You are on page 1of 9

HOTUBA YA MHE.

UMMY MWALIMU (MB) WAZIRI WA AFYA,


MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KWENYE
UZINDUZI WA BARAZA LA USAJILI WA WATAALAM WA AFYA YA
MAZINGIRA NCHINI TAREHE 14/04/2016.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto,
Mganga Mkuu wa Serikali,
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga,
Mwenyekiti wa Baraza la Usajili wa Wataalam wa Afya ya Mazingira
Nchini,
Msajili Baraza la Usajili wa Watalaam wa Afya ya Mazingira Nchini,
Wasajili wa Mabaraza wa Kada za Afya,
Wajumbe wa Baraza la Usajili Wataalam wa Afya ya Mazingira,
Wataalam wa Afya ya Mazingira Nchini,
Wanahabari,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia
afya njema. Pili, napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote kwa kufika
1

kwenu kushuhudia kuzinduliwa kwa Baraza hili la Wataalam wa Afya ya


Mazingira nchini awamu ya tatu. Aidha, nawapongeza sana wajumbe wote
wa Baraza lililopita kwa kuendeleza kazi za kuliimarisha Baraza la Afya
Mazingira.

Leo

hii

tunapokea

wajumbe

wapya

kuendeleza

yale

yaliyoanzishwa katika awamu ya kwanza na ya pili na sasa ni awamu ya


tatu ya utekelezaji. Aidha, ningependa kuwashukuru wote ambao mmeacha
shughuli zenu na kukubali kuitikia wito wa kuja kushiriki pamoja nasi katika
tukio hili muhimu na la kipekee katika historia ya kada ya afya ya mazingira
nchini. Nawashukuruni sana.
Ndugu Mwenyekiti,
Afya ya Mazingira ni eneo muhimu na nyeti, ambalo utekelezaji wake
unajikita zaidi katika kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yale
yasiyo ya kuambukiza katika jamii yetu. Serikali ya awamu ya tano chini ya
Mheshimiwa Rais, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli imeona umuhimu wa
suala hili hususan pale ambapo sherehe za Uhuru zilipobadilishwa na
kuadhimishwa nchi nzima kwa kufanya usafi wa mazingira ili kuonyesha
kuwa maendeleo ya taifa lolote yanategemea afya za wananchi wake.
Kauli mbiu Mtu ni Afya na Kinga ni Bora Kuliko Tiba zimekuwa
zikitumika sana kwa nguvu zamani wakati wa uhuru. Kaulimbiu hizi bado
zina umuhimu katika maisha yetu ya hivi sasa hivyo, tunapaswa
kuikumbusha jamii yetu kuwa kila mwananchi anapaswa kuwekeza kwenye
usafi wa mazingira kwa kuanza

na kudumishaji usafi binafsi, usafi wa


2

nyumba yake ya kuishi, usafi katika eneo lake la kazi, usafi katika vyombo
vya usafiri, usafi katika sehemu za biashara, usafi katika nyumba za kulala
wageni, usafi katika sehemu zinazouza vyakula, usafi na usalama wa
vyakula na maji, usafi katika viwanda, migodi, mashamba, taasisi na nk.
Aidha, ni ukweli usiopingika kuwa kila sehemu inahitaji kuwekwa katika hali
ya usafi na endelevu ili kudumisha kanuni za afya mazingira.
Ndugu Wananchi,
Katika ya miaka hivi karibuni, Serikali imefanya maboresho katika sekta ya
afya nchini ambayo yanalenga katika kuimarisha na kudumisha huduma
bora za afya ya msingi kote nchini. Miongoni mwa masuala muhimu ni
kuweka msingi na taratibu za kuhakikisha watoa huduma za afya
wanazingatia sheria, kanuni, miiko na maadili ili waweze kutoa huduma
kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu. Pamoja na mambo mengine Serikali
imetunga Sheria ya Kusimamia na Kudhibiti Utendaji wa Wataalamu wa
Afya ya Mazingira ya mwaka 2007, na kutengeneza Kanuni za Ujumla za
Sheria zinajulikana kwa jina la kiingereza The Environmental Health
Practitioners (General) Regulations 2011. Kanuni ya 3, 4 na 5
zinazungumzia suala la Usajili, kuorodheshwa na kuandikishwa kwa
Wataalam wa Afya ya Mazingira Nchini. Aidha Kanuni ya 12 ya Kanuni za
Ujumla za Usajili inasisitiza kusajiliwa kwa wataalam wote wenye taaluma
ya Afya Mazingira kote nchini.

Ndugu Wananchi,
Napenda kutoa msisitizo juu ya suala hili kwa kuzitaja huduma za afya ya
mazingira

zinazostahili kusajiliwa na Baraza la Afya Mazingira kama

ifuatavyo; Huduma za kuzoa, kuhifadhi, kusafirisha na kutupa taka,


kunyonya, kusafisha, kusafirisha na

kumwaga maji taka, huduma za

Kuuza vyakula (mahoteli, migahawa ya aina zote, maoko ya mikate,


maduka yauzayo nyama, maduka ya vyakula, viwanda vya vyakula, Kuuza
maji, Kuuza vyakula kwenye sherehe, uuzaji juisi mbalimbali na shughuli
za kukoboa na kusaga nafaka). Huduma za viwanda vinavyozalisha
kemikali, vumbi, mionzi. Huduma zinazozalisha taka hatari zitokanazo na
huduma za kidaktari (health care wastes). Huduma za kusafisha na ufagizi
wa ofisi, mitaa, mifereji ya maji machafu, ukusanyaji na uteketezaji
takataka (incinerators services). Huduma za uangalizi wa dampo na
uchambuzi wa taka rejea (recycling). Huduma ya upuliziaji dawa za
Viuatilifu kwenye maghala, hospitali, mashamba, majumbani, maofisi na
kwenye vyombo vya usafiri. Huduma za Vyoo vya Jumuiya, vyoo vya muda
(mobile and temporary toilets). Huduma za nyumba za kulala wageni,
maeneo ya kuogea (swimming pool), kinyozi na saloons za aina zote.
Huduma zitokanazo na Biashara zinazozalisha machukizo offensive
trades (kuchoma mifupa, kukaanga samaki, kukausha majongoo).
Huduma za utengenezaji majeneza na maziko ya wafu. Haya yote
yamebainishwa katika Kanuni ya Ujumla ya Usajili (GN 388 ya tarehe 25
Nov. 2011).
4

Ndugu Mwenyekiti,
Taaluma ya Afya ya Mazingira ni muhimili muhimu katika kupambana na
magonjwa ya mlipuko. Shirika la Afya Ulimwenguni ambapo Tanzania ni
miongoni mwa mwanachama, lilitengeneza Kanuni za Afya za Kimataifa
(The International Health Regulations) kwa mujibu wa Kanuni hizi
wataalamu wa Afya Mazingira ndio wasimamizi wakuu wa Kanuni hizi na
wana wajibu wa kuhakikisha kuwa wageni wote wanaoingia nchini kupitia
katika mipaka yetu wanakaguliwa kwa kusudi la kuzuia magonjwa
yanayoripotiwa Kimataifa. Nchi nyingi zinazoendelea hivi leo zinakabiliwa
na changamoto ya wataalamu wa afya mazingira kukosa tekinolojia ya
kisasa na endelevu, vitendea kazi duni, mazingira duni yasiyoridhisha
kiafya, hali mbaya ya uchumi, soko la ajira, uzembe na uzururaji, Rushwa,
ushindani wa kitaaluma, mabadiliko ya tabianchi (kuongezeka kwa joto
duniani), matumizi ya kemikali na viuatilifu yasiyozingatia misingi ya afya
mazingira.
Katika sekta ya Afya, kuna changamoto nyingi zikiwemo za ongezeko la
magonjwa ya milipuko yatokanayo na uchafuzi wa mazingira, hususan
ugonjwa hatari wa kipindupindu. Aidha, Afya Mazingira ni suala mtambuka
ambalo linahusisha wadau wengi katika kulitekeleza. Ni muhimu katika
utekelezaji wa majukumu yake, Baraza lishirikishe kwa karibu wadau
mbalimbali kutoka sekta mbalimbali ili kutoa matokeo chanya yenye tija na
ubora wa hali ya juu kwa taifa letu. Ni matumaini yangu kuwa tutafanya

kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kupunguza ama kuondoa changamoto


nyingi zinazotukabili kwa kusudi la kuzuia maambukizi ya magonjwa.
Ndugu Mwenyekiti,
Kwa muda mrefu, kumekuwepo matukio ya ukiukwaji wa maadili katika
utoaji wa huduma za afya ya mazingira nchini, ambapo matatizo ya
kitaalam hutolewa maamuzi bila ya kuzingatia taratibu na misingi ya
taaluma. Hili ndilo lilipelekea kuanzishwa kwa Baraza la Usajili wa
Wataalam wa Afya ya Mazingira nchini kama chombo pekee cha
kusimamia na kudhibiti utendaji wa Wataalamu wa Afya Mazingira nchini.
Utendaji wa Baraza litakalozinduliwa leo unatakiwa kuwa wa kasi zaidi,
katika maamuzi kwa kuzingatia misingi ya utawala bora. Aidha, nawaasa
Wataalamu wa Mazingira nchini mbadilike na kufanya kazi kwa weledi,
umahiri, bidii na kwa kuzingatia mongozo ya maadili na nidhamu ya kazi ili
kuinua hali za Afya za wananchi.
Ndugu Wananchi,
Ni matarajio ya Serikali kuwa kwa kutumia Baraza hili kama chombo cha
Taaluma ya Afya Mazingira, yafuatayo yatainufaisha jamii yote ya
watanzania;
Huduma ya afya ya jamii

hapa nchini itatolewa kwa viwango

vinavyotakiwa na hivyo kuboresha maisha ya wananchi Baraza

litasimamia na kudhibiti utoaji wa huduma ya afya ya mazingira kwa


misingi ya haki.
Wataalam wa kada hii watajiendeleza ili kuinua kiwango cha taaluma
ya Afya Mazingira.
Kuendelea kutengeza kanuni, viwango vya utoaji huduma na kuweka
taratibu sahihi za kiutendaji zinazoendana na wakati.
Kumaliza tatizo la ugonjwa wa kipindupindu nchini na kupunguza kasi
ya magonjwa ya kuambukiza.
Ndugu Mwenyekiti,
Sheria imeweka bayana na kuainisha majukumu na mamlaka ya Baraza
kama ifuatavyo;
Kuweka bayana majukumu ya makundi ya wataalamu wote
wanaostahili kusajiliwa na hivyo kutoa huduma ya afya ya mazingira
hapa nchini chini ya Sheria hii.
Kuweka

bayana

adhabu

zitakazotolewa

kwa

wataalamu

watakaokiuka kanuni, taratibu na maadili vya kitaalamu ya


wataalamu wa fani hii kwa mujibu wa Sheria.
Kusajili wataalamu wa afya ya mazingira kulingana na viwango vya
utaalamu wao pamoja na taasisi zinazotoa huduma za Afya
Mazingira.

Kuweka vipengele mbalimbali vya kisheria ambavyo vitasimamia


utekelezaji wa kazi za Baraza n.k
Kuainisha vyanzo vya mapato mbalimbali ya baraza kwa ajili ya
uendeshaji wa shughuli zote za Baraza.
Ndugu Mwenyekiti,
Katika kuhakikisha kuwa Baraza la kusajili wataalamu wa afya ya
mazingira linafanya kazi yake ipasavyo, sheria imebainisha muhula wa
utendaji kazi Baraza teule, kuwa ni miaka mitatu kuanzia tarehe ya uteuzi
kipindi hiki sio kirefu. Lakini tunayo matarajio makubwa sana kwenu.
Nawaomba kufanya kazi kwa bidii ili kuwa kielelezo, tumieni muda wenu
vizuri katika kufanya maamuzi yenye tija kwa wakati ili kuendeleza taaluma
bila kuruhusu uzembe kazini ili ifikapo Mwaka 2018 kazi zitakazokuwa
zimefanyika iwe kielelezo bora na mfano wa kuigwa na Baraza
litakalopokea kijiti.
Baada ya kusema hayo machache nitoe rai kwa wananchi kutoa
ushirikiano kwa wataalamu hawa wa Afya ya mazingira nchini kwa vile
majukumu yao yanategemea sana ushirikiano wenu. Aidha nawaagiza
wataalamu wa afya ya mazingira nchini kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria,
Kanuni na Miongozo ya Nidhamu na Maadili Kitaaluma. Nitumie fursa tena
hii kuliagiza Baraza litekeleze majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya
Sheria ili kudumisha utawala bora.
8

Baada ya kusema hayo napenda sasa nitamke kuwa Baraza la Usajili wa


Wataalamu wa Afya Mazingira Awamu ya Tatu leo tarehe 14 Aprili, 2016
limezinduliwa Rasmi.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.

You might also like