You are on page 1of 2

SEHEMU ZA MWILI

Mwili wa binadamu unavyo viungo tele.


- Kila kiungo kina kazi yake na ni lazima vyote vishirikiane ili mwili uwe katika
hali nzuri. 
1. Ulimi (tongue)– kiungo cha kuonjea, kilicho ndani ya mdomo.
2. Meno(teeth) – hutafunia chakula.
3. Ufizi(gum,) – nyama ishikiliayo meno.
4. Utaya (jaw)– mfupa unaoyashikilia meno.
5. Koromeo/umio( oesophogus )– mfereji unaotumikia kuteremshia chakula au
kinywaji hadi tumboni. Kifuko kinachotolea mate.
6. Tumbo(stomach) – sehemu ya kupokea chakula na kuanza kukisaga.
7. Uchanga/uchengele/chango (large interstine)– utumbo mwembamba wa
kupitishia chakula kilichosagwa.
8. Moyo/mtima (Heart)– kiungo kisukumacho damu ili ienee mwilini.
9. Mshipa (veins)– mrija au mfereji mdogo unaopitisha damu na pia fahamu katika
mwili wa kiumbe.
10. Neva (nerves)– mishipa ya fahamu mwilini.
11. Ateri(arteries)– mshipa mkubwa uchukuao damu kutoka moyoni.
12. Pafu/lungs – kiungo kinachotumika kusafishia hewa. Hutoa hewa chafu na
kuingiza hewa safi mwilini.

You might also like