You are on page 1of 26

Biashara Yake, Maisha Yake: Usimamizi wa

Biashara na Ujuzi wa Kusoma na Kuandika wa


Kidijitali kwa Wanawake Wajasiriamali Wadogo
Mwongozo wa Mtumiaji

TOLEO LA KISWAHILI
Novemba 2022

Ripoti hii imeweza kufanikishwa kwa ushirikiano wa ukarimu na watu wa Marekani kupitia
Uwakala wa Marekani wa Maendeleo ya Kimataifa (USAID). Muongozo huu ulitolewa chini ya
Mradi wa Frontia za Kidijitali za DAI (Cooperative Agreement AID-OAA-A-17-00033) kutokana
na ombi la USAID wakishirikiana na Mastercard.

1
Jedwali la yaliyomo

I. Utangulizi kwenye mafunzo 3

A. Maelezo ya Mradi 3

B. Nani anafunzwa Mafunzo Haya? 3

C. Malengo ya Mafunzo Haya ni Yapi? 4

D. Mwongozo wa Mtumiaji Ni Nini? 4

II. Ni Yapi Yaliyo Shughulikiwa Kwenye Mafunzo Haya? 5

A. Mfumo wa Taaswira ya Moduli 6

III. Vidokezo vya Waalimu 7

A. Utengezaji wa nafasi za kukidhi mahaitaji ya Wateja 7

B. Jumla ya Vidokezo vya Ufanikishaji 9

C. Vidokezo vya Ufanikishaji wa Mafunzo ya Kina dhidi ya Yale ya Juu Juu 10

IV. Taaswira Kamili ya Moduli Nane 11

A. Mwelekeo 11

B. Ujuzi wa Kusoma na Kuandika Kifedha 12

C. Kufikia na Kustahili Kupata Mkopo 14

D. Ijue Simu Yako 16

E. Malipo Ya Kidijitali 18

F. Usimamizi wa Kifedha 20

G. Usimamizi wa Orodha ya Mali 22

H. Utangazaji wa Biashara 23

2
I. Utangulizi kwenye mafunzo

A. Maelezo ya Mradi

Kulingana na ripoti ya The World Economic Forum’s 2022 Gender Gap, Itachukua miaka 151 ili kuziba
pengo la ushirikiano wa uchumi na nafasi kwa wanawake.1 Zaidi ya hapo, ulimwenguni, ni biashara moja tu
kati ya tatu inayomilikiwa na mwanamke.2 Ni wazi kwamba juhudi zaidi zinahitajika kuwawezesha
wanawake kushiriki kwenye kukuza uchumi, kuwasaidia kumiliki biashara, ndogo ndogo na za wastani
(MSMEs) kama njia ya kuwawezesha kiuchumi, na kuwapa ujuzi unaohitajika kuendesha biashara zenye
faida.

Mwaka wa 2020, USAID walishirikiana na Mastercard’s Center kwenye Ukuaji wa pamoja na washirika
wenyeji ili kutekeleza mradi wa “Project Kirana for Women” kwa wanawake wamiliki na wanaoendesha
biashara ndogo ndogo katika miji miwili nchini India. Mafunzo haya yamekusudiwa kujenga uwezo wa
wanawake wajasiriamali kumiliki na kusimamia kuendesha biashara ndogo ndogo (Karina), na kupata
nafasi ya kutumia huduma za malipo ya kidijitali na fedha, na kuboresha uwakala wao kwenye utunzaji wa
nyumba na kufanya maamuzi ya kibiashara.

USAID na Digital Frontiers waliamuru Strategic Impact Advisors (SIA) kuchukua programu ya kifaa cha
mafunzo kwa wanawake ya MSMEs kwa matumizi ya kidunia. Kifaa hiki cha mafunzo ya, “ Biashara Yake,
Maisha Yake ” kinahusisha moduli nane za mafunzo. Moduli zote nane zinapatikana katika lugha ya
Kizungu, Kifaransa, Kiswahili na Kihispania na ni bidhaa za soko la ki-agnostiki. Kifaa cha mafunzo ni
kipimo na kimetengenezwa kukidhi mahitaji ya mteja, ili kutoa nafasi ya kufanyiwa marekebisho ya
maudhui na kufikia malengo ya shirika lolote lile ama kikundi cha wanafunzi. Utengenezaji wa maudhui
katika moduli hizi unaweza kuongeza uelewa wa maelezo kwa wanafunzi na kujenga kuweza kutumia ujuzi
waliojifunza kwenye biashara zao.

B. Nani anafunzwa Mafunzo Haya?

Hizi moduli nane zilizojumuishwa kwenye hiki kifurushi, zimekusudiwa kutolewa na shirika kwa kikundi
cha wanawake wajasiriamali wadogo. Kifurushi hiki cha mafunzo kinaweza kutengenezwa kukidhi mahitaji
ya mteja na mashirika mbalimbali na watoa huduma ili kuwasaidia kufikia malengo yao. Baadhi ya mifano
ya mashirika mbalimbali na watoa huduma ambao wanaweza kutumia kifurushi hiki cha mafunzo ni
pamoja na:

1
https://www3.weforum.org/docs/WEF_GGGR_2022.pdf
2
https://blogs.worldbank.org/opendata/women-entrepreneurs-needed-stat

3
● Watoaji huduma za kifedha, kama vile benki, Waendeshaji wa mitandao ya simu, na taasisi ndogo
za fedha, zinazotazamia kuleta wateja wapya, kufunza wateja jinsi ya kutumia bidhaa zao na
huduma, na kuboresha kudumisha matumizi ya bidhaa.
● Mashirika yasiyo ya kibiashara ya ndani na Mashirika ya kimataifa yasiyokuwa ya kiserikali
yanayotaka kusimamia ki-binafsi au shughuli za mbali za kusaidia wanawake-wamiliki MSMEs na
umiliki MSME kama njia ya kuwezesha uchumi.
● Mawakala wa ndani na kitaifa wanaoendeleza maendeleo ya biashara ndogo ndogo, wenye uwezo
wa kupata fedha, na waliomo kwenye uchumi wa kidijitali.

Mafunzo haya yamelenga kufundishwa kwa wanawake wajasiriamali wadogo ambao wanafanya kazi au
kumiliki maduka yao ambayo kwa kweli yanauza bidhaa ambazo zinanunuliwa kwa haraka na watumiaji
(FMCG), lakini yanaweza kutengenezwa yakawa maduka ya kuuza bidhaa zingine. Mafunzo haya yanaweza
kufaidi wanawake wanaojihusisha katika biashara kwenye majukumu mbalimbali, yakiwemo:

1. Mwanamke anayesaidia kwenye majukumu ya


kuendesha maduka, na anahitaji ujuzi wa
kibiashara ili kushiriki kikamilifu kuendesha
biashara;
2. Mwanamke anayemiliki maduka madogo ama
yasiyo rasmi ama vioski, na anahitaji kusaidiwa
kupata haki za kiserikali na ujuzi muhimu wa
kusimamia biashara;
3. Wanawake ambao ni wamiliki wa maduka na
wanaendesha biashara kwa kiwango fulani, na
wanawateja wakutosha.

C. Malengo ya Mafunzo Haya ni Yapi?

Kifurushi cha “Biashara Yake, Maisha Yake” kina malengo matatu makuu:
1. Kusaidia wanafunzi kupata ujuzi wa kusimamia biashara wanaoweza kuutumia kupata wateja na
kipato.
2. ​Kuwafunza wanafunzi jinsi ya kutumia huduma za kifedha na simu zao kwenye kuendesha biashara
na shughuli za biashara.
3. Kujenga motisha ya ujasiriamali kwa wanafunzi, uwezo, na ujuzi kupitia mafunzo kuhusu biashara
na ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali.

D. Mwongozo wa Mtumiaji Ni Nini?

4
Huu “Mwongozo wa Mtumiaji” unatoa taaswira ya maudhui yaliyomo kwenye kifurushi hiki cha mafunzo,
utangulizi wa mfumo wa moduli, hatua na mapendekezo ya utengenezaji wa maudhui ya moduli, na
vidokezo vya kuendeleza na kuendesha vikao vya mafunzo. Walimu wanahitajika kupitia mwongozo huu
kabla ya kuanza vikao vya mafunzo ili kuhakikisha kuwa vikao vinahusiana na maudhui na vina maana kwa
wasikilizaji.

II. Ni Yapi Yaliyo Shughulikiwa Kwenye Mafunzo Haya?

Mwelekeo

Ujuzi wa Kusoma na Kuandika Kifedha

Kufikia na Kustahili Kupata Mkopo

Ijue Simu Yako

Malipo Ya Kidijitali

Usimamizi wa Kifedha

Usimamizi wa Orodha ya Mali

5
Utangazaji wa Biashara

Taaswira ya kila moduli inaweza kupatikana kuanzia ukurasa 10.

A. Mfumo wa Taaswira ya Moduli

Kifurushi cha “Biashara Yake, Maisha Yake” kinajumuisha moduli nane zinazopatikana kwenye mfumo wa
PowerPoint. Urefu wa deki za slaidi unatofautiana kwa kila moduli, na ni kiwango cha kuanzia slaidi 35
hadi 53. Kila moduli imegawanywa kwa sehemu nyingi, ikiwa na vigawanyo vya vipande vikiashiria mwanzo
wa mada mpya. Waalimu wanaweza kutumia moduli zote nane kwa pamoja ama moduli moja kabisa.
Waalimu wanaweza pia kuchukua na kuchagua baadhi ya mada kutoka kwenye moduli kwa kutumia
vigawanyo vya sehemu, au kuondoa kabisa sehemu kutoka kwenye moduli. Moduli hizo pia
zimetengenezwa zinaweza kujisimamia zenyewe, na zinaweza kutumiwa kwa mfumo wowote ule.
Tafadhali hakikisha unaongeza jina la shirika lako kwenye taarifa ya ilani ya kujitoa hatiani (kanusho) kwa
jalada la slaidi ya kila PowerPoint iliyotumika wakati wa mafunzo.

Kila moduli inatumia mchanganyiko wa wahusika wanne kutoa masomo ambayo yanawakilisha maeneo
matatu makuu:
● Imani, akiwakilisha Jangwa la Sahara la Afrika
● Ratana, akiwakilisha Asia ya Kusini Mashariki
● Sofía and Mateo, wakiwakilisha Marekani ya Kusini

Wahusika hawa wametengenezwa kutoa maelezo


anuwai ya kijiografia kwenye vifaa vya kufundishia. Pia
tumejumuisha wapenzi waliooana, Sofía na Mateo, ili
kutoa nafasi ya majadiliano ya majukumu ya kijinsia
kwenye utunzaji wa nyumba na utoaji wa maamuzi ya
kibiashara. Angalia sehemu ya taaswira ya moduli
kuanzia ukurasa 11 kwa vidokezo vya jinsi ya
kutengeneza wahusika na mada zao kwenye mafunzo ili
kuakisi baadhi ya masoko.

Vifurushi hivi vya mafunzo vinatumia aina tano kuu za shughuli ili kujumuisha mitindo mbalimbali ya
kufundishia na ya kuigwa, na kubainisha njia za kutoa maelezo. Kila moduli inatumia shughuli mbalimbali
ama zote zilizoorodheshwa hapa chini:

6
1. Masomo ya kuelezeka: Wingi wa moduli unaandikwa kama masomo ya kuelezeka, pale ambapo
wahusika wanaeleza maana, mawazo na mbinu. Masomo katika kila moduli yamegawanywa katika sehemu
mbalimbali ili kusaidia kupangilia maudhui.

2. Maswali ya majadiliano: Maswali ya majadiliano yamejumuishwa kwenye moduli zote ili kuwahimiza
wanafunzi kuakisi juu ya vifaa na kufikiria jinsi ya kutumia masomo kwenye maduka yao.

3. Matukio ya Wahusika: Baadhi ya moduli zina matukio yanayohusisha wahusika wawili


wanaposhirikiana kuelezea tatizo kwenye duka lao. Matukio haya yanatumika kama hadithi fupi, na
yanaweza kutumika pia kutengeneza maswali ya mjadala ya wahusika kuchagua.

4. Kufanya Mazoezi: Baadhi ya moduli zinajumuisha kutoa nafasi ya kufanya mazoezi ya mambo
waliyojifunza katika kipindi cha mafunzo. Nafasi hizi ni pamoja na kufanya mazoezi ya uandishi na kidijitali,
yakiangazia kuanzia jinsi kuweka shughuli za siku kwenye kitabu mpaka jinsi ya kusajili pochi ya simu ama
akaunti ya mobile money.

5. Nyenzo za Nje: Moduli zote, kuna viungio vya nyenzo za ziada za kujifunzia kutoka sehemu
mbalimbali za nje ili kujazia kifurushi cha mafunzo. Nyenzo hizi zinajumuisha masomo ya kutumia sauti,
video na viti vya zana.

III.Vidokezo vya Waalimu

A. Utengezaji wa nafasi za kukidhi mahaitaji ya Wateja

Moduli nane zilizojumuishwa kwenye mafunzo haya ni chanzo-wazi, ili kutoa nafasi ya marekebisho na
utengenezaji wa kukimu maudhui ili kufikia malengo ya shirika lolote lile ama kikundi cha wanafunzi.
Utengenezaji wa kukimu maudhui kwenye moduli hizi unaweza kuongeza ubora wa maelezo kwa
wanafunzi na kuweza kutumia ujuzi waliojifunza kwenye biashara zao. Kwa mfano, Maudhui yanaweza
kuboreshwa kuhakikisha ubora wa bidhaa kifedha au kidijitali na kutoa huduma kwenye soko., au
kuzingatia uwezo wa kifedha wa wanafunzi kidijitali.

Kila moduli inajumuisha “Karatasi ya vidokezo” na mwongozo kwenye maeneo ambayo mashirika yanafaa
kuzingatia utengenezaji wa kukidhi mahitaji.Vidokezo hivi pia vimejumuishwa kwenye sehemu ya taaswira
ya moduli ya Mwongozo huu wa Mtumiaji, kuanzia ukurasa 11. Mfano wa maeneo ya utengenezaji wa
kukidhi mahitaji kwenye moduli yanajumuisha:

7
● Sarafu
● Istilahi maalum za soko (kama vile pochi ya simu
na akaunti ya mobile money)
● Picha za wahusika, mada, na matukio
● Maswali ya majadiliano
● Kufanya mazoezi
● Mifano hai ya kilimwengu ya bidhaa na huduma

Jedwali linalofwata linaonyesha orodha ya nyenzo zilizojumuishwa kwenye kifurushi hiki cha mafunzo
ambacho kinaweza kusaidia utengenezaji wa kukidhi mahitaji na kurahisisha vikao.

JINA LA NYENZO MAELZO YA NYENZO KIUNGIO CHA


NYENZO

Moduli za Usimamizi wa Moduli zote nane zinapatikana katika lugha nne. - Moduli ya Kizungu
Biashara na Ujuzi wa - Moduli ya Kihispania
Kusoma na Kuandika wa - Moduli ya Kifaransa
Kidijitali kwa Wanawake - Moduli ya Kiswahili
Wajasiriamali Wadogo
(Biashara Yake, Maisha
Yake)

Mwongozo wa Utumiaji Mwongozo wa Mtumiaji unapatikana katika - Mwongozo wa Mtumiaji


wa Usimamizi wa lugha nne. wa Kizungu
Biashara na Ujuzi wa - Mwongozo wa Mtumiaji
Kusoma na Kuandika wa Kihispania
Kidijitali kwa Wanawake - Mwongozo wa Mtumiaji
Wajasiriamali Wadogo wa Kifaransa
(Biashara Yake, Maisha - Mwongozo wa Mtumiaji
Yake) wa Kiswahili

Ubunifu wa Maktaba ya Ubunifu wa Maktaba ya mali inatoa mkusanyiko Ubunifu wa Maktaba ya


Mali wa PNGs wa wahusika wanne katika matabaka Mali
mbalimbali, na vile vile aina tofauti za maduka.
Maktaba hiyo pia inajumuisha picha na ikoni,
kama vile michoro ya uzungumzaji, na maumbo.

“Hey Sister! Show Me “Hey Sister!” ni kampeni ya sauti ya kidijitali ya “Hey Sister! Show Me
the Mobile Money!” kusoma na kuandika ya kifedha kwa wanawake, the Mobile Money!”

8
ulioundwa na SIA kwa kufadhiliwa na USAID.
“Hey Sister!” iliundwa kwa ajili ya masoko ya
Afrika na inapatikana katika lugha 16.

Kiti-zana ya Ujuzi wa GSMA MISTT ni mkusanyiko wa nyenzo Bonyeza hapa, ili kupata
Mafunzo ya Tovuti ya zinazopatikana zinazofunza ujuzi muhimu mtalaa wote katika lugha
Simu (MISTT) cha unaohitajika kupata na kutumia tovuti ya simu. tofauti, Mwongozo wa
GSMA Kizi-zana inahusisha masomo mafupi katika waalimu na video.
mfumo wa PDF na video, na inapatikana katika
lugha 10.

Kiti-Zana cha Ujuzi wa Kiti-Zana cha Ujuzi wa Simu cha GSMA Kiti-zana cha Ujuzi wa
Simu cha GSMA kiliundwa na programu ya Muungano wa Simu
Wanawake ya GSMA ili kuboresha jinsi
ambavyo wanawake wa Papua wa New Guinea
wanavyotumia simu zao. Kiti-Zana hicho
kinapatikana katika lugha ya Kizungu.

Taasisi ya Mozilla ya Mradi wa Uangalizi wa Ujuzi wa Kidijitali ulinuia - Mfumo wa ekolijia wa


Uangalizi wa Ujuzi wa kuchunguza athari za ujuzi wa kidijitali kwenye simu za kisasa
Kidijitali matumizi ya huduma za fedha za kidijitali (DFS) - Kila kitu kinachohusu
nchini Kenya. Mtalaa huo wa Kizungu wenye akaunti
sehemu nne unapatikana kwa umma na - Kipi kinawezekana
unajumuisha mbinu mbalimbali za kufundishia. Mtandaoni?
- Kusuluhisha matatizo
kwa kutumia Simu yako

B. Jumla ya Vidokezo vya Ufanikishaji

Orodha ifuatayo inatoa vidokezo vitano vya kuzingatia wakati unapanga na kuendesha vikao vya mafunzo
ukitumia moduli ya maudhui. Kuanzia ukurasa 11, tunatoa orodha ya nyenzo za kila moduli ambazo
waalimu wanaweza kuhitaji kutumia wakati wa kufundishia.

1. Wajue wasikilizaji. Kabla ya kuwezesha mafunzo, hakikisha una uelewa wa jumla wa mahitaji
ya kufundishia na matakwa ya wanafunzi. Zingatia ikiwa kuna mbinu maalum za kufundishia
wanazopenda, mawazo ambayo tayari wana ufahamu nayo, na mada wanazohitaji kufanyia mazoezi

2. Tengeneza Maudhui kukidhi mahitaji. Ili kuhakikisha kwamba moduli zina ubora unaofaa
kwa wanafunzi na masoko yao, zingatia utengenezaji wa maudhui ya kukidhi mahitaji. Kila moduli

9
ina “karatasi ya vidokezo” vilivyotengenezwa kukidhi mahitaji ambavyo vinajumuisha
mapendekezo na mwongozo wa jinsi ya kutengeneza na kuboresha maudhui ya kukidhi mahitaji.

3. Endeleza majadiliano ya vikundi na maswali. Kuwafanya wanafunzi kujadili kwa pamoja


kunaweza kuwasaidia kuelewa maelezo na maudhui waliyojifunza. Zaidi ya hapo, kuuliza vikundi
mara kwa mara ikiwa wana maswali yoyote kutasaidia kuondoa mashaka na wasiwasi kuhusu vifaa
vya mafunzo, na vile vile kugundua sehemu ambazo zinahitaji mazoezi na mwongozo zaidi.

4. Kuwa mwepesi na rekebisha unapohitajika. Ikiwa wanafunzi wanaona vikao vya mafunzo
kuwa vya muda mrefu sana ama baadhi ya mada kuwa ngumu, zingatia kufanya mabadiliko ili
kukidhi mahitaji yao, imma iwe ni kupunguza muda wa vikao ama kutumia muda zaidi kujadili
baadhi ya mada.

5. Himiza mazoezi na vitendo. Tumia muda kwenye kufanya mazoezi na shughuli zilizopo
kwenye moduli. Waite washiriki watumie simu zao kufanyia mazoezi kwa kutumia vipengele
vilivyojadiliwa wakati wa mafunzo, hususan wakati wa vikao vilivyokuwa vinalenga ukuzaji wa ujuzi
wa kidijitali. Kufanyia mawazo mazoezi kunasaidia kuwahimiza wanafunzi kutumia maudhui ya
moduli katika maisha yao wenyewe na biashara.

C. Vidokezo vya Ufanikishaji wa Mafunzo ya Kina dhidi ya Yale ya Juu Juu

Kulingana na urefu wa kila kikao cha mafunzo na muda waotumia wanafunzi kujifunza maudhui, zingatia
uwezeshaji wa mafunzo ya kina au yale ya juu juu.

Mafunzo ya kina: Mafunzo ya kina ni bora sana kwa wanafunzi wanaoshiriki vikao vya mafunzo yenye
dakika 90 au zaidi.Vikao hivyo vinaweza kushughulikia maudhui moduli zote au nyingi, tumia muda wa
kutosha kwa kufanya mazoezi na maswali ya mjadala, na tanua kwenye nyezo za ziada za kufunzia
zilizojumuishwa katika moduli.

Zingatia vidokezo vifuatavyo wakati unatengeneza vikao vya amafunzo ya kina:


● Waweke wanafunzi katika vikundi kulingana na viwango vyao ujuzi wao.
● Wagawanye wanafunzi katika vikundi vidogo vidogo wakati wa kufanya mazoezi na vikao vya
mjadala.
● Tenga muda wa kuwaelekeza wanafunzi kwenye nyenzo za ziada za kujifunzia.
● Waambie wanafunzi wafupishe na wazingatie yale ambayo wamejifunza baada ya vikao malizika.

10
Mafunzo ya juu juu: Mafunzo ya juu juu ni bora kwa wanafunzi na waalimu ambao wana muda mchache
wa kutumia kwa kila moduli. Waalimu wanaofanikisha vipindi hivi wanaweza kuchukua na kuchagua
baadhi ya mada ambazo katika kila moduli ni muhimu kulingana na mahitaji ya kufundishia na wanafunzi.
Vile vigawanyo vya sehemu vinavyogawanya mada katika kila moduli vinaweza kusaidia waalimu kuchagua
mada za kujumuisha kwenye mafunzo ya juu juu.

Zingatia vidokezo vifuatavyo wakati unatengeneza vipindi vya mafunzo ya juu juu:
● Sisitiza mada za moduli moja ama mbili wakati wa kikao ambazo wanafunzi wanahitaji kufanya
mazoezi.
● Waweke wanafunzi katika kikundi kimoja kikubwa wakati wa ufanikishaji.
● Wahimize wanafunzi kutanua wenyewe kwenye vifaa vya ziada vya kujifunzia.

IV.Taaswira Kamili ya Moduli Nane

A. Mwelekeo

Moduli ya mwelekeo inatumika kama utangulizi kwenye kifurushi cha mafunzo na kinashughulikia
malengo, matokeo yaliyokusudiwa, na wahusika wenye mafunzo. Moduli hii pia inatoa nafasi kwa
wanafunzi kufahamiana, kujua uwezo na udhaifu wa biashara zao, tathmini majukumu yao kwenye biashara
zao, na kupanga mustakabali wa maduka yao. Mwisho kabisa, hii moduli inazungumzia hoja ya urasmi wa
biashara na zisizo rasmi, kwa kujadiliana faida za biashara rasmi, mifano ya usaidizi unaotolewa kwa
biashara rasmi, na hatua zinazohitajika kusajili biashara.

JEDWALI LA YALIYOMO MALENGO

● Sehemu ya 1: Utangulizi wa mafunzo na ● Kujifunza kuhusu masomo yanayopatikana


wahusika kwenye mafunzo haya.
● Sehemu ya 2: Kuwa na Maono ● Kuelewa hali halisi iliyopo ya biashara
● Sehemu ya 3: Kuelewa biashara rasmi na yako.
zisizo rasmi ● Kuwa na maono ya biashara yako
● Sehemu ya 4: Kuendesha tathmini ya ● Tambua elimu na ujuzi unaohitaji kukuza
mapungufu kwenye duka lako biashara yako.

SHUGHULI NYENZO ZILIZOPENDEKEZWA KWA


UFANIKISHAJI

11
● Kutaka kujua wahusika wa mafunzo na ● Kipakatalishi au Ngamizi ili kufikia moduli
kikundi chako cha mafunzo. ● Projekta ili kufanya maudhui ya moduli
● Kutathmini hali halisi ya biashara yako. kuonekana kwa ukubwa
● Kuchanganua maeneo yanayohitaji ● Kalamu na karatasi
kuboreshwa. ● Matini kwenye mchakato wa kusajili
biashara (Kwa mfano, URL/Afisi/Maombi
● Fomu ya maombi/maelezo ya jinsi ya
kutuma maombi ya programu za kifedha
kwa wanawake wanaomiliki biashara

Utengezaji wa Vidokezo vya kukidhi mahitaji

● Mada: Hii moduli imegawanywa katika mada mbalimbali kama ilivyoelezwa kwenye jedwali la
yaliyomo. Unaweza kufuta mada ambazo hazihusiani na wewe pamoja na kikundi chako. Unaweza
pia kufuta slaidi yoyote kwenye moduli ambayo hutumii wewe au kikundi chako. Zaidi ya hapo,
matini yote katika hii moduli yanaweza kuondolewa moja kwa moja.
● Wahusika: Hii moduli inatumia mchanganyiko wa wahusika kutoka maeneo tofauti. Unaweza
kubadilisha mhusika yeyote kwa kutumia faili za picha za wahusika kutoka kwenye maktaba ya
ubunifu ya mali.
● Utaratibu wa Maudhui: Slaidi ya 6 na 37 inatoa taaswira ya moduli saba zilizobakia kwenye
mafunzo haya. Unaweza kuchagua moduli ambazo zinahusiana sana na wasikilizaji wako, na
kubadilisha utaratibu wa vile zinavyowasilishwa.
● Maswali ya Majadiliano: Slaidi ya 9, 21, 23, 24, 25, 26, 28, 35 na 36 zina maswali ya
majadiliano. Unaweza kuongeza, ondoa au kubadilisha maswali kama inavyohitajika.
● Matukio ya Mhusika: Slaidi ya 10 – 20 zinamfuatalia mhusika Imani, wakati anajitambulisha
mwenyewe na duka lake. Unaweza kuondoa mhusika na kubadilisha tukio ili kuakisi kikamilifu
kikundi chako pale inapohitajika.
● Usajili na Leseni: Slaidi ya 31 inatoa maelezo kuhusu biashara na leseni za biashara. Unaweza
kubadilisha stakabadhi zinazohitajika kwenye leseni hizi kulingana na soko lako lillivyo. Unaweza
pia kubadilisha aina ya leseni ili kuakisi kikamilifu kikundi chako.
● Ruzuku za Kifedha: Slaidi ya 33 inaorodhesha mifano ya ruzuku za kifedha zinazopatikana kwa
wanawake. Unaweza kuongeza kuongeza mifano mingine inayofaa kulingana na muktadha wako,
na kufuta mifano kama ikihitajika.

B. Ujuzi wa Kusoma na Kuandika Kifedha

12
Moduli ya ufahamu wa kifedha wa kusoma na kuandika unawajenga wanafunzi kuwa na ujuzi na elimu
inayohitajika kuwa na ujasiri wa kufikia na kutumia bidhaa na huduma za kifedha kwenye maisha yao
binafsi na biashara. Moduli hii pia inaruhusu wanafunzi kujua ni bidhaa au huduma gani inayoweza kuwafaa
kwa kutoa tathmini linganishi ya bidhaa mbalimbali, vile vile kuwafunza wanafunzi namna ya kupima
gharama na faida za kubadili baadhi ya bidhaa.

JEDWALI LA YALIYOMO MALENGO

● Sehemu ya 1: Ufunguaji wa Akaunti ya ● Elewa jinsi ya kuweka akiba, kutumia, au


Kifedha kuongeza pesa zako.
● Sehemu ya 2: Akiba
● Sehemu ya 3: Kufanya Bajeti
● Sehemu ya 4: Uwekezaji
● Sehemu ya 5: Bima
● Sehemu ya 6: Mkopo

SHUGHULI NYENZO ZILIZOPENDEKEZWA KWA


UFANIKISHAJI

● Kulinganisha na kubainisha aina tofauti za ● Kipakatalishi na ngamizi ili kufikia moduli


akaunti za kifedha na watoaji huduma. ● Projekta ili kufanya maudhui ya moduli
● Kutengeneza bajeti yako mwenyewe. kuonekana kwa ukubwa
● Kuangalia nafasi za uwekezaji wa biashara ● Simu moja kwa kila mfanikishaji
yako. ● Programu zilizopakuliwa (kama vile pochi
● Kutathmini gharama na faida za bima. ya simu au programu za benki)
● Kujifunza kuhusu majukumu ya mkopo ● Kubajetia ruwaza (karatasi au kidijitali)
katika biashara. ● Kalamu na penseli

NYENZO ZA ZIADA

Masomo ya kusikiliza Sauti: “Hey Sister! Show Me the Mobile Money!”


● Somo la 15: Niweke akiba ya shilingi ngapi?
● Somo la 16: Niweke akiba wapi?
● Somo la 17: Nahitajika ninunue bima?
● Somo la 18: Ni vipi nyumba yangu inaweza kusimamia fedha zetu vyema?
Kubajetia Ruwaza: Google Sheets

Utengezaji wa Vidokezo vya kukidhi mahitaji

13
● Mada: Hii moduli imegawanywa katika mada mbalimbali kama ilivyoelezwa kwenye jedwali la
yaliyomo. Unaweza kufuta mada ambazo hazihusiani na wewe pamoja na kikundi chako. Unaweza
pia kufuta slaidi yoyote kwenye moduli ambayo hutumii wewe au kikundi chako. Zaidi ya hapo,
matini yote katika hii moduli yanaweza kuondolewa moja kwa moja.
● Wahusika: Hii moduli inatumia mchanganyiko wa wahusika kutoka maeneo tofauti. Unaweza
kubadilisha mhusika yeyote kwa kutumia faili za picha za wahusika kutoka kwenye maktaba ya
ubunifu ya mali.
● Maswali ya Majadiliano: Slaidi ya 4, 9, 24, 27, 34 na 44 zina maswali ya majadiliano. Unaweza
kuongeza, ondoa au kubadilisha maswali kama inavyohitajika.
● Istilahi ya Pochi ya Simu: Istilahi “Pochi ya Simu” inatumiwa kwenye slaidi ya 4, 6, na 17.
Unaweza kubadilisha istilahi hizi kwa istilahi ambazo zinaeleweka vizuri kwako na wasikilizaji –
kama vile akaunti ya mobile money, pochi ya kidijitali, n.k.
● Ufunguaji wa Akaunti: Slaidi ya 7 inaelezea hatua za jumla za ufunguaji wa akaunti. Unaweza
kuboresha haya maagizo kulingana na mtoaji huduma au kwa bidhaa maalum ya chaguo lako.
● Aina za Akaunti Rasmi za Akiba: Slaidi ya 18 inaorodhesha mfano wa akaunti za akiba.
Unaweza kufuta au kuongeza mifano ikihitajika.
● Akiba Rasmi na Zisizo Rasmi: Slaidi ya 20 inalinganisha na kubainisha akiba rasmi na zisizo
rasmi. Unaweza kuongeza au hoja kama ikihitajika.
● Zoezi la kufanya Bajeti: Slaidi ya 25 – 26 inatoa mfano wa kufanyia bajeti mhusika. Unaweza
kubadilisha tukio, mhusika, na viwango vya kufanya bajeti.
● Bima ya Jumla: Slaidi ya 37 inaelezea aina mbili za bima ya jumla: Bima ya duka na afya.
Unaweza kuboresha au kubadilisha mifano hii kulingana na hali ya soko lilivyo.

C. Kufikia na Kustahili Kupata Mkopo

Moduli ya anayestahili na kupata mkopo inaelezea njia tofauti za kupata mkopo, jinsi ambavyo uwezo wa
kupata mkopo unatathminiwa, sehemu za kupata mkopo, na vidokezo na ujanja wa kumudu mkopo.
Moduli inazingatia kuchagua mkopo kitamaduni na kidijitali, vile vile kitamaduni na njia mbadala za uwezo
wa kupata mkopo.

JEDWALI LA YALIYOMO MALENGO

● Sehemu ya 1: Aina za Mkopo ● Elewa aina za mkopo rasmi na vyanzo.


● Sehemu ya 2: Utathmini wa anayestahili ● Jifunze kuhusu utaratibu wa kutathmini
mkopo anayestahili kupata mkopo.

14
● Sehemu ya 3: Ni wapi na jinsi ya kupata ● Fahamu umuhimu kutengeneza mkopo na
mkopo malipo ya mkopo kwa wakati.
● Sehemu ya 4: Kusimamia mkopo

SHUGHULI NYENZO ZILIZOPENDEKEZWA KWA


UFANIKISHAJI

● Kulinganisha na kubainisha aina tofauti za ● Kipakatalishi na ngamizi ili kufikia moduli


mkopo. ● Projekta ili kufanya maudhui ya moduli
● Kuweka mkakati jinsi ya kusimamia malipo kuonekana kwa ukubwa
ya mkopo. ● Simu moja kwa kila mfanikishaji
● Programu za mkopo za kidijitali
zilizopakuliwa
● Vikokotozi na karatasi (za mifano ya
wiwango vya riba)
● Kalamu na penseli

NYENZO ZA ZIADA

Masomo ya kusikiliza Sauti: “Hey Sister! Show Me the Mobile Money!”


● Somo la 13: Ni kitu gani cha kuzingatia nikichukua mkopo?
● Somo la 14: Ni tahmini vipi kuchagua mkopo wa kidijitali?

Utengezaji wa Vidokezo vya kukidhi mahitaji

● Mada: Hii moduli imegawanywa katika mada mbalimbali kama ilivyoelezwa kwenye jedwali la
yaliyomo. Unaweza kufuta mada ambazo hazihusiani na wewe pamoja na kikundi chako. Unaweza
pia kufuta slaidi yoyote kwenye moduli ambayo hutumii wewe au kikundi chako. Zaidi ya hapo,
matini yote katika hii moduli yanaweza kuondolewa moja kwa moja.
● Wahusika: Hii moduli inatumia mchanganyiko wa wahusika kutoka maeneo tofauti. Unaweza
kubadilisha mhusika yeyote kwa kutumia faili za picha za wahusika kutoka kwenye maktaba ya
ubunifu ya mali.
● Maswali ya Majadiliano: Slaidi ya 4 zina maswali ya majadiliano. Unaweza kuongeza, ondoa au
kubadilisha maswali ambayo hayahusiani na kikundi chako.
● Istilahi ya Pochi ya Simu: Istilahi “Pochi ya Simu” na “mobile money” yametumiwa katika
moduli hii yote. Unaweza kubadilisha istilahi hizi kwa istilahi ambazo zinaeleweka vizuri kwako na
wasikilizaji – kama vile akaunti ya mobile money, pochi ya kidijitali, n.k. kwa kutumia kifaa cha

15
“tafuta na badilisha”. Istilahi hizo pia zimeandika kwa matini ya rangi nyekundu kwenye moduli
yote.
● Mifano ya Kiwango cha Riba: Slaidi ya 8 inatoa mifano miwili ya kufanya hesabu ya viwango
vya riba. Unaweza kubadilisha istilahi za mifano ya kiwango cha riba na kuboresha sarafu kama
inavyohitajika.
● Watoaji Huduma za Mkopo Kidijitali: Slaidi ya 11 inajadili aina tofauti za watoaji huduma za
mikopo kidijitali. Unaweza kuongeza, au kuondoa watoaji huduma kulingana na wale waliopo
kwenye soko lako.
● Tathmini mbadala ya Mkopo: Slaidi ya 24 inatoa mifano ya programu zinazotumia njia
mbadala za kujua anayestahili mkopo na kumpa alama za mkopo. Unaweza kuongeza, kufuta, au
kuboresha mifano hii kama ikihitajika.
● Watoaji Huduma za Mikopo: Slaidi ya 26 inajadili sehemu tofauti za kupata mkopo. Unaweza
kuongeza au kuondoa watoaji huduma kulingana na wale wanaopatikana kwenye soko lako.
● Kupata Mkopo: Slaidi ya 27 inaelezea hatua za jumla za kupata mkopo. Unaweza kuboresha
maelekezo haya kulingana na mtoaji huduma za mkopo au bidhaa za mkopo unazotaka.

D. Ijue Simu Yako

Moduli ya ijue simu yako inatoa nafasi kwa wanafunzi kufaidi mazoezi ya moja kwa moja kwa kutumia
programu tofauti, matumizi na vipengele vya simu zao kwa matumizi ya kibinafsi na kibiashara. Moduli hii
pia inatoa taaswira ya aina tofauti tofauti za simu zinazopatikana kwenye soko, vile vile vidokezo vya
kutumia simu kwa usalama, kwa mazingatio ya kudhibiti hatari maalum za mitandaoni kwa wanawake na
wasichana.

JEDWALI LA YALIYOMO MALENGO

● Sehemu ya 1: Aina za simu ● Kufahamu thamani ya kuwa na simu.


● Sehemu ya 2: “Jinsi ya kutumia” simu ● Kujifunza jinsi ya kutumia simu yako.
● Sehemu ya 3: Njia za kulinda data na ● Kuelewa jinsi ya kulinda data yako na
maelezo yako mtandaoni maelezo mtandaoni.

SHUGHULI NYENZO ZILIZOPENDEKEZWA KWA


UFANIKISHAJI

● Kutambua vipengele vya simu za kawaida, ● Kipakatalishi na ngamizi ili kufikia moduli
simu maalum na simu mahiri. ● Projekta ili kufanya maudhui ya moduli
kuonekana kwa ukubwa

16
● Fanya mazoezi kwa kutumia programu na ● Simu moja kwa kila mfanikishaji
vipengele tofauti kwenye simu yako. ● Programu zilizopakuliwa
● Weka mikakati ya kujilinda mwenyewe ● Gharama ya data posta kutoka GSMA
mtandaoni. MISST

NYENZO ZA ZIADA

Masomo ya kusikiliza Sauti: “Hey Sister! Show Me the Mobile Money!”


● Somo la 21: Nitaelewa vipi kuhusu muda wa maongezi na gharama za data?
● Somo la 22: Nitatumia vipi programu?
● Somo la 19: Maelezo yangu binafsi yanaweza kutumiwa vipi?
● Somo la 9: Nitajua vipi kuwa habari ni ya kweli?
● Somo la 10: Nitajilinda vipi na utapeli?
● Somo la 20: Nitaepukana vipi na aina tofauti za utapeli?
Zana-Kiti na Mafunzo:
● GSMA: Kiti-zana ya Ujuzi wa Mafunzo ya Tovuti ya Simu (MISTT)
● GSMA: Video za Ufundishaji Ujuzi wa Tovuti ya Simu
● GSMA: Kiti-Zana cha Ujuzi wa Simu
● Mozilla Foundation: Ujuzi wa Uangalizi Kidijitali

Utengezaji wa Vidokezo vya kukidhi mahitaji

● Mada: Hii moduli imegawanywa katika mada mbalimbali kama ilivyoelezwa kwenye jedwali la
yaliyomo. Unaweza kufuta mada ambazo hazihusiani na wewe pamoja na kikundi chako. Unaweza
pia kufuta slaidi yoyote kwenye moduli ambayo hutumii wewe au kikundi chako. Zaidi ya hapo,
matini yote katika hii moduli yanaweza kuondolewa moja kwa moja.
● Wahusika: Hii moduli inatumia mchanganyiko wa wahusika kutoka maeneo tofauti. Unaweza
kubadilisha mhusika yeyote kwa kutumia faili za picha za wahusika kutoka kwenye maktaba ya
ubunifu ya mali.
● Maswali ya Majadiliano: Slaidi ya 4, 6, 9 na 13 zina maswali ya majadiliano. Unaweza kuongeza,
ondoa au kubadilisha maswali kama ikihitajika.
● Istilahi ya Pochi ya Simu: Istilahi “Pochi ya Simu” imetumiwa kwenye moduli hii. Unaweza
kubadilisha “pochi ya simu” kwa istilahi ambayo inaeleweka vizuri kwako na kwa wasikilizaji –
kama vile akaunti ya mobile money, pochi ya kidijitali, n.k. kwa kutumia kifaa cha “tafuta na
badilisha”. Istilahi hiyo pia imeandikwa kwa matini ya rangi nyekundu.
● “Jinsi ya Kutumia” Simu: Slaidi ya 11 – 34 ya moduli hii inatoa maelekezo ya jinsi ya kufanya
shughuli mbalimbali kwenye simu yako. Kulingana na aina ya simu ambayo wanakikundi wengi

17
wanayo, au kiwango cha ufahamu walichonacho wanakikundi kwenye simu zao. Unaweza
kuzingatia kuacha baadhi ya haya mazoezi. Baadhi ya mazoezi haya yanajumuisha maelekezo ya
aina zote za simu, ambapo mengine ni maalumu kwa simu mahiri. Unaweza kubadilisha au kufuta
maelekezo kama ikihitajika. Unaweza pia kubadilisha picha za maelekezo kwa picha za viwambo
kwa kutumia aina ya simu ambayo inatumika sana kwenye kikundi chako.
● Gharama za Data ya Simu: Slaidi ya 16 inaleta wazo la data ya simu. Zingatia kuonyesha
chapisho la GSMA kwenye gharama za data ya simu kama nyenzo ya ziada.
● Mazoezi ya Kuelezea kwa ufupi: Slaidi ya 36 – 37 inatoa mazoezi halisi. Unaweza kubadilisha
haya mazoezi ili kuakisi ujuzi ambao kikundi chako wanahitaji kufanyia mazoezi. Au aina za simu
walizonazo wanakikundi.

E. Malipo ya Kidijitali

Moduli ya malipo ya kidijitali inaelezea jinsi ambavyo wajasiriamali wanaweza kutumia mifumo ya malipo
ya kidijitali katika biashara zao, ikiwemo pochi za simu, akaunti za merchant, na kodi za QR. Moduli
inatoa maelekezo ya jumla ya jinsi ya kufungua na kutumia mifumo tofauti ya malipo ya kidijitali, vidokezo
vya kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanatumia vifaa vya kidijitali na kuwajibika kukusanya malipo kidijitali
na kwa usalama, na mjadala wa faida za wanawake kuboresha ujuzi wao wa kidijitali na kufungua pochi
zao za simu.

JEDWALI LA YALIYOMO MALENGO

● Sehemu ya 1: Thamani ya kujishughulisha ● Jifunze jinsi ya kukubali malipo ya kidijitali


kidijitali kwa wanawake kwenye biashara kwenye duka lako.
● Sehemu ya 2: Utangulizi wa pochi za simu ● Elewa faida za malipo ya kidijitali.
● Sehemu ya 3: Utangulizi wa malipo ya
kidijitali
● Sehemu ya 4:Yanayofaa kufanywa na
kutofanywa kwenye malipo ya kidijitali

SHUGHULI NYENZO ZILIZOPENDEKEZWA KWA


UFANIKISHAJI

● Kufanya mazoezi ya kufungua pochi ya ● Kipakatalishi na ngamizi ili kufikia moduli


simu na akaunti ya merchant. ● Projekta ili kufanya maudhui ya moduli
● Jifunze jinsi ya ku-skani kodi ya QR. kuonekana kwa ukubwa
● Jadili faida za malipo ya kidijitali. ● Simu moja kwa kila mfanikishaji

18
● Programu zilizopakuliwa (Kama vile
programu za malipo ya kidijitali
● Kodi ya QR iliyochapishwa au iliyowekwa
kwa simu ya kisasa/rununu
● Bei ya pochi ya simu/orodha ya bei ya
kupiga simu.

NYENZO ZA ZIADA

Masomo ya kusikiliza Sauti: “Hey Sister! Show Me the Mobile Money!”


● Somo la 2: Naseti vipi akaunti ya mobile money?
● Somo la 5: Naseti vipi akaunti ya merchant ya biashara yangu?
● Somo la 24: Ni vipi alama iliyowekwa ya kidijitali inaweza kutoa nafasi kwa biashara yangu?
● Somo la 12: Haki zangu ni zipi kwa mujibu wa sheria na masharti ya mobile money?

Utengezaji wa Vidokezo vya kukidhi mahitaji

● Mada: Moduli hii imegawanywa katika mada mbalimbali kama ilivyoelezwa kwenye jedwali la
yaliyomo. Unaweza kufuta mada ambazo hazikufai wewe na kikundi chako. Unaweza pia kufuta
slaidi yoyote kwenye moduli ambayo haitumiki kwako na kikundi chako. Zaidi ya hapo, matini
yote kwenye hii moduli yanarekebishika moja kwa moja.
● Wahusika: Moduli hii inatumia mchanganyiko wa wahusika kutoka maeneo tofauti. Unaweza
kubadilisha wahusika wowote ukitumia faili za picha ya mhusika kutoka kwenye maktaba ya
ubunifu ya mali.
● Maswali ya Majadiliano: Slaidi 4, 17 na 24 zina maswali ya majadiliano. Unaweza kuongeza,
kurekebisha au kubadilisha maswali kama inavyohitajika.
● Matukio: Slaidi 8, 13, na 22 inashirikisha wahusika wawili wakifanya mazungumzo kwa kikundi
kusoma. Haya matukio yanaweza kuboreshwa ili kuakisi hali inayokumba kikundi chako.
● Istilahi ya Pochi ya Simu: Istilahi “Pochi ya Simu” na “Mobile Money” zimetumika muda wote
kwenye hii moduli. Unaweza kubadilisha istilahi hizi kwa istilahi ambazo zinaeleweka vizuri kwako
na wasikilizaji – kama vile akaunti ya mobile money, pochi ya kidijitali, n.k. kwa kutumia kifaa cha
“tafuta na badilisha” Istilahi hizi pia zimeandikwa kwa matini mekundu kwenye moduli yote.
● Watoa huduma ya Pochi ya Simu: Slaidi 11 inajadili aina tofauti ya watoa huduma wa pochi
ya simu. Unaweza kuongeza au kuondoa watoa huduma kulingana na wale wanaopatikana kwenye
soko lako.

19
● Shughuli ya Ada za Pochi ya Simu: Slaidi 14 inaelezea ada zinazohusiana na pochi ya simu. Ili
kuwasaidia wanafunzi kuelewa vile orodha hizi za bei zinavyokaa, zingatia kuchapisha orodha ya
bei ya pochi ya simu kutoka kwa mtoa huduma katika soko lako.
● Ufunguaji wa Akaunti ya Pochi ya Simu: Slaidi 15 inaelezea hatua za jumla za ufunguaji wa
pochi ya simu. Unaweza kuboresha haya maagizo kulingana na mtoa huduma au kwa bidhaa
maalum ya chaguo lako.
● Ufunguaji wa Akaunti ya Merchant: Slaidi 25 inaelezea hatua za jumla za ufunguaji wa
akaunti ya merchant. Unaweza kuborsha haya maagizo kulingana na mtoa huduma au kwa bidhaa
maalum ya chaguo lako.
● Kodi za QR: Slaidi 26-27 inajumuisha picha za kodi za QR. Unaweza kupachika picha ya kodi ya
QR mahali unapopenda ili kikundi kufanya mazoezi ya ku-skani kodi ya QR kwa pamoja.

F. Usimamizi wa Kifedha

Moduli ya usimamizi wa kifedha inawaandaa wanafunzi kuweza kufwatilia vyema, kusimamia fedha za
biashara zao. Moduli inaelezea nidhamu ya kifedha, inajadili umuhimu wa kusimamia fedha, na kuwaambia
wanafunzi kuakisi majukumu yao kwenye usimamizi wa kifedha. Wanafunzi wana nafasi ya kufanya
mazoezi ya kutambua matumizi ya biashara zao, kuweka rekodi kwa vitabu, kujaza usajili wa mikopo, na
kutengeneza taarifa ya faida na hasara (P&L Statement).

JEDWALI LA YALIYOMO MALENGO

● Sehemu ya 1: Kutengeneza mpango wa ● Kujifunza jinsi ya kutengeneza mpango wa


kifedha na kutumia udhibiti wa kifedha kifedha.
● Sehemu ya 2: Kubainisha wajibu wako ● Kutambua aina ya rekodi na vitabu
kwenye usimamizi wa kifedha unavyofaa kutumia kwenye biashara yako.
● Sehemu ya 3: Kuelewa gharama za ● Kuelewa jinsi simu yako inaweza
biashara yako kukusaidia uwekaji hesabu.
● Sehemu ya 4: Kuelewa kwanini na vipi
kuhusu uwekaji hesabu

SHUGHULI NYENZO ZILIZOPENDEKEZWA KWA


UFANIKISHAJI

● Kuakisi wajibu wako kwenye usimamizi ● Kipakatalishi na ngamizi ili kufikia moduli
wa kifedha. ● Projekta ili kufanya maudhui ya moduli
● Kujua gharama za biashara yako. kuonekana kwa ukubwa

20
● Kufanya mazoezi ya uwekaji rekodi na ● Simu moja kwa kila mfanikishaji
uwekaji hesabu. ● Programu iliyopakuliwa ya kuweka rekodi
za biashara kwa vitabu kidijitali
● Karatasi au ruwaza za kidijitali kwa
yafuatayo: Jedwali la matumizi ya biashara,
kitabu cha rekodi za kila siku, usajili wa
mikopo, na Taarifa ya Faida na Hasara.
● Kalamu na penseli

NYENZO ZA ZIADA

Masomo ya kusikiliza Sauti: “Hey Sister! Show Me the Mobile Money!”


● Somo la 23: Nitasimamia vipi fedha za biashara yangu?

Utengezaji wa Vidokezo vya kukidhi mahitaji

● Mada: Hii moduli imegawanywa katika mada mbalimbali kama ilivyoelezwa kwenye jedwali la
yaliyomo. Unaweza kufuta mada ambazo hazihusiani na wewe pamoja na kikundi chako. Unaweza
pia kufuta slaidi yoyote kwenye moduli ambayo hutumii wewe au kikundi chako. Zaidi ya hapo,
matini yote katika hii moduli yanaweza kuondolewa moja kwa moja.
● Wahusika: Hii moduli inatumia mchanganyiko wa wahusika kutoka maeneo tofauti. Unaweza
kubadilisha mhusika yeyote kwa kutumia faili za picha za wahusika kutoka kwenye maktaba ya
ubunifu ya mali.
● Maswali ya Majadiliano: Slaidi ya 5, 10, 11, 14, 16, 19, 39, 40 na 52 zina maswali ya
majadiliano. Unaweza kuongeza, ondoa au kubadilisha maswali kama ikihitajika.
● Istilahi ya Pochi ya Simu: Istilahi “Pochi ya Simu” na “mobile money” yametumiwa kwenye
slaidi ya 30. Unaweza kubadilisha istilahi hizi kwa istilahi ambazo zinaeleweka vizuri kwako na kwa
wasikilizaji – kama vile akaunti ya mobile money, pochi ya kidijitali, n.k. istilahi hizi pia
zimeandikwa kwa matini ya rangi nyekundu.
● Gharama za Biashara: Slaidi ya 15 ina chati ambayo inaweza kubadilishwa inayoorodhesha
gharama za biashara. Unaweza kufuta, kuongeza, au kubadilisha gharama kama ikihitajika.
● Uwekaji Hesabu Kidijitali: Slaidi ya 22 inaelezea dhana ya kutumia simu yako ya kisasa kwa
uwekaji hesabu. Unaweza kuongeza programu ya uwekaji hesabu wa kidijitali au wavuti ambao
unatumika sana kwenye soko lako kama mfano.
● Vitabu vya Kumbukumbu za Biashara ya Kila Siku: Slaidi ya 28 inajumuisha mfano wa
kitabu cha kumbukumbu za biashara ya kila siku unaoweza kubadilishwa. Unaweza kubadilisha
tarehe, mauzo, ununuzi na gharama ili kufaa kikundi chako. Slaidi ya 30 – 31 pia inatoa tukio alafu

21
lifuatiwe na kitabu cha kumbukumbu za biashara ya kila siku cha kufanyia mazoezi. Unaweza
kubadilisha tukio na nambari kwenye kitabu cha kumbukumbu za biashara ya kila siku kama
ikihitajika.
● Sajili za Mkopo: Slaidi ya 33 ina majedwali ya usajili wa mkopo wa mteja na msambazaji
unaoweza kubadilishwa. Slaidi ya 35 – 38 pia inatoa matukio mawili ya usajili wa mkopo ya
kupitia. Unaweza kubadilisha matukio na matini kwenye majedwali ya usajili wa mkopo.
● Taarifa ya Faida na Hasara: Slaidi ya 42 inatoa jedwali la taarifa ya faida na hasara linaloweza
kubadilishwa. Slaidi ya 44 – 49 ni mazoezi ya kufanya utengenezaji wa taarifa ya faida na hasara
kulingana na kitabu cha kumbukumbu za biashara ya kila siku. Matini yaliyopo kwenye kitabu cha
kumbukumbu za biashara ya kila na taarifa ya faida na hasara yanaweza kubadilishwa kama
ikihitajika.

G. Usimamizi wa Orodha ya Mali

Moduli ya usimamizi wa orodha ya mali inashughulikia ujuzi muhimu unaohitajika kufanikisha ufuatiliaji wa
bidhaa dukani. Wanafunzi wanapewa mwongozo wa kujua ni kwanini wanahitajika kuwa na mfumo wa
usimamizi wa orodha ya mali, na vile vile vidokezo muhimu vya kuzingatia wanapotengeneza mfumo wao
wenyewe. Moduli hii pia inawawezesha wanafunzi kufanya mazoezi kutumia vifaa vya usimamizi wa orodha
ya mali, ukizingatia njia zote mbili ya kawaida kwa kutumia mikono na kidijitali.

JEDWALI LA YALIYOMO MALENGO

● Sehemu ya 1: Usimamizi wa orodha ya ● Kuelewa msingi wa usimamizi wa orodha


mali ni nini? ya mali.
● Sehemu ya 2: Jinsi ya kusimamia orodha ● Kujifunza kuhusu mifumo ya usimamizi wa
ya mali yako orodha ya mali.
● Sehemu ya 3: Mifumo ya usimamizi ya
orodha ya mali (kutumia mkono na
kidijitali)

SHUGHULI NYENZO ZILIZOPENDEKEZWA KWA


UFANIKISHAJI

● Kutambua na kufanyia mazoezi mikakati ● Kipakatalishi na ngamizi ili kufikia moduli


ya kusimamia orodha ya mali yako. ● Projekta ili kufanya maudhui ya moduli
kuonekana kwa ukubwa
● Simu moja kwa kila mfanikishaji

22
● Kufanya mazoezi kwa kutumia mifumo ya ● Programu iliyopakuliwa ya usimamizi wa
mkono na kidijitali kwenye orodha ya orodha ya mali
mali. ● Ruwaza ya karatasi ya kusajili ununuzi na
bidhaa zilizopo.
● Kalamu na Penseli

Utengezaji wa Vidokezo vya kukidhi mahitaji

● Mada: Hii moduli imegawanywa katika mada mbalimbali kama ilivyoelezwa kwenye jedwali la
yaliyomo. Unaweza kufuta mada ambazo hazihusiani na wewe pamoja na kikundi chako. Unaweza
pia kufuta slaidi yoyote kwenye moduli ambayo hutumii wewe au kikundi chako. Zaidi ya hapo,
matini yote katika hii moduli yanaweza kuondolewa moja kwa moja.
● Wahusika: Hii moduli inatumia mchanganyiko wa wahusika kutoka maeneo tofauti. Unaweza
kubadilisha mhusika yeyote kwa kutumia faili za picha za wahusika kutoka kwenye maktaba ya
ubunifu ya mali.
● Maswali ya Majadiliano: Slaidi ya 16 na 40 zina maswali ya majadiliano. Unaweza kuongeza,
ondoa au kubadilisha maswali kama inavyohitajika.
● Matukio: Slaidi ya 18 – 19 na 35 zimeshirikisha wahusika wawili wakiwa na mazungumzo ya
kusoma kwa kikundi. Matukio haya yanaweza kubadilishwa ili kuakisi hali halisi ambayo kikundi
kinapitia. Badala yake, haya mazungumzo yanaweza kutumika kusaidia kutengeneza maswali ya
majadiliano.
● Mifumo ya Kutumia Mkono Kusimamia Orodha ya Mali: Slaidi ya 32 na 34 ina mifano ya
mifumo ya kutumia mkono kusimamia orodha ya mali katika muundo wa jedwali. Unaweza
kuhariri matini ili kuakisi muktadha wako, kama vile jina la msambazaji, bidhaa, na bei ya
kununulia.
● Mifumo ya Kidijitali ya Usimamizi wa Orodha ya Mali: Slaidi ya 37 inaorodhesha mifano
ya mifumo ya kidijitali ya kusimamia orodha ya mali. Unaweza kufuta mifano ambayo haihusiani na
muktadha wako na kuongeza mifumo ambayo inapatikana kwenye soko lako. Slaidi ya 38 inatoa
maelekezo ya jinsi ya kutumia mfumo maalumu wa kidijitali wa kusimamia orodha ya mali.
Unaweza kubadilisha maelekezo haya kwa mfumo wa kidijitali wa kusimamia orodha ya mali
unaoupenda.

H. Utangazaji wa Biashara

Moduli ya utangazaji wa biashara inaelezea wanafunzi kanuni tano kuu za kuzingatia wakati
wanaposhughulikia kutaka kutangaza biashara zao na bidhaa. Moduli hii inazingatia muonekano wa duka

23
na vile vile kuwepo mtandaoni. Wanafunzi pia wanapata nafasi ya kujifunza kutumia vifaa vya kutangazia
biashara kidijitali, kama vile WhatsApp Business na Google Maps.

JEDWALI LA YALIYOMO MALENGO

● Sehemu ya 1: Wajue Wateja Wako ● Kujifunza njia za kukuza na kutangaza


● Sehemu ya 2: Kumshawishi mteja kununua biashara yako.
bidhaa zaidi au bora na upendekezaji wa ● Kuweka mikakati kabambe ya kuwa na
bidhaa kwa mteja mtagusano mzuri na wateja.
● Sehemu ya 3: Mikakati ya mpangilio wa ● Kutambua njia za kupanua biashara yako.
bidhaa ● Kuwa na ujuzi na masoko ya kidijitali.
● Sehemu ya 4: Kupanua biashara yako
● Sehemu ya 5: Tumia masoko ya kidijitali

SHUGHULI NYENZO ZILIZOPENDEKEZWA KWA


UFANIKISHAJI

● Kutambua vidokezo na ujanja wa ● Kipakatalishi na ngamizi ili kufikia moduli


kutangaza bidhaa zako. ● Projekta ili kufanya maudhui ya moduli
● Kujifunza jinsi ya kuongeza au kuhitaji kuonekana kwa ukubwa
kuweka biashara yako kwenye Google ● Simu moja kwa kila mfanikishaji
Maps. ● Programu zilizopakuliwa (kama vile
● Kufanya mazoezi ya kutumia Biashara ya WhatsApp Business, Google Maps,
WhatsApp. sehemu za masoko ya kidijitali, n.k)
● Kuwa na uwepo wa kidijitali wa biashara
yako.

NYENZO ZA ZIADA

Masomo ya kusikiliza Sauti: “Hey Sister! Show Me the Mobile Money!”


● Somo la 25: Ni jinsi gani ninaweza kutumia simu yangu kidijitali kupanua mauzo?

Utengezaji wa Vidokezo vya kukidhi mahitaji

● Mada: Hii moduli imegawanywa katika mada mbalimbali kama ilivyoelezwa kwenye jedwali la
yaliyomo. Unaweza kufuta mada ambazo hazihusiani na wewe pamoja na kikundi chako. Unaweza
pia kufuta slaidi yoyote kwenye moduli ambayo hutumii wewe au kikundi chako. Zaidi ya hapo,
matini yote katika hii moduli yanaweza kuondolewa moja kwa moja.

24
● Wahusika: Hii moduli inatumia mchanganyiko wa wahusika kutoka maeneo tofauti. Unaweza
kubadilisha mhusika yeyote kwa kutumia faili za picha za wahusika kutoka kwenye maktaba ya
ubunifu ya mali.
● Maswali ya Majadiliano: Slaidi ya 23, 30, 32, 36 na 46 zina maswali ya majadiliano. Unaweza
kuongeza, ondoa au kubadilisha maswali kama ikihitajika.
● Matukio: Slaidi ya 4, 7, 10, na 14 zina “Matukio” ambayo yanalenga kufanya kikundi chako
kufikiria kuhusu kifaa. Unaweza kubadilisha haya matukio ili kuakisi matakwa ya kikundi chako
itakapohitajika.
● Istilahi ya Pochi ya Simu: Istilahi “Pochi ya Simu” na “mobile money” yametumiwa kwenye
slaidi ya 28. Unaweza kubadilisha istilahi hizi kwa istilahi ambazo zinaeleweka vizuri kwako na
wasikilizaji – kama vile akaunti ya mobile money, pochi ya kidijitali, n.k.
● Masoko ya Kidijitali: Slaidi ya 34 inatoa mifano mitatu ya masoko ya kidijitali. Unaweza kufuta,
au kuongeza mifano kulingana na muktadha wako, vile vile kurekebisha maelekezo ya jumla ya
jinsi ya kutumia soko la kidijitali kwenye slaidi ya 35 ili kuakisi soko la kidijitali unalolipenda.
● Maelezo Mafupi ya Biashara kwenye Google Maps: Slaidi ya 37 inatoa maelekezo ya jinsi
ya seti maelezo mafupi ya biashara kwenye Google Maps. Unaweza kubadilisha ikoni na michoro
ya eneo lako kwa picha za biashara kwenye Google Maps.
● Biashara ya WhatsApp: Slaidi ya 38 inaelezea jinsi ya kutengeneza akaunti ya bishara ya
WhatsApp. Unaweza kubadilisha maelekezo ili kuakisi vyema ujuzi kwa kikundi chako, kama vile
kuongeza jinsi ya kufanya kazi tofauti kwenye akaunti yako ya biashara ya WhatsApp.

25

You might also like