You are on page 1of 2

Tanzania Editors Forum

Zanaki Street Plot No. 2285/7, Opp. CCM Office Mtendeni Branch
P.O.Box 75206 Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 22 123236 Mob: +255 715 339090, +255 713 488269

TAMKO LA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)


KUHUSU KUFUNGWA KWA VITUO VYA RADIO 5 NA MAGIC FM
1.0 UTANGULIZI
1.1 JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limeshtushwa na kusononeshwa na hatua ya
Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya Radio; Radio 5 ya Arusha na Magic
FM cha Dar es Salaam, uliotolewa jana Agosti 29, 2016.
1.2 Katika muda wa miezi takriban kumi tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Habari,
Mh.Nnauye amejitokeza mara nne mbele ya VYOMBO VYA HABARI kutangaza
kufuta au/na kufungia VYOMBO VYA HABARI. Alianza kulifuta Gazeti la Mawio,
baadaye alitangaza kufuta mamia ya magazeti na majarida ambayo hayajachapishwa
kwa muda mrefu, ikafuata adhabu ya kulifungia kwa miaka mitatu Gazeti la Mseto na
sasa vituo viwili vya redio.
1.3 Katika tukio la kufutwa kwa mawio, tulihoji ukubwa wa kosa la gazeti hilo kiasi cha
kufutwa. Leo hii tunahoji tena ukubwa wa makosa na pengine historia ya radio husika
siku zilizopita. Ndiyo maana tunasema hili la sasa ni mwendelezo wa ukandamizaji wa
uhuru wa habari.
1.4 TEF inachukulia hatua hii kama mwendelezo wa ukandamizaji wa uhuru vyombo vya
habari nchini na tunashindwa kuelewa dhamira ya serikali ya awamu ya tano kwa
sekta ya habari nchini. Kinachoonekana ni kutumia kila aina ya sheria iliyopo
kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Kimsingi TEF hatuoni nia (spirit) wa
malezi katika uamuzi wa waziri huyo.
2.0 MSIMAMO WA TEF
2.1

Utaratibu uliotumiwa na Waziri kufikia uamuzi huo, umekuwa wa makosa yaleyale ya


siku zote. Pamoja na kwamba vyombo vya habari hufanya makosa, lakini hata pale
makosa yanapotokea taratibu za kuyashughulikia lazima zizingatie misingi ya utawala
bora, haki na demokrasia.

2.2

Mfumo wa kushughulikia matatizo au kasoro za kitaaluma katika vyombo vya habari


ni kandamizi kwani unamfanya Waziri kuwa na mamlaka ya kutoa adhabu kwa
kuzingatia mtizamo wake, hata kama mtizamo huo unakinzana na misingi ya taaluma.

2.3

Kimsingi uamuzi wa Mh. Nnauye unaonekana hauna nia njema ndani yake kwani
Kifungu cha 28 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) alichotumia
kutoa adhabu hiyo, hakimlazimishi kufungia Vituo vya Radio kama alivyofanya.
Kosa la vituo hivyo kwa mujibu wa Waziri ni Uchochezi, lakini hakuweka bayana
maudhui ya vipindi au habari ambazo zilivifanya vituo hivyo kutiwa hatiani na

2.4

baadaye kufungwa kwake kwa muda usiojulikana. Kwa sababu hiyo si rahisi kwa
waandishi wengine wa habari kujifunza kwa makosa ya wenzao kwa kuwa mchakato
uliotumika kushughulikia suala hilo umebaki kuwa siri ya waziri.
2.5

Tunapinga uamuzi wa serikali kuvifungia vituo hivyo sababu na tunatoa mwito kwa
Waziri Nape kutafakari upya suala hili na kuachana kabisa na dhamira hiyo isiyokuwa
na tija kwa nchi yetu.

NEVILLE MEENA
KATIBU WA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
DAR ES SALAAM, AGOSTI 30,2016

You might also like