You are on page 1of 3

22/02/2024

Meneja Mkuu.
Shirika la Umeme,
Zanzibar.

Impitie
Meneja Utawala na Rasilimali Watu,
Shirika la Umeme,
Zanzibar.

KUH: KUWASILISHA RIPOTI YA MAFUNZO YA AFYA NA USALAMA KWA


WAFANYA KAZI WA TAWI LA PEMBA.
Kwa heshma naomba uhusike na mada ya hapo juu.
Idara ya utawala na Rasilimali Watu kupitia Divisheni ya Usalama na Afya Kazini, inaomba
kuwasilisha ripoti ya Mafunzo ya Usalama na Afya sehemu za Kazi kwa Wafanya kazi wa tawi
la Pemba. Mafunzo hayo yalifanyika Tarehr 12/02/2024 kwenye ukumbu wa ZSSF Tibirinzi.
Pamoja na barua hii tunambatanisha na ripoti kamili ya Mafunzo hayo.

Naomba kuwasilisha kwa hatua.

Ahsante.

………………….
(Mwajina P. Juma).
Afisa Uslama na Afya Kazini.
Shirika la Umeme.
Zanzibar.
RIPOTI YA MAFUNZO YA USALAMA NA AFYA SEHEMU ZA KAZI.
UTANGULIZI.
Divisheni ya Usalama na Afya Kazini ilifanya Mafunzo kwa Wafanya Kazi wa tawi la Pemba
ikiwa ni muendelezo wa kazi za kawaida za Divisheni.
Mafunzo hayo yalifanyika siku ya Jumatatu Tarehe 12/02/2024 katika Ukumbi wa ZSSF
tibirinzi.
Jumla ya Wafanya Kazi 32 walishiriki katika mafunzo hayo. Maddumuni ya mafunzo hayo ni
kuongeza uelewa juu ya masuala ya Usalama na Afya Kazini.
Katika mafunzo hayo mada 5 ziliwasilishwa na wakufunzi pia washiriki walipata kujifunza kwa
vitendo juu ya utoaji wa huduma ya kwanza pale wanapopatwa na tatizo la kupatwa na ajali ya
Umeme wanapokuwa kazini.
Miongoni mwa Mada hizo ni:
1. Dhana na Kanuni za Afya na Usalama Kazini
2. Vihatarishi Katika sehemu za Kazi (Workplace Health and Safety Hazard)
3. Hatari na Tathmini za Maswala ya Afya na Usalama sehemu za Kazi
4. Usalama na Afya katika Kazi za Umeme.
NJIA ZILIZOTUMIKA KUFUNDISHIA.
Wakufunzi walitumia njia shirikishi katika kufundisha kwao, hiimikiwa na maana kuwa
washiriki wanafahamu na kuelewa kwa kuchangia juu ya kila mada inayofunsishwa. Vile vile
washiriki waliweza kuchangia, kuliza masuali na kutoa mapendekezo ili kufanikisha mafanikio
ya mafunzo hayo na elimu inafika kwa walengwa kama ilivyotarajiwa.
Mafunzo ya vitendo yalifundishwa ili kuweza kukabiliana na ajali za umeme wakati wafanya
kazi wanapokuwa kazi kwa kutoa huduma ya kwanza mara tu tatizo au ajali inapotokezea.

MALENGO YA MAFUNZO
1. Kuongeza uelewa na ufaham juu ya masuala ya Usalama na Afya sehemu za kazi.
2. Kuelewa na kutambua vihatarishi vinavyowazunguruka wakati wanapokuwa kazini na
jinsi ya kuvitatua.
3. Kufahamu umuhimu wa Usalam na Afya sehemu za kazi ilikuongeza ufanisi wa kazi
katika kuzalisha na kuongeza mapato serikalini.
4. Kupunguza na kuondosha kabisa kesi za ajali zitokananzo na kazi.
5. Kuongeza mashirikiano baina ya wafanya kazi na viongozi katika kusimamia maswala ya
usalama na afya sehemu za Kazi.
MAFANKIO YA MAFUNZO.
1. Washiriki waliweza kuchangia na katika mada zilizowasilishwa.
2. Maswali na mapendekezo mbali mbali yaliweza kulizwa na kupendekezwa na washiriki.
3. Kutengenezwa kwa mashirikiano baina ya idara moja na nyengine.
4. Kupatikana kwa ufumbuzi na changamoto mbali mbali zilizokuwa zinawasumbua
wafanya Kazi,
CHANGAMOTO KWA MAFUNZO.
1. Bajeti ndogo kwa ajili ya mafunzo kunapelekea kutokufia malengo ya kuwafundisha
wafanya kazi wote juu ya maswala ya Usalama na Afya sehemu za Kazi.
2. Kukosekana kwa Ukumbi wa uhakika wa kujitegemea kwa Shirika kwa ajili ya
mafunzo na mikutano.
3. Kukosekana kwa Vifaa kinga kwa mafundi.
MAPENDEKEZO
1. Kuongezewa bajeti ya mafunzo ili elimu iwafike Wafanya Kazi wote.
2. Kununuliwa kwa vifaa kinga kwa mafundi ilikuwalinda na kuwakinga na ajali
wanapokuwa kazini.
3. Kununuliwa kwa Visanduku vya huduma ya kwanza ili kusaidia wa kati wa dharura
ndogo ndogo au ajali.

You might also like