You are on page 1of 5

TABIA ZISIZOMPENDEZA

MUNGU ZINAZOFANYWA NA
VIJANA KATIKA MAHUSIANO
KABLA NA BAADA YA NDOA
Utangulizi:
Ziko baadhi ya tabia ambazo zimezoeleka na zimekomaa ambazo vijana wengi
huzifanya wengine wakiwa wanajua na wengine wakiwa hawajui kuwa ni
mbaya katika mahusiano na hazimpendezi Mungu kabisa. Miongoni mwa tabia
hizo ni kama ifuatavyo;
1. Tabia ya kukaa mda mrefu mpaka usiku wa manane.
Biblia inasema; “Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala…” Zaburi 127:2.
Roho ya unabii inasema; “Tabia ya kukaa muda mrefu hata usiku wa manane imezoeleka,lakini haipendezi Mungu,
hata kama ninyi nyote ni Wakristo.” UKV sura 149, uk. 407 aya 2.
Swali, Kwa nini Mungu hapendi kukaa hadi usiku wa manane? Roho ya unabii inasema; “Saa hizi zilizoendelea sana
huathiri afya,hufanya akili isijiandae kwaajili ya majukumu ya siku inayofuata, na zinamwonekano wa uovu.” UKV, uk.
407. pia 3T. 44,45.
USHAURI WA MUNGU KWAKO: “Ndugu yangu,ninatumaini utajiheshimu kiasi cha kutosha kuachana na uchumba wa
aina hii. Ikiwa kusudi lako ni kumtukuza Mungu,utatembea kwa uangalifu mkubwa…” 3T.44,45. UKV uk. 407 aya ya 2.
Vijana wengi leo wamejikuta katika mahusiano ya kuchati masuala ya mapenzi usiku na mchana na kupoteza muda ambao
wangeutumia kwa masomo, kazi za mikono au kwa shughuli zingine za maana.

2. Kuchangamana na watu wasio na uhusiano na Mungu.


Biblia inasema; “Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;Bali Rafiki wa wapumbavu ataumia”
Mithali 13:20; “Ndugu zangu,nawasihi,waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume na mafundisho
mliojifunza; mkajiepushe nao.” “Lakini, mambo yalivyo,nawaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye
ndugu,akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi;mtu wa
namna hii msikubali hata kula naye.” I Wakorintho 5:11.
Cont…
Roho ya unabii inasema; “Ni hatari kwa Wakristo kuchagua kuchangamana na watu wasio na uhusiano na Mungu, na
watu ambao njia zao hazimfurahishi Mungu….Wengi wanawakaribisha nyumbani kwao ndugu zao wanaopenda mambo
ya upuuzi,wanaopenda maongezi yasiyofaa na yasiyo mtukuza Mungu…..mvuto unaoletwa kwa njia hiyo una nguvu sawa
na ule uliotokea wakati Waebrania walipojichanganya na wakanaani wasiomcha Mungu.” UKV Sura 147, Uk. 402
Rejea Ezra 9:1,2 imeandikwa; “1 Na mambo hayo yalipokwisha kutendeka, wakuu wakanikaribia, wakisema, Watu wa
Israeli, na makuhani, na Walawi, hawakujitenga na watu wa nchi hizi, wamefanya sawasawa na machukizo yao,
yaani, ya Wakanaani, na Wahiti, na Waperizi, na Wayebusi, na Waamoni, na Wamoabi, na Wamisri, na Waamori.
2 Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na
watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe umetangulia katika kosa hili. Tangu zamani, Mungu amekataa
kujiungamanisha au kujichanganya na watu waio na uhusiano naye. Hapa; Vijana wengi ni wahanga katika mahusiano
ima ya kimapenzi au urafiki usiohusisha mapenzi.
3.Uchumba na wasioamini.
Biblia inasema; I Wakorintho 6: 14-18 “14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa
maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye
asiyeamini?16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu
aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu
wao, nao watakuwa watu wangu.17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho
kichafu, Nami nitawakaribisha. 18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,..”
Rejea pia sura ya 150 UKV “Uchumba na Wasio amini”
Cont…
4. Ndoa za utotoni:
Roho ya unabii inasema; “Usiwe na haraka. Ndoa za utotoni hazipaswi kuhamaishwa. Ikiwa mabinti na vijana wa
kiume hawana heshima kwaajili ya madai ya Mungu, ikiwa wanashindwa kusikiliza madai yanayowafunga na dini,
kutakuwa na hatari kuwa hawataweza kuzingatia madai ya mume na mke….Ndoa za haraka haraka hazipaswi
kuhamasishwa. Uhusiano ni wa muhimu sawasawa na ndoa yenyewe na ndoa inamatokeo yanayodumu kwa muda
mrefu na haipaswi kuingiwa kwa haraka bila maandalizi ya kutosha, na kabla ya uwezo wa akili na mwili havijakomaa
kiasi cha kutosha.” UKV Sura 149,uk. 406,407 pia The Ministry of Healing 358. Usiingie kwenye mahusiano ya ndoa huku
ukijua hujakomaa kiakili na kimwili.

5. Tabia ya kufanya urafiki na binti bila kuwahusisha wazazi. Si tendo jema Mungu anachukia. Uchumba wa
Siri haufai.

Tangu zamani uchumba wa Wazao wa wazee wetu wa Imani katika Biblia ulikuwa wa wazi bila kificho.
Roho ya unabii inasema; “Kijana wa kiume anayepata na kufurahia urafiki na binti bila kuwajulisha wazazi
wake,hatendi tendo jema Kikristo kwa binti huyo wala kwa wazazi wake. Kwa njia ya mawasiliano na mikutano ya siri
kijana wa kiume anaweza kuwa na mvuto juu ya akili ya binti;lakini kwa kufanya hivyo kijana wa kiume haoneshi
uungwana wala uadilifu wa roho ambayo kila mtoto wa Mungu anapaswa kuwa nayo.Ili kutimiza lengo lao,watenda
tendo lisilokuwa la kweli na wazi na lisilokidhi viwango vya Biblia,na kuonekana kuwa wasiokuwa wakweli kwa wale
wanaowapenda na wanaojaribu kuwa walinzi wao waaminifu….” UKV Sura 151, uk. 412,413.
Cont…
Nabii anasema; “Uchumba wa uongo unaendeshwa,na mawasiliano ya siri hufanyika, mpaka mapenzi ya binti
asiyekuwa na uzoefu,na mabaye hajui mwisho wa mapenzi hayo,kwa kiwango Fulani huhamishwa kutoka kwa wazazi
wake na kuwekwa kwa mwanaume ambaye mambo yake yanaonyesha baadaye kuwa hakustahili mapenzi yake. Biblia
inalaumu kila aina ya kukosa uaminifu, na inadai utendaji sahihi katika mazingira yote..” UKV ,uk.413 aya 3.
ZINGATIA SANA HILI; “Kama kuna suala ambalo linapaswa lifikiriwe
kwa tafakari tulivu na
uamuzi usiokuwa na msisimko, ni suala la ndoa.Ikiwa kuna wakati ambao Biblia
inahitajika kama mshauri, ni Wakati kabla ya kuchukua hatua inayounganisha watu
pamoja Maisha yao yote.” Nidhambi kuchezeana mioyo kwa kudanganyana. Mungu
hapendi ni tabia mbaya inayokuharibia utu na heshima yako.

Madai ya Mungu kwetu katika suala la mahusiano ni lipi?


Imeandikwa; “4 Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana; 9 Jinsi gani kijana
aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
Mungu hapendi Uchafu katika mahusiano yaani Uzinzi; imeandikwa; Kutoka 20:14 Usizini.
4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na
wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Msangaamos@gmail.com WhtasApp no. 0625838206.

You might also like