You are on page 1of 2

ANZA SIKU NA BWANA.

#0003

SOMO: MUNGU NI UPENDO

Mungu ni Sheria, Kama hakuna Mungu hakuna Sheria.

ISAYA 42:21-22 “Bwana akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.
Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika
magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye,
Rudisha.”

UFUNUO 22:14“Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini
kwa milango yake.”

Mpendwa wa Mungu, shetani hajabadilika na silaha zake ni zilezile; na jambo kubwa linaloshangaza
watu ni kwamba silaha za shetani ni zilezile lakini bado zinatenda kazi kwenye maisha ya watu. Moja ya
kifungo kinachosumbua watu ni kifungo cha tabia.

Shetani ameteka watu wengi, wengine wamegeuza amri za Mungu kwa manufaa yao wenyewe, hii
imekua mbinu moja shetani ametumia kuteka na kufunga watu wa Mungu.

Kuna vitu viwili kwenye Ufalme wa Mungu

1. Vile vya mwisho ambayo vina sifiwa

2. Na vile bila mwisho ambayo vina tukuzwa kama Jina la Bwana Yesu Kristo lina tukuzwa.

Kuna AMRI KUMI ambazo zinapaswa kutukuzwa, sheria za Mungu zinapaswa kutukuzwa

Mungu ni Sheria, kama hakuna sheria, hakuna Mungu.

Adamu alifikiri hakuna sheria alikula tunda, lakini Mungu alimpa adhabu.

Watu wamekata kutii AMRI KUMI za Mungu, wanafata sheria na mashariti ya Shetani.

Ukikataa Amri za Mungu lazima Shetani atajiwekeza za kwake ndani yako.

Sheria za Mungu ni pamoja na amri kumi. Kutoka 20:1-17

Je! kiini cha sheria ni nini? Imeandikwa, Warumi 13:10 "Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo
ndilo utimilifu wa sheria."

Sheria za Mungu ni upendo. Imeandikwa, Mathayo 22:37-40 "Akamwambia mpende Bwana Mungu
wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote hii ndiyo amri iliyo kuu tena ni
ya kwanza na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii mpende jirani yako kama nafsi yako katika amri hizi
mbili hutegemea torati yote na manabii."

Hata ukisema umeshika amri kumi bila upendo ndani yako unajidanganya.
Je! Twaweza kumjua Mungu bila kutii sheria?. Imeandikwa, 1Yohana 2:4-6 "Yeye asemaye nimemjua
wala hazishiki amri zake ni mwongo wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye aliyeshika neno lake
katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli katika hiyo twajua tumo ndani yake. Yeye
asemaye ya kuwa anakaa ndani yake imempasa kunenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda."

Umuhimu wa sheria ni upi? Imeandikwa, Warumi 3:20 "Kwa sababu hakuna mwenye mwili
atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana akutambua dhambi huja kwa njia
ya sheria."

Je! Twaokolewa kwa kutii sheria?. Imeandikwa, Warumi 3:27-31 "Ku wapi basi kujisifu? kumefungwa
nje. kwa sheria ya namna gani? kwa sheria ya matendo? la bali kwa sheria ya imani basi twaona ya kuwa
mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi
tu? siye Mungu wa mataifa pia; kama kwa kweli Mungu ni mmoja; atakayewahesabia haki wale
waliotahiriwa katika imani nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo. Basi
Je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? hasha! kinyume cha hayo twaidhibitisha sheria."

Bwana Yesu Kristo ametuma watumishi wake wakutowe kwenye mitengo, umetekwa kwa mda,
umefungwa kwa mda, Shetani amekudanganya vyakutosha. Utayari wako leo na kuchoka kwako
kutumika na shetani utakufanya kumpokea mtumishi wa Mungu kwajili ya kukufungua.

ISAYA 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri
wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru
wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.”

UFUNUO 3:12 “Wale wanaoshinda nitawafanya wawe minara katika Hekalu la Mungu wangu, na
hawatatoka humo kamwe. Pia nitaandika juu yao jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu,
yaani Yerusalemu mpya, mji ambao utashuka kutoka juu mbinguni kwa Mungu wangu. Tena nitaandika
juu yao jina langu jipya.”

“ Amen”

Ni mimi ndugu yako;Kuhani na Mwl. Harrison Humphrey Mushenyera.


Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa msaada zaidi na ushauri.
whatsap +255 768522999.
harrisonhumphrey25@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba unisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu

You might also like