Professional Documents
Culture Documents
WIMBO:172/171
FUNGU:TITO 1:16
“Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu,bali kwa matendo yao wanamkana,ni wenye
machukizo,waasi,wala kwa kila tendo jema hawafai.”
“Matokeo ya kujua tu maneno ya dini pekee yake huleta chuki kwa wale walio na
imani ya kweli.Sura yenye giza zaidi ni ile inayohusu maasi makuu yaliyotokana na
wenye dini…Watu wengi hujidai kuwa ni wenye dini,lakini dini yao hiyo
isipowafanya kuwa waaminifu hasa,wenye utu
wema,wavumilivu,wastahimilivu,wenye mawazo ya Kimungu,huwa laana kwao
tu,na kwa mivuto yao huwa balaa kwa ulimwengu.”(Tumaini La Vizazi Vyote
UK,166-167)
2TIMOTHEO 3:5 “Wenye mfano wa utaua lakini wakikana nguvu Zake hao nao
ujiepushe nao.”
LUKA 18:9-13 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye
haki,wakiwadharau wengine wote.Watu wawili walipanda kwenda hekaluni
kusali,mmoja farisayo na wa pili mtoza ushuru.Yule farisayo akasimama akiomba
hivi moyoni mwake;Ee MUNGU nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu
wengine,wanyang’anyi,wadhalimu,wazinzi,wala kama huyu mtoza ushuru.Mimi
nafunga mara mbili kwa juma,hutoa zaka katika mapato yangu yote.Lakini mtoza
ushuru alisimama mbali,wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni,bali
alijipiga piga kifua akisema ,Ee MUNGU uniwie radhi mimi mwenye dhambi.”
“Dini ya farisayo haigusi roho.Hatafuti kuwa kama MUNGU katika tabia yake,moyo
uliojawa na upendo na rehema.Analotaka ni dini ihusikanayo tu na mwonekano wa
nje.Haki yake ni ya kwake mwenyewe binafsi matunda ya kazi zake mwenyewe na
zikipimwa kwa vipimo vya kibinadamu…Farisayo na mtoza ushuru huonesha
makundi makuu mawili ya wale wanaokuja kumwabudu MUNGU.”(Lulu Za Uzima
UK,98-99)
“Kuna wengi leo ambao wako katika udanganyifu unaofanana na huo,kwa maana
huku wakiwa na mwonekano wa utakatifu mkuu,sio watendaji wa neno la
Mungu.Nini kinaweza kufanyika ili kuwafungua macho watu hawa wanaojidanganya
wenyewe isipokuwa kuwadhihirishia ,mfano wa ucha Mungu wa kweli na sisi
wenyewe tusiwe wasikiaji tu bali watendaji wa amri za Bwana,hivyo kuakisi nuru ya
usafi wa tabia kwenye njia yao.”(Imani Na Matendo UK,117)
WITO
“Tunahitaji kuongoka kama walivyofanya wayahudi.Kama ukiona nuru
ndogo,hupaswi kurudi nyuma na kusema,nitasubiri mpaka ndugu zangu wawe
wameiona.Kama ukifanya hivyo utaendelea kuwa gizani.”( Imani Na Matendo UK,78
)
“Injili haifanyi maafikiano na uovu.Haiwezi kutoa udhuru kwa dhambi.Dhambi za
siri lazima ziungamwe kwa Mungu kwa siri;bali kwa dhambi za wazi toba ya wazi
huhitajika.”(Tumaini La Vizazi Vyote UK,458)