You are on page 1of 40

Wakala wa Usalama na Afya

Mahali Pa Kazi (Osha)

MWONGOZO WA
KUUNDA NA
KUTEKELEZA SERA
YA USALAMA NA AFYA
MAHALI PA KAZI
USIMAMIZI NA UDHIBITI WA NYARAKA HII
Mwenye Msimamizi Wafaidika Imepitishwa
Nyaraka na:
Toleo Upitishaji Mkurgenzi wa
Mkaguzi maeneo ya
usalama na afya Bodi ya Ushauri
Mkuu kazi
mahali pa kazi
1.0 Saini
©2021 Tarehe
Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

YALIYOMO

Kutambua Waliochangia Kuandaa Mwongozo 3

1. Utangulizi 4
1.1. Muktadhi wa Kisera 5
1.2. Mahitaji ya Kisheria 5
1.3. Malengo ya Mwongozo 5
1.4. Wigo wa Mwongozo 6
1.5. Matumizi ya Mwongozo 6
1.6. Baadhi ya Maneno, Ufupisho na Misemo Iliyotumika 6

2. Uhusika na Majukumu ya Kila Mdau 8


2.1. Uhusika na Majukumu ya Osha 8
2.2. Uhusika na Majukumu ya Mwajiri au Mwenye Eneo la Kazi 8
2.3. Uhusika na Majukumu ya Waajiriwa 9
2.4. Uhusika na Majukumu ya Wadau Wengine 9

3. Muundo Wa Sera Ya Usalama Na Afya Mahali Pa Kazi 10


3.1. Tamko la Sera (Ohs Policy Statement) 10
3.1.1. Namna ya Kupata Tamko la Sera 10
3.1.2. Nguvu ya Tamko la Sera 13
3.2. Utaratibu wa Kutekeleza Tamko la Sera 13
3.2.1. Azma ya Uongozi Kwenye Kutekeleza Tamko la Sera 13
3.2.2. Utaratibu wa Kuainisha Majukumu 13
3.2.3. Ulinganifu wa Sera na Kazi zilizopo Eneo la Kazi 15

4. Utaratibu Wa Kuunda, Kutekeleza Na Kuhuisha Sera 17


4.1. Utaratibu wa Kuandaa Sera 17
4.1.1. Utaratibu wa Kuandaa Majukumu ya Kiwajibu 18
4.1.2. Utaratibu wa Kuandaa Majukumu ya Kimamlaka 18
4.1.3. Utaratibu wa Kuandaa Tamko la Sera 18
4.1.4. Kuandaa Mikakati Itakayopelekea Sera Kukubalika 19

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 1


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

4.2. Utaratibu wa Kutekeleza Sera 19


4.2.1. Kufungamanisha Kazi za Uzalishaji na zile
za Usalama na Afya 19
4.2.2. Kufanya Mawasiliano Yanayohusiana na Sera 20

5. Kuhusianisha Sera 22
5.1 Utaratibu wa Kuhuisha Sera 22
5.2 Ubora wa Sera 22

Viambata 23
i: Mfano wa Tamko la Sera ya Usalama, Afya na
Ustawi Mahali pa Kazi 23
ii: Mtiririko wa Sera na Utaratibu wa Kuitekeleza 24
iii: Orodha Hakiki ya Kupima Ubora wa Sera 26
iv: Uthaminishaji wa Sera 32

Rejea 35

2 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

KUTAMBUA WALIOCHANGIA
KUANDAA MWONGOZO

T aarifa zilizotumika kuandaa mwongozo huu zimetokana na michango ya


wadau wa ndani na nje. Wadau wa nje ambao michango yao imetumika
wanajumuisha maeneo yote ya kazi yaliyosajiliwa na OSHA. Aidha,
majumuisho ya taarifa zilizopelekea kuandaa mwongozo huu yamefanywa
na Mhandisi Robert Mashinji, Ndg. Joji H. Chali na Bi. Ruth Nzota.

Pia, Wadau walioshiriki kuandika mwongozo huu ni Bi. Khadija Mwenda


(Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA), Ndg. Alexander E. Ngata (Mkurugenzi
wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi), Ndg. Joshua Matiko (Mkurugewnzi wa
Utafiti, Mafunzo na Uhamasishaji), Mhandisi Robert Mashinji (Kaimu Meneja
wa Usalama Mahali pa Kazi), Ndg. Jossam Kamaza (Kaimu Meneja wa
Mafunzo na Utafiti), Ndg. Jerome Materu (Meneja wa Afya Mahali pa Kazi),
Bi. Joyce Mwambungu (Mkuu wa Kitengo cha Sheria), Bi. Beatha Mathias
(Kaimu Meneja wa Fedha), Ndg. Joji H. Chali (Kaimu Meneja wa Kanda ya
Pwani) na Bi. Ruth Nzota (Katibu Muhtasi).

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 3


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

1. UTANGULIZI

T aasisi iliyopo kisheria kwa ajili ya kuunganisha jitihada za kumlinda


mfanyakazi au uwekezaji dhidi ya vihatarishi mahali pa kazi ni
Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) inayosimamia
sheria Na. 5 ya usalama na afya mahali pa kazi ya mwaka 2003.

Ndani ya sheria ya usalama na afya mahali pa kazi ya mwaka 2003


kuna vipengele vinavyoelekeza namna na mipaka ya kuunda sera ya
usalama na afya mahali pa kazi kwenye kila eneo la kazi.

Sera ya usalama na afya mahali pa kazi ni nyenzo muhimu inayotoa


mwelekeo wa namna mwajiri au mwenye eneo la kazi alivyoweka
dhamira ya kulinda nguvukazi aliyonayo au atakayokuwanayo dhidi ya
vihatarishi vinavyotokana na kazi au michakato inayoendelea kwenye
eneo lake la usimamizi au umiliki. Aidha, mwajiri anapounda sera ya
usalama na afya katika eneo lake la kazi ni anatarajiwa kuzingatia
sera ya taifa ya usalama na afya mahali pa kazi.

Sera nyingi za maeneo ya kazi zinatofautiana miundo. Hata hivyo,


sera zote zinaunganishwa na namna zinavyozingatia suala la
kutenganisha majukumu ya kiwajibu (Functional Responsibilities) na
Majukumu ya kimamlaka (Functional Authorities).

Maeneo mengi ya kazi hayana sera husika au sera zilizopo haziakisi


dhamira halisi ya mwajiri au mmiliki kwa mujibu wa sheria za nchi,
aina ya uwekezaji, asili ya kazi, aina ya wafanyakazi au vifaa husika.

Pia, maeneo mengi ya kazi yamekuwa na changamoto ya kusimika


sera zinazozingatia majukumu ya kimamlaka au kiwajibu kati ya
mwajiri, mfanyakazi na wadau wengine wakiwemo wakandarasi,
watoa huduma na watu wanaotembelea eneo la kazi (workplace
visitors). Isitoshe, maamuzi ya wigo na namna ya kuunda sera
itakayokidhi mchanganyiko (diversity) wa watu katika eneo la kazi
imekuwa ni changamoto kwa waajiri wengi.

4 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

1.1. MUKTADHI WA KISERA


Malengo ya msingi ya sera ya taifa ya usalama na afya mahali pa kazi ni
kuweka mwelekeo wa namna ya kudhibiti ajali na magonjwa yatokanayo
na kazi. Mwelekeo huo unahusisha kuanzisha na kutekeleza mifumo
itakayojenga utamaduni wa kuzuia ajali na magonjwa yatokanayo na
kazi ambapo ushirikiano kati ya serikali, waajiri, waajiriwa na wadau
wengine wenye maslahi kwenye eneo husika la kazi ni nyenzo muhimu.

Kwa kuzingatia hayo, OSHA itatoa ushirikiano kwa niaba ya serikali


katika kuandaa, kusimika na kufuatilia ufanisi wa sera kwenye kila
eneo la kazi.

1.2. MAHITAJI YA KISHERIA


Sheria Na. 5 ya mwaka 2003 ya usalama na afya mahali pa kazi katika
kifungu cha 96 inaelekeza eneo la kazi au kiwanda chenye wafanyakazi
wanaozidi wanne (4) kutekeleza yafuatayo: -
- Kuunda sera ya kimaandishi ya usalama na afya mahali husika
pa kazi ikionyesha namna wafanyakazi watakavyolindwa dhidi
ya vihatarishi vya usalama au afya vinavyotokana na shughuli
za uzalishaji.
- Mwenye eneo la kazi au mwajiri anatakiwa kuandaa ufafanuzi
unaoonyesha mgawanyo wa majukumu ya kutekeleza sera;
- Kuandaa utaratibu unaohusu jinsi ya kutekeleza sera ya usalama
na afya mahali hapo pa kazi;
-  Kuionyesha au kuibandika sera kwenye maeneo ambako
itasomeka kirahisi kwa wahusika wote wa eneo la kazi;
-  Kuwapatia wafanyakazi wote andiko la sera pamoja na
mwongozo wake wa namna ya kuitekeleza.

1.3. MALENGO YA MWONGOZO


Kutokana na changamoto za kuunda, kusimika na kufuatilia sera za
usalama na afya kwenye maeneo ya kazi, OSHA imeandaa mwongozo
huu ili kuhakikisha sera zinazoudwa zinakidhi mahitaji ya sheria ikiwemo
sera ya taifa ya usalama na afya mahali pa kazi. Aidha, mwongozo huu
unaweka mwelekeo wa namna ya: -
i. Kuzingatia sera ya taifa ya usalama na afya mahali pa kazi
wakati wa kuandaa au kutekeleza sera iliyoundwa kwenye eneo
la kazi;
ii. Kuzingatia sheria ya usalama na afya mahali pa kazi wakati wa
kuandaa au kutekeleza sera iliyoundwa kwenye eneo husika la
kazi;

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 5


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

iii. Kuweka majukumu ya kimamlaka na kiwajibu kwa kila mdau;


iv. Kuainisha mikakati ya kisera inayoendana na aina ya uwekezaji
au asili ya eneo la kazi au aina ya wafanyakazi ikiwemo
mchanganyiko (diversity) na pia aina ya vifaa kwenye eneo
husika la kazi;
v. Kuamua na kuweka wigo wa sera.

1.4. WIGO WA MWONGOZO


Wamiliki wa maeneo ya kazi walioajiri zaidi ya wafanyakazi wanne
(4) wanalazimika kuunda sera ya usalama na afya kwa kuzingatia
mwongozo huu. Walengwa wengine wa mwongozo huu ni: -
- Waajiri au wamiliki wote wa maeneo ya kazi waliopo Tanzania
bara;
- Watu wote wanaojihusisha na ukaguzi au uchunguzi au utafiti;
- Watu wote wenye maslahi ya usalama na afya mahali pa kazi;

1.5. MATUMIZI YA MWONGOZO


Mwongozo huu siyo mbadala wa sheria Na. 5 ya mwaka 2003 ya
usalama na afya mahali pa kazi Sambamba na kanuni zake. Mwongozo
huu umeandaliwa ili kuonyesha njia ya kukidhi matakwa ya sheria na
kanuni husika. Aidha, mwongozo huu unatoa mwelekeo wa mambo
ya kuzingatia wakati wa kuandaa sera ili kukidhi matakwa ya sheria.

1.6. BAADHI YA MANENO, UFUPISHO NA MISEMO


ILIYOTUMIKA
Baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye mwongozo huu na tafsiri
zake kwa mujibu wa nyaraka hii: -
■ OHS – Ni ufupisho ya maneno ya kiingereza yanayomaanisha
Usalama na Afya Mahali Mahali pa Kazi (Occupational Health
and Safety).
■  OSHA – Huu ni ufupisho wa maneno ya kiingereza
yanayomaanisha Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi
(Occupational Safety and Health Authority).
■  KPI – Huu ni ufipisho wa maneno ya kiingereza
yanayoomaanisha Viashiria vya Ufanisi Katika Kutekeleza
Wajibu (Key Performance Indicators).
■  Leseni ya Ithibati – Hii ni nyaraka yenye muonekano wa cheti
inayotolewa kwenye eneo la kazi lenye usajili wa OSHA ikiwa ni
kuashiria eneo husika limekidhi vigezo vya msingi vya kuweka
mifumo ya kuzuia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi. Uhai
wa Leseni hii ni miezi kumi na mbili na inaweza kuondolewa
wakati wowote pale uimara wa mifumo unapotiliwa shaka.

6 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

■ 
Majukumu ya Kiwajibu – Ni yale Majukumu ambayo mhusika
atayatekeleza kama yalivyoainishwa. Mfano wa majukumu ya
aina hii ni wajibu wa kuvaa barakoa kwenye maeneo yenye
vumbi.
■ 
Majukumu ya Kimamlaka – Ni yale Majukumu yanayomtaka
aliyepo eneo la kazi kuchukua hatua halali zenye lengo la
kuzuia ajali, tukio au ugonjwa utokanao na kazi. Majukumu
haya yanatoa mamlaka ya moja kwa moja ya kudhibiti athari
za vihatarishi katika eneo alipo mhusika. Mfano wa majukumu
ya aina hii ni wajibu wa kutowasha mashine ambayo mikanda
yake haijafunikwa.
■ 
Mwongozo – Haya ni maelezo yanayofafanua namna ya
kutekeleza jambo au kazi Fulani kwa kutumia lugha rahisi fasaha
na inayoweza kubadirishwa kirahasi kuwa katika vitendo.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 7


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

2.
UHUSIKA NA MAJUKUMU
YA KILA MDAU

N i dhahiri kwamba sera zinatofautiana kimuundo. Hata hivyo,


sera zote zinaunganishwa na namna zinavyozingatia suala la
kutenganisha majukumu ya kiwajibu (Functional Responsibilities) na
Majukumu ya kimamlaka (Functional Authorities). Vipengele viwili vya
majukumu ya kiwajibu na yale ya kimamlaka ndivyo vinatofautisha
ubora wa sera ya usalama na afya katika eneo husika la kazi.

2.1. UHUSIKA NA MAJUKUMU YA OSHA


Uhusika wa OSHA kwenye uundaji wa sera ya usalama na afya
mahali pa kazi ni kuandaa miongozo itakayotumiwa na wamiliki au
waajiri kwenye maeneo ya kazi wakati wa kuandaa, kutekeleza na
kuhuisha sera;
Aidha, Majukumu ya OSHA kuhusu sera za usalama na afya kwenye
maeneo ya kazi wakati wa utekelezaji wake ni pamoja na: -
i. Kuhakikisha sera zilizoundwa na waajiri au wamiliki wa maeneo
ya kazi hazikinzani na sheria au sera ya tafia ya usalama na
afya mahali pa kazi;
ii. Kuhakikisha sera iliyoundwa kwenye eneo la kazi imeambatana
na utaratibu (mwongozo) unaohusu jinsi ya kuitekeleza;
iii. Kuhakikisha nakala za tamko la sera zimebandikwa kwenye
maeneo yote ambako zitasomeka kirahisi kwa wahusika wa
eneo la kazi;
iv.  Kuhakikisha mwajiri au mwenye eneo la kazi amewapatia
wafanyakazi nakala ya tamko la sera pamoja na utaratibu wa
namna ya kuitekeleza;
v. Kuhakikisha yaliyomo kwenye sera ya usalama na afya kwenye
eneo husika la kazi yanatekelezwa na mwajiri.

2.2. UHUSIKA NA MAJUKUMU YA MWAJIRI AU MWENYE


ENEO LA KAZI
Mwenye eneo la kazi au mwajiri atahusika kufuata miongozo iliyopo
ya kuandaa sera za usalama na afya mahali pa kazi. Aidha, mwenye
eneo la kazi au mwajiri anatakiwa kutekeleza yafuatayo kuhusiana na

8 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

sera ya usalama na afya kwenye eneo lake la kazi: -


i. Kuandaa tamko la sera ya usalama na afya kwenye eneo lake
la kazi;
ii.  Kuainisha majukumu ya kiwajibu na kimamlaka ya mwajiri,
mwajiriwa na wadau wengine wanaohusika na eneo lake la
kazi;
iii. Kuandaa utaratibu au mwongozo wa kutekeleza sera yake ya
usalama na afya kwenye eneo husika la kazi;
iv. Kubandika tamko la sera kwenye maeneo ambako litasomeka
kirahisi kwa wadau hasa wafanyakazi;
v. Kuwapatia wafanyakazi nakala ya tamko la sera pamoja na
mwongozo wa utekelezaji;
vi. Kuwasilisha kwa mkaguzi mkuu wa usalama na afya mahali pa
kazi nakala ya tamko la sera iliyohuishwa pamoja na mwongozo
wa utekelezaji wakati wote anapoomba Leseni ya ithibati.

2.3. UHUSIKA NA MAJUKUMU YA WAAJIRIWA


Mwajiriwa kwenye eneo la kazi analo jukumu la kupokea, kuisoma na
kuielewa sera ya usalama na afya kwenye eneo la kazi alipoajiriwa.
Aidha, mwajiriwa analo jukumu la kisera Kuhakikisha: -
i. Sera inatekelezwa kwenye eneo lake la uzalishaji;
ii. Kutoa michango yenye lengo la kuboresha sera iliyopo;
iii. Kushiriki shughuli za kuhuisha sera

2.4. UHUSIKA NA MAJUKUMU YA WADAU WENGINE


Wadau wengine wanaohusiana na eneo la kazi ni pamoja na watoa
huduma, wakandarasi na wageni wanaotembelea eneo la kazi kwa
sababu mbalimbali Ikiwemo ukaguzi. Wadau wa eneo la kazi wanalo
jukumu la kuzingatia yaliyomo kwenye sera ya usalama na afya
mahali hapo pa kazi. Aidha, majukumu ya kisera ya wadau ni pamoja
na kuhakikisha: -
i. Wanafuata miongozo ya kutekeleza sera;
ii. Wanatoa michango yenye lengo la kuboresha sera iliyopo;
iii. Wanahusianisha sera zao na ile ya wanapotekeleza majukumu.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 9


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

3.
MUUNDO WA SERA YA USALAMA
NA AFYA MAHALI PA KAZI

M wongozo huu unatoa mwelekeo wa namna muundo wa sera ya


usalama na afya kwenye eneo la kazi utakavyokuwa kuwa. Sera
ya usalama na afya mahali pa kazi inatakiwa kuanza kwa tamko (OHS
Policy Statement), Madhumuni ya sera, Majukumu ya kila mdau na
utaratibu wa kuitekeleza. Aidha, sera iliyokamilika inatakiwa kuwa na
utaratibu wa namna ya kuihuisha na kupima ufanisi wake.

3.1. TAMKO LA SERA (OHS POLICY STATEMENT)


Sera ya usalama na afya mahali pa kazi inatakiwa kuanza kwa kutoa
tamko (OHS Policy Statement). Tamko la sera lionyeshe bayana
malengo na mipango ya usalama, afya na ustawi kwenye eneo la kazi.

3.1.1 Namna ya Kupata Tamko la Sera


Malengo na mipango ya usalama na afya mahali pa kazi yanaanzia
kwenye tamko la sera ambalo linaweza kupatikana kutokana na
kufanya mapitio ya: -
- Sera ya taifa ya usalama na afya mahali pa kazi;
- Sheria ya Usalama na Afya mahali pa kazi;
- Kanuni zilizopo zinazohusu moja kwa moja eneo husika la kazi;
- Mipango ya uwekezaji kwenye eneo la kazi;
- Mipango ya Uzalishaji kwenye eneo la kazi;
- Dira na dhima ya eneo la kazi (kama ipo);
- Muundo wa kutekeleza majukumu kwenye eneo la kazi;
- Sera nyingine zilizopo kwenye eneo la kazi zinaweza kufanyiwa
rejea ili kupata maingizo kwenye sera ya usalama na afya
mahali pa kazi;
- Viwango vya vihatarishi kwenye eneo la kazi.

a. Rejea ya sera ya taifa ya usalama na afya mahali pa kazi


 Sera ya usalama na afya kwenye eneo la kazi inatakiwa
kuzingatia malengo ya taifa katika kusimamia masuala ya
usalama, afya na ustawi wa mfanyakazi pamoja na uwekezaji.
Sera ya eneo la kazi ieleze bayana yafuatayo: -

10 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

i. Wigo wa vihatarishi kwenye eneo husika la kazi;


ii. Wajibu wa mwajiri kudhibiti athari za vihatarishi kwenye
eneo la kazi;
iii.  Wajibu wa mfanyakazi kushiriki katika mikakati ya
kudhibiti athari za vihatarishi mahali pa kazi;
iv. Wajibu wa wadau wasio waajiri au waajiriwa kushiriki
katika mikakati ya kudhibiti athari za vihatarishi vya
usalama na afya kwenye eneo la kazi;
v. Namna na muundo kugharamia utekelezaji wa mikakati
ya kudhibiti vihatarishi;
vi. Matokeo yanayokusudiwa kutokana na sera husika;
vii. Vigezo vya kupima ufanisi wa utekelezaji wa mikakati ya
kudhibiti vihatarishi;
viii. Utaratibu wa kutekeleza sera ya usalama na afya mahali
pa kazi;
ix. Utaratibu wa kufanya mapitio ya sera;
x. Saini ya Afisa mtandaji wa juu kwenye eneo la kazi
Sambamba na Afisa rasilimaliwatu husika.

b. Kupitia mipango na malengo ya uwekezaji


 Hatua ya kuandaa au kuhuisha sera ihusishe mapitio ya
mipango ya uwekezaji au Uzalishaji kwenye eneo la kazi kwa
kuzingatia aina ya Vifaa, Mitambo, Mazingira ya uwekezaji,
Jamii itakayolizunguka eneo la kazi, Mwingiliano wa watu
(wafanyakazi, wakandarasi watoa huduma na jamii).


Aidha, aina ya athari zitokanazo na vihatarishi kama
vilivyofanyiwa tathmini ya vihatarishi mahali pa kazi ni muhimu
kuwa sehemu ya maandalizi ya kutengeneza sera ya usalama
na afya mahali pa kazi.

Mwajiri anapoandaa sera ya usalama na afya mahali pa kazi


atatakiwa kuzingatia malengo ya uwekezaji katika eneo husika
la kazi ili kuingiza vipengele vitakavyosaidia sera kudumu kwa
muda mrefu pasipo kuhuishwa mara kwa mara.

c. Kuhuisha au kufanya mapitio ya mipango ya uzalishaji


Kabla ya kuandika sera ya usalama na afya mahali pa kazi,
mwongozo huu unaelekeza kupitia mpango mkakati wa
uzalishaji ili kubaini vipengele vinavyoweza kuhusianishwa na
sera ya usalama na afya mahali pa kazi hasa kwenye ugawaji
wa majukumu ya kila mmoja, Idara, vitengo, uongozi na wadau.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 11


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

Mapitio hayo yataifanya sera kuweka malengo yanayopimika


kwa kuhusisha uzalishaji kwenye eneo la kazi.

Kwa mantiki hiyo, sera itatambua bayana thamani ya kuzalisha


au kutoa huduma pasipo majeruhi au magonjwa yatokanayo
na kazi. Thamani inayopatikana kutokana na kuzuia ajali au
magonjwa yatokanayo na kazi itafsiriwe kama mchango wa kila
mtumishi, Idara na kitengo kwenye pato la taasisi.

d. Dira ya eneo la kazi


Mwongozo huu unaelekeza kuwa, sera inayoandaliwa izingatie
dira ya kampuni au eneo la kazi husika.

e. Dhima ya eneo la kazi


Sera ya usalama na afya mahali pa kazi lazima iendane na
dhima ya eneo la kazi. Maandalizi ya sera yahusishe kuingiza
vipengele vitakavyouwiana na dhima ya uwekezaji katika eneo
husika la kazi.

f. Sera nyingine zilizopo kwenye eneo la kazi


Sera ya usalama na afya mahali pa kazi inatakiwa kuoanishwa
na sera nyingine zilizopo kwenye eneo la kazi ili iweze kuweka
mazingira ya uwajibikaji wa pamoja.

Sera ya usalama na afya kazini ni muhimu ikaweka mazingira ya


uwajibikaji wa kila mfanyakazi katika kuzuia athari za vihatarishi
kwenye eneo la kazi ikiwa ni sehemu ya ajira yake.

Kwa mantiki hiyo, mwajiri au mwenye eneo la kazi anatakiwa


kufanya mapitio ya sera nyingine zilizopo kwenye eneo lake
la kazi ambapo atahakikisha anapata vipengele vinavyoweza
kufungamanishwa na sera ya usalama na afya mahali pa kazi.

g. Vihatarishi kwenye eneo la kazi


 Eneo la kazi linalazimika kufanya tathmini ya mambo au
mazingira yanayoweza kusababisha kumea kwa vihatarishi
kabla ya kuunda sera ya usalama na afya mahali pa kazi. Baada
ya kubainisha vihatarishi, Mwajiri aoanishe mikakati ya sera na
udhibiti wa vihatarishi vilivyobainika. Uoanishaji wa mikakati
ya kisera dhidi ya udhibiti wa vihatarishi unatakiwa kuzingatia
maeneo mtambuka kulingana na mazingira ya kazi. Baadhi ya
masuala au maeneo hayo ni: -

12 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

i. Wigo wa kazi zinazokusudiwa;


ii. Aina ya Mitambo, vifaa, miundombinu au malighafi;
iii. Mahali Mitambo itakapofungwa au ilipofungwa;
iv. Nguvukazi;
v. Majirani na wadau wa nje;
vi. Viashiria vya ufanisi.

3.1.2 Nguvu ya Tamko la Sera


Tamko linatakiwa kutiwa Saini na afisa wa ngazi ya juu kabisa aliyepo
kwenye eneo la kazi sambamba na kuonyesha tarehe ya tamko
ikiwemo mhuri wa Kampuni au eneo la kazi. Aidha, tamko linaweza
kusainiwa na viongozi wengine kadri Kampuni husika itakavyoona
inafaa. Mfano wa tamko umeonyeshwa kwenye Kiambatisho I.

3.2. UTARATIBU WA KUTEKELEZA TAMKO LA SERA


Sera ya usalama na afya mahali pa kazi ni muhimu ionyeshe kwa
uwazi madhumuni na mipango ya utekelezaji wa dhima ya kusimamia
usalama, afya na ustawi kwenye eneo husika la kazi. Sera ionyesha
azma na majukumu ya kila upanda.

3.2.1 Azma ya Uongozi Kwenye Kutekeleza Tamko la Sera


Mwongozo huu unatoa mwelekeo kwamba, sera ijumuishe azma ya
uongozi katika: -
i. Kuimarisha usalama, afya na ustawi kwenye eneo la kazi;
ii. Kuingiza masuala ya usalama na afya mahali pa kazi kwenye
usimamizi wa shughuli za uzalishaji;
iii. Kuwekeza kwenye masuala ya usalama, afya na ustawi wa
wafanyakazi wakati wote wa uhai wa eneo husika la kazi;
iv.  Kuhuisha sera ya usalama na afya mahali pa kazi pale
inapohitajika;
v. Kuhakikisha usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali
pa kazi yanatekelezwa na kila mmoja kwenye eneo la kazi;
vi. Kuweka vigezo vya ufanisi wa kila mmoja kuhusiana na harakati
za kuzuia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

3.2.2 Utaratibu wa kuainisha majukumu


Sera ya usalama na afya mahali pa kazi ni muhimu ionyeshe kwa
uwazi majukumu ya kila mmoja katika eneo husika. Majukumu yalenge
kwenye kudhibiti athari za vihatarishi vilivyobainika wakati wa kufanya
tathmini ya vihatarishi mahali pa kazi. Majukumu hayo yaeleze ushiriki
wa kila mmoja kimamlaka na kiwajibu.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 13


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

a. Majukumu ya mwajiri;
Utaratibu wa kutekeleza sera ufafanue majukumu ya kiwajibu
anayotakiwa kuyatekeleza mwajiri Ikiwemo: -
i. Kuhakikisha utekelezaji wa matakwa ya sheria wakati
wote wa uhai wa eneo la kazi unafanyika kwa ufanisi;
ii.  Kumlinda mfanyakazi na wadau wengine dhidi ya
vihatarishi vyote vinavyohusiana na eneo la kazi;
iii. Kutengeneza mazingira rafiki yenye staha kwa ajili ya
kufanyia kazi;
iv.  Kuwakinga wafanyakazi wanapokuwa kazini dhidi ya
ubaguzi, unyanyasaji, unyanyapaa na udhalilishaji wa
aina yoyote;
v. Kugharamia vifaa na shughuli zote za usalama, afya na
ustawi mahali pa kazi;
vi.  Kuhakikisha anashirikiana na mamlaka za usimamizi
Ikiwemo OSHA ili kuwezesha programu za masuala ya
usalama na afya mahali pa kazi zinatekelezeka kwa
ufanisi;
vii. Kubadilishana (sharing) taarifa za usalama na afya kati
ya mwajiri na wadau wakiwemo wafanyakazi hasa haki
za kulindwa dhidi ya vihatarishi mahali pa kazi.

Sambamba na majukumu ya kiwajibu, mwongozo wa kutekeleza


sera uonyeshe mwelekeo wa majukumu ya kimamlaka
anayotakiwa kutekeleza mwajiri Ikiwemo namna: -
i. Kuanzisha mchakato wa kuhuisha sera kila inapolazimu;
ii. Kuashirikisha wadau wakiwemo wafanyakazi endapo
viashiria vya athari za vihatarishi vitaongezeka au
kubadilika;
iii. 
Kuhakikisha eneo la kazi linakuwa na uelewa wa
pamoja kuhusu nia ya kumlinda mfanyakazi pamoja na
uwekezaji dhidi ya vihatarishi vinavyotokana na shughuli
za uzalishaji au michakato katika eneo la kazi;
iv. Wadau wa eneo husika la kazi wakiwemo watoa huduma,
wakandarasi na wageni watakavyohusika na sera ya
usalama na afya mahali pa kazi;
v. Wakuu wa vitengo, Idara au sehemu wanavyowajibika
kudhibiti vihatarishi vya usalama, afya na ustawi wa
mfanyakazi.

14 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

b. Majukumu ya mwajiriwa;
 Mwongozo wa kutekeleza sera pia ufafanue majukumu
ya kiwajibu anayotakiwa kutekeleza mwajiriwa Ikiwemo
kuhakikisha kuwa: -
i. Anatii kanuni na kufuata taratibu za usalama, afya na
ustawi mahali pa kazi wakati wote akiwa eneo la kazi;
ii. Anatoa ushirikiano kwa mwajiri katika kutoa na kupokea
taarifa za usalama, afya na ustawi mahali pa kazi kadri
anavyozipata au kuzibaini;
iii. Analinda na kusimamia miundombinu ya kudhibiti athari
za vihatarishi mahali pa kazi;
iv.  Kuhakikisha kuwa anajilinda yeye na watu wengine
wanaoweza kuathirika na kazi anazozifanya.

Majukumu ya kimamlaka aliyonayo mwajiriwa yatakuwa ni


sehemu ya uainishaji wa sera ya usalama na afya mahali pa
kazi ikiwemo: -
i. Kusitisha na kutoa taarifa kwa mwajiri kuhusu kazi yoyote
inayodhaniwa kuwa hatari kwa usalama, afya au ustawi
wa mfanyakazi/uwekezaji;
ii. Kutoa taarifa kwa mwajiri au mamlaka zinazosimamia
masuala ya usalama na afya kuhusu ajali au tukio
kwenye eneo la kazi;
iii. Haki ya kupatiwa mafunzo ya uelewa kuhusu afya na
usalama kazini;
iv.  Haki ya kushirikishwa kwenye programu zinazohusu
usalama, afya na ustawi mahali pa kazi.

c. Majukumu ya wadau wengine wa eneo la kazi;


Sera ifafanue majukumu ya kiwajibu anayotakiwa kutekeleza
mgeni (visitor) wa eneo la kazi, mkandarasi, mtoa huduma au
mtu yeyote mwenye maslahi kwenye eneo la kazi. Majukumu
hayo yaonyeshe namna anavyotakiwa kutekeleza sera ya
usalama na afya mahali pa kazi ikiwemo namna wadau hao
watahamasishwa na mwenye eneo la kazi kuhakikisha kuwa
wanatekeleza sheria ya usalama na afya mahali pa kazi.

3.2.3 Ulinganifu wa sera na kazi zilizopo eneo la kazi


Muundo wa sera unahitaji kumfanya kila mmoja awajibike kuhusiana
na masuala ya usalama, afya na ustawi kwenye eneo analotekeleza
majukumu yake.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 15


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

Kwa mantiki hiyo, sera inatakiwa kuweka mwelekeo wa namna ya


kufuatilia ubora na ukamilifu wa taratibu za kusimamia usalama, afya
na ustawi kwenye eneo la kazi. Baadhi ya maeneo ambayo sera
inaweza kuyagusia ni: -
i.  Kuainisha kwenye tamko la sera namna kila mmoja
atakavyowajibika;
ii. Wajibu wa kutekeleza masuala ya usalama, afya na ustawi
yaainishwe au yawe sehemu ya majukumu (Part of Job
description) ya mfanyakazi;
iii. Utaratibu wa Kuhakikisha masuala ya usalama, afya na
ustawi yanajumuishwa kwenye vigezo vya kupima ufanisi wa
mfanyakazi;
iv. Mapitio ya mara kwa mara ya masuala ya usalama na afya
sehemu ya kazi;
v. Taarifa za utekelezaji wa masuala ya usalama, afya na ustawi
mahali pa kazi iwe sehemu ya taarifa nyingine za kutathmini
maendeleo katika utekelezaji wa majukumu kwenye eneo la
kazi.

16 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

UTARATIBU WA KUUNDA,
4. KUTEKELEZA NA KUHUISHA
SERA

M wongozo huu unatoa utaratibu wa kuandaa sera, kutekeleza sera


na kuihuisha. Hata hivyo yafuatayo ni muhimu yakazingatiwa
kwenye hatua zote zilizotajwa kuhusiana na sera: -
i. Sera iandaliwe na mwenye eneo husika la kazi kwa kuwahusisha
wadau;
ii. Zoezi la kuandaa au kuhuisha sera liwe shirikishi likizingatia
ushiriki wa uongozi, wafanyakazi, vyama vya wafanyakazi na
wawakilishi wa usalama na afya mahali pa kazi;
iii. Uandaaji wa sera uzingatie malengo ya eneo la kazi kuhusiana
na ufanisi au uendelevu wa shughuli mbalimbali ndani na nje ya
eneo la kazi;
iv. Sera izingatie vihatarishi vya usalama, afya na ustawi kwenye
eneo la kazi;
v.  Utaratibu ulioainishwa wa kutekeleza sera ufahamike na
uzingatiwe na wadau;
vi. Sera iendane na malengo ya Jumla ya taifa ya kudhibiti ajali na
magonjwa yatokanayo na kazi;
vii. Sera ya usalama na afya ipewe uzito unaoshabihiana na sera
nyingine katika eneo husika la kazi;
viii. Sera ya usalama na afya mahali pa kazi ifungamanishwe na
sera nyingine zilizopo eneo la kazi.

4.1. UTARATIBU WA KUANDAA SERA


Kabla ya kuandika sera ya usalama na afya mahali pa kazi, mwajiri
analazimika kuangalia namna eneo lake la kazi lilivyoainisha
majukumu ya kila Idara, kitengo, wafanyakazi na watoa huduma ili
kubainisha majukumu ya kiwajibu na kimamlaka kwa kila mmoja
kuhusiana na masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.

Majukumu yalenge kwenye kudhibiti athari za vihatarishi vilivyobainika


wakati wa kufanya tathmini ya vihatarishi mahali pa kazi (OHS
Risk Assessment). Majukumu hayo yaeleze ushiriki wa kila mmoja
kimamlaka na kiwajibu.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 17


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

Malengo ya sera ya usalama na afya mahali pa kazi yanatakiwa


kuzingatia mikakati ya eneo la kazi katika kuongeza ufanisi na
kuleta maendeleo endelevu. Maandalizi ya sera yaangalie namna
kila anayehusika katika eneo la kazi atakavyotekeleza majukumu ya
kiwajibu sambamba na majukumu ya kimamlaka. Mchanganuo wote
huo uainishwe kwenye tamko la sera.

4.1.1 Utaratibu wa Kuandaa Majukumu ya Kiwajibu


Maandalizi ya majukumu ya kiwajibu ni muhimu yakazingatia: -
i. Tathmini ya athari za vihatarishi mahali pa kazi;
ii. Ushiriki wa wadau hasa wafanyakazi;
iii. Uoanishaji wa majukumu ya jumla ya kiidara, kisekta, kundi au
sehemu;
iv. Kuhakikisha majukumu yaliyoandaliwa yanapimika;
v. Kuhakikisha kuwa majukumu ya mfanyakazi, Idara au kitengo
yanalingana na ujira au uzalishaji wa Idara/kitengo;

4.1.2 Utaratibu wa Kuandaa Majukumu ya Kimamlaka


Maandalizi ya Majukumu ya kimamlaka ni muhimu yakahusisha: -
i. Matakwa ya sheria ya usalama na afya mahali pa kazi;
ii. Ukubwa wa vihatarishi mahali husika pa kazi hasa athari;
iii. Muundo wa uendeshaji katika eneo la kazi;
iv. Uwekaji wa vigezo vya kutekeleza majukumu ya kimamlaka;
v. Aina ya wahusika katika eneo la kazi watakaopewa majukumu
ya kimamlaka

4.1.3 Utaratibu wa Kuandaa Tamko la Sera


Tamko la sera linatakiwa kuonyesha nia ya uongozi wa eneo la kazi
kufanya yafuatayo ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kulinda nguvukazi
na uwekezaji utakaofanyika au uliofanyika: -
■  Kuanzisha mifumo na programu zitakazojumuisha masuala ya
usalama, afya na ustawi wa mfanyakazi kwenye shughuli za
uzalishaji katika eneo la kazi;
■  Kutii sheria zinazohusiana na usalama na afya wa mfanyakazi.
Au Kuhakikisha sheria zilizopo ndizo kigezo cha chini kabisa
cha kutekeleza masuala ya usalama, afya na ustawi katika
eneo la kazi;
■  Kuweka rasilimaliwatu wenye weledi kwa ajili ya kusimamia
masuala ya usalama na afya katika eneo la kazi;
■  Kuhakikisha kila mmoja kuanzia uongozi hadi wadau shiriki wa
eneo la kazi wanawajibika kutekeleza taratibu za usalama, afya

18 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

na ustawi zilizowekwa kwenye eneo la kazi;


■ 
Kuonyesha umuhimu wa mashauriano kati ya uongozi na
wafanyakazi wakati wa kutekeleza sera;
■ 
Kufuatilia ufanisi wa sera kwa kuweka njia bora za kufanya
mapitio, kuhuisha na kupima matokeo ya utekelezaji;
■ 
Kuendelea kufanya maboresho kulingana na mahitaji;
■ 
Kuifikisha kwa wadau wa ndani na nje kwa namna stahiki
sambamba na kuweka nakala ya sera kwa ajili ya rejea;
■ 
Kutenga muda na fedha za kutekeleza masuala ya usalama na
afya kwenye eneo la kazi;
■ 
Kuainisha utaratibu wa kutumia fedha katika masuala ya
usalama na afya kwenye eneo la kazi.

4.1.4 Kuandaa Mikakati Itakayopelekea sera Kukubalika


Kimsingi, sera iliyoandaliwa inatakiwa kukubalika kwa wadau wa
sehemu ya kazi. kwa mantiki hiyo sera inatakiwa: -
i. Kujumuisha mahitaji ya sheria, kanuni na miongozo wakati wa
kuandaa;
ii. Kuwa shirikishi ikiwemo kuiwasilisha OSHA kila inapohitajika;
iii. Kuzingatia uwazi katika kuweka malengo, majukumu na vigezo
vya kupima ufanisi;
iv. Kuzingatia staha wakati wa kuandaa majukumu ya kila mmoja;
v. Kuzingatia hali halisi ya eneo la kazi inapoainisha majukumu ya
kila mmoja kuhusiana na usalama na afya mahali pa kazi;
vi.  Kutumia lugha inayoeleweka yaani lugha rahisi, fasaha na
inayotambulika.

4.2. UTARATIBU WA KUTEKELEZA SERA


Utekelezaji wa sera ya usalama na afya kwenye eneo la kazi
unatakiwa kuanza kwa kubainisha kazi za usalama, afya na ustawi
kwenye kila mtambo, mchakato au shughuli iliyoainishwa kwenye
sehemu/kitengo husika. Baadaye shughuli za usimamizi wa pande
zote ufungamanishwe.

4.2.1 Kufungamanisha kazi za uzalishaji na zile za usalama


na afya
Utaratibu wa kubainisha kazi za kiutendaji unaweza kutofautiana
kutoka eneo moja la kazi kwenda jingine isipokuwa yafuatayo
yanatakiwa kuzingatiwa ndani ya sera: -
i.  Kuweka wazi umuhimu wa kuweka kanuni au utaratibu wa
usalama, afya na ustawi wa wafanyakazi kwenye eneo la kazi.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 19


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

ii.  Kuonyesha wahusika wa kuandaa, kufanya mapitio na


kusimamia sera;
iii. Kutamka bayana uhitaji wa kuwepo utaratibu wa kuendesha,
kutunza na kufanya matengenezo ya vifaa au Mitambo;
iv. Kuonyesha uhitaji wa kila mwajiriwa mpya kupewa nakala ya
sera akielezwa kwamba sera hii ni sehemu ya masharti ya ajira
yake;
v. Kutamka aina ya programu za Mafunzo zitakazoongeza weledi
ili kuhahakikisha eneo la kazi linazuia ajali na magonjwa
yatokanayo na kazi;
vi.  Kuonyesha muundo wa kutoa taarifa zinazohusu vihatarishi
mahali pa kazi, ikiwemo utaratibu wa kufanya kazi kwenye
maeneo hatarishi;
vii. Kuainisha umuhimu wa kufanya vikao vya mara kwa mara vya
usalama na afya kwenye eneo la kazi.
viii. Sera igusie vipengele vinavyotakiwa kufanyiwa mjadala kwenye
vikao.
ix.  Sera iainishe kwa kifupi maeneo yanayoweza kufanyiwa
wasilisho la maandishi na yale yatakayoelezewa kwa mdomo
(verbally).

4.2.2 Kufanya mawasiliano yanayohusiana na Sera


Mawasiliano yanayohusu utekelezaji wa sera ya usalama na afya
kwenye eneo la kazi ni muhimu yakazingatia: -
■  Ufasaha;
■  Kuonyesha mwelekeo wa dhamira ya uongozi kuunga mkono
mfumo uliyopo wa mawasiliano yanayohusu usalama na afya
kazini;
■  Kuonyesha mwelekeo wa namna uongozi utakavyofanya
uchakataji wa taarifa zinazohusu mwenendo wa usalama na
afya mahali pa kazi;
■  Kuonyesha mwelekeo wa hatua zitakazochukuliwa ili kuongeza
ufanisi wa sera.

Baadhi ya njia zinazoweza kutumika kuiwasilisha au kufanya wasilisho


la sera kwa wadau ni pamoja na: -
i. Mafunzo ya awali (Induction training);
ii. Mwongozo au utaratibu wa kutekeleza sera;
iii. Mijadala ya Kamati za usalama na afya mahali pa kazi;
iv. Vikao kazi;
v. Mgawanyo wa majukumu ya kazi (Job Description);

20 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

vi. Tovuti, Ubao wa matangazo na vikao mbalimbali;


vii. Hotuba na mihadhara kwenye eneo la kazi;
viii. Taarifa za ukaguzi;
ix. Maombi ya Leseni ya ithibati;
x. Mrejesho wa uongozi baada ya kupokea taarifa zinazohusu
usalama, afya au ustawi katika eneo la kazi bila kujali chanzo.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 21


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

5. KUHUSIANISHA SERA

Sera ya usalama na afya mahali pa kazi inatakiwa kufungamanishwa


na sera nyingine zilizopo kwenye eneo la kazi ili iweze kuweka
mazingira ya uwajibikaji wa pamoja. Sera ya usalama na afya kazini
ni muhimu ikaweka mazingira ya uwajibikaji wa kila mfanyakazi katika
kuzuia athari za vihatarishi kwenye eneo la kazi ikiwa ni sehemu ya
ajira yake.

5.1. UTARATIBU WA KUHUISHA SERA


Sera ya usalama na afya mahali pa kazi ni muhimu ikatamka bayana
mazingira yanayoweza kupelekea ifanyiwe mapitio. Baadhi ya
mazingira yanayoweza kuonyeshwa kwenye sera kwamba yakitokea
itafanyiwa mapitio ni pamoja na: -
i. Kupitwa na wakati (kama vile baada ya miezi 6, 12, 18, 24 au
miezi 36);
ii. Mabadiliko ya mfumo wa uzalishaji au utendaji kazi;
iii. Ajali au tukio kutokea;
iv. Baada ya kufanya mapitio ya tathmini ya athari za vihatarishi
mahali pa kazi;
v. Kubadili uongozi au umiliki.

5.2. UBORA WA SERA


Sera ya usalama na afya mahali pa kazi itapimwa kwa kujibu maswali
yaliyoainishwa kwenye Kiambata III ambapo sera iliyo bora inatarajiwa
kupata alama zisizopungua 85 zikiwemo asilimia 12 za kipengele G
(Tamko la Sera). Mpangilio wa ubora umeainishwa kwenye Kiambata
IV.

22 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

VIAMBATA

I: Mfano wa Tamko la Sera ya Usalama, Afya na Ustawi


mahali pa kazi

TAMKO LA SERA YA USALAMA, AFYA NA USTAWI MAHALI PA KAZI


(JINA LA KAMPUNI AU ENEO LA KAZI) Inayo dhamira thabiti ya kufikia lengo la kuweka mazingira
ya kazi yaliyo rafiki, salama na yasiyo hatari kwa afya au ustawi Ikiwemo kuwepo mpango endelevu wa
kufanya maboresho kwa wakati. Lengo hili litafikiwa kwa kufuata au kutii mikakati iliyowekwa na (JINA
LA KAMPUNI AU ENEO LA KAZI) kwa kusudio la kuzidi wajibu ulioainishwa kwenye sheria zilizopo.

Wajibu:
■ U
ongozi utafanya kazi kwa kushirikiana na wafanyakazi hasa Kamati za usalama na afya mahali pa
kazi ili kuchukua hatua stahiki zenye lengo la kudhibiti athari za vihatarishi mahali pa kazi;

■ M
eneja na wasimamizi wanawajibika Kuhakikisha wanaowasimamia wanatekeleza majukumu yao
kwenye mazingira rafiki, salama na yasiyo hatari kwa afya. Wajibu huu unajumuisha kutoa Mafunzo
au maelekezo stahiki Sambamba na kufuatilia malalamiko yaliyowafikia Ikiwemo Mapendekezo ya
kufanya maboresho;

■ 
Wasimamizi, Wafayakazi, Wakandarasi, Watoa huduma na Wageni wanatarajiwa na (JINA LA
KAMPUNI AU ENEO LA KAZI) kutekeleza majukumu yao kwa njia zilizo rafiki kwa afya, usalama na
ustawi wao pamoja na watu wengine;

■ 
(JINA LA KAMPUNI AU ENEO LA KAZI) imedhamiria Kuwezesha Mafunzo, miundombinu – kazi
na maelekezo yote stahiki ili kuhakikisha utendaji kazi ndani ya himaya ya (JINA LA KAMPUNI AU
ENEO LA KAZI) ni rafiki, salama na usio na hatari za afya au ustawi;

■ 
Endapo italazimika, (JINA LA KAMPUNI AU ENEO LA KAZI) itachukua hatua za kinidhamu kwa
yule atakayeshindwa kutekeleza wajibu wa kufanya kazi kwa usalama au asiyetii sheria zilizopo za
usalama, afya na ustawi sehemu za kazi Ikiwemo sera na utaratibu kama (JINA LA KAMPUNI AU
ENEO LA KAZI) ilivyoainisha.

Kudhibiti ajali, magonjwa kazini pamoja na uharibifu wa mazingira ni wajibu wa kila mmoja. (JINA LA
KAMPUNI AU ENEO LA KAZI) inatarajia kila mmoja atashirikiana na (JINA LA KAMPUNI AU ENEO LA
KAZI) kwa kuweka juhudi endelevu za kila siku za kusimamia usalama, afya na ustawi mahali pa kazi na
kwamba kila mmoja atapimwa kutokana na matokeo ya juhudi zake.

Tamko hili limesainiwa leo tarehe ...................................... na: -

........................................ (Saini) ......................................... (Saini)

................................... (Jina Kamili) ................................... (Jina Kamili)

(Cheo) Afisa wa juu anayehusika na rasilimaliwatu

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 23


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

II: Mtiririko wa Sera na Utaratibu wa Kuitekeleza

1. Utangulizi
Elezea Chimbuko la Kuanzisha eneo tajwa la kazi ukionyesha
matarajio yaliyopo ya kukuza uzalishaji kwa kuzingatia ushiriki wa
wadau wa ndani na nje sambamba na uendelevu wa uzalishaji. Pia
onyesha malengo ya kibiashara, kijamii, kiustawi, usalama, afya
na mazingira. Sehemu hii ionyeshe namna sera na sheria za nchi
zitakavyozingatiwa. Aidha, onyesha endapo eneo la kazi tajwa linazo
sera nyingine zaidi ya sera ya usalama na afya mahali pa kazi. Isitoshe,
onyesha namna sera ya usalama na afya mahali pa kazi ilivyo muhimu
ukilinganisha na sera zingine. Utangulizi usizidi maneno 150.

2. Dira na Dhima ya Eneo la Kazi


Dira na dhima ya eneo la kazi iandikwe endapo eneo la kazi linayo

3. Muundo wa Utekelezaji Majukumu


Elelezea muundo wa uongozi wa eneo la kazi ukionyesha kwa
ufupi majukumu ya kila Idara/kitengo baadaye muundo wa vyeo na
majukumu ya kila cheo kiwajibu na kimamlaka. Onyesha fursa iliyopo
ya kuingiza majukumu yanayohusu usimamizi wa masuala ya usalama
na afya mahali pa kazi kwenye majukumu ya kila mmoja kuanzia Idara
hadi cheo kimoja kimoja. Sehemu hii isizidi maneno 500.

4. Vifaa au Michakato Iliyopo Eneo la Kazi


Elezea kwa kifupi vifaa vya msingi vinavyokusudiwa kuwepo au
vilivyopo kwenye eneo la kazi. Aidha, fafanua mtiririko wa uzalishaji
ukionyesha mwanzo wa mchakato hatua kwa hatua hadi matokeo ya
mchakato. Maelezo kwenye eneo hili yasizidi maneno 400.

5. Asili ya Vihatarishi Vilivyopo Kwenye Eneo la Kazi


Fanya uchambuzi wa asili ya vihatarishi vinavyotarajiwa au vilivyopo
kwenye eneo la kazi ukianzia na aina (mfano vihatarishi vya kifizikia)
baadaye namna vinavyopatikana kwenye eneo la kazi. Sehemu hii
isizidi maneno 500.

6. Walengwa wa Sera
Ainisha walengwa wote wa sera ya usalama na afya mahali pa kazi
ukionyesha ushiriki wao katika hatua zote za uhai wa sera. Sehemu
hii isizidi maneno 150.

24 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

7. Tamko la Sera
Andika tamko rasmi la sera ukiacha nafasi ya kusainiwa na Afisa
Mtendaji wa ngazi ya juu kabisa kwenye eneo la kazi sambamba na
saini ya Mwakilishi wa Usalama na Afya Mahali pa kazi anayewakilisha
kitengo/Idara ambayo ni muhimili (core function) ya eneo la kazi.
Tamko lisizidi maneno 350.

8. Utaratibu wa Kutekeleza Sera


Ainisha utaratibu wa kutekeleza sera ukionyesha namna ya kufanya
mawasiliano yenye lengo la kusambaza yaliyomo kwenye sera.
Aidha, bainisha namna utendaji wa kila siku utakavyounganishwa
kwenye wajibu ulioainishwa kwenye sera kuhusiana na sera masuala
ya usalama, afya na ustawi Kazini kwa kila mdau aliyepo eneo la kazi.
Pia, ainisha namna sera itakavyohuishwa Ikiwemo kuiwianisha na
sera zingine zilizopo eneo la kazi. Kipengele hiki kisizidi maneno
500.

9. Wajibu wa Kila Mdau


Ainisha majukumu ya kiwajibu na kimamlaka ya kila mdau
anayetarajiwa kuwepo au aliyepo kwenye eneo la kazi. Kipengele
hiki kisizidi maneno 400.

10. Namna ya Kupima Ufanisi wa Kila Mdau


Fafanua namna kila mdau atakavyopimwa utekelezaji wa majukumu
yake. Sera ieleze kwa kifupi namna vigezo vya kupima ufanisi wa
utekelezaji wa masuala ya usalama, afya na ustawi vitakavyoathiri
KPI ya mdau. Eneo hili lisizidi maneno 250.

11. Namna ya Kugharamia Masuala ya Usalama na Afya


Ainisha uwiano (asilimia) wa mapato ya eneo la kazi itakayotumika
kwenye shughuli za usimamizi masuala ya usalama na afya Kazini. Pia,
eneo la kazi linaweza kuonyesha vyanzo vya mapato yatakayotumika
kuendesha shughuli za usalama, afya na ustawi wa wafanyakazi.
Aidha, ainisha namna ya kusimamia matumizi ya fungu la usalama na
afya mahali pa kazi. Kipengele hiki kisizidi maneno 150.

12. Utaratibu wa Kufanya Mapitio ya Sera


Elezea mazingira yatakayopelekea kufanya mapitio ya sera. Onyesha
atakayekuwa na wajibu wa Kuanzisha mchakato wa kufanya mapitio
ya sera. Eneo hili lisizidi maneno 100.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 25


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

III: Orodha hakiki ya kupima ubora wa Sera

Maswali ya orodha hakiki yaliyoainishwa kwenye kipengele A~K yatatumika


kufanya tathmini ya ubora wa sera ya usalama na afya mahali pa kazi.
Maswali tajwa yanaweza kutumika kama hadidu za rejea wakati wa kuandaa
sera ya usalama na afya mahali pa kazi.
A. Utangulizi
SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 2%)
i. Je, Sera ina utangulizi? (Kama jibu Hapana,
usijibu maswali yanayofuata);
ii.  Je, utangulizi umetambua sera ya taifa na
sheria inayohusu usalama na afya mahali pa
kazi?
iii. Je, utangulizi umeonyesha kwamba usalama
na afya ni sehemu ya uzalishaji endelevu?
iv. Je, utangulizi wa sera umetambua umuhimu
wa wadau wa eneo la kazi ikiwemo OSHA?
v. Je, utangulizi umetambua uwepo au matarajio
ya kuwepo sera zingine kwenye eneo hilo la
kazi?

B. Dira na Dhima ya Eneo la Kazi


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 0.5%)
i.  Je, eneo la kazi linayo dira iliyoandikwa?
(Kama Hapana, usijibu maswali yanayofuata);
ii. Je, eneo la kazi linayo dhima ya kimaandishi?
iii. Je, dhima imetajwa kwenye sera ya usalama
na afya mahali pa kazi?
iv. Je, Dira imetajwa kwenye sera ya usalama
na afya mahali pa kazi?

26 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

C. Muundo wa Utekelezaji Majukumu kwenye eneo la kazi


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 0.5%)
i. Je, Muundo wa uongozi umeelezwa? (Kama
Hapana, usijibu maswali yanayofuata);
ii. Je, majukumu ya kila Idara yameainishwa?
iii. Je, Majukumu ya kila kitengo yameainishwa?
iv. Je, Majukumu ya kiwajibu kuhusu usalama na
afya kwa kila kitengo yametajwa?
v. Je, Majukumu ya kimamlaka kuhusu usalama
na afya kwa kila kitengo yametajwa?
vi. Je, Majukumu ya kiwajibu kuhusu usalama na
afya kwa kila idara yametajwa?
vii. Je, Majukumu ya kimamlaka kuhusu usalama
na afya kwa kila idara yametajwa?
viii. Je, sera imeainisha fursa zilizopo za kuingiza
majukumu ya usalama, afya na ustawi mahali
pa kazi kwenye majukumu ya kila mhusika?
ix. Je, fursa zilizoingizwa zinao uhusiano wowote
na sheria ya usalama na afya mahali pa kazi?
x. Je, fursa hizo zinao mwelekeo wa kutengeneza
mazingira ya kupima ufanisi?

D. Michakato Iliyopo Eneo la Kazi


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 1%)
i.  Je, sera imeainisha vifaa vilivyopo eneo la
kazi? (Kama jibu Hapana, usijibu maswali
yanayofuata);
ii.  Je, sera imeeleza uwezekano wa kuingiza
vifaa zaidi kwenye eneo la kazi?
iii. Je, sera imeelezea mtiririko wa uzalishaji au
shughuli kwenye eneo la kazi?
iv. Je, sera imefafanua aina ya michakato iliyopo
kwenye eneo la kazi?
v.  Je, matokeo ya mtiririko wa uzalishaji
yameelezwa?

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 27


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

E. Asili ya Vihatarishi kwenye Eneo la Kazi


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele Ndiyo Hapana N/A
hiki lina 2%)
i. Je, sera imefanya uchambuzi wa vihatarishi?
(Kama jibu Hapana, usijibu maswali
yanayofuata);
ii. Je, sera imetaja aina ya vihatarishi vilivyopo
eneo la kazi?
iii.  Je, sera imetaja namna vihatarishi
vinavyoweza kuathiri wafanyakazi?
iv.  Je, sera imeeleza namna vihatarishi
vinavyoweza kuharibu uwekezaji?
v.  Je, sera imeainisha dhamira ya mwenye
eneo la kazi kudhibiti vihatarishi?

F. Walengwa wa sera kwenye Eneo la Kazi


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele Ndiyo Hapana N/A
hiki lina 2%)
i. Je, sera imebainisha walengwa? (Kama jibu
Hapana, usijibu maswali yanayofuata);
ii. Je, sera imeainisha ushiriki wa kila mlengwa
wakati wote wa uhai wa sera?
iii. Je, Sera imeweka mwelekeo wa majukumu
ya kila mlengwa?
iv. Je, sera imeitambua OSHA kama msimamizi
wa utekelezaji wa sheria ya usalama na afya
mahali pa kazi?
v. Je, sera imeainisha utaratibu wa kuifikisha
kwa wadau/walengwa?

28 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

G. Tamko la Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 1.5%)
i. Je, sera inalo tamko rasmi? (Kama Hapana,
usijibu maswali yanayofuata);
ii. Je, tamko limeonyesha malengo/mipango ya
usalama, afya na ustawi?
iii. Je, tamko limeweka bayana dhamira ya
uongozi Kuanzisha na kusimamia mifumo na
programu za usalama, afya na ustawi eneo
la kazi?
iv. Je, tamko limeweka dhamira ya kutii sheria,
kanuni na taratibu zinazohusu usalama na
afya mahali pa kazi?
v.  Je, tamko limeweka dhamira ya kutumia
rasilimali watu sahihi au kuwaongezea
weledi wa masuala ya usalama na afya
mahali pa kazi?
vi. Je, tamko limeonyesha dhamira ya kuweka
mipango endelevu ya upatikanaji wa
rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza
masuala ya usalama, afya na ustawi mahali
pa kazi?
vii. Je, tamko limeonyesha dhamira ya kuweka
misingi ya uwajibikaji wa kila mmoja kwa
nafasi yake katika masuala ya usalama, afya
na ustawi mahali pa kazi?
viii. 
Je, tamko limeweka dhamira ya kufanya
maboresho ya sera na mifumo ya usimamizi
wa masuala ya usalama, afya na ustawi
kadiri mahitaji yatakapoelekeza?
ix. Je, tamko limeonyesha dhamira ya kuweka
vigezo vya kupima ufanisi?
x. Je, tamko limetiwa Saini na wahusika sahihi?
xi.  Je, tamko limewekwa tarehe ya kutiwa
Saini?

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 29


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

H. Utaratibu wa kutekeleza sera


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 2%)
i. Je, sera imeainisha utartibu wa kuitekeleza?
(Kama jibu Hapana, usijibu maswali
yanayofuata);
ii. Je, kazi za kiutendaji za usalama, afya na
ustawi kwenye kila eneo la kiuzalishaji au
mchakato zimeainishwa?
iii. Je, sera imeainisha utaratibu wa kuunganisha
kazi za uzalishaji na zile za usalama na afya
mahali pa kazi?
iv.  Je, utaratibu wa kufanya mapitio
umeainishwa?
v. Je, sera imeweka mwelekeo wa namna ya
kufuatilia ubora na ukamilifu wa taratibu za
kusimamia usalama, afya na ustawi kwenye
eneo la kazi?

I. Wajibu wa Kila Mdau


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 1.5%)
i.  Je, majukumu ya kiwajibu ya uongozi
yameainishwa?
ii.  Je, majukumu ya kimamlaka ya uongozi
yameainishwa?
iii. Je, majukumu ya kiwajibu ya wasimamizi
yameainishwa?
iv. Je, majukumu ya kimamlaka ya wasimamizi
yameainishwa?
v. Je, majukumu ya kiwajibu ya wafanyakazi
yameainishwa?
vi. Je, majukumu ya kimamlaka ya wafanyakazi
yameainishwa?
vii. Je, majukumu ya wakandarasi
yameainishwa?
viii. 
Je, majukumu ya watoa huduma
yameainishwa?
ix.  Je, majukumu ya wageni wanaotarajiwa
kwenye eneo la kazi yameainishwa?
x. Je, majukumu ya kila mmoja yanaendana na
sheria na kanuni zinazosimamia usalama na
afya mahali pa kazi?

30 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

J. Namna ya Kupima ufanisi sera


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 2%)
i. Je, namna ya kupima ufanisi wa sera wakati
wa utekelezaji imeainishwa?
ii. Je, utaratibu wa kupima kila mdau aliyetajwa
kwenye sera umeainishwa?
iii. Je, vigezo vya kutathmini ufanisi wa kila mdau
vinapimika?
iv. Je, vigezo vya kupima kila mdau vimeingizwa
kwenye KPI?
v. Je, vigezo vya kupima ufanisi vimehusishwa
na matokeo/thamani ya uzalishaji?

K. Namna ya kugharamia masuala ya usalama na afya


SWALI HAKIKI (Kila swali kwenye kipengele hiki Ndiyo Hapana N/A
lina 2%)
i. Je, vyanzo vya mapato ya kusimamia masuala
ya usalama na afya kwenye eneo la kazi
vimeainishwa? (Kama jibu Hapana, usijibu
maswali yanayofuata);
ii. Je, vyanzo hivyo ni sehemu ya uwekezaji?
iii. Je, muundo wa upatikanaji wa fungu la
kusimamia masuala ya usalama na afya linavyo
viashiria vya udhabiti wa dhamira husika?
iv. Je, sera imeonyesha mwelekeo wa usimamizi
wa fedha za usalama na afya kuhusisha Idara
kuu (core functional department) kwenye eneo
la kazi?
v.  Je, Idara (kitengo) inayoratibu masuala ya
usalama na afya mahali pa kazi ni sehemu ya
wasimamizi wa fungu husika?

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 31


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

IV: Uthaminishaji wa Sera

Maswali ya orodha hakiki yaliyoainishwa kwenye kipengele A~K yatatumika


kufanya tathmini ya ubora wa sera ya usalama na afya mahali pa kazi. Sera
iliyo bora kabisa inatarajiwa kufikia alama zisizopungua 85% zikiwemo
angalau 12% zinazotokana na kipengele G (Tamko la sera). Sera ya ovyo
kabisa haitazidi 40%.
Alama
Daraja Alama Alama za chini
ya za chini za Juu kwenye
Na. ubora kwenye kwenye daraja hii Matokeo
wa daraja daraja zinazohusu
sera hii hii Tamko la
sera
Atapata Leseni ya Ithibati.
Isipokuwa daraja hili
1 A 85% 100% 12% litashuka hadi sehemu
inayoendana na alama za
tamko la sera.
Atapata Leseni ya Ithibati
isipokuwa atatakiwa
Kuwezesha Mafunzo ya
kitengo kinachosimamia
rasilimali watu, fedha na
manunuzi. Aidha, daraja
2 B 70% 85% 9%
hili litashuka hadi sehemu
inayoendana na alama
za tamko la sera lakini
halipanda kama alama za
tamko zimefikia daraja ya
juu.

32 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

Atapata Leseni ya Ithibati


baada ya Kuwezesha
Mafunzo ya kitengo
kinachosimamia rasilimali
watu, fedha na manunuzi.
3 C 55% 70% 7% Aidha, daraja hili litashuka
hadi sehemu inayoendana
na alama za tamko la sera
lakini halipanda kama
alama zimefikia daraja ya
juu.
Mdau atatakiwa
Kuwezesha Mafunzo
ya kuongeza uelewa
(awareness training) ya
masuala ya usalama, afya
na ustawi kwenye eneo
lake la kazi Sambamba
na Mafunzo ya kitengo
kinachosimamia rasilimali
watu, fedha na manunuzi.
Baada ya kukamilisha
4 D 41% 55% 5%
hayo atapata Leseni ya
Ithibatin kwa sharti la
kufanya mapitio ya sera
husika ndani ya siku 120
tangu kupewa Leseni.
Aidha, daraja hili litashuka
hadi sehemu inayoendana
na alama za tamko la sera
lakini halitapanda kama
alama zimefikia daraja ya
juu.

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 33


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

Mdau atatakiwa kuandika


upya sera ya usalama
na afya mahali pa
kazi. Aidha, atatakiwa
kuwezesha Mafunzo
ya kuongeza uelewa
(awareness training) ya
masuala ya usalama, afya
na ustawi kwenye eneo
lake la kazi Sambamba
5 F 0% 40% 5%
na Mafunzo ya kitengo
kinachosimamia rasilimali
watu, fedha na manunuzi.
Isitoshe atatakiwa kuanza
kuitekeleza sera yake
kwenye eneo la kazi kwa
siku zisizopungua120
kisha kuifanyia mapitio.
Baada ya hatua hizo mdau
atapewa Leseni ya Ithibati.

34 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

REJEA

- Tanzania Government, 2003. The Occupational Health and Safety Act


No.5 of 2003, Government Press.
- Tanzania Government, 2010. Sera ya Taifa ya Usalama na Afya Mahali
pa Kazi, Government Press.
- Government of Tanzania, 2015. The Occupational Safety and Health:
General Administrative Rules, Government Press.
- Bowden, A.R., Lane, M.R. and Martin, J.H., 2002. Triple Bottom Line
Risk Management: Enhancing Profit, Environmental Performance, And
Community Benefits. John Wiley & Sons.
- https://www.ccohs.ca/oshanswers/hsprograms/osh_policy.html, 2011
- Occupational health and safety management systems - Guidelines for
the implementation of OHSAS 18001:2007
- Implementation Guidance manual for ILO Guidelines on Occupational
Safety and Health Management Systems ILO-OSH 2001
-  Department of Occupational safety safey and Health, 2011. Guidelines
on Occupational Health and Safety Management Systems, Mashi
Publication Sdn Bhd

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 35


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

36 Ukurasa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha)


Mwongozo wa Kuunda na Kutekeleza Sera ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (Osha) Ukurasa 37


Wakala wa Usalama na Afya
Mahali Pa Kazi (Osha)

Kwa Mawasiliano zaidi:

Mtendaji Mkuu:
S.L.P 519, Dar es Salaam,
Kiwanja Na. MNY/KMB/565, Kinondoni,
Barabara ya Mahakama,
Simu: +255 (0) 22 2760548, Nukushi: +255 (0) 22 2760552,
Barua Pepe: info@osha.go.tz, Tovuti: www.osha.go.tz

SIMU YA BURE: 0800 11 00 91/2

You might also like