yusufu, Daudi, wanafunzi wa YESU. (MDO 7:23, 30-34, 1SAM. 16:13, 2SAM.
5:1-3, MWA. 41:41-45

Toka katika kuongoza kondoo hadi watu. Musa, Daudi. ZAB. 78:71-70, KUT. 3:1-

Toka katika kuongoza nyumba, vitu, wafungwa hadi Taifa lote la Misri.

Toka katika kuongoza watu 400, 600, kabila moja la Yuda hadi Israel nzima. 1SAM. 23:13, 1SAM.30:10, 2SAM
5:1-3

Musa aliona vivyo hivyo juu ya uhitaji wa uongozi ndiyo maana akaomba MUNGU ili apate mtu baada yake.
HES. 27:15-21
Tunahitaji kuandaa watu, kuomba MUNGU tukiondoka wawepo watu wa kuongoza.
Kanisani kuna mahitaji makubwa ya uongozi.
Kukosa maongozi kunaleta udhaifu katika kanisa.
Tuna wajibu kuona kanisa linasimama imara na hii itatokea tukiwa na maongozi imara yaliyoandaliwa.
Jamii hazina nguvu, haina afya, isipokuwa kiongozi akiwa na afya.

Kanisa vivyo hivyo haliwezi kuwa na afya bila uthibiti wa viongozi au imara wa viongozi.

Ulimwengu una shida mbalimbali hata kama kuna shida nyingi. Shida kubwa kuliko zote ni kukosa viongozi.

Ukristo ndiyo unakabiliwa Zaidi kuliko kitu chochote, ni kukosa uongozi. Kusimama kwa taifaau kanisa hutegemea
uongozi uliopo.
Ni hamu ya jamii husika kuwa na uongozi imara. HAMU hiyo ipo kanisani pia. Watu wana hamu ya kupata kiongozi
ambaye wangemtegemea, wangemuelewa, ili wapate kuendelea vizuri katika maisha yao ya rohoni, uongozi
utakaowakuza kiroho.

MAMBO YASEMWAYO KUHUSU KIONGOZI


Je, kiongozi huja kwa namna gani?

Kuzaliwa.
Kuelimishwa.
Uzoefu wa muda mrefu wa maisha.
Mwito wa MUNGU. Sisi watu wa Kiroho tunaamini hivyo. (Imani ya Wayunani ni kuwa uongozi ni zawadi
toka kwa MUNGU). 1SAM. 16:1, 2SAM. 22:1, DAUDI-2SAM. 23:13, 24:16, ELISHA-2FAL.2:1,
YUSUFU-MWA. 42:16

AINA ZA UONGOZI
Kuna aina kadhaa za uongozi.

(1) Kimila-Dikteta. (2NYA.10:8-14)


(2) Uongozi wa watu-Demokrasia/Democracy. (MDO 15:6-22)
(3) Uongozi wa kiholela. (AMU. 21:24-25)
(4) Uongozi wa MUNGU, (Theocracy)-Utawala wa MUNGU.

Kanisani tunahitaji uongozi wa aina gani? Ni uongozi wa MUNGU.(LK 10:33-35,YN 14:16-18, MDO 13:2, 20:28,
1KOR. 12:4-11, MDO 5:1-11)

MBINU ZA UONGOZI.
Uongozi una kanauni zake.
Uongozi una taratibu zake.
Uongozi una mbinu zake.

Kanuni hizo husaidia kufanikisha uongozi ili uwe bora zaidi. Hivyo ni muhimu tukachunguza mbinu na taratibu hizo
ili tuwe na uongozi ulio bora na kufaa.

Kiongozi mwajibakaji, Mfano MUSA, HES. 14:11-18 hajatawaliwa na ubinafsi, anatafuta faida ya wale
anaowaongoza. 2SAM. 24:16-17 aliye tayari ikibidi kuwajibika.

Kiongozi aliyetumia matendo kufanya yeye mwenyewe. (NEH. 2:17, 4:21-23).

Nasi tunahitaji kuzitumia mbinu hizo zinazofaa, kwa kujifunza kutoka kwa viongozi waliopita na jinsi walivyofaulu
katika uongozi wao pamoja na maombi, kujazwa na Roho MTAKATIFU na kusoma neno la MUNGU, basi
tutafanikiwa kuwa viongozi bora.

SIFA ZA KIONGOZI MZURI-BORA.


(1) Ni yule ajitoaye kwa ajili ya wale anaowaongoza kuwatumikia, siyo atumikiwe. NEH.1:4, YESU-MT.
20:26, YN. 13:4-9, Kiongozi mtumishi. MK 10:43, 1FAL.12:8.
Musa aliyeombwa kufutwa katika kitabu cha uzima kwa ajili ya wale aliowaongoza. HES. 14:11-18
Atafanya mengi kwa ajili ya uheri wa hao anaowaongoza.
Atoaye muda wake na vile alivyo navyo kwa uzuri wa hao anaowaongoza.
Ana hamu na moyo wa kuongoza ili watu wafanikiwe, wafaulu, waendelee.
(2) Ni mtu mwenye bidii (Committed), hodari katika mengi, mwenye kujituma. NEH 5:16, 4:21-23, YOSH 1:6-
9)
(3) Awe mwenye hekima kama sulemani ili aweze kuamua vema na kuongoza. 2NYA.1:10. Omba hekima kama
kiongozi, ukijua uzito na mzigo wa kazi yenyewe.
(4) Ni mtu jasiri kama Nehemia hata Paulo mtume. (NEH.4:14, 5:6-7, 10, 13, Gal.2:14-15). Musa alikasirika
hata Daudi alimkabili Goliathi.
(5) Awe mbunifu/creative, anabuni mambo mbalimbali ya maendeleo ya kanisa na kazi.
(6) Awe na maono, aone njia, kule anakopeleka watu na kuonesha mwelekeo. YN.10:4. Wajue unakokwenda na
unayoyafanya. Hata watu wajue utokako na uendako.
(7) Asipendelee bali aamue kwa haki ikibidi kufanya hivyo. NEH.5:7, asijipendelee, au watu wake, asifsnye
kwa upendeleo. YAK. 2:1
(8) Awe na tabia inayovutia, inayotamaniwa na watu.
(9) Awe kiongozi mwenye vitendo, ashiriki majukumu aliyoyatangaza. NEH.4:19-20
(10) Awe muungwana na mwenye upendo. 2TIM.2:24, mwenye kauli nzuri na pia asidharau kutoelewa kwa
watu.
(11) Mpenda haki. 1TIM.5:21-22, unaamua kwa haki. Unatamani watu watendewe kwa haki, unafanya kwa haki.
(12) Uwezo wa kujitawala na kujizuia kwa kutokasirika haraka. 2TIM.4:16, Tito 1:7. Maana watu wanaangalia
sana maelezo yako, kuwa mwangalifu unapojibu watu, mtulivu wakati wa shida.
(13) Awe mtulivu na saburi. 2TIM.4:5, 2:24, 1Thes.5:14, MDO.13:18. Awe mkarimu na mkaribishaji. Tito1:7-
9.
(14) Mwenye msaada wa ushauri kwa kundi. Mal. 2:7-8. Awe na busara ya kawaida na ya MUNGU. MT.10:16.
(15) Anayekubali ushauri kutoka kwa watu mbalimbali unaofanya nao kazi ila ujiangalie ili usipokee kila ushauri
maana ushauri mwingine ni mbovu-Musa alishauriwa na mkwewe-KUT. 18:13-23, Rehoboamu alishauriwa
na kijana. 1Fal.12:8, 2SAM.15:12, 16:23, 16:5-11. Yethro alikuwa kiongozi ndiyo maana mashauri yake ni
ya mtu kiongozi-KUT.18:13-24.
(16) Anayetia moyo watu hata katika mambo madogo. Anayejali mahitaji ya kundi analoongoza-NEH.5:6-13 na
kuwathamini watu-2SAM. 23:13-17
(17) Anayekubali mabadiliko, kwenda na wakati anakubali mageuzi, mabadiliko ni jambo la asilitunaishi katika
ulimwengu unaobadilika. Bila kubadilika basi mambo hayaendi japo pia tupime mabadiliko hayo, si vema
kufuata haraka kila mabadiliko yanayotokea.
(18) Anayegawa majukumu yake kwa wengine-KUT.18:13-23
(19) Anayefanya maamuzi yanayofaa kwa wakati unaofaa.
Akili na uamuzi tulivu ni sifa muhimu kwa kiongozi.
Kutokuepuka tatizo, ni vema kukabiliana na tatizo au jukumu.
Kuwajibika na matokeo ya uamuazi wako.
Unapoamua uwe mtulivu katika shinikizo la tatizo.

MWITO WA KIONGOZI WA KIROHO.


Mungu amewaita viongozi ili waongoze watu kuendelea mbele-KUT.15:22, HES.10:28

Kuwarithisha baraka mbalimbali za Roho, ni wewe mwenye jukumu hilo-YOSH.1:6

You might also like