You are on page 1of 1

TANGAZO KWA WATUMISHI WA KADA ZA AFYA

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA AFYA BAADA YA


KUWA WAMEFAULU MITIHANI YA KUJIENDELEZA- MWAKA 2014.

1. WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STASHAHADA YA JUU
KATIKA VYUO VYA AFYA- SAYANSI SHIRIKISHI WANATAKIWA KURIPOTI
VYUONI TAREHE 4/10/2014 NA MASOMO YATAANZA RASMI IFIKAPO TAREHE
6/10/2014. AIDHA KIPENGERE HIKI CHA TANGAZO PIA KINAWAHUSU
WANAFUNZI WALIOFANYA MITIHANI YA UUGUZI KWA AJILI YA
KUJIENDELEZA KUTOKA ENROLLED NURSE KWA KUJIUNGA NA MAFUNZO
YA STASHAHADA YA UUGUZI.

2. WANAFUNZI WANAOTAKIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA STASHAHADA YA
JUU (AMO, ADO NA VECTOR) PAMOJA NA STASHAHADA YA UUGUZI
(DIPLOMA PROGRAMME FOR INSERVICE) WATATAKIWA KUZINGATIA MUDA
WA KURIPOTI SHULENI KAMA ULIVYOTAJWA HAPO JUU. IWAPO
WATACHELEWA NA KURIPOTI BAADA YA MUDA UTAKAOKUWA UMETAJWA
KATIKA BARUA ZA KUJIUNGA (JOINING INSTRUCTIONS) WATAKUWA
WAMEPOTEZA NAFASI ZAO.

3. WANAFUNZI WOTE WENYE VYETI VYA ASTASHAHADA YA UTABIBU
(CLINICAL ASSISTANT) WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA
STASHAHADA YA UTABIBU (NTA 6 IN CLINICAL MEDICINE) KWA NJIA YA
MASAFA WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA VYUO WALIVYOPANGIWA
IFIKAPO TAREHE 25/10/2014 ILI WAPEWE UTARATIBU NA MWENENDO WA
PROGRAMME YA MASOMO YAO UTAKAVYOKUWA.

4. WANAFUNZI WOTE WENYE VYETI VYA ASTASHAHADA YA MAZINGIRA
(HEALTH ASSISTANT) WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA
STASHAHADA YA MAZINGIRA (DIPLOMA NI ENVIRONMENTAL HEALTH
SCIENCES) WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA VYUO WALIVYOPANGIWA
IFIKAPO TAREHE 25/10/2014 TAYARI KWA KUANZA MASOMO TAREHE
27/10/2014

5. WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA WATATAARIFIWA KWA KUPEWA
BARUA ZA KUJIUNGA (JOINING INSTRUCTIONS) ZITAKAZOTUMWA MOJA
KWA MOJA KUPITIA ANWANI ZAO. HAKUNA MWANAFUNZI
ALIYECHAGULIWA ATAKAYERUHUSIWA KUJA KUCHUKUA BARUA YAKE
WIZARANI-MAKAO MAKUU MOJA KWA MOJA.

You might also like