You are on page 1of 3

WATAABISHAJI WA ISRAELI

FUNGU LA MWONGOZO:1WAFALME 18:17-18/TITO 1:16

WIMBO :173&110

Katika kipindi cha Eliya nabii wa Mungu Aliye hai taifa la Israeli lilipitishwa katika kipindi
cha taabu kubwa kwa muda usiopungua miaka mitatu na nusu kwa kuwa waliacha
kumtegemea Mungu Aliyewapatia mahitaji yote na kuigeukia miungu ya uongo (mabaali na
maashera).Hivyo Mungu aliwatumia muonyaji nyumba hii iliyoasi kabla ya kumwagwa kwa
hukumu juu ya taifa hilo lililoasi amri zake.

Israeli ya leo si taifa lile la kijiografia na kisiasa hapana ,bali wale wote waliomkiri Yesu
kristo ambao wamekuwa warithi pamoja na Ibrahimu kwa njia ya Yesu kristo kwa Imani.

Eliya alishutumiwa juu ya hukumu iliyomwagwa juu ya Israeli kwamba ndiye aliyekuwa
chanzo kwa kuwa alikuwa anapinga miungu yao ya uongo lakini jibu ni si ELIYA bali ni kwa
sababu wameacha SHERIA za Bwana.

Wataabishaji wa Israeli (kanisa) leo wameendelea pasipo kusikia maonyo na hivyo shetani
anawatumia kwa juhudi zote kukamilisha agenda zake katika wakati ambapo kanisa la
Mungu linapata mashambulizi kutoka ndani na nje;

 Hawana kicho katika ibada na hawataki kabisa kubadilika

“Ninajisikia vibaya ninapowaona Watoto na vijana na wazazi wenye dini ambao


hawazingatii utaratibu na utulivu ambao unapaswa kuzingatiwa ndani ya kanisa la
Mungu.Wakati watumishi wa Mungu wanapowasilisha maneno ya uzima kwa watu
baadhi wanasoma,wengine wananong’ona,na wengine wanacheka.Macho yao yanatenda
dhambi kwa kuhamisha mawazo ya wale wanaowazunguka.Tabia hii ikiruhusiwa
kuendelea bila kudhibitiwa,itakua na kwaharibu wengine”.(Ujumbe kwa Vijana,Uk 250.)

“Nyumba ya Mungu mara nyingi inanajisiwa na sabato inakiukwa na watoto wa


kiadventista.Katika mambo fulani wanaruhusiwa hata kukimbia kuzunguka
nyumba,kucheza,kuzungumza na kuonesha hasira zao mbaya…Hili linatosha kuleta
ghadhabu ya Mungu na kufunga uwepo wake kutoka kwenye mikusanyiko yetu.”(Malezi
Ya Watoto,Uk 515-516)
 Wapinzani na vikwazo kwa kazi ya Mungu

“Kwa kuwaleta kanisani wale wanaolichukua jina la Yesu huku wakikana tabia
yake,mwovu hufanya iwe lazima Mungu Adharauliwe,kazi ya injili isieleweke na roho ziwe
katika hatari ya upotevu…si lazima kuwa wote walio kanisani ni wakristo.”(Lulu za
Uzima,Uk 41-42) “Kristo Aliona wazi jinsi kuwapo kanisani kwa ndugu wa uongo
kunavyoweza kufanya ukweli usemwe vibaya.Ulimwengu ungalidharau injili kwa ajili ya
maisha yasiyoongoka ya walimu wa uongo…kwa vile hawa watenda dhambi wamo kanisani
watu watakuwa na hatari ya kufikiri kuwa Mungu anakubali dhambi”.(Lulu za Uzima,Uk 77)

 Hufanya maadili ya kanisa (waamini) kuporomoka

“Wengi wanaokiri kuwa wanakusanya pamoja na kristo wanatawanya mbalia naye.Ndio


sababu kanisa ni dhaifu sana.Wengi wanajihusisha na usengenyaji na kusahihisha
wengine.Kule kuonesha tuhuma mbaya,wivu na kutoridhika wanakuwa vyombo vya
kutumiwa na shetani…Hawaelewi kuwa hawa maskini walioanguka katika tabia,ni kazi ya
ndimi zao zisizozuiliwa na mioyo yao iliyojaa uasi.Ni kwa njia ya mivuto yao iliyowafanya
hawa wakajaribiwa na kuanguka…kutoaminiana,kukosa imani na uasi wa wazi umejisimika
kwa wale ambao,vinginevyo wangeweza kumpokea kristo.”(Lulu za Uzima,uk 240)

 Ni wezi waliojaa choyo na unafiki

“Mioyo ya wanadamu imekuwa migumu kwa sababu ya ubinafsi na kama ilivyokuwa kwa
Anania na Safira,wamekuwa wakijaribiwa kuzuia sehemu ya mauzo huku wakijifanya
kutimiza mahitaji ya Mungu.Wengi huwa wanatumia pesa kwa kufuja katika kuridhisha nafsi
zao…Dhambi hiyo hiyo imekuwa ikirudiwa katika historia ya kanisa na leo inatendwa na
watu wengi sana…Mungu ameonesha chuki yake dhidi ya dhambi hii,na wote waliojitoa
kuwa wanafiki na wenye tamaa,waelewe hakika wanaangamiza roho zao
wenyewe.”(Matendo ya Mitume ,uk 63-64,sehemu ya kwanza kiswahili)

 Hawazai matunda yapasayo toba na hawana badiliko lolote katika mioyo yao (isaya
30:9-10)

“Wachungaji wanahubiri mambo laini ili kuwapendeza wale wenye mioyo ya asili isiyo
badilika.Hawathubutu kumhubiri Yesu na ukweli ukatao wa biblia;kwa maana kama
wakifanya hivyo,hawa wenye mioyo isiyobadilika hawataendelea kuwa kanisani.Lakini kwa
vile wengi wao ni matajiri,lazima waendelee kuwemo ingawa hawafai kuwemo kuliko vile
shetani na malaika zake wasivyofaa.”(maandiko ya Awali,uk 230)

 Wamejaa mizaha

 Wenye kiburi na kiburi cha uzima

 Wanafungamana na ulimwengu

 Wamejaa unafiki

 Hawatoi zaka wala sadaka

 Wasio na maadili ya kikristo

 Wasiotaka maonyo

You might also like