You are on page 1of 1

TANGAZO

NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA


2013/2014

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia
wataalamu wa kada za afya kuwa bado kuna nafasi za kazi katika
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wataalamu wa
kada zilizoorodheshwa hapa chini wanatakiwa kuwasilisha maombi yao ili
waweze kupangiwa vituo vya kazi:
Madaktari Bingwa/ Madaktari Bingwa wa Meno, Madaktari/Madaktari wa
Meno, Mdaktari Wasaidizi/Madaktari Wasaidizi wa Meno,
Matabibu/Matabibu wa Meno, Matabibu Wasaidizi, Mteknolojia wa Meno,
Wafamasia, Watenolojia wa Dawa, Wateknolojia Wasaidizi wa Dawa,
Maafisa Wateknolojia wa Maabara za Afya, Wateknolojia wa Maabara za
Afya, Wateknolojia Wasaidizi wa Maabara za Afya, Maafisa Wauguzi,
Maafisa Wauguzi Wasaidizi, Wauguzi, Maafisa Fiziotherapia,
Wafiziotherapia, wateknolojia wa Macho, Wateknolojia Mionzi, Afisa Afya
Mazingira, Afisa Afya Mazingira Msaidizi, Mhandisi wa Vifaa Tiba na
Mteknolojia wa Vifaa Tiba.
Barua ya maombi iambatanishwe na nakala ya cheti cha kidato cha nne,
cheti cha taaluma na cheti cha kuzaliwa. Waombaji wa kada zenye
Mabaraza ya Taaluma wawasilishe vyeti vya usajili au leseni.
Mwisho wa kuwasilisha maombi tarehe 30/6/2014

You might also like