You are on page 1of 2

TAARIFA KWA VYOMBO

VYA HABARI

Tanzania inahitaji kuwekeza zaidi kwenye miundombinu


na rasilimali watu ili kuboresha ushindani wake
na kujenga ajira nyingi zaidi zenye tija
DAR ES SALAAM, Tanzania, Mei 20, 2016 Serikali mpya ya Tanzania inatekeleza mabadiliko
makubwa ya kuimarisha usimamizi wa fedha na kuzuia rushwa. Hatua hizi zimeanza kuzaa matunda huku
makusanyo ya mapato ya kodi ya kila mwezi yakivuka lengo katika miezi minne ya kwanza ya utawala
mpya. Taarifa ya 8 ya Benki ya Dunia iliyotolewa hivi karibuni kuhusu Hali ya Uchumi wa Tanzania,
inaeleza kwamba hatua hizi zina uwezekano wa kuwa na ufanisi zaidi na endelevu iwapo hatua za
kushamirisha ili kuboresha mazingira ya jumla ya biashara kwa maendeleo ya sekta binafsi zitachukuliwa.
Wakati ukuaji uchumi wa Tanzania kwa wastani uko juu, bado haujaleta kasi ya kujenga ajira. Umasikini
bado ni mkubwa nchini Tanzania huku takribani Watanzania milioni 12 wakiwa bado chini ya mstari wa
umasikini, wakati wengi wa wale ambao sio masikini wakiwa juu kidogo ya mstari wa umasikini. Wakati
huo huo, takribani Watanzania vijana 800,000 wanaingia katika soko la ajira kila mwaka ambako fursa
zenye tija zingali haba.
Tanzania inahitaji kuongeza uwekezaji kwenye miundombinu na rasilimali watu ili kuzidi kufungulia uwezo
wake wa kukua wakati ikiwezesha sekta binafsi kujenga ajira nyingi Zaidi, anasema Bi. Bella Bird,
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini. Hii sio tu itakuwa na matokeo thabiti kwenye kupunguza
umasikini lakini itaendana na vipaumbele vya serikali mpya na dhamira yake ya kufanikisha malengo ya
nchi ya Dira 2025. Mahitaji ni mengi lakini rasilimali ni chache, hivyo mwelekeo thabiti ambapo vipaumbele
muhimu vya maendeleo vinapata fedha kwa ukamilifu utahitajika ili kufanikisha matokeo tarajiwa.
Kulingana na Taarifa hiyo ya Hali ya Uchumi, yenye jina; Barabara Isiyotumika Sana: Kufungulia Fursa za
Ubia baina ya Sekta za Umma na Binafsi nchini Tanzania ikiwa na changamoto za kifedha kutokana na
kupungua kwa misaada, upatikanaji mdogo wa mapato ya ndani, shinikizo kubwa la matumizi kwa ajili ya
kulipa malimbikizo ya madeni na kuhudumia mikopo, Tanzania itahitaji kutafuta vyanzo mbadala vya
kugharamia mahitaji yake makubwa ya maendeleo. Ripoti hiyo inamulika haja ya kuchunguza Ubia baina
ya Sekta za Umma na Binafsi (PPPs) kama njia ambayo haijatumika sana ya kugharamia maendeleo,
inayoendana na Ajenda 2030 ya Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDGs). Hata hivyo, ripoti hiyo
inasisitiza kwamba miradi inatakiwa ichaguliwe kwa uangalifu, itayarishwe vyema na kutekelezwa vyema.
Tanzania inahitaji kuboresha mazingira yake ya biashara kwa ujumla, ambayo ni pamoja na kupitia
maboresho katika upatikanaji wa fedha na umeme kwa ajili ya maendeleo ya sekta binafsi. anasema
Emmanuel Mungunasi, Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia na mmoja wa watunzi wa ripoti
hiyo. Maendeleo endelevu ya sekta binafsi yatakuwa ndio ufunguo wa upatikanaji wa rasilimali pamoja na
fedha na kujenga fursa nyingi za ajira ambazo ni muhimu sana katika kupunguza umasikini.
Tanzania imekuwa na uzoefu mchanganyiko na ubia baina ya sekta za umma na binafsi, anasema
Jeffrey Delmon, Mtaalamu Mwandamizi wa PPP wa Benki ya Dunia ambaye alikuwa mmoja wa
watunzi wa ripoti hiyo. Kinachotakiwa sasa ni kuzingatia huu uzoefu muhimu tulioupata huko nyuma na
kuunganisha na utendaji bora kutoka chumi kubwa zinazoibukia kama vile Brazil, Chile, Mexico na India na
kujenga programu imara ya PPP ambayo inashughulikia changamoto za maendeleo ya miundombinu ya
nchi na kuzalisha ajira.

Ukizingatia kwamba nyaraka za Tanzania yenyewe za sera zinatambua PPP kama ni chombo muhimu cha
kuvutia uwekezaji mpya, ripoti hiyo badala yake inataka pawepo na mwelekeo mpya thabiti tofauti na
mambo kama kawaida, na inatoa kwa muhtasari vipengele muhimu vya kuzingatiwa na serikali katika
kujenga muundo wa PPP ambao unafaa kwa madhumuni haya. Hivi ni pamoja na kutoa mwongozo wa
kimkakati na uongozi wa programu ya PPP; kuhakikisha matumizi ya mbinu za ushindanishi ili kupata
PPP; kutoa rasilimali za kutosha kuelekea kuainisha na kutayarisha PPP na kukuza njia za wazi katika
kutoa msaada wa Serikali kwa PPPs.
Ukizingatia usimamizi imara wa uchumi ambao umesaidia kuendeleza mtazamo thabiti wa sasa wa
asilimia saba, Toleo la 8 linazitaka mamlaka kuendelea kufuatilia viwango vya deni la nchi kwa namna
makini ili kuhakikisha uendelevu wa kifedha na deni unaoendelea.
Hali ya Uchumi wa Tanzania ni ripoti inayochapishwa na Benki ya Dunia mara mbili kwa mwaka kwa lengo
la kukuza mjadala wa sera unaojenga baina ya wadau na watunga sera na kuchochea mdahalo kwenye
masuala muhimu ya uchumi ndani ya nchi.

Mawasiliano:
Washington: Aby Toure, (202) 473-8302, akonate@worldbank.org
Dar es Salaam: Loy Nabeta, (255) 216-3246, lnabeta@worldbank.org

Kwa habari zaidi kuhusu kazi za Maendeleo za Benki ya Dunia na Taasisi zake katika Afrika, tafadhali
tembelea tovuti: www.worldbank.org/africa

Kwa habari zaidi kuhusu Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Tanzania tembelea:


www.worldbank.org/tanzania/economicupdate
Tutembelee katika Facebook: http://www.facebook.com/worldbankafrica
Tufuatilie katika Twitter Twitter: https://twitter.com/WorldBankAfrica
Tuangalie katika YouTube: http://www.youtube.com/worldbank

You might also like