Professional Documents
Culture Documents
Kozi Ya Msingi Ac-1
Kozi Ya Msingi Ac-1
[MASTERGUIDE MAFUNZONI]
MAGESA MASATU
KIONGOZI WA TAALUMA
KANDA YA MBEYA MAGHARIBI
SOUTHERN HIGHLAND CONCEFERENCE (SHC)
1
KOZI YA MSINGI YA WAVUMBUZI KWA MASTER GUIDE MAFUNZONI
UTANGULIZI
Katika hatua za awali za uanzishwaji wake, Kanisa la Waadventista Wasabato halikuwa na
muundo maalumu wa huduma za vijana.Pamoja na kuwepo kwa vijana waliofanya kazi kubwa
ya injili kama James white, John Loughborough, na Ellen Harmon.Vijana hawa waliamua
wenyewe kwa msukumo wa Roho Mtakatifu ndani yao kuwashirikisha wengineukweli
walioupata kutoka katika Neno la Mungu. Kanisa lilivyoendelea kukua, Mpango wa Mungu wa
kuwachagua vijana kuwa mkono wake wa msaada ulifunuliwa kwa watu wakie na hivyo Idara
ya huduma za Vijana ikaanza.
2
SEHEMU YA KWANZA
HISTORIA YA WAVUMBUZI
Wazo la kuwa na Chama cha wavumbuzi lilianza kwa kuanzishwa madarasa manne (4) ndani ya
chama cha JMV na chama kiliitwa Pre-JMV. Madarasa haya yaliitwa Pre-JMV Classes.
Madarasa haya yaliyoanzishwa mwaka 1930 na aliyekuwa Mkurugenzi wa JMV wa GC ndugu
C. Lester Bond yalikuwa ni Busy bee (nyuki wa Shughuli), Sunbeam (Mwali wa Jua), Builder
(Mjenzi), na Helping hand(Mkono wa Msaada).
Madarasa yalikuwa na masomo ya kujifunza Biblia, masomo ya afya, kanuni za maburudisho,
viumbe vya asili na mtoto kujitambua yeye ni nani na mchango wake katika familia yake.
Mwisho wa mwaka vijana hawa walihitimishwa kwa kupewa pini maalumu, skafu na slides.
Lengo lilikuwa ni kukuza nguvu ya uhusiano kati ya watoto na wazazi na kuwezesha kuwepo
kwa maendeleo ya mtoto kiroho, kiakili , kimwili na kijamii.
Mwaka 1939 - Konfensi kuu ya ulimwengu (GC) iliidhinisha rasmi wazo hili la kuwa na
madarasa ya haya ya Nyuki wa Shughuli, Mwali wa Jua, Mjenzi na Mkono wa
Msaada.Madarasa haya yalifundishwa kama sehemuya mtaala wa shule za kanisa hasa
kipengele cha mambo ya kiroho au ibada.
Mwaka 1972 - Washington Conference ilifadhili chama cha watoto kilichoitwa
“Beavers”“ chini ya uongozi wa Carolee Riegel .
Mwaka 1975 - North-eastern Conference ilitolewa taarifa ya kuwa pia na programu za
vyama vya watoto.
Mwaka 1979 - Jina la Pre-JMV lilibadilishwa na kuitwa Adventurers (Wavumbuzi).
1980’s - Hadi kufikia miaka hii conference nyingi zilikuwa na vyama vya watoto
vikiendelea kufanya kazi ya malezi na makuzi.
Mwaka 1988 - Division ya North America, Idara ya watoto ilitoa mwaliko kwa Conference
mbalimbali na wataalamu wa watoto kusoma na kutathmini wazo la kuwa na chama cha
wavumbuzi.
Mwaka 1989 - Kamati ya wajumbe 20 ilikutana kuhuisha mtaala wa wavumbuzi na
kutengeneza tuzo za wavumbuzi, na kuandaa mwongozo wa kuongoza chama cha
wavumbuzi.
3
Kamati hii iliwahusisha wakuu wa shule ya sabato, walimu, waratibu wa huduma za watoto
katika Conference na union, wataalamu wa mambo ya watoto na familia. Chini ya Mwenyekiti
ndugu Norman Middag, Kamati hii ilkwa na wajumbe wafuatao; Debra Brill, Terry Dodge,
Sarah Fanton, Merril Fleming, Joyce Fortner, Donna Habenicht, Jasmine Hoyt, Noelene
Johnsson, Kathie Klocko, Barbra Manspeaker, Kathy Martin, Dixie Plata, Julia Raglin, Toin
ShobeHarrison, Emily Tillman, Claude Thomas, Ruth Walker, Al Williamson na Bob Wong.
Mtaalamu wa Wavumbuzi uliandikwa na Teresa Reeve.
Mwaka 1989 - Chama cha Wavumbuzi kinatambulika rasmi na Konferensi kuu baada
ya mtaala, mwongozo na tuzo kukamilika.
Mwaka 1990 - Programu za wavumbuzi kwa majaribio zinaanza katika Division ya America
Kaskazini (North America (NAD).
Mwaka 1991 - Mwongozo mpya wa utawala wa wavumbuzi (administrative manual), na
tuzo za wavumbuzi (adventurer award) ukaanza. Mwongozo wa tuzo ulitolewa katika lugha
nne(4).
Mwaka 1992 - Programu za Wavumbuzi zinapitishwa rasmi na Konferensi Kuu ya
Ulimwengu kutumika katika makanisa yote katika ulimwengu wa Kanisa la Waadventista
Wasabato.
Mwaka 1993 - Chama cha Wavumbuzi kinatambulika rasmi katika Division ya America
Kaskazini(NAD) baada ya programu zake kuidhinishwa na GC
Mwaka 2000 - Konferensi Kuu ya Ulimwengu inapiga kura ya kumwezesha Mkurugenzi wa
Wavumbuzi kuwa sehemu ya wajumbe wa Baraza la Kanisa.
Mwaka 2016 -Madarasa mawili (2) ya little lamb –miaka 4 na Eager Beaversmiaka 5
yanaongezwa katika huduma za wavumbuzi
Mwaka 2016 - Nembo mpya ya wavumbuzi, na skafu, inaanzishwa kuonyeshwa umuhimu
wa huduma za wavumbuzi kushirikiana na wazazi kwa ukaribu.
Mwaka 2021 - Mwongozo mpya wa Mkurugenzi wa Wavumbuzi unatolewa na Konferensi
kuu (Adventurer Director’s Manual), jina Early Bird limepitishwa kutumika badala ya Eager
Beavers kwa watoto wa miaka 5.
4
FALSAFA NA MAKUSUDI YA CHAMA CHA WAVUMBUZI
I. FALSAFA
Chama cha wavumbuzi ni huduma inayodhaminiwa na Kanisa la Waadventista Wasabato iliyo
wazi kwa watoto wa miaka 4-9. Ni maahli ambapo kanisa, shule, familia zinaungana pamoja
kuisaidia kukua katika hekima na kimo kwa mtoto akimpendeza Mungu na wanadamu Luka
2:52.
Programu zao zimeundwa kumsaidia mzazi katika jukumu lake muhimu la kuwa Mwalimu wa
kwanza na mwinjilisti kwa mtoto wake. Kupitia programu za wavumbuzi kanisa, familia na
shule zaweza kufanya kazi pamoja kumwezesha mtoto kukua akiwa na furaha.
Huduma za wavumbuzi ni huduma za kifamilia. Falsafa kuu ya wavumbuzi ni kujenga huduma
ya mahusiano ya kifamilia kwa kuhakikisha ya kuwa wazazi wanahusishwa na kuunga mkono
Shughuli za wavumbuzi.
II: MAKUSUDI
Chama cha wavumbuzi kinatayarisha programu mbalimbali ili kumwezesha mtoto kukabiliana
na changamoto za kuwa mfuasi wa Kristo na hivyo chama kitahakikisha kufanya yafuatayo:-
a) Kuendeleza tabia ya kristo ndani ya mtoto
b) Kupata uzoefu wa furaha na kupata utosherevu wa kufanya vitu vizuri
c) Kuonyesha pendo lao kwa Yesu katika hali halisi
d) Kujifunza michezo mizuri na kuimarisha uwezo wao wa kuwa na wengine
e) Kugundua uwezo waliopewa na MUNGU na kujifunza namna ya kuutumia kwa faida yao na
kuwahudumia wengine
f) Kugundua ufahamu wao waone kitu gani kinafanya familia kuwa imara
g) Kugundua Dunia/ulimwengu wa Mungu jinsi ilivyoumbwa na kwa nini
h) Kukuza uungwaji mkono wa wazazi kwa mafunzo ya watoto wao.
6
SEHEMU YA PILI
MUUNDO WA CHAMA
Mkurugenzi
Mshauri Mshauri
Darasa la I na II Darasa IV na V na
na III 4 hadi 6 VI 7 na 8 na 9
7
KANISA KUBWA
Kanisa
Shule ya sabato
Wazazi Shule
Mkurugenzi
Staff Staff
Darasa la I na II Darasa IV na V na VI
na III 4 hadi 6 7 hadi 9
MAHITAJI YA UANACHAMA.
Akubali kushiriki katika shughuli za chama cha wavumbuzi ikiwemo nishani, ziara mbali
mbali na mikutano ya chama.
10
SEHEMU YA TATU
UONGOZI:
Viongozi wanao chaguliwa kufanya kazi na vijana tabia zao zinapaswa kuangaliawa.
ii. Washauri
iv. Waelekezaji
11
-Ahudhurie mikutano ya mashauri ya watoto, Semina za watoto zinazoendeshwa na
kanisa,conference, Unioni katika kuwahudumia watoto.
MKURUGENZI WA WAVUMBUZI.
a. Ni mwenyekiti wa chama.
e. Abebe majukumu.
12
MKURUGENZI MSAIDIZI WA CHAMA.
-Maburudisho.
KARANI WA CHAMA.
Ndiye mtunza kumbukumbu zote za chama. Atachukua kazi ya mhazini kama hayupo.
MAJUKUMU YA KARANI.
13
Kutunza Maktaba ya chama na usomaji vitabu.
MHAZINI WA CHAMA.
WAJIBU WAKE.
MSHAURI WA KIKOSI.
MAJUKUIMU YAKE.
MWELIMISHAJI/ WALIMU.
-Majukumu ni kufundisha mambo yote muhimu katika madarasa na onesha misingi yote ya
kanisa.
-Anapaswa afanye kazi karibu zaidi na waratibu wa madarasa kila anacho taka kufundisha na
ahakikishe anatimiza matakwa ya madarasa.
Kutoka 18:1 -
i. Ampende Mungu kwa kiwango cha juu. (Awe mtu wa Kiroho)
ii. Awapende watoto kwa vitendo.
iii. Awatumikie kwa moyo na Kipawa Kinachotamaniwa na Mbingu.
15
iv. Awe mwenye kutawala hisia, kujiheshimu na kuwa na kiasi.
v. Apende mambo ya nje, kwa kuwa ndizo shughuli za watoto zilizo nyingi.
vi. Ajue tabia za watoto.
vii. Mwenye kujielimisha katika fani mbalimbali, ajifunze kutoka kwa wengine.
(Mwenye kupenda kusoma vitabu na kutafiti mambo)
viii. Mwenye uwezo wa Kuongoza (Kiongozi Bora).
ix. Awe na malengo makubwa aanze na yaliyo rahisi.
x. Agawe Madaraka, anaewandaa wengine kuwa kazini / viongozi
xi. Mwenye uhusiano mzuri na wengine.
xii. Anaekubali mambo mapya.
SHERIA
1. Kuwa mtii
2. Kuwa msafi
3. Kuwa kweli
4. Kuwa mkarimu
5. Kuwa na heshima
6. Kuwa msikivu
7. Kuwa tayari kutoa msaada
8. Kuwa Mchangamfu
9. Kuwafikiria wengine
10. kuwa na kicho
Maana ya Ahadi: Watoto waelekezwe kuutambua upendo wa Yesu kwao ili nao wampende.
Kutambua vile Yesu anavyokupenda husaidia kujitoa kumtumikia.
Maana ya sheria Sheria:
1. Kuwa mtii
- Utii kwa wazazi na utii kwa Mungu
2. Kuwa msafi
- Usafi wa kimwili na usafi kiroho (mf. Kufua nguo, kuoga, kupiga mswaki, kusafisha
mazingira nk. Na kiroho:- kusoma neno la Mungu na maombi na kufanya yale yaliyo mapenzi
ya Mungu.
16
3. Kuwa mkweli
- Ndiyo yako iwe ndiyo na hapana iwe hapana. Kuepuka udanganyifu wa namna zote
4. Kuwa mwema
- Wema unajulikana kutokana na zile huduma za mtu kwa wengine zaidi ya kusema tu. Mf.
Wema wako kwa mwenye kiu ni kumpa maji na sio umwambia maji ni mazuri kwa kukata kiu.
5. Kuwa na heshima
- Amri ya tano kati ya zile kumi inazungumzia jambo hili, Baba na Mama huwakilisha watu
wote. Kuheshimu baba na mama kutaongoza katika kumheshimu Mungu.
6. kuwa msikivu
- Kutulia na kusikiliza mashauri na mafundisho ya wazazi, walimu na viongozi wengine.
7. Kutoa msaada
- Kusaidia wahitaji ni kujiwekea akiba kwa Mungu mbinguni
8. Kuwa na furaha
- Ni kinyume cha huzuni. Huboresha afya na kuongeza siku za kuishi
9. Kuwafikiria wengine
- Kuepuka ubinafsi
10. Kuwa na kicho
- Kutetemeka, kuwa na hofu vinavyosababishwa na kuutambua ukuu wa Mungu sio
kutetemeka na hofu kama za aliyekutana na Nyoka au simba.
17
SEHEMU YA NNE
KUWAELEWA WAVUMBUZI.
Tabia za wavumbuzi zimewekwa katika hali ya Kimwili, Kiroho, Kiakili, Kijamii na Kihisia,
Tutaangalia tabia za jumla.
TABIA ZA KIMWILI.(PHYSICAL)
1. Wanapenda kujifunza badala ya kukaa muda murefu ,wana nguvu zisizo mipaka.
2. Wanajifunza kwa kushiriki michezo na shughuli mbalimbali za kutumia nguvu.
3. Wanakua kwa utaratibu mzuri uwiano mzuri.
18
TABIA ZA KIAKILI(MENTAL)
1) Wanapenda kujifunza kwa kutenda na niwadadisi wa vitu vingi.
2) Wanashauku ya kutaka kujua yale yanayo wazunguka.
3) Wanaelewa zaidi vitu wanavyo viona kwa macho.
4) Ni wepesi wa kukariri na ni wepesi wa kufikiri kile wanacho fundishwa.
5) Wanapenda kujifunza mambo tofauti tofauti/mchanganyiko.
6) Wanafurahia hadithi na nyimbo,michezo na maswali vinakuza akili zao.
7) Wanaelewa kile wanachogusa, nusa, ona zaidi.
Miaka 2&3.
Wanapenda kusikia hadithi fupifupi.
Hujifunza mambo kwa kusema wenyewe.
19
Ni umri mzuri wa kukuza tabia.
Miaka 4&5.
Humpenda Mungu sana.
Huwahi sana kwenye vipindi vya S.S kwa wakati.
Hufurahia taratibu za kujifunza biblia.
Hutambua lililo jema na baya.
Huwa na imani kuhusu Mungu.
Miaka 6&7.
Hutaka kumpenda Mungu.
Huwa na utambuzi wa kuelewa jambo.
Husikita pale anapofanya baya.
Hupenda kufanya vyema shuleni na nyumbani.
Ana bidii katika kuabudu.
Miaka 8&9.
Hutamani kumwabudu Mungu.
Huelewa hitaji la wokovu katika maisha yao.
Hupenda kusoma biblia, kuomba na kuombea wengine.
Hujisikia furaha, mwamifu anapowajibika kanisani.
Hujifunza kufanya maamuzi.
Malezi ya wavumbuzi yana misingi yake katika biblia Torati 6:4-9, Waebrania 4:7 hivyo
fundisha kufuata maelekezo ya biblia na miongozo ya wavumbuzi, hata mwendo wako uwe
kielelezo kwa hawa watoto maana wanajifunza kutoka kwako na kuigiza kile unacho kifanya,
unachotamka ili kisiwe tabia kwake.
Lishe duni.
Malezi ya Wazazi.
Upweke.
Kutothaminiwa
Jinsi ya kuwasaidia:-
21
ii. Kuachana au kusambaratika kwa familia.
iii. Malezi mabovu
Jinsi kuwasaidia:-
SABABU:
Sababu
Kufiwa na Wazazi (ni yatima)
Jinsi ya kuwasaidia:-
Uwe nao karibu.
Elewa mahitaji yao.
Wapatie nafasi ya utumishi. (mfano; kuomba, kutumwa kazi, kuongoza ibada n.k)
Sababu:
NB:
Adhabu unayoitoa kwa wavumbuzi iwe inamuonyesha upendo wa Yesu na iwe ni ya upendo
siyo ya kigaidi.
Mafungu ya Biblia: Mithali 22:6, Waamuzi 13:3-5, Mithali 1:10, Kumbukumbu la Torati 6:4-9,
Mithali 16:25, Mithali 23:13-14, Mithali 22:15, Mithali 13:24, Mithali 19:18
23
2. USIKIVU {KUJALI} -Wasikilize vijana wako. 1Wakorintho 12:25
-Tengeneza ratiba ya kuwa nao. Mtunzane.
-Weka nyuma masumbufu na matatizo
yako.
3. PONGEZA. -Wapongeze hata kwa kidogo walicho
fanya.
-Pongeza kwa kundi au mtu mmoja.
-Wape zawadi.
4. UNGA MKONO. Tembea nao kwa kila safari. Wagalatia 6:2
-Omba nao. Tusaidiane kubeba mizigo.
-Unga mkono kwa mema wanayo tenda.
5. TIA MOYO. -Ongea nao maneno ya kutia moyo. 1Wathesolanike5:11
Tianeni moyo mmoja na mwenzake.
6. UPENDO. -Onyesha kuwapenda kwa maneno na Warumi 16:16
matendo.
-Wape msaada pale panapo wezekana.
7. HESHIMU. -Onesha hekima kwa namna unavyo 1Petro 2:17
mjali kila mmoja. Uwaheshimu watu wote.
-Ondoa mawazo na lugha mbaya mfano
matusi, kijiweni n.k.
-Uwe tayari kukubali pale ulipo kosea.
8. USALAMA. -Onesha wanapokuwa na kiongozi wao 1Yohana4:18
wanakuwa na amani. Upendo hufukuza hofu.
-Ondoa hofu.
9. KUTHIBITISHWA -Thibitisha mambo mema wanayo fanya Warumi 14:18.
juu ya tabia yao njema.
10. SHUKURU. -Onesha ulivyo guswa na kile walicho
kifanya.
24
SEHEMU YA TANO
PROGRAM ZA CHAMA
Nukuu:E.G.White (Test Ministers Pg498) “kuna hitaji zaidi kuwajibika kwa mtu binafsi, zaidi ya
kufikiri, kupanga, zaidi ya uwezo wa kufikiri uletwe katika kazi ya Bwana kwa sababu kazi ya
Bwana ni kamilifu kila dakika.”
(Massege to young People) “Tunapo tamani kuwa wakamilifu kama Baba yetualivyo mkamilifu
tunapaswa kuwa waaminifu kwa kufanya mambo madogo vile ambavyo no bora kufanya vyote
katika ubora.”
YALIYOMO KATIKA MRADI WA PROGRAMU.
-Bajeti.
-Ratba.
-Taarifa ya kila mwezi .
-Baraza la kanisa.
-Sare.
-Kumbu kumbu.
-Ufanisi.
-Vyanzo vya fedha.
Ada ya uanachama.
Michango.
Bajeti ya kanisa.
-Kuongoza maisha ya vijana katika maisha ya umilele ni kazi ya muhimu waliyo pewa
wanadamu na inapaswa ipangwe vyema.
-Kiongozi panga programu zenye uwiano juu ya kukuza maisha ya mvumbuzi kiroho, kiakili na
kimwili.
-Mipango ioneshwe kufuatwa kwa uangalifu.
-Programu yenye makusudio ipangwe kwa mwaka mzima, robo, mwezi na wiki.
RATIBA.
Mfano ratiba lazima izingatie
i. Kugundua.
ii. Neno.
iii. Mahudhurio.
27
Mpango huo unakusudiwa:
• Kueleza nini Adventurers inahusu
• Kueleza majukumu ya kila darasa
• Kueleza Ahadi na Sheria
• Kuthibitisha nafasi ya mtoto katika familia yao
• Kuombea kila mtoto katika klabu ya Wavumbuzi
• Changamoto Wageni na familia zao kuwa “dhabihu iliyo hai” kwa ajili ya Yesu Kristo
NB
Vilabu vingine hufanya haya kama hafla mbili tofauti. Wale wanaowafanya kando mara nyingi
hutumia Baraka ya Familia kama tukio la utangulizi na Usajili inapatikana baada ya huduma.
VITU VYA KUANDAA
1. Meza
2. Bendera ya vyama
3. Bendera ya taifa
4. Bango la ahadi na sheria
5. Nembo ya wavumbuzi
6. Mishumaa
Mshumaa mmoja mweupe
Mishumaa ya madarasa ya wavumbuzi kwa rangi zake
Mshumaa mmoja kwa ajili ya ahadi
Mishumaa kumi kwaajili sheria meupe
MANENO YA UTANGULIZI
Chama cha wavumbuzi Ni maahli ambapo kanisa, shule, familia zinaungana pamoja kuisaidia
kukua katika hekima na kimo kwa mtoto akimpendeza Mungu na wanadamu na pia Huduma za
wavumbuzi ni huduma za kifamilia. Falsafa kuu ya wavumbuzi ni kujenga huduma ya
mahusiano ya kifamilia kwa kuhakikisha ya kuwa wazazi wanahusishwa na kuunga mkono
Shughuli za wavumbuzi.
28
Namna ya kufanya induction ceremony
“Mshumaa huu unawashwa ili kuweka roho ya uvumbuzi ndani yake na pia uwakilisha roho
mtakatifu kwa kila mvumbuzi kwenye darasa lake. Pia kuhakikisha Roho mtakatifu akae ndani
yetu na kutusaidia kutumiza malengo ambayo yatatufikisha katika uzima wa milele.” Lakini
nuru hii peke yake haijakamilika wala haitoshi.
Kwa kutambulisha nuru za ziada nimwite sasa Mkurugenzi Msaidizi (anamtaja kwa jina lake).
ambapo ataelezea/wataeleza madarasa ya wavumbuzi.
Madarasa ya wavumbuzi
katika kuanza kwa madarasa ya wavumbuzi na huku mkurugenzi akiwasha kila mshumaa
unaowakilisha darasa husika, mkurugenzi au mkurugenzi Msaidizi anafafanua Madarasa
sita kama ifuatavyo:
1. Kondoo mdogo
Mimi ni kondoo mdogo ninajifunza kuwa Yesu ni rafiki yangu na ananitaka kuwa mtoto
bora kwa kila mtu [maneno ya mwanachama]
Ni darasa ambalo hujifunza kuhusu habari za yesu na hujifunza zaidi namna ya kuwa
mtoto bora (miaka 4 na rangi ya darasa hili ni light blue)
2. Ndege wa awali
Mimi ni ndege wa awali ninakuwa kwa haraka ninafuata maelezo ambayo Yesu
ananifundisha namna ya kufuata [maneno ya mwanachama]
3. Nyuki wa shughuli
Mimi ni nyuki wa shughuli ninashughuli nyingi na ninapenda kufanya bora kwa vile
Yesu anapenda mimi niwe hivyo [maneno ya mwanachama]
29
Ni darasa lenye shughuli nyingi na linajifunza namna bora ambayo Yesu anaweza
kumtumia katika shughuli hizo kwa kufanya yanayompendeza Mungu. (miaka 6 na
rangi ya darasa hili ni njano)
4. Mwali wa jua
Mimi ni mwali wa jua ninapenda kuuliza maswali mengi kuhusu Yesu na kujifunza
kuhusu Yesu na niangaze kwa watu kila siku [maneno ya mwanachama]
Ni darasa ambalo lina maswali mengi na pia hujifunza kuhusu Yesu na namna
anavyoweza kuangaza katika maisha yao. (miaka 7 na rangi ya darasa hili ni orange)
5. Mjezi
Ni darasa ambalo hujifunza kuhusu visa na ni umri ambao unajifunza namna bora ya
kuufanya mwili wake kuwa hekalu la kristo na pia hujifunza namna ya kulitunza
kanisa la Mungu (miaka 8 na rangi ya darasa hili ni blue)
6. Mkono wa msaada
Mimi ni mkono wa msaada kwa kutumia mkono wangu huu Yesu unifundishe
kuwasaidia wengine. [maneno ya mwanachama]
NB
MKURUGENZI
30
unatakiwa kufikia na ukuaji na mafanikio ambayo kila mtafuta njia atapatia uzoefu kama
mwanachama wa chama cha Wavumbuzi.
Ahadi ya wavumbuzi
Maana ya Ahadi:
Natambua upendo wa Yesu kwangu kwa jinsi alivyojitoa kwa ajili yangu na pia nitamwonesha
jinsi nami ninvyompenda.
NB
Mkurugenzi Msaidizi
MKURUGENZI
Sheria za wavumbuzi
“Mimi Ninamwakilisha sheria ya ___________ na pia atatoa ufafanuzi wa maana ya moja kati
ya sheria zifuatazo kulingana na mshumaa aliouwasha.”
31
Maana ya sheria Sheria:
1) Kuwa mtii
2) Kuwa msafi
3) Kuwa mkweli
Ndiyo yako iwe ndiyo na hapana iwe hapana. Kuepuka udanganyifu wa namna zote
4) Kuwa mwema
Wema unajulikana kutokana na zile huduma za mtu kwa wengine zaidi ya kusema tu.
5) Kuwa na heshima
Amri ya tano kati ya zile kumi ya Kuwa heshimu baba na mama na watu wote, pia
hutaongoza katika kumheshimu Mungu.
6) kuwa msikivu
8) Kuwa na furaha
kila siku nitakuwa mwenye furaha na pia husaidia kuboresha afya na kuongeza siku za
kuishi
9) Kuwafikiria wengine
Kuepuka ubinafsi
32
Kutetemeka, kuwa na hofu vinavyosababishwa na kuutambua ukuu wa Mungu sio
kutetemeka na hofu kama za aliyekutana na Nyoka au simba.
NB
MKURUGENZI MSAIDIZI
“Kwa niaba ya Chama cha Watafutanjia Ulimwenguni ninakubali KIAPO cha Wavumbuzi na
wawakilishi wao kwamba watayaishi kiapo na kwa kanuni za sheria za Wavumbuzi”.
3. Hebu sasa wote tuinue mikono ya kulia juu iliyobeba mishumaa ya ahadi ya kujiweka wakfu
kwa kiapo tunapokariri tena ahadi na sheria za watafutanjia.
MKURUGENZI (......atasema)
“Nuru yenu sasa imeangazwa katika nuru ambayo tayari inaangaza katika chama, katika kanisa
lenu na nje ya mipaka ya eneo lenu na ninawaapisha kwa dhati mbele ya wengine kupitia kusudi
ya chama cha wavumbuzi kwamba wote waweze kuona kazi yenu nzuri na kumtukuza Mungu
33
baba yetu wa juu Mbinguni na tunakuamuru mbele ya Wavumbuzi hawa nuru yako iangaze
mbele ya wengine katika Roho ya Mvumbuzi”.
NB
Kama kuna mwanachama mpya baada ya kiapo na kuwasha mshumaa mkurugenzi atasema
maneno yafuatayo, "_________________" (jina la mwanachama mpya), sasa wewe ni
mwanachama kamili wa Klabu ya wavumbuzi"
Ombi kwa ajili ya kuweka wakfu kwamba Mungu akupe nguvu za kuishi kulingana na
maadili ya juu ya klabu yetu na kuwa mwanachama mwaminifu na mwaminifu wa klabu.
Pia ombi maalumu kwa kanisa la kuhakikisha huduma za wavumbuzi vinakuwa hai kanisa
mahalia na pia kusaidia katika malezi ya watoto hao.
MWISHO
Mwanachama mpya
2. Kisha, naibu mkurugenzi, mshauri, watampa mkono wa kumkaribisha katika chama cha
wavumbuzi
KUANDAA PROGRAMU ZA AC
• Programu za mwaka(ndefu).
34
• Programu za robo au kila wiki.
• Programu za madarasa, kuonana na wazazi au ziara mbalimbali, mahubiri na uvishaji pini.
Lini nitakamilisha?
MASWALA YA KIFEDHA.
Chama cha wavumbuzi kinapata fedha toka Kwa kanisa Na ada ya uwanachama. Fedha lazima
zifuate utaratibu wote wa kanisa.
Tafakari yafuatayo:
Tuzo za wavumbuzi.
Vyeti vya kuhitimu.
35
Vitu vya Sanaa.
Miradi ya injili.
Matukio ya konferensi.
Matembezi.
Mikutano na wazazi.
Bima.
d) Vyanzo vya mapato.
Michango mbalimbali.
Bajeti ya kanisa.
Msaada wa mzazi.
FALSAFA YA PROGRAM ZA WAVUMBUZI
Tofauti iliyopo kwa wavumbuzi na watafutanjia ni kwamba program za wavumbuzi zinahitaji
muda mfupi. Program zinazofundishwa kwa kutumia uzoefu na mtaala wa Wavumbuzi, hukuza
utii na uwajibikaji kupitia Nyanja za Kimwili, Kiakili, kiroho, na Kijamii
I: KIMWILI
36
SEHEMU YA SITA
MTAALA WA WAVUMBUZI.
MALENGO YA MTAALA WA WAVUMBUZI.
Mfundishe kuwa na kicho mbele za Mungu maana hatayaacha Mithali 18:18, Kutayarisha
njia uk 168 sehemu ya kwanza.
-Kuwa na mtaala wa wavumbuzi ni kuona mawazo yanayo hitajika kwa wanao fundishwa.
MTAZAMO WA JUMLA
Kuwatazamisha vijana Kwa mambo tofauti na watoto wa ulimwengu wanavyo ishi na kila lengo
limegawanyika katika mambo matatu.
Mtaala wa Wavumbuzi umegawanyika katika Mambo makubwa matano yenye vipengele vitatu
kila moja;
1. Mahitaji ya Msingi:-
• Utayari (Umri).
• Majukumu(Kutumika).
• Vichocheo(shime au tia moyo).
2. Mungu wangu:-
• Mtoto aone kuwa Mungu ni wake
(Kumwonyesha mfano wa Uumbaji, Wokovu ni wake, kuja kwa Yesu
mara ya pili).
• Ujumbe wa Mungu kwangu (Akariri Mafungu)
• Kile ambacho Mungu anataka nitende (kwenda Kanisani, kutoa sadaka).
37
3. Mimi mwenyewe.
• Ajigundue kuwa yeye ni wa pekee.
• Agundue kuwa yeye anaweza kufanya uamuzi wa busara.
• Agundue kuwa yeye anaweza kutunza mwili wake (Usafi, Mazoezi, Kiasi na
muda wa kulala). Kuheshimiana Kijinsia.
4. Familia Yangu:-
• Ajue kuwa ni mmoja wa familia,nini sehemu yake nyumbani.
• Ajue kuwa familia inajali kila mmoja ili aondoe ubinafsi.
• Kusaidia kujijali (Usalama wake, wasifunge mlango mpaka arudi)kujijali na
uwakili.
5. Ulimwengu wangu:-
▪ Aelewe kuwa ulimwengu aliomo ana Marafiki,wazuri na wabaya.
▪ Kuna watu wengine hawafanani (weupe na weusi) wapole na wakorofi, Kanisani na
Barabarani na Shuleni.
ZINGATIA YAFUATAYO:-
1. Panga kwaajili ya mafanikio.
Elewa ubunifu.(Usizidishe dk 20 Katika kufundisha,wabadilishie kazi.)
Soma vyema mtaala ili uelewe.
Pitia kile unachoenda kufundisha.
Shughulika na changamoto maalumu.
4. Vyanzo.
Uwe na vifaa vinavyo hitajika ilio ufanyanye mambo mazuri.
Ni lazima uwe na miongozo ya ziada na kiada.
38
JINSI YA KUWAFUNDISHA
• Kulipenda neno la Mungu.
• Kulipenda kanisa la Mungu.( Kulijali).
• Waandaliwe kwa huduma(nyumbani na kanisani, kutenda kazi.
Anamsikia Mzazi:-
HATUA ZA UFUNDISHAJI:-
1. Anza na Mpango mzuri.
2. Uwe na ratiba ionyeshe mada na vipengele.
3. Ni mara moja au mbili kwa wiki nani Dk 20 tu.
Mfano:-
Watoto ni wepesi kuchoka, kipindi kisizidi dakika 30, na unapofundisha zitumie kwa
kuchanganya mambo, nyimbo, mazoezi kidogo n.k
40
SEHEMU YA SABA
TUZO NA UFUNDISHAJI WAKE
Tuzo za Wavumbuzi ni ujuzi au Elimu inayotolewa kwa Wavumbuzi ili kupanua ufahamu wao
katika mambo mbali mbali. Kiongozi au mwalimu wa Tuzo za Wavumbuzi anatakiwa awe
mbunifu ili kufanya tuzo hizi kuwa na manufaa kwa watoto. Atie moyo kila mtoto kufanya
vizuri. Mwalimu lazima azifahamu vizuni na namna ya kuzifundisha. Tuzo zimegawanyika
katika makundi sita ambayo ni Tuzo za kiroho, Tuzo za kijamii, tuzo za viumbe vya asili, tuzo
za ufundi [sanaa za mikono], tuzo za maburudisho pamoja na tuzo za nyumbani.
NB
Hizi ni baadhi tu kati ya nyingi zipatazo karibu hamsini (50).
Mwalimu lazima awe mbunifu katika ufundishaji wa tuzo hizo na kuwafanya wafurahie.
41
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI UNAFUNDISHA
1. Mruhusu avijaribu vitu vinavyo mzunguka.
2. Tumia nyimbo, hadithi, maigizo na michezo katika ufundishaji.
3. Mfundishe kuwa Yesu ni mwokozi wake kwa kuomba.
4. Mwalimu kuwa mbunifu.
1. Amsha hamu.
kwa kutumia picha, hadithi, vitu halisi au matendo, kadiri inavyowezekana
wafanye watoto wagundue wenyewe, alika wageni, mjadala na picha.
2. Washirikishe katika kutenda, ndivyo anavyoelewa haraka ni njia ya kupima uelewa wao
(zoezi).
Nyimbo za vitendo, Michezo na maswali.
3. Fanya tathmini kagua kazi zao.
i. Fundisha dini,
Kichwani mwake awe Yesu tu.
Jinsi ya Kumheshimu Mungu,
tangu utoto ajue namna ya kuomba na kupiga magoti.
Tafuta muda ambao akili hazijachoka
Fundisho liwe fupi. (Dk 20).
Lifanye somo liwe fupi na la Kupendeza kwa kulingana nao na kufanana nao.
Badilisha mtindo wa ibada au kujifunza Usiwe na staili ileile tu kila siku, ili
wasione ibada kama kitu kisicho na maana.
Dini ipi wanapaswa kufundishwa;
Yakobo 1:27,
Mathayo 22: 37 – 40,
Kumbukumbu la Torati 6: 4 - 9
ii. Wafundishe kuishi maisha ya kiasi.
Tabia ya umimi (changu) kujipendelea iondoke.
iii. Kuepuka mazoea mabaya.
Umri huu wanaingia katika mazoea mabaya kirahisi kwani hawawezi kupambanua
mema na mabaya.
Aina ya chakula vinywaji vinachangia kuwa na mazoea mabaya, hivyo
watenganishiwe.
iv. Wafundishwe kujihusisha na kanisa
(Waebrania 10:25).
v. Jenga mahusiano mazuri kati ya Mzazi, Kanisa na mwalimu.
(Watembelee)
vi. Fundisha heshima na utii.
Picha ya watoto ndio itakayodhihirisha tabia ya Mwalimu.
Kutoka 20:12, Mambo ya walawi 19:32.
vii. Wafundishe watoto kufanya kazi kwa juhudi,
Kuwaacha watoto kukua kivivu ni dhambi
Wajifunze kukunja nguo zao
Kunyoosha nguo zao.
Kuosha vyombo.
Wajifunze kupika.
Kufagia nyumba, uwanja nk.
43
Kutunza bustani za maua, mboga nk.
Wafundishe kutoa zaka na sadaka
viii. Zungumza na Wazazi katika kazi ya malezi ya watoto.
Mithali 14:23; 16:26
Kutoka 20:8,
2Wathesalonike 3:10 - 12
ix. Wafundishe watoto kujali elimu
Mithali 4:13
x. Wafundishe waache mazoea mabaya na kuyaepuka mfano:-
Vinywaji visivyofaa na vinavyofaa kwa mkristo
Vyakula vinavyofaa na visivyofaa
Michezo inayofaa na isiyofaa kutazwa
NB:
Wafundishe kwa moyo maana umebeba maisha ya baadae ya hawa wavumbuzi.
44
SEHEMU YA NANE
FAMILIA YA WAVUMBUZI.
Chama hiki cha wavumbuzi ili kuwasaidia na kuwaunga mkono wazazi/walezi katika jukumu la
kulea mtoto/watoto na kuwafanya watoto wampokee Yesu maishani mwao.
MAWAKALA WANAOCHANGIA MALEZI YA MTOTO
MZAZI/MLEZI
SHULE
(NYUMBANI)
MTOTO
JAMII
KANISA
(MITAANI)
NUKUU:
kutayarisha njia uk, 210. Inasema
“umri wa miaka 0-9 ni mzuri wa kumpandikiza mtoto tabia unayoitaka awenayo”
45
MTANDAO WA FAMILIA YA WAVUMBUZI.
1. Mahusiano ya malezi.
Ulimwengu wa wavumbuzi kitovu chake ni familia, ili kuyaongoza maisha ya watoto
kwa Mungu ushirikiano wa wazazi na familia unahitajiwa uratibeshwe kwa hali zote.
2. Vyanzo vya jamii katika mahusiano ya malezi.
Pia ni muhimu au washiriki wanapaswa kufahamu nini watoto hawa wanachojifunza
jamii/washiriki pia ni chanzo kizuri cha malazi ya vijana hawa.
3. Mtandao wa Programu.
Kunapaswa kuwepo mtandao mzuri wa kazi ya wavumbuzi na wazazi kuhusu program
zinazoendelea.
46
JAMBO LA KUFANYA KUSAIDIA KATIKA MALEZI:-
MADARASA YA WAVUMBUZI
47
SEHEMU YA TISA
HUDUMA ZA WAVUMBUZI
SARE ZA CHAMA.
Sare zinafanya chama kuwa halisi na kionekane kuwa kipo hai.
Inafanya wana chama wakipende chama na kuwaleta pamoja.
Inaleta changamoto na wito kwa wale ambao bado hawajajiunga.
Ni kichocheo cha kujenga moyo wa chama.
Sare inapaswa kuwa safi kwani program za wavumbuzi ni za thamani.
AINA ZA SARE:
1. Official Uniform/Sare za kiofisi
(Huvaliwa na wanachama,walimu, na wakurugenzi wakati wa program.)
2. Sare za kazi.
(Huvaliwa wakati wa shughuli mbalimbali na mafunzo kama Hiking,safari,ziara,kazi za
kijamii.)
3. Staff Uniform/Sare za viongozi.
(Huvaliwa na wakurugenzi)
Sare ya daraja la kwanza wavumbuzi wavulana na wasichana.
Wasichana- Sketi za nevy-blue na shati jeupe la mikono mifupi.
Wavulana- Kaptula au suluari za nevy-blue na shati jeupe la mikono mifupi kora za kawaida.
Viatu vyeusi na soksi nyeupe
Skafu pamoja na slide
Mkanda wa tuzo ni rangi ya Nevy blue.
SARE YA MAOFISA WA WAVUMBUZI.
Wanawake- Sketi nevy blue na shati jeupe mikono mifupi.
Wanaume- Suruali za nevy blue na shati jeupe mikono mifupi.
48
Wanawake & Wanaume sare ndani ya chama mkanda mweusi tai ya nevy blue au skafu za
wavumbuzi.
Mkanda- Mkanda huvaliwa wakati maalumu,Nishani za AY zisivaliwe kwenye mkanda wa
wavumbuzi, Tuzo pekee ndizo zina kaa kwenye mkanda.
Nembo- Patch ya wavumbuzi inavaliwa bega la kulia
Nembo ya dunia ya wavumbuzi inavaliwa bega la kushoto
Crescent ya chama inawekwa kulia juu kidogo ya Patch.
Tuzo za wavumbuzi zinavaliwa katika mkanda.
Pini za madarasa zinavaliwa katika mfuko wa hati au Blauzi upande wa kushoto kuanzia kulia.
SARE ZA KAZI.
Sare za wavumbuzi za kazi ni Shati la light blue au T-shart ya Blue.
Kanisa linaweza kubuni sare ya kazi kwa wavumbuzi lakini iwe nembo ya chama
NB
Nembo ya chama cha wavumbuzi.
Msalaba
Mtoto
Wazazi
Viumbe vya asili [mazingira]
EMBLEM
Adventurer World Logo Adventurer emblem
END
49