You are on page 1of 2

P.O.

Box 1121 Arusha - Tanzania


+255710329617 | sessangroup@gmail.com | www.sessan.net

NAFASI ZA KAZI ZILIZOWAZI JANUARY 2022


1. MHASIBU (ACCOUNTANT)
1.1. NAFASI
Jumla ya nafasi zilizo wazi na zinazotakiwa kujazwa ni: Nafasi 1

1.2. MAJUKUMU
- Kuandaa Taarifa Mbalimbali za Fedha: Mapato na Matumizi, Faida na Hasara n.k.
- Kufuatilia maendeleo ya mauzo na madeni
- Kushauri kampuni katika maswala ya kifedha
- Majukumu Mengine ya idara atakayopangiwa na Mkurugenzi

1.3. SIFA ZA MUOMBAJI


- Mtanzania Kijana mwenye umri usiozidi Miaka 30
- Awe mwaminifu na muwazi katika kazi
- Ajitume na awe tayari kushirikiana na wengine
- Uzoefu wa Miaka angalau Miaka Miwili
- Elimu ya Stashahada au Shahada katika fani ya Uhasibu

2. AFISA MASOKO (MARKETING)


2.1. NAFASI
Jumla ya nafasi zilizo wazi na zinazotakiwa kujazwa ni: Nafasi 2

2.2. MAJUKUMU
- Kutengeneza Mtandao wa Masoko Mapyaya bidhaa
- Kuelekezea Kamuni katika Mitandao na Vyombo vya Habari
- Kufuatilia Kuhusu Elimu ya Bidhaa kwa Jamii
- Kushauri kampuni katika maswala ya Mauzo na Masoko
- Majukumu Mengine ya idara atakayopangiwa na Mkurugenzi

2.3. SIFA ZA MUOMBAJI


- Mtanzania mwenye umri usiozidi Miaka 40
- Awe mwenyekujituma na Mchapakazi
- Awe mjuaji na muongeaji mzuri sana
- Uzoefu wa Miaka angalau Miaka Mitatu
- Elimu yoyote katika ngazi yoyote Chuo chochote - ilimradi awe na mvuto na ushawishi
3. MHARIRI PICHA NA VIDEO (PHOTO & VIDEO EDITOR)
3.1. NAFASI
Jumla ya nafasi zilizo wazi na zinazotakiwa kujazwa ni: Nafasi 1

3.2. MAJUKUMU
- Kuhariri (Editing) picha na video za vipindi vya TV

3.3. SIFA ZA MUOMBAJI


- Mtanzania Kijana mwenye umri usiozidi Miaka 30
- Mzoefu na Mbunifu wa Kazi
- Elimu ya ya kwanzia Cheti na Kuendelea

4. MTAALAMU WA NYUKI (BEEKEEPING EXPERT)


4.1. NAFASI
Jumla ya nafasi zilizo wazi na zinazotakiwa kujazwa ni: Nafasi 1

4.2. MAJUKUMU
- Kusimamia Miradi ya Ufugaji Nyuki
- Kuandaa Taarifa Mbalimbali za maendeleo ya mradi wa nyuki na kushauri kampuni
- Kufuatilia Maendeleo ya Wateja wa Kampuni wanaohusika na Ufugaji Nyuki na Mazao ya nYUKI
- Kuendesha na Kusimamia Mafunzo ya Ufugaji Nyuki kwa Jamii
- Majukumu Mengine ya idara atakayopangiwa na Mkurugenzi

4.3. SIFA ZA MUOMBAJI


- Mtanzania Kijana mwenye umri usiozidi Miaka 30
- Awe Mtaalamu Mfugaji Mzoefu
- Awe tayari kufanya kazi za shambani
- Elimu ya Stashahada au Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki

5. MTAALAMU WA BIDHAA ZA VIPODOZI (COSMETICTS EXPERT)


5.1. NAFASI
Jumla ya nafasi zilizo wazi na zinazotakiwa kujazwa ni: Nafasi 1

5.2. MAJUKUMU
- Kutengeneza bidhaa mbalimbali za afya ya mwili na vipodozi
- Kusimamia Ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni
- Kushauri kampuni katika maswala ya bidhaa mpya na mfumo wa uzalishaji
- Majukumu Mengine ya idara atakayopangiwa na Mkurugenzi

5.3. SIFA ZA MUOMBAJI


- Mtanzania mwenye umri usiozidi Miaka 35
- Awe muungwana na anayejali watu.
- Uzoefu wa kutengeneza bidhaa mbalimbali za afya na urembo
- Elimu ya Cheti na Kuendelea

ZINGATIA: Taarifa zote za Utumaji wa Maombi ya kazi zitatolewa kupitia namba ya kampuni:
Jina: SESSAN ENTERPRISES
Simu: 0742377186

You might also like