Professional Documents
Culture Documents
Nishani Ya Kwata
Nishani Ya Kwata
NISHANI YA KWATA
1. Makusudi 7 ya kwata:-
(a) Amri = inasaidia kudumisha umoja wa taasisi
(b) Motisha= inafundisha nidhamu na umoja wa kundi
(c) Furaha= shughuli za furaha, inakuza matumizi ya ubunifu
(d) Mahusiano= inamsaidia mtu kujifunza kupokea amri na kuzifuata
(e) Uongozi= inamsaidia mtu kutoa amri na kujenga kujiamini
(f) Kujitawala= kutoa usikivu kwa kiongozi
a. Attention (mguu sawa). Kusimama mguu sawa kunahitaji miguu yako kuwa pamoja
na vidole vyako vikiwa kwenye pembe ya nyuzi 45. Mikono yako ikiwa imebanwa
kwenye pindo la suruali yako au gauni au sketi kama vile umeshilia gombo
lililoviringishwa na dole gumba likiwa juu ya kidole karibi nalo (index finger).
Macho yako daima yatakuwa yametazama mbele. Huruhusiwi kuongea labda kama
umeambiwa kufanya hivyo. Karibu amri zote za kusimama vile vile na amri za
kutembea mbele zinatolewa katika mkao huu wa mguu sawa.
b. Gwaride kupumzika. Kama wakati wa mguu sawa, macho yako daima yatakuwa
yakitazama mbele. Wakati wa kuambiwa pumzika mguu wako wa kushoto
unasogea mbali na mguu wa kulia na unakunjwa kidogo nyuma. Mikono yako sasa
inakuwa nyuma mkono wa kushoto ukiwa nyuma ya mkono wa kulia. Grwaride
pumzika ,amri hii inatolewa tu wakati mkiwa mguu sawa. Tumezoea kusema ‘heizi’
mwili legeza.
c. Mguu pande. (stand at Ease). Mguu pande ni sawa kabisa na kupumzika isipokuwa
tu kwa mambo mawili. La kwanza kila jicho na kichwa vinapaswa kumtazama
daima anayetoa amri. La pili, mikono inakuwa imelegea zaidi kuliko la kwanza,
japokuwa mikono inakuwa pale pale kama wakati wa kupumzisha gwaride.
d. Mguu pande ni karibu sawa na kupumzisha gwaride. Japo unatakiwa uwe kimya
na kuweka mguu wako wa kulia vizuri kwa kupokea amri wakati wo wote, japo
hapa unaweza kusogea kama itakavyohitajika. Mikono yako inaruhusiwa kuwa
chini zaidi kuliko inavyotakiwa kwa kupumzisha gwaride. Amri hii inaweza
kutolewa ukiwa mguu sawa, kupumzisha gwaride (legeza mwili) au mguu pande.
e. Usawa wa kulia. Hiki ni kitendo cha watafutanjia kutembea kwa kufuata usawa wa
mstari ulioko upande wa kulia (right flank) ili kuwasaidia kudumisha mstari mmoja
ulio mnyoofu kikamilifu. Wakati wa mwendo huu, watafutanjia wanapaswa kubana
mikono yao katika usawa wa pindo za mavazi yao (sketi au suruali), miguu
huinuliwa juu kwa usawa wa nyuzi 45, na hutembea kwa kwenda mbele, yaweza
kuwa ni kwa mwendo wa haraka au mwendo wa pole.
Kuitisha watafutanjia (FALL IN). kwanza wanasimama mstari mmoja toka mrefu hadi mfupi.
Kisha wanahesabu namba toka kulia namba fupi fupi yaani 1 na 2; wanatengeneza mistari
miwili kisha wanageuka kulia waliohesabu moja na waliohesabu mbili wanageuka kushoto.
Aliye kulia anatulia kisha wanaanza kujipanga mistari mitatu.
UUMBAJI WA MISTARI.
nyekundu
kijani
bluu
pink
nyekundu
kijani
bluu
pink
SAFU.
NAFASI
UMBALI
SHEREHE ZA UFUNGUZI
Hii ni programu ambayo inafanywa kila siku Watafutanjia wanapokutana kwa ratiba zao za
kawaida
Utaratibu wake.
1. Kuwaitisha watafutanjia (fall in)
2. Kupandisha bendera
3. Kuimba wimbo wa Watafutanjia
4. Kukariri ahadi na sheria
5. Taarifa ya mahudhurio ya vikosi mbalimbali vya Watafutanjia
6. Maombi na kutawanyika
Sherehe za kufunga
1. Kuitisha Watafutanjia (fall in)
2. Kushusha bendera
3. Kuimba wimbo wa Watafutanjia
4. Matangazo ya mkurugenzi
5. Ombi la mwisho
6. Kutawanyika
Baada ya maelezo haya mafupi, hakikisha unakuwepo kwenye mazoezi ya mtaalamu wa
gwaride ili kupata hali halisi ya kuwaongoza watafutanjia pamoja na Master Guides wote.
Hakikisha una mwongozo wa gwaride unaokubalika. Kwa sasa tunatumia Mwongozo wa
Amerika ya Kaskazini ambao unapelekana na gwaride la Tanzania. Maelezo mengine
yanatofautiana kidogo sana kulingana na hali yetu ya Kitanzania.