You are on page 1of 4

UALIMU

SAIKOLOJIA
Dhana ya saikolojia.
Saikolojia;Ni taaluma ya kisayansi inayoshughulika na tabia na mwenendi wa binadamu na
wanyama kwa mfumo wa utendaji kazi wa akili na ubongo.Tabia ni matokeo ya mchakato was
ubongo,Ni uhusiano wa moja kwa moja kati ya akili na ubongo hivyo saikolojia inahusiana na
ubongo na akili kwamambo kama vile:
1.Mawazo
2.Fikra
3.Mitazamo
Saikolojia ni taaluma ya kisayansi kwasababu huusisha utafiti was kisayansi katika kuzitambu
tabia na mwenendo was binadamu na wanyama kwa mfumo mzima wa utendaji kazi wa akili na
ubongo.

Tabia;Nikile binadamu anachofanya na kinachunguzwa moja kwa moja.


Akili;No ule mchakato was ndani ambao hauwezi kuchunguzwa moja kwa moja .

CHIMBUKO LA SAIKOLOJIA/CHANZO CHA SAIKOLOJIA

Saikolojia ni neno la kiingereza "psychology"lililo kopwa kutoka katika lugha ya kigiriki likiwa
na muunganiko was maneno mawili nayo ni;
Saiko-Akili/Mchakato was ubongo.
Olojia-Elimu saikolojia.

MATAWI YA SAIKOLOJIA
1.Saikolojia ya Elimu
Ni tawi la kisaikolojia inayoshughulikia ujifunzaji na ufundishaji na matokeo ya na matokeo ya
ujifunzaji na namna bora ya kuwafundisha watoto kwa kuzingatia nadhalia mbalimbali za
ujifunzaji.
Motisho;In kuchochea kuhamasisha na kumsukuma mtoto kufanya kitu Fulani.

Inaangalia tofauti ya ujifunzaji kati ya mtu mmoja na mtu mwingine katika ujifunzaji.

UMUHIMU WA SAIKOLOJIA YA ELIMU KWA MWALIMU


(a).Humsaidia mwalimu kuelewa tabia na mienendo ya mtoto
(b).Humuwezesha mwalimu kuandaa mpango was mafunzo unaoendana na uwezo wa mtoto
(c).Kufafanua matatizo uanayokwamisha matendo ya ujifunzaji kwa mtoto
(d).Kusaidia katika kutoa na kuandaa maadili ya kuwaandaa walimu
(e).Humsaidia mwalimu katika kuandaa zana za kujifunzia
2.Saikolojia ya ushauli nasihi.
Hii huusika na namna ya kutoa tuba kwa watu wenye matibabu ya kisaikolojia kama
vile,UKIMWI,kufeli mtihani,kufiwa na wazazi au ndugu wa karibu.
Ushauli;Hutolewa kabla jambo flani halijamtokea mtu.
Unasihi;Hutolewa baada ya kupatwa na jambo baya.

3.Saikilojia ya viwanda
Hii husaidia kuleta maelewano mazuri kati ya viongozi na wafanyakazi wao kwa lengo la kuondoa
migogoro na misuguano inayojitikeza viwandani na kuleta au kujenga mahusiano mazuri.

4.Saikolojia ya jeshi
Inatumika kuwatambua maadui na mbinu zao ili waweze namna ya kupambana au kukabiliana
nao.
Saikolojia ya Biashara hutumika kutambua tabia za wateja na kujua mahitaji ya bidhaa za wateja.

5.Saikolojia ya Elimu ya jamii


Hushughulikia jinsi watu wanavyofanya kazi pamoja na mahusiano yao ili kujenga uwezo wa
kuishi na watu was aina mbalimbali.

6.Saikolojia ya Mtoto
Ni tawi la saikolojia linalo Fanya uchunguzi na mchakato was kiakili za watoto na mienendo yao
kama kundi la pekee na tofauti kati ya mtoto na mtu mzima husaidia kuchunguza tabia za watoto
kulingana na ukuajiwake.

DHANA YA SAIKOLOJIA YA WATOTO


Saikolojia ya watoto;No tawi la sakolojia inayoshughulika na mambo yanayohusu tabia na
michakato ya kiakili na mienendo ya watoto kama kundi pekee tofauti na watu wazima.
Nimuhimu sana kujifunza saikolojia ya watoto kwakua hutusaidia ufundishaji na ujifunzaji,pia
hutusaidia katika kujifunza tabia za watoto na namna ya kutoa mahitaji kwa watoto kulingana na
hatua za ukuaji wake.

UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA YA WATOTO


1.Kuelewa kiwango cha uelewa wa mtoto katika kupanga na kutoa maelekezo.
2.Kuelewa njia bora za kupima ujuzi na maarifa yaliyo fundishwa.
3.Kujua kiwango cha uelewa cha mtoto wakati wa kufundisha.
4.Humsaidia mwalimu katika kuandaa zana za kufundishia na kujifunzia zinazo endana na watoto
5.Kuekewa njia bora za kupima ujuzi na maarifa yaliyofundushwa
6.Kumwezesha mwalimu kuendeleza tabia njema za watoto

NYANJA ZA MAKUZI YA MTOTO


MAKUZI YA KIMWILI
Haya ni mabadiliko yanayo tokea katika maumbile ya binadamu ambapo maungo ya mwili hukua
kwa kuongezeka urefuna uzito
Mambo yanayopaswa kifanywa ili kuchochea makuzi ya mtoto ni:
1.kuhudhulia kliniki kujua maendeleo ya mtoto kabla na kuzaliwa.
2.kumpa mtoto lishe bora.
3.kumpa mtoto nafasi ya kushiliki michezo mbalimbali.

MAKUZI YA KIAKILI
Haya ni makuzi ambayo huhusihsa iwezo wa ubongo wa mtoto kupokea taarifa mbalimnali na
namna ya kuyumia taarifa hizo.
Kiujumla makuzi ya kiakili ni kuongezeka kwa uwezo wa mtoto kufikiri na kutumia uzoefu
wake kiyatua matatizo katika mazingila yake.
Ongezeko la kiakili linahusu
.Uwezo wa kukumbuka mambo
.Uwezo wa kufikili na kutafakari mambo
.uwezo wa kutumia msamiati wa lugha
.uwezo wa kufanya maamuzi

MAKUZI YA KIHAIBA
Haya ni jumla ya mambo yote yanayomtambulisha mtu na kufanya aonekane na kwa kiasi gani
anafanana au amatofautiana na wenzake.Makuzi ya haiba hubainishwa katika mambo yafuayayo
.Maumbile ya kimwili Mfano unene,urefu
.Uwezo wa kitaaluma mfano kukumbuka anavyopenda na anavyo chukia
.Tabia yake kiujumla mfano adabu,heshima,marigo,icheshi,aibu na kujiamini
Kila mtoto anapaswa apewe maelekezo yanayo stahili kukuza haina inayokubalika

MAKUZI YA KIMAONO
Haya ni makuzi ambayo hujengwa na silka na tabia ya mtuvinayitokana na malezi aliyopata
pamoja na urithiwake.Makuzi haya huhusisha mtoto kujiamini,kujiyambua, kujihisi na kujielewa.
Viashilia vya makuzi ua kimaono ni pamoja na:
.Kuwa na uoga anapokutana na jambo linalomtisha
.Kuwa na hasira anaponyimwa haki yake.
.Kuwa na wivu pale anapodhani yeye alistahili kupewa upendeleo wa huduma flani.
Hukuza tabia ya kueapenda wengine mfano kupenda kukaa na mtu flani.

MAKUZI YA KIJAMII
Haya ni makuzi yanyohisika na jinsi mtoto anavyo jihusisha na jamii yake katika vipindi
mbalimbali vya maisha yake.Makuzi haya pia humwezesha mtoto kuishi pamoja na jamii bila
matatizi.
Viashilia vya makuzi ya mtoto kijamii ni pamoja ma;
.kuwa na marafiki nje ya familia.mfano marafiki wa shuleni.
.jinsi anavyo wasiliana na wenzake wa rika mbalimbali,
Kuchaguliwa na kuchagua
Ni wajibu wa mzazi na walezi na walimu kuwa mfano mzuri wa kuigwa ma watoto kukuza
maadili mazuri yanayo kubalika katika jamii kamavile heshima,kusamehe na kuwa na uvumilivu.
UJIFUNZAJI WA MTOTO WA ELIMU YA AWALI.

You might also like