You are on page 1of 9

KANUNI ZA KUFANIKIWA KUTOKA

KATIKA
UCHUMI MDOGO KWENDA UCHUMI MKUBWA.
Utangulizi:
 Tunaishi katika nyakati ambazo ili mtu aweze kuyamudu maisha vizuri, anahitaji
kuwa na vyanzo kadhaa vya kimapato na sio chanzo kimoja.
 Ujasiliamali ndio moja ya kitu kitakachoweza kuleta suluhisho la kiuchumi na
kuboresha maisha ya mtu.
 Kuongeza kipato zaidi ya mshahara unao upata.

KANUNI ZA KUFANIKIWA KIUCHUMI

1. Mafanikio ya kiuchumi/kibiashara hayaanzii kwenye kuwa na mtaji – bali


maarifa ya biashara yenyewe.
 Kabla hujatafuta mtaji wa biashara unayotaka kuifanya, tafuta kwanza
maarifa ya juu ya hiyo biashara unayotaka kuifanya.
 Mitaji ya watu wengi imeteketea kwasababu walianza kutafuta mtaji wa
biashara kabla ya kutafuta maarifa juu ya biashara anayotaka kuifanya.
 Usichukue taarifa za mtaani ukaenda kukopa mtaji uanze biashara. Mtaji
utapotea na utabaki kulipa deni la mtaji ambao haukufanikisha lengo
“That is called a step back”.

2. Mafanikio ya kiuchumi/biashara yanategemea kiwango cha usimamizi wa


biashara au kitegeuchumi hicho.
 Ni nani unayemuweka kusimamia hiyo biashara.
i. Usitafute watu na kuwapa usimamizi wa biashara kwa Misingi ya
Undugu au Urafiki unless anao ujuzi na uwezo huo wa jukumu hilo.
ii. Usitafute watu na kuwapa usimamizi wa biashara kwa Misingi ya
Ukabila.
iii. Usitafute watu na kuwapa kazi au majukumu kwa Misingi ya
Kumuhurumia Mtu.
o Kwao wazazi wake wote wamekufa kwahiyo ngoja tu tumpe hii kazi
hata kama hajasomea.
o Huyu ni mjane anamzigo mkubwa wa watoto nyuma yake ngoja tu
ajibanze hapa asogeze siku.
o Huyu alizalishwaga sana na wanaume wote wakamkimbia sasa ngoja
tu tumpachike hapa naye yeye apate pate chochote cha kumsaidia.

3. Mafanikio ya kiuchumi/biashara yanahitaji Nidhamu ya Fedha na Matumizi.


Note: Kinachofanya watu wengi washindwe kufikia ndoto za mafanikio ya uchumi
na maisha yao ni tatizo la matumizi mabaya ya fedha yasiyo na nidhamu.
• Jifunze kuweka akiba
o Fungua akaunti hata kama kipato chako ni kidogo.
o Usisubiri mpaka utakapokuwa tajiri ndio utaanza kuweka akiba.
o Usisubiri mpaka utakapokuwa umepata vingi ndipo uanze kuweka akiba.

• Watu waliofanikiwa sana katika maisha ni wale waliojitahidi kujinyima na kujijengea


mazoea ya kuweka akiba kidogo kidogo. (Accumulation).

• Ukipata pesa wekeza kwanza kisha kula kinachobaki. Tofauti ya Masikini na Tajiri
o Masikini akipata pesa anakula kwanza kisha anawekeza kama itakuwa imebakia.
o Tajiri akipata pesa anawekeza kwanza kisha anakula inayobaki.

• Epuka kukopa kwa shughuli isiyo ya maendeleo.


o Jiepushe na kukopa kopa vitu kutoka kwa wafanyabiashara na wajasiriamali
wanaokopesha vitu mbali mbali ambavyo sio vya muhimu.
o Usikope kwajili ya harusi – tafuta michango na ukipata kidogo fanya harusi
ndogo kulingana na kipato chako usitake mambo makuu yatakuumiza.
o Usikope kwajili ya sherehe kama birthday, graduation nk.
o Ukikopa iwe ni kitu cha kimaendeleo.

• Jifunze kuweka vipaumbele juu ya mahitaji muhimu utakayo fanya kwa pesa iliyopo
mkononi mwako.
o Usijaribu kutaka kutekeleza kila hitaji.
o Mahitaji ni mengi hutaweza kuyamaliza.
o Michango ni mingi hutaweza kumchangia kila mtu.
o Madeni ni mengi hutaweza kuyalipa yote kwa mara moja.
o Sio kila unacho kitaka ni lazima ukipate.
o There is difference bebween what you want and what you need.

• Usikope vitu ambavyo vitakuwa vinakunyonya Zaidi badala ya kukuingizia kipato.


o Mfano unakopa gari la kutembelea tu ambalo sio la lazima na halikuingizii kitu
na huna uwezo wa kulihudumia.
o Usikope gari huku huna uhakika wa mafuta au kulihudumia.
o Mahitaji ya gari ni kama mahitaji ya mwanadamu tu:
 Gari linahitaji kula na kunywa.
 Gari linahitaji kuoga.
 Gari linahitaji kwenda hospitali mara kwa mara.
 Gari linahitaji kulipiwa kodi na ushuru wa mara kwa mara.
Kama unakipato kidogo na hujafanya mambo mengine ya kipaumbele, usitangulize
kukopa gari kwanza na hasa gari ambayo sio ya kukuongezea kipato.

• Usipende kukaa na fedha mfukoni, nyumbani au kwenye simu zako.


o Jitahidi uwe na akaunti yako na kila mara weka kiasi chochote kinachoingia.
o Mkononi ibaki pesa kidogo tu ya matumizi madogo madogo.
o Usipende kutembea na ATM card yako kila unapokwenda.
• Usimpe pesa Rafiki yako wala ndugu yako hata kama ni mzazi wako au kaka au dada
akuwekee ili siku ukiwa unazihitaji akupe.
Pesa zako zitunze mwenyewe.
o Fungua akauti yako fungia pesa zako huko.
o Mtaharibu Urafiki wenu,
o Mtaharibu undugu wenu.

4. Dhibiti vyanzo vyako vya msongo wa mawazo


o Msongo wa mawazo unamchango mkubwa sana katika kuudhohofisha uchumi
wa mtu.
o Msongo wa mawazo unapunguza uwezo wa mtu kufikiri kwa kina.
o Msongo wa mawazo unapunguza uwezo wa mtu wa ubunifu.
o Msongo wa mawazo unapunguza uwezo wa mtu katika kufanya maamuzi.
kivipi:
 Ishi kwa kiwango chako
 Social involvement.

 Let your feelings out – Kucheka au Kulia.


 Kula chakula kizuri pale inapowezekana.
 Lala mahari Pazuri – Mahali unapolala pana uhusiano mkubwa sana na kiwango
cha Stres.
 Pata rafiki mzuri unayemwamini wa kumshirikisha mambo yako na hasa yale
yanayo kuumiza usibaki nayo moyoni

MAISHA YA MAFANIKIO
“Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama

Unahitaji Kujua Kweli Hizi Kabla ya Kuchukua Mkopo Wowote!!!!!


Suala la madeni yatokanayo na mikopo linawatesa wengi. Sababu mojawapo ya hali hii
ni kwamba kuna kweli nyingi ambazo watu hawazijui kuhusu mikopo na pia kuna
upotoshaji mwingi sana kuhusu mikopo. Kwa mfano: Je, unajua vigezo vya kuzingatia
kabla ya kuchukua mkopo? Je, unajua wakopeshaji huwa wanammanisha nini
wanapokuambia kuwa “unakopesheka”? Je, unajua kuwa ni hatari kuchukua mkopo kwa
ajili ya biashara mpya? Je, unajua kuwa dhana kwamba huwezi kuendelea bila mkopo
haina ukweliFuatana nami nami katika makala haya ninapoangazia hoja hizi:

Kigezo cha kuzingatia unapochukua mkopo ni kimoja tu >Ikitokea unahitaji kukopa,


kigezo muhimu cha kuzingatia katika kuamua kama uchukue mkopo huo au la ni
kimoja tu. Kigezo hicho ni hiki:-

 Usilipe mkopo kwa pesa zako, bali lipa kwa pesa za watu wengine. Kigezo hiki
kinamaanisha kwamba uchukue mikopo mizuri, mikopo ambayo inazalisha na siyo
mikopo inayokugharimu wewe. Kwa kutumia kigezo hiki, Mkopo pekee unaoweza
kuchukua ni mkopo wa uzalishaji kama vile mkopo kwa ajili ya biashara ambayo tayari
imeshasimama na hivyo unaupeleka mkopo huo moja kwa moja kwenye sehemu yenye
faida, kwa lengo la kuongeza faida zaidi. Faida utakayopata kwenye biashara ndiyo
itatumika kulipa mkopo huo na siyo fedha kutoka kwenye vyanzo vyako vingine.
Hivyo, yakupasa ukokotoe vizuri hesabu zako na ujiridhishe kuwa faida utakayopata
itatosha angalau kulipa mkopo na wewe ukabakiwa na sehemu ya faida.

Usichukue Mkopo Kwa Ajili ya Mtaji wa Biashara Mpya


Kuwa makini na mkopo kwa ajili ya mtaji wa biashara mpya. Usichukue kabisa mkopo
wa aina hiyo. Huo unaweza usiwe mkopo mzuri, kwa sababu unapoanza biashara mpya,
hakuna faida yoyote unayoweza kupata. Lakini pia, unakuwa hauna uelewa wala uzoefu
na biashara hiyo. Ikumbukwe kuwa biashara zina changamoto na hatari (risks) nyingi.
Kabla ya kuchukua mkopo kwa ajili ya kukuza mtaji wa biashara mpya. inashauriwa
kujipa muda wa kutosha ili kujua changamoto na hatari za biashara yako na
ukishaifahamu vizuri, ndipo unaweza kuchukua mkopo kwa ajili ya kukuza mtaji
biashara hiyo. Ukikopa ili upata mtaji wa kuanzisha biashara mpya, utaanza kulipa
marejesho ya mkopo kabla hata biashara haijaanza kukupatia faida. Katika hali hii,
utalazimika kuchukua mtaji kwenye biashara ili kulipa mkopo au kulipa mkopo kwa
kutumia fedha kutoka kwenye vyanzo vingine.

Kujua tofauti kati ya mikopo mizuri na mikopo mibaya Unaweza pia kupata
kitabu kizuri kuhusu elimu ya mikopo na mambo mengine kuhusu fedha
Usihadaike na Kauli za Wakopeshaji Kuna watu huwa wanajikuta wamechukua
mikopo baada ya kushawishiwa na kauli za wakopeshaji na hata watu wengine ambao
wana mikopo. Kwa kuwa siku hizi taasisi za kukopesha ni nyingi, ukiwa mfanyakazi
ambaye mshahara ni wa uhakika au unafanya biashara ya uhakika na una mali za
kuweka dhamana, wakopeshaji watakuwinda sana wakukuposhe maana watakuwa na
uhakika kuwa utaweza kurejesha mkopo wao. Kwa sababu hiyo watatumia kila mbinu
kukushawishi wakitumia kauli mbalimbali. Kumbuka kuwa mikopo ni biashara kama
biashara nyingine. Mojawapo ya mbinu ya kupata wateja katika biashara niushawishi.
Hivyo, wakopeshaji nao wako kwenye biashara, na ili wapate wateja lazima
wawashawishi watu kwa mbinu mbalimbali. Baadhi ya kauli za wakopeshaji ni kama
vile “wewe unakopesheka” au “mfanya biashara asipokopa hawezi kukua kibiashara” au
“Mtu huwezi kuishi bila kudaiwa” au ‘usipokopa utachelewesha maendeleo yako” au
“hakuna mtu anayeendelea duniani bila kukopa” au “kama serikali inadaiwa, sembuse
wewe?” na kauli nyingine nyingi. Kosa ambalo hupaswi kulifanya ni kukopa kwa
sababu tu eti wengine wanakopa au kwa sababu wakopeshaji wamekuambia
unakopesheka au kwamba usipokopa unajicheleweshea maendeleo Mkopeshaji
anapokwambia “unakopesheka” hana maana kuwa mkopo huo utakuwa mzuri kwako au
ana uchungu sana na maendeleo yako, bali anachomaanisha ni kwamba mkopo
anaokushawishi kuchukua, ana uhakika kuwa una uwezo wa kuulipa. Hivyo, usikope
kwa sababu unakopesheka bali kopa kwa sababu unahitaji mkopo na kwamba mkopo
huo ni mzuri kwako.

Je, ni Kweli Kwamba Huwezi Kuendelea Bila Kukopa?


Pamoja na maonyo na mifano halisi ya hatari za mikopo kutoka ndani na nje ya
Maandiko Matakatifu, watu wengi wanapuuzia uwezekano wa hatari hizo kutokana na
kuaminishwa kuwa mikopo ni muhimu sana katika kufikia mafanikio ya kiuchumi. Ipo
dhana katika jamii nyingi duniani hususani katika biashara kuwa ni vigumu kuendelea
bila kukopa.
Baadhi ya watu wanapinga mafundisho yanayotoa tahadhari dhidi ya hatari za mikopo
kwa madai kwamba mafundisho kama hayo yanawafanya watu wasiendelee kiuchumi.
Watu kama hao huwa wanatoa mifano mingi ya watu waliofanikiwa kwa kutumia
mikopo na watu ambao wanasuasua kimaendeleo kwa sababu ya kutokuchukua mikopo.
Hata hivyo, watu hao huwa hawatoi mifano ya watu walio na hali mbaya kimaisha au
kibiashara kwa sababu ya mikopo.

Ni kweli kabisa kwamba mikopo inaweza kukusaidia kupiga hatua kubwa


kimaendeleo. Na ipo mifano dhahiri ya hilo. Lakini si kweli kwamba huwezi kuendelea
bila kuchukua mkopo.
Ipo mifano mingi ya watu ambao walifanikiwa kibiashara na kimaisha bila kuchukua
mikopo bali wamefanikiwa kwa kuzingatia tu kanuni za msingi kuhusu usimamizi wa
fedha zao au biashara zao ikiwemo kuwa na vyanzao vingi vya mapato, kuweka akiba
kwa ajili ya uwekezaji na pia kuwa na nidhamu ya

matumizi ya fedha zao. Huenda watu hawajui, lakini yapo makampuni makubwa duniani
ambayo hayana mkopo wowote na mengi kati ya hayo hayajawahi kuchukua mkopo wa
aina yoyote.
Ukiacha makampuni, wapo pia watu binafsi waliofikia mafanikio makubwa ya kiuchumi
bila mikopo. Kwa leo sitawataja kwa kuwa sijapata ridhaa yao. Naomba kwa leo
nikutajie tu baadhi ya makampuni yasiyo na mikopo.. Baadhi ya makampuni hayo ni
kama ifuatavyo:
Apple – Hii ni kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya Marekani ambayo inaunda na
kuuza bidhaa mbalimbali za teknolojia, programu za kompyuta na huduma za
mtandaoni. Bidhaa za kampuni ya Apple ni pamoja na simu za mkononi za iPhone,
vishikwambi vya iPad, kompyuta za Mac na bidhaa zingine.
Hii ndiyo kampuni inayoongoza kwa thamani kubwa duniani.

Amazon – Hii ni kampuni kubwa kabisa duniani ya uuzaji wa bidhaa mtandaoni. Kwa
kipimo cha mapato na mtaji wa soko, ni kampuni ya pili baada ya Alibaba Group kwa
jumla ya mauzo. Amazon ni kampuni ya pili kwa thamani duniani (nyuma ya kampuni
ya Apple), kampuni kubwa ya intaneti kwa mapato duniani, na baada ya Walmart, ni
mwajiri wa pili mkubwa nchini Marekani. Mwanzilishi wa Amazon ni Jeff Bezos
ambaye kwa sasa ndiye tajiri namba mbili duniani na kabla ya hapo aliwahi kuwa tajiri
namba moja duniani kwa muda wa miaka minne mfululizo (2017-2020) kabla
hajazidiwa na Elon Musk.

 The American Express – Ni kampuni ya Marekani inayojishughulisha na masuala ya


fedha na ndiyo mmiliki wa credit card iitwayo American Exopress ambayo inachukua
karibu robo ya miamala yote ya credit cards nchini Marekani.

Starbucks – Ni kampuni ya kimataifa yenye makao yake makuu nchini Marekani


ambayo inajishughulika na uuzaji wa kinywaji cha kahawa na bidhaa nyingine za
kahawa. Hii ndiyo kampuni kubwa duniani katika biashara hiyo. Kauli kwamba huwezi
kuendelea bila mkopo hasa kwenye biashara si sahihi. Hivyo, ninarudia tena ushauri
wangu kuwa, usichukue mkopo wowote kama mkopo huo utaulipa kwa fedha zako
mwenyewe.
Kigezo pekee cha kuchukua mkopo ni kama mkopo huo utaulipa kwa fedha za wengine.
Mkopo pekee unaoweza kuuchukua na ukaulipa kwa fedha zako mwenyewe ni mkopo
ambao utakuwezesha kuokoa maisha yako au ya watu wako wa karibu. Na utafanya
hivyo baada ya njia zingine zote kushindikana.

Zaidi ya hapo, kamwe usichukue mkopo. Hata hivyo, hata mkopo wa kukuwezesha
kuokoa maisha yako au ya watu wa karibu nao unaepukika ikiwa utajioanga vizuri na
kuweka mipango mizuri ya kukabiliana na dharura na majanga kama vile kuweka akiba
na kuwa na bima

1. MAANA YA UJASIRIA MALI.


Ujasiria mali ni jumla ya mambo mengi yahusikayo katika utoaji wa huduma, na
kujipatia faida. Mfano; Kilimo, ufugaji, biashara, uvuvi, ufundi n.k. Kuna ujasiria Mali
mdogo (wa kawaida), wa kati na wa juu (mkubwa). Mtu atekelezaye hayo ni

2. MJASIRIA MALI.
SIFA ZA MJASIRIA MALI.
 Mbunifu.
 Mvumilivu, asiyekata tamaa.
 Anayekubaliana na kukabiliana na matokeo ; faida au hasara.
 Mwenye kutumia changamoto zake ama za wenzake , kwa kuzigeuza kuwa fursa
na kujipatia faida.

3. Nyenzo za ujasiriamali.
 Utafiti.-Taarifa hizi zitamsaidia mjasiria mali kupanga na kuamua huduma gani
inafaa kwa eneo husika.
 Mtaji.-Kianzio/fedha itumikayo katika ukusanyaji wa mahitaji kwenye uzalishaji
na utoaji wa huduma.
 Bidhaa. Ni jumla ya vitu ama huduma aitoayo mjasiria mali kwa wateja wake
 Wateja. Watu ambao wanaoihitaji kuipata huduma ama bidhaa toka kwa mjasiria
mali, kwa malipo halali na halisi.

AINA ZA WATEJA.
1. Mteja wa kudumu (mteja mfalme)
2. Mteja kuuliza bei. "window shopping" kuuliza bei hata kwa bidhaa asiyotaka
kununua. Akijiridhisha bei, hurudi kununua japo bidhaa moja hapa, nyingine
kule kulingana na unafuu wa bei.
3. Mteja "nipunguzie".
4. Mteja mtafiti- Huyu bei zote anazijua. Anaweza kupata huduma na akalipia bila
kuuliza bei.
5. Mteja deko-Anataka kunyenyekewa na kubembelezwa. Hupenda sana kuomba
kuongezwa, hata ikibidi kwa nguvu au kwa lazima, wana lawama pia.
6. Mteja daiwa- Hata kama ana pesa mfukoni, atataka umkopeshe tu. Wakati
mwingine wasumbufu kulipa na mwishowe nao pia wana lawama.

Mfano sokoni. Ni mahali ambapo mjasiria mali na wateja wake wanakutana kwa ajili ya
kubadilishana huduma kama malipo halali na stahiki.
AINA ZA MASOKO.
1. Soko huria. Kila mtu ana Uhuru wa kuingia na kutoka bila masharti. Ushindani ni
mkubwa na hakuna mfumo wa udhibiti wa bei kati ya muuzaji na mnunuzi.
2. Soko Hodhi. Mtoa huduma anakuwa peke yake tuu. Mf TANESCO. Na aina
zingine za masoko makubwa kulingana na mfumo wa Ujasiriamali mkubwa.

MATANGAZO.
Biashara inafaa kutangazwa kwa mabango na sauti ili wateja wafahamu huduma yako.
Hapa kuna bidhaa, bei, mahali ulipo na promosheni.

UFANISI NA UTEKELEZAJI WA BIASHARA.


Kuna jumla ya mambo matatu yanayotegemeana;- Mahitaji, bei na usambazaji.
1. Mahitaji.Ni jumla ya mambo au vitu vyote anavyotakiwa mjasiriamali kuwa
navyo, ambavyo vinahitajika kwa matumizi ya mteja sokoni.
Kanuni za mahitaji. Mahitaji yanapoongezeka, ni matokeo ya usambazaji au
uzalishaji unapopungua, kusuasua au kukoma. Kwa lugha nyingine kuadimika.
Mahitaji ya bidhaa au huduma yoyote yanapoongezeka, bei yake inapanda au
kuwa juu. Kinyume cha hapo, mahitaji yanapungua.
2. Bei. Ni kiasi halali na stahiki kitumikacho kulipia gharama za bidhaa au huduma
itolewayo au inayohitajka. --Kanuni za bei. Bei huongezeka sokoni, mahitaji
yanapoongezeka. Bei huongezeka usambazaji/ uzalishaji unapopungua. Kinyume
cha hapo, bei inapungua au kushuka.
3. Usambazaji/uzalishaji. --Ni uenezi au utawanyaji wa huduma au bidhaa kutoka
kwa mjasiria mali hadi kwa mteja.

KANUNI ZA UZALISHAJI/ USAMBAZAJI.


Huongezeka mahitaji yanapoongezeka Huongezeka bei inapopanda. Kinyume cha hapo,
uzalishaji/usambazaji unapungua.

5. MAKUNDI YA WAJASIRIA MALI.


Kama ilivyoelezwa kwenye utangulizi, makundi hayo ni:-
1. Wajasiria Mali wadogo. --Hili ni kundi kubwa sana ambalo kila mmoja huwa na
namna ambavyo anaendesha biashara zake.
Utawanyaji au usambazaji wa bidhaa zao hutokea kwake na kumfikia mlaji/mteja
moja kwa moja. Hawana anwani wala ofisi maalum, wengi wao hawajarasimisha
biashara zao TRA, Bima wala kusajiliwa BRELA. Mfano. Wachoma mahindi,
wauzaji wa ubuyu na juisi, petrol kwenye chupa za maji/kupima, Machinga,
wachimba mchanga, wagonga kokoto, mama/baba lishe, boda boda, magenge ya
vyakula, vibanda vya rejareja. Mtaji wao hauna lazima ya kuanza na fedha.
Hawatambuliki na hawaaminiwi sana na taasisi za kuaminika za kifedha mf
mabenki, na bad ala yake, wengi wao huishia kuchukua mikopo ya Kausha damu.
Na madhara yake ni makubwa.
2. Wajasiria Mali Wa Kati. --Kundi hili ni la mtu mmoja mmoja au muungano wa
watu kadhaa na wanafaweza kufanya kazi kama umoja, wenye makubaliano na
mkataba wa ushirikiano kimaandishi. Hupata bidhaa zao toka kwa mzalishaji wa
chini au wajasiriamali wakubwa, huvitunza au kusambaza kwenye maeneo ya
uhitaji. Wanauza Jumla na rejareja.

Wamesajiliwa na kutambulika kwenye mamlaka za serikali, na wanaaminiwa na


kukopesheka kwenye taasisi za kifedha.
3. Wajasiria Mali Wakubwa. --Hawa ni makampuni makubwa ya kibiashara.
Wanatambuliwa, wanaamika, kukopesheka na pia wana miliki hisa na hutoa
gawio la faida yao kwa wateja wao na serikalini pia. Hesabu zao zinakaguliwa na
mamlaka za kisheria. Bidhaa zao huwa zinapatikana kwa mzalishaji wa chini,
huzichakata, kuzihifadhi, kuzisambaza kwa wajasiria Mali wa kati, kisha kumfikia
mteja. Huuza kwa bei ya jumla na kwa wingi wa kipimo, mfano zaidi ya tani
kadhaa kwa mkupuo na mteja mmoja.

7. HASARA KATIKA BIASHARA.


Mahitaji, bei na uzalishaji au usambazaji ni moja ya sababu za biashara au shughuli za
ujasiria mali kudorora.
Hasara ni ya kutabirika na isiyotabirika na isiyotabirika.

i. Hasara inayotabirika.
Kuishiwa na bidhaa Mara kwa Mara - kuuza Hamna. Kuharibika, expired date, kuoza
nk. Magonjwa na wadudu waharibifu, - Kilimo na Mifugo. Bidhaa kukaa muda mrefu
bila kunuliwa au kubaki. Utunzaji wa bidhaa mf kuganda kwa simenti, kuwepo kwa
panya na mchwa, kuchacha na kuharibika kwa vinywaji. Kutozingatia kanuni za
ujasiriamali. Kutowakarimu wateja Kwa lugha za biashara.

Jinsi ya kukabiliana na hasara inayotabirika.


Andaa bidhaa zinazoendana na mahitaji ya wateja. Toa motisha / promotion au punguzo
kidogo la bei bila kuathiri mtaji wako.Chukua tahadhari kulingana na changamoto yako
unayoipata. Tunza risiti za manunuzi na malipo mengine.

ii. Hasara isiyotabirika.


Mlipuko wa majanga mbalimbali, mf ukame, mafuriko, moto, ajali nk Wizi ama
ujambazi. Msukosuko wa Uchumi, kushuka kwa shilingi katika soko la fedha.
Mabadiliko ya Sera za serikali. Mfano kila mfanya biashara kutoa risiti kwa EFD.

JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HII YA HASARA


ISIYOTABIRIKA.
Chukua tahadhari kwa majanga ya moto, wizi na ajali. Kuwa na bima kwa wafanya
biashara wakubwa na wa kati. Kuwa na shughuli mbadala ya uzalishaji mali. --Tunza
kumbukumbu.

8. UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU.
Risiti/stakabadhi, ledger, counter book, Petty cash voucher, computer nk.
KAZI YA KUFANYA. Tambua faida na hasara kwenye ujasiria mali wako. Hapa kuna
faida mbili, faida ghafi na faida halisi.

Faida ghafi. Ni jumla ya mapato yote yaliyopatikana baada au mauzo au utoaji wa


huduma. Inajumlisha mtaji na faida yote.
Faida halisi. Hii ndiyo faida inayochanganua baada ya kupatikana kwa mauzo na
kuondoa mtaji ama kianzio.
Faida halisi = mtaji/kianzio - faida ghafi.

9. JINSI YA KUDUMU KATIKA BIASHARA NA MAONGEZEKO YAKE.


Punguza matumizi yasiyo ya lazima kutoka katika biashara yako.
 Uaminifu wa kweli.
 Weka nidhamu katika fedha na heshimu mwanzo wa faida yako ndogo
unayoipata.
 Uwe mbunifu, anzisha huduma ambazo hazipo.
 Uwe na uzalishaji mbadala.
 Jipangie kiasi cha mshahara na faida yako iendeleze kibiashara.
 Heshimu na endeleza malengo yako.
 Uwe na ukomo wa madeni ya kukopa na kukopesha.
 Pata elimu ya ujasiria mali na usimamizi wa fedha.
 Pata mikopo kwenye taasisi za kifedha zinazoaminika, ili uendeleze biashara
NA SIYO KUANZISHA BIASHARA MPYA.
 Watambue wateja wako na mahitaji yako.
 Faida za uzalishaji mbadala. Kukabiliana na misukosuko katika biashara.
 Kuongeza mtaji.
 Matumizi yako yasiguse mtaji wa biashara,Ni rahisi sana kufanikisha malengo
yako.

10.VIKWAZO KATIKA BIASHARA.


Vikwazo hivi huifanya biashara idumae, isikue na kisha kufa kabisa.
 Ukosefu wa elimu ya ujasiria mali.
 Mwingiliano wa bidhaa.
 Mabadiliko ya bei kiholela.
 Ukosefu wa nidhamu ya fedha na usimamizi wake.
 Mtaji mdogo, au uhaba.
 Utafiti wa masoko kulingana na mahitaji ya huduma ama bidhaa zinazohitajika
kwa wateja Majungu*.
 Miundo mbinu na mawasiliano kuwa duni.
 Ukosefu wa nishati/ umeme wa kuaminika.
 Bidhaa kutoongezwa thamani.
 Mfumo wenyewe wa biashara. Mf Biashara hodhi, huria.
 Kanuni za uhifadhi na utunzaji wa bidhaa

You might also like