Professional Documents
Culture Documents
ENEO:
Ndani ya Dar es Salaam, mwanza ama arusha, kupata eneo linalotosha kuweka
supermarket ndogo unahitaji kati ya Tshs 800,000 hadi 3,000,000 kutegemea na
ukubwa wa chumba cha biashara na wingi wa watu katika eneo husika.
Kuna msemo huwa naupenda sana. Msemo huo si mwingine bali ni ule usemao
“Vidogo Vyavutia”. Tuchukue hiki kiwango cha chini cha Tshs 800,000. Tunalipa
miezi sita inakuwa Tshs 4,800,000. Mh, acha kuguna. Usije ukaogopa mpaka
ukaacha kuwaza kuanzisha biashara hiyo. Jua kuwa asilimia kubwa ya pesa
utayolipa kwenye mini supermarket ni kodi ya upangaji.
LESENI NA VIBALI:
Ili kufanya biashara ya mini supermarket unahitaji vibali mbali mbali na leseni.
Usiumize kichwa juu ya hili maana hata uendapo ugenini unahitaji kujua nauli za
daladala za kule japo hakuna anaejishuhulisha kuulizia. Unachotakiwa kujua ni
bajet ya kuandaa kwa nauli za daladala ama texi kule uendako. Ili usisumbuke na
suala la vibali na leseni weka bajet ya Tshs 600,000 itamaliza kila kitu.
BIDHAA:
Wapo wasambazaji kadhaa walio tayari kusambaza bidhaa mbali mbali kwenye
mini supermarkets. Hawa husambaza mlango hadi mlango. Unahitaji kujiandaa na
kati ya Tshs 10,000,000 na 20,000,000 kujaza bidhaa ndani ya supermarket.
Kwakuwa “Vidogo Vyavutia” acha tuanze na Tshs 10,000,000.
WATUMISHI:
Kwa supermarket ya bidhaa za milioni 10, hapo wapaswa uwe na watu wasiozidi 5
watakaofanya kwa shift ya watatu watatu. Hawa watakugarimu kama Tshs
2,000,000 kwa mwezi.
FAIDA:
Mini supermarkets hutoa faida kati ya Tshs 2,000,000 na 3,000,000 kwa mwezi.
Kwakuwa tumeamua kuanza kile “Kidogo Kinachovutia” faida yetu itakuwa Tshs
2,000,000 kwa mwezi.
CHANGAMOTO:
Huwa hakuna biashara isiyo na changamoto. Changamoto ya kwanza kwa
supermarket ndogo ni wizi. Wamiliki wengi wa supermarket ndogo ndogo
hulalamikia suala la wizi kutoka kwa wateja na watumishi wao. Ni rahisi mtumishi
wako kukwepa wizi wake na kusingizia wateja. Wapaswa kuweka mitego mbali
mbali ya kupunguza suala la wizi ili unufaike na faida itokanayo na biashara yako.
Moja ya mitego hiyo ni cctv camera. Kwa kawaida ukiweka camera hata mbili tu
zitasaidia sana. Hii hugarimu wastani wa Tshs 1,200,000.
Pia kuna bidhaa ambazo hazitouzika kabisa na wapo wateja watakaohitaji bidhaa
ambazo wewe hauna. Hii ni changamoto ila isije kukuvunja moyo kwani
itakusumbua mwanzoni tu na baadae utakuwa mzoefu.
Biashara ya mini supermarket ni biashara yenye faida sana ila huhitaji mtaji
usiopungua Tshs 17,000,000 na uangalizi wa karibu ili kushamiri.