WIMBO:15 & 110. =Mafungu andamizi;Yoshua 24:15 ,Torati 6:6-7 ,Mwanzo 18:19 1.Kuna mambo matatu ambayo shetani hushambulia kwa nguvu na uhakika,ambayo;ndoa,sabato,matoleo (uchoyo wa kurudisha ZAKA na kutoa SADAKA) 1. Ni rahisi kuhubiri nje kuliko katika familia zetu 2. Tunapata umaarufu nje kuliko katika familia zetu 3. Yesu anataka famila zetu ziongolewe na hivyo ndivyo tutakapowavuta wengine kwa Yesu =Mungu kupitia watumishi wake anahitaji matengenezo makamilifu na jukumu hilo takatifu la utume wa familia limekabidhiwa kwa wazazi.Hao watatoa hesabu kwa ajili ya ukengeufu wa familia zao. =BWANA ameshushwa na kuvunjiwa heshima na wasioamini kwa ajili ya mienendo mibovu ya familia zetu =Shetani anajua kama familia zitajiweka imara katika kumtafuta MUNGU wengi wataongolewa na kwamba atakosa mtu wa kumpoteza. ROHO YA UNABII
=Wale ambao wanafuata mielekeo yao wenyewe,katika upendo wa
kizembe kwa watoto wao,wakiwaendekeza katika kupenda tamaa zao za ubinafsi, na wala hawatumii mamlaka ya Mungu kukemea dhambi na kusahihisha uovu,wanadhihirisha kwamba wanawaheshimu watoto wao walio waovu kuliko kumheshimu Mungu.Wana hamu zaidi ya kukinga hadhi zao kuliko kumtukuza Mungu,wanatamani zaidi kuwapendeza watoto waokuliko kumpendeza BWANA na kutunza huduma Yake kutoka katika kila mwonekano wa uovu (Wazee na Manabii,Uk 229). -Mfano wa wale wanao hudumu katika mambo matakatifu unapaswa kuwa ni ule ambao unawavutia watu kuwa na kicho kwa Mungu na hofu ya Kumkosea (wazee na manabii uk 231) -Hajuna laana kubwa juu ya kaya kuliko kuruhusu vijana kufanya watakavyo.Wakati ambapo wazazi wanakidhi kila hitaji la watoto wao na kuwaendekeza katika kile ambacho wanajua si cha kuwafaa,punde watoto wanapoteza heshima zote kwa wazazi wao,heshima zote kwa mamlaka ya Mungu na ya wanadamu,na wanasababishwa kuwa watumwa kama shetani apendavyo.Athari za familia ambayo haikudhibitiwa vyema husambaa na kuleta hasara kwa jamii.Hujikusanya kuwa wimbi la uovu ambalo linawadhuru familia,jumuiya,na serikali mbalimbali (wazee na manabii uk 230).