You are on page 1of 3

TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD

MIKUMI MISSION CHURCH


P.O. BOX 132
MIKUMI – MOROGORO

TANGAZO LA KAZI
Kanisa la TAG – Mikumi Mission Church (MMC) lililopo Katika Mji wa Mikumi Kitongoji
cha Mji-mpya linatoa huduma ya ufadhili kwa watoto wanaoishi katika Kaya masikini na
hatarishi kwa ushirikiano na Shirika la Compassion International Tanzania (CIT).
Mchungaji Kiongozi anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa na uwezo kwa
nafasi ya kazi maalumu ya MTAALAMU WA PROGRAM YA MAENDELEO YA MTOTO NA
KIJANA (Program ya nyumbani ) yaani HOME BASED IMPLEMENTER (HBI).

WAJIBU WA MTAALAMU WA AFUA YA KUNUSURU MAISHA YA MAMA NA


MTOTO- PROGRAM YA NYUMBANI
Atawajibika kwa moja kwa moja kwa Mratibu wa kituo cha huduma ya mtoto, kamati ya
Huduma ya Mtoto, Mchungaji Kiongozi na Shirika la Compassion International Tanzania.
I. Mtendakazi wa huduma ya afya ya mama na mtoto atahusika moja kwa moja na
akina mama watakaonufaika na huduma hii
II. Atatakiwa kutumia asilimia 80% ya muda wake wa kazi kwa kuwatembelea akina
mama hao majumbani mwao na kuhakikisha anatoa mafunzo kwa mama kuhusu
afya ya mama na mtoto.
III. Yeye ndie atakauwa nguzo muhimu katika kuhakikisha kuwa, masuala yote
katika program ya afya ya mama na mtoto yatatekelezwa.
IV. Ni jukumu la mtendakazi huyu kufuatiliwa mwenendo wa namna malengo ya
afya ya mama na mtoto yatakavyosababisha tofauti kwa walengwa katika maisha
yao ya kila siku.
V. Mtendakazi huyu atafuatilia na kuhakikisha kuwa upimaji wa ukuaji wa mtoto
kwa utaratibu uliowekwa.
VI. Awe ni mfano wa kuigwa katika ukristo wake, anayeheshimu na mwenye
kutunza siri za watu.

KAZI MUHIMU ZA MTAALAMU WA AFUA YA KUNUSURU MAISHA YA MAMA NA


MTOTO- PROGRAM YA NYUMBANI
i. Afanye kazi kutokana na wito wa ndani, akitenda kama msemaji wa watoto na
mama zao au walezi waishio katika umaskini na hawana uwezo wa kujisemea
wenyewe.
ii. Kuwatembelea akina mama mara kwa mara ili kufauatilia utekelezaji wa mambo
atakayowafundisha.
iii. Kufundisha akina mama kuhusu namna bora yakulea watoto wao kama njia ya
kuboresha maendeleo ya ukuaji wa watoto kwa akina mama walioandikishwa
chini ya mpango wa huduma ya kunusuru maisha ya mtoto katika kiwango cha
familia.
iv. Atashiriki katika kuandaa mpango wa huduma ya kunusuru maisha ya mtoto wa
mwaka, miezi mitatu, wiki mbili na siku pamoja na kupanga bajeti.
v. Atahakikisha kwamba taarifa ya majumuisho ya shughuli zote zinaandaliwa kwa
wakati uliopangwa na kuwakilisha kwa Mratibu wa Kituo cha Huduma ya Mtoto.
vi. Kuingiza taarifa sahihi kwenye ripoti zinazohusu kitengo cha mama na mtoto.
vii. Kuwatembelea nyumbani na katika shughuli za vikundi zinazo hamasisha
mchakato mzima wa kuyatambua mahitaji ya mama na mtoto
viii. Atahakikisha kuwa anashiriki kikamilifu ibada ya asubuhi ya watendakazi wote
kabla ya kuanza kazi.
ix. Atahudhuria na kushiriki kikamilifu vikao vya watendakazi (staff meeting) mara
mbili kwa mwezi au zaidi itakapobidi. Atahudhuria na kushiriki vikao vyote vya
wazazi.

SIFA ZA MTAALAMU WA AFUA YA KUNUSURU MAISHA YA MAMA NA MTOTO-


PROGRAM YA NYUMBANI.
1. Awe mkristo aliyeokoka na aliyejitoa kikamilifu kwa Bwana Yesu, mwenye
ushuhuda mzuri wa maisha yake ya kila siku.
2. Atahakikisha anahudhuria ibada zote zilizo katika mpango wa Kanisa
3. Atahakikisha anahudhuria ibada za watendakazi za Asubuhi kabla ya kuanza kazi.
4. Awe na elimu ya Shahada au Diploma, mwenye kozi angalau miaka mitatu katika
mojawapo ya fani za huduma za jamii yaani katika elimu, sosioloji, uuguzi, afya
ya jamii, chakula na lishe,maendeleo ya jamii, utabibu au ukunga.
5. Awe na umri kati ya miaka 25-40 mwenye uzoefu katika mojawapo ya masuala
ya huduma za afya ya mama na mtoto kama kupima ukuaji wa mtoto, kutibu
kwa kutumia maji yenye chumvichumvi (Oral rehyadrationsalts), kunyonyesha,
elimu kuhusu VVU, chanjo, kupanga chakula, lishe, kupanga uzazi na elimu ya
mama na mtoto. (Kibali maalumu chaweza kufikiriwa kwa atayezidi umri)
6. Uzoefu wa kazi za kijamii wa miaka miwili unazingatiwa
7. Awe ni mtu mwenye uelewa mzuri katika kuhudumia jamii, mwenye uadilifu,
uwakili na mfuasi wa Yesu Kristo, mtu anayeaminiwa na siyependa kuingilia
taratibu za maisha ya watu wengine.
8. Mtu mwenye nguvu ya msukumo wa ndani katika kutembelea nyumbani kwa
akina mama na kuendesha mafunzo ya kimakundi yanayohusisha wazazi na
watoto wao katika mazingira yasiyo ya darasani.
9. Awe mwenye fikra za kimaendeleo na uwezo wa kuandaa na kutekeleza
miongozo ihusuyo afya ya mama na mtoto.
10. Awe na uwezo wa kutengeneza mazingira yanayoamsha ari ya watoto waishio
katika mazingira ya watu wazima kwa kutumia vyanzo na zana zilizopo.
11. Awe na ujuzi wa kutumia tecknolojia ya habari na mawasiliano kwa vitendo, na
weledi wa kutumia program kama Microsoft package, internet and surfing, na
ujuzi wa kutumia Smart phone na program mbalimbali katika simu.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.
Waombaji wote wenye sifa watume maombi kabla ya tarehe 20 April 2024 saa 10 Jioni.
Wakiambatanisha vifuatavyo:

1. Maelezo Binafsi (CV)


2. Barua ya maombi
3. Nakala ya vyeti vya Taaluma
4. Nakala mbalimbali za kitaaluma( leseni/vibali) zinazoendana na taaluma
uliyosoma
5. Barua ya mchungaji toka kanisa unaloabudu
6. Nakala ya cheti cha kuzaliwa
7. Kitambulisho cha uraia (AU namba ya Nida)

Maombi Yote yatumwe kwa :

MCHUNGAJI KIONGOZI

KANISA LA TAG

MIKUMI MISSION CHURCH (MMC)

P.O BOX 132

MIKUMI-MOROGORO

Vielelezo vyote vitumwe kwa email: petermsimbe15@gmail.com

You might also like