You are on page 1of 10

Mhoji: Tupo kata ya Katavi, na kama nilivyojitambulisha, Mimi naitwa Protesia Prosper,

nimetokea Wizara ya Afya, tuko na wenzangu kwenye kata yenu, tunafanya utafiti
kuhusu maswala ya Afya na chanjo kwa ujumla. Sasa kama nilivyojitambulisha,
ningeomba na wewe ujitambulishe
Mhojiwa: Kwa majina naitwa Benjamin John Kavinde, mkazi wa kata ya Kivavi, mtaa wa
malejera.
Mhoji: sawa, una cheo chochote kwenye jamiii
Mhojiwa: hapana hapana
Mhoji: sawa. Na kama nilivyosema maswala ya chanjo, kuna chanjo zozote zile ambazo
umewahi kuzisikia
Mhojiwa: ndio ndio, chanjo zipo, huwa zinapita hadi mtaani kabisa, watoa huduma nadhani wa
Hospitali
Mhoji: mhmm Chanjo gani ambazo wewe ulishawahi kuzisikia
Mhojiwa: aah mara nyingi huwaga ni chanjo za watoto wadogodogo sanasana, sijafwatilia sana
kujua ni chanjo zipi huwa wanachoma
Mhoji: mhmmm Chanjo nyingine ambayo umewahi kusikia
Mhojiwa: mhhh Chanjo ndo hizo tu sanasana nlizozisikia za watoto toto
Mhoji: watoto, hujawahi kusikia chanjo nyingine
Mhojiwa: chanjo nyingine, zipo, zipo, kwamfano kulikuwa na mlipuko wa Corona
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: walikuwa wanatangaza kwamba kuna hizo chanjo, za Corona
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: mhhh
Mhoji: Kwahiyo chanjo ya Corona ilikuwakwaajili ya Corona. Na hii Corona yenyewe kwa mara
ya kwanza uliisikia wapi
Mhojiwa: Corona, ilisikika kwenye vyombo vya habari hapahapa, maana yake 2018 ilikuwa
inaanza
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: 2019 kama sikosei
Mhoji: aah sawa, ulisikia kwenye redio ama kwenye
Mhojiwa: karibia social media zote, redio, vyombo vya habari, mitandao
Mhoji: sawa. Na walisema huu ugonjwa unaambukizwaje
Mhojiwa: Huu ugonjwa wa Corona. Walitaja dalili zote hizo, ikiwepo kushikana mikono, mtu
anayekohoa maana yake
Mhoji: ambapo inaambukizwa
Mhojiwa: eeeh ndo dalili zake kama hizo
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: Maana yake mkusanyiko wa watu wengi yah
Mhoji: sawa Na dalili zake huyu mtu aliyepata huu ugonjwa
Mhojiwa:dalili zake, kuna kifua kikali, kukosa pumzi nadhani, kwa kubana sana. Nakumbuka
hizo tu
Mhoji: Na watu wanafikiri, au wewe hapo mwenyewe, unafikiri labda inachukua muda gani,
mpaka mtu kuanza kuonyesha dalili. Kwamba sasa kashapata ugonjwa, atakaa nao
kwa muda gani mpaka aanze kuonyesha dalili. Dalili zake unazifahamu lakini
Mhojiwa:eeh dalili zake nazifahamu, maana yake wanashauri wenyewe ukianza kuona dalili
kama hizo za kifua kinabana, unakohoa kwa tabu, kwenye kuhema kule, wanashauri
ufike kwenye kituo cha Hospitali kilicho karibu
Mhoji: aah sawa
Mhojiwa: eeeh
Mhoji: Na ukipata sasa unakaa nazo muda gani mpaka uanze kuonyesha hizi dalili
Mhojiwa: aaah kwenye dalili zake, muda hapo sijajua, kwasababu sijawahi kupata
Mhoji: mhmmm, hujawahi kusikia hata watu wakiwa wanasema, au wakitangaza
Mhojiwa: kwenye matangazo inasikika ila sijafwatilia sana
Mhoji: wewe kwa unavyohisi, ukapita hapo nje, ukakutana na mtu akakuambukiza Corona,
utakaa naye muda gani, mpaka uanze kukohoa, au kufanyaje sijui, mafua kama
ulivosema
Mhojiwa: maana yake hapa nadhani itatembea pamoja tu kama ilivyo dalili ya mafua, kwenye
siku tatu nne (wote wakicheka)
Mhoji: sawa. Labda mtaani kwenu labda, mshamuhisi mtu, ama kuna mtu labda ndo alikuwa
ananyooshewa kidole kwamba yeye ndo, kawaletea Corona katika eneo hili, kwamba
ndo kaja kuwaambukiza Corona
Mhojiwa: Hapana, kwa mtaani kwetu hapa sijawahi kusikia Dalili kama hizo
Mhoji: mhmmm sawa. Na unafikiri labda, kuna kundi la watu ambao ndo wapo hatarini zaidi
kupata Corona
Mhojiwa: kundi
Mhoji: namaanisha labda wazee, watoto, vijana, ni watu gani wewe unahisi wapo hatarini zaidi
Mhojiwa: Corona sanasana ni wazee
Mhoji: Wewe unahisi kwanini ni wazee
Mhojiwa: Umri umeenda alafu baadhi ya kinga zao, zinakuwa zinashindwa kufanya kazi vizuri
Mhoji: mhmmm sawa. Na kwamfano likitokea jambo lolote kwenye hii jamii yetu ya hapa, watu
wa kawaida wanakuwa wanashirikishwa vipi, ushirikishwaji wake upoje, au huwa
wanafanye kuhakikisha labda kila mwananchi anapata taarifa, au kila mtu ambaye
yupo kwenye eneo hili
Mhojiwa: aaah nadhani uongozi wa mtaa huwa unatoa taarifa kupitisha mkutano au kikao
kwenye Ofisi zao, ili watujuze ni nini cha kufanya.
Mhoji: mhmmm Kwahiyo huwaga mna mikutano
Mhojiwa: eeh huwa kunakuwaga na mikutano
Mhoji: aah na kwenye hii mikutano labda kuna watu ambao labda huwaga wanaachwa, au
wanatengwa hivi
Mhojiwa: hapana, huwaga ni wote, wana mtaa wote
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: mhhh
Mhoji: sawa. na Kaka labda nikuulize, wewe ulichanja
Mhojiwa: Chanjo ya Corona hiyo
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: hapana
Mhoji: kwanini sasa
Mhojiwa: eeeh yani kwanini sikuchanja
Mhoji: enheee
Mhojiwa: aaah sikuwepo interested nayo sana(akicheka) Kwasababu tuliambiwa mazoezi sijui
nini, yani baadhi ya mazoezi yanasaidia sanasana.
Mhoji: Kwahiyo wewe ulikuwa unafanya mazoezi
Mhojiwa: eeeh
Mhoji: (akicheka) Haya bana. Na kwenye familia yako kuna pia wale wengine ambao
hawajachanja. Wewe unafikiri wana maoni gani kuhusu hii chanjo
Mhojiwa: aah kwenye kuchanja hiyo tuliambiwa kila mtu na hobi yake yani, Ukiona wewe ni wa
kwenda kuchanja kachanje
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: eehe inategemea na Afya yako yenyewe
Mhoji: (akiguna) sawa. Hamna kuna labda yale maneno maneno ya mtaani watu walivokuwa
wanasema sema kuhusu chanjo labda, hayajachangia kidogo kweli wewe kutokwenda
kuchanja
Mhojiwa: aah hiyo, hiyo kwangu haijachangia, kusema nisiende kuchanja
Mhoji: aah sasa hujaenda kuchanja kwasababu tu unafanya mazoezi
Mhojiwa: eeeh imani yangu ilikuwa kwenye mazoezi
Mhoji: (akicheka) na siku nyingine unaamka labda hujisikii vizuri, hujafanya mazoezi, huoni
kama unakuwa kwenye nanilia hatarishi
Mhojiwa: Hiyo hipo lakini ni asilimia ndogo sana kwangu
Mhoji: mmhh ulikuwa huogopi, ulikuwa hujisikii kama upo kwenye hatari ya kupata Corona,
kipindi kile sasa nazungumzia
Mhojiwa: hapana, kwasababu mimi sio mtu wa kukaa kwenye mikusanyiko ya watu wengi sana
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: eeeeh
Mhoji: Kwahiyo eeh, lakini si upo hapa hapa kazini
Mhojiwa: ndio
Mhoji: na wateja walikuwa wanakuja
Mhojiwa: eeh hapahapa
Mhoji: na mnasalimiana nao
Mhojiwa: eeh kipindi cha Corona kulikuwa kuna maji ya kunawa maana yake kila mteja
anayeingia, lazima anawe na sabuni kabisa, sasa ndo aingie ndani
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: eeeh
Mhoji: kwahiyo ulikuwa unahisi Corona
Mhojiwa: eeh nilikuwa na amani kabisa
Mhoji: haiwezi kukupata
Mhojiwa: ndio
Mhoji: aaah sawa. Na kuna hawa viongozi wa Dini, wa Afya, wa Kisiasa, wa Kijamii,
uhamasishaji wao upoje, au unahisi labda ni kiongozi gani, ndo wana nguvu ya
kuhamasisha zaidi, au ndo wakihamasisha zaidi , watu wanahamasika au
wanawasikiliza
Mhojiwa: hapo kwenye uhamasishaji, maana yake Viongozi wa mtaa walikuwa wanahamasisha ,
kuna mambo ya kuweka hivo vitendea kazi kama maji ya kunawa hayo, sabuni hizo,
enhee. Kwenye Uongozi wa Kidini, wenyewe walikuwa wanahamasisha karibia
kwenye vyote tunavyofanya, tuepuke mikusanyiko kwasababu tulikuwa tunakutana
nao karibia mara nyingi kila jumapili
Mhoji: mhhhh
Mhojiwa: mhh
Mhoji: na unahisi uhamasishaji wao labda, ukiangalia, yani ukiangalia wale wanavohamasisha
na hawa viongozi wa kiserikali wanavohamasisha, sijui watendaji, ni wapi wanakuwa
na kundi kubwa sana, ambalo watu wanahamasika
Mhojiwa: Kundi kubwa linapatikana Kansani nadhani, ndo uhamasishaji wake unakuwa
mkubwa
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: mhhh
Mhoji: sawa. mhhh hivi umesema watu walikuwa wananawa mikono, sasa hivi wakiingia
hawanawi mikono au bado wananawaga mikono
Mhojiwa: hamna kwa sasahivi hawanawi
Mhoji: kwanini
Mhojiwa: Imani kubwa ni kama Corona haipo hivi
Mhoji: Kwani mlitangaziwa kwamba Corona imeisha
Mhojiwa: Hiyo ya kutangaziwa kwamba Corona imeisha hatujaambiwa, ila hata matangazo ya
Corona sasahivi Serikali imekuwa haitangazi kabisa
Mhoji: mhhh
Mhojiwa: mhmmm
Mhoji: Kwani kutokutangazwa ndo
Mhojiwa: tunaamini kwamba wenda Corona haipo tayari
Mhoji: mhmmm, na kama chanjo gani cha taarifa una kiamini zaidi
Mhojiwa: Mimi sanasana ni Social media, mitandao ya kijamii
Mhoji: Yani maana yake, una maanisha hadi facebook uko
Mhojiwa: Natumia sanasana Instagram na Twitter
Mhoji: Huwaga unaziamini
Mhojiwa: ndiyo, kuna vyombo vya habari ambavyo naviamini
Mhoji: Ndo instagram na twitter
Mhojiwa: eeeh
Mhoji: sawa, kuna kingine
Mhojiwa: hapana
Mhoji: mhmmm hivi wewe unaamini hii chanjo ya Corona, inaweza ikamzuia mtu asipate
Corona
Mhojiwa: aaah yani kwenye hiyo chanjo ya Corona, mtu asipate
Mhoji: mhhh
Mhojiwa: asilimia ndogo sana ila inaweza ikazuia siyo asilimia zote mia
Mhoji: mhmm inaweza ikazuia ila kwaasilimia ndogo
Mhojiwa: eeh asilimia ndogo sana
Mhoji: mhmmm, aaahm, wewe unafikiri likitokea jambo lolote, tufanye kazi na viongozi
waliopo au tuunde kamati nyingine mpya. Jambo jipya limetokea au uvumbuzi mpya,
tunatakiwa tuje hapa kwenye mtaa wenu, tufanye kazi na Viongozi waliopo au
itafutwe kamati nyingine mpya
Mhojiwa: aah hapo, bora kuanza na Viongozi waliopo, ila ikitokea labda wenyewe
wameshindwa, imeshindikana, hao wenyewe maana yake wanaweza kuchagua labda
huyu mtu aongoze kwa huu muda, kwa hili jambo mpaka litakapoisha
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: ndio
Mhoji: yani maana yake iundwe kamati nyingine mpya, au
Mhojiwa: Yani, iliyopo ileile iendelee. Ikitokea wameshindwa au imeshindikana, ndo
itengenezwe mpya hiyo
Mhoji: anhaa, kwamfano sasahivi ikitaka kutengenezwa, unafikiri hao watu watawapata vipi
Mhojiwa: waliopo madarakani haohao ndo wata, wenyewe si wanakuwa washashindwa
Mhoji: mhmmm kwahiyo
Mhojiwa: lazima watatafuta option yoyote ile, ile ambayo itatua changamoto hiyo
Mhoji: sawa. Na kwa maoni yako wewe unafikiri Wizara ya Afya imeshughulikia vipi hili swala
la Corona
Mhojiwa: aah imejitahidi sana kwenye janga la Corona
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: imeenda mbali sana
Mhoji: au kuna namna ambavyo ingeongezea ongezea, labda
Mhojiwa: aah imejitahidi sana
Mhoji: imefanyaje
Mhojiwa: imefanya vizuri
Mhoji: (akicheka) huwezi kuniambia vitu ambavyo Wizara imejitahidi navyo
Mhojiwa: aaah Wizara ya Afya imejitahidi sana yani, imeonekana kwa ukubwa baada ya janga
la Corona
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: eeh
Mhoji: mhmmm, kuna mtu mwingine amewahi kuja mtaani kutoa huduma za Afya, ukiachana na
nanilii, na hao wahudumu wetu wa Afya
Mhojiwa: hapana, wanapitaga tu hao wahudumu wa Afya wa chanjo hizo
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: yah
Mhoji: Na hapa kwenye kituo chenu cha karibu, utendaji kazi wa hao wahudumu wa Afya,
unauonaje. Maana yake wanaweza wakawa sababu ya watu kwenda kuchanja au
wakawa saingine pengine, kutokana na kauli au umbali nini, kukawa kuna kikwazo
hapo
Mhojiwa: yani, kuwe kuna sababu labda inayozuia watu wasiende kuchanja
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: aaah hiyo hamna, wahudumu siyo sababu nadhani kwenye chanjo hiyo ni imani ya
mtu binafsi ndo itampelekea yeye aende akachanje au asiende kuchanja
Mhoji: mhmmmm kwahiyo kule kwa wahudumu, utendaji kazi freshi
Mhojiwa: eeeh wenyewe wapo kawaida tu
Mhoji: anhaaaa, na labda unafahamu, au unafikiri serikali itumie njia ggani kushirikisha taarifa
jamii
Mhojiwa: sijaelewa
Mhoji: ulisema taarifa mara nyingi unazipata kwenye redio, kwenye mitandao, kuna labda njia
nyingine bora unahisi serikali ikiitumia, watu wanapata taarifa kwa uharaka
Mhojiwa: aaah hapo nadhani ni mikutano ndo inaweza kufikishia watu wote kwa pamoja, yani
taarifa wakaipata wote kwa pamoja, ni mkutano ndio
Mhoji: sawa, hakuna watu wanaopata shida labda lugha, imeongelewa kiswahili wenyewe
hawajui
Mhojiwa: hapana
Mhoji: labda hawasikiii
Mhojiwa: hamna, kwenye lugha nadhani wote tunaelewana kwa pamoja, kiswahili kinaeleweka
Mhoji: mhmmm sawa. Unafahamu mipango, au sera niseme sijui mikakati ambayo serikali
ilifanya ili kuwahimiza watu kwenda kupata chanjo
Mhojiwa: hapana
Mhoji: mmh, haya makatazo ,mahimizo hivi kuzuia watu wasipate chanjo, yani watu kwenda
kupata chanjo, kuhamasisha watu kwenda kupata chanjo
Mhojiwa: aah kwenye uhamasishaji hapo, hamna hamna
Mhoji: mikakati gani serikali iliweka ikafanya watu wakaenda kuchanja, saingine unakuta hata
walikuwa hawataki kwenda kuchanja, ikabidi wakachanje
Mhojiwa: Hapo nadhani ni kwaajili ya kutoka nje yani, mipaka ukitaka kusafiri, ilifika hatua
yani kama hujachanja
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: huwezi ukatoka. Nadhani hiyo ndo ililazimisha wengi sana wachanje
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: eeeh
Mhoji: sawa. Na swali la mwisho kaka
Mhojiwa: ndiyo
Mhoji: unafikiri serikali itumie njia gani, ili hawa ambao hawajachanja na wenyewe waikubali
chanjo
Mhojiwa: aaah yani chanjo nadhani ukiwaambia watu wachanje, itakuwa ngumu kwasababu
hiyo Corona hawana imani kwamba bado ipo. Kwahiyo ukiwashauri wakachanje
sahizi, aaah sidhani kama wataenda. Labda uweke kikwazo ambacho kitamzuia
kwenye mambo yake, hapo ndo atachanja ili afanye mambo yake, bila ya hivyo,
sidhani kama itakuwa rahisi
Mhoji: Mhmmmm
Mhojiwa: mhh
Mhoji: Tufanya sasa ndo kipindi kile, Coona imepamba moto, chanjo ipo na watu hawataki
kuchanja. Wewe unafikiri Serikali ingefanya nini watu wangechanja
Mhojiwa: aah yani jinsi ya kuwafanya watu wachanje wakati Corona ipo
Mhoji: mhmmmm
Mhojiwa: aah hapo wangekuwa wana imani inayoeleweka kwaajili ya chanjo wangechanja tu.
Kwasababu kilichokuwa kilichokuwa kina , hawaiamini tu tuseme, hawana imani na
hiyo chanjo yenyewe
Mhoji: Hasa hiyo imani tunawapaje
Mhojiwa: unawaaminishaje watu waamini, au
Mhoji: yani tufanyaje ili watu waamini
Mhojiwa: ili watu waamini
Mhoji: eeeh
Mhojiwa: nadhani ili watu waamini inabidi wawe na uhakika, alafu chanjo zenyewe zianzie
hukohuko Serikalini
Mhoji: (akicheka) si imeanzia serikalini hata hivyo. Alianza kuchanja kiongozi wetu mkubwa
Mhojiwa: Sasa unakuta wenyewe hao, mwingine anakubali, mwingine anakataa. Kwahiyo pale
watakaokubali nao, watakaoikataa wengine watakataa
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: nadhani ni umoja kwa wenyewe, huku chini inakuwa ni rahisi
Mhoji: mhmmmm Kaka watu wa huku, wewe ni wa huku?
Mhojiwa: Ndio
Mhoji: kabila gani
Mhojiwa: ni muhehe
Mhoji: aaah muhehe, sawa. Muhehe mna labda mila au desturi ambazo mlikuwa mnazifanya na
ilivyotokea huu ugonjwa wa Corona, ikawa ni changamoto kwenu. Kwamfano,
nikupe mfano labda mlizoea kula pamoja , si ndio?
Mhojiwa: ndio
Mhoji: na ikatokea labda msile pamoja ikawa ni changamoto, labda msikae makundi makundi,
pengine mnakuwaga na mikusanyiko, pengine labda, mlipendelea kushikana mikono,
kusalimiana, lasivyo mnaona kama hiyo salamu siyo, haijakamilika bila kushikana
mikono, kuna vitu kama hivyo.
Mhojiwa: Hamna, yani kwa upande wetu sisi tulikuwa tunasikiliza sana. Tukiambiwa
tusishikane mikono, yani baada ya Corona kuingia, vyote viliachwa havikuleta utata
hivo
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: Ndio
Mhoji: sawa. Mtu alikuwa akipata Corona mlikuwa mnafanyaje
Mhojiwa: mhhh, hatujakutana na mtu mwenye Corona
Mhoji: Kama mngekutana naye
Mhojiwa: Hapo ni kuwaishwa hospitali tu
Mhoji: aya kaka Asante kwa majibu yako mazuri

You might also like