You are on page 1of 14

GLORY OF GOD MINISTRY

P.O BOX 30407 *CELL: +255 755 898557


HEAD OFFICE: KILIMAHEWA, KIBAHA-COAST REGION
Email:gloryofgodministry2011@yahoo.com

GLORY OF GOD CHRISTIAN BIBLE SCHOOL

SOMO: MBINU ZA KUFUNDISHA


MKUFUNZI DR HEZRON MUSALALE

1
MBINU ZA KUFUNDISHA.
MAELEZO YA SOMO:
Ualimu ni moja ya karama za huduma katika kanisa. Ni ofisi kati ya ofisi tano za kanisa la
Mungu (Efeso 4:11) wengine aliwapa au alitoa wawe Mitume, wengine wawe Manabii,
wengine Wainjilisti, wengine Wachungaji, na wengine Waalimu.

Huduma hii ya ualimu hutanguliwa na huduma zingine nne.


Huduma hii hutokea mwishoni kwa maana nzuri kuwa huwezi kuwapata wanafunzi bila
kuwasajili kwanza na kuona kuwa wanafaa kufundishika.

Huduma ya ualimu ni kuimarisha na kutengeneneza watumishi mbalimbali wa kanisa kama


hao niliowataja hapo juu.

Mwanzilishi wa Kanisa duniani Bwana Yesu Kristo alitumia muda wake mwingi kufundisha
kuliko kuhubiri kwa sababu alikuwa anatengeneza watenda kazi ambao baadaye aliwatumia
huko na huko
1. Darasa la mtu mmoja mmoja mfano Nikodemu, Mwanamke msamaria kisimani.
2. Darasa la watu watatu—hasa wale wanafunzi wa Yesu Petro,Yohana, na Yakobu,
kwenye mlima wa ugeuko, bustani ya Gesthmani.
3. Darasa la watu 12—mfano wanafunzi wake.
4. Darasa la watu wengi akitumia hotuba (Lecture) mfano (Math 5:1-11)

Njia alizotumia Bwana Yesu kufundisha na hotuba, majadiliano—mfano ‘hivi watu husema
mimi ni nani?
Wengine husema wewe ni Nabii….Nanyi mwasema kuwa mimi ni nani?

Njia ya maswali na majibu, mifano, kwa njia ya matendo—mf kuwaosha miguu, kuwachukua
wanafunzi watatu kwenda nao kwenye maombi mlimani.
Kwa njia ya mazoezi kwa wanafunziwake alipowatuma kuhubiri na kukemea pepo, semina—
mf alipoingia hekaluni na kuhojiana na wasomiwa wakati huo, kwa njia ya ishara na maajabu,
pia kwa njia ya maisha yake.

Yesu Kristo aliwapenda wanafunzi wake pia aliwajua (Math 9:35-36, Yoh 2:24)
Pia alikifahamu vizuri kile alichokuwa akifundisha na alifahamu jinsi ya kufundisha

ANGALIZO: Kwa hiyo kufunza au kufundisha ni kipawa maalumu toka kwa Mungu , wala sio
wote waliojaliwa kipawa hiki.

KIPENGERE CHA KWANZA: WEWE NI MWALIMU


1. Mwalimu ni nani?
2. Tofauti ya kufundisha na kuhubiri.
3. Mwalimu mzuri ni yupi?

2
a. Mwalimu ni nani:
 Mwalimu ni yule aliye na kipawa cha kutoa/ kugawia maarifa na ujuzi kwa mtu au
watu wasiojua na kufikia mahali pa kujua.
 Mwalimu ni yule anayefanya akili za watu wengine zipanuke katika kujua mambo
na kukaa katika mpangilio.
 Mwalimu ni yule anayezibua ufahamu wa watu wengine na kufikia hali ya
kujiamini.
 Yule anayetoa maelekezo, yule anayeboresha kile unachokifahamu.

Kwa kifupi mwalimu ni yule anayefunza na kuwafanya wengine wajifunze kufikia kubadilika
kitabia.
Wanaojifunza tunasema wamejifunza tunapoona tabia zaozimebadilika kuelekea kwenye
maadili mema ya Neno la Mungu.

b. Mwalimu mzuri:
 Anawaongoza wanafunzi kutoka eneo wanalojua na kuwapeleka eneo ambalo
hawalijui.
 Mwalimu ajiweke kwenye nafasi ya kutaka kujifunza kutoka kwa mwanafunzi na
kumshirikisha mwanafunzi wake kile anachokijua.
 Ni yule anayetegemea majibu ya matatizo au maswali yatoke kwa wanafunzi pia.
Mwalimu asiwe ndiye mwenye majibu peke yake na mwanafunzi wake kama
makinda ya ndege katika kupokea chakula.
 Mwalimu na mwanafunzi huzungumza sio mwalimu peke yake ndiye
mzungumzaji.
 Wanafunzi wapate nafasi ya kueleza uzoefu wao.
 Mwalimu asifikiri kuwa yeye ndiye chanzo cha kila kitu, bali ajue vitu vingine
vitoke kwa wanafunzi.
 Mwalimu hupanga mambo akishirikisha wanafunzi wake.
 Anawapenda wanafunzi, anawajua, anajua anachofundisha na jinsi ya kukifundisha
 Aishi kama anavyofundisha—matendo husema zaidi kuliko maneno (Luka
24:19, Yoh 18:38)
ANGALIZO
Mwalimu mzuri ni yule anayeshirikisha na yeye anakuwa mwezeshaji. (Facilitator)

TOFAUTI YA KUFUNDISHA NA KUHUBIRI


1. Kuhubiri: Ni kutangaza kweli fulani kusudi la kuwashawishi na kuwavuta watu kufanya
uamuzi wa kumfuata Yesu Kristo, mahubiri hayana maswali wala majadiliano, mhusika
ndiye mzungumzaji hadi mwisho na wengine wote ni wasikilizaji.
2. Kufundisha:Ni hali ya kushirikisha somo kwa wanafunzi wako kwa njia ya maswali au
mjadala au mifano. Katika kufanya hivyo upo ujuzi flani wanafunzi wanaongezewa na
kuwafanya wabadilike, kitabia, kimsimamo na kiutendaji kiasi kwamba wanakuwa bora
zaidi kuliko mwanzo.
 Mwalimu ni lazima agawe vipawa vyake kwa wanafunzi wake.

3
 Aonyeshe mwelekeo wake kwa wale anaowafundisha.
 Awe na uhusiano mzuri na Mungu wake.
 Awe na ujuzi wa kutosha namna ya kutumia vifaa vya kufundishia na chumba cha
darasa lake.
 Wajibu wake mkuu ni kufaulisha mpango wa kufundisha kanisani.
Chukua muda mrefu kuwafundisha waanini kanisani mpaka wanakuwa watenda
kazi wazuri.
 Uweze kuzaa waalimu, wachungaji, wainjilisti , mitume na manabii Math 28:19-20
Kwenda itika kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, kuwafanya wayashike yote
niliyowafundisha.

KIPENGERE CHA PILI: MALENGO YA KUFUNDISHA


a. Kuwafikia wengine.
b. Kujua aina za malengo.

Malengo ya somo ni muhimu ili kuweza kupanga, kufunza na kukagua/ Tathmini hatimaye
kutoa taarifa ya mafanikio au mapungufu.
1. Kusudi kubwa la kufundisha ni kuwafikia wengine kupitia mafundisho au elimu ya Neno
la Mungu.
2. Uinjilisti na elimu ya Neno la Mungu ni sawa na mabawa mawili ya ndege inayoruka.
3. Uinjilisti ndiyo lengo kuu la kufundisha Neno la Mungu.
4. Uinjilisti ndiyo lengo la msingi la Ukristo wetu.
5. Kuwafanya wanafunzi wa Bwana Yesu Kristo.

Kwa hiyo malengo yako lazima yaguse Biblia.


Yaguse wanafunzi ambao ndiyo walengwa, mara nyingi walengwa huweza kutofautiana.
Umri, Tabia. Akili. Kimtazamo kuhusu jamii na kiroho.
Hivyo madarasa yao yanapopangwa lazima tofauti hizo zizingatiwe.

Kusudi la pili la kufundisha ni kufikia kiwango cha kujua umuhimu wa ubatizi katika maji
mengi na kasha ubatizo katika Roho Mtakatifu na kubatizwa.
Math 28:19.

Aina za malengo:
a. Kuongeza elimu, kuwa na kweli nyingi za Biblia ni muhimu kwa mwanafunzi wa Biblia,
Ni vema mwanafunzi kuielewa Biblia na kujua ili waweze kujitoa kwa njia sahihi kwa
Kristo Yesu.
Kiini cha injili ni ukweli wa kihistoria wa maisha ya Kristo- Kifo chake na kufufuka
kwake.
b. Kubadilisha mielekeo yao na mitazamo.
Eneo hili hushughulikia hasa hisia na shauku za wanafunzi, wanafunzi haitoshi kujua
ubaya wa dhambi, kinachotakiwa ni wao kufikia hatua ya kuichukia hiyo dhambi na
kuiacha kabisa—pia wafike mahali pa kuhusiana vema wao kwa wao kama watoto wa
Mungu.

4
c. Kubadilisha tabia:
Kubadilisha mwelekeo unatakiwa uendelee kiasi cha kubadilisha tabia yote au haiba yote
ya mwanafunzi, kubadilika tabia kabisa ni hatua ya maana sana katika ufundishaji wetu
wa Neno la Mungu (Math 5:20)
Haki ya wanafunzi wako lazima izidi ya wale wa dini tu.—hawa huonyesha mielekeo
kama imebadilika, imekuwa sahihi lakini tabia zao ni kama mtu yule yule wa zamani
(Luka 11:28, Yak 2:20)
Roho Mtakatifu akiwa namba moja wa kubadilisha tabia ya mtu.

Sifa ya lengo nzuri:


a. Fupi sana
b. Hulenga waziwazi (linakutana na mahitaji)
c. Linaeleweka.
d. Lenye kulenga maisha ya kila siku ili liweze kufikiwa.
e. Lazima liongoze somo.

KIPENGERE CHA TATU: NJIA ZA KUFUNDISHA


1. Mwanadamu atafahamu kuwa njia mbalimbali za kufundisha ni muhimu kwani huongeza
furaha ya kufundisha na kurahisisha ufundishaji.
2. Mwanadamu aelewe kuwa zipo njia ambazo hazifai kwa kundi fulani la wanafunzi.
a. Watoto huelewa zaidi mwalimu ikiwa atatumia njia ya:
 Hadithi, Muziki, Picha, Mwanasesere, Michezo.
b. Watu wazima huelewa zaidi mwalimu akitumia njia zifuatazo:-
 Mhadhara (Hotuba) Mafafanuzi / mifano
 Majadiliano (Kushiriki)
 Maigizo, Kuigiza mwenyewe.
 Ziara na Njia ya kumstusha mwanafunzi aelewe jambo flani ili kujenga ubongo
wake kuwa tayari.
 Njia ya projecti na kazi za nyumbani, Maisha ya Mwalimu nk.
Swali:
Njia gani inafaa zaidi kufundisha?
Jibu:
Ni ile utakayoiona inafundisha kwenye kutimiza lengo au malengo yako.
1. Mara nyingi njia ya hoja huchanganywa katika kufundisha ili kumrahisishia mwalimu
kazi yake.
2. Kwa maana hiyo, njia zote hufaa, cha kuzingatia kila njia itafaa ikiwa itatumiwa kwenye
mazingira yanayoingiliana na njia hiyo.

Soma jedwali hili hapa chini

5
NJIA FAIDA HASARA WATU
WANAO
PENDELEWA
MHADHARA -Mwalimu humaliza somo -Wanafunzi hawashiriki Vijana na watu
HOTUBA haraka. kikamilifu. wazima.
-Mwalimu hufuata mpangilio wa -Ni vigumu kutathmini.
somo lake bila bugudha. -Wanafunzi huchoka
-Mwalimu hutawala somo na haraka.
kuepuka kwenda nje ya somo. -Wanafunzi hulala
-Hufundisha watu wengi kwa darasani
mara moja.

HADITHI NA -Hufahamu kweli ambazo haziko -Kutajua hadithi nyingi. Watoto na watu
MIFANO wazi. -Kutoa hadithi nje ya wazima
-Hukazia mambo muhimu ya somo.
somo. -Kutumia lugha
-Huvuta usikivu wa wasikilizaji. isiyoendana na hadithi.
-Ni rahisi kuiga katika maisha ya
kila siku.
USHUHUDA -Hujenga wengine. -Wengi hawana karama Watu wote
-Hutia moyo wengine. ya kushuhudia. hupenda
-Huleta ujasiri wa kusonga -Kuficha ukweli ulio
mbele. -kutokea au kuongeza.
MUZIKI -Hufurahisha -Huficha ukweli Watu wote hasa
-Huvuta usikivu wa watu. uliotokea au kuongeza. watoto.
PICHA -Huvuta usikivu. -Uhaba wa picha Watoto hasa na
-Huona vitu vinavyofanania na -Ugumu wa kuchora. watu wazima.
somo, hivyo husababisha uelewa.
MICHORO Ya halisi Muda wa kuchora ni
adimu
MWANASESERE Kuvuta usikivu Ni vigumu Kwa watoto
-Huelewesha zaidi (msaada kwa kumwakilisha Mungu.
mwalimu Ni vigumu kutengeneza
na kutumia
MAJADILIANO. Hushirikisha kila mwanafunzi . Mtu mmoja mjanja Zaidi hutumika
Hujenga moyo wa kujianini. kuhadithia kipindi kwa kwa watu wazima
Hoja nyingi hupatikana. nje ya somo.
Waoga hubakia
kusikiliza wengine.
Mwalimu asipokua
makini huweza kuingia
hoja potofu.
Hutumia muda mwingi.
MAISHA YA Ni rahisi kuiga Ikiwa mwalimu haishi Kwa watu wote
MWALIMU kama anavyofundisha.

KIPENGERE CHA NNE: MBINU/NJIA ZINAZOMFAA MWANAFUNZI KUJIFUNZA


Njia ambazo zinamhusisha mwanafunzi kushiriki kikamilifu.
1. Njia ya majadiliano

6
2. Njia ya vikundi.
3. Michezo ya kuigiza.
4. Safari za kujifunza.
5. Project au kwa njia ya vitendo.
6. Mafunzo ya Biblia.

Muhtasari.
a. Njia ya majadiliano-kila mshiriki anahimizwa kusema.
b. Vikundi-huleta habari kutokana na aina nyingi za ujuzi.
c. Michezo ya kuigiza-huleta uhai mpya wa kweli za Biblia.
d. Safari za kujifunza- wanafunzi hujifunza moja kwa moja kwenye ujuzi wa kujifunza.
e. Project/ vitendo—pia huwahusisha wanafunzi kwenye utafiti au kwenye utumishi wenye
manufaa wa kikristo.
Project- kwa kufanya utafiti
Kwa kutumia mifano, kushuhudia, kuhubiri, nk.
f. Mafunzo ya Biblia- huwatia wanafunzi bidii ya kutafuta ukweli mpya na matumizi ya
sehemu za maandiko.

KIPENGERE CHA TANO: JINSI YA KUFUNDISHA


Lengo. 1. Wanafunzi wazingatie sheria za ufundishaji.
2.Walimu hutengenezwa au kufunzwa—ingawa wengine wana vipawa vya kueleza
wengine hata kama hawakwenda shule na kujifunza namna ya kufundisha

A. Mwalimu atafurahia kazi yake iwapo atafanya yafuatayo:-


1. Hutafuata kanuni za ufundishaji.
2. Anaipenda kazi yake.
3. Huwapenda wanafunzi wake.
4. Atajiandaa vya kutosha.
5. Ataliombea somo lake na wanafunzi na yeye mwenyewe.

SHERIA SABA ZA UFUNDISHAJI.


1. Sheria ya mwalimu—Mwalimu ni lazima alijue somo, ukweli, au sanaa anayofundisha.
Mwalimu alijue somo lote mbali na ile sehemu anayoifundisha.
(somo lazima mwalimu alitawale) Hakuna sababu ya kuchukia wakati wanafunzi
wadadisi wanauliza maswali.

2. Sheria ya mwanafunzi—Mwanafunzi mzuri ni yule anayehudhuria somo huku akiwa


makini kusoma.
Wanafunzi ni lazima wafanywe wasikivu.
Wanafunzi uwafanye wafurahie somo kwa:
a. Kutambua wanavyowaza.
b. Kuzuia kelele toka nje ya darasa.
c. Somo lilingane na uwezo wa wanafunzi.
d. Kuwashirikisha wanafunzi somo lako.

7
e. Somo liwe na motisha kwa wanafunzi—yaani somo likutane na mahitaji ya
wanafunzi.

3. Sheria ya Lugha.
Lugha ya kufundishia iwe inafahamika kwa watu wote wawili— mwalimu na
mwanafunzi—Lugha ya kufundishia ni vyema isiwe na misamiati migumu.

4. Sheria ya somo.
Anza somo lako kutoka eneo wanalolielewa wanafunzi na kisha wapeleke eneo
lisiloeleweka, kwa kutumia ufahamu ulio wazi kwao kama msingi wa somo jipya.
a. Husisha somo kwa masomo yaliyopita (marudio ya somo kabla ya somo jipya)
b. Endelea kwa hatua za juu zaidi hatua kwa hatua ya kuelewa wanafunzi.
c. Fundisha kwa kutumia mifano ili kurahisisha kuelewa.

5. Sheria ya utaratibu wa kufundisha.


a. Kufundisha ni kuzindua/ kuzibua na kutumia akili za wanafunzi ili waweze kuelewa
wazo fulani au kufahamu zaidi sanaa inayofundishwa, masomo yanayofundishwa ni
lazima yawe nisehemu ya maisha ya wanafunzi hao.
b. Vinginevyo watakuwa mafarisayo, wanajua Neno la Mungu na kweli zake zote lakini
hawaishi kulingana na kweli hizo.

Hivyo wanafunzi wanapaswa wafanye yafuatayo:


a. Wapewe mambo ya kufikiria watumie akili zao kupambanua na kuujua ukweli.
b. Wafanye uchunguzi/ utafiti, wawe na maswali kama haya yafuatayo.
1. Nani? Kwa vipi? Ni lini? Ninini? Ni wapi? Kwa nini?
Akili mara nyingi za namna hii hukua na kuweza kupambanua na shida za dunia hii.
c. Wafanye wanafunzi wako watosheke (washibe) ili kuwapa nguvu ya kusonga mbele.
Masomo yawasaidie katika maisha yao ya kila siku.
Masomo yakutane na mahitaji yao ya kila siku.

6. Sheria ya kujifunza:
Kujifunza ninini?

Jibu:
Ni kuwaza na kuingiza kwenye fahamu ya mtu wazo jipya la kweli au kufanya sanaa au
ujuzi mpya kuwa sehemu ya maisha ya mtu, ili kufaulu kufanya haya ni lazima
mwanafunzi awe na tabia ya:-
a. Kurudia rudia yale aliyojifunza.
b. Kuyatafsiri- kutambua kuwa wamepata ujuzi huo ni pale wanafunzi watakapoanza
kutoa maoni yao juu ya ukweli walioupata.
Hapa swali la kwa nini? Liweze kutumika na kujibiwa mbali na maswali mengine ya
nani, nini, wapi na kwa vipi?

8
c. Kuyatumia katika maisha yao, Elimu ni nguvu ya kubadili maisha ya mtu. Mtu
aliyesoma kama hawezi kuishi sawasawa na elimu yake, huyo hakusoma na hana haki
kujivuna kuwa amesoma.

Sheria ya marudio na matumizi.


Matokeo ya somo kuwa limeeleweka vizuri ni kufaulu kwa mitihani na ushuhuda wa
wanafunzi, lakini lipo hitaji la:
a. Kurudia rudia, Kuwaza tena, Kujua zaidi, Kuunda tena, Na kutumia yale mambo
maishani.

Sheria itafaulu ikiwa:


a. Kutatiliwa nguvu na kukamilisha ufahamu, Biblia kama hazina ya kweli zetu ni lazima
kurudia rudia mpaka iingie maishani.
b. Kukumbuka na kutilia elimu mhuri, mawazo yanatakiwa yaunganishwe na mengine kila
mara-Ongeza matendo na kuunda tabia.

KIPENGERE CHA SITA: UKUSANYAJI WA HABARI ZA KUFUNDISHA.


Lengo: 1. Mwanafunzi ajue vyanzo vya mafundisho yake ninini?
2. Umakini unahitajika katika kuchagua nini kifundishwe.

a. KUSANYA TOKA KWENYE BIBLIA.


 Msingi wa mafundisho yote.
 Ndiyo mamlaka ya mafundisho yako.
 Tafsiri bora ya Biblia ni Biblia yenyewe. (Biblia inajilinganisha, andiko hili
linajirudia katika kitabu kingine cha Biblia au sura nyingine katika kitabu hicho
hicho.

b. KUSANYA TOKA KWENYE ITIFAKI ZA BIBLIA.


Itifaki ninini?
 Ni kitabu kinachokusanya maneno makubwa ya Biblia.
 Inaweza pia kutoa maana ya maneno na maneno na mambo yanayohusiana na kila
neno.

c. KUSANYA TOKA KWENYE KAMUSI ZA BIBLIA.


 Kamusi ya Biblia hutoa habari kuhusu matukio, watu, mahali, na maneno
yanayotumika kwenye Biblia. (Mwalimu awapeleke wanafunzi maktaba kufanya
zoezi hili)

d. KUSANYA KUTOKA KWENYE VITABU VINGINE VYA MAONI KUHUSU


BIBLIA.
 Husaidia kuelewa sehemu ngumu za Biblia

Angalizo.
9
Vitabu hivi visiwe jawabu la mwisho kuhuso Biblia kwa sababu walioandika ni watu tena watu
wa karne yetu-wasomi.

e. MWONGOZO KWA MWALIMU NA VIFAA VINGINE MSAADA.


 Mwongozo wa mwalimu huongozea elimu yako.
 Mwongozo huu unahitaji kutumiwa pamoja na Biblia, usiwe badala ya Biblia.

f. KUKUSANYA KUTOKANA NA MAMBO YA KISASA.


 Mfano- majarida, magazeti, redio, televisheni, maisha ya wanafunzi, maktaba za
serikali, maduka ya kanda za sauti na video, mashirika mengine ya makanisa.

MAANDALIZI YA MWALIMU
1. Kusoma hayo yaliyotajwa hapo juu.
2. Kukusanya vielelezo- hadithi, picha, mifano, ili yakusaidie kupanga masomo yako ya
mbele.
a. Panga masomo na kuyaandaa kabla ya kufikia muda wa kufundisha ikiwa ni pamoja
na zana/ vielelezo vya kufundishia.
b. Kutana na mahitaji ya kila mwanafunzi.
 Ujue mahitaji ya darasa lako
 Mjali kila mwanafunzi wa darasa lako.
Mfano : andaa picha za kutosha au picha kubwa, ramani/ mchoro utakaomwezesha
kila mwanafunzi kujifunza.
c. Kutana na mahitaji yako binafsi.
 Mwalimu anatakiwa kukua kiroho na kiakili.
 Hivyo mwalimu hana budi awe msomaji wa vitabu kwa utaratibu.
 Kuwa mwombaji na kuombea kazi yako ya ualimu.

3. KUSANYA MAMBO YA KUFUNDISHA.


1. Chora michoro ya kiakili.
Uwe mbunifu wa michoro ya kiakili ili kuwavutia wanafunzi wako (mfano mchoro
wa ndege anayeruka, mchoro wa pembe tatu, nyumba nk.
Fumba macho yako tafakari mandhari unayofundishia na watu waliokua wakisoma
juu yako.
2. Weka somo lako katika maandalizi-maandishi yanahifadhi maarifa kuliko
kutokuandika.
3. Anzisha faili la kutunza masomo yako:
a. Weka picha.
b. Malengo ya masomo.
c. Masomo yenyewe.
d. Kazi za wanafunzi.

KIPENGERE CHA SABA: VIFAA VYA KUKUSAIDIA KUFUNDISHA

10
Lengo: Mwalimu anahitaji msaidizi wakati mwingine hueleza mambo ambayo mwalimu halisi
asingeeleza.

1. VIFAA VYA KUCHOREA PICHA


a. Vifaa vya kutumia masikio.
Sauti ni kifaa muhimu kwa mawasiliano na vyombo vinavyotoa sauti- mfano: vinanda
vya santuri.
b. Vifaa vya macho.
Huwafikia wanafunzi kwa kutumia macho na masikio, maarifa huingia ndani ya akili
za wanafunzi kwa njia zote mbili macho na masikio.
c. Ufundishaji mzuri ni ule wa kuingiza somo katika akili za mwanafunzi kwa njia
nyingi zaidi au kwa kutumia milango yote mitano ya maarifa: Kuona, Kusikia,
Kugusa, Kuonja, Kunusa.
Vifaa hivyo ni vingi mfano—Ramani, picha, matangazo,mbao za kuandikia, chati,
mwanasesere, Tv, video, filamu, ujenzi wa miundo mbalimbali wa matukio- mfano
unaweza kujenga sakafuni mji wa Yerusalemu, sanamu, sanamu aliyoiona Danieli juu
ya falme mbalimbali nk.
d. Vifaa vya kujieleza — wanafunzi hupewa kazi ili wapate nafasi ya kukaa mbele ya
darasa naye akijieleza.
a. Huyu humsaidia mwalimu kujua ni kiasi gani wanafunzi wameelewa.
b. Hujenga moyo wa mwanafunzi kujiamini, kuwa mbunifu, na kuwa mdadisi, kuwa
msikivu sana wakati mwalimu akifundisha
c. Kazi hii ya kujieleza kwa mwanafunzi huonekana zaidi:
 Mwanafunzi anapojieleza mbele ya darasa.
 Katika daftari yake ya kujibia maswali.
 Katika kazi za mikono, kutenda, kupapasa.

UTAFITI
Watafiti wa ualimu wamegundua viwango vya mwanafunzi vya kukumbuka.
Anaposikia hukumbuka 10% yale aliyosikia.
Anapoona anakumbuka 50% yale aliyoyaona.
Anapofanya anakumbuka 90% yale aliyoyafanya.
Anaposema hukumbuka 70% yale aliyoyasema.

Hivyo ni muhimu ziwepo kazi za mikono zitakazofanywa na wanafunzi ili fundisho lako lipate
kueleweka na kukumbukwa na wanafunzi.

KIPEMGERE CHA NANE: KUPANGA SOMO.


Lengo: 1. Ili kuboresha kazi ya kufundisha ni lazima mwalimu agharimie muda na mazoezi
2. Kuzifahamu mbinu za kufundisha.
3. Mpango namna ya kufundisha.
4. Uwezo wa kutoa na wa kukusanya.
5. Kuwa tayari kubadili kidogo kulingana na hali ya wanafunzi wake.

11
NJIA ZA KUPANGA SOMO.
A. Hutegemea akili za mwalimu. Akili bora inatakiwa.
1. Chukua habari tu zinazofaa kufundishwa.
2. Uunganishaji wa habari toka maeneo tofauti tofauti, toka vyanzo tofauti.
3. Fundisha toka yanayojulikana kuelekea yasiyojulikana.

B. Kupanga kwa utaratibu wa miaka:


-Mafundisho ya Biblia hufundishwa kwa utaratibu wa hatua kwa hatua.
-Mwanadamu ana kiwango cha kutambua mambo kufuata akili ya kizazi hicho na miaka.
-Mungu pia amejifunua kwa mwanadamu hatua kwa hatua.
- ufahamu wa mwanadamu hutofautiana kufuatana na umri, aina ya kizazi kilichopo.

C. Kupanga somo kufuata uwezo wa akili na ujuzi wa mwanafunzi.


 Fundisha ukweli wa Biblia ule ambao unafikiri watauelewa
 Ukweli uliomgumu acha kuufundisha mpaka uwezo wao utakaporuhusu.
 Tilia mkazo mahitaji ya wanafunzi na uwezo wao wa kuelewa.
Angalizo.
Mwisho wa somo kufundishwa ndio mwanzo ndio mwanzo wa maandalizi ya somo
litakalofundishwa kesho au juma linalokuja.
a. Mwalimu lazima awe na mtaala wa masomo yake.
Mtaala ninini?
Mtaala ni mtiririko wa masomo yanayotakiwa kufundishwa kipindi hicho.
Mfano: Masomo ya shule ya jumapili, kuna masomo ya miezi sita-sita kwa mwaka.
-Pia huonyesha mipaka ya kukoma yanapofundishwa.
-Hivyo huandaa kulingana na maelekezo ya mitaala.

b. Kusudi la somo likishawekwa bayana ni rahisi kuamua mambo gani yatiliwe mkazo.
Kwa mfano: Mwalimu lazima awe makini Ukweli anaoutaka ukae ndani ya akili za
wanafunzi
 Kichwa cha somo.
 Sehemu za Biblia zinatakiwa kukumbukwa.
 Vidokezo vya somo.

c. Uchague njia utakayotumia kufundisha, fundisha moja au zaidi na mambo ya kufundisha.


 Uchaguzi wako utaangalia umri wa wanafunzi.
 Yaliyomo katika somo—mara nyingi mwalimu anashauriwa kutumia njia tofauti
tofauti ili kuwasilisha masomo yake kwa njia yenye manufaa.
Dokezo.
Muda mwingi unahitajika ikiwa njia za kufundishia zitawahusisha wanafunzi—mjadala,
vikundi vya majadiliano, Ripoti, michezo ya kuigiza, safari za kujifunza.

d. Hakikisha somo lako linahusisha maisha binafsi ya mwanafunzi (maswali,mafafanuzi na


matumizi)

12
MPANGO WA SOMO:
a. Jina la somo
b. Tarehe.
c. Andiko la somo
d. Mstari wa kukumbukwa (mstari wa msingi)
e. Kweli kuu.
f. Lengo la somo.
g. Vidokezo vya somo.
h. Jinsi utakavyoshughulika na darasa (unda hali bora ya kusoma darasani)
i. Maendeleo ya darasa (njia za kufundisha, vifaa vya macho na masikio — mfano:
Projecti, maswali na mafafanuzi.
j. Mwitikio (jambo ambalo wanafunzi wanaweza kufanya kuonyesha uelewa wao.
k. Kazi za nyumbani kwaajili ya somo litakalofuata— mfano: kusoma mistari fulani ya
Biblia au kumweleza mhusika katika habari itakayokuja katika somo linalofuata.

KIPENGERE CHA TISA: NIDHAMU BORA


Lengo: 1. Darasa liwe na nidhamu, darasa likue kiroho.

Darasa lolote litaweza kufanikiwa ikiwa litakuwa na nidhamu bora.


Maelezo: Nidhamu bora ni utaratibu mwema ambao mwanzilishi ni Mungu mwenyewe.
1Kor 14:40 =Mambo yote yatendeke kwa uzuri na utaratibu.
Ili kufanikisha somo hili mwalimu ni lazima:
1. Kutoa mwongozo (utaratibu mwema kusambaa na ukosefu wa nidhamu pia husambaa)
a. Vifaa darasani vikae kwa utaratibu. — vifaa vya kufundishia viwe bora mfano —
Projecti kupangwa vizuri, Asiwepo mwanafunzi ambaye kazi zake zinafanywa na
kupangwa ovyo ovyo, kazi za wanafunzi zivutie.
b. Darasa lipangwe vizuri na viti vyake —wanafunzi wafupi wakae mbele na wafuatiwe
na warefu kidogo na warefu kuliko wakae nyuma ili kila mmoja aweze kuona mbele.
c. Eneo la ufundishaji kusiwepo kelele ambazo sio za lazima—Hakikisha kelele za ndani
na nje ya darasa zinadhibitiwa.

2. Mwalimu awe mfano wa kuigwa na wanafunzi wake.


a. Mwonekano wake wa nje, mavazi, nywele, kiatu, usafi kwa ujumla.
b. Mwonekano wake wa ndani.
 Kiasi (self control) au kujitawala/ kujimiliki.
 Mwalimu aongozwe na Roho mtakatifu.
 Kuwa na tunda la Roho mtakatifu (Gal 5:22)

3. Mwalimu awe na bidii ya kujiendeleza kielimu ili awe na moyo wa kujiamini na


kumtumaini Mungu katika kazi yake.
Mara nyingi ujasiri wa kufundisha somo hupungua ikiwa mwalimu atajihisi kuwa somo
hajalifahamu vizuri.
Hivyo mwalimu hakikisha umesoma vitabu vingine kuboresha ufahamu wako
(kujiendeleza katika yale unayofundisha) hisia mbaya kuwa hukuitwa kuwa mwalimu

13
wakati mwingine husababishwa na kujua kidogo na kutomshirikisha Roho mtakatifu
katika kazi ya ufundishaji.
4. Mwalimu ahakikishe anafanya maandalizi ya somo lake— Mwalimu anatakiwa kuwa
hodari katika kuwaongoza wanafunzi katika somo/ masomo yale anayofundisha kwa
uzuri na mvuto wa kutosha.
Angalizo:
Wanafunzi wanaweza wakawa sababu pia ya kutofanikisha somo lako:
Shida za wanafunzi binafsi:
Kufanya mambo kinyume, kutotulia darasani, matendo ya kutokuwajali wengine,
kutokuwa makini na masomo.
5. Kuboresha nidhamu:
a. Kuelewa kusudi la nidhamu—ambayo hulenga kukuza vipawa vilivyo vyema—
Mfano kuwaongoza wanafunzi kumjua Mungu zaidi, Kusababisha kuwa
wanyenyekevu na uadilifu kwa wanafunzi wote.
Hulenga kurithisha maadili mema toka kizazi hadi kizazi.
Hulenga wanafunzi kumfanania Yesu Kristo ambaye ndiye chanzo cha utaratibu,
Kumbuka ni wa utaratibu. Hufanya sahihi, Kwa wakati sahihi na Kwa watu sahihi.
Kitakachofanya wanafunzi wafanye sahihi kwa wakati sahihi, kwa watu sahihi ni
NIDHAMU chini ya uongozi wa Roho mtakatifu.
b. Weka msingi wa nidhamu, kuwapenda wanafunzi-Kuwajali-kukutana na mahitaji yao
katika mafunzo, Kukuza uwezo wako, Uwe wazi kwa wanafunzi nini unachowataka
wafanye na tabia gani inayotakiwa.
c. Usiwabague wanafunzi— kama wapo wenye shida shughulikia msingi wa shida hiyo
ikiwezekana uimalize— Shida za darasa ni pamoja na utulivu, kuasi, zogo nk.
Shida za ndani, roho zao au ukristo wao haujakaa vizuri.
d. Himiza sana uhusiano mwema—wanafunzi lazima wapendwe na kukubaliwa jinsi
walivyo, Mtu akibadilika ndani huwa mtu mzuri sana, onyesha shauku kubwa ya
kuwasaidia.
e. Waalimu wa kutosha ni moja ya kudumisha nidhamu ya wanafunzi—Mwalimu
mmoja asiwe na wanafunzi wengi kiasi kwamba hushindwa kuwasaidia wengine na
kusababisha zogo.
f. Mwalimu ni lazima kuwaombea wanafunzi wako (panga, fanya bidii, kufundisha na
kuwaombea kwa uaminifu)
g. Mwalimu ni vizuri kupima na kukagua uelewa wa wanafunzi kupitia:
Majaribio, Maswali, Kazi za nyumbani, Projecti, Mitihani nk.
Angalizo
1. Ufundishaji mzuri husababisha maisha ya wanafunzi.
2. Kumjali mwanafunzi, mpango wa ufundishaji kila unapofundisha na nguvu za
Roho mtakatifu na bidii ya mwalimu, ni muhimu sana katika ufundishaji.
3. Kushirikisha elimu kwa vitendo husaidia sana katika swala zima la kujifunza.

Mungu akubariki unapolitendea kazi somo hili.

14

You might also like