You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI,


KIKANDA NA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600

20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WASIFU WA


KATIBU MKUU KIONGOZI MTEULE BALOZI MHANDISI JOHN KIJAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,


amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi tarehe 6
Machi 2016, akichukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue.
Kabla ya uteuzi huo, Balozi Mhandisi Kijazi alikuwa mwakilishi wa Tanzania
nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini
New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi
wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi. Vilevile, hadi uteuzi wake, Balozi Kijazi
amekuwa Mkuu wa Mabalozi wa Afrika nchini India ambaye amekuwa mtetezi mkuu
wa wanafunzi wenye asili ya Kiafrika nchini India.
1

Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi
na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006,
baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India.
Kati ya mwaka 1996 hadi 2002, Mhandisi Kijazi alikuwa Mhandisi Mwandamizi
wa Ujenzi wa Barabara ndani ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kupandishwa cheo na kuwa
Mkurugenzi wa Barabara za Mikoa ndani ya Wizara hiyo hiyo.
Balozi Mhandisi Kijazi alipata Shahada ya Sayansi ya Uhandisi wa Umma
mwaka 1982 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na baadaye Shahada ya Uzamili
katika Uhandisi wa Barabara Kuu kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza
mwaka 1992.
Balozi Mhandisi John Kijazi amemuoa Fransiscar Kijazi na pamoja wamejaliwa
watoto watatu, David, Emmanuel na Richard Kijazi.
Balozi Mhandisi John Kijazi ataapishwa leo tarehe 7 Machi 2016 na Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es
salaam.
-MWISHOImetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa,
07 Machi 2016

You might also like