Professional Documents
Culture Documents
Kwa elimu hii ya saikolojia unaweza kufahamu vyanzo vya tabia flani
kwa binadamu, pia inampa binadamu uwezo wa kujielewa madhaifu
yake na mazuri yake na namna bora ya kuyaepuka (madhaifu) au
kuishi nayo bila kuleta madhara na namna bora ya kuyaendeleza
mazuri aliyonayo.
Pia upatikanaji wa elimu hii ya saikolojia sio kitu kigumu kama watu
wengi wanavyo dhani.
Kuipata elimu hii sio lazima uhudhurie mafunzo maalumu katika chuo
husika kwa sababu maisha yetu kwa asilimia kubwa yametawaliwa na
elimu hii ya saikolojia.