You are on page 1of 4

Introduction  

1. 
Habari ya [asubuhi,mchana,jioni] jina langu ni [Agent name] ,Nakupiga simu kutoka GiveDirectly 
ambalo ni shirika lisilo la kiserekali na ambalo limeshirikiana na [Partner name] kupeana msaada kwa 
wakenya. 
Tulipata nambari yako ya simu kutoka kwa [Partner name] kwa uwezekano wa kukuandikisha kwenye 
mradi huu.  
 
2. 
Nazungumza na Nani?  
 
3. 
Mazungumzo haya yatarekodiwa kwa uhakikisho wa ubora wa huduma zetu, na pia ili kurekodi idhini 
yako kama unakubali au kukataa kushiriki kwa huu mradi 
Unakubali kurekodiwa? Kama ni la nitakata simu. 
 
4. 
Sheria ya Kenya inatupasa tupate idhini kutoka kwa  kila tunaye mwandikisha kwa mradi wetu kwa 
kuandika. 
Kutokana kwa njia ya uandikishaji wa mbali tunaoendesha sasa, uidhinishi utafanyika kupitia kwa SMS 
mwisho wa utafiti huu ambao utatutumia, kuthibitisha kukubali au kukataa kwako. 
Kutuma sms hiyo unahitaji kuwa na 1ksh kwenye airtime yako . 
Unaweza thibitisha kwamba uko na 1 kwa airtime? 
Bonyeza *144#  
 
5. 
Kabla tuendelee na usajili, ni lazima tukuulize kama utakubaliana na masharti yanayohitajika kisheria 
 
6. 
Ijapokuwa hatuna ushirikiano na serikali, kwa kujiandikisha kwa huu mradi, tunaweza hitajika kugawa 
habari yako kwa mashirika ya serikali yanayofuatilia kazi zetu. Hatuwezi hakikishasha kwamba 
hawawezi kukutoa kwa ustahiki wa miradi zingine za serikali. 
Kwa hayo yote, unaweza taka kuwa mfadhiliwa wa givedirectly na utupe idhini ya kuendelea na huu 
mchakato wa usajili?  
 
7. 
Kwa mradi huu, tunapeana pesa kwa wakati huu wa covid-19  kupitia mpesa. Pesa hizi hazina masharti 
wala hazina ushirikiano wowote na mwana siasa yeyote,dini yoyote au kabila lolote.  
Ukiandikishwa kwa huu mradi, tutakutimia 3000 kwa muda wa miezi miwili 
kuna zile hatari unazopaswa kujua kama: 
● Kuna wale watu watakao taka kukuibia  
● maajenti wanaoweza taka kukudanganya  
● watu wa serikali ama wengine wanaoweza taka kukuitisha pesa 
● Kuwa na mvutano na watu kwa familia yako na jinsi inavyofaa kutumia pesa.   
Sisi kama Givedirectly, tutajaribu kukutayarisha na mawaidha lakini iwapo kitu kitatokea na pesa 
hizi,  itakuwa  jukumu lako kukabiliana na swala hilo. Hii hutokea kwa wafadhiliwa wachache lakini 
tulitaka ujue.  
Kwa haya yote ungependa kuwa mfadhiliwa wa givedirectly na utatupa idhini ili tuweze kuendelea na 
mchakato wa kujiandikisha? 
 
 
8. 
Pesa za givedirectly hazipaswi kutumiwa kwa : 
● Shirika lolote ama watu wanaohusika na ugaidi 
● Kitu chochote kile kitakacho hatarisha usalama wa wafadhiliwa wa mradi huu na ama jamii 
ukiwemo na siyo tuu binduki ama silaha 
● Udanganyifu au ufisadi 
● Kukuza shughuli za uhalifu. 
Shughuli kama hizi zinaleta athari kwa mradi huu na jamii,  na kuna uwezekano kusababisha 
kusimamisha kwa kutuma na kurejesha fedha.  
Unakubali kufuata hizi  taratibu za matumizi? 
 
9. 
Sasa naenda kukutumia ujumbe huo wa idhini. Ungependa usome kwa kiswahili ama kiingereza? 
 
***** 
After Consent 
10. 
Unakubali GD ipeane information yako kwa NGOs ama serekali ya kenya, elewa kwamba hii inaweza 
kuathiri kusajiliwa kwako kwenye miradi mingine ya corona 
 
11. 
Majina yako kamili ni yepi?  
 
12. 
Uko na kitambulisho chako na wewe?  
Unajua nambari yako ya kitambulisho? 
 
13. 
Tarehe ya kuzaliwa 
 
14. 
Nisome nambari yako ya kitambulisho tafadhali? 
 
15.  
Umewahi sajiliwa kwa mradi wowote wa givedirectly? 
 
16. 
Sasa nitakuuliza maswali machache ili kuelewa ikiwa una ulemavu. Haya maswali hayata athiri upokezi 
wako wa pesa lakini yatatumika kuhakikisha huduma tutakayo kupatia inalenga mahitaji yako. 
Tafadhali jibu kwa ukweli iwezekanavyo. 
 
Je, una ugumu wa kuona hata ukitumia miwani 
 
● La, sina ugumu 
● Ndiyo, ugumu mdogo 
● Ndiyo, ugumu mwingi 
● Siwezi kabisa 
Je, una ugumu wa kusikia hata ukitumia visaidizi vya kusikia 
● La, sina ugumu 
● Ndiyo, ugumu mdogo 
● Ndiyo, ugumu mwingi 
● Siwezi kabisa 
 
Je, una ugumu wa kutembea au kupanda ngazi 
● La, sina ugumu 
● Ndiyo, ugumu mdogo 
● Ndiyo, ugumu mwingi 
● Siwezi kabisa 
 
Je, una ugumu wa kukumbuka au kuzingatia (concentrating) 
● La, sina shida 
● Ndiyo, shida kidogo 
● Ndiyo, ugumu mwingi 
● Siwezi kabisa 
 
Je, una ugumu wa kujitunza kama vile kuosha mwili mzima au kuvaa  
● La, sina ugumu 
● Ndiyo, ugumu mdogo 
● Ndiyo, ugumu mwingi 
● Siwezi kabisa 
●  
Ukitumia lugha yako ya kawaida unaugumu wa kuwasiliana kama vile kuelewa au kueleweka na wengine 
● La, sina ugumu 
● Ndiyo, ugumu mdogo 
● Ndiyo, ugumu mwingi 
● Siwezi kabisa 
 
 
17. 
Uko na wasiwasi yoyote ya kupokea pesa hizi?  
18.  
Hotline no.0800720406-save 
 
19.  
Pesa zikipotea hatutarejesha 
 
20. 
Hotline no. inafanya kuanzia 7.30am-7.30pm mon-thur 8.30am-5pm fri-sat,ni bure kupiga 
 
21. 
Pin ni siri yako,usiweke pin kawaida kama 1111 au tarehe ya kuzaliwa 
 
22. 
Ukisajiliwa baada ya wiki mbili utapokea shilingi elfu tatu, kisha mwezi ujao shilingi elfu tatu na ndo 
itakuwa ya mwisho na hutoweza kushiriki kwenye mradi mwingine wa GD 
 
23. 
Ni hayo tu, Asante sana kwa wakati wako na kwa kukamilisha fomu hii.  
 
Je, kuna jambo ungependa kuniuliza? 
 

You might also like