You are on page 1of 37

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO

JIMBO LA KUSINI MASHARIKI MWA TAZANIA

MUHTASARI WA MTAALA WA KUFUNDISHA BIBLIA SHULENI

NGAZI YA SEKONDARI

(FOR SECONDARY SCHOOLS)

IDARA YA ELIMU

UMEANDALIWA NA TANZANIA UNION

NA KURATIBIWA NA MKURUGENZI WA ELIMU

SOUTH-EAST TANZANIA CONFERENCE

BOX 6923 DAR ES SALAAM

1
••


UTANGULIZI

Muhtasari huu ni toleo la Tanzania Union la Mtaala wa kujifunza Biblia (2001). Ni kozi ya
Biblia ya muda wa miaka kumi na tatu iliyobuniwa kukidhi mahitaji ya masomo na vipindi vya
dini kuanzia Shule za awali, hadi elimu ya Sekondari (Kidato cha nne). Kidato cha tano na cha
sita watajifunza mada hizi hizi lakini kwa upana zaidi.

Kozi hii imegawanywa katika madaraja matatu.

• Miaka 2 ya Shule ya Awali (Pre-Primary School).


• Miaka 7 ya Elimu ya Msingi (Primary School Education). Miaka 4 ya Elimu ya
Sekondari (Secondary School).

Kozi itafundishwa katika mfumo wa kuendelea kwa mzunguko kama pia. Maana yake ni
mviringo unaoendelea, kwa sababu mada zinazofundishwa hutegemeana moja kwa nyingine na
hurudiwa katika ngazi tofauti kwa kujifunza kwa undani na upana zaidi.

Mtaala huu umekusudiwa kutumika katika kufundisha vijana Waadventista wanaosoma katika
Shule zisizo za kanisa. Kiuhalisia ni vigumu kutoa wakufunzi wa kutosha kufundisha wanafunzi
katika shule hizo zisizo za kanisa maana ni nyingi, inashauriwa Mwalimu / Mkufunzi aunganishe
Madarasa, mfano darasa la 1 na 2, 3 na 4, 5, 6 na 7; pia kidato cha 1 na 2, na 3 na 4.
Inaposhindikana kukawa na mwalimu mmoja basi aunganishe wanafunzi wote wa Sekondari na
atumie taaluma yake kuhakikisha kuwa wanafunzi katika level zote wanamuelewa.

Sehemu ya kidato cha tatu na cha nne cha muhtasari huu kinakamilisha mada ambazo
zimelengwa mahsusi kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya mitihani ya Taifa ya somo la Biblia
(Bible Knowledge).

• Maandiko Matakatifu ndicho kiwango kikamilifu cha kweli hivyo yapaswa kupewa nafasi
ya juu katika Elimu. “kupata elimu yenye thamani inayoligana na jina, lazima tupokee
ufahamu wa Mungu Muumbaji na Kristo Mkombozi kama walivyofunuliwa katika Neno
takatifu” (Education uk.27).
• Mtaala katika Shule zetu ni lazima kiini chake kiwe ni Mungu, Biblia ikiwa ndicho kitabu
cha mwongozo katika kazi ya Elimu.
• Muhtasari umejaribu kuingiza mambo yahusuyo maadili na thamani za Kiafrika kwa
kuchukua mfano na vielelezo vya mambo hayo kutoka jamii mbalimbaliza kiafrika.
• HOJA: “Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha aata atakapokuwa Mzee”
(Methali 22:6).
- Ni kazi ya Wazazi wanaowajibika na kujali, shule makanisani na walimu kufanya kazi
kwa mshikamano katika juhudi ya kutoa mafundisho sahihi ya Kikristo kwa ajili ya
vijana. Mafundisho yatakayowawezesha kuwa watendakazi pamoja na Kristo na
kuwaandaa kwa marejeo yake mara ya pili.

2
“kuwa na jeshi la namna hiyo la watendakazi kama vijana wetu, walifunzwa vyema,
inawezekana kueleza jinsi ya uharaka wa ujumbe wa mwokozi aliye sulubiwa,
aliyefufuka na anayekuja haraka unavyoweza kupelekwa kwa ulimwengu “Ellen
White 1943 uk 555.

MATUMIZI YA MUHTASARI HUU!

Wakurugenzi wa Elimu wa Conference

• Ni waratibu wakuu wa Program hii.


• Wanasimamia na kusaidia walimu walei.
• Wanashirikiana na Makanisa katika kuchagua au kuteua wanafunzi watakaosaidia
kufundisha.
• Watashirikiana na idara ya chaplensia ambao wanahusika na malezi ya kiroho kwa
wanafunzi hasa kuanzia ngazi ya sekondari.
• Wataendesha semina, mihadhara ya kuendesha na kufundisha wakufunzi walei.
• Watajadili na wakufunzi juu ya mada ngumu.
• Watapata marejesho kutoka kwa watumiaji wa muhtasari huu, na kufanya utaratibu wa
kuuboresha zaidi kulingana na badiliko na hitaji.
• Watasaidia katika kusahihisha muhtasari katika msingi wa mapendekezo, mafanikio au
mapungufu ya mtaala.
• Ifahamike kwamba muhtasali huu utakuwa wazi kwa ajili ya mapitio, masahihisho,
nyongeza na maelezo / mapendekezo yatakayoboresha na kuufanya rafiki kwa mtumiaji.

MALENGO:

Malengo yaliyoorodheshwa humu ni ya jumla na yamekusudiwa kwa muhtasari mzima wa


mtaala. Wakufunzi wanategemewa kupanga malengo mahsusi kwa kila moja ya mada
zitakazofundishwa.

Lengo la kwanza na la mbele kabisa kwa mwalimu lapaswa kuongoza maisha ambayo yatafaa
kuwa vielelezo vya kanuni za Biblia zifundishwazo kwa wanafunzi. Kila mada yapaswa
imalizike kwa fundisho la Kiroho.

Wanafunzi wataweza

a) Kumfahamu Mungu kama nafsi.


b) Kufahamu Biblia kama njia ya kumjua Mungu.
c) Kukuza uelewa wao kwa Mungu, ili upewo wao, tegemeo lao, na kusifu kwao viweze
kuongezeka.
d) Kufahamu maandishi ya Ellen White kama ushuhuda mwingine wa ukweli juu ya Mungu.
e) Kufurahishwa katika habari iliyoandikwa ya kila tukio na kufundisha ufunuo wa ukweli
juu ya Mungu.

3
••


f) Kufahamu kwamba kusudi la ibada ni kuwa tunafanana zaidi na yeye aliyetuumba.
g) Kuwa na uzoefu wa mafundisho Makuu 28 ya Waadventista Wasabato.
h) Kufahamu asili ya uasi uliopo katika ulimwengu, mabadiliko yaliyoletwa na uasi huu kwa
watu na tiba yake ipatikanayo katika kumjua Mungu kama kweli ilivyo. Kweli hii ni
uwezo wa Mungu (Warumi 1:16).
i) Kujifunza kwamba kushiriki imani yao na wengine (kushuhudia) ni matokeo ya kawaida
ya ufahamu wao kwa Mungu na kumjua Mungu.
j) Kutambua kwamba, Mungu ambaye ameumba Ulimwengu huru amewapa upendeleo na
Madaraka ya kufanya chaguzi zao wenyewe. Hivyo hudhuhirisha kuwa wanaweza au
hawawezi kupewa dhamana ya Uhuru na Uzima wa Milele.
k) Kutambua ujumbe wa afya kama sehemu muhimu ya mafundisho makuu ya imani ya
Waadventista Wasabato.
l) Kufahamu asili ya mtu kuanguka na kurejeshwa kwa sura ya Mungu (Yoh 3:16).
m) Kufahamu kuwa kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho na maisha
yetu ya kila siku.

MBINU ZA UTENDAJI

Mbinu za kufundisha daima zitakuwa tofauti kulingana na Mwalimu, mada, kundi la Wanafunzi
na daraja lao. Hebu angalia mifano michache ya mbinu ambayo kwa kawaida hutumiwa na
Walimu wengi na kwa viwango flani zimeonekana kuwa zenye kufaa.

A: Mafunzo ya njia wazi: Nikanuni ya kufundisha ambayo mwalimu ni mtoaji mkuu wa habari.
Mwalimu hupitisha kweli kwa mwanafunzi katika njia ya wazi sana kadri iwezekanavyo.
Kinyume na mbinu ya madhara, mbinu ya njia wazi, mwalimu anahakikisha kuwa wakati wa
kutoa mafundisho kunakuwepo na muuingiliano (interaction) – kati ya mwalimu na mwana funzi
ambao utahusisha maswali na majibu, kuangalia upya, mazoezi na usahihishaji wa makosa ya
mwanafunzi.

Faida kuu za kanuni hii ni kuwa:-

- Zaidi ni fokasi ya Kitaaluma, ambapo mwalimu huelekeza, hutawala na hupunguza


muda wa mwanafunzi kujifunza.
- Hutoa nafasi kwa mwalimu kupima kwa usahihi uelewa wa mwanafunzi kwa sababu
mwalimu huweka zana za kujifunzia katika hatua zilizo pangwa na kwa kawaida
atakwenda hatua inayofuata baada ya wanafunzi kuelewa hatua iliyotangulia.

B. MCHEZO WA KUIGIZA

4
Huu ni mfano wa mafunzo ambapo wanafunzi katika darasa huchaguliwa kuigiza hali
wengine huangalia kwa makini na kuchukua kipengele mahsusi cha mchezo wa
kuigizailiwajibu kama mwalimu alivyoelekeza. Mchezo wa kuigiza kama haukuratibiwa
vizuri unaweza kuishia kuwa maburudisho zaidi kuliko mfano wa mafundisho. Kwa
maneno mengine, wanafunzi wanaweza wasifikie ufahamu uliotarajiwa na mwalimu
kushindwa kutimiza malengo yaliyo kusudiwa.
Mchezo wa kuigiza humweka mwanafunzi katika hali halisi ya matukio au shughuli. Kwa
mfano wanaweza kuigiza hadithi ya Yusufu na ndoto zake, Wanawali kumi, Mwana
mpotevu nk.

- Itakuwa rahisi Kwa wanafunzi wazito kujifunza, kuelewa mada ngumu na kuumba
picha katika akili zao ambayo kamwe hawataisahau kwa urahisi.
- Huwasaidia mtu mmoja mmoja kugundua matatizo ya watu, hisia, mitazamo, thamani
na mkakati ya kutatua tatizo.
- Katika ulimwengu wao wa jamii, wengine watakuwa wamesaidiwa kupata kama mtu
binafsi, stadi zao za vipaji kama waigizaji ambavyo vyaweza kutokea kuwa kazi
baadaye.

Hivyo mchezo wa kuigiza wapaswa kupangwa na kuandaliwa vizuri ikiwa fundisho


lililokusudiwa linatakiwa liwe la kufaulu.

C. MASIMULIZI YA VISA

Hii ni mbinu ya kufaa sana katika ufundishaji wa Biblia hasa kwa madarasa ya Shule za
awali na ngazi ya Msingi. Hivyo Mwalimu sharti afanye maandalizi ya kina ya mada, na
kupanga vizuri ili kufanya kisa kuwa hai na cha kusisimua. Matumizi ya lugha rahisi na
vielelezo vilivyochukuliwa kutokana na maisha na shughuli za mahali palepale ni
muhimu sana. “kutoka kinacho fahamika kwenda kwa kisichofahamika”.

Mara chache kwa visa vilivyo rahisi mwalimu angeweza kuwapa wanafunzi kazi ya
kusoma kutoka katika Biblia zaidi kisha kuelezea kisa kwa Wanafunzi wengine darasani.

D. “KAZI MRADI”

“Kazi mradi” zinaweza kufanywa na mtu mmoja mmoja au katika vikundi. Hapa
mwalimu sharti atoe maelekezo sahihi yanayoeleweka akieleza ni nini cha kufanya.

- Baadhi ya shughuli za “kazi


mradi” hujumuisha Vikundi vya maombi.
• Mikutano ya uamsho wa Kiroho.
• Kutembelea kanisa au shule nyingine.
• Kushuhudia.

5
••


• Kwaya.
Zote hizi ni shughuli zinazoweza kutajirisha uzoefu wa Kiroho, na ili kufanikiwa mwalimu
atapaswa kuwa na utaratibu na mipango inayofaa.

E. MIJADALA NA PANALI

Itafaa zaidi ikiwa madaraja ya mijadala au Paneli yatafanyika baada ya kusoma mada
iliyokusudiwa kwa ajili ya maandalizi, ni muhimu kua mwalimu atoe maswali bayana ya mjadala
na asimamie vikundi vya mjadala.

- Weka dakika maalum za mjadala.


- Baada ya mjadala kila kikundi sharti kipewe muda wa kutoa taarifa.
- Mwalimu afanye muhtasari wa taarifa za mjadala mwishoni kwa kutoa majibu ya
kufaa.

F. UCHORAJI NA UFINYANZI

Mbinu ya uchoraji picha za rangi au ufinyanzi wa mambo ni ya kufaa sana naya kupendeza, hasa
kwa wanafunzi wa shule za awali na za msingi.

Pale inapowezekana, wanafunzi waulizwe kuchora picha za rangi ambazo mwishoni


zitawakilisha kisa au shughuli iliyoandikwa katika Biblia.

Sambamba na mbinu hizi, mashauri yafuatayo yatakuwa ni ya msaada kwa mwalimu.

a) Kila somo la Biblia sharti lianze na kumalizika kwa ombi.


b) Kila somo lihitimishwe kwa fundisho la Kiroho.
c) Biblia zitumike katika kila darasa la Biblia huku wanafunzi wakifanya rejea na kusoma
mafungu kutoka katika Biblia zao wenyewe.
d) Walimu watumie zana za kufundisha kama vile projecta, Ramani, Chati, Maumbo,
“Picture Rolls”. Nk.
e) Epuka kubadili somo la Biblia kuwa Hubiri. Hata iwe mbinu ya namna gani, mwalimu /
mkufunzi Mwadventista Msabato sharti amchukue Mwalimu Mkuu Yesu kuwa Mfano
wake. Yeye aliishi kwa kile alichofundisha. Kanuni za Msingi katika ufundishaji wake
zilikumbatia: Upendo, Huruma, Uvumilivu, Urahisi na haki.
Mara kwa mara jaribu kufuata utaratibu ufuatao katika kufundisha somo/mada;
1) Ukumbusho wa somo lililopita kwa ufupi
2) Unganisha somo jipya na ukumbusho

6
3) Fundisha fungu la kukariri kila somo na ni vizuri likawa fupi na wazi kulingana na umri
wa watoto unaowafundisha. Kumbusha kila mara mafungu ya kukariri
waliyokwishajifunza, wasaidie wakariri kwa ufasaha kabisa.
4) Waulize maswali wanafunzi wako na wewe pia uwape nafasi wakuulize maswali,
kuwapima iwapo wamelifahamu somo ulilofundisha vizuri.
5) Somo lifundishwe kwa lugha iliyo rahisi kwa watoto kuelewa.
6) Omba Mungu akuongoze na kukupatia hekima ya kujua namna ya kulitoa somo na
kulifundisha; nakukmbusha tena kila mara kabla ya kuanza somo anza kwa maombi ili
masomo haya yatakaswe kwa ajili ya maisha matakatifu ya mwalimu mwenyewe na
wanafunzi.
KIDATO CHA KWANZA MUHULA WA KWANZA

WIKI 1-2 MUNGU NA NENO LAKE

MALENGO:

1.Mwanafunzi atatambua kwamba maandiko matakatifu yametolewa kwa uvuvio wa Roho


Mtakatifu.

• Mbinu na udhihirisho wa ufunuo

Mwanzo, uvuvio wa Roho mtakatifu na waandishi


SDA BELIEVE FUNDISHO LA 1.

Wanafunzi wanatakiwa kufahamu vitabu vya Biblia, 39 Viko katika Agano la kale na 27
Agano jipya.

 Ajue vitabu vya historia-Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi, Waamuzi


 Manabii wakubwa (Major Prophets) –Isaya, Yeremia, Ezekiel, Daniel, Samweli
 Manabii wadogo (minor Prophets) - Joel, Nahum, Mika, Zefania, Obadia
 Vitabu vya mashairi- Zaburi, Wimbo ulio bora, Maombolezo, Ayubu, Mithali
 Vitabu vya Injili-Mathayo, Marko, Luka, Yohana
 Nyaraka (Epistles)- Wakorintho, Warumi, Wathesalonike, Petro, Yuda, Yakobo.

Neno la Mungu-Biblia ni la pekee sana, Biblia ni kitabu kilichopendwa sana kuliko vitabu
vingine, lakini pia kimechukiwa sana, watu wamekufa kwa sababu ya Biblia, wengine
wameua na kuuawa kwa sababu yake, vita vimeamshwa kwa ajili ya Biblia. Biblia ndio
humdhihirisha Mungu alivyo, ni Maandiko matakatifu, yaliyovuviwa na Roho wa Mungu
(2.Tim3:16)

WIKI 3-4 UUMBAJI

MALENGO:

7
••


1. mwanafunzi ataweza kuelezea dunia/ulimwengu ulivyoumbwa akitofautisha na
dhana za uibukaji.
2. Mwanafunzi aelewe uumbaji wa Mungu na kumtambua Mungu kama muumbaji
wa kila kitu na kuwa wakili mwaminifu kwa uumbaji wake.
• Uumbaji wa mwanadamu, mwanamume na mwanamke (mtu)
(Creation of the universe and of a man)
• Asili ya mwanadamu
• Kuanguka kwa mwanadamu- dhambi yaingia ulimwenguni (The beginning of sin and
suffering)
• Mpango wa Mungu kwa mwanadamu aliyeanguka
• MWANZO 1-3, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 2, NA 58-61

Mwanafunzi atambue kwamba dunia na vyote vilivyomo ni matokeo ya kazi ya


Munguiliyofanyika kwa siku sitana kudhihirisha kuwa dhana ya uibukaji ni ya uwongo wa
Ibilisi. WIKI 5 KIFO NA UFUFUO WA KRISTO

MALENGO:

1.Mwanafunzi atatambua kwamba mshahara wa dhambi ni mauti na kifo cha Yesu ndio
njia ya kutukomboa.

2.Mwanafunzi ataelewa kwamba kufufuka kwa Kristo kulileta tumaini kuwa anazo nguvu
dhidi ya kifo na atatufufua atakaporudi mara ya pili.

• Petro anatabiriwa kumkana Yesu


• Yesu akiwa Gethsemani, Kukamatwa kwa Yesu Yesu mbele ya baraza, na kuhukumiwa
kifo, asulibishwa, Maziko ya Yesu na kufufuka kwake.
• Hatimaye Yesu aonekana mbele za wanafunzi wake.
• MATHAYO 26-28

WIKI 6 KUHESHIMU AMRI YA MUNGU

MALENGO:

1.Mwanafunzi ataweza kujua umuhimu wa kuwa mwaminifu katika matoleo kwa Mungu.

2.Mwanafunzi ataelewa na kuona athari ya dhambi na matokeo ya dhambi.

3.Mwanafunzi atatambua kwamba Mungu ana rehema japo tunatenda dhambi.

8
• Kaini na Habili- sadaka inayokubalika Zaka na sadaka –uwakili wa umilikaji mali.
• Utoaji sadaka wa mapokeo kwa mababu na kwa Mungu
• MWANZO 4:1-16, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 71-79
• Mwanafunzi afahamu kwamba mfumo wa kutoa sadaka za kuteketezwa ulitolewa na
Mungu mara baada ya mwanadamu kuanguka na kufukuzwa bustanini.
• Kaini alikuwa amefundishwa kuwa damu ya mwana wa Mungu ndiyo ingesafisha dhambi
zake. Aliamua kuwa mkaidi.
• Wakazi wa madunia mengine walimwangalia Kaini akitenda dhambi ya kuua!! Je
ukitambua kwamba viumbe vya mbinguni vinakuangalia je jambo hili laweza kukusaidia
usifanye dhambi?

Maswali: Kwa nini Mungu alimuwekea Kaini alama?

WIKI 7-8 KISA CHA NUHU NA GHARIKA MALENGO:

1.Mwanafunzi ataweza kuelezea mwitikio wa Mungu dhidi ya mitindo ya Maisha ya watu


wakati wa Nuhu.

2.Mwanafunzi ataweza kujadili athari ya dhambi ya uzinzi katika jamii ya Nuhu

• Watu wamkataa Mungu


• Nuhu anaitwa kuwa mjumbe wa Mungu
• Nuhu mjenzi na mhubiri
Maisha baada ya gharika
Jengo la kwanza la ghorofa (The tower of Babylon)
MWANZO 6, PATRIARCHS AND PROPHETS SURA YA 95-97, MWANZO 11.
Wana wa Mungu walitokana na uzao wa Seth, na wale wana wa wanadamu walitokana na
uzao wa Kaini, ambao walitanga mbali na Mungu. Muungano usio Mtakatifu kati ya
wana wa Seth na wa Kaini uliongeza kasi ya uovu. Mungu aliwaonya wasioamini kwa
sababu ya hatari aliyoijua, lakini wana wa Seth hawakumsikiliza. Onyo hili bado lipo
hata leo kutooana na wasioamini.
• Baada ya gharika Nuhu alisubiri kwa muda akiwa ndani ya Safina. Je kuna mahusiano
gani kati ya imani na subira?
• Mungu amewatunza watu wake wakati wa zahama, ni kwa jinsi gani Mungu alikutunza
wakati ulipopatwa na changamoto? Toa ushuhuda.

MASWALI:

1.Elezea agano la Mungu kwa Nuhu.

2.Nini madhara ya uzinzi? Je janga la ukimwi limekuwa na matokeo gani katika jamii.

9
••

WIKI 9-10 UTII NA IMANI YA WAZEE (The Patriarchs) MALENGO:

1. Mwanafunzi ataweza kulezea sababu za kuitwa kwa Ibrahimu.

2. Mwanafunzi atajifunza kuwa na imani na utii kwa Mungu.

3.Mwanafunzi ataelezea agano la Mungu kwa Ibrahimu.

• Abraham anaitwa na kutii (The call of Abraham)


• Ahadi ya kuwa taifa kubwa
• Kuzaliwa kwa Isaka na kujaribiwa kwa Abrahamu. MWANZO 12,15 NA 21.

WIKI 11-12 NDOA NA FAMILIA YA ISAKA

MALENGO:

1.Mwanafunzi ataweza kuelezea nafasi ya Isaka katika imani ya Ibrahimu.

2.Mwanafunzi ataweza kuakisi uhalisia wa Maisha ya Esau na Yakobo katika Maisha yake.

10

Isaka amuoa Rebeka
Familia ya Isaka, Esau na Yakobo.
Jukumu la wazazi wa mapokeo ya kiafrika katika ndoa za vijana wao na binti zao
MWANZO 23:1-24, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 171-176 
Isaka alikuwa na Umri wa miaka 37 wakati wa kifo cha Mamake Sarah. 
Sarah alifia Kirjath – arba (mji huu baadaye uliitwa Hebron.
• Katika panjo la Machpela walizikwa Sarah, Abraham, Isaka, Rebeka, Lea na Yakobo.

WIKI 13-14 MWENENDO WA KIKRISTO MALENGO:

1.Mwanafunzi atatambua kwamba tumeitwa kuwa watu wa Mungu kufikiri kuhisi na


kutenda kulingana na kanuni za mbingu.

• Mibaraka ya kuwa na kiasi; Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, tunapaswa kulitunza
• Kuishi vizuri bila matumizi ya madawa ya kulevya, vichocheo, nk
• Afya ya jumla- maji, mazoezi na mlo;
 Mwili wa Mwanadamu asilimia 75 ni maji, lakini maji hupotea tunapotoa jasho na
uchfu mwingine mwilini. Unatakiwa kunywa glass sita hadinane kwa siku. Maji
hutumika pia kusafisha mwili.
 Mazoezi huongeza nguvu mwilini, yanaufanya mwili kuwa imara, huondoa
misongo (stress), huimarisha afya ya ngozi, hupunguza uwezekano wa kupata
magonjwa ya moyo na saratani. Mazoezi si jambo la kuchagua lakini ni la lazima.
Soma Mithali 6:6-13, 14:23)
• Kumbuka mavazi yetu yanatakiwa kuwa ya kawaida tu yasiyo na vikorombwezo vingi,
yawe safi na nadhifu.

WIKI 15-17 KISA CHA YAKOBO

MALENGO:

• Yakobo amdanganya babake


• Ndoa ya Yakobo katika Harani Kurudi kwa Yakobo nyumbani
• Yakobo na familia yake wakaa Misri (Jacob and his family go/dwell in Egypty.
• MWANZO 27:1-41, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 179-182, MWANZO 29-35

WIKI 18-20 UAMINIFU

MALENGO:

1.Mwanafunzi ataweza kuelezea namna Yusufu alivyomtegemea Mungu katika hali zote.

11
2.Mwanafunzi atajifunza kuwa na uwezo wa kushinda majaribu kwa kumwamini na
kumtegemea Mungu.

Yusufu muota ndoto


Yusufu auzwa utumwani
Yusufu katika nyumba ya Potifa na hatimaye gerezani
Tafsiri ya ndoto ya Farao
• Yusufu afanywa mfalme
• MWANZO 37:1-11, PATRIARCHS AND PROPHETS 209-231, MWANZO 39-41,45 .

MUHULA WA PILI

WIKI 1-3 UWEZA WA MUNGU KUOKOA

MALENGO:

1.Mwanafunzi ataelewa kwamba Mungu anao uwezo wa kuokoa

2. Mwanafunzi ataweza kuelezea hali waliyokabiliana nayo wana wa Israel walipokuwa


Misri.

3. Mwanafunzi afahamu kwamba Yesu naye alitukomboa toka utumwa wa dhambi.

4. Mwanafunzi atafahamu Waisraeli waliingiaje Misri.

• Maisha baada ya kifo cha Yusufu


• Kuzaliwa kwa Mussa
• Maisha ya Musa akiwa Midiani
• Kichaka kiwakacho moto
• Wanyenyekevu ndio wanaotumiwa na Mungu
• Mungu ameahidi kuokoa watu wake
• KUTOKA SURA YA 1-3, PATRIARCHS AND PROPHETS UK241-256.

WIKI 4-6 MUNGU AOKOA WATU WAKE KUTOKA UTUMWA WA WAMISRI

MALENGO: 1. Mwanafunzi atatambua kwamba Mungu anao uwezo wa kutuokoa.

12
2.Mwanafunzi ataelewa kwamba Mungu anatoa ulinzi hata tunapokuwa katika shida na
magumu ya dunia hii.

• Musa na Haruni wakutana na Farao


• Mapigo kumi
• Pasaka
• Safari kutoka Misri yaanza
• Kuvuka bahari nyekundu
• KUTOKA 4-6, KUTOKA 11-16, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 257-287.

WIKI 7-9 SAFARI KUZUNGUKA JANGWA MALENGO:

1.Mwanafunzi aweze kujua amri kumi za Mungu.

2.Mwanafunzi ataweza kuelezea namna uasi unavyotokea na adhabu zake.

• Kutoka Bahari ya Shamu hadi mlima Sinai


• Mlima Sinai- Sheria ya Mungu
• Ndama wa shaba- ibada ya sanamu
• Ujenzi wa patakatifu
• Ibada ya waafrika ya mizimu
• KUTOKA 15-16, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 257-287, SDA BELIEVE
FUNDISHO LA 19

WIKI 10-11 SAFARI KUELEKEA KANAANI

• Kutuma wapelelezi 12 kwenda Yeriko


• Uasi wa Kora
• Musa apiga mwamba mara mbili
• Kifo cha Musa
• HESABU 13, HESABU 16:1-49, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 487-493

WIKI 12-13 ISRAELI CHINI YA YOSHUA

Kuvuka mto Yordan

13
• Makazi katika Kaanani
• Vita wakati wa uongozi wa Yoshua
• Hotuba ya mwisho ya Yoshua na kifo chake.

WIKI 14-16 WAFALME WACHUKUA UONGOZI KUTOKA KWA MUNGU.

MALENGO:
1.Mwanafunzi atatambua kwamba zipo nyakati Mungu anaruhusu maamuzi yetu ili
tujifunze.

2.Atafahamu kwamba Mungu anaruhusu viongozi hata wenye tabia zisizofaa kututawala.

• Israeli kutaka kuwa na mfalme


• Mungu awapatia mfalme
• Israeli chini ya mfalme Sauli
• Israeli chini ya mfalme Daudi
• 1. SAMWELI 8, NA 9:10, 1. SAMWELI 16-17:14 PATRIARCHS AND PROPHETS
UK
592-602, 603-615.

WIKI 17-19 ISRAELI CHINI YA MFALME SULEMANI

• Kuimarishwa kwa mfalme Sulemani


• Sulemani aomba hekima
• Utawala wa hekima
• Sulemani ajenga hekalu na ikulu
• Utajiri na ukuu wa Sulemani
• Kushindwa kwa mfalme Sulemani na kifo chake.
• 1.WAFALME 1-11, 1.NYAKATI 28-29, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 750-755

KIDATO CHA PILI

MUHULA WA KWANZA

WIKI 1-3 WAFALME WA ISRAELI

• Kugawanyika kwa ufalme wa Israeli kuwa Yuda na Israeli


• Ufalme wa Yuda
• Ufalme wa Israeli

14
• Kisa cha Ahabu na Eliya
• Kisa cha Ahabu na Nabothi
• Kisa cha nabii Elisha
• Wafalme wengine wa Israeli na Yuda.

WIKI 4 UASI WA ISRAELI

• Sababu za uasi
• Matokeo ya uasi
• Mpango na ahadi za Mungu kuokoa waisraeli wa kimwili na kiroho
• KUMBUKUMBU 9, YOHANA 3:16

WIKI 5-6 KUTEKWA KWA YERUSALEMU

• Yerusalem yatekwa na Babeli/Babiloni


• Miaka ya utumwa
• PROPHETS AND KINGS (WAZEE NA MANABII) UK 452-463

WIKI 7-10 UAMINIFU, TEGEMEO NA KUSHUHUDIA

• Daniel na wenzake wapewa mtihani wa chakula


• Vijana watatu wa kiyahudi wapewa mtihani wa kuabudu sanamu
• Ndoto ya Nebukadneza
• Daniel na rafiki zake watafsiri ndoto
• Sanamu ya dhahabu na tanuru liwakalo moto
• Ndoto ya pili ya Nebukadneza
• Mfalme aliyekula majani kama ng`ombe kwa miaka saba.
• Athari za kiburi
• DANIEL SURA YA 1-4, NA 6

WIKI 11-13 WALIO UHAMISHONI WAREJEA YERUSALEMU

• Mfalme Koreshi asaidia walio uhamishoni kurejea


• Kujenga upya madhabahu, hekalu na kuta
• Upinzani kwa ujenzi mpya
• EZRA SURA YA 1-6

WIKI 14-15 ESTA MALKIA

MALENGO:

15
1.Mwanafunzi ataelewa jinsi Mungu alivyowaokoa watu wake kutoka kwa maangamizi.

2.Mwanafunzi atajifunza kwamba Mungu ni mwaminifu kwa wale wote wanaokuwa


waaminifu

• Esta afanywa Malkia

16
Hila ya Hamani
Msaada wa Esta
• Hamani atundikwa/ anyongwa
• Tarumbeta za wayahudi na ukuu wa Mordekai

Jina la asili la kiebrania la Esther ni Hadasa. Mungu amemtumia msichana/binti tena mwenye
sura nzuri na jasiri kuliokoa taifa lake wakati wa zahama. Tunajifunza kwamba wanawake na
wanaume wanao wajibu au sehemu ya kufanya katika mpango wa wokovu wa watu wake.

Katika Kitabu cha Esther neno au jina Mungu halijatajwa, lakini kazi yake inaonekana. •

ESTA SURA YA 1-10

WIKI 16-17 HISTORIA YA KANISA LETU MALENGO:

Mwanafunzi ataweza kuelezea historia ya kanisa tangu uumbaji hadi kanisa la masalio.

• Mwanzo wa kanisa letu.


• Kazi za kanisa/utume wa kanisa
• Shirika (Organisation) jinsi lilivyo na muundo wake.
• Serikali ya kanisa(mamlaka)
• Dhana ya kanisa kabla ya kuingia kwa Ukristo SDA BELIEVE FUNDISHO LA 12.

WIKI 18-20 KANISA LA MASALIO

MALENGO:

Mwanafunzi ataweza kutambua kanisa la masalio katika kipindi cha kufungwa historia ya
ulimwengu.

• Kanisa la masalio na utume wake Umoja katika mwili wa Kristo.


• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 13. ANGALIA KIAMBATISHO A.

ZOEZI:

Taja tabia zinazolitambulisha kanisa la masalio

17
MUHULA WA PILI

WIKI 1-3 UBATIZO

MALENGO:

1.Mwanafunzi atafahamu ubatizo wa kweli wa Biblia ni upi.

2.Mwanafunzi atapata nafasi ya kuwaelezea na kuwafundisha wengine juu ya ubatizo wa kweli.

• Ubatizo ni nini? Maana ya ubatizo


• Ubatizo wa Biblia
• Ubatizo wa Yesu katika mto Yordani
• Maandalizi kwa ajili ya ubatizo
• Meza ya Bwana na umuhimu wake
• MATHAYO 3, MATENDO 8:27-39, SDA BELIEVE FUNDISHO LA 15 NA 16

WIKI 4-7 KIFO

MALENGO:

Mwanafunzi atajua kwa nini watu wanakufa na nini hatima ya kifo.

• Kifo ni nini?
• Chanzo cha kifo
• Hali ya mfu
• Mwisho wa kifo ni lini?
• Ufufuo- Lazaro afufuliwa
• Imani ya Kiafrika kabla ya Ukristo juu ya kifo na hali ya wafu
• Ufufuo wa mwisho
• 1.THESALONIKE 4:16, MATENDO 2:34, 1.KORINTHO 15:6, YOHANA 11:11-14, ZABURI
6:5,
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 26.
• Wanafunzi watambue kwamba kifo ni usingizi tukisubiri ufufuo. Mathayo 9:24 Wafu hawajui
neno lolote. Mhubiri 9:5
Hakuna kazi wala huduma inayofanyika makaburini na wala hawamtukuzi Mungu huko!!
Mhubiri 9:10
• Madai kwamba wafu huenda peponi ni umizimu ulioanzishwa na Shetani mwenyewe aliposema
`` Hamtakufa hakika`` Mwanzo 3:4

18
• Maandiko matakatifu yamekataza kabisa zoezi lolote lile la kujifanya unawasiliana na
wafu au ulimwengu wa roho. Yeyote yule anayejidai anawasiliana na ndugu zake
waliokufa, anawasiliana na roho za Shetani.
• Kuna fufuo mbili
(a) Ufufuo wa kwanza wa watakatifu unatokea mara Kristo anaporudi mara ya pili
(b) Ufufuo wa pili ni wale waovu ambao unatokea baada ya miaka 1000 ambao unaambatana na
hukumu.

WIKI 8-10 ROHO YA UNABII

• Roho ya unabii ni nini?


• Karama za roho na huduma
• Karama ya Unabii- Ellen G. White
• 1.KORINTHO 12, SDA BELIEVE FUNDISHO LA 17 NA 18 SWALI: Utawajuaje manabii wa
kweli?
1. Ujumbe wake ukubaliane na Biblia-waenende sawasawa na sheria, ISAYA 8:20
2. Anayotabiri yatimie, yatokee, yawe kweli.
3. Anatambua kuwa Kristo alikuja katika mwili, kuzaliwa kwake,kifo chake, ufufuo,kafara ya
upatanisho, kupaa kwake mbinguni na kurudi kwake mara ya pili.
4. Nabii huyo anazaa matunda mema, Mathayo 7:16,18-20. WIKI 11-13 HEMA

TAKATIFU

MALENGO:

1.Mwanafunzi atafahamu kwamba kuna huduma ya patakatifu mbinguni kwa ajili yetu.

2.Atakubali huduma anayoifanya Yesu akituombea na kutupatanisha kule mbinguni.

3.Mwanafunzi ataweza kuelezea jinsi huduma katika hema takatifu ilivyofanyika hapa duniani.

• Hema takatifu hapa duniani


• Hema takatifu mbinguni
• Huduma ya Kristo katika Hekalu la mbinguni WAEBRANIA 8-9.
Yesu alianza huduma ya upatanisho wakati wa kupaa kwake mbinguni. Mwaka 1844 mwisho wa
kipindi cha unabii cha miaka 2300 aliingia katika huduma yake ya pili ya utakaso.

WIKI 14-17 KUJA KWA KRISTO MARA YA PILI

19
MALENGO:

1.Mwanafunzi atajiandaa kwa ajili ya marejeo ya Kristo mara ya pili.

2.Mwanafunzi atatambua kwamba analo jukumu la kuwaandaa wengine kwa ajili ya marejeo ya
Kristo.

• Kuja kwa Kristo mara ya pili kunavotajwa na manabii wa agano la kale


• Kuja kwa Kristo ni halisi
• Kwa nini Kristo anakuja mara ya pili?
• Dalili za kuja kwake mara ya pili
• YOHANA 14:1-3, MATHAYO 24:30, MATENDO 1:9-11, YUDA 1:14-15, ZABURI 50:3,
AYUBU 19:25, 1.THESALONIKE 4:16, SDA BELIEVE FUNDISHO LA 25.

WIKI 18-20 MBINGU MPYA NA NCHI MPYA

• Miaka elfu moja na mwisho wa dhambi


• Dunia mpya
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 27 NA 28.

Kristo anaporudi kama Mfalme wa wafalme anawachukua wateule kwenda nao mbinguni;
Wenye haki waliolala wanafufuliwa na kupaa juu mbinguni waovu wanaangamizwa na
Shetani anabaki peke yake kuzimu (bottomless pit), asipate wa kudanganya tena. Nchi/dunia
inabaki ukiwa na wakati huu watakatifu wanatawala na Kristo kule mbinguni wanapewa kazi
ya kuhukumu ulimwengu Baada ya miaka elfu watakatifu wanashuka katika Yerusalemu
mpya

KIDATO CHA TATU

MUHULA WA KWANZA

WIKI 1-2 MUNGU NA IMANI MBALIMBALI KWA MUNGU

• Je Mungu yupo? Wanaomwamini Mungu mmoja(Theists)


• Wapo wanaokataa mambo yaliyofunuliwa na dini(Deists) na miungu(Polytheists)
Dhana ya Mungu katika muktadha wa Kiafrika kabla ya kuingia kwa Ukristo Mafundisho
ya Biblia kuhusu Mungu
• Utatu mtakatifu
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 1-5.

20
WIKI 3 UUMBAJI

MALENGO: Mwanafunzi atajifunza uumbaji wa kweli kulingana na maandiko


matakatifu na kutofautisha na hadithi zingine za uumbaji.

• Uumbaji au uibukaji
• Hadithi za mapokeo kuhusu uumbaji
• Asili ya binadamu
• Maana na kusudi la uumbaji
• Uumbaji na Sayansi
• MWANZO 1, SDA BELIEVE FUNDISHO LA 6 NA 7

WIKI 4-5 VITA MBINGUNI

MALENGO:

Mwanafunzi atajua kwamba chanzo cha dhambi kilianzia mbinguni

• Mwanzo wa dhambi
• Nafasi ya Lusifa- malaika mkuu
• Jinsi dhambi ilivyoingia katika dunia yetu
• Pambano kuu
• ISAYA 14:13, UFUNUO 12:7-9, SDA BELIEVE FUNDISHO LA 8, PATRIARCHS AND
PROPHETS 34-38, PAMBANO KUU 284-290.

WIKI 6-7 MPANGO WA WOKOVU

• Agano jipya
• Maisha, kifo na ufufuo wa Kristo
• Uzoefu wa wokovu
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 9 NA 10.

WIKI 8-9 NUHU- MHUBIRI NA SEREMALA

• Nuhu aitwa na Mungu na kuagizwa kuonya


• Uasi katika kipindi cha Nuhu

21
• Nuhu anaambiwa kutengeneza Safina na kuhubiri
• Ulimwengu uliharibiwa na gharika
• Nuhu aokolewa na familia yake pamoja na wanyama waliochaguliwa kutoka kila jamii ya
wanyama wenye namna moja
• Upinde wa mvua na ahadi za Mungu
• MWANZO 6-10

WIKI 10-11 WITO WA ABRAHAM.

• Abraham katika Uru


• Abraham anaagizwa kwenda nchi asiyoijua/asiyoifahamu
• Agano na ahadi ya Mungu
• Agano na tohara
• Maana ya tohara miongoni mwa jamii za kiafrika MWANZO 12, 15, 17.

Abraham anaitwa kuacha nchi yake na pia kuacha familia yake na nyumba ya Baba yake, na kamwe
asirudi kwa ndugu zake hao tena damu yake. Hii ilikuwa ni jaribio kali sana.

Nchi ya Kanaani aliyoahidiwa Abraham inaunganisha Palestina, hadi Phoenicia mpaka Syria kusini.
Abraham alikuwa na umri wa miaka 75 alipotoka Haran, kwao.

WIKI 12-13 MUNGU ATIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAMU

• Isaka mwana pekee azaliwa


• Abrahamu aagizwa kumtoa mwanae Isaka kuwa kafara ya kuteketezwa, mtihani mkubwa.
Mungu anatoa sadaka mbadala
• Kifo cha Abrahamu,rafiki wa Mungu
• Wana wa Isaka- Esau na Yakobo
• Familia ya Yakobo
• Yusufu, mwana mpendwa wa Yakobo
• MWANZO 18-19, 21, 27, 37, 42, 46. PATRIARCHS AND PROPHETS UK 138-140, 145157,
183-188.

22
WIKI 14 YUSUFU

• Yusufu anauzwa kuwa mtumwa Misri


• Maisha ya Yusufu huko Misri
• Yusufu mtumwa hatimaye Gavana wanchi
• Wosia wa Yakobo na kifo chake
• Kifo cha Yusufu
• MWANZO 37, 49, 50 PATRIARCHS AND PROPHETS UK 209-231.

WIKI 15 KUZALIWA KWA MUSA

• Maisha ya Musa kama mtoto


• Musa nyumbani kwa Farao
• Musa mchunga kondoo Midiani
• Wito na utume wa Musa
• KUTOKA 2-5 NA 11, PATRIARCHS AND PROPHETS UK 245-283. Maswali
• Haruni alikuwa ni kaka yake Musa, na alimzidi miaka mitatu Angalia Kutoka 7:7
• Miriam alikuwa ni dada yao na aliwazidi wote wawili umri. Mama yao aliitwa
Yokabedi(Jochabed) Baba yao aliitwa Amram mwana wa Kohath.
• Musa alifichwa nyumbani kwa muda gani baada ya kuzaliwa? MIEZI MITATU
• Musa alifichwa katika mto gani? NILE
• Wanafunzi watambue kwamba ni Malaika aliyemwongoza binti mfalme kuelekea kule
ambapo mtoto Musa alipokuwa.

WIKI 16 -17 UKAIDI WA FARAO

• Musa na Haruni mbele ya Farao


• Mungu anamuadhibu Farao Pasaka na kuruhusiwa Mwiko na maana ya pasaka.
KUTOKA 4-6.

WIKI 18-19 UONGOZI NA ULINZI WA MUNGU

• Kufunikwa na wingu mchana na kuongozwa na nguzo ya moto usiku


• Kuvuka bahari ya Shamu
• Maisha ya waisraeli jangwani
• Sheria ya Mungu- Agano pale Sinai

23
KUTOKA 19, WAEBRANIA 8, KUTOKA 33-34, PATRIARACHS AND PROPHETS
287-295

WIKI 20 UASI WA WANA WA ISRAELI.

• Uasi na adhabu
• Kufanywa upya kwa agano

MUHULA WA PILI

WIKI 1-2 KUTEULIWA KWA YOSHUA

MALENGO:

1.Mwanafunzi ataweza kuelezea jinsi Mungu anavyoandaa viongozi kwa ajili ya watu
wake.

2. Atajua sifa nzuri za kiongozi mzuri zinazomwandaa pia kuwa kiongozi wa mfano.

3.Aweze kulinganisha na kutofautisha uongozi wa Musa na ule wa Yoshua

• Kifo cha Musa (The death of Moses)


• Yoshua ateuliwa (Israel under the leadership of Joshua)
• Utekaji wa Kaanani (God commands Joshua to conquer Canaan)
• Kanaani kugawanywa
• Miaka ya mwisho ya Yoshua
• Hotuba ya mwisho ya Yoshua
• KUMBUKUMBU 34, KUMBU 23, YOSHUA 1-2, 20-24, HESABU 32:33-42 na
HESABU 27.

WIKI 3-4 WAISRAELI CHINI YA WAAMUZI


• Debora na Baraka na wimbo wao (The song of Deborah and Barak) Gidioni (Gideon
awashinda wamidian) na kifo chake.
• Abimeleki, Yeftha, Samweli

24
• Samson- kuzaliwa kwake na Mungu alivyomtumia dhidi ya Wafilisti.
• Samson na mwanamke wa Timna, Samson na Delila na kifo cha Samsoni.
• Kuja kwa WAFILISTI.
• Makabila ya Yuda na Simon yateka Adonibezek, Yerusalemu na Hebron Makabila ya
Efrahim na Manasse yateka Bethel.
• WAAMUZI 1-6,8-9,11-16, 1.SAMWELI 1,2,4-8, Waamuzi 21:25

WIKI 5-6 KUZALIWA KWA KRISTO

MALENGO:

1.Mwanafunzi ataweza kuelezea mazingira alimozaliwa Yesu.

2.Mwanafunzi ataweza kujifunza Maisha ya Yesu na kuakisi tabia ya unyenyekevu

• Wazazi wa Yesu
• Tangazo la kuzaliwa kwa Yesu
• (The birth of Jesus is announced; Luke 1:26-56, and Luke 2:1-52)
• Wachungaji wa kondoo na wenye hekima toka mashariki
• Kukimbilia Misri na kurudi Nazareth (The escape to Egypty and the return from Egypty)
• Maisha ya Yesu kama mtoto
• MATHAYO 1,2, TUMAINI LA VIZAZI VYOTE 21,24,28,33,41.
NYONGEZA:
 Nini maana ya jina Imanuel.
 Yesu alizaliwa na kukua na kuishi kama mwanadamu, akaishi na wanadamu ili
aweze kuwakomboa wanadamu wote.
 Nazareth ni mji ambamo Yesu alikulia. Ni mji wa nyumbani kwa Yusufu na
Mariamu. Katika mji huu Yesu alitumia miaka yake 30 kuishi huko, hivyo watu
humwita Yesu Mnazareti.
 Bethlehemu ni mji ambamo Yesu Kristo alizaliwa na matukio mengine
yaliyohusisha kuzaliwa kwake, mfano Mamajusi (Wisemen) kutoka mashariki
walitembelea/walikuja Bethlehemu, mauaji ya watoto wachanga yaliyotangazwa
na Herode (Herod the Great)
 Mfalme Herode alikufa mara tu baada ya kuua watoto wachaanga kule
Bethlehemu.
4.BC WIKI
7 UBATIZO

MALENGO:

25
1.Mwanafunzi ataweza kuelezea nafasi ya Yohana Mbatizaji katika huduma ya Yesu.

2.Mwanafunzi ataweza kuainisha ujumbe wa Yohana mbatizaji na umuhimu wake katika


Maisha yetu leo.

• Yohana mbatizaji, ambatiza Yesu


• Ubatizo wa Kweli
• Yesu ajaribiwa; Mwanafunzi fahamu majaribu matatu aliyojaribiwa Yesu
1) Amuru mawe yawe mkate kama wewe ni mwana wa
Mungu 2) Jitupe chini ikiwa wewe ni mwana wa Mungu 3)
Nitakupa yote haya ukianguka kunisujudia.
 Mwanafunzi ajue majibu aliyoyatoa Yesu;Kama Yesu alishinda majaribu haya
nasi twaweza kushinda, Tumia “imeandikwa” kukabiliana na majaribu
• Wito wa Wanafunzi wa kwanza.,
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 15, MATHAYO 3, MATHAYO 4

WIKI 8-9 HUDUMA YA YESU

• Hotuba mlimani
• Uwezo dhidi ya maradhi na pepo wachafu Uwezo wa kusamehe dhambi.
• MATHAYO 4-7, TUMAINI LA VIZAZI VYOTE 31. MATHAYO 8-9
Wasaidie wanafunzi kuzifahamu heri zote tisa na watie moyo kuwa vijana wapole,
wapatanishi, wenye moyo safi, wenye rehema, n.k
Hebu angalia uwezo wa Yesu
1. Yesu anamponya mtu mwenye ukoma kwa kumgusa
2. Yesu amponya mtumishi wa akida aliyepooza huko Kapernaumu.
3. Yesu amponya mama mkwe wa Petro aliyekuwa na homa
4. Yesu akemea upepo katika bahari akiwa na wanafunzi wake
5. Yesu atoa pepo kwa watu wawili katika nchi ya Wagerasi, pepo watoka na
kuwaingia nguruwe,wateketea baharini
6. Alitoa wengi wenye pepo na wasioweza na aliwasamehe.

WIKI 10 HUDUMA KWA JAMII

MALENGO: Mwanafunzi atatambua umuhimu wa kuchangamana na kuihudumia jamii.

26
• Dalili ya badiliko
• Dalili ya imani
• Yesu achangamana na watoza ushuru na wadhambi
• MATHAYO 9

WIKI 11-14 YESU NA MITUME WAKE

• Yesu awaita mitume kumi na wawili na kuwapa utume wao


• Yesu na Yohana mbatizaji
• Yesu na wataka ishara MATHAYO 10-12,15

Wanafunzi waweze kuwataja kwa majina wanafunzi wa Yesu: Simon Peter, Andrea,
Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo, Tomaso, Mathayo,, Yakobo wa Alfayo,
Thadayo, Simon Mkananayo, na Yuda Isakariote.

Wajue maagizo waliyopewa

1. Kuponya wagonjwa, kufufua wafu na kutoa pepo


2. Mkiingia katika nyumba salimuni
3. Nendeni kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli
4. Maneno ya kuhubiri ni Ufalme wa mbinguni umekaribia
5. Msichukue dhahabu wala fedha wala pesa
6. Kung`uteni mavumbi wasipowasikiliza

WIKI 15-17 YESU NA MIUJIZA

MALENGO:

1.Mwanafunzi atafahamu kwamba Yesu anao uwezo wa kutenda miujiza hata leo

2.Mwanafunzi atakuwa na uwezo wa kutambua miujiza ya kweli na ile ya uongo.

3.Mwanafunzi ataweza kuelezea makusudi ya miujiza aliyofanya Yesu.

• Yesu alisha watu elfu tano


• Yesu atembea juu ya maji Yesu alisha watu elfu nne • MARKO 6, MATHAYO 15.

WIKI 18; MAFARISAYO NA MASADUKAYO

MALENGO:

27
1.Mwanafunzi ataweza kufahamu mafundisho na imani za Mafarisayo na Masadukayo na
jinsi walivyotofautiana.

2.Mwanafunzi ahusianishe mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo kwa makanisa na


dini tulizonazo leo.

WIKI 19; MAFUNDISHO YA YESU

• Sheria za Mungu, Hasira, Uzinzi, uasherati na talaka, Viapo na visasi, kufunga na


kuomba, Upendo kwa maadui, chumvi na Nuru;
• The teachings of Jesus about God`s law, adultery, fornication and divorce, vows and
revenge, fasting and praying, love for enemies, light and salt.
• MATHAYO 5-6.
• Wahimize wanafunzi kuwa kielelezo (model) wanapokuwa shuleni. Walimu na
wanafunzi wenzao wanawaona kama kioo, chumvi ambayo inatakiwa itoe ladha nzuri
kwa wanaotuzunguka, wao ni nuru inayotakiwa kuangaza katika jamii inayowazunguka.
Wawe wavulana na wasichana waadilifu na waaminifu, vijana wanaotegemewa hata
kuwaongoza wengine. Waulize je vijana wetu hapa shuleni mna mvuto gani???

WIKI 20 NDOA NA FAMILIA

MALENGO:

Mwanafunzi atatambua kwamba ndoa ni taasisi takatifu aliyoianzisha Mungu Mwenyewe

• Ndoa ya kwanza
• Ndoa leo zikoje
• Ndoa ya wake wengi, sababu yake ni nini
• Uasherati na uzinzi
• Ndoa katika mtazamo wa kiafrika
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 23, MWANZO 2:18-25.

Maswali: Taja mtu wa kwanza kuoa wake zaidi ya mmoja- Lameki (Ada na Sila).
Vijana wanapaswa kuja kwamba Mungu anachukia Uasherati na Uzinzi, Hii ni sababu
mojawapo iliyosababisha Mungu akachukia na kupunguza umri wa wanadamu kuishi hapa
duniani; soma Mwanzo 6:1-3.

ANGALIA KIAMBATANISHO B

28
KIDATO CHA NNE

MUHULA WA KWANZA

WIKI 1 FAMILIA

• Maana ya Kibiblia
• Jukumu la baba,mama,na watoto
• Familia katika mtazamo wa kiafrika
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 23, EDUCATION UK 20.

WIKI 2-3 YESU ABASHIRI KIFO CHAKE KWA MARA NYINGINE

• Ombi la mama
• Uponyaji wa watu wawili vipofu
• Kuingia Yerusalemu kwa ushindi
• Kutakasa hekalu
• Mtini uliolaaniwa
• Mamlaka ya Yesu yatiliwa shaka
• Mpangaji mwovu
• MATHAYO 20,21

WIKI 4 KAZI ZA YESU NA MIFANO MBALIMBALI ALIYOTOA

• Vazi la harusi
• Kodi kwa kaisari
• Kuwanyamazisha masadukayo
• Changamoto- Kristo ni mwana wa nani?
• Masuto
• Ole saba: Taja ole Saba.
• MATHAYO 22 NA 23

WIKI 5 MAREJEO YA KRISTO

• Dalili za mwisho
• Hekalu labomolewa
• Kuja kwa Mwana wa Adamu
• Kuja mara ya pili kwa Kristo

29
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 25.

WIKI 6 : UWAJIBIKAJI

MALENGO: Mwanafunzi atajifunza kuwa muwajibikaji katika majukumu na fursa


mbalimbali alizopewa na Mwenyezi Mungu.

• Bwana Harusi
• Hukumu
• Wanawali kumi
• Talanta
• Kondoo na mbuzi
• MATHAYO 25

WIKI 7-8 MATUKIO YA MWISHO KATIKA MAISHA YA YESU

• Yesu apakwa mafuta huko Bethania


• Meza ya Bwana ya mwisho
• Kukamatwa na kushtakiwa
• Kusalitiwa
• Kusulubishwa: Kazi ya damu ni nini? Damu ilitumika kama kiini cha utakaso katika
huduma ya hekalu, Soma Mambo ya Walawi 17, maisha ya mnyama yako kwenye damu.
Maziko na ufufuo
• MATHAYO 26-28, SDA BELIEVE FUNDISHO LA 26. WIKI 9 MWENENDO

WA KIKRISTO MALENGO:

Mwanafunzi ataelewa ni jinsi gani anavyopaswa kuenenda kama Mkristo,

• Sinema, Television na Radio


• Muziki na dansi
• Usomaji wa vitabu vya hadithi(novels)
• Shughuli nyingine zisizokubalika
• Uasherati na uzinzi
• KUTAYARISHA NJIA UK 185-192, SDA BELIEVE FUNDISHO LA 22. WIKI 10 :
PENTEKOSTI MALENGO:

1.Mwanafunzi ataweza kuelezea nnini kilichotokea siku ya Pentekoste.

2.Atajifunza kufanya maandalizi kwa ajili ya kumkaribisha Roho Mtakatifu katika maisha
yake.

30
• Roho mtakatifu aja siku ya Pentekosti;
• Petro ahutubia kusanyiko
• Ushirika wa waumini(fellowship)

31

Petro atenda muujiza na kuhutubia watazamaji

• MATENDO 2 NA 3.

WIKI 11 KAZI ZA MITUME

• Petro na Yohana wafungwa gerezani


• Utetezi wa Petro mbele ya Sanhedrin
• Ombi la waumini
• Waumini washiriki pamoja na mali zao
• Anania na Safira wamdanganya Roho Mtakatifu na waadhabiwa
• MATENDO 4 NA 5

WIKI 12: MITUME NA ZAHAMA

1.Mwanafunzi ataweza kuelezea kazi walizofanya mitume kule Yerusalemu.

2.Mwanafunzi ataweza kulinganisha jinsi kanisa linavyowahudumia watu leo


ikilinganishwa na kanisa la awali.

3. Mwanafunzi atagundua kwamba kumtumikia Mungu kuna gharama pia.

• Mitume wateswa
• Saba wachaguliwa
• Stefano akamatwa
• Hotuba ya Stefano mbele ya Sanhedrin
• Stefano apigwa mawe
• Mathayo alikufa kwa kuuawa na upanga mbali kidogo na mji wa Ethiopia • Marko alifia
Alexandria baada ya kukokotwa kikatili kwenye barabara za mji.
• Luka alitundikwa juu ya mti wa mizeituni nchini Ugiriki
• Yohana alitiwa katika pipa la mafuta lichemkalo lakini kwa muujiza wa Bwana hakufa,
baadae akapelekwa katika kisiwa cha Patmo ileafie huko, hakufa. Baadae alikuwa akiwa
mzee tu wa siku.
• Petro alisulibiwa Rumi kichwa chini miguu juu
• Yakobo wa Zebedayo alikatwa kichwa huko Jerusalemu
• Yakobo wa Alfayo alitupwa toka kwenye kinara kirefu cha kanisa halafu akapigwa rungu
lenye msumari hadi akafa
• Batholomayo alichunwa ngozi akiwa hai, hadi kufa
• Andrea alifungwa kwenye msalaba hadi akafa

32

Tomaso alishindiliwa mkuki ndani ya mwili India ya Mashariki (Coromandel)


• Yuda Thadayo alipigwa na mishale mpaka akafa
• Paulo baada ya mateso ya muda mrefu alikatwa kichwa huko Rumi na Mfalme Nero
• MATENDO SURA YA 6 NA 7,Knight`s Master Book of Illustrations, pg 587

WIKI 13 MATENDO YA MITUME

• Mateso ya kanisa; Sauli alihusika kwa kiwango kikubwa kabla ya kuongoka


• Filipo katika Samaria; aliponya viwete, waliopooza, na waliopagawa na aliwabatiza kwa
jina la Bwana Yesu.
• Simon Mchawi
• Filipo na Mkushi
• Ubatizo wa kweli: Yesu aliingia majini, katika mto Yordani, na Filipo na Mkushi pia
wote wawili waliingia majini na kupanda kutoka majini
• MATENDO SURA YA 8 , SDA BELIEVE FUNDISHO LA 15

Swali; Mtume wa kwanza mmishonari huko Samaria aliitwa nani? FILIPO.

Filipo huyu ndiye aliyembatiza Towashi wa Ethiopia wakati akienda Gaza

Baadaye alifuatwa na Petro na Yohana ambao waliwawekea mikono waongofu.

WIKI 14 UONGOFU WA SAULI

MALENGO: Mwanafunzi ataweza kuelezea/kusimulia namna Sauli wa Tarso


alivyoongolewa.

• Safari ya Sauli kwenda Dameski


• Sauli akutana na Yesu kisha aongolewa
• Sauli aingia Dameski na kurudi Yerusalemu
• Aienea na Dorka: Ainea alikuwa amepooza miaka minane, aliishi Lida. Huyu aliponywa
na Petro. Petro alimfufua Tabitha au Dorka mjini Yafa.
• MATENDO 9

WIKI 15 PETRO AFANYA UMISHONARI

• Kornelio amwita Petro


• Maono ya Petro
• Petro katika nyumba ya Kornelio
Kanisa katika Antiokia

33

• Muujiza wa Petro kutoka gerezani Kifo cha Herode

Himiza Wanafunzi kuwa watu wa Maombi, watauwa na wachaji wa Mungu, Mungu


anapendezwa na tabia hizi, anajivunia watu wa namna hii, na anawapenda sana. MATENDO
10 NA 11, NA 12.

WIKI 16 UTUME WAVUKA MIPAKA

• Barnaba na Sauli watumwa huko Saiprus


• Kazi yafikia Pisidia na Antiokia
• Kurudi Antiokia katika Shamu
• Baraza huko Yerusalemu –salaamu na kuaga

MUHULA WA PILI

WIKI 1-2 MITUME NA UTUME

• Timotheo afuatana na Paulo na Sila


• Maono ya Paulo na mtu wa Makedonia Uongofu wa Lidya katika Filipi Paulo na Sila
katika gereza.

Kijana Timotheo alitoka katika wilaya ya Derbe-Listra (Lystra). Maana ya jina hili ni
“aliyeheshimiwa na Mungu”. Alikuwa na umri kati ya miaka 18-20. Ni kijana ambaye
alikuwa tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha na utume na akamruhusu
Kristo amtumie. Mama yake aliitwa Yunisi (Eunice).
Vijana wana nafasi ya kumtumikia Mungu pia, Mfano mzuri ni Timotheo.

• Lidia, mmojawapo wa waongofu wa kwanza wa Paulo alikuwa mwanamke mkarimu, na


alijishughulisha na biashara za kuuza nguo.

SWALI; Ni nini kilisababisha Paulo na Sila watupwe gerezani huko Filipi? Baada ya
kumtoa kijakazi mmoja pepo ambaye kupitia kwa mapepo hayo alitengeneza faida
nyingi kwa ajili ya familia yake, waliona wamepata hasara.

• MATENDO 16

WIKI 3-4 KANISA

• Kanisa la masalio na utume wake Pambano kuu.


• SDA BELIEVE FUNDISHO 8, NA 13.

34
WIKI 5-6 KAZI YA INJILI HUKO THESALONIKE

• Bera, Ikonia, Prisila, Akila, Apolo, na Athene Paulo katika Efeso na fujo kutokea.
• MATENDO 17-19

Paulo akiwa Thesalonike aliingia katika sinagogi la Wayahudi na kufundishana nao neno la
Mungu Sabato tatu; mafungu haya yanaonyesha kwamba Mitume waliendelea kuitunza
Sabato. Tatizo walilokumbana nalo hawa mitume ni kuhubiri habari za Yesu, tena kama
Mfalme.

Paulo alipofika Athene- Ugiriki alichukia sana kuona masanamu, Hii inatupa picha kuwa
Ibada ya kuabudu sanamu ilikuwepo hata wakati wa Yesu na mitume; wanaabudu mungu
asiyejulikana.

WIKI 7-8 UWAKILI

MALENGO:

Mwanafunzi atajifunza kuwa wakili mwaminifu kwa vyote Mungu alivyompatia.

• Kushuhudia
• Muda na uwezo
• Zaka na sadaka
• Matumizi ya zaka
• Mibaraka ya uwakili
• SDA BELIEVE FUNDISHO LA 21

WIKI 9-10 PAULO MAKEDONIA NA UYUNANI

• Paulo awaaga wazee wa Efeso


• Kuelekea na kuwasili Yerusalemu
• Paulo akamatwa na kuhutubia mkutano
• Paulo raia wa Rumi
• MATENDO 20-22

WIKI 11-12 PAULO MBELE YA SANHEDRIN

• Njama ya kumuua Paulo


• Paulo ahamishiwa Kaisaria
• Paulo mbele ya Feliki
• Paulo mbele ya Festo
• Paulo mbele ya Agripa

35
• MATENDO 23-26

WIKI 13-14 PAULO NA UTUME ROMA

• Dhoruba na kuvunjika kwa merikebu


• Pwani ya Melita
• Paul awasili Roma na kuhubiri chini ya ulinzi mkali
• MATENDO 27-28

WIKI 15-16 INJILI YA MILELE

• Ujumbe wa malaika watatu


• Mcheni Mungu na kumtukuza
• Msujudieni aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na vyote.
• Umeanguka Babeli-Tokeni Babeli
• Mtu atakayemsujudia mnyama na sanamu yake na kupokea chapa katika kipaji cha uso,
atapokea ghadhabu ya Mungu.
• Hapa ndipo penye subira ya watakatifu wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu
• UFUNUO 14

Malaika huwakilisha watakatifu wa Mungu wanaojishughulisha na kazi ya kutangaza injili ya


milele.

Neno Babeli linahusisha dini zote ambazo zimetanga mbali na ukweli


Unabii wa kuanguka kwa Babeli unatimizwa wakati wa vuguvugu la Uprotestanti. Watu
kama William Miller walianza kuhubiri ujumbe wa Marejeo mnamo mwaka 1844.

WIKI 17-20: MIFANO YA YESU (THE PARABLES OF JESUS CHRIST)

• Mfano wa Mpanzi- The parable of the sower


• Mfano wa magugu- The parable of weed
• Punje ya Haradali- The parable of mustard seed
• Mfano wa chachu- The parable of Yeast
• Mfano wa hazina iliyositirika- Hidden Treasure
• Mfano wa Lulu- Pearls
• Mfano wa nyavu- The parable of the net
• Mfano wa Msamaria mwema- The good Samaritan
• Mfano wa mjane na hakimu- The widow and the judge
• Mfano wa Farisayo na mtoza ushuru- The Pharisee and the Tax collector
• Mfano wa Sarafu ya dhahabu- The Gold coins
• Mfano wa kabaila na watumwa- The parable of the tenants in the vineyard.

36
MATHAYO 13, LUKE 10:38-42, LUKE 18:1-14, LUKA 19.

REJEA

 Ministerial Association, General Conference of Seventh-day Adventists, Seventh-day


Adventists Believe, Pacific Press Publishing Association, Boise, ID 83653, 2005.

 East-Central Africa Division, History of Redemption study guides, Everlasting


Gospel Publishing Association

 Seventh-day Adventist Bible Commentaries


 The United Republic of Tanzania, Ministry of Education and vocational Training,
Bible Knowledge Syllabus for secondary schools,2012  The Bible.

37

You might also like